NGOJA NISEME NA WEWE BINTI AU WEWE DADA
Tatizo kubwa la wanawake nikuwa wakishazaa na mwanaume Romantiki wanadhani nilazima waolewe wao ndipo wanajipa presha kuwa tuna mtoto wa miaka mitatu hataki kuja kujitambulisha kwetu. Unalazimisha akajitambulishe ajulikane, iko hivi kubeba mimba yake ni kiherehere chako haina uhusiano na kuoana, kama angetaka kukuoa asingesubiri mimba agenda moja kwa moja.
Hivyo usikae unasubiria miaka nenda miaka rudi eti kwakua umezaa naye ndiyo ukajiozesha. Inawezekana kuna wengine kama wewe nao wamezalishwa, wanahudumiwa kama wewe na wao wana matumaini ya ndoa kama wewe. kwa maana hiyo badala ya kuuliza unakuja lini kwetu kujitambulisha basi uliza, hivi ni mimi utanioa au kuna mwingine, akikujibu ndiyo muambie kabisa kuwa kuna mtoto, sidhani kama kuna kitu kingine cha kunichunguza.
Nipe ratiba yako na si mambo ya kesho, sijui mpaka nijenge, sijui mpaka nifanye hiki au kile. Umeshazalishwa acha kuruhusu kudanganywa muda mrefu ndiyo uachwe, utaumia zaidi kwakua una mtoto na ile kuzaa tu unaona kama ni mke hivyo akija akikuacha basi utaona kama vile umetalikiwa. Bora kujua mapema, kama ni ahadi hazieleweki kila siku kesho kila siku kesho kutwa muambie Baba kwaheri kajipange ukiwa tayari mimi utanikuta.
Ninachosema hapa nikuwa si lazima mwanaume uliyezaa naye akuoe, lakini pia kama umezaa na mwanauem ushakua mtu mzima, acha kusubiri miaka miwili mwanaume kuja kwenu kujitambulisha. Chukua maamuzi magumu kama haeleweki anza maisha yako bila yeye kubali kuwa u single mother endelea na maisha, ni ngumu lakini itakua ngumu zaidi pakle ashakuzalisha mtoto wapili halafu anakuambia kwetu wamesema nioe kabila flani.
Inauma zaidi pale ashakuzalisha mtoto wa pili uasikia kuna mwingine naye kazalishwa huko na kahamishia majeshi huko. Ndugu yangu punguza kuvumilia kwa muda mrefu, jipe muda wako kama haeleweki hajajipanga endelea na maisha yako. Kumbuka kuwa kuna wanaume wa shenzi, anajua kabisa hatakuoa hata kwa bahati mbaya lakini ukimchekea anakuzalisha watoto watatu, anakutelekeza na kuoa mwingine na hata kuhudumia hahudumii!
No comments: