JINSI YA KUMPATA MWANAMKE BILA KUMTONGOZA
Haikuwa kazi rahisi kumshawishi Mwalimu Makoba kuweka makala hii katika blogu yake. Alipomaliza kuisoma katika kompyuta yangu, alicheka kisha akasema, "makala yako itaniharibia wanafunzi wangu!" Sikusita, nilijibu kwa hoja madhubuti, "mwalimu, niliyoyaandika humu yanalenga zaidi kumkomboa msichana, kwani akizisoma mbinu zilizoandikwa humu, hawezi kunasa katika mtego. Kunyamaza kimya, ni kuwafanya wazidi kutekwa na mbinu hizi!"
Mwalimu wa Walimu alinitazama kwa udadisi, kisha akasema, "ITAPANDISHWA!"
Sasa tiririka nayo:
Maisha ni ujanja tu mzee mwenzangu. Sasa leo ngoja nikupatie ujuzi kidogo ambao nimeupata mbali sana. Mbali sana mhenga mwenzangu, ng’ambo huko. Unaweza ukampata bila kutia neno! Kimya - kimya.
HATUA YA KWANZA
Njia hii inafanya kazi katika
mawasiliano ya simu. Hususani ‘kuchat’… tena ukitumia WhatsApp ndiyo utaua
kabisa mwananzengo! Sasa ukiwa na namba yake, kama ni namba mpya na bado
hamjafahamiana, hakikisha mnafahamiana vya kutosha, yaani mnazoeana na kuwa
marafiki.
HATUA YA PILI
Sasa mmezoeana. Anza kazi yako
rasmi. Kila unapokuwa unachat naye, tumia zile ‘emoj’ za mahaba, yaani zile
zenye makopakopa! Wakati wa kuanzisha ‘chat’ tumia, mkiendelea na ‘chat’ tumia
na wakati wa kufunga ‘chat’ itumie.
Mfano. “Mambo vipi? Missing u kwa
sana π”
Ajabu ni kwamba hata yeye ataanza
kutumia emoj hizo. Ukiona hivyo mwanakwetu jua mambo yameiva, piga hatua ya
tatu.
HATUA YA TATU
Anza kumuita majina ya mahaba.
Yako mengi sana, anza na ‘my dear’, ‘honnie’, ‘my sweetie’, na mengine mengi
kadiri ya uwezo wako. Tazama mfano huu uone inavyotakiwa kuwa: wakati unafanya
haya, tambua kiingereza hakiepukiki katika mahaba.
“Hi baby! Unafanya nini now?π”
“Owkey, my honnie, tutachat
kesho… nalala π.”
Ni kama uchawi vile. Kwa sababu
ni lazima na yeye ataanza kukujibu kwa majina hayo. Unaona kazi ilivyo nyepesi?
HATUA YA NNE
Jimilikishe taratibu. Tayari
unatumia emoj za mahaba na yeye anatumia, unamuita majina ya kimapenzi na yeye
anakuita hivyo, unasubiri nini? Hebu anza uchokozi huu:
“WEWE: sweetie huwezi amini leo
kidogo nichepukeπ€… ila nikaogopa nikajua ukinikamata sitapona!”
Jibu lake hata kama litakuwa
tofauti, ni lazima liwe na mahusiano na hili:
“YEYE: Ole wako nikukamate, nina
wivu mimi π… mwambie huyo dada akome!”
Sasa mwanakwetu mambo yakifika
hapa unasubiri nini tena? Haya twende hatua nyingine.
HATUA YA TANO
Mtoe ‘out’. Wakati mnaendelea
kuchat, anza kuomba kumtoa ‘out’ ili mkasafishe macho kidogo. Tazama namna
nzuri ya kufanya jambo hili.
“Hi my everything π? Wikend
hii una ratiba gani?” ninaimani swali litajibiwa vyema. Ongezea.
“Oooh… kuna laki mbili
zinaniwasha, nikaona nikizitumia peke yangu nitakuwa sijakutendea haki we
rafiki yangu wa muda wote… can we go out this weekend tukaburudike pamoja π?”
Katika mtego huo hawezi kuchomoa.
Unataka nikuelekeze cha kufanya ukiwa huko out?
Mkitoka, sehemu nzuri zaidi
kwenda ni ‘night club’. Kama ni mnywaji wa pombe, kazi itakuwa nyepesi. Kama
hatumii, mbembeleze anuse japo kidogo. Akikataa usimlazimishe, kufanya hivyo
kutamfanya arejee nyumbani na kukuacha ukizubaa.
Cheza naye mziki taratibu. Wakati
mkiendelea na masaa yakiwa yamekatika mweleze sikioni taratibu, “My dear,
nadhani, kuna chumba hapo mbele kina kiyoyozi siyo cha nchi hii, twende
tukapumzike mama watoto wangu.”
Chukua bajaji nenda kapumzike na
mtoto uliyempata bila kumtongoza! Kesho njoo unishukuru kwa somo hili adimu. π
Natoa angalizo kuwa, somo hili
lisitumiwe kwa lengo la uzinzi. Madhara ya uzinzi yanafahamika na hakuna faida
yoyote kufanya hivyo. MBINU HIYO ITUMIKE KUMPATA MTU UNAYETAKA AWE MKEO!