JIMAMA TAMU
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 16
Hatukujua kwanini anawavizia wanajeshi wanzake na kuwataim kwenda kumuua mmoja mmoja hadi akawamaliza na kuingia kwenye chumba cha mniga alipofungiwa ambapo alimkuta ndo anazinduka tangia apoteze fahamu jioni, yule mwanajeshi wa kike akaenda kumfungulia huku mniga akiwa kimya tu anamuangalia anachokifanya hadi akamaliza kumfungulia, minyororo ile na kumwambia,
'"mniga jikaze nikutoe hapa haraka kabla hawajazinduka hawa wajinga, aliongea yule mwanajeshi wa kike na kumfanya mniga apitishe mkono wake kwenye bega la yule dada mjeshi safari ikaanza ya kutoka huku wapo makini Sana yani hadi wakatoka kabisa ndani ya kambi ya jeshi na kuingia, mstuni huku giza nene limetawara mniga alikuwa anamajeraha kila kona huku kachoka Sana maana tangia atekwe hajakula kitu chochote zaidi ya mateso tu ila kwakuwa msaada aliupata basi alijikaza kiume huku anasikia maumivu kweli michozi tu ikawa inamtoka yule dada ambae bado hatujamjuwa jina lake wala sura yake alimkokota mniga hadi kwenye pango ambalo kulikuwa na giza Sana huku kelele za wadudu zakutisha ila mniga alijikaza hadi wakaingia ndani kabisa ya pango na mdada yule akamwambia,
'"jikaze kusimama pekeyako ili Mimi nifungue mfuniko hapa, mniga akajikaza kusimama huku akisikia maumivu Sana yule dada akafukuwa kidogo mchanga na ukaonekana mfuniko wa chuma pale alipofukua bila kuchelewa akatoa funguo kwenye suruale yake na kufungua kufuli kubwa Sana alipofungua ndo mfuniko ule ukafunguka nao akaenda hadi alipo mniga na kumshika huku akimtembeza talatibu hadi kwenye ule mfuniko aliofungua akatangulia yeye kuingia huku mniga akafuata wakishuka kupitia ngazi iliopo hapo walishuka hadi chini kabisa ambapo kulikuwa giza Sana, hivo yule mdada akaenda sehemu na kubonya swichi ambapo taa zikawaka hapo mniga akabaki kushangaa tu maana palikuwa ni pazuri hatali yani ni Kama nyumba sasa umeingia sebleni ambapo yule mdada alipandisha ngazi hadi juu na kuufunga tena ule mfuniko kwa ndani akamkuta mniga kakaa kwenye sofa huku bado anashangaa shangaa yule mdada akaingia chumbani huku akitoka na hotipoti kubwa Sana ambalo lilikuwa limejaa chakula akatenga mezani na kupakuwa kwenye sahani na kwenda kumpa mniga ambae alikifakamia hata bila ya kunawa maana alivopewa tu yeye akaanza kula tu hadi yule dada akabaki kushangaa na ukumbuke wakatihuo wote yule dada hakumuonesha mniga sura yake zaidi ya kuwa kavaa Kama kininja tu mniga alikula chakula kile na kumaliza yule mdada akachukua sahani kwa mniga na akamuongeza tena ambapo mniga alikichukua na kuanza kula huku akimtazama mdada yule kwa uwizi uwizi na kujiwazia kichwani huyu ni nani harafu mbona pale aliniita jina langu basi inaonekana huyu ananijuwa ila ngoja nisimuulize tu, aliwaza mniga huku akiendelea kula akakimaliza na kumwambia,
'"dada yangu asante Sana kwa kuniokoa maisha yangu na asante kwa chakula kitamu Sana, aliongea mniga,
"'Oh usijari sasa Kama umeshiba twende kwenye chumba cha matibabu ili nikutibu majeraha yako mniga, aliongea yule mdada,
Itaendelea...........