HII NDIO SABABU KWA NINI NAWAPENDA WANAUME
Muda mwingi huwa najiuliza mnatoa wapi hizi nguvu.
Mnaweza kumaliza hata miezi mitano bila hata kujinunulia nguo ili tu ulete chakula mezani (nyumbani).
Unashinda njaa ili familia yako iweze kupata chakula wapate kuishi.
Unaamka unavaa nguo na kuondoka nyumbani bila hata kujua unaenda wapi lakini unarudi nyumbani na pesa baada ya mihangaiko.
Iwe mchana au usiku wengi wenu mmekuwa mkiabishwa,kudhalauliwa na kunyanyaswa kwa ajili ya kuzitafutia ridhiki familia zenu.
Baadhi yenu hamjaweza kupata kazi zenye heshima na unapopeleka karanga nyumbani wanakurushia usoni.
Najua mnakuwa mkijinyima ili watoto wenu wapate chakula, nguo, malazi na elimu.
Mara nyingine mmetukanwa na kunyanyaswa na watu mliowazidi umri lakini mmeyachukua maumivu yote kwa ajili ya wake zenu, watoto na wazazi wenu wanaowategemea.
Mara nyingine haijalishi kama unakazi ama laa!, umepeta umekosa, unatakiwa uitunze familia.
Hilo ni jukumu lako kama mwanaume.
Hilo ni jukumu lako kama mwanaume.
Unalipa mahari kubwa ili umuoe mwanamke unaempenda na mara nyingine unajikuta unaitunza familia yake kwa sababu ndugu zake ni ndugu zako pia.
Mnawezaje kufanya hayo yote ya kushĂ ngaza? Ninawaombea bwana Mungu abariki juhudi zenu.
Jasho lenu lisiwe bure. Mwendelee kuishi kwenye mioyo ya mama zenu, wake zenu, watoto wenu na wote muwapendao .
Nawaombea Mungu aendelee kuwabariki kwa upendo wenu usio na kipimo.
NA HII NDIO SABABU NAWAPENDA SANA WANAUME WENZANGU.
By mzee wa fikra mpenda watu Rais wa iramba ii
No comments: