STORY: KISA MAPMAPENZI TU SEHEMU YA: 11





Duuh yaani usipime huo mshtuko nilioupata baada ya kuelekezewa bastora mpaka nikajihisi mkojo kama vile unataka kunitoka! Benny aliniangalia kwa macho ambayo ayakuonyesha kuwa na mzaha hata kidogo na mimi. "Yaani wewe nguruwe pori ndio unataka kunipokonya furaha yangu kwa Prisca?" Benny alinichachafya huku bastora ikiwa ipo mkononi mwake. Mimi huku ndio usiseme hiyo hali niliyokuwa nikijisikia naijua mimi mwenyewe! "Benny unataka kufanya nini sasa enhe?" Prisca ikabidi aingilie kati kwa kuuliza huku akikaa mbele yangu kunikinga na hili balaa. "Nataka nimfundishe adabu huyo mshamba hawezi kunifanyia dharau" Benny bado alizidi kuunguruma. "Dharau gani aliyokufanyia enhe? kama ni hiyo adabu nataka unifundishe mimi maana ndio niliyemfuata kijana wa watu hana makosa" Prisca alizidi kunitetea. "Unajifanya unajua kuongea wewe mwanamke si ndio enhe?" Benny alimuuliza Prisca. Ghafla Prisca akatoka mbele yangu na kusimama pembeni! "Kama ni wewe ni Mwanaume kweli na unajiamini nataka umfyatulie hiyo risasi yako huyu kijana" Prisca alisema kwa hasira. Benny alibakia amesimama huku akiniangalia kwa ghadhabu sana mpaka mikono aliyoishika bastora yake ikawa inamtetemeka. Eddy yule kaka yake na Prisca akamfuata Benny na kumpokonya ile bastora mikononi. "Hakuna sababu ya kufanya huvi kwa sasa Shemeji, huyu ni wa kwetu tutamfanyizia taratibu" alisema Eddy huku akiiweka ile bastora ya Benny mfukoni mwake kwenye suruali yake ya Jeans aliyoivaa. Kwa muda huu mimi nilikuwa hoi sijiwezi huku kijasho chembamba cha hofu kikinitiririka! "Hivi Dada umekosa kweli Mwanaume wa kuwa naye mpaka umchukue huyu kinyago?" Eddy alimuuliza Dada yake Prisca huku akiniangalia mimi usoni na kucheka kicheko cha dharau. "Kati ya huyu kijana na huyo rafiki yako Benny nani kinyago?" Prisca naye alimuuliza kwa dharau. Eddy alibaki kimya hakuweza kujibu kitu, Beeny akakohoa kidogo na kusema: "Eddy naomba tuondoke hapa haraka sana, kwani kila nikiendelea kumuangalia huyo mpuuzi najisikia kichefuchefu nisije nikamuua bure" alisema Benny kwa sauti ya nyodo. Eddy akamgeukia tena Dada yake Prisca na kumuambia: "Hili jambo ni lazima niwaambie wazazi, yaani siku ya Jana yote ulishindwa kufuatilia biashara tulizoachiwa badala yake muda wako wote ukaupoteza kwa kuwa na huyo Mbwa koko" Eddy naye alitema cheche. "Na uwaambie unachelewa nini sasa?" Prisca alisema na kuhoji kwa hasira. Benny akamshika mkono Eddy na kuondoka naye lakini alipofika kwenye mlango Mkubwa wa kutokea akasimama na kunigeukia mimi! "Kijana wewe ni mbuzi tu sasa umechokoza vita na mimi Simba jiandae kuliwa nyama" alisema Benny kwa ghadhabu huku macho yake yakiwa yamemuiva kama vile pilipili kichaa na halafu akafungua mlango na kuondoka zake huku akiwa na Eddy kaka yake Prisca. Baada ya wale Vidume kuwa wameondoka zao Prisca akanifuata na kunikumbatia hapa nilipokuwa nimesimama! "Nisamehe sana jamani Jose wangu kwa haya yote yaliyotokea" aliniambia Prisca huku akilia machozi. Taratibu nikamuondoa mwilini mwangu na kumwambia: "Nashukuru sana Prisca kwa haya yote yaliyotokea, kumbe umenileta kwako lengo ni kunidhalilisha" nilisema kwa uchungu mwingi sana huku nikibubujikwa na machozi. "Hapana Jamani Jose wangu, sikukusudia kufanya hivyo nisamehe sana kwa niaba yao hawa washenzi" alisema Prisca. "Mimi sina tatizo lolote Dada Prisca, najua ni umasikini wangu ndio umenifanya niwe mwenye kudharaulika na kutolewa maneno yote ya kashfa yasiyofaa hivyo kuanzia sasa nahitaji kuondoka hapa" nilisema huku nikifuta machozi. "Uondoke, unataka kwenda wapi Jose?" Prisca aliniuliza kwa hamaki. "Hapa sio nyumbani kwangu, hivyo narudi zangu kulekule uliponitoa kwenye maisha yangu niliyoyazoea" nilimjibu. Prisca akaenda kuketi kwenye Kochi huku akisema: "Hapana kaka Jose kwa hilo sipo tayari kabisa kukuona ukirudi tena kule kwenye maisha Yale" alisema Prisca. "Sasa unataka niendelee kubakia hapa kwako ili niuwawe na yule Mwanaume wako pamoja na kaka yako?" nilimuuliza kwa ukali kidogo. Pisca akaanza kulia machozi! "Hapana kaka Jose usifanye hivyo jamani kumbuka mimi nakupenda na ndio maana nikawa nipo radhi kuishi na wewe hapa sasa unataka kuondoka unaniacha nani?" Prisca aliniuliza huku akilia kwa uchungu. Nikacheka kidogo kicheko cha uchungu na sio cha furaha halafu nikasema: "Kumbuka ni Jana tu ndio tumekutana kwa Mara ya kwanza na ukanileta hapa nyumbani kwako, sasa utasemaje nakuacha na nani kwani siku zote ulikuwa unaishi na nani enhe?" nilimuuliza kwa sauti yenye msimamo. "Hapana kaka Jose sipo tayari uende ukaishi mbali na mimi japo ni kipindi kifupi sana tumekutana" Prisca bado aliendelea kunibembeleza huku chozi likiendelea kumtiririka mtoto wa kike. Duuh hapa sasa nisipokuwa mtoto wa kiume huyu Prisca ataweza kunishawishi na kuendelea kubakia hapa kwake ambapo tayari Majanga yameshaanza kutokea ikiwa ni Jana tu ndio nimefika hapa Leo asubuhi nuksi ndio hiyo imeingia, apanifai tena hapa kuishi! "Msimamo wangu ndio huo nataka nirudi kule kwangu Uswahilini uliponitoa, japo nimeishi kwwnye maisha magumu lakini nilikuwa na amani" nilizidi kumkomalia. "Sawa nimekuelewa nitakurudisha, lakini naomba kwanza tukaoge wote bafuni halafu tupate kifungua kinywa ndio nikupeleke huko unapotaka kwenda" aliniambia Prisca. Nikakaa kimya nikitafakari nikaona poa sio mbaya ngoja kwanza nioge ili kuondoa Jasho lile la 'Kikubwa' ambalo lilitokana na kasheshe ya kutombana na Prisca usiku was Jana. "Poa nimekubali nitaoga lakini sio na wewe,  mimi nitaoga peke yangu" nilisema. "Kwanini lakini tusioge wote jamani ina maana bado tu una hofu?" Prisca aliniuliza kwa kulalamika. "Hayo ndio maamuzi yangu Dada Prisca naomba uyaheshimu, sitaki mapenzi hapa" nilisema kwa msisitizo. Basi Prisca hakuwa na la kuongezea tena ikabidi tu awe mpole, nikampa ile simu yake ambayo aliiacha kule kitandani na halafu Mwanaume nikaelekea zangu bafuni kujiswafi mwili wangu. Prisca naye akaenda kuoga kwenye bafu lililokuwa chumbani kwake kwani hii nyumba yake inaelekea kila chumba kina choo pamoja na bafu lake humo ndani kwa ndani! Baada ya kumaliza kuoga vizuri Prisca akanichagulia nguo nzuri ya kuvaa ni kati ya zile nguo nyingi alizoninunulia kule Kinondoni ile Jana yake. Muda huu sasa nikamuona Prisca anatabasamu tofauti na pale mwanzoni alipokuwa na huzuni wakati mimi niliposhikilia msimamo wangu wa kuondoka hapa nyumbani kwake, sikuweza kujua ni kwa nini huyu Prisca anatabasamu. Baada ya kumaliza kuvaa na kupendeza sasa tukaelekea mezani kwenda kupata Breakfast ya nguvu asubuhi hii ambapo wale mabinti wawili niliowaona Jana wakati naingia hapa kwenye huu mjengo na Prisca wakiwa ndio wametuandalia hapa mezani. Baada ya kumaliza kupata Breakfast sasa Prisca akachukua begi langu la nguo na mfuko uliojaa viatu akaenda navyo kuvipakia kwenye gari na Mimi nikatoka nje mpaka sehemu ya uwani kwenye maegesho ya magari Prisca akanifungulia mlango wa gari ambalo lilikuwa ni la kifahari mno tofauti na lile gari lake jingine la Jana tulilokuja nalo baada ya kuagana na wale mabinti wake wa kazi wa hapa nyumbani Prisca akaiondoa gari, kama kawaida geti lilifunguka lenyewe bila ya kufunguliwa na mtu yeyote na Prisca akaiingiza gari yake barabarani. Safari ya kurudi tena kwangu uswahilini Kule Kipawa Karakata kama Mimi mwenyewe nilivyoamini kuwa ndio ananirudisha hivi baada ya kumlazimisha kufanya hivyo ili kuepuka dhahama ya kufanyiwa kitu kibaya na Benny yule mpenzi wake wa zamani (Prisca) pamoja na kaka yake Eddy, "Kweli Ng' ombe wa masikini hazai nimeamini, yaani jana tu nimelala nzuri halafu tena leo narudia maisha yangu yale ya Jua na Mvua Duuh" nilijisemea moyoni huku nikisikitika na kujiona Jose mimi sina Bahati. Prisca yeye alikuwa bize na kuendesha gari yake! Kwa upande wangu niliona bora nikaishi maisha yangu ya kifukara kuliko niishi kwenye raha ambapo Luna vitisho. Nikamkumbuka sana bibi yangu aliyopo huko kijijini na nikatamani sana kurudi nyumbani kijijini nikaungane naye maana ndio yeye peke yake aliyebakia akiwa ni ndugu yangu baada ya Mimi kufiwa na wazazi wangu wote wawili, kwani ndugu zangu wengine kama vile wajomba na mashangazi wakiwa hawana habari na mimi. "Dada Prisca samahani nilikuwa na ombi moja kwako tafadhali naomba unisaidie" nilijikuta nasema. Prisca akageuka na kuniangalia huku akiwa bado yupo makini na kuendesha gari! "Ombi gani tena hilo jamani my dear?" Prisca aliniuliza kwa sauti laini. "Ni hivi naomba unisaidie nauli ya kurudi nyumbani kwetu Morogoro nataka nikaishi na bibi yangu kijijini" nilisema kwa sauti ya unyonge. Prisca akacheka sana halafu akaniuliza: "Mpenzi kwahiyo hautaki tena kuishi hapa mjini?" aliniuliza. Nikafikiri kidogo na kumjibu: "Ndio sihitaji tena kuishi hapa mjini, kwani kule ndio vile Jana ulimuambia yule mwenye nyumba avigawe au avitupe vile vyombo vyangu baada ya wewe kunilipia ile kodi niliyokuwa nadaiwa na ukamwambia kuwa mimi nisingeweza kuishi tena pale" nilisema kwa kirefu kidogo. Prisca akatabasamu na kuniuliza tena: "OK poa kwahiyo unadhani kwa sababu hiyo ndio unaona bora urudi kijijini?" aliniuliza. "Ndio hiyo ni sababu tosha kwangu na kingine pia nimemkumbuka sana bibi yangu" nilimjibu. Prisca akacheka sana halafu akaniambia: "OK baby nimekuelewa hakuna shida" alisema na safari ikaendelea na ukimya ukitawala.
Safari yetu moja kwa moja ikatufikisha mbele ya jengo moja kubwa sana la kifahari huku jengo hilo likiwa ni la ghorofa lenye maandishi makubwa yaliyopambwa vizuri yakisomeka= SINZA HOTEL nilishangaa sana imekuaje tena amenileta hapa! "Dada Prisca vipi mbona tumekuja hapa!?" nilimuuliza kwa mshangao. Prisca kwanza hakunijibu kwa haraka swali langu akaipaki vizuri sana gari yake sehemu maalumu ya maegesho chini ya jengo hili la Hoteli halafu akaizima kabisa gari yake na kunigeukia kwa mapozi na kuniambia: "Jose kwanza naomba unisikilize kwa umakini sana upate kujua dhumuni la mimi kukuleta hapa" aliniambia huku akitabasamu. Mimi nilibakia nimeduwaa nisijue anamaanisha nini! Halafu akaendelea tena kusema: "Jose nitakuwa ni mpumbavu sana kama mimi nitaruhusu wewe upotee mbele ya macho yangu" aliniambia kwa utaratibu sana. "Kwahiyo ndio unataka kusema unamaanisha nini Dada Prisca?" nilijitutumua na kumuuliza. Kwanza akatabasamu na kunirembulia macho yake mazuri na kuniambia hivi: "Namaanisha kuwa sipo tayari nilikose penzi lako hata kidogo Jose" aliniambia. Duuh Mwanaume niliishiwa pozi nikashusha pumzi ndefu na kumuuliza tena: "Dada Prisca nitajilinda vipi na yule mpenzi wako wa zamani pamoja na kaka yako?" nilimuuliza. "Kuhusu hao watu naomba uniachie mimi ndio nitajua namalizana nao vipi bila ya wewe kupata usumbufu wowote" Prisca alinijibu. "Sawa nimekuelewa lakini mimi shida yangu ilikuwa ni kwenda tu kijijini kwa bibi yangu" nilisema kwa sauti ndogo iliyopoa. "Hata mimi Jose nna hamu sana ya kumuona huyo bibi yako nimjue, lakini kwa sasa naomba tuingie humu hotelini tukajiachie kwa kupeana Mapenzi motomoto kupita Yale ya Jana halafu kesho asubuhi tutaenda wote huko kijijini" aliniambia Prisca huku akifungua mlango wa gari na kuteremka chini. Mimi nilibakia ndani ya gari nikirafakari nini cha kufanya kama nikubaliane na haya mambo anayoyataka Prisca au nikatae! Nikiwa bado naendelea kutafakari Prisca tayari alishachukua begi langu la nguo na kuniambia: "Baby naomba uteremke jamani ukanipe raha mwili wangu wote unakuhitaji wewe" aliniambia Prisca. Basi tena sikuwa na jinsi ya kukataa ikabidi tu niteremke kwenye gari na kufuata hayo anayoyahitaji, baada ya hapo Prisca akailock vizuri milango ya gari yake na tukaanza kuelekea sehemu ya (Mapokezi) kwenye Hoteli hii ya hadhi yake na baada ya kukamilisha kila kitu kuhusu malipo ambayo Prisca ndio aliyoyafanya kwa kulipia. Tukaingia kwenye lifti tukiwa pamoja na mmoja wa wahudumu akitusindikiza kuelekea sehemu kilipo chumba chetu ambapo ni juu kabisa ghorofani! Baada ya kufikishwa tukaonyeshwa chumba chetu cha kupumzukia na halafu muhudumu huyo wa kike akaondoka zake, ni chumba kizuri sana chenye kila kitu cha thamani ndani yake. "Kabla sijapiga simu kuagiza vinywaji njoo kwanza baby wangu unipe joto lako" alisema Prisca huku akiivua blauzi yake aliyoivaa na kuitupa sakafuni halafu akamalizia kuvua na sidiria yake chuchu za matiti yake sasa nikawa naziona Live. "Vipi tena jamoni my dear ina maana bado tu una wasiwasi mpaka hapa? usihofu kesho asubuhi wote tutaenda kijijini kumuona bibi" alisema Prisca huku safari hii akiiteremsha chini Sketi yake na kubakiwa na nguo ya ndani tu (Chupi) mwilini mwake. "Hii iliyobakia nataka univue wewe hapo baby wangu" aliniambia Prisca huku akinisogelea taratibu sehemu nilipokuwa nimeketi kwenye Kochi dogo lililokuwemo humu chumbani Hotelini, jamani nyie acheni tu.

ITAENDELEA ...







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.