JE UNAHISI MPENZI WAKO AMEPOTEZA MSISIMKO KWAKO?FANYA HAYA KUNUSURU HALI HIYO

MSISIMKO ni jambo la msingi kwa walio kwenye uhusiano wa mapenzi. Ndiyo muongozo wa kihisia kwa wapenzi. Kwa maneno mengine kama mmoja akipoteza msisimko kwa mwenzake ni hatari kubwa sana inayoweza kugharimu uhusiano.Rafiki zangu, katika mapenzi ni jambo la kawaida kabisa kugombana na kufikia hatua ya kutengana kwa muda.Naomba hapa niweke wazi kitu kimoja, nazungumzia zaidi kwenye uhusiano wa mapenzi, kabla ya ndoa. Nazungumza na wachumba zaidi.Inawezekana kukawa kumetokeakutokuelewana baina yenu, mkaachana. Ukiwa nje ya uhusiano wako, ukagundua kwamba chanzo cha matatizo yote ni wewe.Inategemea umemfanyia nini? Labda umemtukana sana, umeharibu samani zake nk, lakini mwisho wa siku unagundua kwamba wewe ni chanzo cha matatizo hayo ya kutengana. Kama kweli mna mapenzi ya dhati, mnaweza kukutana na kujadiliana pamoja, halafu mwisho wasiku mkajikuta mmeamua kurudiana.Kinachowarudisha pamoja ni mapenziya dhati pekee na si kitu kingine chochote, lakini pamoja na penzi hilo, unatakiwa kufahamu kwamba mwenzako atakuwa na majeraha ndani ya moyo wake, atakuwa na vidonda ambavyo vinapaswa kuwekewa dawa ili apone kabisa. Mwenye wajibu wa kumwekea dawa ni wewe mwenyewe! Maneno yako makali, tabia zako mbaya, vituko vya kila aina na hasara ulizomsababishia, zinaweza kuwa sababu ya kumjeruhi moyo wake. Majeraha pia yanaweza kusababishwa na jinsi usivyo msikivu kwake, wakati akiwa anaamini kwamba wewe ndiye mpenzi wa maisha yake   yote.Sawa  , ameamua kurudiana na wewe, kwa sababu anakupenda lakini bado anahisi kama utaendelea na matatizo yako ya zamani. Hakuamini. Anaona anaweza kuwa anatwanga maji kwenye kinu, ambapo ukweli ni kwamba mwishowe maji yote yatamwagika chini.

UTAMTAMBUAJE?Yapo mengi, lakini kwa uchache sana,atapunguza mahaba na wewe. Ninaposema mahaba sina maana ya ngono, namaanisha mambo ya kimapenzi. Anakuwa mgumu kupokeasimu yako, hata akipokea hazungumzimaneno ya kimahaba kama zamani.Ukimwambia: “I love you dear,” yeye anaweza kukujibu kwa kifupi: “Ahsante,” tofauti na zamani ambapo alikuwa akikujibu kwa mahaba mazito:“I love you too my sweetie.” Meseji zako hajibu, hata kama akijibu, atakujibu kwa mkato sana. Anaonekana hana msisimko na wewe.atakuwa mzito hata kuachia tabasamu akizunguza na wewe, hakuamini sana. Hakufuatilii sana, mara nyingi anaonekana mwenye mawazo mengi akiwa na wewe. Hafurahii anapokuwa na wewe na hata uchangamfu wake unapungua.Kikubwa hapo ni kwamba hana imani kama ni kweli umeamua kwa dhati kubadilika na kurudi kwake mzima-mzima! Moyo wake unaendelea kukiri ndani kwamba anakupenda, lakini anashindana na imani kwamba yawezekana usibadilike, anachohofia yeye ni wewe kurudia makosa yale yale! Kama ukiona dalili zote hizo ujuewazi kwamba bado ana wasiwasi na wewe, moyo wake umejeruhiwa. Kufahamu ni hatua ya kwanza, nzuri na muhimu sana kwako, kwani angalau sasa utakuwa unajua upo kwenye uhusiano na mtu wa aina gani, huku ukiwa makini katika kutafuta suluhisho la tatizo lenyewe.
BAINISHA TATIZOKitu cha kwanza kabisa unachotakiwakufanya ni kuonesha kwamba umeshafahamu kwamba hakuamini na hana msisimko tena na wewe. Unatakiwa umfanye ajue kwamba unatambua kinachoendelea, lakini unakiri kwamba ni haki yake kufanya hivyo, maana ni kweli kwamba mkosaji ulikuwa ni wewe.
USIMLAUMUKatika makosa makubwa ambayo hutakiwi kufanya ni pamoja na kumlaumu! Hutakiwi kabisa kumlaumu kwamba anakosea kufanyaanavyofanya. Lakini kwa vitendo, unatakiwa kuanza kumbadilisha taratibu huku ukionesha kumhurumia kwa hali aliyokuwa nayo.Si tatizo kubwa sana marafiki, lakini linahitaji subira wakati ukilishughulikia.
