Simulizi: Je Haya Ni Mapenzi? Sehemu Ya 58-80

Usiku ule Jeff akiwa ametulia chumbani kwake, akaamua kwenda sebleni kama kupoteza muda tu akamsikia mama yake akiongea na simu.
Akajikuta akipata hisia kuwa huenda mama yake alikuwa akizungumza na Dorry kisha akapata mashaka kuwa huenda mama yake anahusika pia katika kumtuma Dorry aongee maneno yale kuhusu Sabrina.
"Mmh kama mama kamtuma basi inamaana kuwa kuna vitu ametambua kuhusu mimi na Sabrina. Hata kama ametambua si atuache wenyewe tu, ila kama mama anahusika sijui kwakweli maana atakuwa ameniudhi sana"
Alikuwa akiyawaza hayo, akasikia kuwa mama yake amemaliza kuongea na simu kisha muda huo huo akasikia simu yake ikiita.
Akainuka na kwenda chumbani kuiangalia, akaona namba ya Dorry akatikisa kichwa na kuamini zaidi kuwa mama yake ndio kamtuma Dorry kusema yale aliyoyasema jana yake.
Jeff akaipokea ile simu na moja kwa moja sauti ya Dorry ikasikika,
"Nimekukumbuka sana Jeff jamani"
Jeff akacheka na kumwambia Dorry,
"Mwambie mama atafute binti mwingine wa kunishawishi mimi ila sio wewe ambaye ulimaliza waswahili na kuwaanza wachina"
"Mbona sikuelewi Jeff"
"Ndio unielewe tu, najua unafanya kazi ya kunipeleleza basi ujue umeshindwa. Na vilevile hata kama nikiamua kuwa na mchepuko basi huwezi kuwa wewe. Kwaheri"
Jeff akaikata ile simu kisha kukaa kitandani kwake akijiwazia ila mawazo yake yote yalikuwa juu ya Sabrina na juu ya ile barua ya Neema, huku akiyafikiria maneno ya Sam.
"Lazima nisimame kiume sasa, lazima nimwambie ukweli Sam. Sijui tutasikilizana ila Mungu anisimamie kwa hili"
Kisha akalala.

Kulipokucha Jeff aliamka kisha akajiandaa na kumuaga mama yake kuwa anaenda kwakina Sabrina ila alimgundua mama yake kutokuwa na furaha kwa siku hiyo,
"Mama vipi unaumwa?"
"Hapana hata siumwi"
"Sasa mbona umepooza hivyo?"
"Mawazo tu mwanangu hata usijali"
Ila Jeff aliweza kuelewa kwa haraka kuwa mama yake atakuwa kaambiwa na Dorry majibu aliyopewa kwahiyo hayakumfurahisha kabisa na ndiomana ameonekana kusononeka kiasi kile.
Jeff akaondoka pale na kuelekea kwakina Sabrina.

Alimkuta Sabrina tayari alikuwa n je akifua nguo za watoto wake na kumsalimia.
Mama Sabrina naye alikuwa pembeni akiwaangalia tu na kumfanya Jeff atoe na salamu ya mbali kuweza kumfikia mama Sabrina kisha akatulia pale ili kuweza kuzungumza na Sabrina ambapo walijikuta wakitazamana kwa dakika kadhaa bila ya kusemeshana chochote ila Jeff mwenyewe akaamua kuumaliza ukimya ule kwa kumuuliza swali Sabrina,
"Umeotaje leo?"
Sabrina akamshangaa Jeff kwa lile swali na kufanya na yeye kuuliza pia,
"Kuotaje kivipi?"
"Yani siku ya leo umeota vitu gani?"
"Kwanini umeniuliza hivyo?"
"Nimekuuliza tu kwani kuna ubaya?"
"Hapana ila nimeshangaa swali lako ukizingatia leo ni kweli nimeota ndoto mbaya sana."
"Ndoto mbaya kivipi?"
"Ni ngumu kuielezea kwakweli"
Jeff akaitoa ile barua ya Neema na kumpa Sabrina,
"Barua yako ni hii uliiangusha"
Sabrina akashtuka na kumuuliza Jeff,
"Umeisoma?"
Jeff akatikisa kichwa kuashiria kwamba ile barua ameshaisoma.
Sabrina akaichukua na kuiweka kifuani kama alivyoweka siku ya kwanza, Jeff akamwambia,
"Kuwa makini usije ukaiangusha tena"
Sabrina akaona ni vyema aipeleke chumbani kwake kwanza kwahiyo akaachilia kufua pale na kwenda ndani.
Muda wote huo mama wa Sabrina alikuwa akiwaangalia na kuona yote yaliyoendelea ingawa hakuweza kusikia kuwa wanazungumzia kitu gani.
Sabrina alipotoka nje akamkuta Jeff amesimama pale pale kisha akatabasamu baada ya kumuona tena Sabrina pale nje na kumuaga kwa kumwambia.
"Ukimaliza kuisoma niambie"
Jeff akaondoka zake.

Mama Sabrina akamsogelea mwanae na kumuuliza,
"Hivi kuna kitu gani kati yako na Jeff?"
"Kivipi mama?"
"Kwani amekuja kufanya nini asubuhi hii?"
"Kuna mzigo ameagizwa na mama yake ndio aliniletea"
"Mmmh"
"Mbona unaguna mama?"
"Hamna kitu"
Kisha mama Sabrina akaenda kuendelea na majukumu yake aliyokuwa akiyafanya, ila Sabrina akatambua tu kuna kitu mama yake amekihisi kuhusu yeye na Jeff.

Sam alikuwa ndani kwake na kumuangalia Ritha hadi pale alipozinduka na kukaa huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake, kisha akakumbuka tukio lililompata na kumtazama Sam huku akijikuta kushtuka na kuongea kwa nguvu,
"No, hapana wewe Sam sio binadamu wa kawaida. Nimefikaje hapa?"
Ritha akainuka na kujiangalia mara mbili mbili, akahisi maumivu kwenye sehemu za siri na kumfanya akumbuke vizuri mchezo mzima.
Hakuweza kuvumilia kwakweli na kutaka kutoka ila Sam akamzuia na kumwambia,
"Tafadhari Ritha naomba iwe siri"
Ritha akamfyonya Sam na kumwambia,
"Kafanye siri na baba yako mzazi mbwa wewe"
Sam akamuangalia tu Ritha bila ya kumwambia neno la ziada kwani swala la kutajiwa baba yake mzazi lilishamuumiza kichwa tayari na kumfanya ajisikie vibaya kwa wakati huo.
Akakaa chini na kutafakari, akaangalia utajiri aliokuwa nao na kila kitu alichonacho.
"Hivi ni kwanini nimeshindwa kumpata baba yangu mzazi hadi leo? Huyu baba popote pale alipo na alaaniwe...."
Akasita kidogo na kujiuliza,
"Kwani amefanya kosa gani hadi alaaniwe? Aah ndio ameniacha mimi nilelewe na baba wa kambo mwenye roho mbaya na kufanya nisipate mapenzi ya mama mzazi ingawa mamdogo naye kanilea vizuri sana. Ila nadhani mamdogo kanilea vizuri kwavile hakuwa na mtoto"
Akafikiria tena, ila akaona ni muhimu amfahamu baba yake ili huyo baba yake aumizwe na mafanikio aliyonayo kwasasa.
"Atambue wazi ingawa hakunilea ila nimefanikiwa sana"
Wazo kuhusu baba yake lilimjia baada ya kuambiwa na Ritha kuwa akafanye siri na baba yake mzazi.

Ritha alipofika kwao akaamua kujitazama vizuri sasa na kujiona akiwa anatokwa na damu.
"Mungu wangu, hivi yule mwanaume ni binadamu kweli? Kwanini nilifikia hatua ya kulala nae? Kwanini sikufikiria haya kabla? Eeh Mungu naomba urudishe muda nyuma tafadhari, naomba urudishe muda kabisa niwe sikuondoka hapa nyumbani kabisa? Mambo gani haya yamenipata jamani?"
Alijisikilizia na maumivu nayo yakamzidia sehemu yake ya siri na kumfanya uzalendo kumshinda.
Akamuita dada yake wa karibu ili aweze kumuomba ushauri,
"Ritha vipi? Tatizo ni nini?"
"Yamenikuta makubwa dada huwezi amini, yani najiona kama naota vile"
"Hebu nieleweshe mdogo wangu, umekuja hueleweki. Nguo imechafuka damu, inamaana umeingia kwenye siku zako bila kujijua?"
"Ni kheri ingekuwa hivyo dada, ila kuna mwanaume mmoja kanifanyia ushenzi sana leo halafu anasema nisiseme"
"Kakufanyia nini?"
Machozi yakamtoka Ritha kwani aliweza kurudisha matukio nyuma kwa haraka sana kasoro tukio la kuzimia tu kwani hakuwa na kumbukumbu nalo.
"Dada, katika maisha yangu sijawahi kukutana na aina hii ya mwanaume ila leo kwa mara ya kwanza nimekutana na mwanaume mwenye maumbile ya tofauti na wanaume wengine"
"Unamaana ana maumbile makubwa?"
"Ingekuwa hivyo nisingelalamika"
Akatulia tena kwa kilio kwani kadri alivyoelezea ndivyo alivyoona moyo wake ukizidi kuumia na kumfanya machozi yamtoke zaidi.
"Dah pole mdogo wangu, itabidi twende hospitali jamani"
Dada wa Ritha aliyejulikana kwa jina la Mage, akainuka ili afanye kama kumuhamasisha Ritha kuwa wainuke na waende hospitali ila alimshangaa Ritha akijinyoosha pale chini na kuwa kimya gafla.
"Ritha, Ritha, wee Ritha wee"
Kimya, akadhani kuwa Ritha anamfanyia mchezo na kujaribu kumtikisa tikisa ila Ritha alikuwa kimya.
Mara Mage akashtushwa na mlio wa simu ya Ritha, akaichukua na kuipokea kwani hata yeye hakujielewa wala kujitambua pale.
Akasikia sauti ikiongea upande wa pili,
"Tafadhari Ritha usimwambie yeyote ile habari utakufa"
Mage akajikuta akiuliza kwa ukali,
"Wee nani wee nani?"
Simu ikakatika na kumfanya Mage apatwe na uoga zaidi kuwa huenda Ritha amekufa, na ndio hapo alipoanza kupiga kelele za kuomba msaada.

Sam alijilaumu kwa kitendo chake cha kupiga simu tu na kuanza kuongea bila kuuliza anayeongea naye.
Mara gafla akapatwa na maumivu ya moyo yaliyomfanya atambue moja kwa moja kuwa kuna tukio limetokea na hakufikiria mbali zaidi ya kufikiria kuwa ameshampoteza Ritha.
"Maskini Ritha jamani, haikuwa kusudio langu jamani. Pole Ritha"
Sam aliumia na kukumbuka maisha yake ya nyuma ambapo alipoteza maisha ya wadada kadhaa na sasa lile swala lake limejirudia tena kwa staili hiyo.
Aliilaumu nafsi yake na alimlaumu mtu wa kwanza kumuharibu yeye kisaikolojia na kimaumbile.
Alijikuta akikumbuka mambo mengi sana.

Barua ya Neema ilimpa mshtuko wa hali ya juu Sabrina alipokuwa akiisoma na kumfanya akumbuke jinsi alivyokuwa anamchukia Sam kwa kukataa kufanya nae tendo la ndoa.
Akajikuta akishangaa tu mlolongo wa maisha yake na kumfanya ajifungie ndani siku nzima akifikiria yale yanayoendelea katika maisha yake.
Na kupata jibu la kwanini Jeff yupo kama sehemu ya maisha yake.

Kwenye mida ya saa moja usiku, Jeff alienda tena nyumbani kwakina Sabrina na kumkuta mama Sabrina sebleni ambaye moja kwa moja alimuuliza,
"Na saa hizi umetumwa tena?"
Jeff akaitikia kwa kichwa tu,
"Haya mfate muhusika yupo chumbani kwake"
Jeff akainuka na kuelekea chumbani kwa Sabrina.
Alifika na kufungua mlango kisha kuingia chumbani mule ambapo Sabrina alipomuona Jeff aliinuka na kumkumbatia kisha akamuachia na kuangalia chini kama mtu mwenye aibu, kisha Jeff akamshika Sabrina usoni na kuiinua sura yake halafu akambusu mdomoni.
Kitendo kile cha Jeff kumbusu Sabrina mdomoni kilionwa na mama Sabrina kwani naye alienda chumbani kwa Sabrina.
Kwahiyo akawashtua kwa mshangao na kuwafanya nao washtuke pia.


Kitendo kile cha Jeff kumbusu Sabrina mdomoni
kilionwa na mama Sabrina kwani naye alienda
chumbani kwa Sabrina.
Kwahiyo akawashtua kwa mshangao na kuwafanya
nao washtuke pia.
Kisha mama Sabrina akauliza,
"Nini kinaendelea?"
Sabrina hakujibu ila naye aliuliza,
"Kwani nini mama?"
Mama Sabrina akatikisa kichwa huku akimuangalia Jeff aliyekuwa kimya kabisa kama hausiki vile na lile swali lililoulizwa.
Kisha kikatawala kimya cha muda mfupi pale ndani kwani hakuna aliyemjibu mwenzie.
Kisha Sabrina akaingizia stori zingine kwa kujifanya kumuuliza Jeff,
"Hivi ulimwambia Sakina kama nimeupata ule mzigo?"
Jeff akaitikia kwa kichwa kumaanisha kukubali kuwa amemwambia,
"Mbona hajaja sasa?"
"Sijui mwenyewe"
Mama Sabrina akatoka na kujua wazi wanajigelesha ingawa hata yeye binafsi anashindwa kuwaelewa kuwa wanamaana gani.

Wakabaki wawili mule chumbani kama ilivyokuwa mwanzoni.
Jeff akamsogelea Sabrina na kumwambia,
"Nisamehe, tatizo langu siwezi kuzuia hisia zangu kwako. Nisamehe tafadhari"
Sabrina hakujibu kitu ila alimsogelea na kumkumbatia kisha akamruhusu kwenda nyumbani.
Jeff hakuongeza neno zaidi ya kumbusu Sabrina kwenye paji la uso kisha kuondoka zake.
Sabrina alikaa na kujiinamia kwani alijiona wazi akimpenda zaidi Jeff sasa tena zaidi ya alivyokuwa akimpenda mwanzo kwani sasa alitamani kuwa nae karibu zaidi.
Alijifikiria sana na muda mwingine kujiuliza kuwa kwanini amepatwa na mawazo ya aina hiyo kwasasa ila jibu ni kuwa ile barua aliyoipata toka kwa Neema kuhusu Sam ndio iliyomshtua.
Akawaza kuwa huenda Sam alikuwa na tatizo alilokuwa nalo yeye zamani,
"Ila mbona Jeff ameweza kulala na mimi bila matatizo? Lazima kuhusu mimi yule mtaalamu alichanganya mada. Na vipi kuhusu Sam, kama idadi ya waliokufa kwaajili yake ni kubwa hivi basi lazima kuna ukweli juu ya hili"
Akawaza na kuwaza ila alijua wazi kuwa maelezo kamili atakuwa nayo Sam tu.

Jeff naye aliporudi kwao, alimkuta mama yake aliyemuuliza
"Ushatoka kwakina Sabrina?"
"Ndio mama"
"Hivi kwanini unanificha Jeff? Kwanini unanificha mama yako?"
"Kukuficha nini mama?"
"Hivi ushawahi kufikiria kuwa mke wa mtu ni sumu?"
"Mke wa mtu ni sumu? Natambua hilo, ila mama nipe tafsiri ya mke wa mtu"
Sakina alimuangalia mwanae na kumuona kuwa anapenda sana masikhara hata kama kitu ni cha kweli ila akaamua kumjibu tu,
"Mke wa mtu ni mwanamke aliyeolewa au anayeishi na mwanaume"
"Nikuulize kitu mama ila usichukie"
"Niulize tu"
"Mtu aliyeolewa akiwa anaishi mwenyewe bila mumewe je huyo ni mke wa mtu?"
"Hivi wewe mtoto wewe una wazimu au? Kwani mtu akiishi mwenyewe ndio nini si alishaolewa tayari"
"Nimekuuliza huku nikichukulia mfano wako. Baba yuko wapi?"
"Mjinga wewe huna akili kama baba yako, nitokee hapa. Ukiongelea wanaume za watu baba yako mtoe kwanza hajielewi. Toka zako hapa umeniudhi sana"
Sakina aliinuka na kwenda chumbani kwake.
Jeff alielewa wazi kuwa amemkera mama yake kwahiyo akajipanga kumuomba msamaha kama akitoka ndani au asubuhi kwani hakuweza kumuita muda huo anaojua wazi amemuudhi.

Sam alikuwa nyumbani kwake huku akijilaumu kwa kitendo chake cha kumaliza hawa wadada,
"Lazima nimwambie ukweli Sabrina, nimwambie ukweli ili moyo wangu upate kuwa huru kwani nimechoshwa na haya matukio kwasasa. Kwanini jamani? Nilishaacha hii tabia zamani ila toka kipindi cha Neema ndio tabia hii ikajirudia kwa kasi sana. Kwakweli sijui la kufanya, nadhani cha muhimu nikae mbali na hawa wasichana"
Alijifikiria sana pia akafikiria kuhusu mazishi ya Neema ambapo hakujua kama wamezika au la na huku akigundua msiba mwingine wa Ritha, kwahiyo hicho kitu kilimuumiza sana na kumfanya akose raha kabisa.
Hata muda huo hakuweza kulala moja kwa moja ila alikunywa kwanza pombe kwa lengo la kupunguza mawazo aliyokuwa nayo.

Dorry akiwa nyumbani kwao pia, ni siku hii akapokea tena ile simu ya maajabu aliyowahi kupokea kipindi cha nyuma ambapo alipigiwa kuhusu matatizo ya Sabrina.
Akasita kidogo kupokea leo ila akaona ni vyema kwa yeye kupokea tu ile simu.
Dorry akapokea na kuanza kuongea,
"Haya leo kuna mapya gani? "
" sina mapya ila nimekupigia kukuaga Dorry, asante kwa kazi uliyonifanyia"
"Ila mbona hujaniambia kuwa wewe ni nani hadi leo? "
" Unataka kufahamu kuwa mimi ni nani? Sipendi nikutishe na wala sitaki unione. Mi niliwahi kuwepo zamani sana kwenye maisha ya ndugu wa Sabrina, nilimpenda huyo ndugu, nilimlinda kwa kila hali na sikupenda kuona akihangamia na ndicho nilichofanya kwa Sabrina huyu. Ila jua kwamba mimi si kiumbe mzuri wala si kiumbe mbaya, kwani kuna wakati nakuwa na roho ya kusaidia ila sitaki kuwa karibu sana na wewe kwa kukuhofia kunizoea sana kisha ulie kwa mazoea yako juu yangu. "
" Kwakweli nakuwa mgumu kukuelewa, kwanini ulinichagua mimi katika kumsaidia Sabrina? Na pia wewe ni nani hadi usionekane? "
" Dorry nimekuchagua wewe sababu imekuwa rahisi sana kukutumia kwa haraka na kuondoka zangu ila mfano ningemchagua Sabrina ingekuwa ni ngumu sana kwa mimi kuondoka katika mwili wake. Sababu kubwa niliwapenda hapo mwanzo ingawa hawakunitaka ila nikawasaidia "
" Na mbona sauti yako mwanzoni ilikuwa ikifanana na sauti ya Jeff? "
" Ninao uwezo wa kuiga sauti ya mtu yeyote nimtake na nilifanya hivyo ili wewe iwe rahisi kunielewa "
" Wewe ni nani lakini? "
" Mimi si kiumbe wa kawaida, usitake kunijua kwa undani zaidi Dorry."
Dorry akashtuka baada ya kusikia kuwa sio kiumbe wa kawaida, ambapo yule mtu aliendelea kuongea
"Na ninauwezo wa kufika hapo ulipo na kukaa karibu yako muda huu. "
Dorry akashtuka zaidi na kujikuta akiachilia ile simu ila muda huo huo akasikia sauti ya mtu akicheka mule chumbani kwake na kumfanya uoga uongezeke ila akasikia sauti ikimwambia,
" Usiogope Dorry siwezi kukudhuru, kwaheri"
Lile neno la kwaheri likajirudia mara kadhaa kama mwangwi kisha kupotea kabisa.
Dorry aliogopa sana na kutoka chumbani kwake, kwakweli ile hali ilimfanya ashindwe kulala mwenyewe siku hiyo.

Kulipokucha, Sam naye aliwaza kwenda kuwapa pole ndugu wa marehemu ila pia akawaza kuzungumza na Sabrina ambaye alijua wazi kuwa kuna haja ya kumwambia ukweli wa mambo yote kuhusu yeye.
"Itabidi tu nifanye hivi, siwezi kuishi na hii siri maisha yangu yote. Lazima nimwambie mtu mmoja nilivyo na mtu huyo si mwingine bali ni Sabrina tu."
Aliyawaza hayo na muda kidogo akapokea simu kutoka namba mpya na kuanza kuongea naye,
"Jana ulipompigia Ritha ni mimi uliyeongea naye, kwa kifupi Ritha amekufa ila kwakweli sikuelewa maneno yako ulisema Ritha asitoe siri kwani akitoa tu atakufa na pia nakumbuka Ritha kuna maneno alikuwa akiniambia na ndio akafa gafla. Kwani wewe ni nani?"
Sam alimsikiliza yule dada na kusikiliza mazungumzo yake ambayo yalitawaliwa na yeye mwenyewe toka mwanzo kisha Sam akamwambia,
"Kama unahitaji kunifahamu njoo unione."
"Nikuone kivipi?"
"Ili utambue kuwa mimi si mtu mbaya kama unavyonifikiria, na pia nimeudhunishwa sana na hizo habari za kifo cha Ritha. Kwani mnazika lini?"
"Tunazika leo, ila kama sio mtu mbaya kwanini ulikuwa ukimtahadharisha Ritha?"
"Nilimtahadharisha kwavile sikutaka afe, sikutaka kumpoteza. Hujui tu ila Ritha ni mtu wa muhimu sana katika maisha yangu. Yani sikutaka kumpoteza kabisa, nimeumizwa sana na kifo chake. Nipe maelekezo ya mahali pa mazishi nije"
Huyu ndugu wa Ritha alimuelekeza Sam bila ya kujua kuwa huyu Sam ndio yule yule mwanaume mbaya aliyeambiwa na nduguye Ritha kabla ya kufa kwake.
Sam alipomaliza kuongea na ile simu akajiandaa kisha kuondoka pale kwake.

Kutokana na ile simu ambayo Dorry aliongea nayo usiku, akaamua kufunga safari ili aende kwakina Sabrina kuwaeleza yote yaliyokuwa yakijitokeza kuhusu yule mtu huku akiamini kuwa huenda ikawa ni msaada kwake kutambua ni kitu gani kilikuwa kikimfatilia katika maisha yake ya kipindi hicho.
Njiani akakutana na Sam kwani huyo Sam alisimamisha gari yake na kumsalimia Dorry,
"Unaenda wapi? Vipi yale matatizo yako yaliisha?"
"Matatizo yangu yamekuwa makubwa kuliko mwanzo, ulinitupa sana na kunisahau. Umefanya nikakosa msaada wala mtu wa kunisapoti kabisa yani"
"Pole sana Dorry, na huyo ndio mwanao?"
"Ndio ni mwanangu"
Sam akacheka na kumuuliza,
"Mbona kafanana na wachina jamani?"
Dorry nae akacheka kwa kujisikitikia,
"Yani wee acha tu haya yangu"
"Haya panda kwenye gari nikupeleke kwanza halafu niendelee na safari zangu"
Dorry akaona ni afadhari kapata lifti na kupanda, Sam naye aliendelea kuzungumza na Dorry kwa kumwambia,
"Unajua unapotaka kumsingizia mwanaume kuhusu mtoto unatakiwa kuwa makini na ujue mwanaume uliyetembea naye mwanzo anafananaje, sio mwanaume mweusi ukamletee mtoto mweupe au mwanaume mweupe ukamletee mtoto mweusi ila afadhari hapo kuna cha kusema kuwa kafanana na mjomba au shangazi sasa wa kwako kazi ipo uzae na mchina usingizie mswahili"
Sam alikuwa anaongea huku anacheka tu ila yale maneno yalimuingia vilivyo Dorry ingawa nae alitabasamu na kumfanya Sam azidi kuongea,
"Kipindi kijacho kuwa makini, msingizie mtu unayeona angalau anaendana na mwanaume ambaye ni muhusika wa ile mimba ila nyie wanawake mnanichekeshaga sana dah"
Sam leo aliongea anachojisikia hadi pale walipofika kwakina Sabrina na kumuacha Dorry ashuke kisha yeye kuendelea na safari yake.

Dorry aliingia kwakina Sabrina na kuwakuta kisha akasalimiana nao, waliitikia ila walimshangaa kuwa siku hiyo imekuwaje yule Dorry kufika eneo hilo.
"Karibu sana"
Mama wa Sabrina alimkaribisha kisha kuanza kuzungumza mawili matatu, ni hapo ambapo Dorry aliamua kumueleza mama Sabrina jinsi ilivyokuwa toka siku ya kwanza anapigiwa simu na yule mtu wa ajabu na maelezo aliyopewa na yale aliyoambiwa kwa jinsi ya kumuokoa na kile alichokifanya katika kupigania maisha ya Sabrina.
Pia akamuelezea simu aliyopigiwa usiku na mtu huyo kuhusu yale aliyokuwa akimuelekeza.
"Eeh mbona kazi ipo? Au hicho kitu ndio kilichompata shangazi wa Sabrina kipindi kile?"
"Alipatwa na nini kwani?"
"Ni historia ndefu ila nadhani mkikutana anaweza akakuelezea ilivyokuwa ila hata mimi nitajaribu kumwambia haya. Kwakweli pole sana"
Sabrina nae akatoka na watoto wake pale nje na kumfanya Dorry awatazame na kujisemea moyoni kuwa lazima wale watoto watakuwa wa Jeff tu.
Muda kidogo Jeff naye akafika pale nyumbani kwakina Sabrina kwaajili ya mambo yake binafsi, akashangaa kumuona Dorry pale na hata Dorry naye hakuweza kuhoji zaidi.
Jeff aliwasimulia kisha akavuta kitu na kukaa pale pale nje halafu akamchukua yule mtoto mkubwa wa Sabrina na kukaa naye.
Mama Sabrina alitulia tu akiangalia matukio yote yanayotendwa na Jeff pale huku akingoja atulie na ajaribu kumuhoji kilichompeleka kwa muda huo.
"Jeff karibu maana sikukukaribisha"
"Asante"
"Saizi huna mzigo?"
"Mzigo? Hapana, nimekuja kusalimia tu"
Jeff alikuwa akicheza cheza pale na mtoto Cherry.

Sam alifika msibani na watu walijaa sana pale kwenye msiba kwani kila mmoja ilionyesha kutokuamini kuwa Ritha amekufa.
Ilikuwa ngumu sana kwa wao kuamini jambo hilo na walionekana kuomboleza sana, na wengine kuzimia haswa wale ndugu wa karibu na Ritha.
Sam aliamua kuwasiliana na yule ndugu wa Ritha ambaye ni kweli alijitokeza kwa Sam ila macho yake yalikuwa mekundu sana na kuonyesha kuwa amelia kupita kiasi.
"Poleni sana dada, taratibu gani zinaendelea hapa?"
"Tunangoja kuaga mwili wa marehemu kisha twende kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele"
Mage aliongea huku akifuta machozi na muda kidogo ikaonekana taratibu za kuaga mwili wa marehemu zimeanza.
Leo Sam aliamua kujipa moyo kwa kwenda kuuaga mwili wa Ritha ingawa hajawahi kufanya hivi kwa wasichana wote aliowapitia.
Sam alipita kuaga ila alipatwa na mshtuko mkubwa sana kwani maumivu aliyoyasikia moyoni mwake yalikuwa zaidi ya yale alipogundua kuwa amekufa.
Kwakweli Sam kwa maumivu yale hakuweza hata kustahimili kwenda kuzika kwani alirudi kwenye gari yake kisha kuamua kumpigia simu Dorry ili tu ampe lifti ya kumrudisha nyumbani kwao.

Dorry alikuwa akimtazama tu Jeff na yule mtoto kisha kumtazama mtoto aliyebebwa na Sabrina na kuona ufanano uliopo.
Akatamani kuuliza jambo ila akasita, muda kidogo akapigiwa simu na Sam kisha akawaaga pale na kuondoka.
Alimkuta Sam nje akimsubiri ampeleke, kisha akapanda kwenye gari na safari ikaanza,
"Umejifikiria nini kuja kunifata?"
"Aah nimeamua tu"
"Na mbona sasa hivi huna furaha, tofauti na nilivyokuona asubuhi?"
"Maisha tu mdogo wangu"
Sam hakuwa na raha kweli kwani aliona maiti ya Ritha ikijirudia rudia kwenye akili yake.
Alimfikisha Dorry nyumbani kwao na kumuaga, Dorry nae akamshukuru kisha akamwambia
"Nawe uwe makini kama watoto ulionao ni wako kweli"
Sam akatabasamu kwavile alikuwa anaelewa kila kitu na kurudi kwake.

Sam alipofika nyumbani kwake aliingia ndani ila sura ya maiti ya Ritha bado iliendelea kucheza na akili yake hadi kumfanya ajilaumu kuwa kwanini alienda kuaga.
Akakaa akijifikiria hilo, mara gafla akashangaa akinaswa kibao cha shavu na mtu asiyemuona.


Sam alipofika nyumbani kwake aliingia ndani ila
sura ya maiti ya Ritha bado iliendelea kucheza na
akili yake hadi kumfanya ajilaumu kuwa kwanini
alienda kuaga.
Akakaa akijifikiria hilo, mara gafla akashangaa
akinaswa kibao cha shavu na mtu asiyemuona.
Sam alishtuka sana na kujiuliza kuwa ni kitu gani kilichomnasa kofi, wakati akijiuliza alishtuliwa tena na kofi lingine na kumfanya akimbilie nje.
Yule mlinzi wake akamshangaa na kumfata kisha akamuuliza,
"Vipi tena bosi nini tatizo? "
" Kuna maajabu humu ndani leo hata sijui kuna kitu gani jamani "
" Kwani vipi tena? "
Sam akamueleza kwa kifupi tu huyu mlinzi wake kuwa anashangaa kunaswa vibao ndani kwake tena na mtu asiyemuona.
" Mmh bosi hadi nyumba yako ina mambo hayo? "
" Kwani wewe unayajua mambo haya? "
" Hapana ila nadhani ni mambo ya kishirikina bosi maana kwa hali ya kawaida hilo haliwezekani itakuwa ni ushirikina tu. "
" Sasa nifanyeje hapo jamani "
" Samahani kwa ushauri huu bosi ila hapo ni kwenda kwa mtaalamu tu"
"Mtaalamu?? Mtaalamu wa nini sasa? "
Yule mlinzi akajaribu kumueleza kuhusu wataalamu anaosemea yeye kuwa ni wale waganga wa kienyeji na kumfanya Sam amuangalie tu kisha akapanda kwenye gari yake na kuondoka kwani kwake aliona hapafai kwa siku hiyo.

Jeff naye pale nyumbani kwakina Sabrina aliaga na kuondoka zake huku akijiuliza kuwa Dorry alienda kufanya nini kule kwakina Sabrina.
Alirudi kwao na kumuuliza mama yake kama Dorry ameenda na pale,
"Kheee kwani Dorry alikuwa mitaa hii? "
" Ndio me nilimkuta kwakina Sabrina na akaniacha pale, nikajua amekuja huku"
"Mmh huyu mtoto mbaya jamani kweli kabisa kashindwa kuja hata kunisalimia!! "
" Ndio upime hapo kuwa uzuri wa mtu si machoni pekee, moyo wa mtu ndio wenye uzuri. Unamsifiaga Dorry hapa tena bila hata ya kufikiria makosa yake. Kakudanganya kuhusu mimba na kulea yasiyokuhusu mwisho wa siku ukaletewa mtoto wa kichina ila bado ukapata moyo eti tukapime DNA ila mama yangu dah. Bado akakimbia kwa makosa aliyoyafanya ila unaendelea kumbembeleza kuwa awe na mimi. Pole sana mama yangu ila mimi kwakweli siwezi kuwa na yule Dorry namjua vilivyo na alinisimulia mwenyewe kila kitu. Kuna siku makaratasi kayatoa yeye maskini mama wa watu ukajua ni ushirikina, mganga kakulia pesa tu hakuna kitu. Pole mama yangu ila sasa ujifunze "
Sakina alijiinamia chini na kuanza kukumbuka hiyo siku ya makaratasi hadi akajua kuwa ni ushirikina kwakweli kwa swala hilo akajiona mjinga sana.
" Duh kumbe ndio nilichezewa mchezo kiasi hicho, kwakweli huyu mtoto hafai hata kunishtua kuwa ni yeye hakuna. Halafu lile liganga liongo sana limekula pesa yangu tu na Mungu alilaani miaka yote "
Jeff alikuwa akitabasamu tu na malalamiko ya mama yake pia alifurahi kwani ilikuwa ni njia nzuri ya kupatana naye.

Sam alienda baa na kunywa pombe ili akili yake ichangamke kwani aliamini kuwa akilewa itamsaidia kukwepa baadhi ya mambo,
" Wachawi dawa yao kuwamwagia pombe tu, hivi huyo mtu wa kuniroga mimi nae anaanzaje jamani. Nitawashughulikia mmoja mmoja. "
Alikuwa akizungumza mwenyewe huku akinywa pombe, muda kidogo aliwasili rafiki yake ambaye ni mmiliki wa baa ile, kisha kusalimiana pale na maongezi madogo madogo kuendelea,
" Hivi kaka mkeo yuko wapi siku hizi? "
" Yupo tu"
"Mbona siku hizi huji nae? "
Sam akajifikiria kidogo na kujiona akimkumbuka Sabrina kisha akainuka pale alipokuwa anakunywa na kumuaga yule rafiki yake kwani aliona ni vyema aende kuzungumza na Sabrina kuliko kuendelea kunywa pombe zisizo na faida kwake.

Sabrina na mama yake wakiwa wanajiandaa kulala washtushwa na sauti ya hodi, hasa mama wa Sabrina alishtuka sana ukizingatia kwa kipindi hiko pale nyumbani kwao walikuwepo wawili tu yaani baba wa Sabrina hakuwepo kwa kipindi hiko.
Mama wa Sabrina akainuka na kwenda kumgongea Sabrina chumbani kwake, Sabrina akatoka
"Umesikia kuna mtu anagonga nje?"
"Nimesikia, hivi atakuwa nani usiku huu?"
"Hata mimi nashangaa"
"Au baba?"
"Hakusema kama atarudi leo kwakweli, hata sijui atakuwa ni nani"
Wakasita kwenda kumfungulia ila mwisho wa siku mama Sabrina akaona ni vyema kwenda kumfungulia kuliko kumuacha nje.
Alifika getini na kumuulizia,
"Kwani wewe nani?"
"Mimi ni Sam mama"
"Sam usiku huu?"
"Ndio mama"
Mama Sabrina aliporidhishwa na ile sauti ya Sam ndipo alipofungua mlango kisha geti kubwa na kumfanya Sam aingize gari yake ndani, kisha akamkaribisha,
"Ila mbona ni usiku usiku jamani?"
"Matatizo tu mama, halafu nimeikumbuka familia yangu"
"Khee familia yako umeikumbuka usiku! Sasa utaondoka saa ngapi?"
"Siondoki, nitalala hapa hapa mama"
"Khee utalala hapa hapa kwa misingi ipi?"
Mama Sabrina aliona hapa Sam akimletea mada zisizofaa na kumshangaa tu ingawa alimkaribisha ndani na kumuita Sabrina ambapo Sabrina nae alimshangaa Sam kufika pale kwao kwa muda ule kisha akamuuliza swali lile lile ambalo Sam ameulizwa na mama wa Sabrina.
"Mbona umekuja usiku Sam?"
"Jamani mbona zamani nilikuwa siulizwi hayo maswali? Vipi siku hizi mnaniuliza kama mwizi?"
"Si kwa nia mbaya Sam, kwanza kumbuka hapo zamani tulikuwa tukiishi kifamilia zaidi tofauti na sasa. Wewe fikiria tu kwa jinsi unavyokaa kimya hata wiki hakuna cha mawasiliano wala nini halafu unaibuka usiku gafla kama hivi lazima tuwe na mashaka na wewe"
"Basi msiwe na mashaka na mimi, nimeikumbuka tu familia yangu na ndiomana nimekuja"
"Sasa ndio usiku? Na utaondoka saa ngapi?"
"Sidhani kama ni vyema kunipangia muda wa kuja kuiona familia yangu, Sabrina kumbuka kwamba wewe ni mke wangu. Haijalishi ni mambo gani yametokea kati yetu bado wewe utabaki kuwa mke wangu. Na vile vile nimeamua leo nije nilale hapa, wala sina mpango wa kuondoka leo"
"Khee Sam, utalalaje kwa wakwe zako? Kuna kipindi uliniambia mwenyewe kuwa si jambo jema kwa mtoto wa kiume kulala kwa wakwe sasa vipi leo unataka kulala kwa wakwe zako?"
"Kwani wakwe ni simba au nyoka hadi waogopwe? Kutokulala kwa wakwe ni kujitunzia heshima tu kwa mtoto wa kiume ila inapotokea dharula inabidi tu mtu alale. Wewe ni mtoto wao na mimi ni mumeo kwahiyo mimi ni mtoto wao pia sasa kwanini nishindwe kulala kwa wazazi? Mi nitalala hapa hapa sebleni hata msihangaike"
Sabrina alimuangalia Sam na kumshangaa anavyoongea kiasi kile ila kwavile alimsikia akinuka pombe akajua wazi si akili yake bali ni akili ya pombe ndio inayomtuma kufanya vile.
Sabrina akaona ni vyema amuandalie chumba cha kaka zake na kumuomba akalale chumbani kuliko kulala sebleni.
Sam alikubali na kwenda chumba alichoandaliwa na Sabrina kwa usiku huo.

Sabrina alirudi chumbani kwake huku akisikitikia akili ya pombe ilivyomuendesha Sam huku akihisi kuwa akiamka asubuhi lazima ataona aibu kwa kulala kwa wakwe zake.
Kisha na yeye akalala kwa muda ule.
Usiku wa manane wakati Sabrina akiwa kwenye usingizi mzito, akajiwa na ndoto.
Alijiona yupo mahali na akamuona mtu mbele yake ila yeye na yule mtu walitenganishwa na mstari mweusi kati yake yani yeye alikuwa upande mwingine na yule mtu upande mwingine.
Kisha yule mtu alimgeukia Sabrina na kumfanya Sabrina amshangae kwavile mtu huyo alikuwa ni Neema.
Sabrina akauliza kwa uoga,
"Wewe si umekufa wewe?"
"Ndio nimekufa, kwani tatizo kuja kukusalimia Sabrina? Mimi na wewe tumetenganishwa na kitu kidogo tu, huo mstari hapo chini"
Sabrina akautazama ule mstari, na kumtazama Neema kwa uoga.
"Basi huo mstari mdogo umetenganisha uhai na mauti, wewe ukivuka huo mstari ni mwisho wako wa kuwa hai na kisha utakuwa mfu kama mimi. Ila mimi nikivuta huo mstari siwezi kuwa hai ila nitakuwa mfu hivi hivi na hiyo ndio tofauti ya mimi na wewe"
Kisha Neema akavuka ule mstari na kumfata Sabrina alipo, na kuendelea kumwambia
"Mwambie Sam, ni mimi niliyemnasa vibao nyumbani kwake. Sijafurahishwa na kile alichokifanya kwangu, kwa wanawake wote waliokufa kipindi hiki kwaajili yake ameweza kuhudhuria mazishi yao. Kwanini kwenye mzishi yangu hakuja? Hiko ndio kimefanya nimnase vibao na hiyo hali itamtesa mpaka pale atakapokuja kuomba msamaha kwenye kaburi langu"
Sabrina alishangaa sana na kuuliza jambo ambalo halikuhusiana kabisa na alichokuwa anazungumza Neema.
"Kheee kumbe wafu wakifa wanaweza kuongea?"
"Sio wafu ila ni viumbe vilivyomo ndani yao ndio vinaweza kuyatenda hayo"
"Kwahiyo wewe ni nani?"
"Mimi ni kiumbe ninayeishi kwenye mwili wa Neema, ila nimesikitishwa na kitendo alichokifanya Sam. Kama na wewe umesikitishwa basi inuka tuvuke wote ule mstari ili uwe kama mimi halafu tumuangalie Sam kama atakuja na kwako"
Sabrina akashikwa mkono na yule mtu hadi karibia na ule mstari ila alipotaka kuvuka akasita, yule Neema akawa anamvuta na kumwambia,
"Njoo Sabrina huku ni kuzuri zaidi"
Ila bado Sabrina akasita, yule Neema akaonekana kama kutaka kumvuta Sabrina ni hapo ambapo Sabrina alishtuka kutoka usingizini huku jasho jingi likimtoka.

Jeff naye akiwa amelala, alijikuta akiongea kwa nguvu na kumshtua mama yake ambaye alienda haraka kumgongea.
Jeff naye akaamka na kwenda kumfungulia mama yake huku akihemea juu juu,
"Vipi mwanangu kwani una matatizo gani?"
"Ndoto mama"
"Ndoto gani maana nimekusikia ukisema kwa nguvu hapana Sabrina hapana usiende. Ni kitu gani Jeff?"
Naye Jeff akashangaa kusikia kwamba hayo maneno alikuwa akiyasema kwa nguvu.
"Kwahiyo mama nilikuwa nasema kwa nguvu kabisa"
"Ndio, sasa unafikiri mimi ningejuaje kwa mawazo yako? Umemuotea vibaya Sabrina au ni nini?"
"Ni kweli, nimeota ndoto mbaya sana na kujikuta nikimzuia Sabrina asiende"
"Kheee sio mamdogo tena ni Sabrina tu inamtosha mmh makubwa haya"
"Mama naona vyema tukaendelee kulala tu, tutazungumza vizuri asubuhi"
Jeff aliona mama yake akitaka kubadilisha mada, hivyo akamuomba kurudi kulala tu.
Jeff alirudi chumbani kwake huku akitafakari ndoto aliyoiota kwani alimuona kamavile Sabrina akitumbukia ziwani tena ziwa lenye kina kirefu.
"Hii ndoto inamaana gani hii? Lazima kesho asubuhi niwahi ili nikamueleze Sabrina"
Alitafakari sana ila na usingizi nao ukakatika kabisa na kumfanya ashindwe kulala tena huku akiangalia tu masaa yanavyoenda kwa kasi na kuikaribisha alfajiri.

Sabrina naye kwa ile ndoto hakuweza kulala tena na kuona kama vile ni mkosi kwa usiku wake.
Alimtazama mtoto wake,
"Anataka nife halafu wanangu niwaache na nani? Hivi inamaana ningevuka ule mstari ndio ningekufa kweli? Mbona mambo ya ajabu haya?"
Sabrina hakuweza kulala tena huku akihofia kurudiwa tena na ile ndoto.
Na kulipokucha alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya chumba chake na alifanya hivyo ili kuangalia kama Sam ataondoka asubuhi hiyo basi aweze kufunga milango yao.

Jeff naye aliamka kwao na kujiandaa kisha akatoka, kabla hajafika mlangoni mama yake akamuuliza
"Unaenda wapi?"
"Hivi unajua kama mi ni mkubwa kwasasa mama?"
"Hata kama mkubwa ila kumbuka bado unaishi kwangu, haya asubuhi yote hii unaenda wapi?"
"Naenda kwakina Sabrina"
"Mmh hata kama kusoma sijui ila picha nimeelewa"
"Ndio maneno gani hayo mama?"
"Wee nenda tu, mi sina usemi"
Jeff akaondoka zake.
Sakina akajifikiria sana juu ya mtoto wake.
"Yani aliyemroga mtoto huyu wallahi amekufa kwamaana angekuwa hai angemuonea huruma. Jeff mwanangu ni mzuri, kila msichana anamtamani. Leo hii kweli akatembee na Sabrina? Mmh! Hivi huyu Sabrina nae haoni aibu kutembea na Jeff, mtoto aliyemlea kweli? Kweli binadamu hatuaminiki, nilimuamini sana Sabrina na wala sikufikiria kama ipo siku atatembea na mwanangu. Mmh Sabrina umenishinda jamani."
Sakina alijikuta akisononeka sana dhidi ya Sabrina ambaye alimuweka kama ndugu yake wa karibu.

Sabrina akiwa pale sebleni, muda kidogo akasikia mtu akigonga mlango na kumfanya ainuke na kwenda kumfungulia.
Alikuwa ni Jeff ambaye aliingia pale getini na kumkumbatia Sabrina ila Sabrina alitulia tu kwa kuhofia Sam kutoka ndani, na muda kidogo kweli Sam alitoka na kumuona Jeff akiwa amemkumbatia Sabrina.
Sam aliwaangalia tu, ila Sabrina alipomuona Sam akamtoa Jeff na kumfanya Jeff naye atazame kule aliposimama Sam akiwaangalia.
Jeff akapatwa na wazo la haraka kuwa aondoke ila akili yake ikamwambia kuwa kuondoka ni nidhamu ya uoga ukizingatia Sam ameshajua kila kitu.
Kwahiyo alichokifanya ni kwenda kumsogelea tu Sam na kumueleza kuwa ameota ndoto mbaya kuhusu Sabrina.
Muda huo Sabrina naye alikuwa karibu yao akiwasikiliza ndipo hapo na yeye alipopata ujasiri wa kuelezea ndoto yake mbele yao.
Na kumfanya Jeff ashangae na kuona alikuwa sawa kumuotea Sabrina kuwa yupo kwenye matatizo.
Sam naye aliikubali ndoto ya Sabrina kwani ndio mambo yaliyomtokea jana yake.
Sam akawauliza Jeff na Sabrina,
"Sasa tunafanyaje kuhusu hili?"
Sabrina akajibu,
"Hakuna jinsi, hapa ni wewe kwenda tu huko kaburini kwa Neema kuomba msamaha"
"Basi itabidi mnisindikize jamani"
Hakuna aliyepinga kwavile wote tayari wana makosa dhidi ya Sam.
Basi Sabrina akaenda kujiandaa na kumuachia mama yake watoto kisha wote watatu kuondoka yani yeye Sabrina, Jeff pamoja na Sam.

Wakiwa kwenye gari Sam alionekana kusikitikia sana maisha yake,
"Tukitoka huko naomba twendeni mahali nikawaeleze siri iliyojificha kwenye maisha yangu. Ila kabla ya yote nakuomba Sabrina wewe ndio uende kuulizia kwakina Neema kaburi lilipo."
Sabrina hakupinga swala hili na ilikuwa rahisi kwa Sabrina kwenda kwakina Neema na kuulizia lilipo kaburi la Neema na ilikuwa rahisi kuelekezwa kwavile baadhi ya ndugu walimuona siku ile hospitali.
Kisha akarudi tena kwenye gari na kuelekea makaburini alipoelekezwa.
Walienda moja kwa moja mpaka kwenye kaburi la Neema.
Wakasimama mbele ya kaburi lile huku Sam akiwa kwenye harakati za kupiga magoti kwa kumuomba msamaha marehemu, mara gafla wakashtuka kumuona Sabrina akianguka chini.

Wakasimama mbele ya kaburi lile huku Sam akiwa
kwenye harakati za kupiga magoti kwa kumuomba
msamaha marehemu, mara gafla wakashtuka
kumuona Sabrina akianguka chini.
Jeff alikuwa wa kwanza kuinama pale alipoanguka Sabrina na kumsaidia kuinuka huku akimpa pole na kumuuliza kuwa tatizo ni nini,
"Kwani vipi Sabrina? "
" Hata sielewi kwakweli, nashangaa tu na mimi"
Sam aliwatazama kwa muda wakati wanainuana kisha akamwambia Jeff kuwa amtoe Sabrina lile eneo la makaburi,
"Tafadhari Jeff, toka eneo hili na Sabrina niacheni mimi kwanza kwa dakika tano nitawafata mlipo. "
Jeff hakupinga kwani aliinuka pale na kuanza kukokotana na Sabrina kwavile alikuwa akichechemea kisha kutoka pale kwenye makaburi na kwenda kusimama mbali kidogo wakimsubiri Sam.

Sam aliamua kupiga magoti pale kwenye kaburi la Neema ili amuombe msamaha, kwavile hiko kitendo kilikuwa ni mara ya kwanza kwake kukitenda kwahiyo ilikuwa anafanya kama kulazimishwa tu kwani hakuwahi kufanya mambo kama hayo kabla.
Alianza kwa kuongea sauti ya kunong'ona ila alikuwa kamavile akizungumza na mtu kwavile alikuwa akitoa maneno ya kuomba msamaha huku akiamini kuwa Neema anamsikia,
"Tafadhari Neema nisamehe, naomba unisamehe sana. Halikuwa kusudio langu mimi kutokuja kwenye mazishi yako. Kwanza nilipatwa na mshtuko mkubwa sana kwa kifo chako kwani mwanzoni niliamini kuwa wewe ni mwanamke pekee uliyeweza kukaa na siri ya maumivu. Nilifarijika kwa wewe kukaa na siri ile huku nikiamini kuwa kuna kipindi nitapata dawa ya kuweza kukusaidia wewe na kukufanya uondokane na yale matatizo. Neema, tambua kwamba haikuwa kusudio langu wewe ufe, sikutaka kukuua Neema na ndiomana nilikuwa nakukwepa. Hata sijui ni shetani gani aliyenipata au aliyetupata hadi kutenda vile. Si kosa langu Neema, sikutaka kukuua. Tafadhari Neema.........!!"
Wakati Sam akiendelea kuongea akashangaa kuona pale mbele ya kaburi la Neema kama video imewashwa.
Kwenye ile video, akajiona yeye na Neema.
Akamuona Neema akichukua dawa na kuweka kwenye chakula ambapo yeye akala kile chakula chenye dawa. Akaona kama akili yake ikichanganyikana.
Kisha akamuona Sabrina akiwa sebleni ameshika simu, mara akamuona kama kateleza na kuanguka chini. Kisha akaona upepo mkali ukimuinua Sabrina pale chini na kisha kumbwaga kwa nguvu ni hapo alipoanza kutokwa na damu mdomoni.
Sam alikuwa akishangaa tu yale matukio aliyokuwa akiyaangalia na kuanza kuunganisha na akili yake.

Sabrina na Jeff walishangaa kuona Sam amekawia kumaliza kule makaburini na kujiuliza kuwa huenda Sam amepatwa na matatizo.
"Mmh mbona kakawia sana?"
"Huwezi jua labda ana mengi ya kuzungumza na marehemu."
"Mmh hapana, twende tukamuangalie bhana Jeff"
"Basi acha niende mie kumuangalia"
"Tunaenda wote"
"Wee Sabrina si ulianguka kule wewe? Unataka twende wote kweli jamani!"
"Ndio tunaenda wote"
Jeff akamsihi pale Sabrina ila hakusikia na kumfanya Jeff aseme kuwa wasiende kabisa,
"Basi tusiende, tuendelee kumsubiria tu."
"Kama hutaki kwenda naenda mwenyewe"
Sabrina akaanza kuongoza kuelekea makaburini na kumfanya Jeff amfate kwa nyuma tu kwani Sabrina alikuwa mbishi haswa.

Walipofika pale kaburini kwa Neema, wote watatu walishtuka kwani ile video iliyokuwa ikionyesha iligeuka kuwa tunguli mbili zilizofungwa vitambaa viwili vyenye rangi nyeusi na nyekundu.
Hiki kitu kiliwashtua sana na Sam alikuwa wa kwanza kukimbia na kuwafanya wao wamfate kwa nyuma.
Sabrina alianguka tena wakati akikimbia na kumfanya Jeff asimame kumsaidia anyanyuke kwanza na aweze kumkongoja kama mwanzo.
Jeff alimuhurumia sana Sabrina ila alimlaumu kwa ubishi wake na kujikuta akisema,
"Watoto wetu wasirithi tu huu ubishi wako"
Sabrina alimkata jicho Jeff ila aliendelea kukongojana nae hadi wakatoka nje ya lile eneo la makaburi.

Sam alikuwa kwa mbali kabisa akiwbngalia hadi pale walipomfikia.
Sam alisikika akiongea,
"Tupandeni kwenye gari jamani tuondoke yani sijui kama nitathubutu tena kuja makaburini"
Wakaingia kwenye gari ila Sabrina aliamua kumuuliza Sam kuwa kimetokea kitu gani kwani hata wao waliunganisha tu mbio.
"Yani ni mambo ya ajabu, ajabu kabisa sijapata kuona wala kuamini mambo haya jamani. Dah makaburini ndio kuna mambo hivi? Nilikuwa nasikiaga stori tu"
Jeff naye akaongea kwa uelewa wake,
"Ila sio makaburini kote kwenye mambo ya ajabu, huwa inategemea tu marehemu kafa vipi halafu pia kwenye marehemu alikuwa akijihusisha na nini enzi za uhai wake. Mbona makaburi mengine yapo kawaida tu huwa mtu anaweza kupita hata usiku wa manane juu ya kaburi na hakuna ubaya wowote"
"Ila kwa stahili hii mimi hunipitishi tena huko makaburini"
Sabrina nae akachangia,
"Kwani kulikuwa na nini? Mbona mi sijaona chochote!"
"Sasa mbona na wewe ulikimbia?"
"Nilikimbia kwavile niliwaona nyie mkikimbia"
"Mi niliona tunguli, na vile Sam alikimbia na ndiomana na mimi nikakimbia"
"Bora yenu na bora huyo Sabrina ambaye hajaona chochote ila alifata mkumbo tu hadi kaumia. Kuliko mambo niliyoyaona mimi jamani, kwakweli nilistahili kukimbia kwa........."
Sam alijikuta akifunga breki kwa gafla kwani alikuwa akiendesha huku akiongea.
Ila kuna mtu alitokea mbele ya gari yao na kumfanya afunge breki kwa gafla sana.
Wote watatu wakamuangalia yule mtu pale mbele kisha Sam akawaomba washuke kwa pamoja ili wamuulize kuwa yule mtu alikuwa na shida gani na kwanini alisimama barabarani hadi wao kutaka kumgonga.
Wakashuka na kumfata yule mtu ambapo naye alisogea pembeni ya barabara, Sam alikuwa ni mtu wa kwanza kumuuliza kuwa alikuwa na tatizo gani,
"Mbona ulisimama barabarani kwani tatizo ni nini? Hujui kama ni khatari? Ningeweza kukugonga pale"
"Nilijua usingenigonga na hata kama ungegonga basi usingenigonga mimi"
"Wewe ni nani na kwanini ukafanya hivyo?"
"Mimi ni mganga wa kienyeji, kazi hii sijaianza jana wala juzi. Ni kazi ambayo nimeifanya kwa muda mrefu sana toka nikiwa mdogo, katika uganga wangu sijawahi kumfata mteja ila wewe nimekufata"
Sam akashangaa na kuhamaki,
"Kwani na mimi ni mteja wako?"
"Wewe ni mteja wangu ndio, nishatengeneza dawa nyingi kwaajili yako bila ya wewe kujijua."
"Kivipi? Sikuelewi ujue!"
"Nielewe tu, ni hivi kuna mtu alikuwa anakuja kwaajili ya kukutengeneza wewe ni hapo uteja wa mimi na wewe ulipoanza. Mule ndani kwako nimeshaingia mara nyingi sana, na bila kunihitaji tena mimi nakuhakikishia kuwa ile nyumba yako hautaweza kuishi vizuri kwakile ambacho kimo ndani yake."
Sam akawaangalia wakina Sabrina kama wao wanajaribu kumuelewa huyu mganga kwavile yeye alishavurugwa na habari za makaburi akaona ni ngumu kumuelewa.
Sabrina alipoona Sam akiwaangalia sana aliamua kutoa ushauri,
"Sam, twende naye nyumbani kwako basi kwani hakuna jinsi hapa ukizingatia leo tumefata wenyewe haya mambo"
Sam hakupinga kwavile Sabrina ameongea ukizingatia ndiye mwanamke pekee anayemuamini ingawa ameshamsaliti kwa mara kadhaa.
Kisha wakapanda kwenye gari pamoja na yule mganga halafu safari ya kwenda kwa Sam ikaanza, hapo kwenye gari walikuwa kimya kabisa kwani hakuna aliyeweka stori ya aina yoyote ile.

Walipofika nyumbani kwa Sam walishuka na kuingia ndani kwa pamoja huku mlinzi wa Sam akiwakaribisha na kuwaangalia tu.
Waliingia na kwenda kukaa sebleni huku wote wakimsikiliza yule mganga kuwa anataka kufanya nini, ambapo yule mganga alianza kwa kuongea nao,
"Kwanza na huyu mwanamke namfahamu vizuri sana"
Huku akimuonyeshea Sabrina na wote kuwa kimya wakimshangaa kuwa Sabrina amejulikana vipi kwa yule mganga ila Jeff akahisi kuwa huenda vile ambavyo Sabrina alikuwa akipelekwa na mama yake yani Sakina kwa waganga hao. Ila Sabrina naye aliamua kuhoji kuwa yule mganga anamfahamu vipi,
"Kheee na mimi unanifahamu! Umenifahamia wapi?"
"Sio kwamba mmewahi kuonana na mimi la hasha ila mimi nimekuwa nikiwaona katika shughuli zangu za kiganga."
Ilibidi wawe makini na waweze kumsikia kuwa anataka nini kutoka kwao na kipi kilichompeleka kwao, yule mganga aliamua kuwaeleza kwa kifupi,
"Walikuja wabinti wawili wakiwa na lengo moja tu ila mmoja huyu alimsindikiza mwenzie. Waliitwa Rose na Neema, kwenye darubini yangu nilimuona huyu Rose akimshawishi Neema kuwa waje kwangu na kwavile Neema alijawa na tamaa dhidi ya kijana aliyeitwa Sam aliamua tu kufata ushauri wa rafiki yake kisha wakaja kwangu.
Mi kama mganga huwa hakuna kinachonishinda. Wao walihitaji Sam amsahau mkewe hilo halikuwa gumu kwangu ila tatizo huyu mke hata kama angesahaulika ingekuwa ngumu kukubaliana na hilo hata angeweza kuharibu dawa kwani katika darubini yangu niliona huyu mwanamke akiwa katika ulinzi mzito uliojificha"
Bado walitulia wakimsikiliza ila pale mwanzoni ilikuwa ngumu kumuelewa kuwa amedhamiria kitu gani.
Sabrina aliuliza kwanza,
"Neema unayemzungumzia hapa ni huyu marehemu au ni nani?"
"Ni huyo huyo marehemu hata huyo Rose ni marehemu pia"
Yule mganga akaendelea kuwaeleza kuhusu dawa ambazo aliwapatia na masharti ambayo aliwapa,
"Dawa zilikuwa za kumdhuru mke na kumvuta mume, ipo ambayo iliwekwa chini ya mti pale nje na ipo ambayo iliwekwa ndani baada ya Neema kukubalika kwa Sam kwa njia ya madawa. Ile iliyochimbwa chini ya mti nje ilikuwa na lengo kuwa huyu mke asiweze kufika hapa na kama akiweza basi adhurike. Ile dawa ilitolewa kabla ya kifo cha Neema, ya humu ndani sasa ni kulinda penzi yani mume asiweze kwenda kwa mkewe. Dawa hii itakuwa ikimuangalia kwa kila anachokifanya na inaweza kumpa adhabu iwapo akimkera muhusika ambaye ni Neema na ndicho kilichotokea kwako Sam"
"Bado sijakuelewa kabisa yani"
Sam alimwambia yule mganga kuwa hakuna anachoelewa.

Yule mganga aliamua kwanza kutoa ile dawa aliyowaambia kuwa ipo mule ndani na kufanya wote kubaki midomo wazi, kisha akawaeleza jinsi Sam alivyowekewa dawa kwenye chakula na jinsi dawa aliyomtupia Sabrina ilivyomtesa.
"Kilichonifanya nijionyeshe kwenu ni hii dawa tu ambayo ilikuwepo humu ndani kwani sikuwa na la kufanya na pia hii dawa haikutakiwa nije kuitoa kishirikina. Ilitakiwa nije kama nilivyo na ndiomana nikafanya hivi ila kwa kifupi Sam tambua kwamba haikuwa akili yako wewe kumchukia mkeo na wala kwa mkeo haikuwa makusudi ya Mungu yeye kuumwa kiasi kile, ni mambo tu ya duniani"
Jeff alielewa ni jinsi gani mama yake anapenda kwenda kwa waganga kwani hiyo ya kutokuaminikuwa kitu fulani ni mipango ya Mungu ndio kilichomfanya awe maarufu kwa kuhudhuria kwa waganga na kudanganywa.
Akajikuta akimuuliza mganga huyu kama anamfahamu mama yake,
"Hivi mama yangu humfahamu kweli?"
"Anaitwa nani?"
"Anaitwa Sakina"
Yule mganga akafunga macho ya dakika kadhaa kisha akaadha kumuelekeza Jeff kuhusu Sakina anayehisi ndiye mama yake,
"Sakina ninayemuona mimi kuwa ndio mama yako yupo hivi, aliachwa na mumewe miaka ya nyuma iliyopita. Historia yake ni kwamba yule mwanaume alitafutiwa kwao na kuolewa nae ila hawajawahi kupendana katika maisha yao. Aliishi na yule mwanaume ila mwanzoni mwanaume huyo alimuheshimu sana mkewe na kuanza kumpenda ingawa ni mwanamke aliyechaguliwa kwao. Ila katika pita pita mwanaume huyo akapata mwanamke ambapo yule mwanamke alimkorogea madawa ya kumvuta. Kitendo hicho hakikukubaliwa na mama yako, naye akaenda kwao na kumletea madawa mumewe. Huyu mume alikuwa njiapanda kachanganywa na madawa, kuna mdada alikuja kwangu akidai kuwa huyu kijana ni yeye ndiye aliyestahili kuolewa nae, nikamtengenezea dawa. Kwahiyo yule mume aliondoka kimoja kwa mama yenu, na nina uhakika hadi leo hamjamuona wala hamjui alipo"
Jeff alishangaa sana kwani yote yalimlenga mama yake kweli, na sasa akaelewa sababu ya baba yake kutokuonekana tena nyumbani.
"Ila wewe mganga ni mbaya kwakweli, tena ni mbaya sana. Kwanini madawa yako unafanya mtu anaisahau familia yake? Hebu ona huyo baba hata mimi mtoto wake kanisahau kweli? Sijapenda dawa zako jamani. Kwanza mapenzi gani haya ya madawa jamani?"
Akawaangalia kwa zamu Sam na Sabrina kisha akauliza tena,
"Je haya ni mapenzi? Kweli jamani, yani mtu anapenda kwa madawa? Sasa ndio mapenzi gani haya?"
Jeff alionyesha kuchukizwa sana na hii stori aliyoelezewa na huyu mganga kumuhusu mama yake kwani siku zote alijipa matumaini kuwa ipo siku baba yake atarudi ila kumbe kuna mtu kamfunga kwa madawa.
Jeff aliinuka pale na kuanza kuondoka kwani alishaumizwa tayari.

Jeff alitoka nje kabisa na hakuna aliyemzuia kwani hata alipokuwa akitoka ndani yule mganga alipotaka kumzuia, Sam alimwambia amwache tu aende kupumzika.
Jeff alitoka kabisa kwenye eneo la nyumba ya Sam huku akielekea stendi kupanda daladala.
Gafla mbele yake akatokea yule mganga na kumwambia,
"Turudi, bado hatujamalizana mi na wewe"
Jeff akashtuka kwavile alimuacha ndani huyu mganga.
Ni hapa ambapo Jeff aliamua kukimbia ila mbele kidogo alijikwaa na kuanguka.


"Turudi, bado hatujamalizana mi na wewe"
Jeff akashtuka kwavile alimuacha ndani huyu
mganga.
Ni hapa ambapo Jeff aliamua kukimbia ila mbele
kidogo alijikwaa na kuanguka.
Alipoinuka alijikuta mlangoni kwa Sam na kuamua kukimbilia ndani kama ishara ya kukwepa kinachomfata.
Sam na Sabrina wakamshangaa kwa ujio wake wa kuhema wakati aliondoka kwa hasira.
Sabrina alikuwa wa kwanza kuinuka na kumshika Jeff kwani alikuwa kama mtu aliyepandwa na wenge,
"Vipi wewe Jeff, una tatizo gani?"
Jeff akaangaza kote na kuwaona wote yani Sam pamoja na yule mganga wakiwa wamekaa tu wakimuangalia na kumfanya ashangae zaidi kwani yule mganga ndiye aliyemfanya ajikwae na kuanguka.
Sabrina ilibidi amfanye Jeff akae kwenye kiti ili aweze kutulia kwavile aliona hapa swali lake likiwa halijajibiwa.
Yule mganga alikuwa kimya tu na kuwaangalia katika harakati zao za kumtuliza Jeff, kisha walipotulia ni hapo ambapo yule mganga alianza tena kuzungumza,
"Hamtakiwi kunifanyia hasira mimi, wafanyieni hasira binadamu wenzenu wasiopenda maendeleo yenu ila kunifanyia hasira mimi ni sawa na kusumbua miyoyo yenu tu. Tulieni hapa kwanza ili tumalizane kwa amani kabisa"
Sam naye akauliza,
"Kwani kipi kimempata huyu mwenzetu?"
"Akili yake ikitengemaa atawaambia yeye mwenyewe. Ngoja tumalize haya kwanza"
"Haya nakusikiliza, tuambie cha kufanya ili tumalizane nawe."
"Cha kufanya ni hivi, mnatakiwa kunipa gharama zangu za kuweka mambo ya hapa sawa"
"Hilo sio tatizo, kuna lingine?"
Huyu mganga akakaa kimya kwa muda kwanza kwani alijua kuwa hawa watahitaji msaada mwingine kutoka kwake ila hakuna walichomuomba zaidi ya kutaka amalize yale mambo yake aliyoweka kwenye nyumba ile.

Mama Sabrina alishangaa sana kwa Sabrina na hao wakina Sam kukawia kurudi kiasi kile,
"Hivi hawa watu hawa wana akili gani? Hivi hawajui kama kuna watoto wadogo wamewaacha humu ndani jamani?"
Alikuwa na kibarua kizito kwa siku hiyo cha kuwabembeleza wajukuu zake wote wawili.
Muda kidogo akafikiwa na ugeni, mgeni huyo alikuwa ni wifi yake mdogo na kumkaribisha kwani alishamaliza swala la ugomvi wake na yeye.
"Karibu sana"
"Mbona watoto wote umebaki nao mwenyewe?"
"Wee acha tu yani, wajina wako kaondoka hapa asubuhi na mapema akiwa na mumewe ila hajarudi hadi muda huu"
"Kwani ameanza tena kuishi kwa mumewe?"
"Hapana, ila alikuja tu kumsalimia"
"Afadhari maana napatwa na hisia mbaya sana dhidi ya nyumba ya mumewe"
"Hisia zipi hizo?"
Shangazi wa Sabrina hakujibu ila alimchukua yule mtoto mdogo wa Sabrina na kumshika kisha kubadili mada baada ya kumuangalia tu,
"Kheee huyu mtoto kila anavyoendelea kukua ndio anavyozidi kufanana na kale kakijana ka Sakina. Ama kweli dunia haina siri"
Mama wa Sabrina alimuangalia kwa makini na kumuuliza kuwa anamaanisha kitu gani,
"Unajua wifi yangu huwa una maneno ya mafumbo sana wewe, sijawahi kukuelewa kwa haraka kwakweli. Unamaanisha nini?"
"Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye sikio haambiwi sikia. Kusoma hujui hata picha huoni? Siongei mengi siku hizi sababu sitaki kugombana na watu hususani wajina wangu"
Mama Sabrina akatulia kidogo ili kuepusha maneno na yeye.

Sakina nae akiwa nyumbani kwake alijikuta akifikiria kuhusu Sabrina na Jeff,
"Hivi kama kweli huyu Jeff mwanangu anamahusiano kweli na huyo Sabrina hivi mi nitafanyaje jamani? Mbona kinaona kama nazidi kuchanganyikiwa? Ngoja niende leo nikazungumze na Sabrina nipate ukweli wa mambo."
Akatoka pale kwake na kuanza kuelekea kwakina Sabrina.

Yule mganga akaanza tena kuendelea na hoja zake ambapo aliwauliza wakina Sam,
"Vipi hamtahitaji msaada mwingine toka kwangu?"
Huku akimtazama Jeff na kuuliza tena,
"Hata wewe huhitaji msaada wa kuweza kumrudisha baba yako?"
Jeff alimuangalia tu yule mganga bila ya kujibu chochote na kufanya Sam aongee kwa kumsihi yule mganga kuwa amalizane nao tu,
"Mganga tumefurahi kukufahamu, iwapo kutakuwa na tatizo lolote basi tutakuita tena kwahiyo hakuna tatizo kwa sasa. Tumalizane tu na mambo haya kwanza."
Basi yule mganga akaamua kumwambia kwanza Sam kiasi anachohitaji kwa muda huo ambapo kwa Sam haikuwa tatizo sababu pesa alikuwa nayo ila aliwaomba waondoke wote ili aweze kwenda kumtolea mganga huyo pesa toka kwenye mashine za kutolea hela.
Kwahiyo wakainuka pale na kwenda kupanda kwenye gari ya Sam kisha safari ikaanza hadi pale Sam alipofika kwenye kituo cha kuwekea mafuta na kusimamisha gari kisha yeye kwenda kwenye mashine ya kutolea pesa.
Kwenye gari alibaki yule mganga pamoja na Sabrina na Jeff ambao wao walikuwa wamekaa kiti cha nyuma cha gari lile.
Yule mganga akawaangalia na kusema,
"Halafu ninyi ni wapenzi, halafu hamtaki niwasaidie shauri yenu."
Jeff na Sabrina wakatazamana huku Sabrina akitamani huyu mganga aende zake tu maana aliona anawaharibia mambo yao tu.
Jeff aliiona hasira ya Sabrina kwa yule mganga hivyo akaamua kumshika mkono Sabrina.
Yule mganga aliwaangalia zaidi na kumfanya apate kingine cha kuongea,
"Tena mapenzi yenu ni siri, kumbuka wewe ni mke wa mtu"
Huku akimuangalia Sabrina na kumfanya Sabrina azidi kupatwa na hasira na kumjibu,
"Kama mke wa mtu je!"
Jeff akamziba Sabrina mdomo kwani alijua ataendelea kuropoka zaidi, ni muda huo Sam alirudi kwenye lile gari na kukuta Jeff kamziba mdomo Sabrina,
"Kwani vipi jamani?"
Jeff alimuachia Sabrina ila yule mganga ndiye aliyejibu tena lengo lake likiwa kuwakomesha Sabrina na Jeff,
"Kwani wewe hujui?"
"Kujua nini?"
"Hujui kama mkeo ana mahusiano na huyo kijana!"
Sam hakuongea kitu zaidi ya kuwaangalia tu Sabrina na Jeff ambapo Sabrina aliinamisha kichwa chini.
Sam akatoa pesa na kumkabidhi yule mganga kisha akamwambia,
"Niambie pa kukurudisha sasa"
Yule mganga akamuomba Sam amshushe hapo hapo kwenye kituo cha mafuta.
"Hapana, haitakuwa njema kukuacha hapa. Wee niambie tu pa kukupeleka"
Kisha akamuelekeza, na safari ikaanza huku wakiwa kimya kimya kwenye gari.

Sakina nae alifika kwakina Sabrina na kumkuta mama wa Sabrina na shangazi mtu.
Aliwasalimia na kumuulizia Sabrina,
"Huyo Sabrina hayupo, ameondoka hapa asubuhi na mapema akiwa ameambatana na Sam pamoja na Jeff. Walisema watawahi kurudi ila nashangaa kuwa hawajarudi hadi muda huu, sijui tatizo ni nini kwakweli"
Sakina aliinama kwa dakika kadhaa akimfikiria mwanae kuwa imekuwaje kaondoka na watu hao.
"Kumbe Jeff ile asubuhi alikuja huku kweli!"
"Mwanao hapa imekuwa ni sehemu ya salamu yake ya asubuhi, kila siku lazima apite hapa"
Hoja hiyo ilizidi kumpa maana Sakina na kujikuta akimuuliza mama wa Sabrina,
"Hivi mama, wewe unahisi nini kinaendelea hapo?"
"Kuendelea kivipi? Sijui chochote kwakweli"
Shangazi wa Sabrina akadakia kama kawaida yake,
"Kusoma hamjui hata picha hamuoni loh!"
Sakina akauliza tena,
"Unamaana gani shangazi?"
"Kaa hapo na umshike huyu mtoto umbembeleze kidogo"
Sakina akakaa kisha shangazi akamkabidhi Sakina yule mtoto mdogo wa Sabrina amshike.

Sam alimfikisha yule mganga mpaka kwenye eneo alilosema kisha akashuka ili awaache waende.
Sam akageuka nyuma sasa na kusema,
"Sabrina, njoo ukae hapa mbele tafadhari"
Sabrina hakupinga, akashuka na kwenda kukaa kwenye kiti cha mbele karibu na Sam huku wakimuacha Jeff siti ya nyuma.
Sam akaondoa ile gari huku akitabasamu ila Jeff na Sabrina walikuwa kimya kabisa.
Walipokuwa njiani, Sam akamuona mtu aliyemfahamu na kumfanya asimamishe gari.
Mtu huyo alikuwa ni Aisha yani yule dada aliyekuwa akiishi na marehemu Neema kabla ya kifo chake.
Sam akaona ni vyema wampe lifti dada huyo,
Akamuuliza kwanza,
"Unaelekea wapi Aisha?"
"Naenda nyumbani"
"Tafadhari naomba panda kwenye gari tukusogeze kidogo"
Kisha Aisha akapanda na kukaa pamoja na Jeff kwenye ile siti ya nyuma.
Kabla Sam hajaondoa gari, akaona ni vyema akiwatambulisha kwanza,
"Aisha, huyu ni mke wangu anaitwa Sabrina"
Kisha akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Huyu anaitwa Aisha, ni mdada aliyekuwa akiishi na Neema kabla ya kifo chake"
"Namkumbuka huyu, nilimuona nyumbani kwa Neema siku mauti ilipomkumba"
Sam akashtuka kidogo kusikia kuwa Sabrina alikuwa nyumbani kwa Neema siku aliyokumbwa na mauti, na kwamaana hiyo Neema alimwambia siri yote Sabrina na ndiomana ikafa.
Ingawa Sam alishtuka ila hakupenda hawa wagundue mshtuko wake, kisha akamtambulisha Jeff kwa Aisha,
"Na huyo ni kijana wetu anaitwa Jeff"
"Mmh kama nimewahi kukuona mahali vile"
Sabrina akategesha sikio lake kwa umakini ili asikie kuwa ni wapi ambapo huyo Aisha alimuona Jeff ila muda huo huo Jeff nae akajibu,
"Itakuwa uliniona siku ile hospitali nilipomfata Sabrina"
Sam akaona jinsi gani mzunguko wa siri yake umezidi kuwa mpana hivyo akaamua waendelee na safari yao sasa kwani utambulisho ulishaisha.
Kisha akamfikisha Aisha eneo lake husika, wakati Aisha anashuka alimpa simu Jeff amuandikie namba yake kwa madai kuwa kuna jambo anataka kumwambia, kisha akaijaribisha pale na kuita halafu yeye akashuka.
Kwakweli kitendo cha Aisha kubadilishana namba na Jeff kilimuumiza sana Sabrina ni hapo alijua kuwa amejawa na wivu wa mapenzi, tena mapenzi ya Jeff ila hakuweza kusema ni jinsi gani ameumizwa kwa kumuhofia Sam atamuonaje.

Safari ya sasa ilikuwa ni kurudi kwakina Sabrina, ni hapa ambapo Sam akaongea kwanza,
"Jamani, niliwaambia kuwa kuna mengi nataka tuzungumze ila kwa yaliyotokea leo nimekosa hata muda wa kuyaongelea. Najua Sabrina unatakiwa kuwahi nyumbani sababu ya mtoto, ngoja tukuwaishe ila tafadhari sana ninachohitaji kuzungumza nanyi ni muhimu sana. Sasa sijui tufanyaje!"
Jeff akachangia,
"Nadhani ni vyema kama tutazungumza kesho"
Sam akakubaliana na hili wazo kwani aliona kidogo lina mantiki kwavile muda ulikuwa umeenda kweli.
Kwahiyo safari ya kurudi ikaendelea.

Sakina alikuwa katulia kabisa huku kamshika mtoto wa Sabrina ambapo shangazi akamuuliza,
"Umeelewa nini hapo?"
Sakina akatingisha kichwa kuwa hajaelewa chochote,
"Basi ngoja nikubadilishie swali, vipi mtoto unamuonaje?"
"Namuona ni mtoto mzuri na mwenye afya"
"Kafanana na nani?"
Sakina akaguna kwanza kwani jibu ni wazi kuwa mtoto huyo kafanana na Jeff, ila hakutaka kutoa jibu la moja kwa moja kwanza kwani alimtazama mama wa Sabrina ambaye ni bibi wa mtoto na kumuuliza kwa kujishuku,
"Eti mtoto si kafanana na wewe bibi yake?"
Mama wa Sabrina akacheka tu, ni hapo ambapo shangazi akaongea tena,
"Najua wazi mnafahamu ukweli ila mnajaribu kuukwepa ukweli huo. Haya mambo hayanihusu ni juu yenu wenyewe katika jitihada zenu za kukwepa ukweli."
Sakina na mama Sabrina wakatazamana tena.
Muda kidogo wakina Sabrina nao walikuwa wamerudi.
Wakasalimia pale kisha Sam akaaga kuwa anaondoka, ni hapo ambapo shangazi wa Sabrina nae akaaga ili aweze kupata lifti ya Sam.
Ila Sam kabla ya kuondoka akamuita kwanza Sabrina pembeni na kumwambia,
"Sabrina, ingawa kwa yote yaliyotokea tafadhari niheshimu. Nipe heshima yangu kama mumeo."
Kisha Sam akaondoka huku akiambatana na shangazi wa Sabrina.

Nyumbani walibaki wanne sasa, Sabrina, Sakina, Jeff na mama Sabrina ambapo Jeff nae alijifanya kuaga kuwa anaenda nyumbani.
Sakina nae akaona ni vyema aongozane na mtoto wake.
Kwahiyo wakaondoka.
Ni hapo hata mama Sabrina aliona ni bora atumie muda huo kupumzika kwani kazi ya kubembeleza watoto wawili kwake ilikuwa mtihani tena kwa siku hiyo ukizingatia kuwa walisumbua sana kwahiyo akaona vyema akapumzike tu.

Sam alimpeleka shangazi wa Sabrina hadi anapoishi kisha yeye kuondoka.
Ingawa alifanya mizunguko yote hiyo kwa siku moja ila bado hakuwa na amani ya kurudi nyumbani kwake na kuamua kurudi tena kwakina Sabrina ili akapumzike huko.

Bado Sabrina aliumizwa na kile kitendo cha Jeff kubadilishana namba na Aisha.
Akaamua kuchukua simu ya mama yake na kuwasiliana na Jeff kwa kumuonya kuwa asiwasiliane na yule dada.
"Tusiongee kwenye simu Sabrina, acha nije huko kwanza"
Muda kidogo Jeff alifika kwakina Sabrina na kumkuta Sabrina pale sebleni.
"Tena naomba uifute hiyo namba sasa hivi"
"Hata jina sijaiandika, usinifikirie vibaya Sabrina tafadhari"
Sabrina akajisikia aibu kidogo kwa wivu aliokuwa nao dhidi ya Jeff ukizingatia kuwa Jeff ni kijana mdogo sana kwake.
Sabrina akasimama na kuangalia pembeni kwa aibu yake.
Jeff naye akasimama na kwenda nyuma ya Sabrina na kumkumbatia na kusahau kuwa wapo sebleni.
Jeff alimkumbatia kwa nguvu sana Sabrina na kufanya roho yake isuuzike.
Wakiwa kwenye staili ile, mlango wa kuingilia sebleni ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sam. Na mbele yao alitokea mama yake Sabrina kutoka chumbani kwake, kwahiyo macho ya mama Sabrina na macho ya Sam yalikutana katika kumshangaa Jeff na Sabrina.

Wakiwa kwenye staili ile, mlango wa kuingilia
sebleni ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Sam.
Na mbele yao alitokea mama yake Sabrina kutoka
chumbani kwake, kwahiyo macho ya mama
Sabrina na macho ya Sam yalikutana katika
kumshangaa Jeff na Sabrina.
Macho ya mama Sabrina yaliwashtua sana Sabrina na Jeff kwani ndio alikuwa upande wao, Sabrina alijiondoa haraka kwenye mikono ya Jeff ambaye alikuwa kwenye harakati za kumbusu.
Sabrina alivyojiondoa kwenye mikono ya Jeff ndipo alipogeuka nyuma ili ayakwepe macho ya mama yake ila hapo akagongana na macho ya Sam na kujikuta akikumbuka neno la mwisho la Sam kuwa anahitaji kuheshimiwa.
Aibu ikamjaa zaidi Sabrina na kujikuta akimfata Sam kama kuhitaji kumkaribisha ili kujigelesha na kuiondoka aibu ile ingawa imesha mfedhehesha.
"Karibu Sam"
Sam alimuangalia Sabrina na kutikisa kichwa kama ishara ya kusikitika.
Mama Sabrina nae akaona wazi kuwa kitendo cha yeye kuendelea kuwa hapo na kushangaa kitazidi kumkasirisha Sam, hivyo akajifanya kamavile hakuona na kuelekea jikoni.
Jeff alikuwa kasimama pale pale huku akiogopa hata kugeuka na kumtazama Sam ambapo akaisikia sauti ya Sam ikisema kwa taratibu kabisa,
"Umeshinda Jeff, mtoto mdogo lakini umenishinda akili"
Jeff alikuwa kimya kabisa kwani hata uoga ulianza kumjaa na kutamani hata kurudisha masaa nyuma.
Ile hali aliyokuwa nayo Jeff, Sam aliielewa vizuri sana.
Akamfata na kumshika mkono kisha akatoka naye nje, kitendo hicho kilimpa mashaka Sabrina na kuamua kuwafata ili kuona kitakachoendelea.
Ila Sam alipofika na Jeff nje akamwambia,
"Nenda nyumbani, ila kesho njoo unisindikize na mke wangu tukielekea nyumbani kwetu"
Jeff alitikisa kichwa tu kwani uoga aliokuwa nao kwa muda huo ulikuwa wa hali ya juu.
Kisha akaondoka huku akiwa haamini kama ameweza kuondoka salama.

Sabrina alipoona kuwa Jeff kaondoka ndipo na yeye aliporudi ndani huku Sam akiwa nyuma yake ambapo alimuuliza swali kwa sauti ya chini tu.
"Wakati naondoka nilikwambiaje Sabrina?"
Sabrina alikuwa kimya kanakwamba hajasikia swali aliloulizwa na Sam ambapo walifika pale sebleni kisha Sabrina akakaa na Sam nae akakaa ambapo akamwambia tena,
"Kesho tutarudi nyumbani."
Sabrina bado akajifanya hajasikia na kuamua kumuuliza swali lingine Sam,
"Kwani na leo unalala hapa hapa?"
Sam akatabasamu tu kwani alijua wazi kuwa Sabrina anakwepa kile ambacho alikisema na kuamua kumuitikia tu kuwa atalala pale pale.
"Basi ngoja nikakuandalie kile chumba cha jana"
Sabrina aliinuka na kwenda kuandaa chumba hicho.
Muda mfupi tu akatoka tena mama Sabrina na kumfata Sam pale kwenye kochi na kumwambia,
"Samahani mwanangu kwa yaliyotokea"
"Usijali mama"
"Ushaingiza gari yako ndani? Kama bado twende nikakufungulie geti uingize"
Kisha Sam akainuka na kuelekea nje ili aweze kuingiza gari.

