Nilichojifunza kupitia kibwagizo cha Upepo wa kisulisuli
Kuna kibwagizo ambacho kimendelea kukamata vilivyo katika utawala wa mitandao ya kijamii kibwagizo cha " Upepo wa Kisulisuli" kupitia kibwagizo hicho nimejifunza vitu vifutavyo:
1. Katika kizazi hiki kuna changamoto kubwa kuwa vijana wengi wa kiume wameandaliwa kuwa wavulana; Wala sio wanaume. ndiye maana siyo rahisi kwa vijana wa kiume kuweza kuoa, wengi wa vijana tangu kidato cha kwanza wako boarding school hawajui hata namna familia inavyoendeshwa ukiwambia kuoa kwao ni msamiati mpya.
2. Wengi wa wazazi/walezi hawajandaa vijana katika namna ya kuweza kuwa mke na Mume; ni wazazi wachache ambao huwa wanapata muda ama wanatenga muda wa kuongea na vijana wao kuhusu wajibu ulio mbele yao wa kuwa mke na Mume kwa hiyo mbele wanaona Giza.
3. Vijana hawajijitengezea tabia za kuolewa ama kuowa: hakuna mtu ambaye anapenda mtu Bila sababu labda MUNGU pekee, mojawapo ya sababu itayovuta ama kufukuza watu kwenye maisha yako ni tabia,mabinti wengi, vijana wengi ukiangalia tabia zao unaona kabisa hakuna waowaji Wala waolewaji labda wadangaji.
4. Jamii inatengeza watu kuwa kwenye mahusiano wala sio watu wa kuwa kwenye ndoa. Jamii kwa sasa imetengeza watu ambao kwa kijana wa kiume kudate na wasichana kumi kuisha kuwatelekeza ni jambo la kawaida, kuwa na mahusiano kisa kuachana ni jambo la kawaida.
Mimi nafikiri kama mambo hayo machache yakirekebishwa na mengine yanayofanana na hayo nafikili misururu ya wadada wa kutaka maombi ya kuolewa,na misururu ya vijana kutafuta wake sahihi itapungua asanteni naomba kuwasilisha.

No comments: