KWANINI MWANAMKE AKIPENDWA HUISHI MAISHA YENYE FURAHA NA AMANI?.
Soma mkasa huu;
Hii inahusu mwanaume ambae alikuwa hana kazi akaoa mtumishi wa bank ambae alikuwa na mshahara usiopungua $1500 Sawa na pesa ya kitanzania Ml 3.6, ila huyo dada walikuwa wakipendana sana na mumewe na hata kila akipokea mshahara anamkabidhi wote mumewe ili apangie matumizi, huyu dada pia alikuwa akifanya hata kazi za nyumbani kwake kama mama kila atokapo kazini bila kujali kuwa yeye ndo anahudumia familia, japo marafiki walikuwa wakishauri na kumbeza kuwa kwanini ahudumie familia na bado afanye kazi za nyumbani ila yeye hakuacha kumpenda na kumheshimu MUMEWE... Mungu akasaidia pia mumewe akapata kazi, lakini kabla ya kupata kazi Bwana huyu alikuwa akililia moyoni sio kilio cha huzuni ila ni namna gani alimpata MKE MWEMA! Jamaa akakusanya hela akanunua gari jipya akamkabidhi mkewe yeye akaendelea kutumia usafiri wa umma, baada ya mda akanunua gari jingine akamkabidhi mkewe na yeye akawa anatumia lile la zamani, Mungu akawabariki wakajenga wakawa na maisha mazuri na ya furaha, siku moja mke akiwa katika kufanya usafi kabatini, mara akaona file limefichwa kwa siri, akilichukua na alipoliangalia kwa juu limewekwa picha yake ya harusi, akalifungua na akakuta documents za mali yao yote na zikiwa zimeandikwa majina yake, alipogeuza kwa nyuma akakuta picha ya mumewe, na kwa chini yake kuna maneno yameandikwa, "MKE WANGU NDO MAISHA YANGU, MKE WANGU NDO KILA KITU KWANGU". alitokwa na machozi ya furaha, Dada akalia kwa kuona KWANINI MUMEWE ALIAMUA KUFANYA HIVYO? Hii inatifundisha kuwa hakuna magumu yanayodumu milele kikubwa ni uvumilivu na upendo, Lakini tusiitafute AMANI NA FURAHA pasipo kujitoa kwa wenza wetu, Maandiko yanasema KIPIMO UPIMIACHO NDICHO UTAKACHO PIMIWA... Kila nafsi inapenda kuburudika JE WEWE ULIWAHI KUMBURUDISHA MWENZA WAKO? Ikiwa unao moyo wa kushiriki meza moja na MWENZA ASIYE NA KITU BALI ANALO PENDO LA DHATI KWAKO Hebu sema AMEN kuwajenga wengine wasio na IMANI kwamba MUNGU WETU HAKUTUUMBA MASIKINI bali juhudi na kunia mamoja ni ngao kwenye MAHUSIANO NA NDOA ZETU! Hakuna aliyezaliwa na kitu bali TUNATAFUTA.
#Elista_kasema_ila_Sio_she
No comments: