MAMBO MATANO (5) YATAKAYOKUSAIDIA ILI UWEZE KUFANIKIWA
Je una shauku ya kutaka kuongea na Mungu moja kwa moja? Ili akupe majibu yako kwa habari ya maisha yako?! fuata kanuni hizi ili uweze kufanikiwa moja kwa moja katika mambo unayoyafanya au unayotaka kufanya:
1. Kuwa mtu wa kusamehe, usipende kubeba vinyongo vya kutowasamehe wengine, kwani kufanya hivyo kuna kuweka katika mazingira ambayo kimisingi utashindwa kufanya mambo yako na kijamii yaletayo mafanikio. Lakini pia kumbuka kama hautakuwa mtu wa kusamehe pia hata wewe utashindwa kusamehewa pia.
2. Ichukie dhambi na uiache kabisa, kuwa mtu wa toba, jikague moyo wako na matendo yako kila siku, omba rehema za Mungu unapoona umeenda kinyume na maagizo yake.
3. Acha tabia ya kuwasengenya na kuwasema watu na watumishi wa Mungu, wapende na uwaombee, maana siyo kazi yako kuhukumu. Wapende na wengine, mtu akikosea muite muonye kwa upendo na umuombee acha tabia ya kusengenya wenzio, unajichelewesha.
4. Kuwa mtu wa maombi, maana yake siyo kila siku ushinde umejifungia, hapana kuwa mtu wa maombi ni kutafakari matendo makuu ya Mungu kila wakati, acha kuwaza ujinga na uovu.
5. Tenga Muda maalumu wa kuongea na Mungu wako. (muda wa maombi) na kutafakari neno lake.
Mpaka kufikia hapo hatuna jambo la ziada, tunakutakia utekelezaji mwema

No comments: