Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? Sehemu Ya 45


Safari ilikuwa moja kwa moja hadi hospitali ambapo Sabrina alikuja kuchukuliwa upesi kama mgonjwa mahututi na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha daktari kwa matibabu.
Sam alitulia nje akingoja majibu huku akijikuta kuongea peke yake, daktari alimuita ili kumuhoji kidogo kuhusu kilichompata mkewe.
"Kwani imekuwaje Mr. Sam?"
"Kwakweli daktari sielewi, sijui kama alianguka au ilikuwaje"
"Wewe niambie tu unavyo elewa wewe"
"Ninachokumbuka ni kuwa, mimi nilienda kulala na kumuacha mke wangu sebleni. Nilipoamka asubuhi sikumuona chumbani na kuamua kwenda kumuangalia sebleni. Ndio hivyo nikamkuta yupo chini na damu zimetapakaa"
Daktari akasikitika kwa kutingisha kichwa kisha akamwambia Sam,
"Pole sana Bwana Sam"
Sam akashtuka na kuuliza kwa tahamaki,
"Vipi tena, mke wangu amekufa?"
Daktari alimuona Sam akinyong'onyea kabisa na gafla akaanguka na kupoteza fahamu.
Daktari akawa na kazi mbili sasa ya kumshughulikia Sabrina na kumshughulikia Sam.

Sakina akiwa nyumbani kwake, alijikuta akitaka kwenda nyumbani kwa Sabrina ili kumshauri zaidi kuhusu swala la kwenda kwa mtaalamu.
Akajaribu kuipiga simu yake ila haikupatikana,
"Atakuwa kwake tu, naenda hivyo hivyo"
Sakina akajiandaa na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa Sabrina.

Sakina alifika na kumkuta yule mlinzi akiwa getini kama kawaida,
"Sabrina yupo ndani?"
"Sijui, inawezekana yupo"
"Yani hujui kama yupo au hayupo? Kheee mnaishije humu?"
"Tunaishi kawaida tu, ila mzee asubuhi aliondoka kwa kasi sana, nadhani alikuwa akiwahi ofisini. Mama atakuwepo tu ndani"
Sakina akaingia na kuanza kuifata nyumba ilipo, kadri alivyozidi kusogea akasikia sauti ya mtoto inayoonekana alilia sana na inaelekea kukauka.
Sakina akashangaa kuwa iweje Sabrina amuache mtoto alie kiasi kile.
Alipofika mlangoni akagonga ila mlango haukufunguliwa na kujaribu kuita ila hakuitikiwa.
Akajaribu kufungua mlango na kuona ukifunguka hata kushangaa kuwa kumbe mlango ulikuwa wazi.
Alitembea hadi sebleni na kuona zile damu pale chini, akashtuka na kushangaa.
Aliposikilizia sauti ya mtoto akagundua kuwa ile sauti inatokea chumbani.
Akasogea na kugonga kisha kuita ila hakuitikiwa na kumfanya ajipe ujasiri wa kufungua mlango na kuingia.
Alimuona mtoto kitandani akionekana kulia sana hadi kuanza kukaukiwa na sauti.
Alimchukua na kumbeba mgongoni ila bado hakuelewa kilichotokea, aliamua kutoka na mtoto tu ili kwenda nae nyumbani kwake.

Wakati anatoka getini, mlinzi hata hakuwa na habari yoyote ila Sakina nae alitoka bila hata ya kumuaga wala kumuuliza chochote na kuondoka zake.
Alifika kwake na kumtafutia maziwa kwanza mtoto yule kisha kumnyeshwa ambapo alikunywa na kulala kisha Sakina akaanza kumkorogea uji.
Alijikuta akijiuliza maswali bila ya majibu,
"Kweli utajiri hauna maana, mlinzi kama yule anafaida gani ndani? Mlinzi asiyejua kama bosi wake yupo au hayupo? Na huyu Sabrina kapatwa na nini? Simu yake haipatikani wala mumewe hapokei simu. Hawa watu wanajielewa kweli? Unamuachaje mtoto mdogo kama huyu ndani peke yake?"
Alisikitika sana huku akiendelea kukoroga ule uji ili akishtuka ampe kisha aende kwa mama wa Sabrina kumuhabarisha.

Mama wa Sabrina na mumewe wakiwa nyumbani bila wasiwasi wowote wala taarifa yoyote.
Alishangaa kupigiwa simu na kuambiwa kuhusu hali ya mtoto wao na mkwe wao.
Ile simu iliwafanya waondoke pale nyumbani kwa haraka kuelekea hospitali.

Walifika hospitali na kukuta Sam ameshazinduka kwa muda huo kwa huduma aliyopewa, ila hawakutaka kumsumbua kwanza kwa kumuuliza maswali kwahiyo wakaacha apumzike kidogo.
Wakamuuliza daktari kuhusu mtoto,
"Mmh hawajaja na mtoto hapa"
Wakajiuliza kwa haraka haraka kuwa mtoto atakuwa wapi na jibu lao likawaelekeza kuwa lazima ameachwa nyumbani,
"Maskini mjukuu wangu ameachwa peke yake"
Ikabidi wajihimu ili kwenda kumuangalia mtoto.

Walifika kwa nyumbani kwa Sam, kama kawaida mlinzi aliwafungulia mlango na moja kwa moja wakaingia ndani tena bila ya kumuuliza chochote kile.
Ila ndani hawakukuta mtoto na kufanya watoke na kwenda kumuuliza mlinzi,
"Eti mtoto yuko wapi?"
"Mtoto! Si yupo na mama yake"
"Hivi akili yako ni nzima kweli? Unajua mama yake alipo"
"Si yupo ndani"
Ikabidi wamueleweshe kuwa yupo hospitali ila mlinzi alikuwa akishangaa tu,
"Sio unashangaa, mtoto yuko wapi?"
"Nimekumbuka, atakuwa ameondoka na yule dada wa mama mwenye nyumba"
"Dada wa mama mwenye nyumba? Yupi huyo, kwani kulikuwa na msichana wa kazi humu?"
"Hapana, ila aliyekuja kumchukua ni yule dada kabisa wa mama"
"Kivipi mbona hueleweki?"
"Namaanisha dada wa Sabrina, yule dada yake kabisa"
"Sabrina ana dada? Dada yupi? Tuna mtoto mmoja tu wa kike huyo dada ni dada yupi? Anaitwa nani?"
"Jina lake limenitoka ila linafanana na jina la mama humu"
Wakafikiria kwa haraka haraka na kuhisi kuwa huyo mtu lazima atakuwa Sakina tu kisha wakaondoka mahali pale.

Sakina alipompa yule mtoto uji, alijikuta akimuangalia sana hata hisia zake zikampeleka mbali.
Akakumbuka kipindi Jeff alivyokuwa mdogo, alivyokuwa akimlisha, anavyofanya. Alijikuta akiguna tu,
"Mmh ila huyu mtoto kafanana na mwanangu jamani, yani kila kitu kama mwanangu Jeff kasoro tu huyu ni wa kike ila kafanana sana na mwanangu"
Alikuwa akimuangalia sana na kuona kamavile amembeba Jeff mdogo,
"Sijui Dorry akijifungua mtoto atafanana na mwanangu kama hivi! Mmh duniani wawili wawili ila kwanini mtoto wa Sabrina ndio afanane kiasi hiki na mwanangu Jeff?"
Alijiuliza sana ila mwisho wa siku aliamua kukubaliana tu na hali halisi kuwa mtoto yule ni wa Sam na Sabrina.
Wakati akifikiria hayo, walifika wazazi wa Sabrina na kumkuta Sakina akimpa uji yule mtoto.
Wakashukuru sana pale na kuamua kumuaga Sakina kwani waliamini kuwa sasa mtoto yupo kwenye mikono salama.
"Yani nilijaribu kuwapigia lakini simu iliita tu bila ya kupokelewa"
"Kuchanganyikiwa mwanangu yani simu tumeacha nyumbani"
Basi Sakina akawaaga pale ili waweze kuwahi kumuona Sabrina.
Wakati wanatoka, wakapishana na Dorry ambaye alikuwa anaingia nyumbani kwa Sakina, akawasalimia pale kisha na wao kuondoka.

Dorry alitulia kidogo na kumsalimia Sakina ambapo alifurahi sana kumuona.
Ila alimshangaa yule mtoto,
"Mtoto wa nani huyo mama?"
"Mtoto wa mdogo wangu huyu, mzuri eeh!"
"Ndio ni mzuri, kafanana na Jeff huyo balaa"
Sakina akamuangalia yule mtoto tena na kutabasamu.
"Ni kweli kafanana na Jeff hata mi nimeliona hilo mwanangu."
"Kwani Jeff kafanana na nani kwenye ukoo wenu? Maana damu yake itakuwa kali sana kumfananisha ndugu yake namna hii"
Sakina akaguna kidogo na kusema,
"Natumaini hata huyo mjukuu wangu atafanana nae kwa vizuri sana maana damu ya mwanangu ni kali kwakweli"
Dorry akaitikia kwa kutikisa kichwa na kumfanya Sakina amuangalie kwa jicho la wasiwasi kidogo kisha kuendelea na mambo mengine.

Hali ya Sabrina haikuwa nzuri sana, na wote walikuwa wakingoja majibu ya daktari kuhusu hali yake.
Daktari hakuwaambia moja kwa moja na kufanya wazidi kusubiri.
Kwavile Sam alikuwa tayari anajitambua, wazazi wa Sabrina waliamua kutumia nafasi hiyo kumuuliza kilichotokea ila aliwajibu kama ambavyo alimjibu daktari alipoulizwa kuhusu swala hilo.
"Sasa sijui tatizo ni nini hapo. Haya mambo ni makubwa sana"
Wakapeana moyo na kuendelea kusikilizia hali ya Sabrina.

Sakina akiwa pale nyumbani na Dorry muda kidogo akapigiwa simu na mtoto wake na kumfanya afurahi sana,
"Tena leo nipo na Dorry hapa"
"Aah sawa ila hana umuhimu kwangu"
"Hana umuhimu kivipi wakati ana mzigo wako!"
"Mzigo wangu? Mzigo gani?"
Sakina akapewa ishara na Dorry kuwa asiseme chochote, alibadilisha mada ila hakuelewa kwanini amemzuia kusema,
"Mbona umekaa kimya mama? Achana na Dorry huyo hanihusu. Ila naomba nikuulize, mbona mamdogo Sabrina hapatikani?"
Sakina aliamua kumueleza Jeff hali halisi ilivyo na kuhusu mtoto wa Sabrina kuwa yupo nae pale.
"Maskini mamdogo jamani, ndiomana jana moyo uliniuma sana. Tafadhari mama kaa vizuri na huyo mtoto Cherry"
"Usijali mwanangu"
Kisha simu ikakatika, Sakina aliamua kumuuliza Dorry kuwa kwanini hataki Jeff aambiwe ukweli kuwa ana mimba yake,
"Mama, nataka kumfanyia Jeff surprise. Nataka siku akirudi twende uwanja wa ndege na mwanae kumpokea"
Sakina akatabasamu na kuona kuwa Dorry yupo sahihi.

Shangazi wa Sabrina naye aliitumia siku hii kwa kumuita James ambaye ni kaka wa Sabrina kwa lengo la kumkomesha wifi yake.
"James, unaniamini mimi?"
"Ndio nakuamini shangazi"
"Basi kwa ufupi tu, mimi ni shangazi yako jina yani sio kwa damu. Na yule baba yako nae ndio hivyo hivyo"
"Sikuelewi shangazi! Unamaana gani?"
"Deo sio baba yako mzazi"
James alijikuta akishtuka sana na kujishika kifuani na muda huo huo akaanguka chini.

Wazazi wa Sabrina wakiwa pale hospitali, daktari aliwaita pamoja na Sam ili kuwaambia hali ya Sabrina ilivyo.
"Jamani, nina habari mbaya kidogo ya kuhusu Sabrina"
Wote wakashtuka kusikia habari mbaya.

Wazazi wa Sabrina wakiwa pale hospitali, daktari
aliwaita pamoja na Sam ili kuwaambia hali ya
Sabrina ilivyo.
"Jamani, nina habari mbaya kidogo ya kuhusu
Sabrina"
Wote wakashtuka kusikia habari mbaya.
Mama wa Sabrina akamkazia daktari macho kamavile anamtishia kama akitoa habari mbaya.
Daktari akapumua kidogo na kumuangalia mama wa Sabrina kisha akasema,
"Sio mbaya sana jamani ndiomana nimesema kidogo. Msiniangalie kwa macho makali kiasi hicho"
"Basi tuambie daktari"
"Kwasasa Sabrina ameamka, ni jambo la kumshukuru Mungu ila tatizo ni kuwa amepoteza kumbukumbu yani kwakifupi hajui chochote kuhusu yeye wala nani"
Wote wakapumua kidogo, kisha Sam akauliza,
"Kwani kwa uchunguzi wako daktari umegundua kuwa tatizo ni nini?"
"Inaonekana alivyoanguka aliumia maeneo ya kichwani ndiomana kumbukumbu zimepotea. Kwahiyo mtakapoingia kumuona mchukulieni kama alivyo na mjitahidi kumuelekeza yale ya msingi ili iwe rahisi kwa yeye kurudisha kumbukumbu zake."
Wakakubaliana pale na daktari kisha akawapeleka kwenda kumuona Sabrina.
Na kweli walimkuta akiwashangaa tu, kwavile na giza nalo liliingia wakaamua wamuache apumzike kwanza.
Wakaongea na daktari na kuona kuwa ni vyema waje kesho kwaajili ya kumuelekeza kuhusu familia yake.
Kwahiyo wakaaga na kuondoka pale hospitali.

Moja kwa moja kabla ya kwenda kokote, sam alihitaji kumuona mtoto wake kuwa anaendeleaje, kwahiyo wote wakaelekea nyumbani kwa Sakina.
Walifika na kumkuta Sakina akiwa amembeba mtoto yule mgongoni.
"Yani katoka kuamka muda sio mrefu utafikiri amenusa kuwa mnakuja. Karibuni sana"
Sam alimchukua mwanae, kisha wakamueleza hali ya Sabrina na kumshukuru kisha kumuaga.
Ila Sakina akamwambia mama wa Sabrina,
"Si mtaondoka kesho asubuhi?"
"Ndio, kesho asubuhi"
"Basi tutaenda wote, na msihangaike chakula cha mtoto mi nitakiandaa"
Wakakubaliana pale kisha kuondoka na kumruhusu Sam kuelekea kwake, na wao kurudi na mtoto nyumbani.

Sam akiwa njiani kwenda kwake, akajiwa na mawazo ya gafla kuwa kwanini Sakina anaonekana kujali sana kuhusu yule mtoto.
"Au anajua kama ni mjukuu wake? Mmmh inawezekana anaujua ukweli yule ila sidhani"
Alijifikiria sana na kujipa maswali sana kuhusu Sakina kujua ukweli kuhusu Sabrina na Jeff.
"Mmh! Nadhani hajui, maana angejua basi lazima angeropoka kwangu"
Alienda na mawazo hivyo hadi nyumbani kwake.
Alipofika tu nyumbani kwake, akamkuta yule mlinzi getini na kumuona mdada aliyemzoea pale pale.
Mdada huyo alikuwa ni Neema.
Sam aliingiza gari yake ndani kisha akashuka na kwenda kumsalimia Neema pamoja na kumkaribisha.
"Karibu sana Neema"
Kisha akaongozana nae hadi ndani kwake.
Neema akashtuka kuona ile damu chini pale na kumuuliza Sam kilichotokea.
Sam akamueleza kama alivyowaeleza wazazi wa Sabrina na daktari, Neema akasikitika sana kisha akachukua maji na dekio na kusafisha pale sebleni.
Muda wote Sam alikuwa akimuangalia tu Neema anavyojishughulisha.
Alipomaliza, Sam akamshukuru na kumwambia,
"Asante Neema"
"Aah usijali, ni lazima nikusaidie. Wewe ni rafiki yangu bwana"
Kisha akamuuliza,
"Hivi umekula kweli?"
Sam akatikisa kichwa kuonyesha kwamba bado hajala.
"Basi ngoja nikaangalie cha kuandaa nipike ule"
"Hapana Neema, usihangaike juu ya hilo. Acha tu tukale kwenye hoteli"
"Hapana, leo utakula nitakachokuandalia mimi"
"Hapana Neema"
Ikabidi Neema asimlazimishe sana na kukubaliana nae kwenda kula hotelini.

Muda kidogo waliondoka pale na kwenda hotelini kula.
Wakati wanakula, Neema akasema tena,
"Ila mi sijapenda kuja kula huku wakati kwako pale una jiko. Ila sio tatizo ipo siku nitakuandalia"
Walipomaliza kula, Sam aliamua kumrudisha kwanza Neema nyumbani kwake kisha yeye kurudi kwake.

Ingawa ilikuwa ni usiku tayari, ila Neema alihitaji sana japo ushauri tu kuhusu Sam.
Na moja kwa moja usiku ule ule akaenda kwa rafiki yake Rose, mtu aliyemuamini kuliko wote.
"Nipe ushauri rafiki yangu tafadhari maana haya mambo yananishinda"
"Kwahiyo wewe unampenda sana huyo mwanaume hadi unatamani uwe mke wa pili!"
"Ndio nampenda sana ila kila ninachofanya imekuwa ni kawaida tu yani haiwi vile ninavyotaka mimi"
"Usijali, nitakupeleka kwa mtaalamu matata huko juu, ila twende kesho alfajiri sawa!"
"Sawa, ila hata yule wa mwanzo alikuwa matata, mbona limefanikiwa lile dili la mwanzo"
"Kwahiyo mkewe kalazwa kweli?"
"Ndio, kwisha khabari yake na kumbukumbu kapoteza"
"Wow, hiyo ni hatua nzuri sasa. Kilichobaki ni rahisi, kumdaka tu huyu mwanaume na huyo mkewe akirudiwa na fahamu anashangaa kuwa tayari upo mke mwenza. Kwani mtaalamu mwanzoni alisema itakuwaje hadi mke alazwe?"
"Mtaalamu alisema kuwa, popote yule mwanamke atakapoanguka hata kama akianguka kidogo basi ndio hapo hapo ugonjwa utampata. Na ndivyo ilivyokuwa kwa huyu mke wa Sam"
Wakafurahi kwa ule ushindi wa awali na kusubiri ushindi wa pili sasa utakaowezesha Sam kuwa upande wao.

Sam alirudi nyumbani na kumfikiria mkewe Sabrina, pia alifikiria kuhusu Neema,
"Huyu ndio mwanamke sasa, anajua kusafisha nyumba na kumjali mwanaume. Ila ndio hivyo nishaoa tayari"
Aliamua kwenda kulala sasa.
Wakati amelala akajiwa na njozi, akamuona Sabrina akiwa sebleni pale, akamuona alivyoanguka.
Mara gafla akaona kitu kama upepo kikimnyanyua Sabrina na kumponda tena pale chini.
Sam akashtuka sana kutoka usingizini huku akitetemeka na kujiuliza kama kuna ukweli wowote kwa kitu alichokiota.
"Mungu wangu, mtoto wa Sabrina tumboni atakuwa mzima kweli? Huo upepo je ni nini? Au mauzauza yangu tu!"
Hakuweza kulala tena, hadi kunakucha.
Asubuhi na mapema alidamka na kuelekea hospitali kumuona Sabrina.

Alipofika aliwakukuta wazazi wa Sabrina wakiwa na Sakina nao wamefika muda sio mrefu.
Aliwasalimia pale kisha wakaongozana wote kwenda kumuona Sabrina ambaye bado hakuwa na fahamu kabisa, kwahiyo wote kwake aliwaona ni wageni.
Walijaribu kukaa nae karibu na kumwambia baadhi ya mambo, wakampa mtoto wake amshike kidogo.
"Mmh! Mimi nina mtoto? Aah mnanitania nyie"
Wakamsikitikia kwani Sabrina hakujielewa kabisa.
Wakamuuliza daktari uwezekano wa kurudi nyumbani na Sabrina,
"Huyu tutamruhusu kesho au keshokutwa, ngoja tuangalie hali yake kwanza"
Basi wakakaa pale na kuondoka huku wakipanga kurudi jioni, ila Sam hakuondoka alikuwa pale pale hospitali kumuangalia Sabrina.

Muda kidogo Sam akapigiwa simu na Neema,
"Vipi Sam umekula?"
"Hapana, bado sijala"
"Basi usijali, leo nimekuandalia chakula kizuri sana. Naomba ufike kwangu tafadhari"
Sam hakutaka kukataa kwani akaona kuwa atamfanya Neema ajihisi vibaya na kuamua kwenda nyumbani kwa Neema.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Na alipofika tu akaandaliwa chakula na Neema na kuanza kula huku wakibadilishana mawazo.
"Inaonekana unampenda sana mkeo Sam"
"Ni kweli nampenda sana na sitegemei kumpenda mwanamke mwingine yeyote kama ninavyompenda Sabrina"
"Hongera zake maana ni wanaume wachache sana wenye upendo wa namna hiyo"
Sam akatabasamu, kisha akamuaga Neema kuwa anarudi hospitali kumuangalia Sabrina.

Sam alipoondoka tu, Neema akaenda tena kwa rafiki yake Rose.
"Mbona kama dawa haijafanya kazi dada?"
"Kwanini?"
"Sam alikuja, kala kile chakula nilichomuwekea dawa ila cha kushangaza kaniaga na kuniambia kuwa anarudi hospitali kumuangalia mkewe"
"Usijali mdogo wangu, kila kitu taratibu. Hebu tuangalie hadi kesho, kama ikibuma tuwasiliane na yule mtaalamu maana alituahidi wazi kuwa ile dawa inafanya kazi haraka sana"
Wakakubaliana kusubiri hadi kesho yake.

Sam akiwa njiani kuelekea hospitali, gafla akaona moyo wake kuwa mgumu kwenda.
"Aah ngoja nirudi nyumbani tu, hata hivyo sioni umuhimu wa kwenda"
Kwahiyo Sam akageuza gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake.

Wazazi wa Sabrina walirudi hospitali jioni ile ila Sam hakwenda.
"Atakuwa amepumzika kidogo tu maana huyu kijana ana moyo sana"
Mama wa Sabrina akajipa matumaini juu ya hilo.
Kisha wakazungumza na daktari ambaye aliwapa uhakika wa Sabrina kuruhusiwa kesho.
Baada ya hapo wote wakarudi nyumbani.

Shangazi wa Sabrina bado alikuwa na James yule kaka wa Sabrina nyumbani kwake, kwani alipoanguka mwanzoni alimpa huduma ya kwanza na kisha kukaa nae pale nyumbani kwake.
"Shangazi, naomba leo niondoke kwani najua hata mke wangu atakuwa na mawazo na mimi"
"Sawa, ila pole kwa huo ukweli niliokupa. Sikukusudia kukuumiza ila nilitaka tu uujue ukweli mwanangu James"
"Nashukuru shangazi na nimeamini kuwa siri ya mtoto anayo mama ingawa hujanitajia kuwa baba yangu mzazi ni nani"
"Hilo kamuulize mama yako, ila kama atashindwa kukutajia basi mi nitakupeleka hadi kwa baba yako mzazi"
Basi James akamuaga tena shangazi yake pale na kuondoka.

Alifika kwa mkewe akiwa na mawazo sana, hata Joy akapatwa na mashaka juu ya hali ya mumewe.
"Hujaonekana siku mbili hapa, si kawaida yako James ndiomana shangazi aliponipigia simu na kusema nisiwe na mashaka upo kwake nikaamini hilo. Leo umerudi ila ukiwa umejawa na mawazo. Nini tatizo mume wangu? Niambie mimi pengine naweza kukusaidia"
"Hapana Joy usijali, kila kitu huenda kwa ngazi. Kwahiyo muda ukifika nitakwambia tu ukweli, ngoja nipate uhakika kwakweli"
"Sasa mimi ndio mwandani wako, usiponiambia mimi utamwambia nani tena? Tafadhari James niambie ukweli mume wangu"
James akafikiria sana na kuona wazi kuwa atakaposema ukweli basi atakosa raha zaidi kwani hakujua mkewe nae angemuongezea kwa maneno yapi, kwahiyo alikazana kumwambia kuwa atamwambia ukweli muda ukifika ingawa Joy naye alijipanga kuendelea kumbembeleza hadi amwambie ukweli wa mambo yanayomfanya awe na mawazo kwa kiasi kile.

Sam akiwa nyumbani kwake, alishangaa kichwa chake kutawaliwa na picha ya Neema. Mawazo yake yote kuwazia uzuri wa Neema,
"Huyu mwanamke mzuri, umbo lake la kuvutia, anajua kujali na sifa zake zote ni nzuri. Kwanini nisiwe na huyu mimi? Kwanini muda huu namuwaza sana?"
Akafikiria kisha akalala.
Kulipokucha asubuhi na mapema, Sam akaenda kuoga na kujiandaa kwenda hospitalini kumuangalia Sabrina.
Mara gafla moyo wake ukasita na kuwa mgumu,
"Kwani nikienda mimi ndio atapona? Hapana, madaktari watamsaidia pale. Ngoja niende kwenye kazi yangu"
Sam akaondoka na kwenda kazini.

Wazazi wa Sabrina walipoenda hospitali walishangaa kwa kutokumuona Sam kabisa ile asubuhi, na walipompigia simu iliita tu bila ya kupokelewa.
"Sijui kapatwa na matatizo? Itabidi tukitoka hapa uende ukamuangalie baba Sabrina"
Walikubaliana juu ya hilo kisha daktari naye akawapa ruhusa ya kurudi na Sabrina nyumbani kwao.
Walirudi nyumbani kisha baba wa Sabrina kwenda kumuangalia Sam nyumbani kwake na ofisini kwake kama atakuwepo.

Muda kidogo, baba wa Sabrina alirudi nyumbani.
"Umempata Sam?"
"Mmh yule kijana nahisi akili yake haipo sawa kwa leo, hebu tumuache kwanza"
"Kwani imekuwaje?"
"Nimempata, nimemkuta kwenye ofisi yake ila majibu aliyonipa mmh tutajadili siku nyingine"
Mama wa Sabrina alibaki kushangaa tu kwani hakuelewa kama Sam anaweza kuwa na majibu mabaya kiasi cha kumuudhi vile mkwe wake.

Sakina naye alienda kwa wakina Sabrina ili kumsalimia Sabrina na kuangalia hali yake.
Kwahiyo yale mazungumzo kuhusu Sam akayasikia kidogo na kusema lazima kutakuwa na kitu maana yeye mawazo yake yalikuwa yakimtuma kwenye ushirikina tu.
Kwahiyo hakukaa sana pale na kuwaaga.
Alipofika kwake napo akajiandaa upesi upesi na kumuaga Dorry kuwa atarudi badae.
Safari yake ilikuwa ni moja kwa moja kwa mtaalamu,
"Leo siendi kule ana watu wengi sana yule. Ngoja niende kwa huyu wa bondeni hadi nijue leo maana siwezi kulala na hili dukuduku"
Wakati anakaribia kufika likamjia wazo kuhusu mtoto wa Sabrina kuwa kwanini kafanana na Jeff.
"Mmh! Au Sabrina alichepuka na kutembea na shemeji zangu! Ngoja nikaulize na hili pia."
Sakina alifika na kuingia moja kwa moja kwa mtaalamu.
Kisha kukaa,
"Eeh eleza shida yako mama"
"Kwanza kabisa, kabla ya yote niangalizie kama huyu mtoto wa Sabrina ni wa mumewe kweli"
Mtaalamu akacheka, kisha akasema,
"Yule mtoto si wa mumewe"
"Mmmh amezaa na nani sasa?"
"Ni damu yako"
Sakina akashtuka na kumuangalia kwa makini yule mtaalamu.

"Eeh eleza shida yako mama"
"Kwanza kabisa, kabla ya yote niangalizie kama
huyu mtoto wa Sabrina ni wa mumewe kweli"
Mtaalamu akacheka, kisha akasema,
"Yule mtoto si wa mumewe"
"Mmmh amezaa na nani sasa?"
"Ni damu yako"
Sakina akashtuka na kumuangalia kwa makini yule
mtaalamu.
Kisha akamuuliza,
"Damu yangu kivipi?"
"Inamaana hujua ninachomaanisha kwa kusema ni damu yako?"
"Sijui ndio"
"Basi huo na uwe mtihani kwako, nenda ukajitafakari utapata jibu kwa ninachomaanisha"
"Inamaana huwezi kuniambia?"
"Ndiomana nimekupa kama mtihani, halafu nenda umchunguze vizuri yule unayehisi ni mkweo"
"Kivipi?"
"Nenda kamchunguze tu"
Sakina akaonekana kuchukizwa na lile jibu la mtaalamu na kumfanya aondoke bila ya kumuaga wala kumuuliza swali jingine.

Akiwa njiani ni njia nzima kumlaani yule mganga tu,
"Miwaganga mingine kama michoko, yani mi nimeenda kwake linipe jibu eti na lenyewe linanipa mtihani ndiomana halina watu. Kesho asubuhi nitawahi kwa yule mtaalamu wangu. Hili choko limenikera sana"
Alichukia sana hadi anaingia nyumbani kwake alikuwa akiongea peke yake huku akimlaani yule mganga.
Alimkuta Dorry ndani akiwa ameandaa kila kitu, na kumkaribisha kwa ukarimu sana, hadi akajikuta akiongea kimoyo moyo.
"Miwaganga mingine bhana, sasa binti mzuri kama huyu nimchunguze kitu gani maana huyu ndiye mkwe wangu."
Alimalizia kwa kuongea kwa sauti,
"Ndiomana yule mganga hana wateja pale"
Ikabidi Dorry amsikilize kwa makini huyu mama mkwe wake na kumuuliza kuwa anazungumzia kitu gani.
"Hamna kitu, ila kuna miwaganga inaishi kwa uongo tu. Mi nilijiuliza kuwa kwanini huyu mganga hana wateja kumbe ni liongo bhana"
"Pole mama, kakudanganya nini tena?"
"Yani wee acha tu mkwe wangu"
"Ila mama, waganga karibia wote ni waongo sio wa kuwaamini kabisa"
Huku akikumbukia alivyochukua yale makaratasi halafu mama mkwe wake kuambiwa na mganga kuwa yale makaratasi yaliondoka kichawi.
"Hujui tu Dorry, wamenisaidia sana hapa mwanangu"
Dorry hakutaka kumpinga zaidi kwa kuhofia kugundulika.
Kwahiyo akamuitikia kuhusu swala lake la kubadilisha mganga kama alivyopanga mwenyewe.

Sam alitoka ofisini na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwake ila alipokuwa njiani alijikuta akitamani kumuona Neema.
Hamu ile ilimzidia na kumfanya ageuze gari na kuelekea kwa Neema.
Alipofika alikuta mlango umefungwa, akajaribu kumpigia simu ila haikupokelewa na kujikuta moyo wake ukiumia sana.
Akaamua kukaa na kumsubiri kidogo, ila muda ukaenda bila Neema kurudi na kumfanya Sam aumie zaidi na kuamua kuondoka kuelekea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake alijifikiria sana, alifikiria tatizo lake ni nini.
"Mbona sijisikii kwenda kumuona mke wangu niliyempenda sana? Kwanini niende kumuona mtu asiyenihusu halafu niumie kiasi hiki?"
Sam hakujielewa kabisa, alijiona kuchoka sana na kuamua kwenda kulala.

Kulipokucha kama kawaida akajiandaa na kwenda kazini kwake ila mawazo yake yote yalikuwa kwa Neema tu na akapanga kwenye mida ya saa nne aende tena kumuona Neema maana alikosa raha kabisa kwa kutokumuona jana yake.
Kwahiyo muda aliopanga ulipofika tu akatoka ofisini na kuelekea nyumbani kwa Neema.
Alipofika, aligonga na kufunguliwa na Neema kisha akaingia ndani.
Neema alikuwa akifikicha macho kuonyesha kuwa alikuwa amelala.
"Karibu Sam"
"Khee umelala muda huu Neema?"
"Uchovu tu, kwani saa ngapi saivi?"
"Saa tano hii ndio bado umelala!"
"Sina la kufanya ndiomana nikalala hadi muda huu"
Basi Sam akatulia mule ndani akimuangalia tu Neema.
Muda kidogo alifika rafiki wa Neema ambaye hakujua kama ndani kuna mtu kwani alianzia mlangoni kuongea huku akifungua mlango,
"Kheee Neema sebene la jana ndio ume......"
Akashtuka kumuona mgeni ndani na kumsalimia,
"khabari yako shemeji"
Sam akamuangalia na kuitikia,
"Nzuri tu"
Neema nae akatoka ndani na kuanza kusalimiana na rafiki yake ambaye alikuwa ni Rose kisha akamtambulisha kwa Sam,
"Huyu ni rafiki yangu mkubwa sana, anaitwa Rose"
Kisha akamgeukia Rose na kumwambia,
"Na huyu anaitwa Sam"
Rose akamuangalia Sam kwa jicho la aibu kisha wakasalimiana tena.
Muda kidogo Sam akawaaga na kuondoka.
Neema alipobaki na rafiki yake huyo waanza kujadiliana kuhusu Sam,
"Mmh sijui atanikumbuka?"
"Kwanini?"
"Si unakumbuka mpango wetu wa kipindi kile?"
"Nakumbuka ndio, kwani ulikutana nae kweli?"
"Nilikutana nae ndio"
"Mmh tuipotezee hiyo, jifanye kama sio wewe siku nyingine"
Wakakubaliana kuhusu hilo swala.

INAENDELEAA



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.