NI KWANINI WANAWAKE WAZURI WENGI WAO HAWAOLEWI???

SOTE tunakubaliana au tunafahamu kwamba hakuna mwanamke mbaya. Ila katika mazingira ya kawaida wapo ambao wanakuwa na umbo fulani la kuvutia zaidi ya wengine. 
Kuna wanawake ambao wana mwonekano wa kuwa kama vile pambo. Kwa kawaida, wanawake wa aina hii huwa wanakuwa na kasumba zao. Ule uzuri huwa unawazuzua mno akili zao kutokana na vile ambavyo anaona, kila mwanaume anayekutana naye anamuwewesekea. Anapata jeuri ya kuona kwamba yeye ni mzuri.

Hapo ndipo kichwa kinapovimba. Anapata kiburi kama chote kwamba hawezi kubabaishwa na mwanaume. Akiachwa leo, kesho tu atapata mwanaume mwingine. Na huyo mwingine naye akizingua, atapata mwingine haraka tu bila kujua kuwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa, huwa wanazingatia zaidi tabia na siyo uzuri.

Mwanamke akiwa na mtindo wa maisha ambao haumuwezeshi kutulia na mwanaume mmoja, basi asitarajie kupata mwanaume wa kumuoa kirahisi. Anafahamu soko lake ni kubwa kuliko wengine, hivyo ni ngumu mno kuwa na hofu ya kukosa mwanaume wa kumuoa. Anajikuta yeye ni mtu wa wanaume tofautitofauti, kutulia na mmoja hawezi.
Ndugu zangu, aina hii ya maisha ilivyozoeleka ndiyo imezua kasumba kwamba mwanamke mzuri hawezi kuolewa. Wanaume wengi wamejazana maneno kwamba, wanawake wa aina hii ni viburudisho tu. Wanawake wa kuoa wapo wengi, lakini si wao.

Mtu anakuwa na mkewe nyumbani wa kawaida sana, lakini nje anakuwa kiburudisho cha aina hiyo ili kusuuza moyo wake. Nyumbani anaye wa kuishi na kuzaa naye watoto. Kiburudisho kinatumika kwa wakati tu anapokuwa anataka kuburudika.

Mathalan anataka kutoka kwenda viwanja vya starehe, kwenda mahali ambapo ataonekana ana mwanamke mzuri ambaye wengine pia watammezea mate. Atamtumia kwa siku hiyo, halafu mwisho wa siku anamuacha, anarudi kwa mkewe.

Lakini hapa tutafakari pamoja, ni kweli kwamba wanawake wazuri hawafai kuolewa? Kwamba ni kweli wanaume wote wana mawazo hayo? Je,  ni kweli wanawake hawa wazuri nao wameridhika na kasumba hiyo kwamba wao ni wa kutumika tu?

Watatumika na wanaume hadi lini? Mustakabali wa maisha yao utakuwa ni nini hapo baadaye? Hii siyo sawa, hili suala huletwa na akili ya mwanamke mwenyewe. Mifano ipo mingi tu. Wapo wanawake wazuri mno ambao wameolewa na ndoa zao hazina vurugu zozote.
Walifanikiwa kivipi? Kujitambua. Walijua thamani yao. Mwanamke si chombo cha starehe, mwanamke anapaswa kuheshimika. Kumbe pamoja na uzuri, heshima yake ni kitu cha msingi zaidi. Wewe kama ni mzuri, huna sababu ya kuutumia uzuri huo vibaya.

Ukifanya hivyo ni tabia yako mwenyewe na ni uamuzi wako binafsi. Unaleta tu sura mbaya kwa wanawake wa aina yako, lakini si kwamba wote ndiyo wapo hivyo. Wapo wanawake ni wazuri, lakini wanajiheshimu, wanavaa vizuri na wanaishi kwenye ndoa miaka nenda rudi.

Achana na kasumba ya kwamba mwanamke mzuri hafai kuolewa, anafaa sana. Kikubwa ni akili ya mwanamke mwenyewe. Akichagua kuwa chombo cha kutumika ni yeye, akiamua kutulizana pia inawezekana kabisa.

Anayejitambua, atajiheshimu, ataitafuta thamani ya mwanamke kuolewa. Atajitunza, atavaa mavazi ya kujisitiri. Kichwa chake hakita-chetuka kwa kuona anato-ngozwa sana. Zaidi atam-chagua mmoja mwa-minifu na mwenye mapenzi ya kweli, basi atafanya naye maisha.




USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.