MKATAE MTU ANAE KUFANYA KITAFUNIOš„ KWANI ANAKUPOTEZEA MUDA WAKO!
Ni rahisi kuinywa chai☕ kavu kuliko kula kitafunwaš„ bila chaišµ au majiš„ Kwanini nasema hivyoš¤·š½♂ Mtu anapokufanya wewe wa mpito maana yake wewe sio lazima utembee nae kwenye maisha yake, Yaani hata usipokuwepo yeye maisha yake yanasonga, Ni hatari kukutana na mtu ambaye kwa akili yake ameji-tune kuwa nawe kwa sababu zake tu wala sababu hizo hazimfanyi asiendelee bila wewe, Unajua siri iliyoko ndani ya MOYO wa mwenzio ni ngumu sana kuijua, Maneno matupu hayaleti uhalisia wa yaliyojificha ndani yake, Leo nataka nikutofautishie Kati ya mambo matatu muhimu kwenye MAHUSIANO;
■ KUJITOA
■ KUSHIRIKI
■ MUDA
Nitachambua kwa ufupi sana ila naomba unielewe, KUJITOA ni kumtekelezea MwenZio kile anahitaji, Mtu akijitoa anaweza kutajwa ni MOYO kwa kufanya hivyo, KUSHIRIKI ni kuwa upande wa kile ambacho kiko mbele ya mwenzio, Mtu anaposhiriki jambo la mwenzie maana yake anatajwa kuwa na MOYO kwa kutenda hilo, MUDA ni kusimamisha ya kwako ili uwe na mwenzio na kwa tendo hilo ni MOYO umemtuma kutenda hilo... Yote ni Mazuri kati ya hayo lakini lililo na nguvu kuliko yote ni moja tu KUSHIRIKI! Mtu anaposhiriki ujue KAJITOA Kwani huwezi kushiriki bila kujitoa ushiriki, wala huwezi KUSHIRIKI bila MUDA kwa maana hiyo huwezi kushiriki bila kuwa na Muda, Ni nani AMESHIRIKI NAWE?
Kumpata ambaye atashiriki nawe maana yake atakupa MUDA WAKE Lakini pia ATAJITOA KWAKO... Pendelea zaidi mtu wa KUSHIRIKI kuliko anaejitoa bila kushiriki maana wengi hujitoa wala wasishiriki, Ni bora ashiriki ndani utaona kujitoa na atakupa Muda wake, Kataa kuwa kitafunwa Kwani HUWEZI KUONA AKISHIRIKI ila kwa sababu zake anaweza KUJITOA kwa sababu anazo sababu zake.
#Elista_kasema_ila_Sio_she
No comments: