Mambo yanayochangia Upungufu wa nguvu za kiume


 LEO ninataka tuangalie kwa kina mambo yanayochangia tatizo hilo upungufu wa nguvu za kiume. Ningependa tulio katika ndoa, ukishaisoma makala hii tuwahusisishe wenza wetu nyumbani au mpigie rafiki yako na kumueleza kuwa ana nafasi ya kujilinda kupoteza
nguvu za kiume na hivyo kuwa na uhakika wa amani nyumbani.
Nasema amani kwa sababu tatizo hili huingilia amani nyumbani kwani kuna kuhisiwa kuwa mwanaume anajihusisha na nyumba ndogo maarufu. Uzoefu katika vituo vyetu vya Marie

Stopes kina mama ndio huja kutafuta ushauri kwa nini mzee kabadilika na wafanye nini ili kumrudisha nyumbani. Zifuatazo ni sababu amabazo kitaalamu zinatajwa kuchangia kupungua kwa nguvu za kiume na nyingi kama si zote zinaepukika.

Msongo wa mawazo: Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale

watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

1. Unywaji pombe kupita kiasi: Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

2. Unene. Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

3. Kutokufanya mazoezi: Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

5. Matatizo ya kisukari: Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

5. Umri: Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu

nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.