FAIDA ZA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANANDOA
1. Linajenga ukaribu zaidi kwa wanandoa
Tokana na majukumu ya kifamilia ambayo yanaenda yakikua kwa kasi na kufanya baadhi ya wanandoa kutokuwa na wakati wa kuwa karibu zaidi kunakuwa na muda mchache kwa baadhi kubadilishana mawazo.
Wanandoa wengine wamefaulu kwa kuhakikisha kila siku/au mara kadhaa kwa juma kujulishana habari zao wanapokuwa hawapo pamoja. Tendo la ndoa linaweza tumika kama wakati muafaka wa kila mmoja kutiririka na kuongea mambo mbalimbali na hata kupanga mipango yenu ya kimaisha. Hilo hutokea pale mnapokuwa mnataka kujianda, nusu fainali au baada ya mchezo kuisha tegemeana na mtiririko wenu upo vipi.
2. Kumwelewa Mwenzi wako
Tendo la ndoa lina lugha yake… Tendo hili haliishi tu katika kufurahia na kufika kileleni bali pia linasaidia kumwelewa na kumsoma mwenzi wako. Ndio maana ni vema sana kumjulia mwenza wako kitabia na mwenendo kwa kuhusisha tendo hilo.
Ikiwa wenza mna tabia ya kushirikiana na kuhusishana katika masuala ya kila siku ni rahisi kutambua kuwa mwenza wako siku hiyo kachoka, kachukizwa (iwe na wewe ama mtu mwingine), ana mawazo, ana wasiwasi, hana raha n.k.
Haijalishi kuwa mwenza wako yupo katika hali ipi wengi hujitahidi hilo lisiwe kikwazo kwa tendo la ndoa (hasa wanaume) – Hivyo ni rahisi kumjulia tokana na namna mnavyokuwa faragha kujua kuna jambo ama la. Ni wazi wakati mwingine kunaweza kuwa na jambo na mwenzi wako asikuhusishe, kupitia tendo la ndoa unaweza pata viashiria.
3. Inasaidia wanandoa kupata Watoto
Watoto wana raha yake katika ndoa, na wana nafasi kubwa sana katika kuweza kuimarisha ndoa, kuleta furaha katika familia, kuwajenga na kuwa komaza kama wazazi na pia kuwaunganisha zaidi wanandoa kama mwili mmoja.
Si wote wamejaaliwa kupata watoto (my heart goes out to them) – ila ukweli ni kuwa mara nyingi hiki ni kipengele muhimu katika ndoa ambacho wanandoa wenyewe na jamii hutarajia kuwa muhimu kufanikisha ili ndoa ionekane kuwa ina mafanikio. Niongeze kuwa tumepishana kutafsiri mafanikio ni nini katika ndoa, ila wengi huwa na msimamo wa kuwa watoto ni muhimu katika ndoa.
4. Kutatua ugomvi/mgogoro kati ya wenza
Ugomvi haukwepeki hata kama mwapendana vipi (ingawa frequency ya ugomvi hupishana kati ya wanandoa). Tendo la ndoa linazungumza mambo mengi sana…. Kitendo cha kukutana kimwili na mwenza wako kwa namna moja wapo inakuwa ni akili na mwili wako kukubali kuwa umejitoa kwa mwenzi wako kwa wakati huo.
Kuna makabila ambayo hata uwe umegombana vipi na mke/mume wako, ikitokea tu ukalala naye na kufanya tendo la ndoa haijalishi kosa lilikuwa ni lipi inachukuliwa limesamehewa na yapaswa kusahau na kusonga mbele.
5. Kupunguza uchovu/Msongo wa mawazo
Ndoa ni moja ya njia kwa baadhi kuweza kupunguza uchovu alio nao na kwa wengine hata msongo wa mawazo. Tendo likifanywa vema na kwa ustadi, huweza kumwondolea mwenzi wako uchovu au msongo wa mawazo kwa kiwango kikubwa.
Unafuu huo utegemea lakini, wengine inakuwa tu unafuu wakati wa tendo hilo na hali wengine hupata nafuu ya muda mrefu. Hivyo ikiwa mwenzi wako yupo katika hali hiyo katika kutafuta namna ya kuhakikisha anapata unafuu, unaweza tumia tendo la ndoa kama silaha ya kumrudisha mwenzi wako katika hali nzuri.
6. Linajenga heshima ndani ya ndoa (hasa kwa wanaume)
Hili linawezekana pande zote (mke na mume) mmelipa umuhimu wa pekee tendo la ndoa hadi mkiwa faragha wote hufurahia tendo hili hadi kuna wakati mwajihisi mpo mwili mmoja kama si ndani ya ngozi moja. Tunarudi palepale, kuwa ni muhimu ukampenda mtu wako, ukapenda hilo tendo, mengine yanafuata mkiwa faraghani.
7. Linatumika kupata unachotaka/Kulaghai (hasa kwa wanawake)
Hili linategemea unalifanya kwa namna ipi… Ukilifanya kana kwamba ni hongo ya lazima na kuwa wamaanisha hutokubali kuwa faragha bila kutimiziwa kitu Fulani – Hapo inakuwa ni tatizo na ndio ulaghai wenyewe.
Ila lifanywapo kwa upendo, utani wa kimapenzi, kwa kutoa maneno matamu na kubembembeleza, husaidia kuongeza ashiki kwa wapenzi (inaweza isiwe kwa wote) na huku pia ukifanikiwa kupata kile ambacho unataka mwenzio akiwa katika mood nzuri.
No comments: