STORY: 💕KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 18




******************
ILIPOISHIA.
Sikutaka kuamini macho yangu kama ndio kweli hawa washenzi wameamua kunitenganisha na hiki kiungo changu muhimu kwenye huu mwili wangu! Chozi la uchungu bado liliendelea kunitiririka!.

👉👉 ENDELEA NAYO SASA 👇👇
Sikujua msaada wangu nitaupata wapi katika eneo hili la watu wabaya ambao wameamua kunifanyia ubaya mkubwa kupitiliza. "Jamani naombeni mnisamehe sitorudia tena kuwa na yule binti kwenye mahusiano" nilijaribu kubembeleza huku nikilia machozi. Lakini hakuna aliyenijali zaidi ni sauti tu za vicheko vya kebehi ndio walivyokuwa wakinicheka, nilimuona Benny akicheka sana mpaka akafikia hatua ya kugongeshana viganja vya mikono yake na Eddy ambaye naye pia alikuwa anacheka kuonyesha suala la mimi kukatwa hili 'Gobole' langu ndio limewafurahisha sana. Mabaunsa nao  wakazidi kunidhibiti kwa nguvu huku wakinipanua miguu yangu ili kumpa nafasi nzuri huyu Daktari wa kichina apate kunifanyia huo ukatili kwa urahisi, kama kawaida yake mchina huyu bado aliendelea kutabasamu na lile tabasamu lake la kukenua meno yake kama vile Ngiri wa porini. Sikuwa na jinsi tena ya kufanya zaidi tu ya kukubali matokeo na kusubiri hicho wanachotaka kunifanyia kipate kutendeka. Nilifumba macho yangu sikutaka kushuhudia kabisa hili tukio la kikatili, Daktari huyu wa kichina kwanza kabla hata ajaanza hiyo shughuli ya kulifyeka 'Gobole' langu akaingiza mkono wake kwenye mfuko wake wa koti lake jeupe la kidaktari na kutoa kichupa kidogo cha dawa aina ya (Spirit) ile ya kukaushia damu kwenye jeraha au ya kukaushia vidonda na halafu akachukua donge la pamba na kuichovya kwenye hiyo dawa (Spirit) pamba ilivyolowana vya kutosha akaja na kulishika 'Gobole' langu (Uume) na kuanza kuipaka dawa hiyo. Taratibu nikaanza kusikia muwasho wa hiyo dawa kwenye maeneo yangu haya Nyeti ya uzazi, kwani kama unavyojua Spirit jinsi inavyowasha au kuchachawa pindi inapogusa kwenye ngozi, "Eeeh Mungu baba ninusuru mimi mja wako na mtihani huu mzito, sina msaada mwingine ninaoutegemea zaidi yako baba yangu uliyeumba mbingu na ardhi" nilijikuta nikimuomba Mungu kimoyomoyo huku nikiwa nimefumba macho nikisubiria Kisu cha daktari wa kichina kipate kufanya kazi yake. Mara ghafla bila ya kutarajia tukasikia mlango wa humu chumbani ukigongwa kwa nguvu sana na kupelekea wote tupate kushtuka sana! "Wewe ni mpumbavuu gani unayegonga mlango kwa fujo kiasi hichoo?" Benny aliuliza kwa hasira. Sauti iliyokuwa kwa nje kwenye korido ikasikika ikimjibu: "Boss ni mimi hapa Samson, nimekuletea simu yako kukujulisha kuwa mzigo umekamatwa bandarini" ilisema sauti ya mtu huyo. Kwa haraka sana nikamsikia Benny akimzuia Daktari huyu wa kichina kuendelea na hii kazi ya kuukata Uume wangu. Hapo sasa ikabidi hata hawa mabaunsa waliokuwa wamenidhibiti nao waweze kuniachilia na mimi nikajikuta nafumbua macho yangu. Nikamuoña Benny akienda kuufungua mlango ule yeye mwenyewe na baada ya hapo akaingia Mwanaume mmoja mrefu sana na aliyejazia mwili wake kwa mazoezi. "Enhe Samson hebu niambie kwanza nini kimetokea huko?" aliuliza Benny kwa pupa mara baada ya huyu jamaa anayeitwa Samson kuingia humu chumbani. "Boss mzigo wote wa madawa ya kulevya umekamatwa wakati ndio tunatoka eneo la bandari" alisema huyo Samson. Benny akacharuka sana akaanza kufoka kwa hasira! "Inakuaje mkamatwe kizembe na wakati pesa nimewapeni ya kuondoa nuksi yeyote?" Benny alihoji. Samson alionekana kunywea na halafu kwa sauti ndogo akasema: "Boss pesa uliyotupatia kama Rushwa ya kuwahonga maaskari wameikataa na mzigo wote wameushikilia, baada ya taflani kutokea tukaamua kuutelekeza mzigo" alisema Samson. Benny akakasirika zaidi mpaka akamzaba kibao Samson! "Pumbavuuu sana mnawezaje kuuacha mzigo mkubwa na wa thamani kama ule!?" Benny alichachamaa. Wakati Benny huko akiendelea kubwatuka ovyo kama vile amekunywa maji ya chooni, mimi huku kwa upande wangu nilikuwa nasubiria wamalize hayo malumbano yao halafu lile zoezi la kulisambalatisha 'Gobole' langu liendelee tena kama kawaida kwani ndio vile tena Daktari wa kichina (Lee Cheñ) alikuwa ameshika sindano ya Ganzi pamoja na kile Kisu kidogo mkononi mwake, Eddy akamshauri Benny ni vyema wangeenda hukohuko bandarini kuukomboa huo mzigo wao wa madawa ya kulevya uliokamatwa. "Sawa tunaweza kwenda, je vipi kuhusu huyu Kikaragosi?" Benny alimuuliza Eddy huku akinigeukia mimi na kuniangalia kwa hasira sana. "Kuhusu huyu mpuuzi wala usijali, kwani tayari yupo kwenye mikono yetu muda wowote tunaweza kumshughulikia" Eddy alisema huku akitabasamu. Basi baada ya hapo Benny akaanza kuongea na yule Daktari wa kichina kwa lugha ya kiingereza japo sikuweza kujua walichokuwa wanaongea kwa sababu ya mimi kutokuijua lugha hiyo, lakini nilihisi Benny alimwambia kwanza wasitishe hili zoezi la kuufyeka kabisa huu Uume wangu na badala yake walishughulikie kwanza hili jambo la hayo madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko bandarini. Nikamuona Daktari huyu akikusanya vile vitendea kazi vyake alivyokuwa tayari ameviandaa kwa ajili ya kunifanyia Ukatili ule na kuvirudisha kwenye mkebe wake maalumu, pia Benny akamuagiza yule Samson adumishe ulinzi hapa kwa kunilinda mimi mpaka wao watakaporudi na halafu wataendelea na lile zoezi tena. "Usifikiri ndio umenusurika wewe mpumbavu, adhabu yako bado ipo palepale ni lazima tuuondoe huo Uanaume wako unaokupa jeuri" Benny aliniambia na halafu wote kwa pamoja wakatoka na kuniacha humu chumbani peke yangu nikiwa nimefungwa vilevile kwenye hiki kiti na minyororo huku nikiwa sina nguo hata moja mwilini mwangu. Sikuamini kabisa kama nimenusurika na na ule ukatili japo nilijua hiyo baadae wakirudi wataendelea tena na ufedhuli wao lakini kwa muda huu nilijiona ni mwenye afadhali angalau. "Mungu baba endelea kunionyesha muujiza wa kuokoka sehemu hii ya hatari usiniache niangamie peke yangu nishike mkono ewe Mungu wangu" nilijisemea kwa kusali huku nikimuomba Mungu kwa sauti ndogo ya moyoni. Niliajiapiza kwa dhati endapo kama nitafanikiwa kutoka salama sehemu hii basi huyo Prisca sitatamani hata nimuone katika maisha yangu yote hapa duniani, kwani yeye ndie chanzo cha haya Majanga yanayonikuta hivi sasa kwa kuleta mambo ya Mapenzi na kusababisha matatizo kwa upande wangu. Pia nikamkumbuka dereva John jinsi alivyoniambia nimuepuke Prisca Jana usiku kule Hotelini, kwani angeniletea matatizo na hatimaye matatizo yenyewe ndio haya sasa, nikaukumbuka ule usemi wa wahenga kuwa: LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO BASI LAJA Duuh kwangu ndio hivyo limekuja tena mapema sana. Nilikaa kwa kipindi kirefu humu chumbani pasipo na kutokea mtu yeyote wa kuja hata kuniangalia niliendelea kubakia kwenye hiki kiti huku minyororo niliyofungwa ikiniumiza sehemu za mikononi na miguuni, Njaa Kali pamoja na Kiu ya maji vilianza kunisumbua lakini hata hiyo hamu yenyewe ya kula sikuwa nayo kabisa nilikuwa nasubiria hatima yangu kutoka kwa Benny pamoja na Eddy warudi kutoka huko walipoenda ili watimize ule Unyama wao waliopanga kunifanyia na yule Daktari wao wa kichina. Niliendelea kuwasubiri huku nikiendelea kumuomba Mungu wangu.
*************
Kwenye majira niliyoyahisi ni ya jioni sana hatimaye mlango wa humu chumbani nikaona unafunguliwa na yule jamaa Samson aliyekabidhiwa jukumu la ulinzi akàingia akiwa yupo peke yake huku akitabasamu. Mimi nilibakia tu namuangalia. "Aloo my friend nimekuja kukuangalia, vipi  unaendeleaje?" aliniuliza huku akiufunga mlango kwa ndani. Sikumjibu kitu nilinyamaza kimya! "Hata ukininyamazia lakini naomba utambue mimi ndio msaada wako mwenye uwezo wa kukuokoa hapa" aliniambia Samson. Sikumulewa anamaanisha nini nilijua labda ananikejeli tu, akaanza kunisogelea na kunifungua hii minyororo niliyofungwa hapa kwenye kiti na baada ya kunifungua kabisa akanipa nguo zangu na kuniambia: "Naomba uvae nguo zako ndugu yangu, sio kila mtu ni m'baya kwako wengine sisi tunajua nini maana ya ubinadamu" aliniambia Samson huku akiliangalia sana 'Gobole' langu na kutabasamu halafu akaniambia: "Aisee watu wana roho mbaya sana, yaani wanataka wakuondolee huo Utamu wako hivihivi!" alisema. Mimi sikuweza kusema kitu chochote niliendelea tu na kuvaa nguo zangu! Baada ya kumaliza kuvaa Samson akaniambia nimfuate, nami nikamfuata japo sikujua anataka kunipeleka wapi lakini niliona bora tu nimfuate hivyohivyo, tukatoka mle chumbani na kutokezea mpaka kwenye ile korido Samson alikuwa yupo mbele yangu nami nikimfuata nyuma yake kwa upande wa sebuleni zilisikika sauti za wale mabaunsa wengine inaonyesha walikuwa wanacheza Kamari pamoja na kuvuta Bange. Samson akafungua mlango wa chumba kingine na kuniambia niingie humo ndani, nikajikuta moyo wangu unasita kuingia kwenye hicho chumba. "Nimekuambia mimi ndio msaada wako, sasa mbona auniamini na unaniogopa enhe?" aliniuliza Samson huku akiwa amekunja sura yake. Nikashusha pumzi ndefu na mimi pia nikamuuliza: "Sawa ninaweza kukuamini, je vipi kuhusu Benny pamoja Eddy?" nilimuuliza. Samson kwanza akacheka sana na baada ya kumaliza kucheka akaniambia hivi: "Ingia kwanza huko chumbani, halafu nitakuambia kila kitu kuhusu Benny na huyo Eddy" aliniambia. Basi sikuwa na jinsi ikabidi niingie kwenye hicho chumba ambacho kwa ndani kilikuwa ni kizuri sana chenye kila kitu cha thamani, nikaenda kuketi kwenye Kochi dogo nililolikuta humu ndani chumbani. "Najua ndugu yangu una njaa sana, tangu ulivyotekwa asubuhi haujakula kitu chocgote mpaka sasa hivi, subiri kidogo nikakuletee chakula na kinywaji halafu ndio tuongee vizuri" aliniambia Samson na kunikonyeza halafu akatoka chumbani kwa mwendo  wa haraka sana na kuniacha mimi nikiwa nimeduwaa nisijue kitu chochote kinachoendelea humu  ndani. Baada ya muda Samson akarudi akiwa amebeba chakula kwenye Hotpot pamoja na sahani ndogo yenye vijiko, akuja peke yake pia alikuja na Baunsa mwingine aliyejazia vyema mwili wake. Njemba huyo naye alibeba Jagi lenye Juisi na Glass Samson na huyo jamaa  waliniangalia na kuishia kutabasamu halafu wakaenda kuweka vile vitu walivyokuja navyo juu ya meza ndogo na baada ya hapo wakaanza kunifuata hapa kwenye hili Kochi sehemu nilipokuwa nimeketi mimi humu ndani!.

ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.