SABABU ZA WANAUME KUKOSA HAMU YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA

Natumai utakuwa mzima wa afya kabisa msomaji wa safu ya afya katika Mtandao huu? Ambapo leo Tunazungumzia Mada ya sababu za wanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo la Ndoa. Kama ilivyo matatizo mengine tatizo la kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa huwakumba wanaume vilevile ila sio kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwa wanawake. Katika Makala haya tutaaangalia kwa kina sababu za tatizo hili kwa wanaume na athari zake na mwisho tutajifunza njia za kutatua au kuondokana na tatizo hili. 

Mwili wa mwanadamu uliumbwa ukiwa na matamanio na matatmanio haya si mabaya kama mwenye mwili atakuwa na uwezo wa kujitawala. Wanaume wengi huvutiwa zaidi na hisia za kushiriki tendo kwa kuona baadhi ya maungo kwa wanawake, kusikia sauti na hata migusano. Kuna wanaume wengi ambao wapo lakini wamekuna awana haja au kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa na wanajiona kama ndio wamefanikiwa kujitawala kumbe ni wagonjwa. 

Habari njema ni kwamba pamoja na tatizo hili kuwasumbua watu wengi kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa, kwa kutumia mimea tiba na matunda tiba. 

Unachotakiwa kufanya kama umejaribu kutumia njia mbalimbali ili kuondoa tatizo hili bila mafanikio basi wahi mapema kwa wataalamu ufanyiwe uchunguzi sambamba na kusaidia kuliondoa kabisa tatizo hilo na ukarejea katika hali ya kawaida. 

Baadhi ya watu wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka. Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. 

Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili. 

Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanaume kukosa hamu ya kushiriki tendo limekuwa ni chanzo kikubwa katika kuleta migogoro katika ndoa nyingi. 

Wanaume kwa kawaida ni wabishi sana na huwa hawapendi kuaibika hivyo mtu anaweza akawa na tatizo ila hapendi mwenzi wake ajue kama anatatizo ambalo kumbe angeliweka bayana angepata ushauri wa namna ya kulitatua. Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake,Ambapo kwa mujibu wa Tabibu wa Tiba Mbadala Simon Rusingwa kutoka Sigwa herbal Clinic inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, ni sawa na uwiano wa mwanamme mmoja mwenye tatizo hili katika kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. 

Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali kama sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hukosa raha wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake. 

Tuanze kwa kuangalia sababu au vyanzo vinavyopelekea mwanaume kukumbwa na tatizo hili la kukosa hamu ya kushiri tendo la ndoa. Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. 

Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili. 

Mahusiano Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke 

Uhusiano kati ya mwanume na mwanamke ambao ni wanandoa una mchango mkubwa katika kujenga au kubomoa matamanio ya mwanaume. Kama kutakuwa na matatizo ya mahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Ni vema ukajihoji kama mahusiano yako na mwenza wako yapo sawa. Na mara nyingine unaweza ukawa umekuwa katika mahusiano kwa mda mrefu kiasi ambacho umemzoea hali inayopelekea kukosa hamu ya kushiriki nae tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi. 

Matumizi Ya Madawa Na Pombe 

Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na; Madawa ya high blood pressure, Madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, Madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone. 

Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni 

Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. Kama thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo. 

Umri Kuwa Mkubwa 

Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanaume homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanaume huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi. 

Uchovu. 

Wakati mwingine uchovu hupelekea mtu kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Na ikiwa mtu atakuwa anasongwa na shughuli nyingi zinazochosha mwili kiendelevu hamu ya kushiriki tendo la ndoa huanza kupungua na ikizidi basi baadaye mwanaume husika atakosa hamu ya kushiriki tendon la ndoa na itahitaji uangalizi mkubwa ili arejee katika hali yake ya kawaida. Vilevile kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha. 

Msongo Wa Mawazo 

Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha hali inayopelekea kushindwa kuyafanya mambo yako ya kawaida kiufanisi. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi. Mwanaume anasongwa na mawazo kiasi cha kuathiri katika ufanisi wa shughuli zake anaweza kupoteza hamu ya kushiriki tendo la ndoa. 

Kuwahi kufika kileleni 

Katika vitu ambavyo wanaume wengi hawapendi vijulikane na wenzi wao ni tatizo la kuwahi kufika kileleni. Kila mwanume hupenda aonekane ni rijali au mwanaume kamili mwenye uwezo wa kushiriki tendo la ndoa bila shida yoyote. Na imezoeleka katika jamii zetu ikiwa mwaume atakuwa ana tatizo la kuwahi kufika kileleni anaweza akatangazwa mtaa mzima kila mtu ajue, hali hii hupelekea aibu kubwa na fedheha. 

Katika mazingira kama hayo mwanume mwenye tatizo hata hajatangazwa na mwenzi wake amemtunzia siri hiyo, anajihisi kuwa hafai. Hali hii humfanya kila anapopata hamu ya kushiriki tendo la ndoa aogope kushiriki tendo na mwenza wake kwani ataabika. 

Usikose kufuatilia mwendelezo wa makala hii ambapo sehemu ya pili ya makala hii itazungumzia njia za kuondoa tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ili kurudisha heshima ya nyumba yako





USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.