MADA YA LEO NI KITANDA!



WALENGWA NI WANAWAKE NA WANAUME.
Habari za leo wapendwa. 
Nimatumaini yangu mpo salama, na kama kuna ambae hayupo vizuri ki afya, nampa pole na namuombea mungu ampe siha njema. 
Bila kupoteza muda, nataka kuingia moja kwa moja katika mada yetu ya leo, ambayo ni KITANDA! Labda kabla sijaingia rasmi kwenye mada, nitoe sababu ya kwa nini, nimeamua kuanza na mada ya KITANDA! 
KITANDA ni muhimili muhimu sana wa kuupumzisha mwili wa mwanaadam. Na katika KITANDA ndipo wanaadamu wengi sana tumeanzishiwa hapo! Hivyo basi kwa mantiki hiyo, utaona KITANDA, kilivyokuwa na umuhimu wa pekee katika mada hii. 
KITANDA kikiwa kibovu, kinakuwa kama uwanja wa mpira wa miguu, ambao una mashimo na mabonde, kwa vyovyote vile, timu hata ingekuwa na kiwango kizuri namna ya timu kubwa duniani, hapo kiwango chake kitafifia, kutokana na ubovu wa uwanja! 
Maana yake ni kwamba, KITANDA kikiwa kibovu, kwa uchakavu, au kulegea, unapokuwa katika kutoa burudani, huwezi kucheza mechi katika kiwango cha juu, kwani utakuwa unakiogopa KITANDA kisilie, ukasikikwa nje aidha na watoto au wapangaji wenzio, kama umepanga, kiasi hata watu wawe hawapo karibu, muwe peke yenu wahusika, lakini zile kelele zitawaghasi, na kuwaondosha katika mchezo, kwani mtacheza taratibu huku akili zenu badala ya kuwa mchezoni, nyie mnakisikiliza KITANDA kinalia au hakilii?!!! Hivyo ni muhimu zaidi ya sana, ili burudani na viwango viwe bora, ni kufanya mapenzi, katika KITANDA imara na kizima! Kuna vitanda vingine havilii, ila godoro lake, limekwisha sana, kiasi linawaumiza wahusika, sasa badala ya kupata raha ya Sexy, kinyume chake wanapata maumivu, nakupelekea kuwatoa mchezoni! Mara nyingi hawa huwa hawawezi kuenda zaidi ya ‘kimoja’ hawafanyi tena! Kwani migongo na magoti yao itakuwa imepata suluba kubwa. 
Baada yakupata faida kubwa ya KITANDA, sasa niingie kwenye MADA yenyewe! 
Pamoja na umuhimu huo wa KITANDA, baadhi ya wanawake, wamekuwa hawakipi thamani KITANDA chao! Utakuta KITANDA hakitandikwi hadi wakati wa kulala, kinakung’utwa kidogo kutoa mchanga, akiamka asubuhi, anaendelea na shughuli zake bila ya kujali KITANDA chake, hayo ni makosa makubwa kwa mwanamke! 
Pia wapo baadhi ya wanawake ambao, wanatandika VITANDA vyao shuka nzuri na za thamani kubwa sana, lakini akija Bwana/mume wakati wa kulala, wanatandua shuka hizo na kutandika shuka zisizo na thamani, ukiwauliza mbona umetoa shuka nzuri unatandika hii shuka ya hovyo? Anakujibu, sasa wewe unataka ichafuke?!!! Yaani anamjibu mpenzi wake, mkavu na haijalishi hata kama shuka hiyo, pesa za kununulia amelipa huyo bwana! Haya ni makosa makubwa sana, ndiyo ukitaka kuwajua baadhi ya wanaume walioathirika na kutandikiwa shuka chakavu wakati wa kulala, anamwambia mwanamke mpya ambae anajua faida ya kulala katika shuka nzuri hasa wakati wa majambo, Mbona shuka hutoi?! 
Wapo wanawake wengine baadhi yao, KITANDA kinakuwa ndiyo Stoo, huko uvunguni utakuta chupa za soda, sufuria, na mabindo ya nguo chafu yamejaa tele! Hata akifagia uvunguni fagio haliwezi kupita kutokana na wingi wa vitu vilivyokuwa huko uvunguni! 
Wapo wanawake wengine baadhi yao, wanakiweka KITANDA sehemu moja tangu masika ya mwamka huu hadi masika ya mwakani, KITANDA hakibadilishwi, wanawake namna hii, wanakosa ubunifu mkubwa katika akili zao, kwani mwanaume kwa kitanda kukaa sehemu moja muda mrefu, anakizoea na hata Sexy atakayokuwa anafanya ni ya kawaida sana! Ukilinganisha na Sexy mpya, namaanisha sehemu nyingine tofauti! 
Nachukua nafasi hii, kupitia darasa hizi, wanawake wenye Ila hizi mbadilike, ili mlete changamoto ndani ya mahusiano. Kwani mapenzi yanataka utulivu wa hali ya juu, ndiyo maana kama hujatulia akili zako zikiwa hazipo katika Sexy, huwezi kufika kileleni hata iweje! Na wanaume ambao wanawake zao, ni wasafi wa miili yao na VITANDA vyao, mnapaswa kuwapongeza wapenzi wenu, ikiwa watakitoa kitanda kutoka upande mmoja na kwenda upande mwengine, kwani mara nyingi jambo hili hulifanya mwanamke peke yake, akitaraji mpenzi wake akija, akute mabadiliko! Sasa mwanaume anaingia ndani na kukuta kumepambwa na yeye badala ya kumpongeza mwenzake, utakuta anamwambia wewe kuhangaika wewe, kwani ulikuwa huna kazi ya kufanya?! Tanda lote hili umelihamisha peke yako?! Siyo vyema kufanya hivyo kwani kunamvunja nguvu mwenzio! Naomba kila mwenye tabia zilizoelezwa hapo abadilike kisha ataona mabadiliko makubwa katika ndoa yake! KITANDA ni mada ndefu sana, kama nikiieleza yote, inaweza kuwa na eneo kubwa sana, kwa kuwa mada hizi walengwa wakubwa ni watu wazima, inatosha kwa haya machache, naomba tukutane kesho katika mada nyingine muda na saa kumi kamili Alasiri.
Asanteni sana.








USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.