NANI KAKWAMBIA UTAMU WA DODO NI KULA NA MAGANDA???


SILAHA ya mwanamke ni kujua kuchamba haswa kama unayo maneno bibi. Sio unamchamba mtu kwa maneno ya kwenye kamusi inahusu? Katu bibi wee, mi nakuchamba kwa maneno ya Uswahilini upo hapo? Eeeh, nazungumza na nyinyi msio na haya wala hamjui vibaya… kutwa kiguu na njia kutafuta madanga mjini. Tena madanga yenyewe mmezidisha staili kwa vikorombwezo vya kuruka ukuta, huu si uchuro? Mna hatari nyinyi hadi nawaogopa!
Hivi ni nani aliwaroga nyie waja msiojua vibaya? Somo wenu nani nyinyi wenzetu labda tumjue, tumpe vidongo vyake maana huyu mwalimu wenu ni sawa na kipofu. Mnajidhalilisha, mnaharibu miili yenu kwa starehe za kupita.
Ata kama ndio njaa, bibi ifike mahali jamani wanawake wenzangu tuseme na njaa zetu. Unajiona mjanja kuruka ukuta, umejiandaaje uzeeni kwako? Niulizeni mimi mwenzenu sina hamu na michezo hiyo maana nilishaelezwa madhara yake enzi zangu.
Acheni kujitoa ufahamu, mtakuja juta. Nani kakwambia utamu wa dodo ni kula na maganda yake? Mwanamke uwe na nakshi za kulimenya, kulikatakata na kuliweka kwenye sahani, upo hapo bibi? Eeh hata mua sio kula tu sehemu laini, kuna utamu wake wa kuchanganya na fundo.
Shoga nakupasha upashike bibi mchana kweupe, tumia akili ya kuzaliwa kuyafanya maisha yawe rahisi. Mwanaume kama kapanga kukusaliti atakusaliti tu. Cha msingi wewe timiza majukumu yako tu kucheza vizuri kunako sita kwa sita.
Mpe raha za mwanzo, katikati na mwisho. Sio mwanamke unaingia tu kwenye segere unalianza kulicheza goma. Hujaandaa uwanja, hujakoroga uji uwe mlaini, wewe huyo tu unaanza kusonga ugali. Nikwambie ukweli utaaibika, utaolewa mchana, usiku utaachika bibi.
Raha ya ndizi ujue kuimenya sio kula na maganda yake bibi. Tena kuimenya sio kama vile unagombana na mwizi au unaenda kumdai mtu aliyekataa kulipa vikoba! Mikono yako iwe laini na inamenya taratibu kama hutaki vile. Ikiwezekana imba nyimbo laini kwenye maiki, sio mbaya kuliko kuruka ukuta.
Utamfurahisha huyo anayependa ufirauni huo, lakini ukikutana na mwingine atakuona hufai kanisani wala msikitini. Wewe ni zaidi ya pepo aliyekemewa na Yesu kwenye vitabu vya dini. Bibi starehe zipo nyingi ila sio hiyo ya kujidhalilisha.
Niulizeni mimi enzi zangu mwanaume hapindui, akija kwangu hatoki kirahisi. Najua kumpetipeti, kumpa madikodiko na mechi zilizokwenda shule. Raha ya mechi mabao, nilikuwa nachenga kama Messi. Najua kuimba na kipaza sauti, najua kukaa mkao wa burudani na nyimbo kama zote.
Mechi zangu zilikuwa na maandalizi, magoli kama yote. Ndio magoli mengi tu mwanaume lazima anifunge, najua kumshawishi. Sasa akishafunga magoli ya kutosha kuna nini tena? Hizo nguvu za kutaka kuruka ukuta anazitoa wapi kwa mfano? Haloooo, amkeni na muache michezo ya hatari kwa afya zenu.




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.