STORY: 💕KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 19




*******************
ILIPOISHIA.
"Oyaa  wee boya chagua moja basi kama umekubali tukugueze ili utoroke au utasubiri Benny arudi aje kuukata huo Uume wako?" sauti ya yule jamaa mwingine ilinishtua kwenye mawazo!.

👇ENDELEA NAYO👇
Kwa upande wangu niliona huu sasa nao ni mtihani mwingine mgumu sana mbele yangu. "Jamani kusema ukweli wangu hilo jambo siwezi kulikubali" nilisema. "Unasemaje wewe, yaani unawezaje kukataa kitu ambacho sisi tayari tumeshakipanga? " yule Jamaa ambaye jina lake sikuweza kulijua aliniuliza huku akinikazia macho yake. Nikaona hapa nikileta unyolinyoli na kutia huruma hawa washenzi watanifanyia kweli huo mchezo m'baya, hapa dawa yao ni kukomaa kiume liwalo na liwe nikajiweka sawa na kuwaambia: "Kwanza mimi tayari nilishachagua kifo mbele ya huyo Benny wenu, sasa mnapotaka kuniletea hayo masharti yenu ya kipuuzi mimi nashindwa kuwaelewa naombeni mniache kama ni kufa au kukatwa Uume tayari nilishajitolea lakini huo mchezo ambao mnataka kunifanyia kiukweli sipo tayari" nilijitutumua na kusema hivyo. Samson na yule jamaa wakaangaliana na halafu wakacheka sana  Samson akaniambia: "Hapa hata iweje ni lazima tutakula huo mzigo wako, maana hapa tulipo tuna ugumu sio mchezo kwa muda sasa hatujaona uchi upoje" Samson alisema huku akifungua suluari yake na kulitoa nje 'Gobole' lake lililokuwa tayari limedinda ile kiroho mbaya. Mpaka kufikia hapa nikaona sasa ngoja nijitetee nikapiga mahesabu ya harakaharaka nikaona lile Hotpot la chakula walichoniletea ili nipate kula lipo pale mezani pamoja na jagi la juisi na Glass zake. Kwa kasi ya umeme nikanyanyuka kwenye kochi nilipokuwa nimeketi na kwenda kulichukua lile Hotpot halafu  nikampiga nalo usoni Samason mpaka chakula chote kikamwagika chini. Hilo  lilikuwa ni pigo la ghafla ambalo hakuna aliyelitegemea. Yule jamaa mwingine akiwa bado ameduwaa asiamini kile kitendo nilichokifanya naye nikamtandika na lile jagi la juisi kichwani mwake. "Mamaa weeee nakufaaaa" jamaa alipiga yowe la maumivu. Samson alikuwa bado yupo chini anaugulia maumivu usoni. Sasa nikajikuta nimepata mzuka wa kuendelea kupambana na hawa watu japo sikuwa na silaha za maana. "Washenzi nyie kama mnaona hicho kitendo ni kizuri jigeuzeni wenyewe, kwani na nyinyi pia si mna matako?" niliwauliza kwa hasira. Jagi lile juisi nililompiga nalo yule jamaa lilikuwa ni la udongo hivyo lilipasuka na juisi yote ikamwagika chini na kwa Bahati nzuri niliweza kumjeruhi kichwani kwani alichanika mpaka na damu ilikuwa inamtoka. "Aisee sikubali yaani wewe unathubutu vipi kupambana na sisi?" alisema yule jamaa huku akinifuata kwa kasi. Kabla hata ajanifikia tayari nilikuwa na Glass mkononi mwangu hivyo nayo nikamtupia lengo kumpiga nayo usoni. Akafanikiwa kuikwepa na kunicheka kwa dharau. "Wewe hata uangaike vipi hapa leo ni lazima hayo matako yako utatoa, na Dudu tutakushindilia" aliniambia kwa kunitambia huku akizidi kunisogelea. Nikaona sasa nimekwama kwani sikuwa naona tena silaha ya kuwapiga nayo hawa washenzi ili nizidi kujitetea. Mara ghafla kwa upande wa nje ikaanza kusikika milio ya risasi. Samson na yule jamaa wakashtuka sana hata na mimi pia niliweza kushtuka. "Oyaa Samson ni akina nani hao huko nje?" yule jamaa alimuuliza Samson. "Wee fala nini! sasa unaniuliza mimi hao wakina nani na wakati wote sisi  tupo ndani, sasa nitajuaje?" Samson alisema kwa hasira. Milio ya risasi ilizidi kurindima huko nje na kusababisha hawa jamaa wanisahau mimi kwa muda. "Oyaa Samson huko nje sio poa kabisa, hebu twende kwanza tukaangalie" alisema yule jamaa na bila ya kupoteza muda wakatoka mbio kuelekea huko nje. Ndani nikabakia peke yangu humu chumbani, nikafikiria nitoke nje kwani hawa jamaa walivyotoka walisahau kunifungia mlango nadhani hiyo milio ya risasi iliwachanganya. Nikaweza kuhisi labda hao watakuwa ni Polisi ndio wamewavamia hawa jamaa hapa kwenye hili jumba lao. Nikaona ngoja nibakie humuhumu chumbani nisitoke nje maana Polisi wanaweza kuhisi labda na mimi ni mmoja wa hawa Magaidi halafu wakanishambulia kwa risasi, nilichokifanya nikaingia uvunguni mwa kitanda na kujificha kimyaa. Baada ya nusu SAA hali ya utulivu iliweza kurejea tena lakini huko nje na mpaka humu ndani ya hili jumba kulikuwa kumepoa kabisa, sikuweza kujua kwenye hilo pambano ni upande gani ambao ulishinda kama ni Polisi au hawa Magaidi walioniteka, nikiwa bado nipo chini ya uvungu wa kitanda natafakari Mara ghafla nikasikia sauti za vishindo vya viatu vikitembea kwenye ile korido ya hili jumba na vishindo hivyo vilikuwa vinakuja huku kwenye hiki chumba nilichokuwemo mimi. "Ooho Mungu wangu, naomba hao watu wanaokuja wawe ni watu wema kwangu" nilijisemea kwa sauti ya taratibu huku nikitetemeka. "Yuko wapi huyoo kijana mliyemteka, mmeficha wapi?" niliweza kuisikia sauti ya ukali ikiuliza hivyo mara baada ya kuwa watu hao kuwa wameshaingia humu chumbani. "Tulimuacha humu chumbani afande" niliisikia sauti ikijibu na sauti hiyo niliweza kuigundua ni ya Samson. Nilivyosikia ametamka neno afande basi nikajua hawa ni mapolisi na wamekuja hapa kunikomboa, hivyo sikutaka tena kuendelea kubakia chini ya uvungu wa kitanda ikabidi nijitokeze. "Nipo huku afande ni mimi hapa ndio niliotekwa" nilisema huku nikijionyesha hadharani. "Pole sana kijana, vipi upo peke yako au kuna na wengine?" aliniuliza askari mmoja wapo. "Nipo peke yangu afande" nilimjibu. Basi yule askari akaenda mpaka chini ya uvungu wa kile kitanda ili kuhakikisha, "Aisee mkuu kuna silaha humu uvunguni" alisema askari huyo huku akizichomoa silaha nzitonzito zilizokuwa zimefichwa huko uvunguni. Nikishangaa sana kwa kukutwa na hizo silaha na wakati mimi nilijificha humohumo chini ya kitanda na sikuziona au labda kwa vile nilikuwa nimechanganyikiwa na kujawa hofu. Basi askari hawa walioingia humu chumbani idadi yao walikuwa sita wakamdhibiti Samson na kumfunga pingu mikononi halafu wakazichukua hizo silaha ambazo zilikuwa ni bunduki kubwa NNE na baada ya hapo tukatoka mpaka nje, sikuamini macho yangu kama ni kweli nilikuwa nimekombolewa na askari Polisi hawa. "Lakini walipajuaje hapa na ni nani aliyewaambia kuwa nimetekwa?" hilo ndio swali ambalo nilijiuliza moyoni mwangu. Nikahisi labda ni Prisca ndio atakuwa ameripoti Polisi juu ya huku kutekwa kwangu na hawa watu wa Benny kule Hotelini majira  Yale ya asubuhi. Kwenye mapambano Yale magaidi wanne waliweza kuuawa mmoja wapo akiwemo yule jamaa aliyetaka kunifanyia ule ushenzi na Samson pale mwanzoni, pia magaidi wengine wengi waliokuwa ndani ya hili jumba waliweza kukamatwa na kudhibitiwa chini ya ulinzi Mkali wa jeshi la Polisi miongoni mwa waliokamatwa pia alikuwepo na yule Daktari wa kichina (Lee Chen) aliyetaka kulikata 'Gobole' langu, baada ya hapo magari mengi ya Polisi yaliweza kufika hapa kwenye eneo hili la tukio na Polisi walipofanya upekuzi wao waliweza kukamata silaha nyingi sana pamoja na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya ambayo yalifichwa ndani ya vyumba kwenye hili jumba lao. Baada ya hapo msafara wa kuekekea kituo kikuu cha Polisi ukaanza na watuhumiwa wote wakiwa wamekamatwa kasoro Benny na Eddy ndio sikuwaona, baadhi ya askari Polisi walibakia kudumisha ulinzi hapa.
**************
Hatimaye kwenye majira ya usiku tuliweza kuwasili mpaka kituo kikuu cha Polisi kilichokuwa kipo katikati ya jiji la Dar es salaam na wale watuhumiwa wote waliokamatwa walienda kuwekwa Selo (Mahabusu) na zile maiti za wale Magaidi waliouawa zilipelekwa kuhifadhiwa Hospitali, mimi nilipelekwa kwanza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya mkuu wa kituo kwa ajili ya mahojiano kidogo. Kutokana na uzito wa hili tukio nadhani ndio maana mkuu wa kituo alikuwepo bado yupo ofisini kwake. "Pole sana kijana kwa matatizo yote uliyoyapata" mkuu huyo alisema huku akinipa mkono wa pole. "Ahsante nashukuru sana afande" nilisema huku tukishikana mikono. "Vipi walikupiga na kukuumiza popote kwenye mwili wako?" aliniuliza. "Ndio walinipiga na kuniumiza usoni pamoja na kichwani" nilisema. "Pole sana kijana ngoja sasa hivi utapelekwa hospitali kwa matibabu, tulipata taharifa ya kutekwa kwako na binti mmoja hivi aliyejitambulisha ni mpenzi wako anaitwa Prisca je unamfahamu huyo binti?" aliniuliza tena. "Ndio afande namfahamu, je yeye yuko wapi?" nilimjibu na kumuuliza. Afande akajiweka sawa na kuniambia: "Huyo binti kwa sasa ameenda Hospitali kushughulikia na kuuhifadhi mwili wa kaka yake aitwae Eddy ambaye ni muhusika wa hilo tukio lako la utekwaji pamoja na mtuhumiwa mwenzake aitwae Benny, majira ya mchana walikuwa wanawakimbia Polisi Bahati mbaya gari lao lilienda kugongana na Lori na hatimaye wote wawili wakafariki dunia" afande huyo alinieleza kwa kirefu na hapo ndio nikagundua kuwa kumbe Benny na Eddy wamekufa. Afande aliendelea kuniambia: "Mpenzi wako Prisca alituambia kuwa mlivamiwa ghafla leo asubuhi wakati mnatoka Hotelini, ndio akatupatia ramani ya kufika huko ulikopelekwa na wale watu kwa kuwa yeye alikuwa anapafahamu ni kwa mpenzi wake wa zamani ambaye ndio huyo Benny aliyekufa" afande alisema. Duuh kwangu ilikuwa ni kama ndoto, kwanza nilimshukuru Mungu kwa kuweza kuninusuru na Yale maswahibu yote ya wale washenzi. Pili sikuweza kuamini kama Benny na Eddy wamekufa kwani wao ndio wahusika wakuu waliotaka kunifanyia ule ukatili wa kunikata 'Gobole' langu. Mara ghafla mlango wa humu ofisini ukafunguliwa na askari Polisi mmoja wa kike akaingia huku kwa nyuma yake akifuatiwa na Prisca pamoja na yule dereva John, Prisca alitabasamu kwa furaha baada ya kuniona mimi. Lakini kwa jinsi nilivyotokea kumchukia ghafla Prisca kutokana na haya majanga aliyoniletea ya kutekwa na kunyanyaswa pamoja na kudhalilishwa na akina Benny pamoja na yule kaka yake Eddy. sikutaka hata kumuangalia usoni nikajikuta naangalia pembeni mpaka huyu mkuu wa kituo aliweza kunishangaa!.

ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.