TTCL yatoa gawio kwa Serikali
Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema mwaka huu wanatoa gawio la Sh. 2.1 Bilioni kwa Serikali kutokana na kukua kwa mapato ukilinganisha na mwaka uliopita.
Ameyasema hayo leo Jumanne ya Mei 21, 2019 katika hafla ya utoaji wa gawio kwa Serikali iliyoenda sambamba na uzinduzi wa awamu ya pili ya huduma ya video conference.
“Gawio hili ni ongezeko ya Sh.600 milioni zaidi ya kile tulichokitoa mwaka jana na tunaahidi kuwa kadri huduma zetu zitakavyozidi kuimarika tutakuwa mstari wa mbele katika kutimiza wajibu wetu wa kisheria wa kuchangia pato la taifa.” Amesema Kindamba.
Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuboresha huduma kwa wateja kwa kufanya vituo vyao kuwa katika viwango vya kimataifa na wameongeza uwezo wa teknolojia na miundombinu kwa kampuni hiyo.
“TTCL imeendelea kuwa mwajiri mkuu katika sekta ya mawasiliano, tuna wafanyakazi takribani 1,500 nchi nzima.” Ameongeza Kindamba

No comments: