STORY: KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 14




*******************
Ikabidi ninyanyuke kitandani na kujiandaa kwenda kuufungua mlango ili niweze kumjua ni nani huyo anaegonga. Baada ya kufika hapo mlamgoni nikakizungusha taratibu kitasa cha mlango huo na kuufungua, macho yangu yakakutana ana kwa ana na Prisca aliyekuwa anatabasamu huku akiwa yupo na kijana mmoja hivi mtanashati ambaye sikuwa  namfahamu vyema. "Ooho baby pole sana kwa kukuacha peke yako kwa muda mrefu" alisema Prisca huku akinikumbatia. "Hamna wala usijali tayari nilishauzoea upweke" nilisema huku nikimpokea begi dogo alilokuwa amekuja nalo pamoja na mkoba wake. Na baada ya hapo nikawakaribisha mpaka ndani chumbani Prisca moja kwa moja akaenda kwanza kujibwaga mpaka kitandani na kuvua viatu vyake virefu alivyovaa. "Kaka John karibu sana hapa ndio Hotelini nilipokuambia unilete, na huyu hapa ndio huyo rafiki yangu niliyekuambia kesho tunatarajia kusafiri naye anaitwa Joseph au Jose" alimtambulisha kwangu yule kijana niliyemfahamu kwa jina la John Mara baada ya kumsikia Prisca akimtaja. "Aaah nafurahi sana kukufahamu bwana Jose" aliniambia kijana huyo John huku akinipa mkono. "Na mimi pia nimefurahi kukufahamu bwana John karibu sana" nilisema huku nikiupokea mkono wake na kushikana. Prisca akatabasamu na halafu akanibia: "Baby huyo ndie dereva ambaye kesho tunatarajia atatupeleka ile safari yetu ya kwenda kijijini kumuona bibi" Prisca alinifahamisha. "Sawa hakuna shida kabisa, nafurahi kusikia hivyo" nilisema. Kwa muda huu mimi pamoja na huyo dereva John tulikuwa tumeketi kwenye kochi kubwa ambalo lilikuwemo humu chumbani kwenye hii Hoteli na Prisca yeye alikuwa amejilaza kitandani. "Kwahiyo nimeona sio mbaya nimlete hapa aje apaone ili kesho asubuhi na mapema aweze kuja kutuchukua" Prisca aliendelea kuniambia. "Sawa mpenzi hakuna tatizo yote ni sawa tu" nilisema. Mara ghafla kabla atujaendelea na mazungumzo yetu zaidi, Simu ya mezani amabyo ni humu chumbani Hotelini ikaanza kuita! Kwanza tukashtuka sana halafu Prisca akaniangalia mimi na kuniuliza: "Vipi kuna huduma yeyote ambayo uliagiza huko mapokezi?" Prisca aliniuliza. "Hapana sijaagiza chochote" nilimjibu. Basi Prisca akusema tena kitu chochote akanyanyuka na kuiendea meza ndogo iliyokuwa na simu hiyo halafu akaipokea na kuuweka mkonga wake sikioni! "Aloo nakusikiliza, ongea  tafadhali" Prisca alianza kwa kusema hivyo. Maongezi ya upande wa Pili atukuweza kuyasikia vyema Ila Prisca baada ya hapo ndio tulimsikia akiuliza: "Wapoje hao watu na wamesema wana shida gani?" Prisca alimuuliza muhudumu upande wa Pili kwenye simu. Pia atukuweza kumsikia amemjibu nini Prisca, zaidi tu Prisca ndio tulimsikia hapa anasema: "Basi nakuja sasa hivi hapo chini waambie hao watu wanisubiri hapohapo" alisema Prisca na kukata simu. "Kuna watu wawili wanaume wapo hapo chini, wana shidà ya kuonana na mimi" Prisca alisema. "Ni akina nani tena hao?" nilimuuliza kwa sauti ya wasiwasi. "Mmh kusema ukweli hata sijui ndio nataka nishuke hapo chini nikawaone" alisema Prisca. "Lakini dàda Prisca mbona unajiamini hivyo, je kama wakiwa ni watu wabaya?" dereva John aliuliza. "Ndio maana ninataka kuwafuata hapohapo mapokezi nikàwaone, sijataka kuwaelekeza huku juu chumbani tulipo moja kwa moja" Prisca alisema na baada ya hapo akafungua mlango wa chumbani na kutoka akabonyeza vitufe (Bataan) vya lifti na kuteremka nayo chini ya hii Hotel. Humu chumbani nikabakia mimi pamoja na dereva John, wasiwasi ukaanza kunivaa kama vile nguo moyoni mwangu juu ya hao wageni wanaume wawili waliokuja hapa Hotelini ambao Prisca ndio ameenda kuonana nao huko chini. "Isije kuwa hao wageni wenyewe ni wale jamaa Benny pamoja na Eddy kaka yake Prisca?" nilijiuliza mwenyewe moyoni. "Samahani kidogo ndugu yangu naomba nikuulize kitu" dereva John alisema na kunishtua kwenye dimbwi la mawazo. "Hamna shida unaweza tu kuniuliza" nilisema huku nikijiweka sawa kumsikiliza anataka kuniuliza kitu gani. "Ni hivi huyu dada Prisca wewe upoje naye na ni nani wako?" dereva John aliniuliza kwa sauti ndogo ya chini mno. Kwanza nikashusha pumzi halafu na Mimi nikamuuliza swali badala ya kumpa jibu la swali aliloniuliza: "Kwani wewe wakati mnakuja huku Hotelini alikuambia anakuja kwa nani wake?" nilimuuliza dereva John. "Dereva John akacheka kidogo nadhani alicheka kwa sababu ya Mimi kumuuliza swali kabla ya kumjibu yeye lile swali lake aliloniuliza hapo mwanzoni. " Mimi aliniambia anakuja kwa rafiki yake wa kiume ambaye ndie wewe hapo na kesho ndio safari ambayo nawapeleka" alinijibu dereva John. "Basi ndio hivyohivyo alivyokujibu na ndio ukweli upo hivyo" nilisema. "Sikiliza Jose ngoja nikuambie kitu ndugu yangu, jaribu kumuepuka huyu binti Prisca atakuletea matatizo sana na ukinibishia utakuja kunikumbuka" aliniambia dereva John kwa msisitizo japo aliniambia kwa sauti ya chini sana. "Matatizo, ni matatizo gani tena hayo atakayoniletea?" nilimuuliza kwa sauti iliyopagawa. "Najua kama mpo kwenye mahusiano ya kimapenzi, sasa ndugu yangu jaribu kumuepuka huyu binti kabla ajakuletea balaa huko mbele" aliniambia dereva John na kuzidi kuniacha njia panda. Lakini kabla sijaongea kitu chochote Mara gjafla mlango wa humu chumbani ukafunguliwa na Prisca akaingia! Ikabidi tuvunge kwa kupotezea kile tulichokuwa tunaongea Mimi na dereva John japo tayari kilishaanza kunichanganya Akili yangu. "Mmh vipi dada Prisca kwema huko utokapo?" dereva John aliuliza kishambenga. Prisca kwanza akatabasamu na halafu akaniangalia mimi na kusema: "Huko ni kwwma tu ni wageni wangu wa mambo ya biashara ndio waliokuja" Prisca alisema. John akaweza kuamini, lakini mimi kwa upande wangu nilihisi hao wageni sio watu wema! "Sasa kaka John wewe nenda nyumbani kajiandae na upumzike halafu kesho asubuhi mapema uwahi hapa kuja kutuchukua" alisemà Prisca. Basi dereva John ikabidi aage na kuondoka, lakini kabla ajaondoka alipewa kiasi cha pesa na Prisca ambacho Mimi sikuweza kujua ni kiasi gani cha pesa hizo. Prisca akamwambia hiyo Pesa aende akafanyie usafi (Kuosha) hiyo gari ambayo kesho asubuhi ndio tutasafiri nayo na pesa nyingine aende Sheli akajazie mafuta ya kutosha (Full Tank) na pia akampa na Pesa ya matumizi yake  binafsi, dereva John nilimuona akichekelea na kushukuru sana baada ya kuupokea mpunga huo (Pesa) na baada ya hapo akaaga na kuondoka. Wakati yupo mlangoni dereva John aligeuka nyuma na kuniangalia kwa jicho Kali sana lenye ujumbe ndani yake wa kunikumbusha Nisipuuzie kile alichoniambia pale mwanzo! Duuh mbona haya sasa ni majanga tena? Baada ya dereva John kuwa ameshaondoka humu chumbani Prisca akanisogelea hapa kwenye kochi ambapo nimeketi na kutaka kunishika mkono wangu ili aninyanyue na anipeleke kitandani. Lakini mwanaume niligoma! "Baby vipi tena jamani?" aliniuliza kwa sauti laini kama ya kulalamika flani hivi. "Kwanza kabla ya kuendelea kitu chochote hapa, naomba uniambie ukweli kuhusu hao wageni uliotoka kuonana nao ni akina nani?" nilianza kuunguruma. "Sasa baby jamani si taratibu nitakuambia, ujue mwenzio nna hamu na wewe nimekumiss mchana kutwa" aliniambia huku akifungua vifungo vya blauzi yake pamoja na kunilegezea macho. Sikumjali nikanyanyuka zangu kwenye kochi na kwenda kusimama mbali kabisa! "Jamani Jose mpenzi wangu vipi tena, mbona sikuelewi eti?" Prisca aliniuliza huku safari hii akiimalizia kuiondoa kabisa blauzi yake mwilini na kubakia matiti nje hakuvaa sidiria. Mwili ulianza kunisisimuka baada ya kuziona chuchu zake zilizosimama kifuani lakini Mwanaume ilibidi nijikaze na kujifanya kama vile simuoni! "Sikiliza dada Prisca huu sio muda wa mapenzi sasa nataka uniambie kuhusu hao watu wawili uliokutana nao huko chini ni akina nani?" nilizidi kujifanya kuchachamaa. "Hee Jose vipi tena my dear, umeniita Dada na wakati tayari umeshauona mwili wangu au unajifanya umeasahau enhe?" aliniuliuza huku akinisogelea. Nguo aliyobaki nayo kwa chini ni suruali flani hivi ya mpira iliyom'bana sana (Tight ) na kusababisha mzigo wa Hip's alizojaaliwa kuwa nazo niweze kuuona vyema bila ya kusahau na 'Chura' wake huko nyuma! "Hapa Prisca bila ya kuniambia hao watu ni akina nani, usiku wa leo akitafanyika kitu chochote" nilizidi kumpa wakati mgumu Prisca. Nikamuona amesimama ghafla huku akiwa amejishika mikono kiunoni mwake amekasirika na kuniamabia: "Hao watu waliokuja ni Benny pamoja na kaka yangu Eddy, haya sasa unasemaje mpaka hapa?" Prisca alisema na kuniuliza kwa Shari huku akiwa amechukia kwelikweli. Nilishusha pumzi ndefu na mwishoni kwa sauti ndogo iliyopoa nikasema: "Naona wameamua kunifuatilia ili wanipige bastora na kuniua kabisa" nilisema kwa unyonge. Prisca alikuja karibu yangu na kuniambia: "Najua unaogopa sana mpenzi wangu, lakini ngoja nikutoe hofu My love hakuna lolote baya litakalokukuta  ukiwa na Mimi" Prisca aliniambia kwa sauti ndogo ya kutokea puani huku akianza kunipapasa mwilini mwangu. "Sawa je walipajuaje hapa Hotelini, au uliamua kuwaelekeza kuwa umenileta hapa?" nilimuuliza huku nikijaribu kuiondoa mikono yake laini mwilini mwangu. "Nahisi walitufuatilia sisi bila ya kujua wakati tulipokua tunakuja hapa na yule dereva John, lakini nimewaambia nimekuja kupumzika hapa nipo peke yangu hivyo tayari wameshaondoka" Prisca aliniambia. Mawazoni mwangu nilijiona hapa bado nipo hatarini kwa  kuingia kwenye mikono Eddy kaka yake Prisca na Benny asiyekubali matokeo ya  kuwa ndio tayari ameachwa na Prisca. "Usiogope baby wangu nipo tayari kukulinda kwa gharama yeyote ile, na sitakuwa tayari kushuhudia ukipatwa na matatizo" aliniambia Prisca kwa sauti ya 'Mahaba' na hapahapo bila ya kutarajia tayari ameshausogeza mdomo wake mdomoni kwangu tayari kabisa kwa kupata denda. Sijui na mie naye nipoje eti nikajisahau nikajikuta nampa ushirikiano kiurahisi! Tukaanza kunyonyana mate juu juu huku tukipapasana kwenye miili yetu kwa hisia Kali za kimapenzi, mwishowe tukaenda kuangukia kitandani fasta kitendo bila kuchelewa nikaivua ile suruali yake aina ya Tight pamoja na Chupi nami huku akinisaidia kuondoa nguo zangu mwilini. Kuja kutahamaki wote hatuna nguo hata moja kwenye miili yetu! Mimi tena huku 'Gobole' langu ndio tayari nilikuwa nimeshalikoki kabisa kwa kumfyatulia risasi Prisca aliyekuwa yupo hoi bin taabani amezidiwa kimapenzi hapa kitandani akisubiria tu kuadhibiwa, Lakini Mara ghafla tukashtushwa na sauti ya mlango uliokuwa unagongwa kwa Fujo sana. Kwa haraka Mimi na Prisca ikabidi tuachiane kama vile tumepigwa na Shoti  ya Umeme na kubakia tunaangaliana!. 

ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.