STORY: KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 17




******************
ILIPOISHIA.
Kitendo cha kumuona Benny na Eddy nikajua hapa tayari kumeshakuchaa!.

👉👉ENDELEA NAYO SASA👇👇
Baada ya wote kuwa  wameingia humu ndani chumbani mlango ukafungwa kwa ndani na ufunguo. Benny akasimama na kujishika kiuno chake kwa mikono yake yote miwili akionekana kama vile aamini kuwa ni mimi hapa ndie anaeniona mbele yake! "Si unajifanya wewe ni kidume sana sasa mbona umekamatwa kiurahisi?" Benny aliniuliza kwa kebehi na kuanza kunifuata hapa kwenye kiti nilipofungwa. Kundi lile la wale mabaunsa watatu pamoja na Eddy na yule daktari wa kichina nao wakamfuata Benny kwa nyuma kuja hapa sehemu nilipo. "Kwa hakika wewe mpuuzi siku hii ya leo hapa utapata taabu sana" Benny aliniambia kwa dharau. Mimi nilibakia tu kimya kama vile kuku aliyenyeshewa na mvua. Halafu Eddy kaka yake Prisca akanifuata na kunishika kidevu akaunyanyua juu USO wangu na kuwa kama tunaangaliana hivi. "Yaani itakuwa ni kichekesho duniani pote  kama wewe msenge ndio utakuwa ni Shemeji yangu, Ptuuuu" alisema Eddy na kunitemea mate usoni kwangu. Watu wote waliokuwemo humu chumbani wakaanza kucheka kuonyesha kuwa wamefurahishwa na hiki kitendo cha Eddy kunitemea mate mimi. "Yaani wewe ni Kapuku tu, hauna hadhi ya kummiliki dada yangu Prisca na nina wasiwasi wewe utàkuwa umemroga ili akupende" Eddy alizidi tu kunichambua kama vile karanga. "Aisee Eddy mbona unauweka usiku? huyu sio wa kumchelewesha" alisema Benny na kunisogelea halafu akaanza kunipiga  ngumi za mfululuzo usoni na kupelekea nione maruweruwe pamoja na maumivu makali yasiyoelezeka. Nilianza kulia machozi kama vile mtoto mdogo! "Mwanaume Rijali siku zote huwezi kuliona chozi lake hadharani, sasa wewe mbona unalia na wakati unajifanya Rijali kwa Prisca?" Benny aliniuliza huku akitabasamu. Halafu akaendelea tena kuniambia: "Ok hebu tuachane na hilo jàmbo, unajua tuna mambo mengi ya kufanya hivyo tumekujà hàpa kwa sababu yako wewe tu unamuonà hapa huyu dokta wa kichina?" aliniuliza Benny huku akimgusa begani mchina huyo aliyekuwa anatabasamu kwa mtindo wa kukenua meno yake kama vile Ngiri wa porini. Mimi sikumjibu kitu chochote niliendelea kuyasikilizia maumivu ya zile ngumi zake za dabodabo alizonipiga usoni Benny. "Hata ukinyamaza najua kuwa unasikia, huyu anaitwa Dokta Lee Chen yupo hapa kwa kazi moja tu kwako ya kukutibia endapo kama tutaelewana" aliniambia Benny. Hapo nikajikuta namuangalia usoni Benny kama vile kumsoma ili nipate kujua ni kuelewana juu ya kitu gani. "Aaah aaah najua una hamu ya kutaka kujua ni maelewano gani ambayo nimemaanisha, sasa ni hivi bila ya hata ya kupepesa macho nataka ukubaliane na moja kati ya haya mawili nitayokuambia" Benny aliniambia kwa utulivu, na halafu akaendelea tena kuongea: "Hapa nataka uchague kufa kwa maumivu makali ya kipigo utakachokipata, au tuukate huo Uume wako unaokupa Jeuri ya kutomba mademu wa watu na baada ya kuukata Dokta Lee Chen atakutibia na kukushona vizuri halafu sisi tutakuachia urudi kwa Prisca wako mkaendelee na mapenzi yenu" Benny aliniambia bila hata ya aibu. Duuh kwangu huu ulikuwa ni zaidi ya mtihani, hivi kuna maana gani tena ya kuishi hapa duniani kama kile kitu kinachokupa Heshima kitaondolewa? Japo sikuwa na fedha ya kunifanya niheshimike na watu lakini Heshima yangu pekee ninayoringia ni hili 'Gobole' langu lililomsurubu Prisca mpaka akatoa machozi ya Utamu kitandani. Eti leo hii hawa mafirauni walikate hapa huo si utakuwa ni uwendawazimu endapo kama nitakubali? Jibu rahisi hapa la kumpa huyu mshenzi Benny pamoja na hawa watu wake ni kwamba waniue tu! "Nimekubali kufa muheshimiwa, naombeni mniue haraka sana sitaki kufedheeshwa na ulimwengu" nilisema kwa uchungu huku nikilia machozi. Benny àkamgeukia Eddy huku akitabasamu na kumwambia: "Umekiona kidume hiki? Kimeamua kufa na utamu wake eti" alisema Benny kwa dharau. Eddy akaishia tu kucheka! Benny akanigeukia tena mimi na kuniambia: "Kwa jinsi nilivyokuchukia wewe nadhani hiyo ndio adhabu sahihi ninayostahili kukupa, nataka nikutie aibu ya kukufeedhesha halafu nione kama huyo Prisca atakupenda tena kamwe sitaki kukuua" Benny aliniambia huku akimaanisha hicho anachokisema. "Lakini muheshimiwa mimi kosa langu ni lipi mpaka unipe adhabu kubwa kiasi hicho? Prisca mwenyewe ndie aliyeanza kunipenda" nilijitutumua na kusema hivyo. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana! Benny alikunjuka na Teke Kali la ghafla lililonipata vyema kifuani kwangu na kupelekea hiki kiti nilichofungiwa nacho na minyororo kubinuka kwa nyuma, na kwa Bahati mbaya nilifikia kujipigiza kichwa changu ukutani na kuumia vibaya sana sehemu ya nyuma kwenye kisogo. "Yaani wewe mpumbavu unadiriki kweli kunitambia hapa mbele yangu, eti Prisca ndie amekupenda!?" Benny alibwata kwa hasira. Kwa haraka wale mabaunsa wakaja na kukinyanyua tena hiki kiti na kukiweka vizuri. Maumivu makali niliyokuwa nikiyasikia kichwani kwa muda huu yalifanya niichukie dunia ghafla na kutamani hata Mtoa Roho angekuja kuitoa Roho yangu, dunia yote niliiona mbaya nililia sana kwa uchungu! Lakini hakukuwa na MTU wa kunihurumia. "Mvueni hicho kibukta haraka sana, Dokta Lee Chen apate kufanya kazi yake" Benny aliwaagiza wale mabaunsa waje kunivua Mimi hii boksa niliyobakia nayo mwilini, bila ya kupoteza muda Njemba zikaja na kuanza kunivua boksa yangu kwa haraka. Sikuwa na nguvu ya kuwazuia kwani ndio hivyo tena nilikuwa nimeshalegea na kipigo pia ukizingatia kiti cha chuma nilichofungwa na minyororo nacho kiliweza kunidhibiti! Baada ya muda mfupi nilikuwa mtupu kabisa (Uchi) na 'Gobole' langu lenye kunipa heshima yangu ya kuwa Mwanaume Rijali liliweza kuonekana Live bila chenga, Benny na Eddy wakajikuta wanaangaliana nadhañi walikuwa wanashangaa jinsi Mungu alivyonibariki kuwa na 'Gobole' kubwa la kumridhisha mwanamke yeyote mwenye kiu ya kuhitaji kutimiziwa kiu yake ya  Kimapenzi. Benny nilimuona akiliangalia 'Gobole' langu kwa macho ya wivu sana na kutamani kama vile yeye ndie àngekuwa analimiliki. Nikakumbuka Prisca aliwahi kuniambia kuwa Benny ana 'Kibamia' ajawahi kumridhisha kimapenzi hata siku moja kitandani! Sasa kwa Style hiyo kwanini Benny asinionee wivu? Benny akaanza kuongea na huyu Daktari wa kichina kwa kutumia lugha ya Kiingereza ambayo Mimi hapa (Jose) sikuwa naifahamu kabisa, halafu baada ya hapo Dokta Lee Chen akavaa (Gloves) mikononi mwake na kuchukua vifaa vyake vya kazi ambavyo ni Kisu kidogo kilichoonekana ni kikali sana na Mkasi pamoja na lundo la Pamba nadhani ya kukaushia damu bila ya kusahau na Sindano niliyohisi ni ya Ganzi. Dokta huyo  akaanza kunisogelea huku akiwa anatabasamu tayari kabisa kwa kuja kulisambalitisha 'Gobole' langu, wale mabaunsa watatu wakaanza kunidhibiti vizuri ili nisilete Purukushani. Benny na Eddy wao walikaa pembeni kushuhudia Mchezo utakavyokuwa huku wakiwa wananicheka na kuona wananikomoa. Sikutaka kuamini macho yangu kama ndio kweli hawa washenzi wameamua kunitenganisha na hiki kiungo changu muhimu kwenye huu mwili wangu! Chozi la uchungu bado liliendelea kunitiririka!.

ITAENDELEA ....







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.