Faida za limao au ndimu kilishe na afya
Zifuatazo ndizo faida zitokanazo na utumiaji wa limao na ndimu kilishe na kiafya;
Kusaidia uwiano sahihi wa pH ya mwili kuuwezesha kufanya shughuli mbalimbali.
Ina vitamin C na kemikali mimea ambayo husaidia kutibu mafua na mfumo wa upumuaji. Pia kuboresha afya ya ngozi, fizi (kuzuia fizi kutoka damu, ukavu wa ngozi ikiwemo kuchanika midomi na pua kavu), moyo, figo, misuli, maini na ubongo kwa kupambana na sumu mbalimbali mwilini. Pia husaidia kukata uchovu wa mazoezi au marathon.
Husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kunywa sharubati yenye mchanganyiko wa limao au ndimu, au bilauli ya maji ya limao au ndimu nusu saa kabla ya kula.
Pia tindikali zilizonazo husaidia kuzuia au kupambana na vijiwe vya figo, gout (mlundiknoi wa uric acid kwenye viungo na mwili). Husaidia kufyonzwa na kubadilisha madini ya chuma kwenye vyakula jamii ya mimea na kufanya iweze kutumika kutengeneza damu (ferrous iron).
Ganda la limao pia lina virutubisho, kemikali mimea na mafuta kwa wingi. Ganda lake au mafuta husaidia kutibu mafua, kuchua misuli au hutumika kwenye vinywaji kuleta ladha au kama tiba mvuke kwa magonjwa ya msongo wa mawazo, au magonjwa ya mifumo ya fahamu.
Matumizi ya mara kwa mara Husaidia kupambana na kisukari, shinikizo la damu (kutokana na wingi wa potassium) na ulemavu wa macho.
Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu Husaidia kuzuia saratani mbalimbali mwilini.
Husaidia mchakato wa kuzalisha nguvu mwilini.
Mambo muhimu ya kuzingatia.
Inashauriwa kuongeza limao/ndimu kwenye mboga za majani kama tembele na chai ili kusaidia ufyonzwaji na utumiwaji wa madini ya chuma mwilini toka kwenye mboga hizo.
Faida hizi pia zafanana na jamii zote za malimao yakiwemo machungwa, madalansi, machenza nk japo baadhi ya faida zinaweza kuwa kwa wingi au kidogo kwa kila tunda
Inashauriwa kutumia moja ya matunda hayo kila siku ili kuboresha lishe na afya zetu.
Angalizo
Wapo wanaotumia limao kuondoa kichefuchefu au kuzuia kutapika, ila limao halizuii kutapika, bali inapelekea kutapika kutokana na uchachu wake. Hivyo waweza tumia parachichi au tunda baridi (lisilo chachu) kuzuia kutapika.
No comments: