KUJICHUBUA NA HASARA ZAKE



Kujichubua (kwa wenye asili ya afrika-ngozi nyeusi)ni kitendo cha kuondoa uasili wa ngozi na kubakia na rangi tofauti na ile ya asili,kitaalamu kujichubua ni kuondoa upper layer (ngozi ya juu) na kubakiza daraja la pili au hata chini ya hapo.Mara zote ngozi ya juu ndio yenye vichocheo vya meranini ambavyo ndio huunda rangi nyeusi safi na pia inakinga dhidi ya magonjwa yanayoshambulia ngozi.Kujichubua hutofautiana baina ya mtu na mtu au sehemu (mazingira) kutokana na upatikanaji wa mahitaji hayo ya kujichubulia.Zipo njia mbili ambazo mara zote hutumika kubadili huo mwonekano wa ngozi:-

njia ya asili ambazo hutegemea zaidi matumizi ya mitishamba pamoja na matunda ambayo huchanganywa kwa utaalamu wanao ujua wao wenyewe kwa matokea wanayotarajia.
njia ya kisasa ambayo hutegemea zaidi matumizi ya bidhaa za kiwandani zenye kemikali kali zikitumika kama mafuta na vipodozi mbalimbali.Pia kuna wale wanagaramia kununua vidonge ambavyo ni maalumu kwa kazi hiyo,ipo njia ya upasuaji na kuwka vipandikizi ambavyo huua nguvu ya meranini na kumfanya mtu aonekane rangi tofauti na weusi.

Kujichubua kunaweza kuwa kwa hiari au pasipo hiari yako mwenyewe,ingawa kama hujatarajia kufanya hivyo basi ni rahisi kuachana na matumizi ya kitu fulani ambacho unaona kinapelekea wewe kupoteza asili ya ngozi yako.Zipo baadhi ya bidhaa hasa mafuta na vipodozi hubebeshwa viambata vyenye sumu ya kuua uasili wa ngozi yako (viambata vya kuchubua) bila kuoneshwa katika maelezo kuwa inaleta matokea hayo.Ukisha itumia kwa muda fulani ndio huweza kuonesha matokeo ya kile ambacho kimebebeshwa ndani,hivyo kama siyo lengo lako hasa basi ni muhimu kuachana nayo.

Kila nchi duniani ina sheria na taratibu zake katika kuthibiti na kuboresha afya ya wananchi wake,na pia zipo bidhaa ambazo hutengenezwa kwa usafirishaji wa nje tu na siyo matumizi ya ndani ya nchi hivyo kuwa makini wakati wa kuchagua vipodozi na mafuta ya ngozi yako.kutumia bidha zisizo na ubora au kutumia bidha zenye kemikali zinazoharibu asili ya ngozi yako huufanya mwili kukosa kinga dhidi ya mashambulizi ya magonjwa mbalimbali pamoja na kuwa vigumu uponaji wa vidonda katika ngozi yako.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.