UTAENDELEA KUWA ‘SINGLE’ KAMA UNATAKA KUTONGOZWA NA MWANAUME SIRIASI!

Ukikutana na mwanamke ambaye amepitia mengi katika mahusiano, labda kashaumizwa mara kadhaa au mara moja lakini alikuwa anapenda sana, atakwambia kuwa hawaamini wanaume na hataki kupenda tena. Hiyo ni baada tu ya kuumizwa, lakini baada ya kukaa na kutulia utamsikia akisema, nataka mwanaume siriasi, sitaki mtu wa kunichezea na kuniacha.
Hapo ndiyo shida kubwa huanzia na Dada yangu inawezekana bado uko single kwakuwa unatafuta mwanaume siriasi. Labda nikwambie hakuna, ni nadra sana mwanaume anapotongoza anakuwa siriasi, kwamba labda anataka kukuoa au anataka kuwa na mahusiano na wewe ya muda mrefu. Labda tuangalie mfano huu, halafu jiulize kama inawezekana akataka kukuoa.
Upo umekaa sehemu, umemuona Kaka mzuri umemtamani, kaja kukusalimia, hujawahi kuonana naye kabisa, anaomba namba yako na kwakua nawewe kakuvutia unaamua kumpa. Kesho yake anakupigia simu anakwambia kuwa, yuko siriasi, anakwambia ashachezea maisha na sasa anataka mtu siriasi.
Kwakuwa unamuona mstaarabu basi unamuamini au kwakuwa anakufuatilia miezi sita bila kukata tamaa unamwamini na kuona kweli yuko siriasi labda anataka kukuoa kweli. Lakini hebu jiulize, huyu Kaka ulikuwa humfahamu kabisa, mmekutana siku moja na anakuwa siriasi na wewe, kakupenda saa ngapi, kajua tabia zako saa ngapi.
Lakini swali jingine hivi nikweli hakuwa na mtu, kwamba miaka yote hiyo alikuwa anasubiri tu upite mtaani kwao, uajiriwe ofisini kwao, mpande basi moja. Lakini ina maana hiyo miezi sita aliyokuwa anakutongoza alikuwa hana mtu, kwamba kwakuwa amekuona basi anaachana na mpenzi wake hafanyi tena mapenzi kwakuwa tu anasubiria umkubali? Inawezekana kweli, sijui ila kwangu hapana haiwezekani.
Sasa kama haiwezekani kinachotokea hapa ni nini? Kinachotokea nikuwa kila mwanaume, labda tuseme wanaume wengi, anapokutongoza iwe umemkubalia ndani ya siku moja au baada ya miaka kumi alikuwa anataka kutembea na wewe, afurahie maisha basi, mwingine hata hakujua kama utamkubali lakini alikutongoza hivyo hivyo.
Asilimia kubwa wanakuwa na watu wao, hata kama si siriasi lakini wapo hivyo hawawezi kukusubiria mpaka kukubaliwa na hawasimamishi maisha yao kusubiri kukubaliwa. Sasa utajiuliza usiriasi unakujaje, kama kila mtu ana mtu itakuaje mimi kuolewa. Iko hivi anakuoa kwakuwa amekufurahia zaidi, amekupenda kuliko mwingine.
Kwamba mnapoanza mahusiano mnapoanza kuwa siriasi anatakiwa kukuchagua wewe au hao wengine, lakini hawezi kuwa siriasi na wewe hata kabla hajakupata hiyo ni ngumu. Kusema akwambie atakuoa kabla hajakupata, atakwambia kweli lakini hatamaanisha, hivyo mwanaume akijifanya anataka kukuoa hata kabla hajakujua jina la pili jua ni staili yake ya kutongoza.
Sasa wewe ufanye nini hapa?
Hebu acha kutafuta watu siriasi na tafuta mtu ambaye unaona anakuvutia kwanza kimuonekano na pili namna anavyokujali na kukuheshimu. Huo ndiyo usiriasi unaoutaka lakini kama utakutana na mwanaume mwezi unataka akajitambulishe kwenu, aongee kuhusu ndoa, unaanza kumwambia namna ulivyo umizwa na kulialia.
Kama utakutana na mwanaume mwezi unaanza kumpa mashariti, kumchunguza na kumpa majukumu ya kukuhudumia kama mkewe, kuanza kumwambia kuhusu kukulipia kodi ya nyumba, sijui ndugu zako wanaumwa na matatizo yako akikataa ukasema hakupendi basi Dada yangu hebu tafuta Kiti ukae kwani utakaa hapo “Single’ Muda mrefu, badilika, furahia mahusiano.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.