UFAFANUZIYapo maudhi madogo madogo ambayo mtu anaweza kuwa hayapendi, lakini kwa sababu yanajirudia mara kwa mara yanazidisha chuki na hatimaye kupoteza msisiko kabisa.Kuna maudhi/makosa makubwa ambayo mwenzi anaweza kuoenekana amesamehe lakini kumbebado yanafukuta kwenye moyo wake. Haya mambo yapo marafiki zangu. Ni vyema kufuatilia ili kufahamu tatizo   lilipo.Yote kwa yote, hapa tunadili zaidi na suala la kupoteza msisimko ambalo sasa, kwa kuwa unaupenda uhusiano wako ni kazi yako kuhakikisha unamrudisha mwenzi wako katika haliyake ya kawaida. Wiki iliyopita nilishauri kuacha kabisa kulaumu badala yake kushughulikia tatizo husika.Sasa twende tukaone zaidi juu ya mada hii ambayo naamini itawatoa wengi gizani.
ULIMI WAKO VIPI?Kuna watu wengine wanashindwa kuelewa kwamba kauli chafu pekee inatosha kabisa kumuudhi mpenzi na akapoteza hisia za mapenzi kwa mwenzake. Majibu ya hovyo, kauli nyepesi ambazo hazina uungwana na heshima zinatosha kabisa kumkimbiza mpenzi wako.Ufanye ulimi wako uwe mtamu, zungumza na mwenzako kwa mapenzi motomoto. Achana na kauli moto au zile zilizokosa mahaba. Jenga mapenzi kwa mwenzako, achana na mazoea.Maana kuna wengine, kwa sababu ameshazaa, basi utasikia mama naniii, baba Joseph n.k. Achana na majina hayo, mwite kwa majina ya kimapenzi au jina lake halisi, utafaulu kudumisha hisia za mpenzi wako.
DHARAU NI MBAYAHata kama mpenzi wako si mwerevu katika maeneo fulani, usimwoneshe dharau. Inawezekana ana udhaifu fulani katika mambo yake, hupaswi kumuonesha kwamba yeye si lolote. Jambo kubwa kwa mwenzi wa aina hiyo ni kumfundisha.Yes! Kumpa ujuzi, maana umeshagundua kwamba ana udhaifu katika eneo fulani, mwoneshe njia. Mtu yeyote akigundua kwamba anadharauliwa, haonekani kama ana mchango katika jambo fulani, huchukia.Ataanza kwanza kujichukia mwenyewe, halafu mwisho wake atamchukia mtu ambaye anamshusha thamani kwa kumdharauhalafu hatma yake, atapoteza msisimko kwa mtu huyo. Akimuona tu, moyoni anajisikia huzuni. Hawezi kuwa na furaha kwa mtu ambaye anamdharau.
JENGA TABIA YA KUMSIFIAHakuna mtu ambaye hapendi kuonekana anaweza. Akijua anaonekana anaweza, hujiamini sana.Huu ndiyo ukweli ambao hakuna anayeweza kuukimbia. Hata wewe bilashaka unapenda kusifiwa kwamba unaweza kitu fulani.Mmwagie sifa mpenzi wako, akivaa vizuri mwambie, akitengeneza nywele vizuri msifie…kifupi mfanye ajione kwamba yeye ni muhimu kwako. Atakapogundua kwamba yeye ni muhimu kwako, utakuwa umefanikiwakwa kiasi kikubwa sana kuteka hisia zake.
FARAGHA SASANamna ya kuwasiliana faragha pia husababisha kupoteza au kuamsha hisia za mpenzi wako. Utakuta mwingine anamwambia mpenzi wake bila woga, kwamba hawezi mapenzi, hilo ni kosa kubwa sana kwa   wapenzi.Ni sawa na kumtukana. Katika hali ya kawaida, ukimwambia mpenzi wako hawezi mapenzi, ni dhahiri utakuwa umekata moja kwa moja hisia zake. Hata mkikutana siku nyingine atakuwa hajiamini, atajiona anakwenda kukutana na mtu ambaye hawezi kumridhisha.Kuliko kumsema, ni bora kumfundisha.
OMBA MSAMAHA Kuomba msamaha ni kiunganishi kikubwa cha mapenzi. Hapa sitazungumza sana, maana naamini kila mmoja anafahamu maana ya msamaha na wakati muafaka wa kuutumia. Usibaki na vitu moyoni, kama unajua kweli umemkosea mwenzako, haraka sana mwombe msamaha na muendelee na mambo mengine.Kubaki na vinyongo husababisha hasira ya kudumu, ambayo mwisho wake hutafuna msisiko na hivyo kukosa furaha katika uhusiano wenu.Haya ni mambo ya msingi kabisa kwako kuyazingatia ili uweze kuwa bora na kuhakikisha msisimko kwa mwenzi wako unakuwa wa kudumu. Ndiyo nguzo ya penzi.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.