Wanaume wenye Mahawara Kuweni Makini, Mnalogwa

Jumamosi ya juzi nikiwa ndani mwangu nafuatilia Bunge, nilisikia hodi ikabidi nikajue ni nani, alikuwa ni Jirani yangu (Binti) ana miaka kama 24-26 hivi, toka nimehamia hapa sijui ana shughuli gani inayomwingizia kipato au inayomfanya aishi hapa mjini, Baada ya kumkaribisha ndani akaanza hivi.

(Jina Langu) samahani, nikamjibu...bila samahani...(Jina lake), nina shida ya sh.30,000/= naomba unisaidie,(kwa kuwa nimezoena nae sana akaanza kunisimulia)

Kuna hawara yake ni doctor hapa ...juzi yake alimwambia kuwa "hamtaki tena kuanzia Juzi hiyo" huyo hawara yake ana mke na watoto 3.

Ni yeye (hawara) ndiye anayemlipia kodi ya nyumba, anamsomesha chuo cha Hotel management na ndiye anayemtunza kwa maana ya chakula.

Sasa kodi inaisha mwezi wa kwanza mwakani na ada ya chuo anadaiwa na imebaki sh. 700,000/= na pesa ya kwendea field Zanzibar hana.

Akaniambia kuwa, ...Nimepata mtaalamu (mganga) ameniambia nimpe sh. 30,000/= ili anipe dawa nimvute, (Amchomee) ili kurudisha mawasiliano halafu nyingine atamwekea kwenye chakula au kinywaji ili "akiomba kiasi chochote kile cha pesa apewe"

Sikuwa na iyana ila nimuuliza swali moja, kwa nini usitumie njia ya mazungumzo? akasema nishajaribu sana but hataki! "sasa mimi nitaishije hapa wakati ada nadaiwa, kodi ya nyumba inaisha mwakani"?

Nilimpa sh. 30,000/= akaenda.

Jumapili (jana) huyo hawara yake alisalimu amri yy mwenyewe kwa yeye kuanza kumpigia simu (kwa mujibu wa huyu binti) jamaa alimuuliza "upo wapi"? demu akajibu nipo nyumbani, Njoo .....bar...sasa kilichojiri huko jana sikijui nadhani leo ataniambia tu..

Kwa hiyo, wanaume tuwe makini sana na mahawara kwani yawezekana unaye na unatamani ujinasue kwake ila moyo wako unakufa ghafla na kuamua kuendelea naye hadi sasa. Pls, tuwe makini sana




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.