MANENO SITA USIPOYATUMIA UTAACHWA NA UMPENDAE




Ukitumia maneno mazuri kwa mpenzi wako unampa furaha na kumwonyesha kuwa yeye ndiye mtu wa kipekee kwako duniani.
Kama unaye mpenzi, anza kutumia , maneno haya sita na uhusiano wako utakuwa wenye raha;

1. Nimebahatika kuwa nawe

Mweleze mpenzio vile unajisikia furaha kuwa naye Kumwelezea mpenzio vile unajisikia kubahatika kuwa naye katika maisha yako ina uzito zaidi kuliko ” Love You”.

2. Pole/ Samahani

 Unapokosa mwambie mwenzio “pole” Kusema Pole baada ya kukoseana au majibizano madogo huongeza mapenzi katika ndoa yenu.

3. Nimekusamehe

Ni vigumu kwa mtu kuomba msamaha lakini ni vigumu zaidi kusamehe mtu. Msamaha ni jambo muhimu sana katika uhusiano.
Ni ngumu sana kuifanya mara kwa mara lakini ndiyo huongoza na kupeana mwelekeo wa ndoa. Haina haja kushikilia mabaya ili kuharibu ndoa yako. Msamehe tu!

4. Nipo hapa kwa ajili yako

Ukimpenda mtu, mkubali kwa jiinsi alivyo kwa uzuri au ubaya. Hakuna aliyekamilika. Wakati mwenzako anapitia magumu, hakuna maneno yanayompa nguvu kuliko ” Nipo hapa kwa ajili yako” kutoka kwa ampendaye.
Maneno haya humhakikishia mwenzio kuwa una yeye katika hali zote za kimaisha.

5. Nakuamini

Related image
Ndoa hupata majaribu hata ikiwa ya miaka hamsini! Lakini la muhimu sana ili kudumisha mapenzi katika ndoa ni uaminifu. Habari Nyingine: Inashangaza: Mume amuuza mkewe kwa mtalii! Ukimwambia mwenzako unamuamini, basi umeondoa hisia za mbaya kumhusu kama wivu ambao ni hatari sana kwa ndoa

6. Nimejitolea kwako kikamilifu

Related image
  Kujitolea kwa hakika kwa mpenzio huonyesha kuwa ulimchagua yeye pekee, kawa mwaminifu na hilo litamfanya ajisikie kapendwa kwa dhati.
USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.