HATMA YA MAHUSIANO YAKO NI NINI?:

No photo description available.

👉Kudate ni jambo rahisi sana, Ila kuna siku ukiwaza na kutafakari kwanini unadate utajikuta umeshapoteza muda wako, pesa zako na hata kupoteza muelekeo wa maisha kwa mtu ambae hujui kwanini ulikuwa nae na kwa Lengo gani?

👉Katika kizazi cha Leo ukiondoa mapenzi 'sex' katika mahusiano Utagundua kwa asilimia kubwa ya wanaume hawana jambo lingine la maana kuwafanya wawepo kwenye mahusiano, Vile vile ukiondoa Pesa 'Utajiri' katika mahusiano Utagundua asilimia kubwa ya wanawake hakuna jambo lingine wanalohitaji kwenye mahusiano la ziada.(Muangalie Eva pale bustanini na tamaa yake ya kutaka kumiliki hata vilivyokatazwa na Mungu)

👉Kizazi cha sasa Bila pesa asilimia kubwa ya wanawake wataona haina haja ya wao kuwa katika mahusiano na Bila Sex wanaume wataona haina haja ya wao kuwepo katika mahusiano.
Wanawake wengi wanalalamika sana kwamba wanaume wanapenda sana sex akishakufunua mara mbili tatu basi ule upendo wa mwanzo unapungua.

Hivyo hvyo wanaume wanalalamika sana kwamba wanawake wanapenda sana pesa inamaana wakishazipata wakizitumia na zikiisha/ukiishiwa basi wanakuhama hakuna mapenzi ya mwanzo tena hutafuta mwenye pesa mwingine, Hii ndio hasara ya mahusiano yenyewe sasa.

👉Hatma yako ya mahusiano ni nini, Jiulize je, nitatumiwa mpaka lini, nitaolewa na nani kwa mtindo huu, kijana jiulize je pesa zangu zitatumika mpaka lini, je nina mpango gani wa kuwa na maendeleo, je ninahitaji familia na je nitaitunza vipi kama pesa yangu inatumika kununua mwili wa mtu ili kukidhi haja ya muda mfupi?

Usiingie kwenye mahusiano bila malengo ndugu yangu, Utakuta unapoteza muda kwa mtu ambaye siyo yule aliyebeba ndoto na hatima yako ya maisha.

👉Kabla hujafikiria kuwa na mtu fulani yatathimini maisha yako. Fikiria unatakiwa kuwa mume au mke wa mtu, unatakiwa kuwa baba au mama wa familia, Je huyo uliye naye ndiye mwenza wako sahihi au unajiegesha tu ili maisha yasonge?
Je ndiye mzazi mwenzio, Je ndiye mkeo au mumeo mtarajiwa?
Usikae tu na mtu ili na wewe uonekane upo kwenye mahusiano, Kaa na mtu kwa malengo. Epuka mahusiano ya kujiegesha, mahusiano ya Kuiga, mahusiano ya kujionyesha yatakusababishia majuto.

👉Ni wakati wetu sote kubadili mtazamo, mahusiano yamekuwa fashion kila mtu analia na upande wake, wanaume walia kwamba wanawake wanapenda pesa japo sio wote ila asilimia kubwa pesa imekuwa kupaumbele katika mahusiano yao kukiko utu, na vile vile sex imekuwa kipaumbele katika mahusiano ya wanaume wengi kukiko kuwaza maendeleo ya kweli.

Tujifunze kuongeza thamani katka mahusiano. Ikumbukwe mahusiano sio starehe tu, Bali ni kupeana mbinu za kimaisha na kujua nini mnataka kufanya katika umoja wenu, mmekutana ili kufanya nini.



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.