Njia 10 za kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia...!!!
Huwa tunatumia mda mwingi sana hapa tukiongelea, sehemu gani nzuri ya
kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini
cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, na kadhalika..
Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea huwa ni kama theruji kwenye
mlima kilimanjaro, ila volukano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya
wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia kumi
za kuwa mkufunzi wa kiumeni na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe
wanakuhangaikia.
Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu
juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila
kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu
wanawake.
Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.
Kitu kimoja wanaume wengi wanacho kiharibu na kupoteza nafasi yeyote ya
kuwafanya mwanawake aanze kumfuatilia kwa kuharibu mambo tokea mwanzoni,
ni pale mwanaume unapopata nafasi na kuanza 'aaahaa' na 'eeehee, si
unajua.. aahaa', na kuonyesha tabia ya kutojiamini na kuwa na wasiwasi,
tabia ambayo humfanya mwanamke asivutike tena na wewe, ukimuuliza
mwanamke yeyote ni kitu gani anachovutiwa kwa mwanaume, cha kwanza
atakuambia anapenda mwanaume anayejiamini.
Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote
anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa
mchezo wa kutongoza toka moyoni bila hata kufikilia utaongea nini au
kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea
mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba
kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, "Halo, mie ndo
yule dada tuliobadilishana namba", mwenyewe anaanza kujinogesha,
kukufatilia na kukuwinda.
Namba 2. Muonyeshe changamoto.
Hili kiumeni tumeshaliongelea, mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa
umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji
kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye
kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo),
mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye
mapenzi yanamuendesha hana la kufanya zaidi ya kumlamba miguu, kama
waswahili wasemavyo "Ukimwonyesha mwanamke unampenda sana, lazima
atakusumbua", wanawake hawavutiki na mwanaume fala, mwanaume ambae
anaweza kumpelekesha jinsi yeye anavyotaka, sasa atawezaje kukufatilia
wakati havutiki na aina hio ya wanaume, tofauti na hapo anajua tu lazima
mwenyewe utajipeleka.
Tokea binadamu kuumbwa, mwanamke huwa anapenda kitu ambacho hawezi
kukipata, na hata kama akikipata na akajua kakipata lazima hamu ya kuwa
nacho imwishie na kukitaka kingine ambacho hana uwezo nacho, ndivyo
fikra na akili ya mwanamke ilivyo, umenielewa hapo jamaa?
Onyesha changamoto, mwonyeshe hutawaliwi na tamaa na huendeshwi na
mapenzi, unamambo mengi ya kufanya, na kama una marafiki wa kike
hakikisha anawajua, ili ajue kumpenda yeye ni uamuzi na sio lazima maana
wapo wengi, muonyeshe wewe ni kati ya wale wanaume wachache kupatikana,
mwanaume lijali ambaye wanawake wote wameumbwa kutoka kwenye ubavu wake
mmoja tu kati ya mbavu nyingi alizonazo. Hivi haujawahi kuona mwanamke
anampenda sana mwanaume halafu mwanaume hana hisia na huyo msichana,
unajua msichana huwa anakuwaje?
Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.
Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna
uhakika mkubwa ataendelea kukufikilia kuwa wewe ni mwanaume wa aina
hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye
lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae
utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia
gani na wanaume wa aina hii. Kwahio ukianza na maswali ya kuonyesha
tabia ya kifala, patishia.. huyo mwanamke ataanza kukufikilia kuwa
utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huwo
ndo utakuwa mwisho wako.
Kwahiyo ni vizuri ukaondoa kabisa maswali ya kuonyesha kama wewe ni mtu
ambaye hujiamini, maswali kama "Kwa hio ni aina gani ya wanaume
unaowapenda?", au "Vipi, hivi mie naendana na wewe?" baya zaidi ni "Hivi
unamvulana?" Hivi unauliza anamvulana ili iweje, kama umevutika naye
fanya yako kwanza, uhusiano ukiwa umejenga muhimili mwenyewe atajua
sheria zinasemaje, tafadhali usijaribu maswali ya namna hii.
Namba 4. Usimfatilie sana.
Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii
kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa
rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo
hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo
mwanamke, au husubili na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya
yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja,
uhusiano wa wewe kuumia na mawazo na kujipendekeza kwake kwa kumramba
miguu na kumfanya yeye asikujali. Iwapo akiwa anakutarajia kuwa utafanya
hivi hapo kutakuwa tena hakuna kipaumbele kwa upande wake, hakuna ile
hali ya kumfanya akufatilie wewe na kukutaka, tofauti na hapo kumfata
fata kunampa maana nyingine mwanamke ambae ndo kwanza ameanza kupata
hisia kwako, kunampa maana kuwa amekutana tena na Fala mwingine.
Ukimwonyesha tabia ya kumuhitaji sana lazima atakuona wa kawaida usio na
uzito wowote kwake, ila ukijionyesha wewe ni kiumbe ambae haupatikani
kirahisi, kiumbe wa nadra ambae akikukosa maishani mwake lazima atakuja
kujutia nafasi, kutamfanya akutake na kuanza kukufatilia kwa ukaribu
maana tayari anakuwa ameshagundua anakuhitaji wewe na wewe ndie yule
mwanaume lijari aliyekuwa anamsubiria, maana upo tofauti na wanaume
wengine anaowapuuzia.
Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani.
Habari ya Mjini: Wanawake wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume,
na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo
wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi
cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe
ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo
haziitajiki, kumnunulia zawadi bila sababu, kwa hio acha kumnunulia
zawadi bila sababu na kumpa sifa pale ambapo haziitajiki, sio kwamba
kidogo tu kabadili pozi, tayari na wewe umeshamsifia, kabla siku
haijaisha tayari umeshamsifia mara 100. Mwisho wa siku atakuona
unamsifia sifia tu kumshika masikio bila kumaanisha chochote kile
ukiongeacho, na juu ya zawadi atakuona unampa mpa zawadi ili kununua
upendo wake na wala hauna mapenzi yeyote ya dhati kwake.
Badala yake mwambie ulikuwa unamfikilia leo au mwambie umemuota jana,
ili ajuwe yupo akilini mwako unamfikilia badala ya kumpa sifa mpaka
azione za kawaida, unavyomsifia mara chache ndo husuda yake ya kutaka
kusifiwa na wewe inavyokuwa kubwa, ndivyo atakavyokuwa na tamaa ya
kusikia maneno kutoka kwako.
Namba 6. Mwingie kwenye kichwa chake.
Kumfanya mwanamke awe anakufukuzia, inakubidi umfanye mwanamke awe
anakufikilia badala ya wewe kuwa ndie unayemfikilia, na njia moja ya
kufanya jambo hilo lifanikiwe kwa urahisi ni: Kataa au zipuuzie mialiko
au vitendo unavyovipokea tokea kwa mwanamke, ukitaka ufanikiwe kwa uzuri
zaidi fanya uonekane upo bize na sio mtu wa kupatikana kwa wepesi.
Mwambie, "Aah, unataka tutoke ijumaa hii? Sijui. Kuna ishu nyingine
inatokea siku hio na sidhani kama huyu msichana ataniruhusu nisifike".
Fanya hivyi kwa usahihi na hatoweza kukutoa akilini mwake.
Namba 7. Mringishie
Hii hatua ina umuhimu wake, kumfanya mwanamke aanze kukufatilia lazima
ugeuze baadhi ya mambo, hii nikimaanisha lazima ujiweke wewe uwe kama
mchaguzi, na mwanamke anatakiwa ajionyeshe kuwa anafaa kuwa na wewe.
Ila inabidi ufanye hii hatua kwa kuzingatia usije ukaonekana kama
unajiona, tafuta staili ya kuifanya, fanya maongezi ya kirahisi kama
kumuuliza "Hivi ni nini kinachokutofautisha wewe na wasichana wengine
niliokwisha kuwa nao kimahusiano?" au "Ni vitu gani vitatu ambavyo
unauhakika mwanaume atavipenda kwako, na tafadhari usiniambie uzuri",
Muulize hivi ukiwa kama vile unafanya maongezi ya kutania na huyo
mwanamke ataanza kuvutiwa na wewe kwenye maongezi, na hii haina uchawi.
Na pia unaweza kuwa umemwahidi kitu ambacho unajua anakipenda ila
ukatumia pia kumcheleweshea kumpa, ukawa unamtamanisha kwa maneno
mazuri, hali hii inaongeza mvuto zaidi wa kukitaka hicho kitu na
kuongeza mvuto zaidi juu yako ila kuwa mwangalifu asigunduwe
unamringishia.
Namba 8. Mfurahishe na Mchekeshe.
Kicheko ni kitu kilicho na nguvu sana kuuteka moyo wa msichana, na
inabeba sababu ya kisayansi. Kumfanya mwanamke afurahie kuwa na wewe ni
njia kuu ya kumfanya awe anafikiria kutumia muda wake na wewe na
kukufikiria wewe pia.
Kwahiyo mfanye mwanamke achekelee na hata kama akiwa na msimamo kiasi
gani, kibaiolojia atajikuta anavutika na wewe kwa sababu ya hisia nzuri
anavyojisikia akiwa na wewe, hiyo hisia hawezi kuipuuzia zaidi ya
kuendelea kukuwaza na kutaka kufahamu ulipo ili akufuatilie umpe
tabasamu jingine.
Namba 9. Usionyeshe karata zako zote.
Hii njia ndio nayoipenda kupita njia zote ndani ya kiumeni.com kwa
sababu ni njia rahisi na nzuri zaidi na inamfanya mwanamke afanye kazi
zote, unachotakiwa kufanya ukikutana na mwanamke kwa siku ya kwanza
usiwe kama redio, unatangaza matangazo yako yote, unaweza kuanza kufanya
hivi kwa kutojitambulisha jina mpaka hapo atakapokuuliza jina lako, au
kwa kumuwekea kichwani fikra ya "Labda." Mwambie "Sikia, natakiwa nirudi
nikawape kampani rafiki zangu, labda ntaweza kukuona baadae."
Kwa njia hii kunamfanya asikutambue na akilini anabaki na labda, Labda
ananitaka? labda kavutika nami? na siku zote mashaka na kutokujua ni
njia moja nzuri sana ya kutengeneza mvuto. Ukimfanya apate zile hisia za
kukutaka kukujua, zile hisia za mvuto wa kutaka kukufahamu, kutamfanya
aanze kukufuatilia bila yeye kutokujua anafanya hivyo.
Namba 10. Acha kumfatilia.
Kama kila saa unashindwa kujizuia kumfatilia msichana, kutaka kujua
anafanya nini, yupo wapi, kwa njia hiyo huwezi kufuzu kuwa na uwezo wa
kumfanya msichana aanze kukufatilia wewe.
Kwa hiyo njia ya mwisho ni kuacha kumfatilia. Na hapo ndipo hiyo tabia
ya kumfata fata mwanamke kama katoto kanyonyacho kinavyomlilia mama
akiwa hayupo itakavyoisha. Utakuwa tofauti na wanaume wengine
wanavyokuwa, wanawake watakuona mtu unaejiamini na kijua kile utakacho
kutoka kwenye maisha yako mwenyewe na watavutika na wewe kwa mvuto wa
mafanikio sio mvuto wa kupewa ahadi hewa. Anza kutengeneza tabia ambazo
zinawavutia wanawake, tabia ambazo zitakuweka juu na kukufanya uwe kile
mwanamke anachotamani kuwa nacho, tabia ambayo inampa mwanamke hamu ya
kukutaka kukujua zaidi, kutaka kukufahamu, kutaka kukaa karibu yako,
kutaka kukupa vitamu alivyonavyo ili mradi tu awe na wewe.
No comments: