KABLA HAMJAACHANA TAFAKARINI MAMBO HAYA KWANZA

89017597_2759750844061018_2798085702019973120_n.jpg?_nc_cat=106&_nc_sid=110474&_nc_eui2=AeF6Oo85UrIMK4U6hVOdBM7KVEDSWjDVxDHCu8LI42gYcWb08t4Uq2dRY4ZbeBQ5Ehw0PYI7B2pv7kyP60ASagECVF3Y4zsKqEABf-MkchUsSg&_nc_ohc=tl42GB8_yVgAX-fEOkY&_nc_ht=scontent-mrs2-2
Ndoa au mahusiano hugeuka maumivu makali mno na msiba moyoni pale ambapo mtu unaempenda, uliyempa thamani kubwa moyoni na kuwapuuza wengine leo ANAKUSALITI anavunja ahadi zenu mlizojiwekea, anakiuka kiapo chenu kuwa hamtokaa mtengane mpaka kifo ndio kiwatenganishe. Sio bure kama mliku a mnapendana kweli inabidi usikurupuke kukubali na kuridhia maamuzi ya kuachana bali yabidi ufanye uchunguzi ujue chanzo na kiini cha tatizo ujiridhishe nini kinapelekea muachane. Tafakari mambo yafuatayo kwa kina:

1. Jipe nafasi ya kutosha kutafakari kama ni kweli sasa hana maana tena hata kama amekukera

2. Chunguza kwa makini kama kuna hali inayomfanya kuwa hivyo na jaribu kumsaidia aitatue na awe kama mwanzo

3. Orodhesha kila baya na jema na ona upande upi umezidi na hata mmoja ukielemewa angalia wewe umechangia upande upi katika hayo.

4. Kumbuka mahusiano ya kimapenzi sio sawa na mchezo wa ngonjera ambao una wimbo wa kuingilia na wa kutokea. Usitoke na wimbo wa mbwembwe nyingi za kumponda halafu baada ya kuumizwa huko uliko ukaanza kuutafuta wimbo wa kumrudia

5. Mapenzi ni kupitia changamoto na vikwazo mbalimbali mkiwa pamoja na kisha kuyatatua kwa pamoja.

6. Shetani unayemjua ni bora kuliko malaika usiyemjua. Hapa kumbuka hakuna mahusiano yasiyo na matatizo yake hivyo vumilia ulipo.

7. Mapenzi ya mwazo huwa na kila aina ya furaha ingawa ni wachache wanaoweza kubakia na hali hiyo hivyo kuwa na msimamo hapo ulipo

8. Kama unahitaji furaha na mahaba ya dhati anza kwa kutengeneza hapo ulipo usije tegemea kuwa kuna mtu atakupa furaha kabla ya wewe kuitengeneza furaha hiyo.

9. Ushawishi wa zawadi na fedha sio mapenzi kwani hata changudoa siku hizi wanatoa zawadi za pipi ukiwachukua lakini wao wanatengeneza mazingira ya kukukamua hela vyema hivyo

ikubali hali yako.

10. Hakuna hali inayodumu, kama unamkimbia kwa kuwa ni maskini au ana maswahiba yake binafsi kumbuka hayo ni mapito na baada ya kila usiku mchana nao huja na mambo mapya.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.