MJINGA vs MJANJA WA MJINI

! MJINGA !
Mjinga akimaliza la saba anaanza biashara ya kuchoma mahindi halafu atauza miwa, atalima viazi huku akikatisha mkaa.
Baada ya miaka miwili mitatu ivi atafungua duka la nguo atasafiri kwenda Dar kufunga mzigo.... Kila hela atakayopata ataitunza kwa nidhamu kuu.
Wafanyabiashara wenzake watamshauri aende benki akachukue mkopo ili akuze biashara yake
Atakubali ataenda benki na watamuuliza tukikukopesha utafanyia nini mkopo huu
Mjinga atajieleza wazi kua akikopeshwa atapanua duka lake, atainunua nyumba aliyopanga fremu kwa ajili ya duka na atanunua fuso la kusomba mzigo wake badala ya kukopa kwani hela anayotumia kulipa kodi na kukodi mafuso ni mara nne ya hela ya kulipa mkopo.
Baada ya miaka miwili mjinga kamaliza deni na kachukua mkopo mwingine kanunua mabasi manne ya kwenda Dar Mbeya Songea na watu watasema ni mchawi kaua wazazi wake wakati walikufa wakiwa na umri wa miaka kati ya 85 - 109
#MJANJA WA MJINI#
Huyu atapiga misheni town na kufanikiwa kuchukua mkopo mkubwa huku akiweka hati ya nyumba ya urithi kama dhamana.... Akiishapata mkopo atanunua BMW X6 ya kupigia misele akitanua na michepuko na ataitisha bonge la pati kujipongeza kupata mkopo.... Atatesa sana mjini kila kona .
Hela itakapokaribia kuisha atainvest kwenye biashara ya madini atauziwa vichupa akiambiwa almasi..... Baada ya miaka miwili atafilisiwa na nyumba itapigwa mnada na atasema karogwa %MSOMI SASA%
Huyu atafanya kazi weee lakini hakuna savings kwani kila anachoingiza kina matumizi yake kisomi..... Atakapochoka kuteswa mjini atachukua mkopo...... Atanunua gari ya familia.... Ataezeka nyumba yake ya mbezi.... Atabaki na deni la kulipa mpaka amalize huku akiandamwa na barua za default.. Huyu hana wa kumlaumu ila ujuaji wake... Wakuu
Tumheshimu mjinga., Ana nidhamu ya hela na kipaji cha biashara... Kupata hela sio kazi bali kuitunza na kuiheshimu.




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.