STORY: KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 15





Kwa haraka mimi na Prisca ikabidi tuachiane kama vile tumepigwa na Short ya Umeme katika miili yetu tukabakia tunaangaliana kwa hofu hapa kitandani. "Ooh Mungu wangu angalia hawa watu wamekuja sasa kuniuwa kabisa" nilisema kwa sauti ndogo huku mikono yangu yote miwili nikiwa nimejitwika kichwani mwangu sambamba na kulia machozi. Cha kushangaza nikamuona Prisca wala hata hakuwa na wasiwasi! "Sasa baby kama wewe ndio umepagawa kiasi hicho, mimi huku ndio nitakuwaje jamani?" aliniuliza huku akitabasamu. Sikuweza kumjibu kitu chochote nikabaki tu kumuangalia huku machozi bado yakiendelea kunitoka, moyoni mwangu niliona leo ndio mwisho wa maisha yangu umefika kama hiyo hodi inayobishwa hapo mlangoni itakuwa ni ya Benny pamoja na Eddy. Prisca kwa kujiamini kabisa akachukua Taulo lililokuwa kando ya kitanda na kujivisha mwilini mwake halafu akaliendea lile begi dogo ambalo alikuja nalo humu Hotelini na kulifungua. Macho yalinitoka baada ya kumshuhudia Prisca akilifungua begi lake na kutoa bastora ndogo! "Usiogope mpenzi hakuna mjinga yeyote anayeweza kutusumbua hapa" aliniambia Prisca na halafu bila hata ya kupoteza muda akaelekea pale mlangoni kwa mwendo wa taadhari na kuufungua kwa ghafla mlango huo. Kumbe aliyekuwa anagonga mlango alikuwa ni muhudumu wa hapa Hotelini. "Samahani dada ulikuwa umeisahau simu yako wakati ulipokuja kuonana na wale wageni wako pale mapokezi" alijieleza kwa kirefu muhudumu huyo baada ya kumuona Prisca akiwa na ile bastora mikononi mwake. "Sasa mbona aukupiga simu ya humu mezani kunijulisha?" Prisca alimuuliza yule muhudumu huku akiipokea simu yake. "Niliona tu ni bora nikuletee, lakini samahani kama nitakuwa nimefanya makosa kuileta bila taharifa" alisema muhudumu huyo. Baada ya hapo Prisca akaufunga tena mlango wa chumbani Mara baada ya yule muhudumu kuwa tayari ameshaondoka zake na kurudi chini kuendelea na majukumu. "Dooh kumbe niliisahau simu mapokezi wakati nilipoenda kuonana na wakina Benny na kaka Eddy" alinifahamisha Prisca. Hapo sasa kidogo nikajiona angalau nina afadhali, maana nilijua ndio tayari 'Kishanuka' kama wanavyosema watoto wa mjini. Prisca akairudisha ile bastora yake mle kwenye begi alipoitoa na pia simu yake akaiweka mezani. "Kumbe unamiliki silaha na wewe?" nilimuuliza huku nikijilaza kitandani. "Yeah ndio ninaimiliki kwani huwezi kujua balaa linaweza kukutokea kwa muda gani natembea nayo kwa usalama zaidi" alisema Prisca na halafu akalivua lile Taulo na kuliweka kando halafu akaja tena kupanda kitandani, "Usihofu mpenzi wangu sasa mambo yote yapo shwari nipe raha ile tuliyoikatisha" aliniambia Prisca huku akishika 'Gobole' langu liliokuwa limelala Doro baada ya kukatishwa 'Stimu' na kule kugongwa kwa mlango hapo mwanzo. Fasta 'Gobole' langu likaweza kupata tena Chaji baada ya kushikwashikwa na mikono laini ya Prisca, yaani kitendo bila kuchelewa nikamkunja na kum'binua Prisca hapa kitandani na kuanza kumpelekea moto Mkali wa mapenzi na kumuacha akijinyonganyonga huku akilalamika kwa Mahaba! Baada ya kuhakikisha tayari tumeshakata kiu zetu za kimwili kwa mapenzi motomoto tukajinyanyua kitandani kwa uchovu mwingi na kuingia bafuni kwenda kuoga. Huko napo kama kawaida tukafanya michezo yetu ya kimalavidavi huku tukiogeshana pamoja na kusuguana kwa raha zetu. Hatimaye tukatoka bafuni na kurudi tena chumbani huku miili yetu sasa ikiwa ipo safi kabisa! Baada ya hapo tukavaa vizuri nguo zetu za usiku kwa ajili ya kulalia na Prisca akaweza kuagizia chakula hukuhuku chumbani atukutaka kushuka chini kwa kuhofia labda Benny na Eddy  wanaweza kuwa wanatutegea ili watuone kama tupo pamoja. Kwa kuwa muda nao ulikuwa umeenda sana baada ya kumaliza kula chakula cha usiku na vinywaji kidogo tukaamua kupanda kitandani na kulala.
*************
Asubuhi na mapema mimi ndio nilikuwa wa kwanza kuamka hapa kitandani. Nikamuangalia Prisca nikamuona bado amelala hana hata habari nadhani ni kwa sababu ya ile shughuli pevu ya kimapenzi tuliyoifanya usiku wa Jana yake. Nikataka nimuamshe kwa kumtingisha lakini moyo wangu ulisita baada ya kuuona mwili wake karibia wote upo wazi huku shuka tulilolitumia kwa ajili ya kujifunika wakati tunalala likiwa lipo pembeni, mwili wangu nao ukaanza kupatwa na hisia Kali za kimapenzi baada ya kuuona mwili wa mrembo Prisca kama vile unaniita! "Hapana leo ndio safari sio vyema kufanya haya mambo itakuwa ni sawa na kujitia nuksi safarini" nilijisemea moyoni na kuzipuuzia kabisa hisia zangu hizo ambazo zilitaka kunitawala asubuhi hii. Nilichokifanya tu nikamfinya kwenye chuchu za matiti yake ili apate kuamka! "Bwana Jose nini huko mbona unakuwa mgomvi unanifinya" alilalama Prisca. "Tayari kumekucha hebu amka tujiandae" nilisema. Kweli Prisca akaamka na baada ya kusalimiana tukaingia tena bafuni kwa ajili ya kupiga mswaki pamoja na kuoga kabisa na halafu tukarudi chumbani na kuvaa vizuri nguo zetu kwa ajili sasa ya safari ya kuelekea Morogoro kwenda kumuona bibi yangu huko kijijini. Mara simu ya Prisca ikaanza kuita! Akaangalia anaepiga akagundua ni yule dereva John. Baada ya Prisca kuipokea simu yake akajulishwa na dereva huyo kuwa yeye (John) tayari ameshawasili hapa maeneo ya Hotelini na yupo kwenye sehemu ya Parking (Maegesho) anatusubiri ndani ya gari, "Ok John tunaomba utupe dakika kumi tutakuwa tumeshashuka hapo chini" alisema Prisca na kukata simu. "Baby sasa twende zetu, John anatusubiri huko nje kuhusu mambo ya chai tutakunywa hukohuko juu kwa juu" aliniambia Prisca. "Mimi nipo tayari ni wewe ndio unaepoteza muda na huko kujipodoa kwako" nilimuambia kwa kumtania. Prisca akacheka na halafu tukachukua mabegi yetu na kutoka humu chumbani tulipofika kwenye korido ya hii Hoteli tukaingia ndani ya Lifti na kuanza kuteremka kwenda chini. Lifti hiyo moja kwa moja ikatufikisha mpaka pale sehemu ya mapokezi ambapo baada ya kusalimiana na muhudumu wa hapo Prisca akakabidhi funguo ya chumba na halafu tukaanza kutoka ndani ya jengo la hii Hoteli, baada ya kufika nje kabisa tukaanza kuelekea sehemu ya Maegesho ya magari ambapo dereva John ndipo alipokuwa anatusubiri sisi. Kwa asubuhi hii hapa kwenye mazingira ya Hotelini hakukuwa na purukushani ya aina yeyote zaidi ni magari tu ya wateja yaliyokuwa yameegeshwa kwa mpangilio sehemu maalumu ya Maegesho huku wenyewe wakiwa bado wamelala ndani ya Hoteli, Nikiwa nimeshikana mikono na Prisca tukitembea kuifuata gari sehemu ilipo. "Huyu John naye sasa ndio nini, gari kaja kuipaki huku mbali kote yaani mpaka atusumbue kuifuata!" Prisca alilalamika. "Lakini ajafanya vibaya usimlaumu sana, si kama hivi kidogo tunafanya mazoezi ya kutembea" nilisema huku nikitabasamu. Mara ghafla ikatokea gari aina ya SUBARU (FORESTER) ya rangi nyekundu nyuma yetu ikija kwa kasi kubwa sana! Kwa mshtuko tulioupata tukajikuta mimi na Prisca tunaachiana mikono ambayo tulikuwa tumeshikana. Gari hiyo ilipotufikia ikafunga break Kali sana na kusimama halafu milango ya nyuma ikafunguliwa na Njemba zipatazo Tatu (Baunsa) wenye maumbo makubwa kama ya wale wapiganaji wa Mieleka wakaja kunikamata mimi! "Jamani kwani vipi nimefanya nini?" nilijaribu kuwauliza. "Tulia wewe Kenge maji, ngoja ukaonyeshwe show huku na vidume" aliniambia njemba mmoja wapo kwa sauti nzito huku akinibeba juu juu kama vile kiroba cha mahindi na kunipeleka kwenye ile gari yao. Prisca akukubali kuona hiki kitendo kinachofanyika akalitupa chini begi alilokuwa amelibeba na kutukimbilia! "Nyie washenzi mnampeleka wapi mpenzi wangu?" Prisca aliwauliza kwa sauti hawa majamaa huku akiwakimbilia. Lakini alipowafikia hawà jamaa wawili wa nyuma wakamsukumiza chini kwa nguvu na Prisca akaweza kudondondoka, kwa upande wangu tayari nilishafikiswa mpaka kwenye hiyo gari ya hawa 'Wakora' na kuingizwa ndani yake kwa ulazima! "Jamani kama nimewakosea basi naombeni mnisamehe" nilibembeleza. Lakini hakuna aliyenijibu kitu chochote wakanipokonya begi langu na kulitupa nje ya gari. "Oyaa masela fasta basi huyo demu tuachane naye, mkuu katuagiza tumchukue huyu Ngedere wa kiume tu" alisema jamaa mmoja niliyemkuta ndani ya gari na kwa haraka hawa majamaa wengine nao wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea sehemu isiyojulikana ikaanza huku gari hiyo ikiondoka kwa mwendo wa kasi sana kutokea kwenye Geti kubwa la hii Hoteli, Kwa mbali nikaweza kumuona Prisca pale sehemu alipodondokea akilia kwa uchungu sana na inaelekea pia atakuwa ameumia. Mimi humu ndani ya hii gari ya hawa majamaa nisiowajua nilikuwa nimedhibitiwa ile kisawasawa sikupata hata nafasi ya kuweza kufurukuta niliwekwa MTU kati huku kwenye siti ya nyuma kabisa, Kicwani kwangu nilibakia na maswali mengi sana ya kujiuliza juu ya hawa 'Mabaunsa' walioniteka mimi nilijiuliza ni nani huyo aliyewatuma waje kuniteka au watakuwa ni Benny pamoja Eddy ndio wahusika wakuu wa hili tukio langu. Gari hili la watekaji lilipotoka nje kabisa ya eneo la Hotelini liliweza kuingia mpaka kwenye barabara kuu ya Lami na kuanza kutokomea kwa kasi kubwa sana huku na mimi nikiwemo nimetekwa ndani yake!.
 
ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.