STORY: 💕KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 20




*******************
ILIPOISHIA.
Mara ghafla mlango wa humu ofisini ukafunguliwa na askari Polisi mmoja wa kike akaingia huku kwa nyuma yake akifuatiwa na Prisca pamoja na yule dereva John, Prisca alitabasamu kwa furaha baada ya kuniona mimi. Lakini kwa jinsi nilivyotokea kumchukia ghafla Prisca kutokana na haya majanga aliyoniletea ya kutekwa na kunyanyaswa pamoja na kudhalilishwa na akina Benny pamoja na yule kaka yake Eddy. Sikutaka hata kumuangalia usoni nikajikuta naangalia pembeni mpaka huyu mkuu wa kituo aliweza kunishangaa!.

👇ENDELEA NAYO👇
Kiukweli nilijisikia vibaya sana kumuona tena Prisca mbele za macho yangu. "Waooh baby wangu Jose pole sana jamani, siamini kama ningekuona ukiwa mzima" Prisca alisema huku akiwa bado na tabasamu lake usoni la kupendeza akitaka kuja kunikumbatia. Nikacharuka Mwanaume! "Naomba uishie hapohapo wewe dada, kuanzia sasa mimi sio mpenzi wako kabisa" nilisema kwa hasira. Prisca akajikuta amesimama ghafla hata ile hamu ya kutaka kuja kunikumbatia ilimpotea akabakia ameduwaa. "Lakini jamani mimi kosa langu nini Jose, mpaka unihukumu kwa makosa ya watu wengine?" aliniuliza. Yaani nilijikuta nimejawa na hasira mpaka nikashindwa kuongea niliishia tu kulia machozi huku nikihema juu juu kwa fujo. Ikabidi mkuu wa kituo aingilie kati hapa. "Kijana hebu punguza jazba kwanza, huyu binti si ni mpenzi wako sasa mbona unamkaripia hivyo?" aliniuliza. "Hapana afande kwa haya mambo yaliyonitokea sina hamu tena ya kuwa na mapenzi naye" nilisema huku nikiendelea kulia. Prisca naye akawa analia dereva John akaanza kum'bembeleza. "Usiseme hivyo kijana kumbuka ni yeye ndie aliyeleta taharifa kwetu na sisi ndio tukaja kukukomboa huko ulipokuwa umetekwa, je bila yeye tungejuaje kama wewe  umetekwa?" Mkuu wa kituo aliniuliza huku akinikazia macho yake ya kiaskari. "Sawa afande nakubali hilo, lakini mambo yaliyotaka kunikuta huko sina hamu nayo kabisa, mbaya zaidi waliotaka kunifanyia ukatili ni watu wake wa karibu Benny mpenzi wake na Eddy ambaye ni kaka yake" niliendelea kusema. Hapo Prisca akaingilia kati na kusema: "Jamani Jose huyo Benny mbona sio mpenzi wangu tena, zamani nimeshaachana naye japo yeye bado alikuwa ananifuatilia" Prisca alisema huku akijifuta machozi. Mkuu wa kituo akashusha pumzi na halafu akaniambia: "Unasikia kijana hebu jaribu kumuelewa mwenzako kuwa huyo mtu tayari alishaachana naye, pia fikiria hapo alipo amefiwa na kaka yake lakini ameacha huko kila kitu na kuja hapa kituoni kukufuatilia wewe ili ajue usalama wako upoje kama ungekuwa hauna umuhimu kwake si angekuacha tu" alisema mkuu wa kituo. Hapo kidogo jazba yangu ikaweza kupoa na kujikuta nikirudi kuketi tena kwenye kiti. "Pole sana Jose na matatizo yote yaliyokupata ndugu yangu" dereva John aliweza kunipa pole. "Ahsante sana nashukuru tayari nimeshapoa" nilimjibu huku nikijiinamia chini uso wangu maaana dereva John alinionya juu ya Prisca kuwa atakuja kuniletea matatizo. Baada ya hapo mkuu wa kituo akaendelea na maongezi ya kutuweka sawa. "Jamani ndio kama hivyo mambo hayo yameshatokea cha msingi ni kumshukuru Mungu kuwa hilo jambo limeisha, japo binti nakupa pole sana kwa kumpoteza kaka yako Eddy" alisema mkuu wa kituo huku akimuangalia Prisca. "Ahsante nimeshapoa, kaka yangu Eddy ubishi wake ndio uliomponza tangu mwanzo familia nyumbani tulimuonya juu ya kufanya urafiki na Benny kwani hakuwa mtu mzuri lakini akutaka kusikia" Prisca alisema kwa huzuni. Hata na mimi nilijikuta namuhurumia sana Prisca kwa hilo japo huyo kaka yake (Eddy) naye alitaka kunifanyia ubaya. "Basi hayo yamepita tayari hawa watuhumiwa wengine ambao tumewakamata tutawafungulia mashtaka na kuwafikisha mahakamani ili sheria ipate kufuata mkondo wake" alisema mkuu huyo wa kituo. Basi baada ya hapo akaturuhusu na kutuambia kuwa tunaweza kwenda nyumbani lakini kesho yake asubuhi nilitakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano zaidi na kutoa maelezo yangu juu ya kesi hii kama unavyojua mimi ndio mlalamikaji mwenyewe. Prisca akaahidi kunisindikiza kunileta hapa kituoni hiyo kesho, basi tukaweza kuondoka kurudi nyumbani.
*************
Tukiwa tupo njiani kurudi nyumbani, ndani ya gari mimi na Prisca tulikuwa tumeketi siti ya nyuma huku dereva John akiwa yupo makini na kuendesha gari huko mbele. "Jose naomba sana unisamehe kama nitakuwa nimekukosea, pia kwa niaba ya marehemu kaka yangu Eddy naomba na yeye umsamehe" Prisca alsema huku machozi yakimtoka taratibu. "Usijali hayo yote yamepita tangu nilipokuwa bado nipo mikononi mwa watu wabaya nilimuachia Mungu hili jambo, nashukuru sana Mungu amenijibu na hatimaye nipo mzima kama hivi" nilisema. Prisca akajiegemeza kifuani kwangu na kuniuliza: "Pole sana jamani, vipi lakini walikupiga na kukuumiza?" Nikatabasamu na kumjibu: "Wamenipiga kiasi tu sana, Benny alinipiga ngumi usoni pamoja na teke kifuani lakini kuna kitu kikubwa alitaka kunifanyia ambacho ni kibaya sana" nilisema. Prisca alishtuka sana kunisikia nimesema hivyo. "Kitu gani hicho alichotaka kukufànyia yule mshenzi?" Prisca aliniuliza. "Usijali nitakusimulia mitihani yote niliyokutana nayo huko tukifika nyumbani" nilimjibu na kumtuliza. "Ok baby lakini ngoja kwanza tupitie hospitali ili ukapatiwe matibabu na ukaangaliwe vizuri labda inawezekana umepata madhara yeyote" alisema Prisca. "Hapana sidhani kama nimeumia sana, maumivu niliyasikia pale mwanzoni lakini kwa sasa baada ya kuwa huru najisikia vizuri hapa naomba nipate maji ya kuoga pamoja na chakula maana tangu tulivyokula wote Jana usiku kule Hotelini basi ndio sijala tena kitu chochote" nilisema. "Daah jamani pole sana mpenzi wangu" Prisca alisema kwa kunionea huruma. Safari ya kuelekea nyumbani kwa Prisca ikaendelea.
Baada ya muda mchache tuliweza kuwasili mpaka nyumbani kwa Prisca ni kule maeneo ya Mbezi Beach dereva John akaiingiza gari ndani ya uzio (Fen's) na alipoizima gari tuliweza kuteremka na kuingia ndani ya mjengo huo wa kifahari, lakini tulipofika ndani dereva John akaaga kuwa anaondoka anarudi kule Mikocheni ambapo ni nyumbani kwa akina Prisca kulikokuwa na shughuli zote za msiba wa Eddy wakisubiriwa wazazi tu warudi kutoka nje ya nje walipoenda kwa ajili ya shughuli za kibiashara. Lakini Prisca hapa aliniambia kuwa tayari ameshawajulisha juu ya kifo hiki cha kaka yake Eddy na wamepanga kurudi hapa baada ya siku tatu (3) ili waje kumzika. Basi dereva John akaondoka na kutuacha  mimi pamoja na Prisca. "Sasa baby twende kwanza bafuni tukaoge, halafu ndio mambo mengine yafuate" aliniambia Prisca nami sikuwa na kipingamizi tukaenda zetu bafuni kuoga, yaani haya Mapenzi ni kitu cha ajabu sana! Eti kwa muda huu tayari nikajikuta nasahau zile kashikashi zote za wale magaidi wakina Benny na Eddy za kutaka kunikata 'Gobole' langu eti Kisa Mapenzi Tu. Pia wale washenzi wengine Samson na yule mwenzake walivyotaka kunigeuza shoga! Mbele binti mrembo Prisca yote hayo nilijikuta nayasahau, sasa sijui kama ndio kweli wangefanikiwa kunifanyia ukatili ule mambo yangekuaje lakini Mungu akupenda majanga Yale yanitokee. Baada ya kumaliza kuoga ambapo Prisca alinisaidia kuniogesha vizuri sana na hatimaye tukarudi chumbani akanichagulia nguo nzuri za kuvaa kwa usiku huu na baada ya kupendeza tukaenda zetu sebuleni kujumuika kula chakula cha usiku ambacho kilikuwa tayari kimeshaandaliwa na wale mabinti wanaomsaidia kazi Prisca hapa nyumbani kwake. Kwa sababu ya njaa Kali niliyokuwa nayo Mwanaume nilikula kwa haraka kama vile nakimbizwa mpaka Prisca mwenyewe alinishangaa! "Pole sana my dear kweli nimeamini ulikuwa na njaa sana" Prisca aliniambia huku akitabasamu. "Yaani we acha tu, njaa nimekuja kuisikia baada ya kufika huku lakini nilipokuwa kule kwa Benny hata hamu ya kula sikuwa nayo, mambo yao waliyotaka kunifanyia yanatisha sana" nilisema na baada ya kumaliza kula chakula tukaweza kuingia chumbani kwa ajili ya kulala. Leo Prisca akanitaka nilale chumbani pamoja na yeye sikuweza kumkatalia nilikubali. "Jose hebu niambie kwanza mpenzi wangu, wakina Benny walitaka kukufanyia kitu gani hicho kibaya?" Prisca aliniuliza na kukumbushia mara baada ya kuwa tayari tumeshapanda kitandani. "Duuh yaani sijui hata nianzie wapi kukusimulia, lakini kwa kifupi yule jamaa ni katili hafai kabisa katika jamii  bora hata alivyokufa" nilisema. "Benny ni mshenzi sana namjua vizuri sana mambo yake, ndio maana niliona bora niachane naye tu haya niambie alitaka kukufanya nini?" Prisca aliniuliza huku akiniangalia usoni. Nikaona sio mbaya ngoja nimwambie: "Alitaka kunikata huu Uume wangu ili kunikomoa nipate aibu na pia aone kama wewe utaendelea kunipenda" nilisema. Prisca akaahtuka sana! "Wee Jose unasema kweli alitaka kukufanyia hivyo yaani akate huo utamu uliokuwa nao, halafu yeye angeweza kuniridhisha na kile Kibamia chake?" Prisca aliniuliza kwa mshangao. "Ndio alitaka kuukata sasa sijui saa hizi ningekuwa na hali gani kama angefanikiwa" nilisema. "Shenzii kabisa, na ndio maana Mungu amewalaani wamekufa kabla hata  awajafanikiwa hilo lengo lao" Prisca aliniambia. Mimi nikaishia kutabasamu. Prisca akajisogeza karibu yangu na kuniambia kwa ndogo laini: "Jose mpenzi wangu najua kama umetoka kwenye matatizo makubwa huko ulipokuwa, lakini nilikuwa naomba tupeane burudani ya kimahaba usiku huu wa leo ili tujiliwaze mioyo yetu kwa haya magumu yaliyotokea" aliniambia Prisca huku tayari mdomo wake akiwa ameshauleta mdomoni kwangu ili kunyonya denda na mikono yake laini ikianza kulipapasa 'Gobole' langu. Nikajikuta napata msisimuko wa ajabu mwilini mwangu, lakini bado sijasahau Yale yaliyotaka kunikuta nikabaki najiuliza Je nikubali au nikatae kwanza mpaka nianze kusahau Yale majanga ya akina Benny, nikajikuta nipo njia panda huku Prisca naye akazidi kunifanyia visa vyake vya kimapenzi kwenye huu mwili wangu!.

ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.