Jeff aliingia kwao na kumkuta mama yake pale sebleni ila alisahau kumsalimia tena na kupitiliza chumbani.
Sakina akahisi kuwa lazima kuna kitu kwa mwanae kwani ile hali haikuwa ya kawaida. Na akajua tu kuwa ni ni lazima hicho kitu kipo huko alipotoka Jeff kwa wakati huo na kwa haraka haraka akahisi tu lazima atakuwa ametoka kwakina Sabrina hivyo akaamua kuinuka na kwenda kwakina Sabrina ili kuchungulia kuwa kuna kitu gani kilichotokea.
Alifika karibia na kwakina Sabrina na kuona kuna gari ikiingia ndani na kuigundua kuwa ile ni gari ya Sam.
Akatamani kwenda kuulizia ila akajiona kuwa ataonekana ni mmbea sana na kuamua kurudi nyumbani kwake ila alipofika tu akamuita mwanae Jeff ambaye alitoka pale sebleni na kumsikiliza mama yake,
"Una matatizo gani kwani mwanangu?"
"Kwanini mama?"
"Mbona ulipita hapa bila hata ya kunisalimia halafu akili yako inaonyesha kuwa haupo sawa kabisa"
"Nisamehe kwa kutokukusalimia mama ila nipo kawaida tu kwani sina tatizo lolote mama"
"Haya na leo kutwa nzima ulikuwa wapi toka asubuhi ile?"
"Kheee mama jamani ndio unanifukuza hapa nyumbani au? Nina mengi ya kuzungumza na wewe yangu ila yapo ya muhimu zaidi nitakwambia ila kesho"
"Hapana, naomba uniambie muda huu huu. Unajua watu kama sisi tukiambia kuna kitu cha kuambiwa huwa hatupendi kusubiri tafadhari sana niambie leo leo tena muda huu"
Jeff akacheka kidogo kwani alimtambua vizuri mama yake kuwa ukimwambia kitu si mtu wa kusema kuwa asubirie yani yeye hupenda kuambiwa hapo hapo ingawa mara nyingine humfanyia ngumu ya kutokumwambia.
Ila leo aliamua kumdokezea tu kwa yale aliyoambiwa kuhusu baba yake,
"Kwahiyo umeacha kufanya kazi zako ukaanza kufatilia kuwa baba yako alipatwa na nini!"
"Sio hivyo mama, hii khabari imekuja tu bila hata mi kuihitaji ila nimeona wazi kuwa itakuwa na umuhimu sana katika maisha yangu na yetu pia"
Kisha Jeff akamwambia mama yake jinsi alivyoelezwa kukutana kwa mama yake na baba yake ila kabla hajamalizia mama yake aliinuka na kwenda chumbani.

Sakina alionekana kushikwa na uchungu sana kwani kule chumbani alienda kukaa na kujiinamia huku machozi yakimtoka kwa mfululizo kwani alikumbuka alivyokuwa akiishi na mumewe, mambo yaliyotokea na mpaka mwisho wa siku kutokomea kabisa kwenye macho yake na macho ya mwanae. Kwa muda huo alikuwa na maumivu sana ila alimsikia mwanae akimgongea mlango na kumfanya afikirie sana na kuona kuwa mwanae hana makosa na anatakiwa kujua ukweli wa mambo yote ukizingatia kwasasa mwanae ameshakuwa mtu mzima.
Moyo wa huruma dhidi ya mwanae ukajaa na kuamua kwenda kufungua mlango ili akaendelee kuzungumza na mwanae,
"Nisamehe mwanangu."
"Usijali mama naelewa, na pole sana mama yangu"
Sakina alimuangalia mwanae kisha akaenda naye sebleni ili wakae na waweze kuzungumza.
Sakina alianza kwa kumwambia mwanae,
"Sikia Jeff mwanangu nikwambie kitu kuhusu mi na baba yako, yani haya mapenzi haya wee yaache tu"
"Kwani mama wewe na baba si mlikuwa mnapendana lakini?"
"Kupendana ndio, lakini kupendana kwetu ni kulitengenezwa"
"Kivipi mama?"
Jeff alikuwa makini sana kumsikiliza mama yake,
"Kabla ya mimi kuwa na baba yako, alikuwepo kijana mmoja ambaye alinipenda sana na hata mimi nikampenda. Tatizo kwa yule kijana ni kuwa alikuwa masikini kipindi hicho, hakuwa na uwezo hivyobasi kwetu hawakumkubali kabisa na kunitafutia kijana mwingine ambaye ndio huyo baba yako. Kwa kipindi hicho alionekana kuwa na nia sana ya kuoa na ndipo aliponiona na nikaja kuishi nae mjini. Maisha yalikuwa mazuri sana kabla ya lile lishetani kuingilia mapenzi yetu. Nimefanya kila jitihada za kuweza kumrudisha baba yako kwenye mstari lakini juhudi zangu zimegonga mwamba kwani ndio kwanza yametokea mashetani makubwa zaidi na kumtokomeza baba yako. Kwakweli huwa naumia sana nikimfikiria, tungekuwa tunafurahia maisha yetu ila ndio hivyo kaniachia wewe tu"
"Pole sana mama, ila Mungu ni mwema. Tumuombee tu baba kuna siku atatukumbuka familia yake"
"Hata mi naamini hivyo mwanangu"
"Ila mama huyo aliyekuwa akikupenda zamani yuko wapi siku hizi?"
"Yani maisha haya yaache tu huwa hayatabiriki, saivi ana maisha yake mke na watoto. Ni mfanyabiashara mkubwa sana huwezi hata kufikiria kuwa ni yeye, roho huwa inaniuma sana najutia kwa kusikiliza maneno ya watu kuwa nitakufa masikini nikiwa na yule mwanaume ona sasa hapa nilipo hata sijielewi"
"Ila je huyo mtu bado unampenda mama? Na vipi yeye bado anakupenda?"
"Hayo maswali sitaki, hebu tukalale kwanza"
Sakina aliyasema hayo huku akitabasamu na akionekana kama kujifuta tu machozi, hivyo Jeff akaamua kumuaga tu mama yake kisha yeye kuelekea chumbani kwake kwani alijua wazi kuwa kuendelea kuzungumza nae ni kuzidi kumpa uchungu.

Jeff alipoingia chumbani kwake alienda kukaa kitandani na kujikuta akitafakari maneno ya mama yake na kuwaza jinsi maneno ya watu yanavyovunja mahusiano,
"Ila kwakweli mimi nina haki yote ya kuwa na Sabrina kwanza nampenda halafu na yeye ananipenda, pili bila ya mimi pengine Sabrina angeshakuwa marehemu kwa siku nyingi sana. Ingawa Sabrina ni mkubwa kwangu ila mimi ndio nimeshampenda, na kama ingekuwa ni hairuhusiwi kwa kijana mdogo kumpenda mdada basi ingekuwa ngumu kwa mimi kumpenda Sabrina. Ila hadi nimempenda na kumuacha siwezi basi ni wazi kwamba Mungu aliniandikia kuwa niwe nae. Haya mengine ni mapito ya muda tu kwani najua kuwa ipo siku Sam atagundua jinsi upendo wangu ulivyo kwa Sabrina ni zaidi ya upendo wake. Kwakweli nampenda sana Sabrina na ni Mungu pekee ndiye anayetambua upendo wangu kwa huyu dada"
Jeff alijifikiria sana na akawaza pia jinsi atakavyokutana na Sam kesho yake na kama atamuuliza tena kuhusu alichokuwa anafanya na Sabrina, ni hapo ambapo moyo wake ukaghairi kwenda kuwasindikiza wakina Sam kwa siku hiyo ya kesho.

Sam alipoamka asubuhi alitoka sebleni na kumkuta Sabrina nae akiwa tayari pale sebleni na kumuomba kuwa aanze kujiandaa ili warudi kwenye nyumba yao.
Hata mama Sabrina alipotoka ndani, Sam alimpa hoja hiyo hiyo.
"Ila mwanangu mbona mapema sana? Hata baba yenu sijamwambia kuhusu hili."
"Ila mama, kumbuka kwamba Sabrina ni mke wangu na pia nina uwezo wa kulea watoto ninao sasa kwanini nisiichukue familia yangu?"
"Lakini kumbuka kuwa baba Sabrina alishakataa hilo swala"
"Naelewa mama ila kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa, najutia makosa niliyoyafanya hapo awali ila kwasasa naomba nipe ruhusa tu nikaendelee kuishi na mke wangu"
Mama Sabrina alijitahidi kumuomba Sam kuwa amuache Sabrina pale ila Sam hakukubali na kuendelea na hoja zake ambazo kweli zilikuwa za msingi na kumfanya mama Sabrina kuwaruhusu tu.
Ila kabla ya kuondoka akamvuta mwanae pembeni na kuzungumza nae kidogo,
"Kwakweli kile kitendo kilichotokea jana usiku baina yako wewe na Jeff sijakipenda, tena sijakipenda kabisa. Sabrina mwanangu hebu jaribu kufikiria kuwa una watoto na kubwa zaidi una mume. Halafu jambo lingine ni kuwa sijaona mantiki ya wewe kuwa karibu na Jeff kiasi hicho na hata ile simama yenu ya jana na mabusu yenu sikuyaelewa kwakweli. Tafadhari Sabrina mwanangu usitake kuniaibisha mama yako, utanitia aibu jamani. Yule Jeff ni kama mdogo wako au mwanao, haendani kabisa na wewe. Hebu kaache kale katoto kakawe na watoto wenzie, usinitie aibu jamani"
Sabrina alikuwa ameinama tu akiangalia chini ila maneno ya mama yake yalimuingia vizuri ingawa mama Sabrina aliona kamavile hasikilizwi na kuamua kumuuliza,
"Hivi unanielewa kweli Sabrina?"
"Nakuelewa mama ila usinifikirie vibaya"
"Nisikufikirie vibaya vipi wakati mambo nayaona wazi! Sabrina watoto wako bado wadogo, tulia ulee watoto na mumeo acha tabia za kuruka ruka. Nilikuwa nakuamini sana na wala sikuwa na shaka nikikuona na Jeff ila jana umenipa mashaka kwakweli. Kuwa makini Sabrina tunza ndoa yako"
Mama Sabrina alimaliza hapo kumpa mwanae semina fupi ya kuhusu ndoa.

Sabrina alirudi alipo Sam na kumtaarifu kuwa tayari waende ila mama Sabrina hakuweza kuwaruhusu kuondoka na watoto wote kwa siku hiyo, hivyobasi wakaondoka na yule mdogo sana.
Wakati wanaondoka Sam akakumbuka kuhusu Jeff na kumwambia Sabrina kuwa wakampitie Jeff kwanza,
"Kwanini tumpitie Jeff jamani si twende tu"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana Sabrina, kumbuna niliwaambia jana kuwa kuna mambo napenda tuzungumze. Nadhani ni vyema kama mambo hayo tukienda kuzungumza nyumbani kwangu ndiomana nataka twende na Jeff"
Sabrina hakuwa na pingamizi na ukizingatia kuwa dereva mwenyewe ndio huyo huyo Sam basi wakaamua kumfata huyo Jeff ambapo ni Sam mwenyewe aliyeshuka kwenda kumuita.

Jeff alitoka ndani na kumuona Sam,
"Vipi wewe Jeff, hapa tumekufata wewe kwani jana nilikwambiaje? Twende basi."
Jeff alijigelesha kidogo ila badae akakubali kutokana na ushawishi wa Sam, kisha safari ya kuelekea kwa Sam ikaanza.

Walifika nyumbani kwa Sam kisha Sam akawaambia kuwa na chakula kitakuja hapo kwani alishatoa oda hotelini.
Kwavile mtoto alikuwa amelala ikambidi Sabrina akamlaze kisha yeye kurudi sebleni ambako Sam alianza kuongea,
"Ni kipindi kirefu sana kwa mimi kuishi na mke wangu ila mke jina"
Jeff na Sabrina wakatazamana tu, kisha Sam akamuangalia Jeff na kusema,
"Jeff mbona umekaa mbali sana, hebu sogea hapa karibu na Sabrina"
Kisha Jeff akasogea na Sam akaendelea kuongea,
"Najua nyie wawili mnapendana sana, ila nataka mnifanyie kitu kimoja tu ili nijiridhishe na upendo wenu"
Sabrina alikuwa wa kwanza kushangaa haya maneno na alikuwa wa kwanza kuuliza,
"Kivipi?"
Sam akacheka na kusema,
"Kumbe kweli mnapendana, sasa chagueni nyie cha kufanya muda huu ili nijiridhishe dhidi ya upendo wenu"
Jeff na Sabrina wakatazamana tena kwani hakuna aliyejua cha kufanya.
Sam akawashtua sasa na kusema,
"Nyie watu, sitaki masikhara mjue! Fanyeni chochote mnachojua kabla sijawachagulia mimi cha kufanya"
Kisha Sam akatoa bastora yake na kufanya uoga uwashike.

Jeff na Sabrina wakatazamana tena kwani hakuna
aliyejua cha kufanya.
Sam akawashtua sasa na kusema,
"Nyie watu, sitaki masikhara mjue! Fanyeni
chochote mnachojua kabla sijawachagulia mimi
cha kufanya"
Kisha Sam akatoa bastora yake na kufanya uoga
uwashike.
Jeff akatamani kufanya kile anachokiwaza yeye ila akiangalia macho ya Sabrina yalikuwa yakipinga na kumfanya Jeff asubirie Sabrina afanye anachokitaka.
Sam aliwaelekezea ile bastora sasa na muda huo Sabrina akainuka na kwenda kumkumbatia Sam kwa gafla, ni kitendo ambacho Sam hakukitarajia kwakweli na kujikuta akiishusha ile bastora.
Sabrina alimwambia Sam kwa sauti ya chini kabisa,
"Kwanini unatufanyia hivi Sam? Najua wewe si mtu mbaya na wala huwezi kufikia hatua ya kutudhuru sisi ila kwanini unapenda kututishia maisha kila siku kwa bastora yako?"
Sam aliirudisha ile bastora, kisha akamtazama Jeff aliyekuwa amekaa kwa uoga.
Sam alimuangalia Jeff huku akimuuliza swali Sabrina,
"Kwanini umekuja kunikumbatia?"
"Nakujali na kukupenda"
Sam akacheka na kusema,
"Unanijali na kunipenda kisha unazaa na mwanaume mwingine halafu unasingizia kuwa ulibakwa!"
Sabrina alikaa kimya ila Sam akaongea tena na kumuomba Sabrina akae kwanza ambapo Sabrina alikaa pale pale pembeni ya Sam.
Kisha Sabrina akatoa ile barua ambayo alipewa na Sakina mara ya mwisho ili aisome.
Sam alianza kuisoma barua hiyo na kumuomba Jeff awapishe kidogo ambapo Jeff alitii na kutoka nje.

Sam aliisoma ile barua taratibu na alipoimaliza alimuangalia Sabrina na kumuuliza,
"Uliielewa hii barua?"
Sabrina akatingisha kichwa kuwa ameielewa, kisha Sam akamuuliza tena,
"Ni nani mwingine aliyeisoma hii barua"
"Ni Jeff"
"Aliipataje?"
Sabrina akamueleza Sam jinsi ilivyokuwa hadi Jeff kuipata barua hiyo na kumrudishia,
"Inamaana Jeff nae anajua kila kitu?"
"Ndio anaelewa kama nilivyoelewa mimi"
"Ok, tuachane na hayo. Tafadhari Sabrina niambie kilichopelekea wewe kunisaliti mimi? Na kwanini ulienda kutembea na Jeff bila kujua kasoro yangu?"
"Sam, ni kweli nimefanya makosa hata moyo wangu huwa unajutia. Ila Sam naomba na mimi nikuulize, hivi ni mwanamke gani anayeweza kuishi na mumewe ndani bila kufanya chochote kinachopelekea wao kuona kuwa ni kweli wapo kwenye ndoa? Sam nimeishi na wewe bila kujua tendo la ndoa likoje, ila mimi sio mwanamke tangatanga kama unavyonifikiria"
"Nalijua hilo Sabrina na nilijua kama wewe sio tangatanga kitambo sana ndiomana nikakuchagua huku nikiamini kuwa wewe utaenda kulimaliza tatizo langu. Na kweli kwa kiasi fulani ulinisaidia sana bila ya wewe mwenyewe kujua, na kama asingetokea Neema na kunipa madawa basi ni hakika kuwa asingekuwepo mdada mwingine tena kufa kwaajili yangu. Ila swali langu bado lipo palepale kuwa kwanini ulinisaliti na kusingizia kuwa ulibakwa?"
Sabrina kwa siku ya leo aliamua kuweka aibu pembeni na kumueleza Sam kilichotokea ile siku ambayo alibakwa kweli na Jeff.

Kule nje Jeff naye aliamua kuondoka huku akiamini kuwa ni rahisi kwa Sam na Sabrina kuelewana wakiwa wawili kuliko akiwepo na yeye.
Akiwa njiani akakutana tena na Aisha yule binti aliyekuwa akiishi na marehemu Neema kisha akasalimiana nae.
"Mbona hukunitafuta jamani!"
"Kwa bahati mbaya namba ilifutika labda unipe tena namba yako"
"Hakuna tatizo ila nitachukua na yako pia"
Kisha Aisha akamtajia Jeff namba yake akaiandika kwenye simu na kuomba aijaribishe kuipiga ambapo aliipiga.
"Hivi unaishi kwako au kwenu?"
"Naishi kwetu"
"Aah yani mi nakuona kuwa nakufahamu kabisa, licha ya kuonana hospitali ila nahisi kuna mahali pengine nilipowahi kukuona. Nitakumbuka tu, basi nitakutafuta kesho ili unielekeze kwenu nije kukutembelea"
"Sawa hakuna tatizo"
Wakaagana na kuondoka, kwakweli Jeff alimshangaa sana huyu Aisha kujiweka karibu naye kiasi kile,
"Mmh huyu mdada atakuwa ananitaka tu hata sio bure, mara kunifananisha sijui nini na nini wakati mi nipo kwenye harakati zangu na mke wa mtu"
Kisha akajicheka mwenyewe na kuendelea na safari yake.

Sam alimsikiliza Sabrina kwa umakini sana na kugundua kosa lilikuwa kwa Jeff kumbaka Sabrina kwani asingembaka yote yasingeweza kutokea kama ambavyo yalivyotokea.
Kisha akamuomba Sabrina kuwa amuite Jeff pale nje.
Sabrina alitoka na kuangaza nje ila hakumuona Jeff na kuamua kumuuliza yule mlinzi wa Sam,
"Khee mbona ameondoka muda mrefu tu"
Ikabidi arudi ndani kumueleza Sam kuwa Jeff alishaondoka, naye Sam akatabasamu na kusema,
"Itakuwa Jeff kaogopa bastora yangu wakati kumdhuru siwezi"
Sabrina alimuangalia tu kisha akakaa ambapo Sam akamuuliza jambo tena Sabrina,
"Ni kitu gani unapenda kujua kuhusu mimi?"
"Vipo vingi tu, kwanza kabisa ningependa kujua kuhusu maisha yako. Pili ningependa kujua kuwa kwanini umeishi na mimi kama mke ila bila ya kufanya tendo la ndoa na tatu napenda kujua ukweli wa mambo kuhusu barua niliyopewa na marehemu Neema"
"Ni hayo tu?"
"Na nne ningependa kujua kuwa kwanini unapenda kuishi na mimi ingawa nimeshazaa watoto wawili nje."
"Hilo swali la mwisho ni jepesi sana Sabrina, nang'ang'ania kuishi na wewe ingawa umenisaliti ni kwavile nakupenda, na pia siwezi kumdhuru Jeff ingawa najua ndio mwizi wangu kwavile nakupenda wewe na kama nikimdhuru yeye basi nitakuumiza wewe ila uwezo wa kumdhuru ninao tena mkubwa tu ila sitaki kumdhuru kabisa na pia kuna kitu kwenye moyo wangu kinanizuia sana kufanya hivyo, usiulize kuwa ni kitu gani ila kifurahie kitu hiko kwani mimi kiuhalisia ni katili sana na huyo Jeff ningekuwa nimemmaliza siku nyingi sana kwani sijamjua jana wala juzi kuwa ndiye mwizi wangu ila nimetulia nikimuangalia tu"
Sabrina akapumua kidogo huku akisubiri majibu ya maswali yake mengine, ambapo ni Sam aliyeendelea kuongea,
"Kwahiyo unataka kujua maisha yangu tangu kuzaliwa kwangu?"
"Ndio nataka kujua"
Sam akamueleza Sabrina kwa kifupi kuhusu maisha yake, akamueleza kamavile alivyowahi kumueleza dada yake Joyce ambaye ni mke wa James.

Jeff alienda kwanza moja kwa moja kwakina Sabrina kumuangalia yule mtoto wao wa kwanza ambapo alimkuta akicheza na bibi yake yani mama Sabrina.
Jeff alifika pale na kusalimia, yule mtoto naye yani Cherry alikuwa akitembea kwa kipindi hicho na moja kwa moja akaenda kumkimbilia Jeff na kumkumbatia hata mama Sabrina akashangaa,
"Khee wewe Cherry umekuwaje leo!"
Jeff akambeba kisha akaenda kukaa nae pale karibu na mama Sabrina kisha akamsalimia tena ila kwa furaha zaidi kwani alifurahia vile alivyopokelewa na Cherry.
"Haya karibu, hivi unajua kama usiku wa jana nilikuona? Ni kitu gani kinaendelea baina yako wewe na Sabrina?"
Jeff akajifanya kushangaa kwa muda kidogo kisha akajibu,
"Hakuna chochote kinachoendelea"
"Jeff, mi ni mtu mzima tena najua mengi kushinda wewe kwahiyo ni vigumu sana kunificha mimi ila ninachokwambia ni kuwa unatakiwa uwe makini sana yule Sabrina ni mke wa mtu. Halafu hivi hujihurumii jamani? Na udogo huo kweli? Unajua Sabrina amekupita miaka mingapi wewe? Yule ni mkubwa sana kwako, kwanini unataka kufanya vitu ambavyo vitakufanya ujute hapo badae? Kwanini ujitese kwa mtu mzima wakati vijana wenzio wapo? Kingine heshima iliyopo kwetu ni kubwa sana, mama yako ni kama mwanangu na kwanini utake kuharibu ukoo Jeff? Kufanana na watoto isiwe sababu ya wewe kujifanya ndio baba yao, kila mtu anatambua kuwa Sabrina ni mke wa mtu kwanini wewe hutaki kuheshimu hilo? Sijapenda kwakweli ulichofanya jana"
"Ila bibi umenifikiria vibaya tu, mi namuheshimu sana Sabrina na wala hakuna kibaya nilichofanya jana zaidi ya kumkumbatia. Kwani hairuhusiwi ndugu kukumbatiana?"
"Usitake kupoteza maana Jeff, laiti kama ile ingekuwa ni kukumbatiana tu wala nisingekuwa na mashaka ila nilikushuhudia kwa macho yangu ukipeleka midomo yako kwa Sabrina, haipo sawa hiyo. Heshima inatakiwa ichukue nafasi yake, Sabrina anakuchekea sana na ndiomana yote haya yanatokea ila angekuwekea ukali isingefika hapa ilipofikia. Narudia tena sijapenda na sitapenda ijirudie"
Simu ya Jeff ikaanza kuita wakati mama Sabrina akiendelea kuongea na kumuomba kidogo aongee na simu, naye alimruhusu kisha Jeff akapokea simu ile na mpigaji alikuwa ni Aisha,
"Vipi Jeff ushafika nyumbani?"
"Ndio nipo nyumbani tayari, vipi wewe"
"Hata mi nipo nyumbani, msalimie mama"
"Haya nitamsalimia, badae"
Kisha Jeff akakata ile simu na kumfanya mama Sabrina aulize,
"Ni nani huyo maana nimesikia sauti ya kike kwa mbali"
"Ni mchumba angu huyu bibi"
"Unaona sasa ambavyo vijana hamridhiki, yani mchumba unaye ila macho juu juu kwa wake za watu. Mtakufa huku mnajitazama"
Jeff akaona kuwa maneno yamezidi kuwa mengi hivyo akaaga ili aondoke.
Wakati anaondoka, Cherry naye akaanza kumlilia kuwa aondoke nae na kumlazimu mama Sabrina amchukue Cherry na kumbeba mgongoni ili amtulize kisha Jeff akaondoka.

Sabrina alisikitishwa sana kuhusu Sam na wazazi wake, akajifikiria kama angekuwa ni yeye angejisikiaje.
"Kwahiyo yule uliyenipeleka kule Arusha na akaja kwenye harusi sio mama yako mzazi?"
"Ndio, yule ni mamdogo ila ananipenda kama mwanae wa kuzaa kabisa"
"Na kwanini mama yako hakuja kwenye harusi?"
"Najua mama anatamani sana ila kuna kitu kimemfunga, ila najua ipo siku tu atarudisha moyo wake na atakuja kuniona mwanae"
"Kwani ulifanya kipi kikubwa?"
"Nilichofanya ndio kitakuonyesha na kukujibu maswali yote ya mwanzo kule juu na pia utaelewa kwanini sijawahi kukupeleka kwa mama na kwanini hakuja kwenye harusi yangu. Mama mdogo kanilea, kwakifupi ananifahamu sana kwani kanilea toka nikiwa mdogo. Alifukuzwa na mumewe ila aliendelea kunilea mimi. Kwa upande wa mama sasa ni ananijua kushinda vile anavyonifahamu mamdogo kwavile niliweka chuki wazi kwa kizazi cha mumewe ila bado anatambua kuwa mimi ni mwanae na ninaamini kuwa bado ananipenda katika moyo wake ingawa kawa mgumu kunisamehe"
"Basi niambie ulichomfanya mama yako na hao wengine"
"Ni historia ndefu kidogo ila kwavile nimejitolea kukujibu maswali yako yote basi sina budi kukueleza hali halisi ilivyo na kwanini nipo hivi"
Sabrina alitulia kwani alitaka sana kujua kuwa ni kitu gani kilichotokea kwa Sam.

Jeff naye alirudi kwao na kumkuta mama yake akiwa ametulia sebleni na kumsalimia, ila mama yake akamuuliza swali lililomshangaza kidogo,
"Hivi ni lini nitamtambua mkwe wangu Jeff?"
"Kwanini mama?"
"Hivi unajua furaha ambayo niliipata siku ya kwanza kusikia kuwa Dorry ana mimba yako? Hivi unajua wazo lililokuwa kichwani mwangu wakati Dorry anajifungua? Mtoto hakufanana na wewe ila bado niliendelea kujipa matumaini kuwa ni mjukuu wangu hadi pale nilipoona kuwa mtoto anazidi kufanana na wachina. Tafadhari Jeff fanya kitu cha kunifanya mama yako nifurahi, nipo tayari kumlea mjukuu wangu kwa hali na mali"
Jeff akafikiria kidogo jinsi mtoto Cherry alivyomlaki na akafikiria kama ndio angekuwa anaishi nae pale nyumbani kwao ingawa anaona wazi kuwa ni jambo lisilowezekana.
Baada ya ukimya kidogo akaamua kumpa moyo mama yake,
"Usijali mama, mkweo nitakuletea hivi karibuni"
"Na iwe kweli mwanangu"
Kisha Jeff akainuka na kuelekea chumbani kwake, huko akafikiria namna ya kumpanga Aisha ili amlete kwao na aweze kumwambia mama yake kuwa ndiye mkwe ila pia akamfikiria Sabrina kuwa atamuona ni msaliti.
"Ni kweli Sabrina ni mke wa mtu ila nampenda sana na nilimuahidi kuwa sitamuacha kamwe kwani sijali chochote, sasa nikimtambulisha huyo hata kwa utani tu atanielewa kweli?"
Jeff alijikuta akifikiria sana swala hilo.

Sabrina bado alihitaji kusikia kutoka kwa Sam ambaye alimuomba wale kwanza kwani chakula kilishafika.
"Usijali, nimeamua kukueleza na nitakueleza kila kitu ila subiri tule kwanza"
Sabrina alikubaliana na ile hoja ya Sam huku akila na kuanza kuwaza zaidi atakachoelezwa na Sam.
Walipomaliz a kula sasa, Sam aliamua kuanza kumueleza Sabrina.

"Katika ujana wangu niliamua kulipa kisasi, na kisasi hicho nilianza kwa familia yangu mwenyewe yani kwa watoto wa baba yangu wa kambo.
Sikuwa na uwezo kipindi hicho yani sikuwa na pesa ndio kitu kilichofanya wengi wasinipende na wadada wengi wanikatae. Ni hapo nilipoamua kwenda kwa mganga wa kienyeji lengo kuu lilikuwa kumkomesha baba wa kambo kabla ya kushughulika na mengine. Yule mganga akanipa dawa ili nikaweke kwenye maji ya kuoga huyo baba.
Nikafunga safari siku hiyo na kwenda kwa mama, nikamkuta kaandaa maji ya baba ya kuoga ni hapo nikaona kuwa nimepata nafasi ya kuweka dawa yangu.
Mama alivyotoka tu bafuni, nikaenda kumimina ile dawa yote kisha nikatoka nje na kukaa mbali kidogo na bafu ili kusikilizia majibu ya ile dawa atakavyooga yule baba.
Muda kidogo nilimuona mama akitoka ndani kwa hasira huku akisema kuwa ni bora tu akaoge mwenyewe hapo nikaelewa wazi kuwa lazima baba amekataa.
Nikataka nikimbilie bafuni ili nikamwage yale maji ila kabla sijafika bafuni mama alikuwa kashaingia tayari.


Mama alivyotoka tu bafuni, nikaenda kumimina ile
dawa yote kisha nikatoka nje na kukaa mbali
kidogo na bafu ili kusikilizia majibu ya ile dawa
atakavyooga yule baba.
Muda kidogo nilimuona mama akitoka ndani kwa
hasira huku akisema kuwa ni bora tu akaoge
mwenyewe hapo nikaelewa wazi kuwa lazima baba
amekataa.
Nikataka nikimbilie bafuni ili nikamwage yale maji
ila kabla sijafika bafuni mama alikuwa kashaingia
tayari.
Ikabidi nitumie akili yangu ya ziada.
Ni hapo nilipoamua kukimbilia bafuni kwa kuhofia mama asije kuoga yale maji.
Kwakweli nilimkuta mama kashatoa nguo zote ila sikujali zaidi ya kumwaga ile ndoo na kuondoka bila kujua ni jinsi gani mama amechukizwa na kile kitendo changu.
Niliondoka pale nyumbani kabisa na kurudi kwa mamdogo huku nikitamani kumwambia kilichotokea ila nikaona aibu.
Kesho yake nikajifungasha tena ili niende kumuomba mama msamaha ila nilipofika yani hakuna aliyenisalimia hata mama aliyekuwa akinipokea peke yake aliniona ni mtoto mbaya huku kila mmoja akidai kuwa nina laana na ndio hapo nilipoamua kurudi tena kwa mamdogo na kuvunja ukimya, nilimueleza kilichotokea kwakweli mamdogo alisikitika sana na kuniambia kuwa dada yake ana haki ya kuchukia kwa kile kitendo ila laiti kama angejua nilifanya vile kumuokoa basi angechukia ila sio sana ila akaniambia kuwa na kama ningemueleza ukweli mama lengo la hiyo dawa ndio angenichukia zaidi.
Nikamuuliza mamdogo kwahiyo nifanye nini sasa akaniambia nitulie na mama atanisamehe mwenyewe, nikafikiria sana bila ya kupata majibu na siku zikaenda bila ya mama kunisamehe.

Kitu kingine kilichokuwa kikiniumiza katika maisha yangu ni kuwa hakuna mwanamke aliyeweza kunikubali moja kwa moja kutokana na hali ya maisha yangu nilikuwa nikimtegemea sana mamdogo ambaye naye hakuwa na shughuli maalumu ya kufanya. Roho ilikuwa ikiniuma sana haswa nilipokuwa nikienda nyumbani kwa mama mzazi na kufukuzwa na wanae na pale hata wanawake wa mitbni waliponikataa hapo nilijiona kuwa nina laana kweli aliyosema mama, nikalaumu kitendo changu cha kwenda kwa mganga kwani ni bora mwanzo nilichukiwa na bac wa kambo tu ila kitendo cha kuchukiwa na mama pia kiliniuma ukizingatia yule baba alikuwa na watoto wawili wa nje wa kike yani hawakuwa wa mama yangu ila mama aliwapenda kama watoto wake sasa kwanini mimi nichukiwe kiasi kile? Niliumia sana, kwenye ukoo napo karibia kila mtu alinichukia yani hawakuwa karibu na mimi kabisa zaidi ya huyo mama mdogo tu.
Siku moja nilikaa na mamdogo na kuongea nae kuwa kwanini inakuwa hivi, majibu yake yalikuwa haya,
"Mwanangu, katika dunia usitegemee kwamba utapendwa na kila mtu haswa pale ambapo utaonekana huna kipato. Jitahidi mwanangu, tafuta kazi na ukipata ifanye hiyo kazi kwa bidii na usisikilize watu wanasemaje bali usikilize moyo wako. Pesa ndio kitu pekee kitakachokupa kiburi, pesa itafanya hawa wanaokuona hufai sasa waje kukuomba msaada. Fanya kazi mwanangu, niangalie mimi na mambo yote yaliyosemwa juu yangu ila bado nipo tena ngangari kabisa, sitaki presha za watu sababu nasikiliza moyo wangu"
Swala la mamdogo kuwa nifanye kazi kwa bidii likaniingia sana kichwani mwangu, na ndicho nilichokuwa nikifikiria kwani nilihitaji kupata heshima katika jamii, nilihitaji kuheshimika ni hapo nilipopata wazo la kuzamia Mererani hata mamdogo hakujua kama naenda Mererani sababu nilimwambia kuwa naenda kutafuta kazi tu.

Nilikutana na changamoto nyingi sana lakini sitaweza kukuelezea ila cha msingi elewa kwamba utajiri wangu na pesa yangu niliibahatisha huko.
Nilipata hela kweli na kisha kuzamia mgodi mwingine huko Mwadui nako Mungu alinibariki kwakweli.
Ni hapo nilipofikiria swala zima la kuwekeza katika mali mbali mbali na ndipo nilipojenga ile hoteli Arusha ambayo ni sehemu mliyowahi kufika na kunikuta.

Pesa na mali zilinipa kiburi ila zilifanya wengi watambue uwepo wa Sam. Ni hapo nilipojenga nyumba Arusha na kumuomba mama mdogo akaishi huko, sikuweza kumwambia mama kwani bado hakutaka kunisamehe na kunisema kuwa nimelaanika.
Yote hayo hayakuwa tatizo kwangu, ila kuna tatizo moja ambalo huwa najuta na kujuta sana kuwa kwanini nililifanya. Nilitaka kukomesha baadhi ya watu ila mwisho wa siku nikajikomesha mwenyewe hadi leo najutia hili kosa.
(Hapo Sam alinyamaza kwa muda na kuinama kama mtu anayefikiria sana, kisha akainuka na kuendelea kuongea)
Kitendo cha wadada kunifata sababu ya pesa zangu kiliniumiza na kusema kuwa lazima nitawakomesha hao wanawake kwani kuna hadi wale niliowahi kuwapenda zamani sababu ya umaskini wangu wakanikataa ila nilipokuwa na pesa ndio hao hao wakajileta kwangu tena, nikajiapia kuwa lazima niwakomeshe hao wanawake wenye tamaa ni hapo nilipopata wazo la kwenye kwa mganga wa kienyeji.
Nilipata taarifa kuwa kuna mganga mashuhuri yupo Sumbawanga na wala sikujali umbali wa Arusha na Sumbawanga kwahiyo nikafunga safari kutoka Arusha mpaka Sumbawanga kwaajili ya kukutana na huyo mtaalamu na kwavile kipindi hicho nilikuwa na pesa kwahiyo swala hilo halikuwa gumu hata kidogo.

Namkumbuka yule mtaalamu alikuwa ni mzee mmoja hivi ila ni marehemu tayari, alinipokea vizuri sana na kusema kuwa shida yangu anaijua tokea mbali na alichoongezea nakumbuka alisema,
"Nina dawa ambayo niliitengeneza siku nyingi sana ila haikupata wa kuijaribisha ila kwavile wewe umekuja naomba nikueleze na najua kuwa lazima utaipenda dawa hiyo"
Nikawa makini sana kumsikiliza mzee huyo aliyeonekana kuwa na nia ya hali ya juu kunisaidia kwa kile ninachokitaka.
Nakumbuka alisema kuwa ananipa dawa ya jini ila jini hilo halitanidhuru kamwe ila nitawadhuru hao wanawake ninaowachukia halafu pia jini hilo litasaidia biashara zangu na zitaimarika zaidi.
Niliifurahia sana hiyo dawa kwani niliona nimepata dawa moja kwa kazi mbili, kwanza kuwakomesha wanawake na pili kuimarisha biashara zangu.
Nikakubali pale na ndipo aliponipa masharti ya dawa ile kwanza kabla hata ya kunipaka wala kuniambia kuwa naitumiaje. Aliniambia hivi,
"Kwanza kabisa hii dawa hakuna atakayejua kama unayo kwani itakuwa ndani yako. Mwanamke anapotaka kukutana na wewe kimwili, akikufanyia manjonjo hata kidogo tu hii dawa itakulazimu ulale nae kwani utapatwa na nguvu ya ajabu sana. Ukilala nae yeye atapatwa na maumivu makali sana, mpe onyo moja kuwa asimwambie mtu kwani akikiuka atakufa tu ila asiposema ataendelea kuteseka. Na katika biashara yako mambo yatazidi kuimarika kila unapolala na mwanamke."
Niliiona kuwa hiyo ni dawa bora sana ya kuwakomesha wanawake wote wenye tamaa ya pesa na wala sikufikiria mara mbili zaidi ya kumwambia kuwa anitengenezee dawa hiyo.
Naye hakusita na kuanza kunitengenezea dawa hiyo ambapo alinichanja sehemu za siri na kunipaka kisha akanichanja kwenye paja na kuchukua damu yangu kidogo na kuiweka kwenye chupa ambapo akaifunga muda huo huo halafu pale aliponichanja akanipaka dawa.
Muda kidogo akaifungua ile chupa na kusema ameshanikabidhi hilo jini ila halitakuwa karibu na mimi kama majini mengine yafanyavyo ila lenyewe litakuwa karibu pindi tu nitakapokuwa nataka kufanya mapenzi.
Niliona ni jambo jema sana ingawa kuna kitu aliniahidi na huwa nakikumbuka hadi leo, aliniambia hivi
"Pindi ukichoshwa na hii dawa itakupasa urudi tena kwangu ili niliondoe hilo jini. Kumbuka kuwa mimi ndiye niliyelitengeneza na hakuna mwingine yoyote wa kuweza kuliondoa zaidi ya mimi. Na tena nitaliondoa kwa kulirudisha tena kwenye ile chupa."
Niliona ni zoezi dogo sana na sikuwa na shaka kwani nilijua kuwa pindi nikikamilisha adha yangu na kuwakomesha wanawake wote wenye tamaa basi nitarudi tena kujirudisha kwenye hali yangu ya kawaida.
Tulimaliza shughuli pale na kulipa pesa kwaajili ya mizimu kisha nikaondoka zangu.

Nakumbuka nilikaa wiki nzima bila ya kukutana na mwanamke yoyote kimwili kisha nikaanza shughuli kwa kukutana na yule mwanamke aliyewahi kunikataa sababu ya umaskini wangu. Ila alinikubali kwa haraka sana sababu ya pesa zangu nami nikaamua kumtumia vilivyo.
Na muda nakutana nae kimwili alitaka kukimbia kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye mwili wangu na hapo ndipo nilipojifunza kuzima taa kabla ya kukutana na mwanamke kimwili, ila nilikuwa na nguvu ya ajabu sana na kuamua kutumia nguvu hiyo ila mwisho wa siku ilikuwa kama kumbaka na alizimia pale pale.
Na nilipomaliza nilijilaumu sana kwa kile kitendo ila ndio hivyo ilishatokea tayari.
Alipozinduka alilia sana na nikampa onyo la kutokusema ila aliporudi kwao tu baada ya muda moyo uliniuma sana na nikaja kupata taarifa kuwa amekufa.
Nilitamani niende kwa mganga siku hiyo hiyo kuikataa ile dawa ila upande mwingine wa moyo ukawa mgumu sana kufanya hivyo.
Nilifikiria sana ila nikapatwa na wazo la kwenda kumuumiza mtoto mmoja wa baba yangu wa kambo halafu ndio niende kwa mganga kuitoa hiyo dawa.

Nikafunga safari hadi nyumbani kwa mama, kwavile nilikuwa na pesa wakanipokea vizuri sana hata mama alikuwa amenisamehe tayari kwa kosa lile la mwanzo.
Nilitumia pesa yangu kumlaghai yule mtoto wa baba naye akaingia laini hadi kufikia hatua ya kulala nae ambapo ndio nikamuachia janga kama la mwenzie na kumpa onyo kuwa asiseme.
Na hapo roho yangu ikawa imetulia ila nilijua wazi ikibumbuluka tu basi kazi ninayo.
Nikapanda gari yangu na kufanya safari ya kurudi Arusha.
Nikiwa njiani moyo uliniuma sana na kunifanya nirudi kwa mamdogo kwani nilijua wazi kuwa kule ndio nitapata habari zote.
Mamdogo aliponiona tu akaniambia kuwa ameambiwa mambo ya ajabu sana na mama kuhusu mimi eti nimekuwa muuaji, nilijifanya kukataa pale kuwa sio mimi ila mamdogo akaniambia kuwa mama kasema hatotaka kuniona tena katika maisha yake.
Nilijua wazi kuwa mama kaambiwa ukweli na kufanya moyo uniume zaidi.
Kesho yake nikasafiri na kwenda Dar es salaam ili nikafanye maisha huko na nilipofika kwakweli mji ulinipokea kwa shangwe na kufanya nijenge ofisi ile kubwa na kuanza biashara zangu na wala sikujishughulisha na maswala ya wanawake kwa kipindi hicho kwani nilijali kupata pesa kwanza Nilikaa mwezi mzima bila ya kuwa na mwanamke wa aina yoyote yule, ila walianza wenyewe kujipendekeza kwangu na ikawa kila nikilala na mwanamke namuachia janga kisha mimi naendelea zaidi, na yakawa kweli yale maneno ya yule mganga kuwa ninapomtesa mwanamke kwa janga hilo basi mimi ndio napata pesa zaidi na ndiomana haikuwa tatizo kwangu kuwamaliza.
Kwakweli nilichafua mji huu kiasi kwamba wengi waliniogopa na ndio hapo nilipoacha biashara zangu kwenye usimamizi kisha mimi kurudi Arusha ila napo sikukaa sana nikafanya safari ya kwenda Sumbawana ili nikaitoe ile dawa na niwe huru na niweze kuoa sasa.

Nilifika kule Sumbawana na kukutana na janga, yule mganga alikuwa amekufa.
Hapo ndio sikuelewa cha kufanya kabisa kwani matumaini yangu yakapeperuka yote muda huo huo kwavile nikikumbuka maneno yake kuwa ni yeye tu wa kunisaidia.
Nikakata tamaa na kurudi Arusha, nilikaa wiki na kusafiri kuelekea Dubai huko nikakaa miezi mitatu bila ya kukutana na mwanamke yoyote huku nikiendelea kufanya mambo yangu ya maendeleo na kuendeleza biashara zangu chini ya usimamizi niliouweka kwa watu ninaowaamini.
Nilitafakari sana mambo yangu na kuona kuwa licha ya wanawake kunitenda vibaya ila na mimi nimewatenda vibaya sana. Nikaona ni vyema nikikutana na mwanamke nimsaidie tu hata kama moyo hautaki, kisha nikarudi Tanzania na kwenda kuishi moja kwa moja Arusha, na baada ya siku mbili tangu nirudi alikuja mwanamke baada ya kumsaidia aling'ang'ania kulala na mimi nami nikajikuta nikifanya hivyo bila kutaka na kummaliza ila ndio nilivyozidi kuwa na mali kushinda mwanzo yani huyu mwanamke alinipa bahati sana sijui kwavile nilikaa muda mrefu kidogo bila kukutana na mwanamke? Ila kitendo cha kummaliza huyo mwanamke pia kiliniumiza, na baada ya wiki ndipo ulipokuja wewe na familia yako na kunikuta hapo nje ya hoteli kwakweli maelezo yako na maelezo ya wazazi wako yalifanya niingiwe na moyo wa imani sana ndiomana nikajitolea kukusafirisha ili ukasome"
Sam alipofika hapo alipumua kidogo kwani alikuwa na mengi sana ya kumueleza Sabrina ila Sabrina nae alipoona Sam amenyamaza kumueleza ikabidi amuulize sasa maswali ambayo bado yanamtatizo kutoka kwa huyu Sam na kutokana na story aliyomuelezea,
"Eeh Sam niambie basi kuwa kwanini uliamua kuwa kimapenzi na mimi hadi kunioa ingawa ulijijua kuwa unamatatizo? Na kama ulikuwa na nia ya kunimaliza mimi kama hao wengine kwanini hukufanya hivyo kwangu na kuwamalizia wakina Neema? Na kwanini....."
Kabla Sabrina hajauliza walisikia kamavile nyumba ikitetemeka na kumfanya Sam naye amuulize Sabrina kwa hasira,
"Kwanini umemtaja Neema......"
Nyumba ikazidi kuwa na tetemeko na kuwafanya wapate kizungu zungu ndani.

"Eeh Sam niambie basi kuwa kwanini uliamua
kuwa kimapenzi na mimi hadi kunioa ingawa
ulijijua kuwa unamatatizo? Na kama ulikuwa na nia
ya kunimaliza mimi kama hao wengine kwanini
hukufanya hivyo kwangu na kuwamalizia wakina
Neema? Na kwanini....."
Kabla Sabrina hajauliza walisikia kamavile nyumba
ikitetemeka na kumfanya Sam naye amuulize
Sabrina kwa hasira,
"Kwanini umemtaja Neema......"
Nyumba ikazidi kuwa na tetemeko na kuwafanya
wapate kizungu zungu ndani.
Tetemeko lile lilifanyika kwa dakikaz kama tano ila liliwasumbua sana kwani walishindwa hata kusimama na kubaki pale pale wakitingishika na kupepesuka kila walipotaka kusimama.
Hali ilipotulia wakajikuta wakitazamana, Sam akahamaki kwa nguvu,
"Ndiomana sipendagi mambo ya waganga kwa sababu waongo, ona sasa kilichotokea"
Sabrina nae akauliza,
"Sasa tufanyaje? Tutoke?"
Kabla Sam hajajibu kuna mtu aliwagongea mlango ikabidi Sam ainuke kumfungulia, alikuwa ni mlinzi wake.
"Vipi Omary, kuna tatizo?"
"Sio tatizo sana bosi ila kuna yule mzee wa siku ile amekuja tena, yupo nje anakusubiri"
Sam akafikiri kwa haraka na kujua kuwa ni lazima atakuwa ni yule mganga wa kienyeji na kwa haraka zaidi akawaza kuwa huenda anahusika na kilichotokea muda mfupi uliopita.
Sam akamuuliza tena mlinzi wake,
"Yupi huyo? Yukoje?"
Mlinzi akamueleza Sam jinsi alivyo yule mzee na kumfanya Sam kuelewa vizuri kuwa ndio huyo huyo mzee anayemuongelea yeye.
Akageuka na kumuangalia Sabrina kisha akamwambia,
"Unaona sasa, huyu mganga nae kashafanya kitega uchumi chake hapa. Anafanya mambo ili badae aseme kuwa anataka kutusaidia. Eti yupo nje"
Sabrina nae akajibu,
"Si huwa anauwezo wa kuingia ndani kimiujiza, sasa leo kwanini akuite nje? Mwambie aingie tu."
"Ila kweli Sabrina"
Kisha Sam akamuangalia yule mlinzi wake na kumwambia kuwa amwambie yule mzee aingie tu.
Yule mlinzi nae akawauliza,
"Hivi waganga mnawajua vizuri au? Wanaweza fanya chochote usipofata wanachotaka."
Sam naye akamjibu,
"Omary hata usijali, mi waganga nawajua sana kupita unavyofikiria na ndiomana nimekwambia mwambie aje mwenyewe tu"
Ikabidi yule mlinzi atoke na kwenda kumueleza yule mganga pale nje.

Jeff pale kwao akafikiria sana, akaifikiria ile barua iliyoachwa na Neema na kujua wazi kuwa Sam yupo kumpa maelezo Sabrina kuhusu ile barua,
"Na vipi kama Sam akiamua kufanya na Sabrina kile alichofanya na Neema hadi kudhurika mmh!"
Aliwaza kuwa Sam anaweza kumfanyia Sabrina kama adhabu ya kumsaliti ndio pale alipopata wazo la kurudi tena kwa Sam na kusema kuwa anatakiwa kujikaza kama mwanaume na aweze kukabiliana na chochote kile.
Kisha akaondoka pale kwao akiwa amejipanga vilivyo sasa.
Ingawa alijua hadi kufika tena kwa Sam muda nao utakuwa umeenda sana.

Yule mlinzi wa Sam alienda kumwambia yule mzee kuwa aingie ndani,
"Wameniruhusu wenyewe?"
"Ndio bosi mwenyewe kasema uingie"
Yule mganga akaingia hadi alipofika mlangoni na kuona kuwa mlango umefungwa na kwa maadili yake ya muda huo hakutakiwa kugonga ikabidi atoke nje na kumwambia yule mlinzi wa Sam,
"Huyu bosi wako kajifanya mjanja eeh! Mwache hanijui vizuri na nitamuonyesha kuwa mimi ni nani"
Kisha yule mzee akaondoka hata yule mlinzi wa Sam hakuona kama ni vyema kwa yeye kubaki na jambo lile moyoni kwahiyo akarudi tena na kuwagongea wakina Sam kisha akawataarifu alichosema yule mganga, Sam naye akajibu
"Kwakweli wasitake kunichanganya jamani, tena mi nilimuheshimu tu siku ile mtu gani yeye kazi kuharibu tu watu hata wasiotaka huduma zake. Mi na Sabrina tumeteseka kumbe chanzo ni yeye, nilimuheshimu sana siku ile na waniache tu nipumzike kwasasa"
Sabrina nae akachangia,
"Amelbniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu"
"Na kweli, sasa hawa waganga wanataka kunizidishia laana tu. Kama siku zingine aliweza kuingia kwangu bila tatizo lolote kwanini leo ashindwe? Simjui kweli yakinizidia nitamtafuta"
Kisha akamwambia mlinzi wake akaendelee na kazi yake.
Walitulia na Sabrina pale huku wakimjadili yule mganga na kuepuka kutaja jina la Neema,
"Sasa mahali ikitulazimu kutaja jina lake tusemeje?"
"Tuseme tu yule mtu maana hilo jina litatuletea balaa bure na hivi umekataa kumfata huyo mzee ndio tutazidisha balaa zaidi bure."
Sabrina aliongea na kufanya wakubaliane kuwa watasema tu yule mtu bila ya kutaja jina.
"Basi jibu maswali yangu Sam"
"Nitakujibu tu Sabrina ila acha kwanza moyo wangu utulie"
Wakakaa pale na muda kidogo Sabrina akamsikia mtoto akilia na kwenda kumchukua ili aweze kumnyonyesha.
Alipotaka kumnyonyesha akashangaa kuona kuwa maziwa hayatoki,
"Sam, eti maziwa hayatoki"
Mtoto nae alizidi kulia kwavile hakupata haki yake,
"Kwanini hayatoki sasa?"
"Hata sielewi, hebu ona!"
Sabrina akajaribu kutoa ziwa na kukamua ambapo hayakutoka maziwa kabisa wala chochote,
"Khee mbona makubwa haya leo, yani maziwa yangu hayatoki kabisa wakati yanatokaga mengi sana"
"Sasa ndio nini hiki jamani? Kitu gani hiki"
"Labda yule mganga wako kaamua kunifanyia vipi"
Wakatazamana bila kujua cha kufanya kwa haraka na mtoto naye aliendelea kulia tu.
Ikabidi Sam atoke akaangalie japo maziwa ya ziada waweze kumpatia mtoto.

Sabrina alibaki mwenyewe akimbembeleza mtoto kwa kila staili.
Muda kidogo Sam akawa amerudi na maziwa ya unga kwa watoto, Sabrina akamkorogea mtoto na kuanza kumnywesha ambapo alikuwa kidogo na kuyakataa kisha kilio kikaongezeka zaidi.
"Huyu mtoto naye mbona shida eti kayakataa maziwa tena"
"Sasa tufanyaje?"
"Twende hospitali tukamueleze daktari labda anaweza kutusaidia"
"Sabrina, huu ni ushirikina unafanyika hapa hata hospitali hatutasaidika"
"Sasa unafikiri Sam tutafanyaje na mtoto analia kiasi hiki?"
Hawakujua cha kufanya ila tu walikuwa wakimbembeleza mtoto anywe yale maziwa.

Jeff naye alipofika akashangazwa na sauti ya kilio kwa mtoto na moja kwa moja alifika na kuingia ndani kwani muda huu Sam hakufunga kama mwanzo.
Naye alianza kwa kuwauliza kuwa ni kitu gani kimetokea mpaka imekuwa vile, ikabidi Sam amueleze kwa kifupi tu kuhusu ujio wa yule mganga na jinsi Sabrina alivyojikuta kuwa maziwa hayatoki kwa muda huo na mtoto anavyokataa maziwa waliyomletea.
"Mmh huu ni ushirikina tu"
"Ndio hata mi nimemwambia Sabrina hivyo ingawa anang'ang'ania kuwa twende hospitali."
Jeff akamkumbuka hapo hapo yule daktari aliyesaidia hadi Sabrina kujifungua salama kabisa na kuwaeleza kuwa kwanini wasiende huko kwani aliona yule daktari kuwa na uwezo mkubwa zaidi ingawa hakumueleza wazi Sam kuwa ni kitu gani kilitokea siku ya kujifungua kwa Sabrina.
Basi wakapanda kwenye gari kisha safari ya kuelekea huko hospitali ikafanyika.
Mtoto alilia na mwisho wa siku akalala tena na kutulia.
"Mmh bora amelala jamani maana si kwa kilio hiki wapendwa."
"Mambo yatakuwa sawa tu, najua hukumbuki Sabrina ila yule daktari ana utambuzi wa hali ya juu jamani yani hata kama mtu wamekuchezea yeye anajua kwahiyo atagundua haraka kuhusu huyu mtoto na atatuambia kitu sahihi cha kufanya"
Waliongea huku safari ya kwenda hospitali ikiendelea hadi pale walipofika.

Waliingia hospitali na kwenda moja kwa moja kwa daktari aliyemtibia Sabrina kwa maelekezo ya Jeff kwani ndiye pekee aliyejua kisa na mkasa wa Sabrina wakati wa kujifungua.
Walimkuta yule daktari akiwa ofisini kwake huku akiendelea na mambo yake ya kuandika andika.
Yule daktari naye alipowaona tu akamkumbuka Jeff na kumuuliza,
"Vipi tena kijana, mkeo kapatwa na tatizo gani?"
Sam akamtazama Jeff kwa kujijulisha vile kuwa yeye ni mume wa Sabrina wakati mume halali ni yeye.
Jeff alitambua hilo ila kwavile alihitaji kuangalia hali ya maisha ikabidi amjibu dokta vile inavyotakiwa,
"Kuna tatizo daktari, mke wangu hatokwi na maziwa"
"Na mbona mmekuja watatu ofisini?"
"Huyu ni bosi wetu na anajua kila kitu kuhusu sisi ndiomana tumekuja nae"
Huku akimuonyeshea Sam na kumfanya Sam azidi kujisikia vibaya ingawa yule daktari aliwaambia wakae ili ampime Sabrina ila kabla hajampima akasita kidogo na kuwaomba wampatie mtoto kwanza.
Sabrina akamkabidhi yule daktari mtoto ambapo daktari alimshika mtoto huku akitikisa kichwa na kuuliza,
"Hivi kwanini mtu kutaka kumtesa malaika kama huyu? Huyu ni mtoto mdogo sana, watu hawajui tu kama watoto wanalindwa na Mungu. Mlitaka kumpa maziwa huyu mtoto ila yakawekwa uchafu gafla na akayakataa"
Sam akamuangalia Sabrina kwani kweli walimpa maziwa mtoto ambapo aliyakataa maziwa hayo.
Huyu daktari naye akawatazama kanakwamba akihitaji uthibitisho kwa kile alichokisema, naye Sabrina akaitikia kuwa ni kweli ilikuwa hivyo.
Daktari akamtazama Sabrina, kisha akamtazama Jeff na kusema,
"Hili si tatizo kubwa kama ambavyo mtengenezaji analifikiria kuwa ni kuwa ila litakuwa ni dogo endapo utakuwa na imani. Najua wewe kijana unanishangaa sana, ukweli ni kwamba mimi nisingekuwa nimesoma basi ningekuwa mganga wa kienyeji au kama ningeshika sana dini basi ningekuwa nabii. Ninachoweza kufanya huwa nasema naweza na ninachoshindwa huwa natoa angalizo kabisa kuwa nimeshindwa. Kwa kusema haya ni hivi, siwezi kumtibu mtoto huyu wala mama huyu kwa dawa yoyote hapa"
Ile kauli ikawashtua kidogo na kuwafanya watazamane huku wakifikiria cha kufanya ili Sabrina na mtoto wawe huru.
"Sasa tutafanyaje daktari?"
Sam aliuliza kwa mshangao kidogo.
"Msijali, cha kufanya ni imani tu"
Kisha akamuangalia Jeff na kumuuliza,
"Je, una imani?"
"Ndio imani ninayo"
"Basi inuka, shika matiti ya mkeo na uyaamuru yatoe maziwa huku ukiamini kuwa Mungu atatenda hilo"
Jeff akainuka na kufanya kama daktari alivyomwelekeza kisha akakaa.
Daktari akawapa mtoto na kuwaambia,
"Haya nendeni, tatizo lake limeisha"
Walimchukua mtoto na kuondoka kama kwa mashaka hivi yani kama vile hawaelewi kinachoendelea hadi walipopanda kwenye gari na Sam akawa wa kwanza kuuliza,
"Hivi huyu daktari mmemuelewa jamani?"
"Hata sijamuelewa"
"Haya tuachane na hayo, eeh Jeff na Sabrina inamaana ndio mmeshajihalalisha na huku kuwa nyie ni mke na mume?"
Jeff na Sabrina wakatazamana, na wala Sabrina hakuwa na jibu ukizingatia hakujua chochote kilichotokea wakati wa ugonjwa wake ndipo Jeff alipoamua kueleza ukweli wa kilichotokea huku akiwaomba msamaha.
"Huna haja ya kuomba msamaha Jeff kwani mambo yapo wazi kabisa kuwa huyo mtoto kwa Sabrina ni wako ingawa sitaki hata kufikiria kuwa ilikuwaje kuwaje hadi ikawa hivyo aaarghh"
Mtoto naye akaamka na kuanza kulia tena, Sabrina akampa ziwa na muda huu maziwa yalikuwa yakitoka vizuri sana na kumfanya Sabrina afurahie,
"Eti maziwa yanatoka"
Sam alijibu kwa haraka sana,
"Lazima yatoke si yameshikwa na mwizi bhana"
Sabrina akawa kimya na Jeff naye akawa kimya kabisa huku wakitazamana kwa aibu.

Sam alipeleka gari hadi nyumbani kwake na muda nao ukawa umeenda tayari.
Walifika na kuingia tena ndani huku Sam akionekana kuwa na mawazo sana.
Walikaa sebleni ila Sam aliinama kuonyesha kuwa bado kuna kitu anafikiria sana.
Alijiuliza kuwa kwanini hawezi kumdhuru Jeff, hata kama ni sababu ya kumpenda Sabrina ila bado haikuwa sababu tosha ya kumfanya yeye ashindwe kumdhuru Jeff.
Akajikuta akiinua kichwa na kuongea kwa nguvu,
"Hivi wewe mtoto una nini wewe?"
Jeff naye alimtazama tu Sam bila ya kusema chochote na kumfanya Sam amuulize tena,
"Hivi wewe Jeff una nini lakini? Unajua sikuelewi!"
Kisha akamuangalia na Sabrina halafu akauliza,
"Ni kweli alikubaka au kwa mapenzi yako tu ukaamua kulala naye? Hivi Sabrina unajijua kwamba wewe ndio tiba yangu? Hivi unajua kwamba wewe ndio ulitakiwa kunitoa kwenye hili janga? Badala yake ukaharibu masharti yote kwa kwenda kulala na huyu mtoto. Hivi mi niwafanyeje lakini"
Sabrina alimuangalia Sam na kusema,
"Mbona sikuelewi Sam, umepatwa na nini tena gafla?"
"Roho inaniuma mjue, tena nikifikiria kuwa kijana mdogo kama Jeff wa kunipiku mimi kweli? Na pesa zote nilizonazo kweli?"
Sabrina akaona itakuwa shida na kuamua kuinuka ili akamlaze mtoto kwanza ila alipofika chumbani akashangaa alichokiona na kuamua kuwaita Sam na Jeff nao walishangaa walichokiona kwani walimuona mtoto mwingine mdogo kama mtoto wao akiwa amelala kitandani.


Sabrina akaona itakuwa shida na kuamua kuinuka
ili akamlaze mtoto kwanza ila alipofika chumbani
akashangaa alichokiona na kuamua kuwaita Sam
na Jeff nao walishangaa walichokiona kwani
walimuona mtoto mwingine mdogo kama mtoto
wao akiwa amelala kitandani.
Walijikuta wakiguna kwa pamoja, Jeff akawa wa kwanza kuongea,
"Mmh haya majanga jamani"
"Sasa tufanyaje?"
"Huyu mtu hawezi kutuacha jamani mpaka apate anachotaka"
Sabrina alijikuta akiyasema hayo kwani hakuelewa kitu, Jeff naye akaongezea kuwa bora waondoke tu eneo lile.
Pia akaongezea kuwa,
"Tena kabla ya kuondoka tujue kwanza mtoto wetu ni yupi"
"Hapana, mi najua wangu ni huyu wa mikononi wa pale kitandani simtambui jamani"
"Ila mkumbuke yule mganga anatuchezea akili humu ndani, tuondoke tukiwa na uhakika kabisa wa mtoto"
"Uhakika ninao, mwanangu ni huyu wa mikononi"
"Basi kama una uhakika tutokeni, tuondokeni hapa kwani naona si sehemu sahihi tena."
Wakakubaliana hivyo na kutoka nje bila ya kujua kuwa waelekee wapi kwanza.
Ila walipofika mlangoni tu, Sabrina akajihisi maumivu ya moyo dhidi ya mtoto aliyemuacha ndani na tena akajihisi mikoni ikichoka sana kwa yule mtoto aliyembeba kwani alikuwa na uzito usio wa kawaida.
Akawasimamisha Sam na Jeff kisha akampa Sam yule mtoto ambebe,
"Hebu jaribu na wewe kumbeba mtoto huyu"
Sam akamchukua na kushangaa,
"Mbona kawa mzito sana?"
Wakajikuta wakiguna na kubaki na mshangao.
Jeff akaona ni bora wakamchukue yule mtoto wa ndani kwani huyu wa mikononi aliwapa mashaka tayari.
Akaingia na kutoka na yule mtoto.
Sam alipoona Jeff kashatoka na yule mtoto yeye akampa yule mtoto Sabrina na kumwambia kuwa akamlaze ndani, Sabrina nae hakusita na kwenda kumlaza.
Wakati Sabrina anaenda kumlaza yule mtoto, Sam akamshika mkono Jeff na kuelekea nae kwenye gari, wakapanda na kuanza kulitoa gari nje kwanza ili wakamsubirie Sabrina nje.

Sam aliona Sabrina kakawia kidogo na kuamua kumfata ndani.
Alipoingia ndani alimuona yule mtoto akiwa amemng'ang'ania Sabrina yani alikuwa hataki kuachilia nguo ya Sabrina ili aondoke.
Sam akaona ule mtihani sasa ila akapata wazo la haraka haraka na kumpa wazo hilo Sabrina kuwa avue hata blauzi yake na kumuachia yule mtoto kisha yeye aweze kukimbia ila wakati anamalizia kutoa ile blauzi alishtukia akizabwa kibao cha hali ya juu na yule mtoto hadi kupatwa na kizunguzungu na kufikia hatua ya kutaka kudondoka ndio hapo ambapo Sam akawahi na kumdaka kisha kutoka naye nje huku akisikilizia maumivu ya kibao kile.

Moja kwa moja Sam alienda na Sabrina hadi kwenye gari na kupanda.
Sabrina alijishika shavu tu kusikilizia maumivu yale na kusahau kama mwilini amebakiwa na sidiria tu kwavile blauzi ilibaki ndani.
Sam alimpa pole pale huku akiondoa gari, Jeff alijikuta akisikitika tu
"Duh ya leo kali, sasa tunaenda wapi jamani?"
"Nyie tulieni tu, mtaona tutakapoenda"
Ndipo alipomtazama Sabrina na kugundua kuwa amebakiwa na sidiria tu,
"Ngoja nisimame hapo kwenye duka la nguo nikuchukulie mtandio"
Sam akasimamisha gari na kushuka.
Sabrina nae akajiangalia na kujicheka,
"Hii kweli balaa, alikuwa akiongea huku akitetemeka kwani bado ule uoga wa mwanzo alikuwa nao.
Jeff alimpa pole tu huku akimuangalia mtoto aliyekuwa mikononi mwake kwa muda huo.
Sam naye aliporudi alikuja na blauzi pamoja na mtandio ambapo Sabrina aliona ni bora avae tu ile blauzi kwanza kisha safari ikaendelea.

Mlinzi wa Sam alikuwa akishangaa tu kile kilichoendelea pale kwani hata yeye hakuelewa kitu hususani kile kitendo cha kumuona Sabrina akitoka ndani na sidiria tu ndio kilimpa mashaka zaidi na kumfanya ajiulize kuwa kuna nini ndani.
Akatamani kwenda kuangalia kuwa kuna nini ila akapatwa na mashaka kidogo kwani alihofia kuwa hicho kitu kinaweza kikamkimbiza na yeye pia hata kumkosesha amani ya kuendelea kulinda hapo kwahiyo akaona vyema abakie pale nje.
Muda kidogo akawasili yule mzee na kuwa kama akiwaulizia wakina Sam tena,
"Hawapo, wameondoka tena muda sio mrefu"
"Wameenda wapi sasa?"
"Kwakweli sijui maana sijaagwa na hapa wameondoka hai hai kamavile kuna kitu kimewapata"
"Hivi huyu kijana kwanini ni mbishi kiasi hiki? Hajui kama mimi naweza kufanya lolote? Hajui kama mimi ni mtu mbaya kuliko anavyofikiria? Mwambie nitamuharibu, nitamuhangamiza kama hanijui vizuri"
"Usimfanyie hivyo mzee wangu, si unajua tena ndio ajira hizi na sisi tunategemea hapa! Familia zinatutegemea wengine kwa kazi hii hii sasa ukimuangamiza tutaishije wengine hapa jamani?"
"Tatizo lake ana kiburi sana, na kiburi chake ndio kitakachomponza. Sasa natoa nafasi ya mwisho na ya upendeleo kwake, nitakupa namba zangu. Yani akirudi tu hapa nipigie na umwambie anisubiri hapa nje akikiuka nitajua mimi cha kufanya"
Kisha yule mzee akamtajia mlinzi wa Sam namba zake naye akaziandika na kuahidi kufanya kile alichoambiwa kisha yule mzee akaondoka zake.

Sam alitaka kuwapeleka mahali pengine ila akasita kidogo na kuona kuwa ni vyema waelekee nyumbani kwakina Sabrina kwanza kwani hata muda nao ulikuwa umeenda.
Walimkuta mama Sabrina naye akawakaribisha ingawa hakuwatarajia.
Sabrina akaona ni vyema amueleze mama yake kwa kifupi kilichotokea ili asiwe na maswali mengi.
"Mmh poleni, hata hivyo mna moyo jamani. Mbona ni mambo ya kishirikina hayo na yanatisha balaa"
"Yani mama wee acha tu hata sijui huyu mzee anataka nini"
Sam akajibu kawaida kabisa,
"Nyie muacheni tu nitamkomesha najua na yeye hanijui vizuri mimi. Yule mganga ni kichaa kwakweli, kwake aende mtu mwingine halafu aje kutusumbua sisi wakati ameshaturoga wee hadi tukafanya mambo ya ajabu ila nitamkomesha"
Hakuna aliyemuelewa Sam kuwa atamkomesha vipi yule mganga zaidi ya kumsikia kuwa atamkomesha.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ila leo itabidi nilale hapa maana sitaweza kwenda kulala kwangu kwa mauzauza yale"
"Hakuna tatizo mkwe wangu hapa vyumba vipo vya kutosha tu kwahiyo usiwe na wasiwasi."
Sam akamshukuru mkwe wake pale kwani mama huyu wa Sabrina hakuwa na tatizo lolote dhidi ya Sam kama ambavyo mumewe alikuwa akimchukia Sam kwa kipindi hicho na uzuri ni kwamba mara zote ambazo Sam amelala pale basi baba Sabrina hayupo na hiyo ikawa ni salama kwake.

Kwavile muda nao ulienda kidogo, Jeff akawaaga na kuondoka akielekea kwao ila njia nzima alikuwa akimuwaza mwanae na yale majanga ya Sam,
"Eeh Mungu nilindie mwanangu, laiti kama ningekuwa na uwezo ningemchukua ili niishi nae mwenyewe"
Aliongea maneno hayo wakati tayari amefika kwao na bila kujua kuwa mama yake amemsikia wakati akitamka hayo.
Alipoingia ndani tu mama yake akamuuliza,
"Jeff kumbe una mtoto! Sasa kwanini hutaki kuniambia mwanangu?"
Jeff akakaa kwenye kochi na kusema neno kwa mama yake,
"Hata nikikwambia huwezi kunielewa mama, kwani huwezi tambua ni jinsi gani nampenda yule mwanamke"
Sakina akamuuliza mwanae kwa mshangao,
"Mwanamke gani? Sabrina?"
Jeff akashtuka huku akitamani kumwambia mama yake kuwa ndio huyo huyo ila akasita kidogo kwani aliona wazi kuwa mambo hayajatulia kwahiyo mama yake angeweza kufanya hata varangati.
Ni hapo naye akajifanya amemshangaa mama yake,
"Kheee Sabrina!! Sabrina gani mama?"
"Kwani humjui? Si yule mama yako mdogo"
Jeff akacheka kidogo kama kuziba maana kwa mama yake,
"Jamani mama, si ushasema ni mama mdogo jamani sasa ndio inakuwaje hapo?"
"Aah basi tuachane na hayo"
Jeff akainuka na kuelekea chumbani kwake huku akimuachia maswali lukuki mama yake kwani bado hakumuelewa mwanae.

Usiku wakiwa wamelala, Sakina akajiwa na ndoto ambayo ilimshtua sana.
Kwenye ndoto ile alimuona Sabrina akiwa amesimama huku kamshikilia yule mwanae mikononi na kumwambia Sakina
"Hivi wewe Sakina lini utakubali kuwa huyu niliyemshika ni mjukuu wako? Lini utaamini kuwa mimi na Jeff tunapendana? Hivi ni nani kakwambia kuwa mapenzi yanachagua? Penzi ni kama jani huota popote. Naomba ukubali tu na umshike mjukuu wako"
Sabrina akawa kama anampa Sakina yule mtoto ila kabla hajampokea akatokea Sam na kumwambia,
"Ole wako umpokee huyo mtoto, najua hunijui vizuri. Nitakufanya kitu mbaya"
Ikabidi asimpokee ila akamuona Sabrina akianguka na yule mtoto mikononi ndio hapo aliposhtuka kutoka usingizini na kujikuta akikaa huku akijiuliza kuwa ile ndoto inamaana gani katika maisha yake.
Akajikuta akiwaza kuwa asubuhi na mapema aende kwakina Sabrina.

Kulipokucha tu, Sakina aliamka na kuoga kisha akatoka na kuelekea kwakina Sabrina.
Alipofika alimkuta Sabrina akiwa amesimama huku kambeba mtoto mkononi na Sam akiwa mbele yake kanakwamba kuna kitu wanazungumza pale nje.
Alisogea na kuwasalimia ambapo Sabrina alimkaribisha vizuri tu Sakina na wakasalimiana nae vizuri kabisa,
"Karibu ndani Dada, na mbona asubuhi asubuhi hivyo?"
"Aah nimekuja kuwasalimia tu"
Kisha akasogea kamavile anahitaji kumshika mtoto ambapo Sabrina alimkabidhi mtoto yule kisha akaingia nae ndani na kuwaacha Sabrina na Sam pale nje.

Sabrina alikuwa anataka Sam amueleze atakachoenda kufanya na yule mzee,
"Usiwe na mashaka Sabrina, mi huwa sikosei nikipanga jambo ingawa kwako nilikosea"
"Ila uwe makini Sam, kwani kumbuka kwamba yule mzee ni mganga wa kienyeji na anaweza kukudhuru akitaka. We fikiria tu kama ndani ameweza kutufanyia vituko kiasi kile sasa ukimfata si ndio balaa"
"Usijali Sabrina, mi naenda kumpa pesa yule mzee na hatotusumbua tena"
"Ila zikiisha atasumbua tena tu, si unajua pesa ni mwanaharamu? Na hata siku moja mtu haridhiki na pesa hata awe bilionea"
"Nimekwambia usijali, yule mzee shida yake ni pesa na mimi nitaenda kumpa pesa ili asinisumbue tena"
Sabrina akaona ni vyema amuache akafanye hiko anachoona yeye kuwa ndio sahii kwake na kuagana nae pale.
"Nitakuja badae halafu tutamaliza mazungumzo yetu na muhafaka wetu"
"Sawa hakuna shida, kwaheri"
Sam alienda kupanda gari yake na kuondoka kisha Sabrina akarudi ndani kwao.

Sabrina akafika mlangoni na kusimama kwa muda kwanza kwani alikuwa akimuangalia Sakina jinsi anavyomuangalia mtoto wake akatabasamu kwani alijua wazi kuwa Sakina kuna kitu anakihisi kuhusu yule mtoto ila anashindwa kumuuliza.
Muda kidogo Sakina nae akajihisi kama akiangaliwa na kujikuta akiinua kichwa na yeye halafu macho yake yakagongana na Sabrina na kuliona lile tabasamu la Sabrina na kujikuta akimuuliza swali ambalo hata hakupanga kumuuliza kwa muda huo,
"Hivi huyu mtoto anaitwa nani tena?"
"Anaitwa Sam, niliamua kumpa jina la baba yake"
"Aah umefanya vizuri mwaya"
Huku akiendelea kumuangalia mtoto yule na kumkadilia.
Sabrina akapita pale na kuelekea chumbani kwake huku akimuacha Sakina pale sebleni na yule mtoto.

Sakina alitafakari kidogo na kukumbuka hospitali maneno yale ya manesi wakati Sabrina anajifungua.
Akakumbuka na kauli ya Jeff ya kusema kwamba aliamua kujifanyisha ni mume wa Sabrina ili kuokoa maisha ya Sabrina.
Akamtazama na mtoto sasa anavyofanana na Jeff na kujiuliza kuwa kwanini wanamficha huku akifikiria pia kuwa Sabrina aliwezaje kumkubali mtoto mdogo kama Jeff? Yani Sakina alijihisi akili yake kutokujisoma vizuri kabisa.
Muda kidogo Jeff nae akafika pale kwakina Sabrina kwani hakujua kama mama yake nae yuko pale.
"Mama, kumbe umekuja huku?"
"Ndio, mbona na wewe umekuja?"
"Mie nimekuja kuwasalimia mama"
" Mmh na mimi nimekuja kusalimia pia"
Yule mtoto nae aliposikia tu sauti ya Jeff akageuza shingo na kumuangalia na kuanza kama kulia.
Ikabidi Jeff amchukue mtoto huyo na kumbeba yeye, na muda kidogo akalala akiwa kwenye mikono ya Jeff na kumfanya Sakina azidi kupatwa na mashaka dhidi ya Jeff na Sabrina ila ndio hivyo hakuwa na uhakika kwa anachokiwaza.

Sam alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake na kumkuta yule mlinzi nje ambaye alimueleza kila kitu kuhusu yule mzee.
"Kwahiyo huyo mzee ndio kakuachia maagizo hayo Omary?"
"Ndio alivyoniambia"
"Basi mpigie simu aje, me nitamsubiria"
Yule mlinzi wa Sam akachukua simu na kumpigia yule mzee na muda kidogo alikuwa amefika eneo lile kanakwamba hakuwa mbali na eneo lile.

Sam akasalimiana na yule mzee kisha akaingia nae ndani ya geti sasa.
Muda kidogo yule mlinzi wa Sam akasikia mlio wa risasi na kumfanya nae aingie ndani ya geti, akashangaa kumuona yule mzee chini huku damu ikiwa imetapakaa eneo lile.


Muda kidogo yule mlinzi wa Sam akasikia mlio wa risasi na kumfanya nae aingie ndani ya geti, akashangaa kumuona yule mzee chini huku damu ikiwa imetapakaa eneo lile.
Sam alikuwa amesimama huku kashikilia silaha yake mkononi, yule mlinzi alimshangaa sana Sam ambapo Sam akaongea kwa ukali,
"Unashangaa nini wewe kwani hujawahi kumuona mtu aliyekufa? Huyu mzee si ndio mchawi mashuhuri basi mi nataka kuona uchawi wake unavyoshindana na kifo."
Yule mlinzi bado akamtazama tu Sam kwani hata uwezo wa kumzuia hakuwa nao.
Sam akamuomba yule mlinzi kusaidiane kumbeba yule mzee kisha wakampakiza kwenye buti ya gari ya Sam ambayo ilikuwa pale ndani.
"Sasa shughuli nimemaliza, Omary nitakupeleka kwenye nyumba yangu nyingine ukalinde huko kwani hii nitaipiga bei."
Mlinzi aliitikia tu kwani hakuwa na namna yoyote ya kumbishia bosi wake huyu.

Sabrina akatoka chumbani ili amchukue mtoto ila alipowakuta pale sebleni Jeff na mama yake ikabidi ajifanye anawashangaa wote wawili.
"Jamani leo vipi mama na mwana kuja mapema mapema?"
"Si kwaajili ya kuwasalimia jamani kwani kuna ubaya?"
"Hakuna ubaya dada yangu"
Kisha Sabrina akamchukua mtoto na kumpeleka chumbani.
Alimlaza na kukaa chini huku akitafakari kidogo kwani alishapatwa na hisia kuwa kuna kitu Sakina atakuwa amekihisi baina yake yeye na Jeff, akajikuta akiongea mwenyewe
"Mapenzi jamani mapenzi kwanini mapenzi? Ni kweli nilikuwa nampenda Jeff ila si kimapenzi kwani nilimpenda kawaida kama mtoto tu. Iweje leo nimpende kimapenzi? Iweje nimpende wakati alinibaka mara ya kwanza? Hivi mapenzi gani haya? Mbona yananichanganya jamani kwani nafikia hatua hata ya kutamani kuishi naye duh mapenzi haya, aliyesema kizunguzungu hata hakukosea."
Mara akafatwa na mama yake na kupewa simu,
"Simu hii ongea nayo amekuulizia wewe"
Sabrina akachukua ile simu na kuanza kuongea nae, akagundua kuwa ni yule mlinzi wa Sam na kuamua kumsikiliza kwa makini sana,
"Hebu jaribu kuwasiliana na bosi maana naona kamavile hatokuwa sawa , mpigie kwa simu yake ile nyingine sababu hii kaiacha ndio nimeamua kuwapigia huko"
Sabrina alimsikiliza kwa makini sana na ikawa ngumu kumuelewa kwani yule mlinzi hakusema kuwa Sam kapatwa na nini zaidi ya kusema anahisi hayupo salama.
Simu ilipokatika, Sabrina akamrudishia mama yake kwani ilikuwa ni simu ya mama yake.
Alichekecha akili yake na kukumbuka kuwa Sam alipoondoka alisema anaenda kwa yule mzee ndipo hapo alipopatwa na mashaka kisha kwenda kumuomba mama yake simu ili ampigie Sam.

Akawasiliana nae ila Sam alionekana kawaida tu kuwa hana tatizo lolote,
"Upo sawa kweli Sam?"
"Nipo sawa ndio, hata usiwe na mashaka"
"Vipi yule mzee ulienda kuonana nae?"
"Tutaongea vizuri nikija hata usijali"
Sam akakata simu na kumfanya Sabrina abakiwe na jibu la njiapanda tu kuwa asijali.
Akamrudishia simu mama yake aliyekuwa sebleni kwa muda huo kisha yeye akarudi chumbani.
Jeff nae na mama yake wakamuaga pale mama Sabrina na kuondoka zao.
Walipokuwa wanatoka wakapishana na James akiwa na mkewe Joyce pamoja na watoto wao ikabidi nao warudi ndani ili wasalimiane vizuri.
Wakina James walikuwa wamechangamka sana na walionekana kuwa na furaha kwa kipindi hicho baada ya kile kipindi cha mkangaranyiko wa matukio ambao uliwapata.
Mama yao aliwakaribisha vizuri sana na alifurahi sana kuwaona.
Akawachukua wajukuu zake na kuwashika kwa pamoja kwavile alikuwa na furaha sana kwa kile alichokiona mbele yake.
"Karibuni sana jamani, maana najihisi raha kuwaona"
"Tumekaribia mama, tuliwakumbuka sana kwakweli"
Mtoto wa kwanza wa Sabrina baada ya kusikia zile kelele kelele naye akaamka na kutoka pale sebleni, na alipofika tu akawashangaa kwa muda halafu akaenda moja kwa moja alipo Jeff ingawa James naye alimuita ili amsalimie,
"Kheee mama huyu ndio mtoto wa Sabrina?"
"Eeh ndio Cherry huyo"
"Khee amekua huyo hadi raha, ameanza na kuongea tayari?"
"Anaongea makorokocho tu, anaelewana na huyo huyo aliyembeba"
Joy nae akachangai,
"Halafu kafanana nae sana"
Mama Sabrina nae akaongezea,
"Khee mnamshangaa huyo kwavile hamjamuona yule mdogo ndio kafanana nae balaa"
Sakina alikuwa kimya kabisa ila Jeff naye aliishia kutabasamu tu.
Sabrina nae akatoka ndani na kuwakuta na ile mada.
Akawasalimia pale na kuongea mawili matatu ambapo Jeff na mama yake wakaaga tena na kuondoka ila yule mtoto wa Sabrina kama kawaida akaanza kumlilia tena Jeff na kumfanya Sabrina acheke na kusema,
"Hivi wewe mtoto una matatizo au? Umeanza lini kumlilia Jeff!"
Mama Sabrina nae akaongezea,
"Sio leo tu, ni mara kwa mara akija anamlilia"
Sabrina akamchukua mwanae na kumbeba ambapo Joy nae akaongea,
"Nadhani amejua kama anafanana nae ndiomana anamlilia"
Sabrina akaguna tu huku Jeff na mama yake wakitoka na kuwaacha wale ndani wakizungumza.
Sabrina akakaa chini na kumchukua yule mtoto wa kwanza wa kaka yake na kumpakata pamoja na mwanae kisha akawa kama anachombeza,
"Mbona huyu nae hafanani na baba yake?"
Joy akatulia kwanza na kupooza,
"Kafanana na babu yake huyo"
Sabrina akaguna na kucheka tu, kisha akasema,
"Kweli mtoto sio lazima afanane na baba yake jamani kwani anaweza kufanana na yeyote duniani kutokana na uumbaji wa Mungu"
James hakuchangia hapo wala mama Sabrina hakuchangia zaidi ya Joy kutabasamu tu na kubadilisha mada kwani alijua wazi kuwa mada ile ingeenda ndivyo sivyo.

Jeff na mama yake walitoka kwa kina Sabrina pamoja tena vizuri kabisa ila njiani Jeff akamuaga mama yake kuwa kuna mahali anaenda, Sakina hakuwa na pingamizi zaidi ya kuagana nae tu kisha Jeff akaondoka zake.
Sakina alifika nyumbani na kujitafakarisha sana kwani aliona ni jinsi gani kila mtu anawafananisha watoto wa Sabrina na mwanae Jeff na kumfanya aendelee kupata uhakika wa mawazo yake ingawa hakvaka kukubaliana na ukweli huo kwani bado hakuweza kuamini kama Sabrina anaweza kulala na Jeff hadi kufikia hatua ya kuzaa naye.
Kwakweli ilikuwa ni ngumu sana kwa Sakina kukubaliana na hali halisi na kumfanya atamani usiku na mchana kumuuliza Sabrina ukweli wa mambo yote.

Jeff alikuwa ameenda stendi kumfata Aisha kwani alimtaarifu kuwa amefika na kweli alimkuta pale kituoni akimsubiria.
"Karibu sana Aisha, nilijua masikhara ujue"
"Yani ulijua natania Jeff? Hapana nilikuwa namaanisha kabisa"
"Basi sawa, karibu sana kwetu. Ila naomba nikuombe kitu"
"Niombe tu usijali Jeff"
"Pale nyumbani nitamwambia mama kuwa wewe ni mpenzi wangu kwahiyo usikatae tafadhari"
Aisha akatabasamu kwa furaha,
"Hilo sio tatizo Jeff yani sio tatizo kabisa hata usijali. Mi nitakubali chochote utakachosema"
Basi wakaanza kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwakina Jeff.
Njiani wakaona gari ya Sam ikisimama mbele yao ambapo Sam alishusha kioo na kuwauliza wanapoelekea.
"Tunaenda nyumbani"
Jeff ndiye aliyejibu, kisha Sam akawaomba wapande kwenye gari ili awasogeze kidogo nao wakapanda.
Sam aliwapeleka hadi mlangoni kwakina Jeff ila kabla hawajashuka akauliza swali,
"Kumbe nyie mnafahamiana kiasi hiki hadi mnaenda nyumbani pamoja?"
Hapo ndio Aisha akadakia kujibu,
"Ndio, Jeff anaenda kunitambulisha kwao kama mke mtarajiwa"
Sam alibaki kushangaa na kuwaacha washuke, hata Jeff nae alimshangaa Aisha kwa jibu lake lililotolewa haraka haraka kiasi kile.
Kisha wakaingia ndani halafu Sam akaondoka zake.

Walimkuta sebleni mama yake na Jeff, ambapo Jeff alipoingia tu alianza kwa kumwambia mama yake,
"Mama, nimekuletea mgeni leo"
"Karibuni sana, ila kabla ya yote naomba umtambulishe tafadhari"
Jeff akatulia kimya kwa muda kwani akili yake ilikuwa kama inamzuia kwa kile anachotaka kusema na moyo wake nao ulikuwa unapingana na jambo lile.
Ila Aisha alipoona ukimya umetawala akaamua kuvunja ukimya huo kwa kusema,
"Mimi ndio mchumba wa Jeff mama"
Huku akitabasamu tu na kumfanya Sakina nae atabasamu ingawa kidogo amemshangaa huyu binti kwa kujitambulisha mwenyewe.
Ila akamkaribisha hivyo hivyo kwa ukarimu na furaha ingawa Jeff alikuwa kimya kabisa akimuangalia tu Aisha na kumfanya hadi mama yake amshtue.
"Vipi kwani una tatizo gani? Mbona kimya gafla?"
"Hapana tatizo mama, ila nilikuja nae huyu kwa lengo la kukusalimia tu mama angu. Ila naomba utupe ruhusa yako tuondoke mama"
"Kheee hata kukaa kidogo jamani! Mbona muondoke mapema hivyo? Subirini tule kwa pamoja tufurahi ndio muondoke"
"Hapana mama, kuna mahali tunataka kuwahi tafadhari mama"
"Hapana kwakweli, hapa mmefika na wala siwezi kuwaruhusu muondoke bila ya kupata baraka ya chakula cha pamoja. Ni haraka tu chakula kitakuwa tayari sababu nilishakibandika wanangu jamani"
Jeff hakuwa na la ziada, ikabidi tu atulie na kufata lile analosema mama yao.

Sam nae alifika kwakina Sabrina na kuwakuta mule ndani kisha akasalimiana nao kama kawaida na wao wakamkaribisha sana.
Pia akafurahi kumuona dada yake Joyce kwani ni kipindi kirefu hajaonana nae.
Muda kidogo akamuomba Sabrina na wakainuka kwenda kuongea kidogo,
"Naomba twende nyumbani Sabrina"
"Mmh hapana Sam, sipo tayari kurudi pale tena. Najua yule mzee atatusumbua tu, nawapenda wanangu Sam"
"Usijali, nishamaliza tatizo la yule mzee"
"Umelimalizaje?"
"Hata usijali Sabrina, wewe niamini kuwa lile tatizo limeisha na hata hivyo hatutaenda tena nyumba ile"
"Tutaenda wapi sasa?"
"Kuna nyumba nyingine nitawapeleka, huijui nyumba hiyo ila ndio itakuwa urithi wa watoto wangu"
Maneno haya ya urithi wa watoto yakamuingia akilini kidogo Sabrina kwani anajua wazi kuwa Sam hana mtoto yeyote isipokuwa wale wawili tu ambao sio wake kwa kuzaa.
Sabrina akakubali ila kwa sharti kuwa nyumba hiyo isiwe kule kule kwa mwanzo yani iwe kweli, naye Sam akamuhakikishia na kumuomba akawaandae watoto.
Sabrina aliingia ndani na kumuacha Sam sebleni kisha yeye akaenda kuwaandaa wale watoto wao.
Muda kidogo akatoka na kuwaacha watoto sebleni halafu yeye akatoka nje, na moja kwa moja akaanza kuelekea kwakina Jeff kwani alihitaji awasindikize.

Sabrina alifika kwakina Jeff na moja kwa moja akaingia ndani kama kawaida yake, akawakuta wapo mezani wakila. Naje moja kwa moja akawafata eneo lile na kumshangaa Aisha pale.
Sakina alimkaribisha vizuri Sabrina,
"Karibu tule Sabrina, leo tumepata ugeni. Nimetembelewa na mchumba wa Jeff bhana anaitwa Aisha"
Jeff aliinama chini tu huku akimsikiliza mama yake akimaliza hoja zote kwa wakati mmoja.
"Usijali dada, nilikuwa na shida na Jeff kidogo ila kwavile unakula malizia basi halafu uje nyumbani, kuna kitu naomba ukanisaidie"
Kisha hakungoja jibu la yeyote kati yao na kuondoka.
Alirudi nyumbani kwao huku moyo ukimuuma sana.
Akamuona Sam akiwa nje ambapo alipomkaribia tu alimuuliza,
"Mbona umetoka nje?"
"Nilikuwa nakuangalia wewe, mbona uliondoka? Ulienda wapi?"
Akatafuta uongo wa haraka na kuukosa ikabidi tu amwambie ukweli kuwa alienda kumuita Jeff kuwa aje amsaidie baadhi ya vitu.
"Sasa yuko wapi?"
"Tuondoke tu kwanza mizigo yenyewe kidogo tu"
Sam akaelewa kabisa kuwa lazima Sabrina kamkuta Aisha kule ndiomana kamaindi ila akamkubalia na kuchukua begi mbili za nguo na kupakia kwenye gari kisha kuchukua watoto wote wawili ingawa mama yake aling'ang'ania kubaki na yule mkubwa ila Sabrina alimuahidi mama yake kumleta huyo mtoto kwa wakati mwingine kisha wakaondoka.
Ikabidi mama Sabrina amwombe James wamuachie yule mtoto wao wa kwanza japo kwa siku mbili tu,
"Mama jamani, ila tushamzoea chautundu wetu"
"Mwacheni bwana nikaekae nae kidogo"
Wakakubaliana juu ya hilo na wakakubali kumuachia mtoto huyo.

Sam alienda moja kwa moja na Sabrina kwenye nyumba mpya na kweli ilikuwa nzuri sana.
"Sasa siku zote alikuwa anakaa nani humu?"
"Hii nyumba haijawahi kukaliwa na mtu, ni mpya kweli. Kesho nitamleta huku yule mlinzi wa kule."
"Itakuwa vizuri"
"Ila usijali, binti wa usafi yupo anakuja asubuhi na kuondoka jioni"
Sabrina bado hakuelewa kuwa maandalizi ya ile nyumba yalianza lini.

Jeff alipomaliza kula tu alitoka pamoja na yule Aisha kisha wakamuaga mama yao.
Wakaelekea kwakina Sabrina pamoja kwani Aisha hakutaka kuachwa ndani tu.
Ila hawakumkuta Sabrina na kuambiwa kuwa ameondoka na mumewe.
Moja kwa moja akajua wamerudi tena kwao.
Akaamua kuaga pale na kuondoka huku akijiuliza kuwa kwanini Sabrina amewapeleka tena watoto wake wote kwenye ile nyumba ya mabalaa.
Akajikuta akisema kwa nguvu sasa,
"Anataka kunipotezea watoto yule"
Aisha akauliza,
"Watoto gani tena?"
Jeff akamgelesha pale kisha akamsindikiza Aisha na alipopanda gari tu naye akapanda kuelekea nyumbani kwa Sam.

Jeff alifika nyumbani kwa Sam, ila kabla hajasogelea geti akahisi kichwa chake kikiwa kizito sana na kumfanya afikirie kuwa kuna kitu.
Pale getini hakumkuta mlinzi wa Sam, ila geti lilionekana kurudishiwa tu.
Hivyobasi akaamua kulisukuma na kuingia ndani.
Akashangaa kumuona mlini wa Sam akiwa chini huku damu zikimtoka.

Hivyobasi akaamua kulisukuma na kuingia ndani.
Akashangaa kumuona mlinzi wa Sam akiwa chini huku damu zikimtoka.
Jeff akashtuka sana na kutamani kumsogelea ili amtingishe na kuona imekuwaje.
Ila kabla hajafanya hivyo, moyo wake uliingiwa na mashaka na kumfanya asite kwenda kumgusa yule mlinzi.
Akaamua kutoka nje ili ajaribu kumpigia simu Sam na kumuuliza.
Ila alipotoka nje, akashangaa kumuona yule mlinzi wa Sam akiwa amekaa pembeni ya geti kwenye kiti kama kawaida yake.
Hapo ndipo palipomfanya Jeff apatwe na mashaka zaidi na kujikuta akianza kukimbia.
Yule mlinzi nae akamshangaa na kuanza kumkimbilia ila kitendo hicho ndio kilichozidi kumpa Jeff hofu na kujikuta akiongeza mbio kushinda mwanzoni.
Yule mlinzi aliamua kurudi tu kwani hata hakuelewa kuwa ni kitu gani kimemfanya Jeff akimbie kiasi kile kwakweli hakumuelewa kabisa na akarudi kwenye kiti chake kukaa.

Yule mlinzi akatafakari kidogo kuwa Jeff sio chizi hata akimbie kiasi kile na kuhisi wazi kuwa lazima kuna kitu tu ingawa hata yeye hakuingia tena kwenye nyumba ya Sam tangu siku ile walipotoa mwili wa yule mzee.
Akatamani akachungulie kuwa kuna nini ila akasita kidogo kisha akajiuliza,
"Hata hivyo, amepitaje pitaje huyu bila ya mimi kumuona jamani? Au muda ule nilipozunguka nyuma kidogo?"
Hakupata jibu ila akaona wazi kuwa kwa tukio hilo ni ushirikina ambao umechukua nafasi mahali hapo.
Naye akasita kuingia ndani na kuamua kubaki hapo hapo nje.

Jeff alikimbia hadi kituo cha daladala kisha akapanda daladala na kurudi kwao.
Njia nzima alikuwa akitafakari kile ambacho amekiona, alikuwa akijiuliza maswali bila ya majibu kuwa kitu kama kile kinawezekanaje,
"Ile nyumba ni mauzauza siku hizi halafu Sabrina naye kaenda huko huko, hivi kwanini hajihurumii jamani!"
Akapata wazo la kumtafuta Sam hewani ili aweze kumuuliza kuhusu jambo lile ila simu ya Sam iliita tu bila ya kupokelewa na kumfanya azidi kupatwa na mashaka dhidi ya wakina Sabrina na kutamani hata Sabrina angekuwa na simu basi angempigia moja kwa moja.
Ikabidi arudi tu nyumbani kwao na moja kwa moja akaenda chumbani kwake ili apate utulivu na kutafakari.

Kwa upande wa Sam na Sabrina ilikuwa furaha tu kwani Sabrina alifurahia sana ile nyumba mpya aliyopelekwa siku hiyo na kujiona kuwa ameridhika sana.
Sam alimuaga kidogo Sabrina kwa muda huu na kwenda zake mjini.
Sabrina alibaki na watoto wake, akawaangalia walivyofanana na Jeff akafikiria na stori ya Sam.
"Ingawa Sam hakunimalizia story yake, ila inaonyesha wazi kuwa bila ya Jeff hata mi ningekuwa katika mlolongo wa wadada waliokufa sababu ya Sam."
Akatafakari pia kauli ya Sakina kuwa yule Aisha ni mchumba wa Jeff,
"Mmh huyu nae anataka kuniumiza moyo tu, najua anatamani sana kuujua ukweli ila tatizo ni kuwa akigundua huo ukweli nitaweka wapi sura yangu jamani?"
Aliamua kutulia tu kwani aliona wazi kuwa sio jambo jema kuwaza kitu ambacho anajua wazi kuwa kitamgharimu maishani.
Muda kidogo akainuka na kuelekea chumbani.
Akaiona simu ya Sam kitandani na kuichukua, akaiangalia na kukuta kuna simu ambazo hazikupokelewa kama tano, hapo akagundua kuwa Sam amesahau simu yake ndiomana imekuwa vile.
Sabrina akaichukua ile simu ili kuangalia kuwa nani aliyekuwa akipiga, ila kabla hajabonyeza ile simu ikaanza kuita tena na namba ilitokea bila jina, Sabrina akaipokea ile simu ila kabla ya kusema 'halow' yule mtu kwenye simu akaanza kuongea na ilikuwa ni sauti ya kike,
"Nilikuwa najaribisha namba yako, mambo vipi lakini? Nipo hapa nje ya nyumba yako."
"Wee nani?"
"Mi nani? Kwani na wewe nani? Mpe mwenye simu wee vipi!"
"Mwenye simu katoka, na mimi ni mke wake sema unataka nini?"
Ule upande wa pili ukacheka,
"Mke wake? Acha kunichekesha dada, toka lini Sam ameoa? Hebu acha kuniletea miujiza, hebu mpelekee simu bhana"
"Kheee mbona unachekesha wee dada, ndio kujifanya unamfahamu Sam sana au? Na kama ungekuwa unamfahamu basi ingekuwa rahisi kwako kutambua kama Sam kaoa. Mimi ni mke wake na nimezaa nae watoto wawili, tena uwe na adabu siku nyingine"
Kisha Sabrina akaikata ile simu na kumfanya alalamike peke yake huku akimshangaa huyu dada,
"Yani ndiomana Sam anawamaliza kiurahisi, wajinga sana hawa. Mtu unamwambia kabisa kuwa mimi ni mkewe ila bado anang'ang'ania"
Ile simu ikaanza kuita tena kwa namba ile ile, Sabrina akaipokea tena,
"Wee dada mi najua kama Sam anamsichana wa kazi ila sio mke kwahiyo kumfanyia kazi Sam kusikufanye ujiite mke umesikia wee malaya eeh! Na umwambie Sam nipo hapa nje ya geti namsubiria"
"Sikia wee dada na unisikilize kwa makini, kama nyumba ya Sam unaijua sana basi ingia. Nini kumsubiria getini kwani mlango huuoni? Si uingie kama wewe unaijua sana hii nyumba"
"Hebu njoo unifungulie geti wee malaya niingize gari yangu"
Sabrina hakumjibu ila akamsonya yule mwanamke na kuikata ile simu halafu akaizima kabisa na kukaa chini akiongea mwenyewe,
"Hivi huyu Sam huyu ananitakia nini mimi? Kwanini anilete kwenye nyumba ambayo kuna wanawake zake wanakujaga jamani? Yani na kufunga kote ndoa kule bado kuna watu hawajui kuwa Sam kaoa? Ila ngoja huyo mwanamke agonge hilo geti nitamkomesha"
Sabrina alitulia ila hakusikia mtu yeyote akigonga na kuamua kwenda kuchungulia nje ila hakuona kabisa uwepo wa mtu yeyote na kuamua kurudi ndani.

Jeff alipopiga tena simu ya Sam na kukuta haipatikani akazidi kupatwa na mashaka kuwa lazima kuna mabalaa yatakuwa yamewapata tu na kujikuta akikosa raha zaidi na kuamua kwenda kwakina Sabrina ili ajaribu kumueleza alichokikuta na vile ambavyo hawapokei simu na sasa hawapatikani kabisa.
Alimkuta mama Sabrina akiwa na mjukuu wake mtoto wa James ila James na mkewe hawakuwepo yani walishaondoka.
Jeff akamueleza alichokutana nacho kwenye nyumba ya Sam,
"Kwahiyo wewe ndio ukakimbia sasa?"
"Mama hali ni mbaya kwakweli, nisingeweza kubaki eneo lile. Niliogopa sana"
"Na kweli hiyo hali inatisha, ila Jeff kwahiyo sasa nimekuwa mama yako na sio bibi tena eeh!"
"Aah ni bibi, nisamehe tafadhari. Akili yangu haipo sawa"
"Basi hakuna tatizo, ushasema ile nyumba inamatatizo kwasasa cha msingi tuendelee tu kutafuta mawasiliano yao kwani hata tukisema tuende sijui kama itasaidia. Au ngoja"
Mama Sabrina akafikiria kidogo na kugundua kuwa ana namba ya mlinzi wa Sam na kuamua kuipiga namba hiyo.
Ila alipoipokea tu akawaambia kuwa hawapo kule,
"Sasa watakuwa wapi jamani?"
"Sijui labda wameenda hotelini maana bosi anapenda sana kwenda hotelini"
Ikabidi wakubaliane hivyo na waamini hivyo tu.
Jeff alikubali kwa shingo upande tu kisha akaaga na kurudi nyumbani kwao kwani giza nalo lilishaingia.

Sam aliporudi nyumbani kwake akamshangaa Sabrina kwani hakuna na furaha kama aliyokuwa nayo mwanzoni.
"Vipi tena Sabrina kuna tatizo?"
Sabrina hakutaka kueleza kwani alikuwa na hasira muda huo.
Sam alitambua kama Sabrina alikuwa na hasira ingawa hakujua hasira hizo zimesababishwa na kitu gani kwa muda huo.
Sam akatoa mfuko mdogo mweusi na kumpa Sabrina,
"Chukua hiyo ni zawadi yako"
Sabrina alichukua na kumshukuru Sam ingawa bado hakuwa na furaha.
"Ifungue uone, mbona umeishika tu? Ifungue uonge kuna nini"
Sabrina akafungua na kukutana na simu nzuri mpya na ya kisasa.
"Nimeamua nikuletee simu ili usikae bila mawasiliano"
Sabrina akatabasamu sasa, kisha Sam akainuka na kuelekea zake chumbani kulala.
Sabrina aliiangalia ile simu mara mbili mbili na kuona kuwa kweli Sam kajirudi kwasasa.
Ila alitulia pale sebleni kwa muda sana huku akifurahia ile simu na huku akiogopa kwenda kulala chumbani na Sam kwani alikuwa akijiuliza
"Hivi kwa mfano Sam akinigeuka na kutaka kulala na mimi? Inamaana na mimi ndio itakuwa mwisho wangu kama wale wengine? Na watoto wangu je hawa nitawaacha na nani? Hapana ngoja nilale chumba kingine, ila kama Sam alikuwa na nia mbaya na mimi si angeshanifanyia tangu zamani! Mmh ila naogopa"
Akainuka na watoto wake na kwenda kulala nao chumba kingine.
Aliwalaza watoto na yeye akalala pembeni yao huku akitafakari kuhusu ile simu na akatamani sana kumpigia mtu, kwavile ilikuwa na vocha kwahiyo swala la kupiga halikuwa gumu kwake.
Ila akaona ni vyema aanze kupiga kesho yake ila kila alipojigeuza swala la kupigia simu mtu muhimu sana maishani mwake lilimjia kichwani, na mtu huyo alikuwa ni Jeff.
Akaamua kuichukua simu na kuandika namba ya Jeff kwani namba yake ilikuwa kichwani kisha akaipiga na kuanza kuisikilizia.

Jeff akiwa amekaa chumbani kwake na mawazo sana, akashtuliwa na mlio wa simu na kushangaa kuona ni namba mpya na kumfanya ajiulize kuwa ni nani aliyempigia usiku ule.
Jeff akapotea ile simu na kusikia sauti ya Sabrina,
"Khee Sabrina, Sam yuko wapi?"
"Kalala"
"Huogopi kunipigia usiku? Na je huogopi kulala nae karibu?"
"Kwahiyo hujapenda nilivyokupigia?"
"Hapana sio hivyo Sabrina, tena nimewatafuta toka mchana na hata muda huu nilikuwa sijalala sababu ya kukuwaza wewe na watoto. Mko wapi kwani?"
"Sam katuleta kwenye nyumba yake mpya"
"Afadhari maana nilikuwa na mawazo sana. Nakupenda jamani Sabrina"
Sabrina akakaa kimya kidogo kwani hili neno kila alipoambiwa na Jeff alijikuta akisisimka sana yani tofauti na akiambiwa na Sam.
Wakati Jeff akimsikilizia Sabrina aongee mara akasikia sauti ya kiume ikiita Sabrina na sauti hiyo ilikuwa ya Sam, na muda huo huo simu ikakatika na kujua wazi kuwa Sabrina amekata simu ile baada ya Sam kumshtukia akiongea nayo.

Sabrina alikata ile simu kwa haraka sana baada ya kusikia sauti ya Sam akimuita, na muda huo huo Sam akafungua mlango wa kile chumba na kuingia ndani. Swali la kwanza alilomuuliza,
"Mbona umekuja kulala huku badala ya kuja kulala chumbani kule na watoto"
Sabrina hakuwa na jibu zaidi ya kumtazama Sam tu,
"Usiwe unaniogopa Sabrina, hivi utaniogopa hadi lini? Na kama ningekuwa na lengo la kukudhuru mbona ningefanya hivyo zamani sana? Ila kwavile watoto washalala basi lala nao tu ila kipindi kingine uwe unajiuliza kwanza kama unachofanya ni sahihi kabla ya kukifanya. Haya sasa kukupa simu imekuwa tatizo, usiku ulikuwa unaongea na nani?"
Sabrina bado alikuwa kimya kwani hata hakuelewa aseme nini ukizingatia ni kweli kafanya makosa.
Sam akamuangalia Sabrina na kusema tena,
"Ndiomana wanawake mnapigwa, na mkipigwa mnadai kuwa mnaonewa ila kwakweli ni makosa yenu. Mimi leo sitasema sana acha nikalale tu"
Sam akatoka na kwenda kulala, Sabrina nae akaweka simu pembeni na kulala sasa kwani hakuamini kama Sam angemuachia tu ukizingatia anajua wazi kuwa ni nani aliyempigia simu kwani alihisi kuwa lazima Sam amesikiliza kidogo mazungumzo yao.

Kulipokucha Sam alikuwa wa kwanza kuamka na kumfata Sabrina chumbani kwake, baada ya salamu tu akamuuliza
"Sabrina, simu yangu iko wapi?"
Sabrina akanywea kidogo kisha na yeye akamuuliza Sam kwa upole sana,
"Ile uliyoniletea jana?"
"Hapana, hiyo ni yako sio yangu bhana na kama nikikuuliza kuhusu hiyo basi nitakuuliza kuwa simu yako iko wapi na sio simu yangu"
"Sawa, simu ipi unayoiulizia sasa?"
"Naulizia simu yangu niliyoiacha jana chumbani nilipoondoka"
Sabrina akakumbuka kuwa hiyo simu alipoizima aliiweka sebleni na kuamua kwenda kuichukua kisha akamuomba msamaha Sam kwa kuizima simu hiyo.
"Na kwanini uliizima sasa?"
Sabrina ikabidi tu aeleze kuhusu mdada aliyepiga simu jana na jinsi walivyojibishana,
"Nisamehe Sam tafadhari"
"Sio tatizo hilo, itakuwa alikuwa anazungumzia nyumba ya kule. Sabrina, hakuna mtu anayepafahamu hapa hata ndugu zangu hakuna ila nitawaleta tu na wewe ukiwa hapa hapa. Ila ngoja niende kule kwangu nikamuangalie Omary kwanza na nione uwezekano wa kumleta huku"
Sam alitoka na kupanda kwenye gari yake kisha akaondoka.
Sabrina alitulia ila alijua wazi kuwa lazima Sam ataenda kumtafuta yule dada wa jana ingawa hakumjua ni nani.

Sam akiwa anaelekea nyumbani kwake akaona kuwa ni vyema ampigie pia huyo dada aliyeongea na Sabrina jana ila simu iliita bila ya kupokelewa akahisi kuwa amechukia kwa kitendo cha kuzimiwa simu.
Ikabidi aendelee tu na safari yake hadi nyumbani kwake na kumkuta mlinzi wake akiwa pale nje kama kawaida.
Sam akasalimiana nae na cha kwanza kabisa ni kumuuliza kuhusu mdada aliyempigia simu Sabrina kama alikuwa hapo,
"Mmh kwakweli sijamuona bosi, kuna muda nilizunguka nyuma labda ndio alikuja muda huo"
"Haya na hii gari hapa nje ni ya nani?"
"Hata sijui bosi, toka jana ipo hapo hapo. Nadhani ilikuja muda niliozunguka nyuma"
"Ila wewe Omary hujielewi jamani, sijui unafikiri kazi yako ni nini hapa"
"Nisamehe kaka"
"Haya fungua geti niingie"
Mlinzi akatoa funguo ila alivyosukuma geti akashangaa kuwa lipo wazi na kujiuliza kuwa ilikuwaje hadi akasahau kulifunga geti hilo.
Ikabidi tu waingie ndani ya geti hivyo hivyo kabla ya Sam kuanza kumgombeza tena.
Walipoingia walishangaa kumuona mwanamke akiwa chini chali na damu zikimtoka huku mkoba wake na vitu vingine vikiwa hovyo hovyo.
Sam alipomuangalia vizuri yule mwanamke aliona kabisa kuwa ni mwanamke anayemfahamu.

Sam alipomuangalia vizuri yule mwanamke aliona kabisa kuwa ni mwanamke anayemfahamu.
"Kheee Mungu wangu, huyu mwanamke amefikaje humu? Omary amefikaje huyu?"
"Hata mimi sijui bosi"
"Unaumuhimu gani wewe wa kuendelea kuwa hapa wakati kila kitu hujui? Tunafanyaje sasa? Si nilikwambia kuwa asiingie mtu humu ndani jamani!"
Mlinzi hakuwa na cha kujitetea na kumfanya awe kimya tu kwani kila kilichotokea alishangaa kuwa kilitokeaje na ndipo akakumbuka kile kitendo cha kumuona Jeff akitoka mule ndani huku akikimbia na hata alipomuuliza alikimbia zaidi na ni hapo alipoamua kumwambia Sam kuhusu Jeff,
"Kwahiyo hukumpata kumuuliza?"
"Alikimbia bosi, yani alikimbia utafikiri kaona kitu gani"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sam akafikiria kidogo cha kufanya na jinsi ya kuweza kumsaidia yule dada aliyeanguka pale kwahiyo akawa anajiuliza kama ampeleke hospitali au ampeleke kwa mganga,
"Hata sijui nielekee nae wapi kwakweli, eti nimpeleke kwa mganga au hospitali?"
"Mmh! Huu ni ushirikina bosi kwahiyo hata ukimpeleka hospitali ni kazi bure tu."
"Kwahiyo unashauri twende kwa mganga?"
"Ndio bosi"
"Unadhani kuna atakayenielewa wakati nimeshammaliza mwenzao? Ila ngoja najua cha kufanya, haya mambo yatakuwa sawa tu"
Sam akampita yule mwanamke pale chini na kwenda kufungua mlango wa ndani kisha akaingia ndani kabisa, mlinzi alibaki pale nje akishangaa tu kwani hakuelewa ni kitu gani kinamfanya Sam ajiamini kiasi kile kwani alionekana kutokuwa na uoga wowote na akajiuliza ni vipi ameweze kumuua yule mganga mashuhuri halafu yeye hajadhurika? Na vipi yale mambo ya ajabu yote yaliyotokea pale kwake ila bado anapata ujasiri wa kuingia ndani peke yake? Yule mlinzi aliwaza sana kwani hata yeye tu kwenda kumsogelea yule mwanamke pale chini hakuweza.

Ilipita kama nusu saa Sam akiwa bado ndani na kumfanya mlinzi wake apatwe na mashaka zaidi ila muda kidogo alimuona Sam akitoka ndani na akamuona yule dada akiinuka pale chini na kuwa kama akijishangaa hivi.
Sam alienda moja kwa moja kwa huyu dada na kumwambia,
"Pole sana Janeth"
Yule dada akamtazama Sam na kumkumbatia, ila alipoinuka na kumtazama yule mlinzi wa Sam ilikuwa bado kidogo aanguke tena,
"Vipi Janeth, huyu ni mtu wa kawaida tu"
"Ila ndio nilimkuta hapa chini akitokwa na damu"
Mlinzi wa Sam akashtuka na kuuliza na yeye tena kwa mshangao,
"Ulinikuta mimi nipo chini natokwa damu? Jamani mbona makubwa haya!"
"Ndio nilikukuta wewe na nilipokufata chini ukanikaba na sikumbuki kilichoendelea hadi sasa"
"Wee mdada utakuwa umechanganyikiwa sio bure, sisi tumekushangaa wewe hapa ulikuwa chini unatokwa na damu halafu saivi imekuwa ni mimi loh"
"Ni wewe ndio na nguo zako hizo hizo"
Sam akaona pale mlolongo utakuwa mrefu sana na kuamua kuokota mkoba wa huyu dada kisha kutoka naye nje.
"Kwahiyo na hii ndio gari ulilokuja nalo?"
"Ndio Sam ila nikapatwa na mabalaa"
Akafikiria kidogo na kuuliza,
"Halafu huku nilikuja jioni mbona saa hizi ni kama bado asubuhi?"
Sam hakutaka kumuelewesha kwa muda huo zaidi ya kumsaidia kupanda kwenye gari tu.
Kisha akamwambia yule mlinzi wake,
"Nitamtuma dereva aje achukue hii gari ya nje, ila tafadhari usimruhusu mtu yoyote kuingia hapo kwa kipindi hiki"
"Sawa bosi nimekuelewa"
Sam akapanda kwenye gari ya yule mdada kisha wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa yule mdada.

Jeff alikuwa na furaha sana siku ya leo ukizingatia kuwa hata ile asubuhi Sabrina alimpigia simu na kumuhakikishia kuwa wapo salama kabisa huku akitamani kwenda kuwaona ila Sabrina alikaa kumuelekeza kwani alihofia pale endapo Sam atagundua swala hili kwahiyo yeye swala la kuwasiliana nae tu lilikuwa ni kheri kwake kwahiyo wakakubaliana kwenda siku atakayopelekwa na Sam.
Muda huu Jeff alikuwa chumbani kwake tu akitafakari hatma yake na Sabrina, ndipo alipopigiwa simu na Aisha.
"Mambo Jeff"
"Poa tu, mbona asubuhi asubuhi"
"Nimekumiss Jeff, huwezi amini ila usiku nimekuota"
"Sawa basi tutaongea badae"
Jeff akakata ile simu kwani hakutaka kuweka mazoea ya karibu sana na Aisha kwani aliona dalili zake hazipo sawa kabisa.
Akaenda zake kuoga na kutoka pale ndani kwao kwa kumuaga mama yake,
"Haya, mi siku hizi sikuulizi maana ushakuwa mtu mzima"
Jeff akacheka tu na kuondoka zake.

Sam alienda hadi nyumbani kwa yule dada,
"Hapa ndipo nilipofikia Sam"
"Kwanza umerudi lini Janeth?"
"Nimerudi juzi"
Kisha akafikiria kidogo na kumuuliza Sam,
"Kumbe Sam umeoa!"
"Nimeoa? Nani kakwambia huo upuuzi?"
"Mmh jamani!"
Kisha akamsimulia majibu aliyopewa jana alipopiga simu.
"Huyo mtu mzushi bhana, mi wala sijaoa."
"Yani nikabaki na mshangao kuwa Sam umenisaliti kweli! Sasa nimeamini kuwa bado unanipenda"
"Ndio Janeth, nakupenda sana. Vipi mzigo umefika nao salama?"
"Tena zaidi ya salama, kwani nimefika na mzigo wote safari hii"
"Wow, ubilionea huo"
Sam akamkumbatia huyu dada kwa furaha.
"Tena leo usiondoke humu, nataka unipe kile ulichoniahidi kwa kipindi kirefu"
"Kipi hicho Janeth?"
Huyu dada akasogea na kuwa kamavile anamnong'oneza Sam,
"Penzi lako"
Hilo neno lilimsisimua sana Sam ila hakutaka kufanya ubaya kwa siku hiyo,
"Kwanini tusifanye siku nyingine Janeth wangu?"
"Mimi nataka leo, yani tusipofanya kwakweli sitakupa ule mzigo"
Sam akafikiria kwa muda kidogo kuhusu swala hilo na kuona wazi kuwa huo mzigo ni wa muhimu sana kwake kuliko maisha ya huyu dada.
"Hilo sio tatizo Janeth, mi wala sitaondoka humu. Nionyeshe basi huo mzigo wenyewe"
Janeth akainuka na Sam kwenda kumuonyesha huko alipoficha mzigo huo.
"Kheee kweli wewe Janeth ni khatari, yani umeweza kuficha mzigo wote huo?"
"Ndio, yani nilikuwa natumia akili sana katika kusafirisha mzigo huo Sam, huwezi amini kwa akili niliyotumia hapo ndiomana nimekawia kurudi."
"Hadi mie nilikata tamaa kuwa utarudi Janeth nikahesabia kuwa nimepata hasara tu ila umefanikisha Janeth. Nashukuru sana"
Wakafurahi sana kwa pamoja kisha wakarudi walipokaa mwanzo "Na hapa unapoishi ni kwa nani?"
"Nimekodi hapa, nimelipia pesa kiasi kwani najua bosi wangu upo utalipa tu sina shaka kwa hilo"
Sam akatabasamu tu na kusema,
"Hakuna tatizo, nitalipa tu Janeth hata usijali"
"Ile pesa uliyonitumia kipindi kile ndio nikanunulia hiyo gari"
"Hapo ulifanya jambo la akili sana na nitakupa na gari nyingine"
Janeth akafurahi sana na kusahau yote yaliyomkuta nyumbani kwa Sam kisha akainuka na kwenda kuoga kwanza.

Sabrina akiwa pale nyumbani akasikia honi ya gari, moja kwa moja akajua ni Sam amerudi.
Akaenda kufungua geti na gari ikaingizwa ndani na ilikuwa gari ambayo Sam aliondoka nayo asubuhi.
Ila gari iliposimama, aliyeshuka hakuwa Sam bali alikuwa ni kijana mmoja ambaye alishuka na kumsalimia Sabrina kwanza ila kabla Sabrina hajaitikia ile salamu akaulizia kwanza alipo Sam,
"Kwani Sam yuko wapi?"
"Sijui mama, mi alinipigia tu simu kuwa nikachukue gari yake kule nyumbani kwake na kunielekeza niilete huku"
"Mmh makubwa haya, sawa basi nashukuru"
Yule kijana akaondoka zake na kumuacha Sabrina akijiuliza kuwa Sam kaenda wapi na kujiambia kuwa huenda ameamua kwenda na gari nyingine.
Alirudi tu ndani na kucheza na wanae huku akibonyeza bonyeza simu yake.
Akajiwa na kumbukumbu ya namba ya Francis na kuamua kumpigia ila ile simu ilipokelewa na mdada,
"Samahani, namuomba mwenye simu"
"Mwenye simu mimi ni mkewe kwahiyo unaweza ukaniachia maagizo yake"
"Kumbe Francis kaoa?"
"Ndio, ulitaka kumnyemelea? Kaoa na tuna mtoto tayari, kaa huko usitake kunivunjia ndoa"
"Mmh sikuwa na maana mbaya dada, akija mwambia Sabrina nilimpigia nimsalimie"
Kisha Sabrina akakata ile simu na kujiona kuwa hata yeye anamakosa kumfokea yule mdada wa jana aliposhangaa kuwa Sam kaoa,
"Inawezekana nae alikuwa kama mimi kutokujua kuwa Francis kaoa ingawa Fredy alishawahi kuniambia kuwa Francis ana mwanamke. Ila yule dada wa jana nae hakuwa na kauli nzuri kwangu"
Akakumbuka siku ya kwanza kukutana na Francis kwani alikuwa ndio mwanaume wa kwanza kuvutiwa nae na alikuwa wa kwanza kumfanya ayaone mapenzi machungu.
Akamtafakari sana kisha akaendelea na shughuli zake zingine.

Sam nae hakuwa na ujanja wa kuondoka zaidi ya kumsubiria huyo Janeth, na alipotoka tu bafuni akaenda moja kwa moja alipo Sam huku kajifunga khanga yake tu yenye maji maji.
Sam akaona isiwe shida na akaona ni vyema amalizane nae tu kisha akawatafute wadada wengine ili atimize lengo lake.
Janeth nae alijikoki haswaa akitaka kufaidi penzi la Sam, ila Sam bado alikuwa anasita,
"Kwanini unanifanyia hivyo Sam jamani? Kwanini hutaki kunipa mimi?"
Janeth aliongea hayo kwa sauti ya hamasa na huku akimsogelea Sam na kuanza manjonjo yake ili kumvutia zaidi na kweli Sam naye akavutia, na pale mambo yalipokuwa sawa Sam alimuomba Janeth ageuke ili atimize lengo lake na alipogeuka tu alipiga kelele zisizokuwa na kifani kisha akazimia ila Sam hakumuachia hadi alipomaliza haja yake ndio akamuweka vizuri sasa huku akimuhurumia kuwa ataenda na maji.
Alivaa vizuri nguo zake na kumfunika vizuri Janeth huku akimpa pole.
Kisha akamuinua na kwenda kumpeleka chumbani na kumlaza kitandani kwani hakutaka kumzindua kwa muda huo kwanza mpaka abebe mzigo wake.
Akakaa pale na kumpigia simu kijana wake mkubwa wa biashara hiyo na akamuelekeza pale.
Yule kijana alipofika akapewa ule mzigo na kama kawaida akapeleka sehemu husika wanapotunzia malighafi zao hizo.

Alipoondoka yule mtu sasa ndipo Sam alipoenda na glasi ya maji na kummwagia mwagia Janeth ili azinduke, naye akazinduka na kukaa pale kitandani na kujishangaa kidogo, kumbukumbu nazo zikamrejea huku akisikilizia maumivu makali ya sehemu za siri na kujikuta akilia tu.
"Unenifanya nini Sam? Mbona umenifanyia kitu kibaya sana jamani"
"Nisamehe Janeth, sikutaka kukufanyia hivyo ila ni wewe mwenyewe umelazimisha nikufanyie hivyo. Tafadhari nisamehe sana"
"Umenifanyia dhambi Sam, hapa penyewe nimekufa halafu wewe unaniua tena jamani kwanini umenifanyia hivi? Umenitumia kwa biashara zako na nimefanya bila kinyongo yani fadhila zake ndio kifo?"
"Hapana Janeth, usimwambie mtu nitahakikisha unapona"
"Napona nini wakati umeniongezea tatizo juu ya tatizo, mimi hapa nilipo ni muathirika"
"Kheee ni muathirika? Kwahiyo umenipa mimi ukimwi?"
"Ndio lakini hata hivyo wewe umeniumiza"
Sam akachukia kusikia kuwa yule dada ameathirika na kujikuta akiongea kwa hasira,
"Kwahiyo lengo lako lilikuwa ni kunimaliza mimi kwa ukimwi Janeth? Haya nashukuru kwa ukimwi ulionipa ila huu nitakufa taratibu tofauti na wewe"
Kisha Sam akainuka na kuondoka kabisa.
Janeth akabaki peke yake huku akiugulia maumivu yale.

Sam aliamua kuchukua gari ya kukodi ambayo ilimpeleka moja kwa moja kwenye nyumba yake ya awali kisha akashuka na kama kawaida yule mlinzi wake alikuwepo pale pale getini.
"Haya niambie kuna mauza uza mengine yaliyotokea wakati sipo?"
"Hakuna bosi"
Kisha Sam akaingia ndani na kutoka na gari yake nyingine, halafu akamwambia tena mlinzi wake.
"Narudia tena, usimruhusu mtu yeyote kuingia humu ndani. Sawa?"
"Sawa bosi"
Sam akaondoka huku akili yake ikicheza na idadi ya wasichana ambao anataka kukutana nao kwa siku hiyo ili kuondokana na lile tatizo lililopo kwenye nyumba yake.
"Natakiwa kukutana na wadada watano, Janeth kashawafungulia njia wenzie. Nilitaka kupuuza jambo hili ila huyu Janeth kaniudhi leo na kwavile ameanzisha sina budi kumalizia. Kwahiyo yeye tayari, bado wanne sasa."
Moja kwa moja akaenda baa ya kwanza na kubahatika kumshawishi muhudumu kwa pesa yake kwahiyo akaondoka nae na kwenda nae hotelini huko akamuachia maumivu kama aliyoyapata Janeth kisha akampa pesa na kumwambia asiseme.
Sam alitoka hapo na kumuacha yule dada akilia tu kisha yeye akaenda kwenye baa nyingine ili akutane na mwingine, na alipomaliza hapo akaenda nyingine kwa lengo lile lile huku akijiambia kuwa,
"Mchezo kama huu niliufanya miaka hiyo iliyopita, hatimaye leo imejirudia. Kwakweli lazima nitimize lengo langu"
Kwahiyo akafanya njia ile ile ya kushawishi wadada kwa pesa.

Sabrina alitulia nyumbani bila ya kupata mawasiliano yoyote toka kwa Sam, hadi giza linaingia hakutafutwa na Sam na kuamua ampigie simu,
"Ila Sam unachonifanyia sio sawa kabisa, yani wewe toka umeondoka asubuhi kweli hadi muda huu hata kunipigia simu jamani! Uko wapi sasa?"
"Usijali, narudi sasa hivi"
Kisha Sam akakata ile simu, na muda huo alikuwa ametoka kumliza mdada mwingine hotelini, na kuamua kurudi nyumbani kwake baada ya simu toka kwa Sabrina.

Sam alifika nyumbani kwake na kuingia ndani, akasalimiana na Sabrina pale kisha kuingia chumbani kwake ila kabla hajafanya chochote akakumbuka kuwa katika ile idadi ya wanawake watano kwa siku hiyo amekutana na wanne tu yani bado mmoja na kama akipitiliza siku basi kesho ataanza upya tena idadi itakuwa mara mbili ya siku ya leo.
Akawaza kuwa afanyaje sasa na wakati kasharudi nyumbani, akili nyingine ikamwambia kuwa kwanini huyo mmoja asimalize kwa Sabrina.
Hapo Sam akaamua kumuita Sabrina chumbani.

Akawaza kuwa afanyaje sasa na wakati kasharudi nyumbani, akili nyingine ikamwambia kuwa kwanini huyo mmoja asimalize kwa Sabrina.
Hapo Sam akaamua kumuita Sabrina chumbani.
Sabrina aliyekuwa akimaliza kuwaandaa watoto wake ili walale vizuri, akaamua kuitii ile sauti ya Sam iliyomuita na kuinuka ili aende ila huyu mtoto mdogo akawa analia akaamua kumuweka begani na kwenda nae.
Alimkuta Sam amekaa kitandani ambapo swali la kwanza aliloulizwa Sabrina lilikuwa ni kuhusu mtoto,
"Huyo bado hajalala mpaka muda huu?"
"Ni leo tu ndio kachelewa kulala"
"Haya, niambie na leo utalala chumba gani?"
"Kule naona kumekaa vizuri zaidi"
"Kwahiyo na mimi nije kulala huko?"
Sabrina hapo akakaa kimya bila ya jibu, kisha Sam akamuuliza tena,
"Nini maana ya mke Sabrina?"
"Mke ni mwanamke aliyeolewa na anakuwepo kwa dhumuni la kumsaidia mumewe kwa kila kitu kama kupika, kufua, kuosha vyombo na mengineyo"
"Bado hujajibu swali langu Sabrina, ni kwanini mwanaume anaamua kuwa na mke ndani?"
"Ili amsaidie hizo kazi"
"Ngoja nikuulize tena, inamaana mwanaume akiwa mwenyewe hatoweza kupika? Kufua na kuosha vyombo? Au mwanaume hawezi kumuajiri mtu kwaajili ya kufanya kazi hizo hadi aoe? Je maana ya kuolewa ni kwenda kumpikia mume, kuosha vyombo na kufua tu? Nini maana ya ndoa? Kwanini watu wanaamua kufanya hivyo?"
Moja kwa moja Sabrina akatambua kile ambacho kinamaanishwa na Sam kwa wakati huo na kujikuta hata akishindwa kumjibu kwani alijua wazi kuwa ni kigumu kwake.
"Mbona kimya tena Sabrina? Wewe ni mke wangu si ndio?"
Sabrina akaitikia kwa kutikisa kichwa, Sam akainuka na kumsogelea Sabrina kisha akamshika bega na kumwambia,
"Hata mchungaji siku ya ndoa alikiri kuwa hawa si wawili tena bali wamekuwa mwili mmoja. Sabrina unatakiwa kunipa haki yangu kama mume wako tena wa ndoa kabisa"
Sabrina aliinama na machozi yakamtoka na kumuangukia mtoto aliyekuwa amembeba ambapo Sam akamsogelea karibu na kumkumbatia, kisha akamwambia
"Kamlaze mtoto Sabrina unipe haki yangu"
Ni hapa ambapo Sabrina akaamini kuwa Sam anamaanisha kile anachokisema ukizingatia alikuwa akisisitiza kabisa.

Sabrina alitoka mule chumbani na mwanae huku akielekea chumba kingine, alimuangalia mwanae aliyekuwa akilia bado na kumuweka pembeni kisha na yeye kukaa kitandani na kujikuta akitokwa na machozi mfululizo.
Moyo wake ulibeba mzigo ukubwa sana wa maumivu huku akiwahurumia watoto wake na kujua wazi yale aliyokuwa anasema kwamba wanawake wanaponzwa na tamaa basi na yeye ameangukia kwenye kundi hilo la wenye tamaa kwani kama angebaki kwao basi yasingemkuta hayo ukizingatia anaujua ukweli wote kuhusu Sam ila kingine akawaza kuwa kama angebaki kwao bado ingekuwa ni ngumu sana kwake kujieleza kwa mama yake.
Sabrina alilia sana bila ya kujua cha kufanya kwa wakati huo, na mtoto wake naye alikuwa akilia hata yule aliyemlaza sebleni yani Cherry naye aliamka na kuanza kulia.

Sam alitoka hadi sebleni na kumkuta Cherry akilia ambapo Cherry alipomuona Sam alishuka pale kwenye kiti na kumfata Sam ili ambebe ambapo Sam alimnyanyua mtoto yule na kumuweka begani.
Siku zote Sam alikuwa na upendo sana kwa huyu mtoto Cherry, alijikuta akimpenda kama mwanae wa kumzaa kabisa na kile kilio chake cha kutoka usingizini ndicho kilichomsononesha na kumfanya ambebe huku akimbembeleza.
Akajikuta pia akisikia sauti ya kilio cha yule mtoto mdogo wa Sabrina ila haikumuumiza kama sauti ya Cherry ilivyomuumiza.
Akiwa amembeba Cherry begani, Sam akaenda nae chumbani alipo Sabrina na kumkuta akiwa kajiinamia akilia.
Sam akamtua Cherry kwenye mikono ya Sabrina na kumwambia,
"Mpende sana huyu mtoto"
Kisha akawaacha pale na kutoka, na aliondoka kabisa kwa muda huo kwani Sabrina alisikia tu mlio wa gari ya Sam likitoka.

Sabrina akajifuta machozi sasa na kuanza kuwabembeleza watoto kwanza kwani wote wawili walikuwa wakilia.
Alimuangalia sana Cherry na kutokuelewa kuwa kwanini Sam anampenda sana mtoto huyo kwani alihisi kuwa ndio aliyemsaidia kusamehewa na adhabu ya Sam.
Ingawa ilikuwa ni usiku, Sabrina hakutaka hata kufikiria alipoenda Sam kwani alichofikiria kwa muda huo ilikuwa ni kuhusu yeye na watoto wake tu. Akili ya haraka haraka ikamjia kuwa atoroke pale nyumbani kwa Sam huku akijiwazia kuwa ataondokaje kwa usiku huo? Akaona jambo rahisi ni kuwasiliana na Jeff na kumuelekeza hata maeneo ya yeye alipo ila tatizo lilikuwa kwamba lile eneo bado mgeni kwahiyo hakulijua vizuri na kumfanya kufikiria hata uwezekano wa kupata labda gari ya kukodi.
Vyote vilikuwa ni vigumu kwake na kumfanya aone vyema kupiga simu kwa Jeff tu na muda huo huo akachukua simu yake na kumpigia Jeff,
"Nina matatizo Jeff "
"Matatizo gani tena?"
"Naomba tuonane halafu nitakueleza tatizo langu"
"Tuonane muda huu Sabrina? Tuonane wapi?"
"Ngoja nitakwambia, subiri nipate gari ya kukodi"
Kisha Sabrina akakata ile simu.
Akawaandaa watoto wake, mmoja akambeba mgongoni na mwingine akamshika mikononi kisha akaanza kuondoka.
Alipofika mlangoni ili afungue mlango akashangaa ni mgumu, alipoujaribisha tena akagundua umefungwa kwa nje,
"Sam kanifungia mlango nadhani alikuwa na wazo langu kabla yangu"
Ikabidi arudi na kukaa kisha akaona vyema kuwa bora aende chumbani tu kulala na watoto kwani hapakuwa na namna nyingine.

Jeff alikuwa na mshangao tu na kubaki na maswali kuwa Sabrina kapatwa na nini kwa wakati huo ila alitulia kwa muda bila ya Sabrina kupiga simu tena wala kusema kinachoendelea kwa wakati huo, hivyobasi akaamua kumpigia simu yeye mwenyewe ili amuulize vizuri,
"Sabrina mbona kimya tena, kwani tatizo ni nini?"
"Tatizo ni Sam kafunga mlango"
"Kivipi? Kwani Sam yuko wapi?"
"Sijui alipo ila usijali, nikipata nafasi tu nitakueleza kilichotokea"
"Kwanini usinieleze sasa hivi Sabrina? Nieleze tu, kwani kuna tatizo gani?"
Sabrina aliamua kumueleza Jeff kwa kifupi kile kilichotokea,
"Unaona sasa Sabrina mama angu, huko unajitafutia makubwa tu yani. Huyo Sam si mtu mzuri na anaweza kukugeuka na wewe kama alivyowageuka hao. Ingawa sijui chochote kuhusu Sam ila ile barua ya Neema ilijieleza kila kitu"
"Usitaje jina hilo Jeff"
"Jina gani? Neema au?"
"Ndio hilo hilo usilitaje, ile nyumba ya mwanzo balaa zote zililetwa kwa jina hilo"
"Haya tuachane na yote hayo halafu tuangalie cha kufanya sasa baada ya hayo yaliyotokea"
"Sijui cha kufanya, nishauri chochote tu Jeff"
"Mmh ningekuwa napajua huko ingekuwa rahisi, ila ngoja na mimi nifikirie cha kufanya"
"Sasa itakuwaje? Naangamia mwenzio huku ujue"
Mara akasikia muungurumo wa gari na kujua kwa vyovyote vile Sam amerudi tayari na kujikuta akikata simu kwa uoga akihofia kumkera zaidi.

Sam aliingia ndani kwake na moja kwa moja akaenda chumbani kwake kulala huku akifikiria alichokifanya muda mfupi uliopita na yote aliyoyafanya kwa siku hiyo.
"Ni kweli nimefanikisha malengo yangu ila hiki nilichokifanya mwishoni sijakipenda kwakweli. Sam mimi nitakuwa na dhambi ngapi? Ni wangapi wamelia sababu yangu? Ni wangapi wameteseka, kwanini nimekuwa hivi mimi?"
Alijisikitikia ila ndio tayari alishatenda matendo ambayo hayafai kabisa katika jamii.
Sam alijifikiria sana na bado kile kitendo alichokifanya mwishoni kilisumbua akili yangu na kumfanya asikitike sana kwani huwa hapendi kuwaumiza mabinti wadogo na kwa siku hiyo ndio alichokifanya katika harakati zake za kuhakikisha kuwa anatimiza kile alichoamriwa.
Sam hakuweza kulala kabisa sababu ya mawazo na kumfanya aamue kuchukua vinywaji vyake vikali na kunywa ili tu kutuliza mawazo.

Jeff akajaribu tena kupiga namba ya Sabrina ila haikupokelewa kwavile Sabrina alishamweleza kuhusu kilichotaka kumpata akajikuta akiwa na hofu juu ya hilo na jambo la haraka kwake kwa wakati huo aliona ni bora aende tena kule kwa Sam kwa zamani akamuulize yule mlinzi ingawa alishakutwa na majanga ila alijipa moyo hivyo hivyo kuwa lazima akapate jibu ukizingatia tayari ameshajua kuwa ile nyumba ina matatizo gani.
Kwahiyo Jeff akaamua kutoka nyumbani kwao na kumuaga mama yake,
"Jamani Jeff usiku huu!"
"Kuna vitu naenda kushughulikia mama"
"Hata kama sio kwa usiku huu Jeff"
"Mama, mimi ni kijana mkubwa sasa na nina mishe nyingi tu ndiomana kuna kipindi nilikwambia kuwa nikapange ila ukasisitiza niendelee kuishi hapa basi niachie uhuru mama yangu. Najielewa na ninatambua ninachokifanya mama. Usiwe na mashaka yoyote juu yangu"
Sakina hakuw na neno zaidi ya kumruhusu tu mwanae afanye anachotaka, kisha Jeff akatoka na kuondoka.

Jeff alienda hadi stendi ila kwa muda ule ilikuwa ngumu kidogo kupata usafiri wa daladala hivyobasi akaamua kusogea kwa madereva wa bodaboda na kukodi moja wapo ili imfikishe mahali angalau apate daladala, lakini walipokuwa njiani wakamuona dada mmoja akiwa amekaa pembezoni mwa barabara huku akilia.
Huruma ikamshika Jeff na kumfanya amuombe yule dereva wa bodaboda asimamishe ili aweze kumuhoji maswali yule dada ila dereva wa bodaboda alionekana kuwa na harakati za kuwahi abiria wengine,
"Utaniongezea pesa kaka"
"Ila mbona nyie mpo hivyo jamani yani unajali pesa kuliko utu!"
"Nipo kutafuta pesa hadi usiku huu na kama ningejali utu basi ingekuwa nimelala muda huu"
"Basi nitakuongezea hiyo pesa"
Jeff akashuka na kumfuata yule dada, alipommulika na mwanga wa simu yake alimuona wazi kuwa yule dada bado ni mdogo sana hata akamshangaa kwa usiku ule,
"Umekumbwa na nini binti?"
Huyu dada alilia tu na alishindwa kujibu, Jeff akamuomba ainuke nae ili aende nae kwao.
Ila yule binti alipoinuka, sketi yake ilionekana kulowa damu na kumfanya Jeff aulize tena
"Kwani umetoa mimba"
"Hapana"
Huyu binti alijibu huku akilia.
Jeff akamuomba mwenye bodaboda ili wapande pamoja na yule binti,
"Itabidi uniongezee hela tena maana haturuhusiwi kupandisha mishikaki"
"Nimekwambia hakuna shida nitakuongezea tu"
Jeff akapanda na yule binti kisha wakaanza safari ya kurudi kwao na kusahau kabisa kilichomtoa kwao kwa usiku ule ni nini kwani alijikuwa na huruma iliyopitiliza dhidi ya yule binti.

Sabrina alikuwa ndani katulia kabisa akiogopa hata kupokea simu aliyokuwa anapigiwa na Jeff kwani alijua wazi kama Sam akimsikia basi ataamua kufanya kitu chochote kile hata kama ameghairi kwahiyo kwa wakati huo akaona ni vyema alale kabisa na kuzima simu yake kabisa.

Jeff alifika nyumbani kwao na kushuka na yule binti, akamlipa pesa dereva wa bodaboda kisha yeye na yule binti kuelekea ndani kwao ambao Jeff aligonga kwanza mlango na mama yake kwenda kufungua.
Sakina akamshangaa Jeff akiwa ameambatana na yule binti,
"Vipi tena jamani?"
"Nimemkuta huyu binti njiani mama, anaonekana kuwa na shida nikaamua kumsaidia"
Kwa jinsi yule binti alivyokuwa ikambidi Sakina atoe khanga yake na kumfunika kisha kumuongoza bafuni akaoge na aweze kuwaeleza vizuri.
Alipomaliza kuoga, Jeff akapendekeza waongee nae kesho kwani ni usiku sana na wangemuacha apumzike tu ambapo Sakina aliafiki hilo na kumpeleka chumba cha kulala wageni ili apate kupumzika kwa usiku huo kisha Jeff nae akaenda chumbani kwake na alipojaribu kuipiga simu ya Sabrina haikupatikana tena ila akaona ni vyema swala la Sabrina ashughulike nalo pia kesho yake,
"Najua kama Sabrina kapatwa na tatizo basi atatokea msamalia mwema wa kumsaidia kama mimi nilivyomsaidia binti huyu."
Kisha akaamua kulala tu.

Kulipokucha kwa upande wa Sabrina, aliamka na watoto wake kama kawaida na alipotoka sebleni alimkuta Sam yupo pale sebleni amekaa tu.
Sabrina akamsalimia ila Sam hakuitikia na kumfanya Sabrina ahisi kwamba kaamua kumchunia tu.
Kisha akawakalisha wanae na kwenda kuwaandalia chakula, akarudi na kuwalisha ila bado Sam alikuwa kakaa vile vile na kumfanya Sabrina apatwe na uoga kidogo kwani si kawaida ya Sam kabisa.
Sabrina alipomalizana na wanae akaamua kumfata tena Sam pale kwenye kiti ili amuulize kilichomsibu,
"Sam mbona upo kimya sana?"
Sam hakujibu, na kumfanya Sabrina ajaribu kama kumuinua kichwa Sam alimshangaa akiwa ametoa tu macho na wala hayazunguki.
Sabrina uoga ukamjaa zaidi, na alipomuachilia kile kichwa akashangaa akianguka kwenye kochi.

Sam hakujibu na kumfanya Sabrina ajaribu kama kumuinua kichwa Sam alimshangaa akiwa ametoa tu macho na wala hayazunguki.
Sabrina uoga ukamjaa zaidi, na alipomuachilia kile kichwa akashangaa akianguka kwenye kochi.
Kitendo kile bado kidogo kimfanye Sabrina akimbie kwani mule ndani watu wenye utambuzi wao ni wawili tu yani yeye na Sam halafu Sam ndio huyo kapatwa na tatizo, hakujua afanye nini na kuona akili yake ikichanganyikiwa kwani Sam alikuwa kamavile mtu aliyekufa kabisa.
Sabrina alikaa pembeni akijiinamia kwani hakujua kitu cha kufanya kwa muda huo.
Wakati Sabrina akiwa amejiinamia, yule mtoto wao Cherry aliinuka alipo na moja kwa moja akaenda alipo Sam na kumfanya Sabrina atake kumkataza kwani alimuona akiinuka na kuelekea kwa Sam ila roho nyingine ilimwambia amuache ili aone kuwa yule mtoto anaenda kufanya kitu gani.
Cherry alipomfikia Sam, akawa kama anamgusa usoni ila mikono yake ikaelekea kwenye pua ya Sam na gafla Sam akainuka na kupiga chafya kama mara tatu kisha akamtazama Cherry na kutabasamu ambapo Cherry nae alikuwa akitabasamu kisha Sam akamnyanyua mtoto yule na kumuweka miguuni mwake.
Sabrina alikuwa akishangaa tu hiki anachokiona kwa muda huu kwani hakukielewa kabisa ila Sam alionekana kawaida kamavile hakuna kitu chochote kilichotokea kwake.
Ni hapa sasa Sabrina alipoamua kuvunja ukimya na kuuliza,
"Sam una tatizo gani?"
"Tatizo? Kivipi?"
"Unajua hali niliyokukuta nayo haikuwa ya kawaida kabisa ila hapo unaonekana upo kawaida tatizo ni nini?"
"Kwani umenikuta na hali gani?"
Ikabidi Sabrina amueleze alivyokuwa na jinsi Cherry alivyomsogelea, ila cha kumshangaza Sabrina ni kuwa Sam hakuzungumzia ile hali bali alifurahia kitendo cha Cherry tu,
"Ooh wow, ndiomana nakapenda haka katoto jamani. Badae nitamletea zawadi yake, mtoto ana akili sana huyu ndiomana nikampa hili jina"
Sam alikuwa na furaha tu kisha akainuka na kumuweka Cherry halafu yeye akaenda chumbani kwake na kumfanya Sabrina abaki na maswali tu bila majibu yoyote yale.

Kwa upande wakina Jeff ilikuwa tofauti kidogo kwani iliwabidi wawahi kuamka kutokana na sauti ya kilio iliyotoka kwa yule binti wa usiku.
Sakina aliona ni vyema wamuhoji huyo binti kisha wampeleke kwa mjumbe kwavile kulishaanza kupambazuka tayari.
"Kwani binti unaitwa nani?"
"Naitwa Amina"
"Nini kimekupata? Kuwa wazi ili iwe rahisi kwetu kukusaidia"
"Ona damu zinavyonitoka na sehemu za siri zinaniuma nalia kwa uchungu ila nimeambiwa nisiseme"
"Usiwe muoga binti, napenda kujua tatizo ni nini na kwanini upo hivyo ili nijue jinsi ya kukusaidia"
Sakina alikuwa akimbembeleza binti huyu ili aongee kinachomsibu, Jeff nae alikuwa pembeni akisikiliza kwa makini kwani huruma yake kwa yule binti ilikuwa ya hali ya juu.
Sakina aliendelea kumbembeleza yule binti ili aseme ukweli wa kilichomsibu,
"Amina, hata usiwe na mashaka sisi tunataka useme ukweli halafu tujue tunaanzia wapi kukusaidia"
"Ni hivi jamani, mimi nilikuwa na wenzangu tulienda disko yani kwa mara ya kwanza katika maisha yangu kwenda disko hata nyumbani hawajui kama nilienda huko. Wakati tumetoka disko tukajikuta hatuna pesa kabisa ya kuweza kupata usafiri wa kurudi nyumbani ndipo wenzangu wakatoa ushauri kuwa tuombe lifti. Tukakubaliana hilo na kwenda barabarani kusimamisha gari za kuomba lifti cha kushangaza tulipofika barabarani kuna gari ikaja wenzangu wakapanda na kuniacha peke yangu nilishtukia tu hawapo hapo ndio nikachanganyikiwa zaidi kuona Asha na Rose wameniacha mwenyewe ikabidi nami nisimamishe gari kweli likasimama na nikamuomba lifti akakubali ila wakati nipo kwenye gari yake alinirubuni na kuniingila kimwili....."
Hapo alinyamaza na kuangua kilio tena,
" Jamani pole sana binti yani alikubaka?"
"Ndio, na bora kama angekuwa mwanaume wa kawaida ila alikuwa ni jini"
Na kulia tena, Sakina akashikwa na huruma pia kwa huyu binti kwani siku ya kwanza kufanya makosa ndio siku hiyo hiyo akakutana na mabalaa.
"Pole sana, kwahiyo hakuwa mtu alikuwa ni jini! Mungu wangu, ulijuaje sasa kama ni jini?"
"Alipokuwa ananiingilia, maumbile yake yalibadilika na kuwa na miba yani bila huruma akaniingilia hivyo hivyo"
Sasa Amina alizidisha kilio zaidi tena kilikuwa kilio cha kwikwi hata Sakina nae machozi yakamtoka kwani aliweza kuhisi ni maumivu gani yule binti kayapata alipokuwa anaingiliwa kimwili na huyo mtu, alijikuta akimuhurumia sana kwani kwa yale maelezo tu hata yeye mwenyewe alihisi kuumia.
Yule binti aliendelea kuelezea huku akilia,
"Nililia sana na kupiga makelele ila hakunionea huruma kwakweli yani hakunionea huruma kabisa. Na alipomaliza akapeleka gari yake mbele na kunishusha kisha akaniambia kuwa usimwambie mtu yoyote na kunitupia pesa chini kisha akaondoka. Muda ule ule nikiwa nalia wakatokea vijana wawili vibaka na kunipora kila kitu na kuniacha pale nikilia. Sijui mimi nitawaeleza nini wazazi wangu jamani"
Amina alikuwa akilia tu, Sakina akamsogelea karibu kama kumbembeleza na kumlaza kifuani mwake kwani alikuwa akilia sana ila gafla waliona kimya na hakutoa sauti yoyote wakajua kuwa amenyamaza sasa,
"Pole sana Amina"
Jeff nae akaongea kwa masikitiko,
"Inaumiza sana hii hacri jamani ila atapona tu Mungu atamsaidia jamani"
"Na bora kanyamaza sasa"
Kisha Sakina akamuangalia yule binti pale kifuani pake na kumwambia,
"Usijali binti, mimi nitakutetea kwa wazazi wako. Kwani wanaishi wapi?"
Sakina akashangaa kimya yani yule binti hajibu tena na wala halii tena,
"Vipi amelala au"
"Hata sijui"
Kisha Sakina akawa anamuweka pembeni kwa kumuita, ila alivyokuwa anamuweka akashangaa kumuona kalegea kabisa yani wala hatingishiki tena,
"Mungu wangu, nini hiki?"
Sakina aliinama na kusikiliza mapigo ya moyo ya yule binti ila hakuyasikia na kumfanya agundue kuwa yule binti hapumui tena.
Sakina akajikuta akirukia pembeni,
"Inamaana amekufa?"
"Nini mama amekufa?"
"Ndio, hebu muangalie kwanza"
Sakina alihisi kuchanganyikiwa sasa, Jeff aliinama na kumsikilizia yule binti naye akagundua kuwa amekufa,
"Khee mama tutafanyaje sasa?"
"Kwakweli sijui tutafanyaje maana hapa nilipo hata akili imenipotea"
Walijikuta wakimuangalia mara mbili mbili yule binti bila ya kujua wafanye nini.

Sam alipotoka chumbani kwake akamwambia Sabrina,
"Sitaki utoke humu ndani ndiomana unaona kuwa nilikwambia kama kuna msichana wa kazi atakuwa anakuja ila hujamuona hadi leo kwavile nimemsitisha kwa muda. Najua hapo ulipo unamawazo ya kutoroka ila usiwe na wazo hilo ukiwa na mimi"
Sabrina alikuwa kimya akimsikiliza tu Sam kwa anachoongea,
"Jana nilitingwa na ndiomana nikafikia hatua ile Sabrina ila kwakweli mimi siwezi kukufanyia chochote kibaya yani siwezi kabisa ila jana nimefanya dhambi sana"
Hapa ndio Sabrina akauliza kuwa ni dhambi gani ambayo Sam anaiongelea,
"Kwani umefanya dhambi gani Sam?"
"Ngoja nikwambie ukweli Sabrina ingawa bado sijakumalizia historia kuhusu mimi na kwanini nimefikia hatua ya kufunga ndoa na wewe"
Sam akakaa kimya kidogo na kuwa kama mtu anayefikiria jambo ambapo wakati huo Sabrina nae alitulia kabisa akimsikiliza Sam.
"Niambie basi huo ukweli"
"Jana nilipatwa na matatizo Sabrina, unajua yule mzee kule nyumbani kwangu bado ananisumbua"
"Mzee gani?"
"Yule mganga au umemsahau?"
"Namkumbuka, si ulisema kuwa unaenda kumaliza kiburi cha yule mzee wewe!"
"Ndio nilimaliza kiburi chake"
"Ulikimalizaje sasa na jana amekusumbuaje?"
"Yule mzee nilimuua na ....."
Sabrina akashtushwa sana na hii kauli ya Sam kuwa alimuua yule mzee tena alimshangaa Sam kwa kuongea vile tena kwa ujasiri kabisa,
"Sasa mbona unashtuka? Inambna hujawahi kusikia mtu kauwawa au ni vipi?"
"Hapana nimeshangaa tu kwani sikujua kama tatizo ungelimaliza kwa kumuua yule mzee kwahiyo ulimuua vipi?"
"Kwani wengine wanaua vipi? Mi nilimpiga risasi tu na ukawa mwisho wa habari yake"
Sabrina alibaki kutoa macho tu kwani aliweza kugundua kuwa Sam ni katili kwa kiasi gani ila hakutaka kujionyesha mshtuko wake kwa kuhofia kugeukiwa na yeye.
"Sasa ndio umemuua jana?"
"Sijamuua jana, ni siku kadhaa zimepita tangu nimuue ila cha kushangaza kuna matukio ya ajabu sana yanatokea pale nyumbani"
Sam akamueleza Sabrina kuhusu tukio la yule dada kutokwa na damu, na yale maelezo ya Sam yakamfanya Sabrina aelewe moja kwa moja kuwa huyo mwanamke ndio huyo aliyebishana nae majuzi yake na kumwambia aingie ndani.
Kwahiyo Sabrina alikuwa ametoa macho tu akimsikiliza Sam na yale maelezo yake, ambapo Sam aliendelea kuelezea kwa alichokifanya jana sasa,
"Niliona hali itazidi kuwa mbaya ukizingatia nataka kuuza ile nyumba, ikabidi niingie ndani kwanza ili nikaongee na malaika wangu"
Hapo napo Sabrina akashangaa ila akaona kama akionyesha mshangao wake basi Sam anaweza akasimama kumsimulia kuhusu hilo tukio kwahiyo akatulia kumsikiliza Sam,
"Malaika wangu akaniambia kuwa natakiwa nitoe kafara ya wadada watano na kafara hiyo inatakiwa nilale na hao wadada ila wewe uliponipigia simu na kufanya nirudi ilikuwa bado mdada mmoja na kama nisingefanikisha jana basi ningetakiwa leo kuanza upya tena mara mbili ya jana. Kwahiyo nisamehe sana kuhusu jana"
"Kwahiyo jana ulitaka kunitoa kafara na mimi?"
"Nisingeweza fanya hivyo kwa mapenzi niliyonayo kwa Cherry, umeona na leo alivyoweza kunirudisha? Huyu mtoto ni baraka sana katika maisha yangu na ninakuapia leo kuwa lazima nimletee zawadi"
Sabrina bado alikuwa na swali kuhusu huyo malaika anayeongelewa na Sam kwani bado hakuelewa kabisa, ni hapo alipoamua kumuuliza Sam,
"Na huyo malaika ni nani?"
"Kwani hujui malaika? Ni jini anayenilinda, yule niliyepewa kipindi kile nilipokuwa na nia ya kuwakomesha wanawake. Huwa siwezi zungumza naye wakati kuna mtu ndiomana huwa naingia mahali peke yangu"
Sabrina alizidi kushangazwa tu na maelezo ya Sam kwani bado yalimshtua na kumfanya azidi kumuona Sam ni mtu wa ajabu kwa kila neno kwani swala la kuongea na jini kwa binadamu wa kawaida halikuwa swala la kawaida.
Kisha Sam akamueleza kwa kifupi kile alichokifanya usiku,
"Nilipoondoka hapa nilikuwa nawaza mwanamke wa kwenya kumalizana nae na mawazo yangu yakalenga moja kwa moja kwa wadada wanaojiuza ila kwa bahati mbaya au nzuri nikamkuta mdada njiani aliyesimamisha gari yangu nami nikampakiz a kwenye gari kisha kumalizana nae ila kile kitendo kinaniumiza hadi muda huu"
"Kwanini kile kitendo kinakuumiza?"
"Jua tu kinaniumiza, ila ngoja nikalete zawadi ya Cherry. Hoja ni ile ile sitaki utoke nje Sabrina"
Kisha Sam akainuka na kutoka kabisa, ule mlango akaufunga kwa nje kama alichokifanya usiku.
Sabrina alibaki akitafakari tu yale maelezo ya Sam.

Baada ya Sam kuondoka Sabrina bado hakuelewa kuwa Sam ni mtu wa aina gani na kama anaweza kuutoa uhai wa mtu yeyote bila ya uoga, vipi kwa uhai wake sasa. Kwakweli Sabrina alijiona yupo kwenye moto ambao unachochewa kila kukicha bila ya yeye kujua.
Ni hapa alipoamua kwenda kuichukua simu yake na kujaribu kumpigia simu Jeff ili aweze kumueleza kwa kifupi tu, ila ile simu iliita sana bila ya kupokelewa na kumfanya Sabrina ajiulize kuwa Jeff anatatizo gani na kwanini hapokei simu yake.
Kisha akaona ni vyema kuwasiliana na kwao pia ili asalimiane na mama yake kwa muda huo.

Jeff na Sakina bado hawakujielewa cha kufanya na yule Amina kwani kwa upande wao ilikuwa ni mtihani mkubwa sana ukizingatia yule alikuwa marehemu tayari na hata ndugu zake hawawafahamu.
"Tutafanyaje sasa jamani!"
"Mama, tumpeleke tu hospitali maana hakuna namna nyingine"
"Ujue ni kesi hii Jeff! Hali ni mbaya mwanangu sijui hata mimi jamani"
Mara wakasikia mtu akigonga mlango na kuwafanya washtuke wote wawili ila yule mtu alipoona hakuna majibu aliamua kuingia ndani mwenyewe kwavile mlango haukufungwa na funguo, akawakuta Jeff na mama yake wakimshangaa tu kwani hawakutegemea ujio wake, na huyu alikuwa ni baba wa Jeff. Naye aliwashangaa pia,
"Vipi nyie hamkutegemea kuniona!"
Walikuwa kimya tu, kisha huyu baba akaangalia chini na kushangaa, halafu akawauliza
"Huyu mwanangu Amina amefika vipi huku?"
Jeff akashtuka pia kusikia kuwa Amina ni mtoto wa baba yake kwahiyo ni ndugu yake.

Walikuwa kimya tu, kisha huyu baba akaangalia chini na kushangaa, halafu akawauliza
"Huyu mwanangu Amina amefika vipi huku?"
Jeff akashtuka pia kusikia kuwa Amina ni mtoto wa baba yake kwahiyo ni ndugu yake.
Jeff akamtazama baba yake na kumuuliza kwa mshangao,
"Kumbe huyu ni mwanao pia?"
"Ndio ni mwanangu na jana ameaga na wenzie kuwa wanaenda kujisomea sasa nashangaa yuko hapa. Nini tatizo kwani?"
Jeff na mama yake hawakuwa na jibu ukizingatia yule Amina alikuwa amekufa pale chini.
Baba wa Jeff alipoona kimya na hakuna anayemjibu, akaamua mwenyewe amsogelee Amina ili amshtue na ajue ni vipi amefika pale.
Akashangaa kumgusa yule mtoto naye kulegea kabisa, ni hapo hofu ikamjaa kwenye moyo wake kuwa huenda yule mtoto amekufa.
Alipomsogelea na kusikiliza mapigo ya moyo akaona kweli hayaendi, alijikuta akiinuka kwa hasira na kumkunja Sakina huku akiongea kwa ukali,
"Mmemfanya nini mwanangu Sakina? Umemfanya nini?"
"Jamani Mussa usiwe mkali kwa kitu ambacho hukijui, sasa mimi nimfanye nini mtoto huyu jamani? Kwa kosa gani? Kwanza hata sikujua kama mwanao na hata kama ningejua nisingeweza kumfanya chochote kibaya"
"Huwezi wapi mwanamke mchawi wewe, ndiomana huna wazazi wote umewaua kichawi nina uhakika hata huyu mwanangu umemroga. Sasa nampeleka kwa mganga nikipata uhakika tu nakuletea hapa umle nyama mchawi mkubwa wewe"
Mussa akamuinua Amina na kumuweka begani kisha akatoka nje na kumuweka kiti cha nyuma cha gari yake kisha akapanda na yeye na kuondoka pale.

Sakina alikaa chini akilia kwa uchungu sana kwani ile kauli ya kusema kuwa hana wazazi kwavile amewaua kwa uchawi ilimuumiza sana na kufanya awakumbuke wazazi wake, akumbuke ajali iliyoua wazazi wake kwa mpigo na kumfanya awe yatima toka siku hiyo.
Sakina alikuwa akilia kwa uchungu sana huku Jeff akimbembeleza mama yake kwani yeye ndiye aliyekuwa chanzo cha yote kwa kumpeleka yule binti pale nyumbani kwao.
"Kosa langu ni nini haswa? Kukubali kumpokea yule mtoto? Kukubali kumsaidia? Kweli ng'ombe wa maskini hazai na akizaa basi ni dume na dume lenyewe shoga yani mimi wa kusemwa nimeua wazazi wangu mimi? Hivi kwa uchungu na mateso niliyopitia hao wazazi si wangekuwa faraja kwangu mimi. Kwanini mimi? Kwanini likiibuka hili linakuja lingine kubwa?"
Sakina alikuwa akiongea kwa uchungu sana na ilionyesha ni jinsi gani moyo wake umeguswa na swala lile.
"Mama tulia na tufikirie cha kufanya kwani kulia hakutamaliza haya matatizo mama yangu. Tulia tu mama tujue cha kufanya"
"Unafikiri tutafanyaje kwa hili jamani!"
"Mama, nawajua sana waganga wa kienyeji walivyo waongo sasa hapa jibu ni kwamba yule baba ataambiwa kwamba umeua halafu atafanya alichokiongea na kukuliza zaidi ya hapo na hilo litakuwa tatizo juu ya tatizo nami sipo tayari kuona mama yangu ukidhalilishwa mbele ya macho yangu"
"Sasa tufanyeje mwanangu?"
"Tuondoke hapa nyumbani mama"
"Kwahiyo tukimbie? Yani nikimbie nyumba yangu kwa kosa ambalo sijafanya kweli?"
"Mama usitake kukuza mambo, sio kwamba tunakimbia kwasababu tunaogopa hapana ila bora nusu shari kuliko shari kamili"
"Na tutaenda wapi sasa?"
"Popote mama ilimradi tuepuke tatizo hili. Tafadhari mama usipuuze wazo langu, sitaki tupate tatizo juu ya tatizo."
Sakina hakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na mwanae tu kwani varangati ambalo lingezuka hapo alilihisi kabisa lingekuwaje na jinsi gani lingemuumiza.
Tatizo ikawa pa kuelekea sasa,
"Mama usizubae na kutoa machozi kwani hata ukilia haita saidia. Chukua mkoba wako tuondoke hapa mama"
Jeff nae akawa amepakia baadhi ya nguo zake kwenye begi lake la mgongoni kwaajili ya kuondoka.
Kisha akamuhimiza mama yake na wakatoka na kufunga milango yao yote ya ndani na nje vizuri.
"Sasa mama tusipite hiyo njia ya barabara, twende tukapite uchochoro halafu tutokee kama kwakina Sabrina tuzunguke kule nyuma tukatokee barabara ya chini"
Sakina hakuwa na pingamizi na kuamua kupita kama alivyosema Sakina.

Jeff na mama yake wakiwa njiani karibu na barabara ya nyuma waliyopanga kutokea kuna gari ikasimama mbele yake na kumfanya Sakina atake kukimbia kwa kuhofia kuwa huenda akawa baba Jeff,
"Usiwe na uoga huo mama, hakuja na gari hiyo"
Kwenye gari hiyo alishuka Sam na kuwataka wapande ili awapeleke waendako, nao wakapanda.
"Haya sasa niwapeleke wapi?"
Sakina aliinama tu kwani hakujua hata waseme nini, ndipo Jeff alipoamua kumueleza Sam kwa kifupi tu,
"Kwakweli hatuna pa kwenda kwasasa kwani kuna matatizo yametufika na kufanya tuamue kukimbia nyumba yetu"
"Matatizo gani tena jamani? Poleni sana, basi twendeni kwangu halafu tutaelezana tu"
Sakina alishukuru sana kwani hakutegemea jambo lile kwa wakati ule na kujikuta akisema,
"Kweli kila jaribu lina mlango wa kutokea. Najua yote haya yataisha"
Jeff alimsogelea mama yake na kumkumbatia kama ishara ya kumtia moyo kwa yale yaliyotokea.

Safari ilikuwa ni moja kwa moja nyumbani kwa Sam ambako aliwakaribisha ndani na kumkuta Sabrina sebleni ila Sabrina alishangaa kuwaona,
"Kheee vipi tena jamani?"
Huku akijiwa na wazo la sentensi ya Sam wakati anaondoka kuwa atamletea Cherry zawadi kwahiyo hofu yake ikawa huenda Sam kaamua kumleta Sakina na Jeff kama zawadi kwa Cherry.
Sam nae aligundua mshtuko wa Sabrina na kumwambia,
"Usijali mke wangu, hawa wamepatwa na matatizo ndiomana nimekuja nao. Lile swala letu bado lipo pale pale"
Sabrina akapumua kidogo huku akiendelea kuwasalimia Sakina na mwanae ingawa hawakuelewa kuwa Sabrina na Sam walikuwa wakiongelea mambo gani.
Sakina alimkumbatia Sabrina huku akitokwa na machozi, ndipo Sam alipowataka wakae ili waweze kuelezea kilichotokea.
Ni hapo ambapo Jeff alipoamua kuelezea alivyokutana na Amina usiku ila hakueleza kuwa alikuwa akielekea wapi.
Akaelezea pia jinsi huyo binti alivyokufa kwenye mikono yao na jinsi alivyokuja baba yake na kumshutumu mama yake kuwa anahusika na kifo hicho na jinsi walivyoamua kuondoka kwenye nyumba yao.
Sam aliwapa pole na aliweza kujua kwa haraka kuwa huyo binti ni yupi,
"Poleni sana na mmefanya jambo la busara kuondoka. Mi nitawasaidia jamani na yote haya yataisha"
Sabrina nae akauliza kanakwamba hakuelewa vizuri ile habari,
"Huyo dada alikutana na jini?"
"Ndio, kwa maelezo yake ni kuwa alikutana na jini na ndio aliyemfanya vibaya tena nadhani atakuwa amemnyonya damu. Masikini Amina jamani kumbe ni dada yangu tena wa damu dah!"
Jeff aliongea kwa masikitiko ila Sam aliendelea na msisitizo wake wa kusema kuwa atawasaidia kwa kila kitu na atahakikisha kuwa kila kitu kitakuwa sawa.
Wakati wanaendelea na mazungumzo hayo, simu ya Sabrina ikaita na alipoangalia anayempigia akaona namba ya simu ya mama yake na kumfanya aipokee na kumsalimia ambapo mama yake alianza kwa kumueleza,
"Yani mwanangu huku kuna habari mbaya sana, kama una namba nyingine ya Sakina au namba ya Jeff wapigie na waambie wasirudi kwao kwasasa"
"Kwani kuna nini mama?"
"Yani watu wamejaa pale kwao ni vurugu tupu, yupo yule mumewe anashutumu kuwa Sakina ni mchawi. Kuna wengine wapo na mapanga hapa yani hali ni mbaya"
"Basi mama ngoja niwatafute hewani"
Sabrina akaikata ile simu huku akimtazama Sakina na kumuonea huruma kwakweli.
Akawaambia alichoambiwa na mama yake muda huo.
Jeff naye akamtazama mama yake na kumwambia,
"Unaona sasa mama! Pale nyumbani tusingeondoka wangeweza kutufanyia mambo mabaya sana"
Sakina naye aliongea kwa masikitiko,
"Ila kwa akili ya baba yako Jeff anaweza kufanya chochote pale. Mi namjua vizuri sana, anaweza hata kuvunja nyumba ili anikomeshe tu"
Sam akawapa moyo,
"Jamani msijali, hakuna chochote kibaya kitakachofanywa pale, nyie niaminini mimi"
Kisha Sam akatoka na kuwaaga kuwa anaenda kushughulikia swala hilo.

Sabrina alikaa pale na wakina Sakina ila kila akifikiria alichosimuliwa na Sam na walichozungumza Jeff na mama yake akaona kuna uhusiano juu ya huyo binti kuwa ndio yule yule aliyetelekezwa na Sam usiku na kufanya atamani kuwaeleza ila hata kama angewaeleza ingekuwa kazi bure kwani Sam ni mtu mwenye pesa na kadri anavyofanya hayo matukio ndio anazidi kujiongezea wigo wa pesa kwahiyo Sabrina akaona ni vyema awe kimya ili asije zidisha tatizo juu ya tatizo.
Sakina nae alikuwa kasinzia pale pale sebleni na kumfanya Sabrina amuamshe na kumuongoza kwenye chumba cha kupumzika ila Jeff alitulia pale sebleni huku akitafakari mambo mbali mbali.
Sabrina aliporudi sebleni alimkuta Jeff akiwa amekaa huku amempakata Cherry na kumfanya Sabrina atabasamu tu na kuwaza kuwa endapo angeishi na Jeff mambo yangekuwaje.
Muda huo Jeff nae alikuwa akitafakari kitu kile kile kuwa angeishi na Sabrina ingekuwaje na wote wakajikuta wakitazamana kwa muda mmoja na kutabasamu kisha Sabrina akaelekea chumbani kumuhudumia mtoto wao mdogo ambaye alimsikia akilia kwa muda huo.

Nyumbani kwa Sakina kulikuwa na balb kweli kwani walijaa ndugu, majirani na jamaa wengi wa mama Amina huku makelele mbali mbali yakiendelea na kufanya wapita njia na majirani wa pale kusimama ili wajue kuna nini.
Mama Sabrina alisikitishwa sana na kile kitendo kwani ilikuwa kanakwamba Mussa hajawahi kuishi na Sakina kiasi cha kwenda kumdhalilisha kiasi hicho, na hata majirani wengine walimsikitikia Sakina na wengine walionekana kuamini kuwa ni kweli Sakina ni mchawi.
"Huyu mwanamke atakuwa ni mchawi kweli tu jamani, mtu gani huwa hatembelei wenzie hata hali hawajulii wenzie huyu ni mchawi kweli"
Ni mama Sabrina pekee aliyeonekana kuwarekebisha kauli hawa watu,
"Jamani sio kwa hivyo mnavyosema, Sakina kwakweli si muongeaji sana lakini ni mtu anayejali matatizo ya mwingine sana. Toeni mfano wa msiba wowote uliotokea hapa mtaani ambao Sakina hakuhudhuria na wala kushughulika nao"
Wakakaa kimya,
"Si mnaona mnakosa majibu? Sakina sio mbaya kiasi hicho mnachoongea tena ni mtu mwenye upendo sana. Ni nani kauguliwa na nduguye halafu Sakina ajue na asiende kumuona? Najua hakuna kwahiyo msimpe ubaya mtu wakati hamumfahamu vizuri"
Maneno ya mama Sabrina yaliwaingia wengi na kuwafanya waanze kumuhurumia Sakina kwani lile lililompata lilikuwa ni tatizo tu kama matatizo mengine.
Wakati wakizungumza pale na kelele zikiendelea kila upande walishangaa kuona gari za polisi zikiwa pale na watu wote walipewa amri moja ya kusambaratika na kweli walitii amri na pale alibaki Mussa, mama Amina pamoja na maiti ya marehemu Amina ambapo wale askari walisaidiana kumpakia marehemu Amina kwenye gari kwani walikuwa wameenda na gari ya kubeba wagonjwa mahututi pale pamoja na madaktari wawili kisha kuondoka na wazazi wa Amina pale na kuelekea hospitali moja kwa moja.

Mama Sabrina akiwa karibu kidogo na eneo la tukio alishangaa kuona gari ya Sam ikiwa imeambatana na zile gari za askari na moja kwa moja akapata jibu kuwa Sam ndie aliyefanya kuwaita wale askari na kuhisi kuwa lazima Jeff atakuwa alimpigia simu na ndiomana imekuwa rahisi kwa Sam kufanya vile na kwasababu ya pesa zake imekuwa ni rahisi sana kwani kwa mtu mwenye uwezo mdogo asingeweza kuchukua askari ili wamsaidie pale.
Baadhi ya watu waliona kuwa hawajatendewa haki kusambaratishwa pale kwani wao waliona ni sahihi kabisa wakidai kuwa kile kitendo ni komesha uchawi.

Sam alipomaliza yale maswala akaamua kuweka ulinzi wa muda kwenye nyumba ya Sakina kisha akaamua kurudi nyumbani kwake.
Akiwa njiani akamuona Aisha na kuamua kusimamisha gari ili ampakie.
"Ulikuwa unaenda wapi Aisha?"
"Nilikuwa naenda hapo nyumbani kwakina Jeff"
"Basi wakina Jeff hawapo huko ila ngoja nikupeleke walipo"
Sam akamwambia Aisha apande kwenye gari kisha na yeye akapanda na safari ya kuelekea nyumbani kwake ikawadia.

Muda huu Cherry na mdogo wake walikuwa wamelala na Sabrina alienda kuwalaza chumbani kwani hakupenda wapate usumbufu wa usingizi wa mchana kisha yeye akarudi sebleni na kujikuta wapo wawili tu yani yeye na Jeff.
Kwa pamoja wakatazamana kwa macho kama ya uoga hivi kisha Jeff akasogea alipo Sabrina na kumuwekea mkono begani ila Sabrina alikuwa kimya tu huku kama mapigo ya moyo yakienda mbio na kumfanya Jeff kugundua kwa haraka kuwa akitakacho yeye ndio akitakacho Sabrina, kwahiyo akajikuta akimtazama kwa karibu sana tena huku macho yake yakiwa yamejawa na tamaa ya hali ya juu.

Sam alifika nje ya nyumba yake na hakutaka kuingiza gari ndani kwani alijua kwa vyovyote vile ni lazima atoke tena ukizingatia kuna vitu bado hakutimiza.
Wakashuka kwenye gari huku akimwambia Aisha,
"Wewe nenda moja kwa moja ufungue ule mlango wa kuingia ndani hata usijisumbue kugonga utachoka pale mlangoni bure, ngoja mi nipaki vizuri gari yangu hapa nje"
Aisha akaingia getini na moja kwa moja akaenda alipoelekezwa, na alipofungua mlango tu akashangaa kumuona Jeff na Sabrina wakinyonyana ndimi zao.


Aisha akaingia getini na moja kwa moja akaenda alipoelekezwa, na alipofungua mlango tu akashangaa kumuona Jeff na Sabrina wakinyonyana ndimi zao.
Aisha aliduwaa pale mlangoni kwa dakika kadhaa akiwatazama tu.
Muda huo huo nao wakashtuka kuwa mlango umefunguliwa na kujikuta kwa pamoja wakimtazama Aisha.
Wakiwa wanatazamana, Sam nae alikuja na kumshangaa Aisha kuwa ni vipi amesimama mlangoni,
"Mbona umesimama tu, karibu"
Sam aliingia vizuri na Aisha nae akafata nyuma na kwenda kukaa huku bado akimtazama Jeff na Sabrina ambao nao walikuwa kimya tu, ni hapo Sabrina alipoamua kujigelesha kwa kumkaribisha Aisha,
"Karibu sana"
Ila Sam akamshushua Sabrina pale pale,
"Inamaana muda wote aliosimama mlangoni hukumuona?"
"Hapana ila nilikuwa najiuliza kuwa kaletwa na nani"
Kisha Sam akamuomba Sabrina amfate na kuelekea nae chumbani.

Pale sebleni alibaki Aisha na Jeff ambapo Aisha aliamua kusogea kwenye kochi alilokaa Jeff kisha akamuuliza,
"Ni huyu mwanamke unayempenda?"
Jeff aliitikia kwa kichwa akimaanisha kuwa ndiye, kisha Aisha akaendelea kuongea na kusema,
"Ila huyu mwanamke si ndie mke halali wa huyu kaka?"
"Wakati dada yako anatembea na huyu mwanaume kwani hakujua kama ana mke halali?"
Aisha akakaa kimya kwa muda kwani hakutegemea kupewa jibu lile na Jeff, kisha akasema tena,
"Kwahiyo huyu mwanaume anajua kama wewe unatembea na mke wake?"
"Ngoja nikuulize, hivi wewe kinachokufanya useme kuwa mimi natembea na huyu mwanamke ni nini?"
"Si nimewakuta hapa mnanyonyana midomo"
"Kwahiyo nikinyonyana nae midomo ndio natembea nae? Sikia nikwambie Aisha, wewe sio mpenzi wangu kwahiyo si ruhusa kwako kuangalia njia zangu. Mambo yangu uyaache kama yalivyo na wala hayakuhusu"
Aisha alinyamaza na kumtazama tu Jeff huku akijiona wazi kuwa ndoto zake zote za kuwa na Jeff zimeyeyuka ingawa alijitahidi kutabasamu tu ili kuonyesha kwamba hajachukia.

Muda kidogo Sabrina na Sam wakatoka ndani, kisha Sam akawaaga tena ila Aisha nae akasimama na kuaga hata Sam ikabidi amuulize,
"Kwahiyo ndio umemaliza maongezi yako hapo!"
"Ndio tayari halafu kuna mahali nataka kuwahi"
"Basi twende"
Sam hakutaka kujua kuwa ameshaongea nini na Jeff ila kwavile alisema kuwa mazungumzo yake yameisha basi akaona ni vyema wakiondoka tena kwa pamoja kwani muda huo ndio alipanga kwenda kumchukulia Cherry zawadi.
Walitoka mule ndani na kuwaacha Jeff na Sabrina ambapo Jeff alimwambia Sabrina,
"Kuna umuhimu mkubwa sana wa kufunga ule mlango ili mgeni akija basi agonge"
"Kwani ametuona?"
"Ndio tena katuona vizuri kabisa"
"Mmh sasa itakuwaje? Yani hisia ni mbaya sana, tafadhari Jeff tusiwe tunakaa karibu karibu"
"Sabrina kwakweli nakupenda, na mapenzi ni hisia. Ni ngumu sana kwa mimi kuficha hisia zangu juu yako kwani ukweli bado utabaki pale pale kuwa nakupenda sana"
Haya maneno ya Jeff yalikuwa yanamuingia vizuri sana Sabrina kwani aliweza kuyahisi vilivyo katika moyo wake na kujikuta akimtazama tu na kumpa nafasi ya ziada kwa Jeff kuzungumza,
"Unajua nini Sabrina, sisi tunapendana na hilo halifichiki. Unanikataa sababu ya udogo wangu ila swali ni kuwa mara ya mwisho sikukuridhisha? Na kama mdogo hafai mbona nimeweza kufanya uitwe mama sasa? Mapenzi hayaangalii umri, dini, kimo, umbo, kabila wala rangi. Mapenzi ni kama jani huota popote. Kwakweli tunapendana Sabrina na hilo halifichiki kabisa."
"Sasa unataka tufanye nini Jeff maana mimi nimeshaolewa tayari"
"Hilo sio tatizo kwani hata mimi nimekuwa na wewe wakati tayari upo kwenye mahusiano na hadi unaolewa tayari ulikuwa ni mimba yangu. Kama niliweza kufanya yote yale nikiwa na akili yangu ile ndogo ni vipi nishindwe kwa sasa?"
Muda huo Sakina nae alitoka chumbani na kuelekea moja kwa moja pale sebleni alipo Jeff na Sabrina.
Kisha akakaa na kuwasalimia halafu akawaambia,
"Mbona kimya tena wakati nimewasikia kama mkipiga stori jamani!"
Sabrina akatabasamu tu kisha Jeff akamwambia Sabrina,
"Mi namweleza ukweli mama"
Sabrina akabadilisha sura na kumfanya Jeff anyamaze ila Sakina akang'ang'ania kuelezwa huo ukweli.
"Hakuna lolote mama, nilikuwa natania tu"
"Mmmhh"
Sakina akaishia kuguna tu, kisha mambo mengine yakaendele.

Sam akiwa kwenye gari na Aisha, alimuuliza kwanza sehemu ambayo itakuwa nzuri akimuacha kisha Aisha nae akapata upenyo hapo kuongea ya moyoni mwake ambapo alianza kwa kumuuliza swali Sam,
"Hivi utajisikiaje endapo ukagundua kuwa mkeo ana mwanaume mwingine?"
"Kwakweli kwa mwanaume yeyote mwenye wivu kama mimi ukimuuliza hilo swali atakujibu kuwa ni maumivu tu kwani hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa na umpendae."
"Unampenda sana mke wako eeh!"
"Ndio nampenda tena zaidi ya sana"
"Sasa mbona ukatembea na dada yangu?"
"Mmh Aisha yani unakuwa kamavile binti wa kijijini jamani! Kwani hujui mapenzi yalivyo? Kuna wakati mtu unateleza ila dada yako nilimpenda pia na nilikuwa tayari kumsaidia kwa chochote ingawa hakuhitaji msaada wangu"
"Sawa nimekuelewa, vipi kwasasa una mwanamke yeyote wa nje?"
"Hapana, sina mwanamke yeyote zaidi ya mke wangu. Na mbona umeamua uniuliza maswali hayo?"
"Kuna kitu nimeona nyumbani kwako na ndiomana nimekuuliza"
Sam akashtuka kidogo na kumuuliza Aisha kwa makini kuwa ni kitu gani alichokiona hadi kumfanya amuulize maswali yale,
"Ila kabla ya yote ngoja nikuulize. Jeff una muamini kwa kiasi gani? Na kwanini yupo pale kwako? Je unafikiri ni sahihi yeye kuwa pale?"
Sam akaanza kupata kama picha kuwa huenda Aisha kuna kitu alikiona kikifanya na Sabrina na Jeff na pengine ndio kilichomsababisha asimame mlangoni kwa muda kidogo.
Ni hapa Sam alipomuuliza vizuri Aisha,
"Niambie ni kitu gani umekiona Aisha au ni nini kimefanywa na Sabrina pamoja na huyo Jeff"
"Mmh ila naogopa kuvunja ndoa"
"Hapana, wee niambie tu. Napenda mtu anayeongea ukweli"
Kisha Sam akafungua droo ya mbele kwenye gari yake na kutoa pesa kidogo kisha akampa Aisha ili amwambie,
"Kwakweli nimeshangaa sana, kwani nilipofungua mlango nimewakuta wakinyonyana midomo tena wamejiachia kabisa. Kwakweli imeniuma ukizingatia yule dada ni mkeo"
Sam akapumua kidogo kisha akamwambia Aisha,
"Asante kwa taarifa Aisha, sijui huyu mke wangu ananitakia nini mimi yani kumpenda kote ninakompenda huku bado anapata ujasiri wa kuwa na mwingine!"
"Tena sio kuwa na mwingine tu ila anawezaje kuwa na huyo mwingine kwenye nyumba yako mwenyewe?"
"Kwakweli hapo ndio pagumu jamani sijui nimfanye nini huyu mwanamke"
"Dawa ya wanawake wa aina hiyo ni kuwaolea mke wa pili tu"
Sam akatabasamu kidogo na kumwambia Aisha,
"Aah kumbe, ila si hata wewe utafaa ili nilipe fadhila za yale wazuri niliyowahi kutendewa na dada yako"
Aisha akatabasamu tu kisha akasema,
"Nimeshafika, nishushe hapo"
Sam alipofika akasimama kisha kumwambia Aisha ampatie mawasiliano yake ya sasa naye akafanya hivyo kisha akampatia pesa zingine kidogo na kumuaga ambapo Aisha akashuka na kuondoka.

Sam akatafakari sana mule kwenye gari yake,
"Naelewa kabisa kama Sabrina amezaa na Jeff ila moyo wangu haukubaliani na ukweli huo ndiomana huwa namwambia aniheshimu ila kwanini anafanya hivi? Huyu Sabrina kwanini nampenda sana? Kwanini siwezi kufanya kibaya juu yake? Na mbona haniheshimu huyu Sabrina jamani? Jeff na mama yake niliamua kuwasaidia kutokana na yale matatizo yao chanzo ni mimi mwenyewe ila huyu Sabrina mbona anatia aibu jamani? Na huyu Jeff asiye na fadhila yani na kumsomesha kote kule ndio fadhila zake ni kupambana na mimi kuwa anaouwezo wa kumchukua Sabrina? Hivi huyu Sabrina anajivunia kwavile ananifahamu vizuri au ni kitu gani? Ni kweli nimejitolea kwake na pia najitolea kumwambia kila kitu kuhusu mimi ila siku yake ni moja tu tena siku ambayo hatonisahau kamwe katika maisha yake. Haiwezekani awe ananidhalilisha kwa kiasi hiki ilihali najitambua na kujielewa vilivyo"
Kisha akaondoa gari yake na kuelekea kwenye mambo yake.

Ilikuwa ni usiku tayari watu wakiwa wamejaa kwenye msiba wa kumlilia Amina ambaye walipanga kuwa azikwe kesho yake.
Wazazi wa Amina nao wakajipanga kuwa haiwezekani mtoto wao afe peke yake.
"Kwakweli sikubaliani na hili swala baba Amina, ikiwa mwanetu kafa na aliyemuua anajulikana kwanini basi huyu aliyemuua asizikwe pamoja nae"
Wakakubaliana na kuona ni kweli huyo mtu anapaswa kufa kama alivyomuua Amina na wakaona njia ya pekee ni kupanga na mganga kuwa watakapokuwa wanamzika Amina basi na huyo mtu afe muda huo huo.
Yani hawa watu ingawa walikuwa wamefiwa ila bado walikuwa na tatizo moja lile lile yani dhidi ya mtu huyo aliyemuua mtoto wao.

Sabrina nae kwa usiku ule akaenda kumuonyesha Jeff pia chumba cha kulala,
"Kwahiyo na wewe Sabrina huwa unalala kwa mumeo?"
"Mmh hapana yani toka tumehamia nyumba hii sijawahi kulala nae chumba kimoja. Naogopa Jeff, usinione hivi kwakweli naogopa"
"Basi njoo ulale na mimi"
"Wee Jeff, tusimruhusu shetani kutawala akili zetu kwani mwisho wa siku tutatenda dhambi"
"Hapana sio shetani, haya ni mapenzi yangu kwako tu Sabrina"
Sabrina akaona ni vyema atoke kwenye kile chumba ili kuepusha mambo makubwa zaidi kutokea dhidi yake na Jeff.
Alimfata Sakina pale sebleni ambaye aliuliza tu kuwa mbona Sam kachelewa,
"Aah atarudi tu"
"Kwani ndio kawaida yake kuchelewa?"
"Ni kawaida ndio ila mara moja moja."
Sakina hakuwa na la kusema zaidi kwani haikuwa sawa kwa yeye kufatilia familia ya Sabrina.

Kwenye mida ya saa sita usiku ndipo Sam alipowasili tena nyumbani kwake na kumkuta Sabrina akiwa mwenyewe sebleni akimngoja ila Sam alikuwa tayari ameshakunywa pombe za kutosha na kumfanya aongee sauti ya kilevi.
"Saizi eti ni mwanamke mzuri unamngoja mumeo arudi ndio ukalale wakati mchana unanyonyana midomo na kijana mdogo"
Sabrina alielewa ile sauti ya kilevi ya Sam na akajua wazi kuwa akijibishana nae hapo tu basi atajiumbua mwenyewe kwahiyo akaamua kuwa kimya tu huku akitaka kumuongoza chumbani akalale,
"Sabrina hata usijisumbue, mi naenda mwenyewe. Haya vipi huyo bwana mdogo wako kalala?"
Sabrina akaona hapo ni hatari zaidi na kuamua kuelekea chumbani kwa watoto kulala na kumuacha Sam akiwa mwenyewe pale sebleni kwani aliona kuwa kitendo cha yeye kuendelea kukaa nae pale sebleni ndicho ambacho kingemsababisha kuwa aumbuke ndiomana akaamua kuelekea chumbani.
Sam nae alibaki pale pale sebleni na mwisho wa siku akalala kwenye kochi.
Ila yale maneno ambayo Sam aliyazungumza usiku ule kwa Sabrina ni kwamba yote yalisikiwa na Sakina kwavile hakuwa amelala kihivyo kutokana na alishalala mchana.
Kwahiyo aliweza kusikia yote na kumfanya aanze kutafakari kuwa Sam alikuwa anamaanisha kitu gani kumwambia vile Sabrina.

Kulivyokucha, Sabrina alikuwa wa kwanza kutoka chumbani akiwa na watoto wake kwani siku hiyo nao waliamka mapema sana.
Alipofika sebleni akamshangaa Sam kuwa alilala pale pale sebleni ila hakutaka kumsumbua bali alikazana kushughulika na watoto wake ili awaogeshe kwanza na kuwabandikia uji.
Ila asubuhi ile ile akapigiwa simu na mama yake,
"Mama, mbona leo asubuhi sana"
"Mmh mwanangu, yani nimejikuta nikimuhurumia sana Sakina jamani"
"Kwani vipi tena?"
"Usiku kuna mambo nimeyaota kuhusu pale nyumbani kwa Sakina, sasa leo nilipodamka tu nikasema niende kwanza nikachungulie. Nimekuta pale karibu na kwa Sabrina imepasuliwa nazi yenye maandishi, halafu kuna kitambaa chekundu na yai viza limepasuliwa hapo yani hata sijui wanaashiria nini"
"Mmh makubwa hayo mama, ila Sakina hana kosa lolote mama yani huo ubaya utawarudia wenyewe."
Kisha akakata simu huku akimsikitikia Sakina, na muda huo Sakina nae alikuwa ametoka chumbani akija hapo sebleni.
Sabrina akaona si vyema kwa Sakina kumuona Sam akiwa amelala pale sebleni hivyo akalazimika kumuamsha ili akalale chumbani, ambapo Sam aliamka vizuri tu kisha akaanza kuelekea chumbani ila kabla hajafika chumbani alianguka na kumfanya Sabrina amkimbilie.
Alipofika pale alipoanguka akaona damu zikimtoka Sam puani.

Sabrina akaona si vyema kwa Sakina kumuona Sam akiwa amelala pale sebleni hivyo akalazimika kumuamsha ili akalale chumbani, ambapo Sam aliamka vizuri tu kisha akaanza kuelekea chumbani ila kabla hajafika chumbani alianguka na kumfanya Sabrina amkimbilie.
Alipofika pale alipoanguka akaona damu zikimtoka Sam puani.
Sabrina akashtuka sana ambapo Sakina nae alisogea pale na kumfanya ashtuke pia,
"Khee jamani kapatwa na nini?"
Sakina akamuita Jeff ambaye naye alitoka kwa haraka huku wakijadiliana cha kufanya.
Sabrina akakumbuka siku alipomuuliza Sam kuwa kwanini likitokea tatizo anaenda chumbani kwake akakumbuka jinsi alivyosema kuwa anaenda kuongea na malaika wake na ndio hapo Sabrina alipowaomba wakina Jeff wasaidiane nae kumbeba Sam na kumpeleka chumbani, nao hawakusita na kufanya hivyo ambapo walimuingiza na kumpandisha kitandani kwake kisha wote wakatoka na kumuacha Sabrina ambapo akamfunika shuka kiasi kisha kutoka na kuurudishia ule mlango wake.

Sakina na Jeff walishangaa kile kitendo kuwa mtu akianguka badala ya kumpeleka hospitali unampeleka chumbani.
Sakina akaona vyema amuulize Sabrina,
"Hivi tupo sawa kweli Sabrina kumpeleka mgonjwa chumbani badala ya hospitali?"
"Dada, mi ndio namfahamu vizuri Sam na hadi nimechukua uamuzi huo ujue namfahamu vizuri sana na tukimpeleka hospitali hapo tutammaliza tu"
"Kwani karogwa?"
"Kwakweli sijui ila ndio hivyo tukimpeleka hospitali tutammaliza"
Kisha Sabrina akatulia na kuanza kufikiria kitu, akakumbuka simu ambayo alipigiwa na mama yake kuwa kwakina Sakina imevunjwa nazi na yai viza na kuna kitambaa chekundu. Mawazo yake yakaenda moja kwa moja kuwa huenda vitu hivyo vimeenda kumuathiri Sam ndiomana ameanguka gafla huku moyoni mwake akimuombea apone kwa hali na mali kwani ingawa kuna muda anamtesa ila ndiye anayemfanya aendelee kuficha aibu ya watoto wake.
Kila mmoja alikuwa na mawazo yake mwenyewe dhidi ya Sam ila wote walimuombea apone kwa siku hiyo.

Muda ukawa umepita sana kwani na jioni nayo ilianza kuingia bila ya Sam kutoka na kufanya wote wapatwe na mashaka.
Sabrina alikuwa na uoga sana, akatamani kitokee kitendo cha siku ile kile alichokifanya Cherry kwa Sam na kumfanya azinduke.
Kwa akili ya Sabrina muda huo alitamani kumpeleka Cherry kwani ndiye aliyeona kuwa anaweza kumsaidia Sam ili wasimpoteze ila anampelekaje ikiwa Jeff yupo kwani alihisi kuwa lazima angepaniki ukizingatia nae Cherry ni mwanae.
Ikabidi Sabrina aamue kumuita kidogo Jeff jikoni ili apate kuzungumza nae.
Jeff alimfata Sabrina jikoni ambapo Sabrina alimueleza Jeff alichomuitia,
"Kwanza nashukuru sana kwa kuheshimu uwepo wangu Sabrina, kweli wewe ni mwanamke wa pekee sana. Ilimradi umeniambia na hiko ndio pekee cha kumsaidia Sam basi mimi sina tatizo lolote ila upendo wangu kwako uko pale pale"
"Jeff jamani, hebu acha hayo maneno kwanza ipo siku tutakutwa na Sakina tukizungumza hayo. Sina cha kujitetea mwenzio"
Kisha wakatoka na kurudi tena sebleni halafu Sabrina akamshika mkono Cherry na kwenda kumuingiza chumbani kwa Sam ambapo Sam alikuwa vile vile kama ambavyo walimlaza mwanzoni.
Kisha Sabrina akatoka ila muda huu akarudishia kidogo tu mlango ili kama Cherry nae akitaka kutoka aweze kutoka.
Kisha yeye akarudi na kukaa sebleni ambapo Sakina naye alikuwa hapo huku akitamani sana kujua kuwa kwanini Sabrina amempeleka Cherry chumbani kwa Sam.

Alikaa na swali lake ila uzalendo ukamshinda na kufanya aulize,
"Sabrina, mbona umempeleka mtoto kwa mgonjwa?"
"Nimeona anasumbua sumbua hapa ndiomana nimempeleka akamuone baba yake"
"Ndio na kumuacha huko huko jamani!"
"Ndio ili acheze cheze nae"
"Kwani kashazinduka tayari?"
Kabla Sabrina hajajibu, wakamuona Sam akitoka chumbani huku kambeba Cherry mikononi na wote wakawa kimya wakishangaa tu kile wanachokiona kwa muda huo kwani hawakutegemea kuwa Sam angezinduka kwa kuwekwa chumbani tu.
Sam akawasalimia pale na kukaa kwenye kiti huku akifurahiana na Cherry kisha akauliza mida na kuchukua simu yake ambayo ilikuwa pale pale sebleni,
"Dah huyu mtu kanipigia sana simu jamani, huyu ndiye nilimuagiza zawadi ya malaika wangu Cherry halafu sikuweka sauti na ndiomana hata nyie hamkusikia"
Sakina akatamani kujua kuwa Sam amezindukaje na kuhusu zile damu zilizokuwa zikimtoka puani ila hakuweza kupata jibu na hakuweza kuuliza pia zaidi ya kumuangalia tu Sam huku akimshangaa kwa kitendo kile.
Sam aliamua kumpigia simu mtu yule na kumwambia amletee hiyo zawadi muda huo, hata Sabrina akajiuliza kuwa hiyo zawadi ni ya aina gani hadi inaagizwa kiasi kile. Kwahiyo akatulia kwa hamu kuweza kuiona hiyo zawadi ambayo Cherry analetewa ingawa bado hakuelewa uhusiano wa Cherry na kuzinduka kwa Sam.

Sabrina aliamua kwenda kuandaa chakula sasa kwani muda ulikuwa umeenda sana na kumuacha Sam sebleni akiwa na wakina Sakina.
Sam alianza kumueleza Sakina kuhusu habari za nyumbani kwake,
"Sasa kule kwako usiende hadi wiki ipite, mambo yatakuwa sawa kabisa"
Jeff akauliza,
"Hawatamfata tena mama?"
"Hawataweza kumfata na hakuna chochote kibaya watakachomfanyia. Amini maneno yangu Sakina"
"Nakuamini shemeji yani hilo halina ubishi, nakuamini vizuri sana"
Muda kidogo simu ya Sam ikaita ambapo aliipokea muda huo huo kisha akainuka akiwa vile vile kambeba Cherry na kutoka naye nje.
Sabrina aliwaona wakitoka kwahiyo naye akatoka jikoni na kuwafata nje ambapo alimuona kijana mmoja na gari pembeni huku Sam akimuuliza Cherry,
"Umeipenda hii gari mwanangu"
Cherry alionekana kukubali kwa kutingisha kichwa.
Sabrina alisimama pale akiwa kaduwaa tu kuwa Sam kamnunulia gari mtoto wao Cherry.
Alimuangalia tu pale Sam akiagana na yule mtu aliyepeleka pale lile gari kisha akatoka na kuondoka.
Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Hili ni gari la Cherry, vipi na wewe umelipenda?"
Sabrina alikuwa akistaajabu tu na kushindwa hata kujibu.
Sam alipomuona Sabrina kaduwaa tu, akaenda ndani na kuwaita Sakina na Jeff, nao wakatoka nje kisha akawaonyesha ile gari,
"Vipi mnaionaje hii gari ni nzuri eeh!"
Nao wakaisifia kwavile ilikuwa ni nzuri kweli, kisha Sam akawaambia tena,
"Basi nimemnunulia mwanangu wa kwanza Cherry"
Kisha wakaongea ongea pale na kurudi ndani ila Sabrina alijikuta ameunguza mboga kwavile alivyokuwa anashangaa pale nje na kusahau kuwa kuna mboga amebandika.
Sam alipogundua kuwa Sabrina ameunguza mboga akamwambia,
"Usijali mke wangu hata usihangaike nayo, leo nina furaha sana. Jiandaeni wote tukale chakula hotelini"
Maamuzi ya Sam yalikuwa yakimshangaza sana Sakina kwani alimuona Sam kuwa mwanaume wa tofauti na wa pekee sana hata lile wazo la kufikiria kwamba kuna kitu kinaendelea kati ya Sabrina na mwanae Jeff likapotea kwani akapata imani kubwa sana kuwa wale watoto ni wa Sam na ndiomana ameweza kumnunulia Cherry gari ya gharama kiasi kile.

Walipomaliza kujiandaa, wakatoka wote na gari walilotoka nalo ni lile ambalo Sam amemzawadia Cherry.
Moja kwa moja wakaenda kwenye hoteli kubwa sana huko walikula na kufurahi ila ni Jeff pekee ambaye hakuwa na furaha ila alionekana kuilazimisha furaha tu.
Muda kidogo Sakina akainuka na kuelekea maliwatoni, kufika huko akakutana na mdada mmoja ambaye ni muhudumu wa ile hoteli ambaye alimsalimia na kuanza kumuuliza,
"Samahani dada, hivi wewe pale ndugu yako ni mwanaume au mwanamke kati ya wale wawili yani yule Sam na mkewe?"
"Ni mwanamke, kwanini umeniuliza hivyo?"
"Nduguyo kawezaje kuishi na Sam au stori nilizowahi kuzisikia ni uongo? Na kama ni uongo mbona kuna rafiki yangu majuzi tu hapo kammaliza pia?"
"Sijakuelewa dada"
"Kwa stori nilizowahi kuzisikia kuhusu huyu bosi ni kuwa kila mwanamke anayelala nae ni lazima amuumize sana na humpa onyo la kutokusema kwani akisema tu ni lazima afe kwa stori hizo ni kuwa hakuna mwanamke aliyewahi kulala nae akapona kwani wote hushindwa kuvumilia na kuamua kusema halafu mwisho wa siku huwa wanakufa. Sasa huyu nduguyo amewezaje kuishi naye kwa kipindi chote hicho hadi sasa ana watoto wawili"
"Kwakweli inakuwa ngumu kukuelewa, unajua mambo mengine huwa ni siri ya ndani ila hata hivyo kama hizo stori zingekuwa kweli basi angekufa siku nyingi sana yule mdogo wangu. Sikia nikwambie, mtu anapokuwa tajiri kama Sam alivyo watu wengi huwa wanatengeneza stori za uongo ili kumuharibia sifa yake. Sidhani kama kuna ukweli wowote katika hiyo stori"
"Dada, naongea kitu ambacho nina ushahidi nacho kabisa. Hapo majuzi huyu bosi alikuja hapa hotelini na kumtaka rafiki yangu, kwavile huyu bosi ana hela yule rafiki yangu hakutaka kupoteza hiyo bahati huku tukijipa moyo kuwa huenda zile zilikuwa stori tu kwani tushamuona mara kadhaa akija hapa na mkewe kipindi kile wakati mkewe ni mjamzito.
Rafiki yangu aliondoka vizuri na huyu bosi ila kesho yake alinipigia simu huku analia, ikabidi niage ofisini na kwenda kumuangalia. Alinielezea mambo ya kusikitisha sana aliyofanyiwa na huyu bosi na alipomaliza kunielezea tu ni hapo hapo akafa. Kwakweli nilichanganyikiwa dada usione hivi"
Sakina akaanza kidogo kuvutiwa na maelezo ya huyu dada kisha akajikuta akimuuliza kwa makini,
"Pole sana kwa kumpoteza rafiki yako, ila alikupa maelezo gani?"
Yule mdada alianza kumueleza Sakina vile alivyoeleza na rafiki yake ambaye ni marehemu.
Sakina akashtuka sana kwani aliona wazi ni jinsi gani haya maelezo yanaendana na yale waliyopewa na marehemu Amina. Akajikuta akiwa na mashaka kuwa huenda Sam ndiye aliyemdhuru Amina na ndiomana kaamua kuwasaidia kwa urahisi kabisa bila ya tatizo lolote.
Sakina aliganda kwa dakika kadhaa akitafakari kile alichoambiwa hata yule aliyemwambia naye akamshangaa,
"Dada mbona umekuwa kimya tena?"
"Mmh wee acha tu, kuna kitu nafikiria hapa ila asante sana kwa taarifa"
Kisha Sakina akaenda kujisaidia na kurudi kule walipo wakina Sabrina.

Sakina alikaa pale akimuangalia Sam bila ya kummaliza na alimuangalia Sabrina aliyeonekana kwa sura mbili yani sura ya furaha na sura ya mashaka. Jeff ndio kabisa kwani alionekana yupo kama hayupo, kisha walipomaliza waliinuka ili kuondoka ila Sam aligundua mashaka aliyokuwa nayo Sakina kwa wakati huo kwani aliweza kuitazama sura yake vilivyo kisha akamuuliza,
"Una tatizo shemeji?"
Sakina akajibu kwa sauti ya kujishtukia,
"Hapana sina tatizo lolote shemeji"
"Usijali kitu Sakina, pale kwako patakuwa salama kabisa ila kama nilivyokwambia subiri wiki ipite ndio uende"
Sakina aliitikia ila alikuwa na mawazo mengi sana kumuhusu Sam kuwa kwanini amempa itikadi kama za kiganga vile kuwa asubiri wiki ipite. Alikosa jibu kabisa, safari nayo ya kurudi ikaanza na wote kuingia ndani ya gari kwaajili ya kurudi.

Nyumbani kwakina Sabrina siku hiyo usiku alirudi baba wa Sabrina na kumfanya mama wa Sabrina afurahi sana na kumkaribisha mumewe huku wakiongea mawili matatu.
"Sabrina yuko wapi?"
Mama Sabrina aliinama chini na kuanza kujieleza kuwa Sabrina amechukuliwa na mumewe,
"Kwanini umemruhusu mtoto Joy? Si uliona kabisa akili ya yule mwanaume ilivyokuwa jamani!"
Baba wa Sabrina alionekana kuchukizwa sana na kitendo cha Sabrina kurudi kwa Sam.
"Sikia Deo, kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa. Mema mangapi yamefanywa na yule kijana kwetu? Yani tumchukie sababu ya baya moja tu jamani? Hebu tufikirie na utu kidogo mume wangu, kwanza wale wanawatoto tayari na wanapendana. Tusiwafanyie hivyo"
Deo akafikiria na kukubaliana na mkewe kuhusu hilo swala, pia mama Sabrina akamueleza mumewe kuhusu wakina Sabrina kuhama walipokuwa wakiishi awali kisha Deo akasema,
"Ila itabidi nikawaone kwanza huko walipo"
"Hilo halina tatizo na itakuwa vyema tukienda wote"
Muda kidogo baba Sabrina akapokea simu ya kikazi Arusha, alipomaliza kuongea nayo akamwambia mkewe,
"Yani hii kazi yangu haifai kabisa kila siku nasafiri, yani siwezi kuwaruhusu watoto wangu wa kiume kufanya kazi ya namna hii kabisa maana hata huwezi kufurahia na familia yako. Kesho nasafiri tena mke wangu"
Mama Sabrina alimuitikia tu kwani ilishakuwa kawaida sasa kwa yeye kuishi mbali na mumewe.
Kwahiyo wakaongea pale na mwisho wa siku wakaenda kulala tu.

Kulipokucha kwa upande wakina Sabrina ni kuwa Sam aliamka asubuhi na mapema na kwenda zake kwenye kazi na biashara zake kama kawaida tena ukizingatia kuwa jana yake hakwenda popote zaidi ya hotelini usiku kutokana na matatizo yaliyompata.
Kwa upande wa Sakina, bado alikuwa na maswali mengi sana na akaona ni vyema ampate mtu wa kumshauri kwahiyo akatoka na kumuaga Sabrina,
"Unaenda wapi sasa? Kumbuka Sam amesema usiende kwako dada mpaka wiki ipite"
"Siendi kwangu, kuna mahali tu kwa ndugu yangu naenda"
Sabrina hakuweza kumzuia zaidi kwahiyo akamuacha aende.

Sakina akiwa kwenye daladala alikuwa na mawazo sana, akaona vyema aende kwanza kwa mama Sabrina ili akapate ushauri huko na ajue kwa undani kuwa ni kitu gani kilitokea wakati hayupo.
Alipofika kwa mama Sabrina alikuta kufuli kwenye geti ikiashiria kwamba hakuna mtu mule ndani.
Sakina alivyoona vile akaamua kwenda nyumbani kwake japo kuchungulia tu.

Alipoikaribia nyumba yake aliona ukimya uliotawala katika eneo lile, alipoangalia pembeni akaona kile kitambaa chekundu kilichowekwa na vipande vya nazi pembeni.
Mara akaanza kuhisi kizunguzungu na kuanguka pale pale.


Alipoikaribia nyumba yake aliona ukimya uliotawala katika eneo lile, alipoangalia pembeni akaona kile kitambaa chekundu kilichowekwa na vipande vya nazi pembeni.
Mara akaanza kuhisi kizunguzungu na kuanguka pale pale.
Hapakuwa na msaada wowote kwani hakuna mtu aliyekatisha eneo lile kwa muda ule na kumfanya Sakina awe pale pale chini kwa muda mrefu.

Mama Sabrina akiwa ametoka kumsindikiza mumewe, alijikuta roho yake ikimshinikiza kuwa aende akachungulie nyumbani kwakina Sakina kuwa huenda amerudi.
Alipofika akashangaa kumuona Sakina chini akiwa hajitambui, ikabidi aite watu na kuwaomba msaada. Ni wachache waliosogea kusaidia hata kuita gari ili wamuwahishe hospitali ila wengine hawakutaka hata kusogelea eneo lile wakiamini kwamba Sakina ni mchawi kutokana na maneno waliyoyapata siku ya kifo cha Amina.

Walipofika hospitali, Sakina akapelekwa moja kwa moja kwa daktari ambapo akatundikiwa dripu ingawa bado alikuwa hajazinduka.
Mama Sabrina alikuwa nje ya chumba cha daktari huku akiwaza kilichompata Sakina kwani hakupata jibu kabisa, muda kidogo Sakina akatolewa kwa daktari na kupelekwa kwa wagonjwa mahututi kwani hakuwa na fahamu kabisa.
Hali hiyo ilizidi kumtisha mama Sabrina na kukosa hata wa kumsaidia pale.
Alijikuta akitafakari mtu anayeona ni rahisi akimpigia simu na kuja kumsaidia.

Jeff alipotoka chumbani akashangaa kumuona Sabrina mwenyewe na kumuuliza,
"Eti mama yuko wapi?"
"Ametoka kidogo"
"Ametoka! Ameenda wapi? Au kaenda nyumbani?"
"Hapana, nimemuuliza hapa kasema anaenda sijui kwa ndugu yenu gani huko kumsalimia. Kwani nikamkumbusha pia kuwa kaambiwa asiende kule kwake hadi wiki iishe."
"Ngoja nijaribu kumpigia nijue alipo"
Jeff akajaribu kumpigia na kuona kimya, ndio hapo mashaka na wasiwasi ukaongezeka.

Sam akiwa ofisini kwake sasa ndipo akapokea simu kutoka kwa mama mkwe wake ikimuelezea hali iliyotokea,
"Naomba uje unisaidie baba, Sakina kapatwa na matatizo nipo naye hospitali huku"
Sam akashangaa kuwa imekuwaje tena Sakina aliyemuacha nyumbani kuwa huko? Akajiuliza kuwa ni kitu gani kimetokea mpaka ikawa hivyo.
Aliona maswali yake yakikosa majibu hivyo akaamua kutoka pale ofisini kwake na kuelekea huko hospitali alikoelekezwa.

Alipofika hospitali alimkuta mama Sabrina akiwa pale nje na kuanza kumuuliza kilichotokea,
"Kwakweli sijui baba angu, yani mie leo asubuhi nilitoka kumsindikiza baba yenu alikuwa anasafiri. Niliporudi nyumbani nikahisi moyo ukinituma kuwa nikachungulie kwa Sakina, na kweli nimeenda na kumkuta chini hajitambui kabisa ndio nikaita watu tukasaidiana kumleta hospitali"
Sam akafikiria kidogo bila ya kumjibu mama Sabrina, kisha akachukua simu yake na kumpigia Sabrina na kusogea pembeni ili aweze kuongea nae,
"Sakina yuko wapi?"
"Ametoka"
"Nani aliyemruhusu kutoka jamani? Mi nilisemaje jana? Mbona mnapenda kuchukua maamuzi ya haraka hivyo?"
"Mie sikuweza kumzuia jamani, yule si mtoto mdogo"
"Unajua kilichompata sasa au unaongea tu"
Hapo Sabrina akashtuka na kuuliza kwa makini kuwa Sakina kapatwa na nini.
Sam akamueleza kuwa wapo hospitali muda huo na huyo Sakina ni hajitambui kabisa.

Sabrina alishtushwa sana na ile taarifa na kuamua kumwambia Jeff ambaye naye alihisi kuchanganyikiwa kabisa na kumpigia tena Sam hospitali ilipo kisha Jeff akaondoka pale nyumbani akielekea hospitali kumuona mama yake.
Pale nyumbani alibakia Sabrina na watoto wake ambapo Cherry alikuwa akicheza tu kama kawaida na huyu mdogo alikuwa amelala.
Sabrina alitulia kimya na kukaa kwenye kochi, mara akamsikia Cherry akisema
"Mama, bibi mbishi"
Sabrina alishtuka na kumuangalia vizuri yule mwanae kisha akamuuliza kwa mshangao,
"Umesemaje?"
Cherry akacheka kitoto kisha akaendelea kucheza kama kawaida.
Sabrina alimuangalia mwanae bila kummaliza kwani ni wazi hakuweza kuongea vizuri aliweza kusema mama na baba tu ila huu uwezo wa kuunganisha neno bibi mbishi kautoa wapi? Na kwanini aseme bibi mbishi? Sabrina alijikuta akimuangalia mwanae Cherry tena na tena ila Cherry aliendelea kucheza bila habari.

Sam akiwa kule hospitali, akili yake ikafanya kazi haraka sana kuwa lazima amtoe Sakina pale hospitali kwani akiendelea kuwa pale lazima atakufa tu kwa zile sindano za hospitali.
Kwahiyo Sam akaenda kuongea na daktari na kumpa pesa kidogo ambapo daktari akakubali kuwa mgonjwa akachukuliwe tu.
Kisha mgonjwa akatolewa na kwenda kuwekwa kwenye gari ya Sam.
Mama Sabrina akashtuka na kuuliza,
"Vipi tunamuhamisha hospitali?"
Sam akaitikia ndio, muda kidogo Jeff nae akawasili na kuwakuta pale wakianza kuondoka ikabidi nae apande kwenye gari kuendelea na safari kwani alijua kuwa mama yake anapelekwa hospitali nyingine.
Jeff alimuangalia mama yake kwa masikitiko sana kwani alionekana kutokuwa na fahamu kabisa.

Sam alipeleka gari hadi nyumbani kwake, Jeff akashangaa kuwa kwanini wamemrudisha nyumbani,
"Mbona tumekuja huku?"
"Mama yako kakosea masharti na kama tukiendelea kumuacha hospitali basi ujue wazi tunampoteza"
"Na je hapa nyumbani?"
"Ngoja tumuingize ndani halafu nitakueleza vizuri kwani naona sasa ni ngumu sana kwako kunielewa"
Wakasaidiana kumuingiza ndani, mama Sabrina ndio alikuwa akishangaa kabisa, Sabrina nae akawashangaa pia ila wakina Sam wakampeleka Sakina moja kwa moja kwenye chumba alichokuwa analala mahali hapo.
Kisha wakatoka nje na kumuacha humo, kila mmoja alitaka kauli toka kwa Sam kuwa ni nini cha kufanya.
Mama Sabrina ndio kabisa hakuelewa kitu ingawa alifurahia kuwaona wajukuu wake.
Sam alikaa kimya pale sebleni kwa muda, Jeff alihitaji kujua hatma ya mama yake, muda kidogo Sam akainuka na kuelekea chumbani kwake. Ikabidi Sabrina amuulize mama yake kilichotokea, naye akawaeleza kama alivyoshuhudia.
Sabrina alisikitishwa sana kujua kwamba Sakina alienda nyumbani kwake ingawa alimkataza.
"Mungu atusaidie apone tu"
Mama Sabrina nae akatoa ushauri,
"Jamani kama hayo mambo ni ya kishirikina mnaonaje tukampeleka kwa wanamaombezi ili aombewe jamani?"
Jeff na Sabrina wakatazamana bila hata ya kuchangia pointi kwa kile kilichoongelewa.
Sam naye akatoka pale sebleni na kuwaambia,
"Sakina atazinduka ila akili yake haitakuwa sawa kwa kipindi hiki, itabidi tuwe nae makini sana"
Kisha akamuomba mama mkwe wake arudi nyumbani tu kupumzika, na akamwambia Jeff ndio afanye hiyo kazi ya kumrudisha mama Sabrina nyumbani kwa kutumia gari ya Cherry.
Hakuna aliyepinga kwani wote hawakuwa na uwezo wa kupinga mawazo ya Sam ukizingatia ndiye anayetambua yote anayoyafanya kwa kipindi hiko.
Kisha Jeff akatoka na mama Sabrina na kuondoka nae.
Walipoondoka tu, Sam akamuomba Sabrina aende dukani akamnunulie maziwa, Sabrina nae hakuweza kupinga kwavile alihisi kuwa huenda ikawa dawa kwa tatizo lililomfika Sakina.

Sabrina akiwa njiani kuelekea dukani akili yake ikachemka kidogo na kuona kama kuna mchezo unataka kuchezwa na Sam, sababu kwanini amwambie mama yake apelekwe na Jeff halafu kisha amuagize yeye dukani.
"Mbona mara zote huko dukani huwa anaenda mwenyewe! Kwanini leo aniagize mimi? Lazima kuna kitu Sam anataka kufanya. Je ni kitu gani hicho hadi asitake kionekane? Huyu Sam mbona ana mambo ya ajabu jamani, yani sielewi kitu mimi kwakweli"
Kwavile dukani kwenyewe hakuwahi kwenda, akashangaa umbali wa maduka kwenye mtaa ule na kumfanya azidi kupatwa na mashaka kuhusu kinachofanywa na Sam muda huo.
Akatamani ageuze akashuhudie, ila kwavile alishafika mbali ikabidi tu akubaliane na hali halisi kuwa liwalo liwe.

Mama Sabrina nae akiwa njiani na Jeff aliamua kumuuliza maswali kadhaa Jeff,
"Hivi unamuonaje Sam? Kwanini kaniambia nirudi nyumbani?"
"Kwakweli hata mimi binafsi huwa simuelewi, unajua yule anaelewana na Sabrina tu labda siku ukipata muda uzungumze nae"
"Sasa kwanini yule mgonjwa amuweke ndani? Jeff kumbuka yule Sakina ni mama yako na tukimpoteza hatutampata mwingine!"
"Naelewa hilo, ila ni yeye Sam aliyempa onyo mama la kutokwenda nyumbani hadi wiki iishe sasa sijui vipi mama akaenda. Nadhani Sam anajua cha kufanya ili mama azinduke ndiomana kamtoa hospitali"
Mama Sabrina alisikiliza haya maelezo ya Jeff na kustaajabu kuwa ni jinsi gani wamekuwa na imani kubwa kiasi kile juu ya Sam, ila hakutaka kuongea zaidi hadi wakafika nyumbani kwake.

Sabrina aliamua kurudi nyumbani sasa kwani alizunguka maduka kadhaa ya pale bila ya kupata hayo maziwa aliyoagizwa na Sam.
Aliporudi nyumbani alishangaa kumuona Sakina yupo tayari kwenye kochi tena akiwa mzima kabisa huku Cherry akiwa pembeni yake akimrukia rukia.
Sabrina alimuangalia Sakina na kujaribu kumuuliza ila Sakina alikuwa kimya tu.
Sam naye akatoka chumbani ambapo moja kwa moja Sabrina akamuuliza,
"Mbona Sakina mwenyewe haongei?"
"Kwani nilisemaje mwanzo? Si nilisema kuwa atapona ila akili yake haitakuwa sawa"
"Kwahiyo ndio hata kuongea hatoweza?"
"Mtu akili haipo sawa sasa ataongea nini? Si atakuwa kama chizi? Ni mara mia awe katika hali hiyo hiyo ya ukimya kwani akiongea ataongea makorokocho na kuwa kama chizi"
"Haya, na umewezaje kumzindua?"
"Wewe shukuru kuwa amezinduka, hayo maswala ya umewezaje waachie wahenga"
"Na hayo maziwa uliyoniagiza hata sijayapata"
"Basi hakuna tatizo, siyahitaji tena"
"Kwahiyo ulitaka kunihangaisha tu!"
Cherry akawatazama na kucheka, ambapo Sabrina akamtazama mtoto wake yule na kujiuliza kilichomchekesha ni kitu gani, kisha akamuangalia Sam na kumwambia
"Halafu huyu mtoto ananishangaza sana siku hizi, ona hapo sasa amecheka nini? Au amecheka ulivyonihangaisha?"
"Kheee Sabrina vipi mama hutaki mtoto acheke?"
"Mmh jamani Sam, kucheka sio tatizo ila hu yu mtoto ananishangaza siku hizi mfano leo kaongea eti bibi mbishi, amewezaje huyu kuunganisha maneno hivyo?"
"Kwahiyo hutaki mtoto aongee, mbona umekuwa na mambo ya ajabu Sabrina? Hivi hujui kama kuna watu wanashinda kwa wa waganga ili watoto wao waweze kuongea. Wewe mwanao anaongea unaona makubwa, usiwe na mawazo hasi kila siku. Nakuamini sana Sabrina wewe ni mwanamke shupavu ndiomana nimeishi nawe hadi leo"
Sabrina akaingiwa akilini na maneno ya Sam kisha kuachana na mawazo ya tofauti kabisa.

Jeff naye aliporudi aliona hali halisi ya mama yake na kuambiwa anavyotakiwa kuishi nae hadi kipindi atakapo rudiwa na akili yake kabisa.
"kwahiyo kuna kipindi akili yake itarudi?"
"Ndio na atakuwa mzima kabisa ila sio kwa sasa"
"Na huko nyumbani ndio turudi kama ulivyosema?"
"Ndio ila kuna utaratibu nitauangalia kwanza."
Kwavile muda nao ulikuwa umekwenda wote wakaamua kwenda kulala kama kawaida na wala Sam hakumlazimisha tena Sabrina kwenda kulala nae chumbani ila tu alimpa maagizo ya kwenda kumuangalia Sakina mara kwa mara.

Kulipokucha, Sam alijiandaa kwaajili ya kwenda zake ofisini kwake kama kawaida na kumuaga mkewe.
"Kama nilivyokwambia jana, mnatakiwa kuwa makini sana na Sakina na muwe nae karibu kama mtoto"
"Hilo sio tatizo Sam"
Kisha Sam akamsogelea Cherry ambaye naye alikuwa macho kwa wakati huo halafu akambusu kwenye paji la uso na kuondoka zake.
Sabrina alitulia tu akiwaangalia baba na mwana wakiagana.

Mchana wa siku hiyo wakiwa wamekaa sebleni, Sabrina aliamua kumueleza Jeff kuhusu mambo anayoyafanya mtoto wao Cherry.
Jeff nae akauliza,
"Na kwanini Sam kampenda sana huyu mtoto?"
"Sijui kwakweli, na jana huyu mtoto ameongea hadi nimemshangaa"
"Kuongea sio tatizo si ndio anajifunza maneno huyu, ila bado nashangaa upendo wa Sam kwa huyu mtoto"
Mara Cherry nae akawajibu,
"Kwani akinipenda kuna tatizo?"
Jeff na Sabrina walitazamana kwa mshangao.


Mara Cherry nae akawajibu,
"Kwani akinipenda kuna tatizo?"
Jeff na Sabrina walitazamana kwa mshangao.
Kisha wakamtazama Cherry aliyeonekana akiendelea kucheza bila ya habari yoyote.
Jeff akamuuliza Sabrina,
"Hivi nilichosikia kimetoka kwa huyu mtoto au ni nini?"
"Ndio ushangae sasa na ninapokwambia kitu uelewe, mimi siwezi ongea jambo hovyo hovyo. Nilimsikia na ndiomana nikakwambia"
Jeff akamtazama tena Cherry na kufanya kama anamuita ili asogee karibu ambapo Cherry nae akasogea alipo Jeff.
Kisha Jeff akamuuliza Cherry,
"Kumbe unaweza kuongea mwanangu?"
Cherry alionekana kucheka kitoka na kujizungusha zungusha kisha akatoka pale alipo Jeff na kurudi kucheza.
Jeff akamtazama tena Sabrina ambapo Sabrina alicheka huku akitikisa kichwa kama kusikitika kisha akasema,
"Yani haya makubwa, ni kweli watoto wengine huwa wanawahi sana kuongea ila si kwa stahili hii ya kuunganisha maneno kama mtu mzima jamani"
"Sasa unamaana gani Sabrina?"
"Sina maana yoyote ila sielewi kitu kuhusu mwanangu kwani nabakia nikimshangaa tu."
"Usijali kuna kitu nitajaribu kufanya"
Gafla wakamsikia Cherry akicheka na kusema,
"Huwezi"
Sabrina na Jeff walizidi kupatwa na mashaka dhidi ya mtoto wao, Sabrina aliinuka na kumshika Jeff mkono kisha akasogea nae pembeni na kumuuliza,
"Unamuelewa kweli?"
"Simuelewi kwakweli"
Jeff alikuwa akisikitikia tu majibu ya mtoto wao kwani alionekana kutoa majibu yaliyonyooka kama ya mtu mzima.
Maongezi yao yakaishia hapo huku kila mmoja akiwaza ni kipi kinaendelea kwa yule mtoto.

Sam aliporudi nyumbani, alimnyanyua Cherry na kwenda naye chumbani ambapo walikaa huko hadi muda ambao Cherry alilala kisha Sam akampeleka kwa Sabrina akalale.
Kesho yake Sam alifika pale na binti ambapo akamtambulisha kwa Sabrina kuwa amemleta pale ili awe anasaidia kazi.
"Anaitwa Keti huyu binti, nimeona unahangaika sana peke yako mke wangu"
Sabrina alifurahia ule ujio wa Keti kwani ni kweli kazi zilikuwa zikimbana sana peke yake ila hakujua kuwa Sam amempeleka yule msichana wa kazi pale kwa lengo lipi ila alipofikiria kidogo akili ikacheza na kumwambia kuwa licha ya yule msichana wa kazi kuwa pale kwaajili ya kusaidia kazi basi huenda pia amempeleka ili awe anampa taarifa kinachotendeka kati yake na Jeff.
Kwahiyo Sam alipoondoka tu, Sabrina akampa Jeff taarifa hiyo ili wawe makini mule ndani.

Maisha yaliendelea ila Sabrina hakupendezewa kabisa na ukaribu uliokuwepo kati ya Jeff na Keti kwani alimuona kama Keti akimuangalia Jeff kwa jicho la tamaa sana.
Ikabidi amtahadharishe Jeff,
"Kuwa makini na huyu mdada bhana, mimi simuamini kwakweli"
"Usiwe na mashaka Sabrina, niamini mimi siwezi kufanya jambo lolote baya"
Kabla hata hawajamaliza maongezi yao, Keti nae akawasogelea kanakwamba kuna kitu anahitaji.
Hii hali haikumpendeza kabisa Jeff, alijiona kukosa uhuru na pia alizidi kutokumuelewa mtoto wao Cherry.
Wazo la kuondoka na Cherry likamjia, hivyobasi akatamani tu apate siku ya kumuomba Sam ruhusa ya wao kurudi nyumbani kwao wakiwa na Cherry kwani alitaka sana kujua kwanini yule mtoto anaongea maneno ya kiutu uzima tena kwa kujiamini tofauti na umri wake.

Ilipopita wiki sasa, Jeff akamuuliza Sam kama anaweza kurudi na mama yake nyumbani,
"Ndio inawezekana ila ni nani atakayekuwa karibu na mama yako hapo nyumbani kwenu?"
"Nitamtafuta mtu wa kunisaidia kwa hilo ila ingekuwa vyema kama ningeenda na huyu Cherry ili hata angalau awe anampa kampani"
Sam akacheka na kusema,
"Hebu acha kunichekesha Jeff, yani niwape mwanangu mkaishi nae nyie! Are you serious kweli? Mwanangu mimi nimeshindwa hata kumuacha kwa bibi yake kule niwape nyie? Hapana haiwezekani kabisa. Siwezi kukubali mwanangu atoke kwenye himaya yangu, labda ukatafute mtu wa kukaa na mama yako na huyo mtu nitamlipa ila sio kumchukua mwanangu"
Jeff akatafakari kidogo na kuona ni vyema akakae na mama yake nyumbani kwao kwani hata pale kwa Sam hakuwa huru sana na hakuweza kukaa karibu na Sabrina kama mwanzoni hivyo akaona wazo la yeye kwenda nyumbani kwao na mama yake ni vizuri sana na ndio hapo alipochukua jukumu hilo la kuondoka na mama yake ambapo Sam alijitolea kuwapeleka huku akihakikisha usalama wao.
"Jeff usiwe na shaka yoyote, tafuta tu mdada wa kazi mimi nitamlipa halafu wewe nitakuajiri kwenye kampuni yangu. Yani usiwe na mashaka kabisa, hakikisha tu unampata dada wa kukaa nyumbani na mama yako"
Jeff aliposikia swala la kupewa kazi na Sam ndipo alipoamua kutoa hoja ingawa muda mfupi uliopita alikuwa amepooza kutokana na majibu aliyopewa na Sam kuhusu Cherry,
"Basi itakuwa vyema kama tukienda na huyu mdada wa kazi uliyemleta hapa kwako kwani naona amemzoea vizuri mama yangu"
"Aah hapo umenikumbusha kitu kweli, ngoja nizungumze na huyu mdada. Najua atakubali tu"
Basi Sam akamuita yule dada ma kumueleza ambapo hakuwa na pingamizi lolote lile basi wakajiandaa na kumsaidia Sakina kupanda kwenye gari kisha Jeff akaingia ndani kumuaga Sabrina ambapo Sabrina alionekana kununa tu mpaka Jeff aliamua kumuuliza Sabrina kilichomfanya anune.
"Mbona upo hivyo Sabrina nini tatizo?"
"Yani Jeff siku zote upo hapa, hata kuniambia kama mtaondoka leo hapana ila saizi ndio umeona umuhimu wa kuniaga kweli?"
Muda huo yule dada wa kazi nae akaja kumuaga Sabrina kuwa naye anaondoka nao.
"Nani kasema kuwa na wewe uende?"
"Kaka ndio kaniambia"
"Kwanini sishirikishwi jamani! Na kazi humu atanisaidia nani? Haiwezekani Keti, wewe unatakiwa ubakie hapa"
Sam akaja na kuwashtua kuwa waende, Sabrina alitamani kuzuia ila alijua wazi hataweza kwani Sam huwa akiamua kitu kaamua.
Ila akamuuliza tu,
"Mbona gafla lakini jamani Sam? Mbona hukunitaarifu? Halafu Keti mnaondoka nae sasa kazi humu atanisaidia nani?"
Sam akacheka kisha akamwambia Sabrina,
"Nitakuja tuongee vizuri nikirudi"
Kisha kumtazama Keti na Jeff kuwa waende.
Sabrina alitoka nje na kumuaga Sakina kisha akarudi ndani na wao kuondoka.

Sabrina alibaki na mawazo tu kuwa kwanini mambo yale yamekuwa haraka kiasi kile.
"Mbona Jeff kachukua uamuzi wa haraka vile, na kwanini Sam awaambie kuwa waende na Keti? Kuna nini hapa kati?"
Akawaza sana bila ya kupata jibu huku akifikiria jinsi Keti alivyokuwa akimuangalia Jeff pale ndani, jinsi alivyokuwa akionyesha matamanio ya wazi wazi kwa Jeff halafu ndio wakaishi huko wawili kwakweli alihisi kupokonywa tonge mdomoni na moyo ukamuuma sana.

Sam aliwafikisha wakina Jeff kwao na walifika salama kabisa bila ya tatizo lolote.
Kisha Sam akatoka pale na kuwaaga huku akisema kuwa anaelekea kwanza kwa mkwe wake kumsalimia.
Keti nae alifurahi pale kwani alijua wazi kuwa ni lazima majukumu yatakuwa yamepungua ukizingatia hapo kazi yake kubwa itakuwa ni kumtazama Sakina.
Jeff sasa aliamua kumuelekeza Keti vyumba vyote vya mule ndani na kumwambia majukumu ya pale yatakavyokuwa.
"Hakuna tatizo, nadhani kwa hii wiki moja tu umeweza kuona utendaji wangu wa kazi kwahiyo hilo sio tatizo na ninakuhakikishia wazi kuwa mama yupo kwenye mikono salama"
Wakaongea kidogo pale na kuendelea na shughuli zingine.

Sam alipita kwa mama Sabrina ila hakumkuta na kuamua kuondoka tu.
Akiwa njiani, simu yake ikaita alipoangalia ilikuwa ni namba ngeni na kuipokea ila akagundua kuwa mpigaji alikuwa ni Aisha yani yule binti aliyekuwa akiishi na Neema.
"Niambie tu Aisha"
"Mbona umekuwa kimya toka siku ile?"
"Ni kweli, ila kuna matatizo kidogo yalitokea hapo kati yani kichwa changu kikavurugika sana"
"Pole jamani, matatizo gani tena?"
"Mama Jeff alipatwa na matatizo akalazwa yani leo hapa nimetoka kuwarudisha nyumbani kwao. Yani mambo yameingiliana sana, ila kama utakuwa na muda basi tuonane kesho jioni"
Aisha alikubaliana na Sam pale kisha akakata simu ambapo kwa muda huo Sam alikuwa akielekea nyumbani kwake.

Sabrina bado hakuridhishwa na kile kilichotendeka siku hiyo na aliona kamavile Sam kamfanyia makusudi tu ili amkomeshe.
Ni hapa alipotafakari sana na kuamua kuchukua simu kisha kumpigia Jeff,
"Unajua Jeff mimi sijawaelewa kwakweli, kwanini mmeharakisha hivyo kuondoka?"
"Sikia Sabrina, sio kwamba tumeharakisha hapana ila muda nao ulifika. Kumbuka Sam alisema kuwa baada ya wiki tunaweza kurudi nyumbani ila angalia hapo ni karibia wiki mbili tupo hapo na huku tukiendelea kushuhudia maajabu ya mtoto wetu Cherry"
"Hata kama, na kwanini uamue kuondoka na Keti?"
"Sabrina kwanza elewa sikuwa na ubaya wowote, nilikuwa tu namuomba ruhusa Sam nikashangaa kashaamua na kuturudisha. Lengo langu ilikuwa ni kuondoka na Cherry ila majibu niliyopewa wee acha tu hadi nikaamua kuondoka na Keti"
"Majibu gani ulipewa?"
Kabla Sabrina hajajibiwa tayari Sam alikuwa ameingia ndani na kumfanya Sabrina aikate ile simu ambapo Sam alimsalimia kisha akaelekea chumbani kwake.

Muda kidogo Sam akatoka chumbani na kukaa sebleni kisha akamwambia Sabrina,
"Niulize maswali yako yote nipo tayari kukujibu"
"Sam ulichofanya sio sawa kwakweli, mimi ni mke wako nastahili kushirikishwa kila kinachoendelea humu ndani"
"Kitu gani hujashirikishwa?"
"Kwanini umemuondoa Keti bila hata kuniambia jamani?"
"Kwani kuondoka kwa Keti wewe kumekupunguzia nini?"
"Kumenipunguzia nini? Jamani Sam, Keti si alikuwepo hapa akinisaidia kazi jamani!"
"Kwani kabla ya Keti, ni nani alikuwa akikusaidia kazi?"
"Nilikuwa nafanya mwenyewe"
"Sasa tatizo ni nini?"
"Sam kumbuka wakati nimekuja hapa ile siku ya kwanza uliniambia kuwa kuna mdada wa kazi alikuwa anakuja kufanya kazi na kuondoka halafu ukaahidi kumleta. Nikajua alipokuja Keti ndio umemleta, vipi tena leo unanigeuka?"
"Kwahiyo tatizo sio Keti ila tatizo ni mdada wa kazi basi usijali kesho nitakuletea mwingine"
Kisha Sam akainuka na kuelekea tena chumbani kwake.
Kwakweli majibu ya Sam yalimfanya Sabrina apatwe na hasira maradufu kwani hakutarajia kupewa majibu ya namna ile.
Na hapo akapata jibu kuwa lazima Sam kafanya hivyo kumkomesha tu huku akihhsi kuwa huenda Sam ameongea na Keti kuwa akamshawishi Jeff ili yeye aumie tu.

Usiku ulipofika, Sabrina hakujisikia hata kulala kwani mawazo yake bado yalikuwa kwa Jeff na Keti kwani muda mwingi alihisi akisalitiwa.
Ndipo usiku ule alipoamua kumpigia tena simu Jeff,
"Sabrina unajua mi nakuhurumia sana, usipende kunipigia simu usiku maana utashindwa cha kujitetea hapo endapo Sam akakufuma"
"Hapana Jeff, napatwa na hisia mbaya juu yako jamani. Kwanini uondoke na Keti?"
"Sabrina naomba usiwe na mashaka yoyote mama yangu, hakuna kitakachotokea kati yangu na Keti. Yupo hapa kwa lengo moja tu la kumuhudumia mama yangu basi na si vinginevyo. Hata hivyo Sabrina hujui tu nawaza nini juu yako, nawaza sana jinsi ya mimi na wewe kuweza kuondoka kwenye hiki kifungo tulichokuwa nacho. Tafadhari usiwe na mawazo mabaya. Mimi nakupenda na nitazidi kukupenda, usiongee neno lolote ila nakuomba ukate simu na ulale."
Sabrina akatii na kukata ile simu kisha akalala huku akiwa na imani kwa yale maneno aliyoambiwa na Jeff kwa wakati huo.

Kulipokucha asubuhi na mapema, Cherry aliamka na kutoka chumbani kwa Sabrina kisha akaelekea chumbani kwa Sam.
Sabrina nae aliamua kuamka ili afanye kazi ndogo ndogo.
Wakati Sabrina akiwa sebleni, Sam nae akatoka akiwa tayari kashajiandaa kwaajili ya kwenda kazini ila kabla hajaenda akamwambia Sabrina,
"Nisikilize kwa makini Sabrina, upo hapa hadi leo kwavile nakupenda na licha ya hivyo ujue kuwa mtu pekee anayefanya nikujali hivi hadi sasa ni huyu mtoto Cherry. Hivyobasi nakuomba sana uniheshimu Sabrina, maswala yako ya kuongea na simu usiku sitaki na siku nikikukuta unaongea na simu usiku hata sijui nitakufanyaje ila kuwa makini mi natoka"
Kisha Sam akambusu Cherry kwenye paji la uso kwani alikuwa ametoka nae chumbani, kisha akawaaga na kuondoka.
Sabrina akapata picha moja tu kuwa Cherry ndiye aliyemwambia Sam kuwa yeye alikuwa akiongea na simu usiku.
Sabrina alimuangalia huyu mwanae bila ya kummaliza kisha akajisikia kumuuliza,
"Kwahiyo wewe ndio umemwambia baba yako kuwa nilikuwa naongea na simu usiku?"
"Ndio nimemwambia"
Sabrina alimuangalia huyu mwanae aliyeonekana kuongea kama mtu mzima, ikabidi naye amchukulie kama alivyo na kumuuliza.
"Kwanini umemwambia sasa?"
"Nimemwambia kwavile najua hapendi uongee usiku"
Sabrina aliamua kumkazia macho mwanae sasa na hapo akagundua hali ya tofauti kwenye macho ya mwanae na kumfanya ashtuke.


Sabrina aliamua kumkazia macho mwanae sasa na hapo akagundua hali ya tofauti kwenye macho ya mwanae na kumfanya ashtuke.
Kile kitendo cha kushtuka kwa Sabrina kikasababisha apate swali toka kwa mwanae,
"Kilichokushtua?"
Sabrina hakuweza tena kumtazama mwanae na kumfanya akwepeshe macho yake na kisha akaondoka pale sebleni na kuelekea jikoni huku akili yake ikiwa na mawazo mengi sana dhidi ya mwanae.

Sabrina akiwa jikoni alijikuta akiwa na mawazo mengi sana,
"Hivi huyu ni mtoto niliyemzaa mimi kweli? Kwanini kawa hivi jamani? Kwanini huyu mtoto wangu mdogo anijibu majibu ya ajabu kama mtu mzima? Imekuwaje kwa huyu mtoto jamani?"
Akakumbuka siku ya harusi yake na Sam kwani ndiyo siku aliyojifungua mtoto huyo.
Akakumbuka jinsi mwanae huyo alivyokuwa wakati wa utoto wake na kumfanya ahisi kwamba kuna kitu hakipo sawa dhidi ya mtoto wake.
Akayatafakari pia macho ya mwanae jinsi alivyoyaona muda mfupi uliopita na kujikuta akikumbuka kidogo stori za kutisha, hapo hapo akaamua kuachana na mawazo hayo kwani alijua lazima itamchanganya tu.

Jeff akiwa kwao ile asubuhi akapigiwa simu na Sam kuwa aende ofisini kwake.
Jeff hakutaka kuchezea bahati hiyo kwani muda huo alijiandaa na kuelekea ofisini kwa Sam ambapo alimkuta pale ofisini akimsubiri.
"Tena nilitaka kutoka ila kwavile nilikwambia uje sikuweza tena ikabidi tu nikusubirie uje. Karibu sana"
Jeff akafurahia ukaribisho ule aliopewa na Sam.
"Sasa nataka uanze kufanya kazi hapa kwenye ofisi yangu Jeff ili usihangaike tena au unaonaje?"
"Mbona nilishakubali toka jana, tena nashukuru sana"
"Basi leo nitakupa mtu wa kukuonyesha kazi za hapa kisha kesho utakuja kuanza kazi rasmi sawa!"
Jeff aliitikia kwani kwa upande wake ile ilikuwa ni bahati kubwa sana ukizingatia kuna vijana wengi ambao wanatafuta ajira bila ya mafanikio ila yeye amepata ajira kwa Sam bila hata ya kumuomba kwani toka kipindi cha mwanzo alitamani ila alishindwa kumueleza Sam moja kwa moja.

Jeff alipomaliza kuelekezwa na kijana ambaye Sam alimkabidhi ikabidi aage na kuondoka sasa ila Sam alikuwa na kazi nyingi sana hata hawakuweza kuongea zaidi.
"Kesho uwahi tutaongea mengine hapo"
"Sawa hakuna tatizo"
Jeff alirudi kwao na kumkuta mama yake na Keti wakiwa sebleni kisha akamuona na Aisha.
"Khee Aisha!"
"Mbona unashangaa Jeff? Nimekuja kuwatembelea tu"
"Umejuaje kama tumerudi?"
"Jana niliwasiliana na shem Sam ndiye aliyeniambia kama mmerudi"
Jeff akatikisa kichwa kidogo kuashiria kama amemuelewa kisha akaelekea chumbani kwake.
Alikaa kitandani kwake na kutabasamu kidogo kwani kitendo cha kupata kazi kirahisi vile kilimpa furaha kwani alichowaza kwa muda huo ni kupata pesa kwani aliona kitu pekee kilichopungua katika maisha yake hayo ni hakuna kingine zaidi ya pesa tu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakutaka kuwa na mawazo dhidi ya binti yake Cherry kwani aliona wazi kuwa hata kama akiwaza haitamsaidia kitu.

Muda kidogo Aisha alimuita Jeff kwa lengo la kumuaga, naye Jeff hakusita kutoka na kumsindikiza.
Wakiwa njiani Jeff alimuuliza Aisha,
"Mbona leo umeondoka mapema?"
"Jana niliongea na Sam na akasema nionane nae leo jioni'
"Unaenda kuongea nae kuhusu nini hiyo jioni?"
Aisha akashangaa hili swali toka kwa Jeff na kumfanya apatwe na hisia kuwa huenda Jeff anampenda sasa amepatwa na wivu kusikia anaenda kuzungumza na Sam.
"Mmh ni mazungumzo tu Jeff"
"Yanahusu nini?"
Aisha akatabasamu tu kisha Jeff akamwambia tena,
"Kuwa makini Aisha usije sema hukuambiwa. Pesa, mali na dhahabu haviwezi kufikia thamani ya utu wako. Wewe ni mtu muhimu sana, jipende, jithamini na ujiheshimu"
"Mmh Jeff mbona umeongea yote hayo jamani! Yani kukwambia kuwa naenda kuonana na Sam imekuwa vibaya jamani?"
"Hapana si vibaya ila nimekwambia tu kama mtu wangu wa karibu."
Kisha Jeff akaagana na Aisha pale halafu yeye akarudi kwao.

Jeff aliporudi kwao akajikuta gafla moyo ukimuuma sana dhidi ya Aisha na kujikuta akitamani kumzuia Aisha kwenda kuonana na Sam,
"Mmh ila sidhani kama Sam atamfanyia Aisha kitu kibaya ila hata hivyo kwani Aisha hakumbuki kilichompata dada yake kweli? Eeh Mungu mnusuru Aisha"
Akafikiria tena kitu kidogo na akili ikaanza kucheza kuhusu kifo cha Amina huku akijipa jibu kuwa huenda Sam anamfahamu Amina na ndiye aliyemfanyia mambo mabaya ila tu hakuwa na uhakika na kitu anachokifikiria.

Sabrina alitamani apate mtu wa kumshirikisha kuhusu mwanae yani vile amuonavyo kwa kipindi hiko.
Akaenda tena sebleni huku akiwa na mawazo mengi.
Alikaa pembeni ya mtoto wake mdogo aliyekuwa amelala, kisha Cherry nae akamfata Sabrina na kwenda kukaa kwenye miguu yake, ni hapo Sabrina alipoamua kumuinua mwanae huyo na kumuweka kwenye miguu yake kwani hata afanyeje yule atabaki kuwa mwanae tu.
Cherry alipopakatwa, akaitumia fursa hiyo kumuangalia mama yake na kumuegemea, Sabrina aliweza kuhisi upendo alionao mtoto yule juu yake.
Kisha akapata tena wazo la kumtazama machoni ila kama mwanzo, macho ya mwanae yalimshtua na kumpa mashaka kiasi.
Muda kidogo Sam nae alikuwa amerudi pale nyumbani kwake, ni hapo Sabrina akaona ni vyema amuulize Sam kuliko kubaki nalo peke yake moyoni.
"Sam, hebu angalia macho ya Cherry yalivyo. Kwanini yapo tofauti na wengine? Na mbona mwanzo hakuwa hivyo?"
Sam akatabasamu kisha akamchukua Cherry toka mikononi mwa Sabrina na kuelekea nae chumbani tena bila ya kumjibu chochote Sabrina.
Kwakweli kitendo hiki kilimfanya Sabrina ashangae tu kwani hakutegemea kutokujibiwa chochote kwa wakati huo.
Hivyobasi akainuka na kumnyanyua yule mtoto wake mdogo na kwenda kumlaza chumbani kwake.

Sabrina akiwa chumbani akamsikia Sam akimuita.
Sabrina akatoka na kwenda alipoitwa ambapo alimkuta Sam sebleni,
"Sabrina, mtoto kalala na nimemlaza chumbani kwangu tafadhari muache mule mule hadi nitakaporudi"
"Khee unaondoka tena? Mi nilijua ndio umesharudi tayari!
"Nilikuwa nimesharudi kwakweli na sikuwa na ratiba ya kutoka tena ila kuna jambo naenda kufanya mara moja. Kwahiyo tutaonana badae"
Sam akatoka na kuondoka zake.
Sabrina alibaki mwenyewe kwani wanae walikuwa wamelala, yule mdogo alimlaza chumbani kwake na mkubwa chumbani kwa Sam kwa mujibu wa Sam.

Sam akiwa njiani kuelekea kwenye jambo alilotaka kufanya kwa wakati huo, akapigiwa simu na alipopokea akagundua kuwa ni Aisha.
"Unakumbuka ulisema kuwa tuonane leo jioni eeh!"
"Ooh dah bora umenikumbusha maana nilishasahau kabisa. Uko wapi sasa?"
Aisha akampa Sam maelekezo ya eneo alilopo kisha Sam akamwambia asubiri na kwenda kumfuata pale alipo.

Aisha alipanda kwenye gari ya Sam na safari ya kwenda hotelini ikafanyika.
Walipofika hotelini, Sam akakodi chumba na kumuomba Aisha waende wakaongee chumbani, Aisha nae hakuwa na wasiwasi wowote kisha wakapandisha pamoja hadi chumbani.
Wakati wanaongea, Sam aliamua kumuomba Aisha jambo moja tu huku akimuahidi kumbadilishia maisha yake,
"Kwahiyo nikikupa mapenzi tu ndio utanifanyia vyote hivyo?"
"Ndio Aisha, niamini mimi"
"Kwani mapenzi yangu mimi yana kitu gani kikubwa hadi unifanyie vyote hivyo Sam?"
Sam akakaa kimya kwa muda bila ya kujibu chochote, kisha Aisha akaendelea kuongea,
"Mimi ni mwanamke jasiri sana Sam, unadhani naweza kukubali kufanya mapenzi na mtu asiyempenzi wangu?"
Sam hakujibu kwa mara nyingine ila akavuta begi yake ndogo ambayo ametembea nayo na kutoa kibunda cha pesa kisha akamkabidhi Aisha.
Kwakweli pesa ni sabuni ya roho kwani pesa ile ilimfanya Aisha asahau kabisa msimamo wake na kujikuta akikubali kulala na Sam.

Kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo ambavyo Jeff aliumia moyo wake kuhusu Aisha na hakujua ni kwanini moyo unamuuma kwa kiasi kile, ila alipojaribu kupiga simu iliita tu bila ya kupokelewa na kumfanya akubaliane na hali halisi tu.
Akaamua kulala ila usingizi aliupata kwa shida sana kwani mawazo yake yalielekea kwa Aisha tu.

Sabrina akiwa nyumbani mwenyewe akajiuliza sasa ni kwanini Sam amlaze mtoto chumbani kwake? Hilo halikuwa tatizo ila tatizo lilikuwa ni kwanini aseme kuwa amuache mule mule hadi arudi?
Sabrina akawaza na kujipa jibu mwenyewe kuwa huenda Sam kasema vile ili mtoto asipate usumbufu.
Akafikiria pale na kuamua kwenda kumchungulia mwanae.
Alipoingia chumbani kwa Sam hakumuona Cherry kitandani wala nini na kumfanya ajiulize kuwa amemlaza wapi,
"Si amesema kuwa amemlaza humu chumbani! Mbona hayupo sasa?"
Sabrina akatoka mule chumbani ili amuulize Sam kwenye simu kuwa mtoto amemuweka wapi ila kabla hajapiga simu, Sam nae alikuwa amesharudi.
Kabla hata ya salamu, Sabrina alianza kwa kumuuliza Sam,
"Mtoto yuko wapi?"
"Si Cherry"
"Si yupo chumbani amelala!"
"Mbona nimeenda na sijamkuta"
"Nani aliyekutuma uende ukamuangalie?"
"Jamani Sam umechelewa kurudi, unadhani ni nani wa kumuangalia mtoto kama sio mimi?"
Sam hakumsikiliza zaidi Sabrina kisha akaenda zake chumbani kwake na kumuacha Sabrina pale sebleni huku akisubiria kuletewa mtoto wake.

Mawazo ya Sabrina yakazidi kutanuka sasa kwani akafikiria kuwa kama mtoto alilazwa kweli chumbani kwanini yeye asimkute. Na pia kwanini hajampa jibu lolote zaidi ya kwenda chumbani tu?
Wakati akifikiria hayo, Sam alitoka chumbani huku akiwa ameambatana na Cherry kisha akamwambia Sabrina,
"Mtoto huyu hapa, nenda kamlaze chumbani kwako sasa"
"Mbona mimi nilipoingia sikumkuta?"
"Labda macho yako yana makengeza"
Kisha Sam akarudi zake chumbani kwake na Sabrina nae akaenda chumbani pia.

Sabrina akiwa chumbani aliamua kumpigia simu Jeff na kumueleza kilichotokea siku hiyo na kuhusu macho ya Cherry,
"Yani macho ya mtoto yamenitisha Jeff, macho makali kama ya paka halafu yanacheza cheza"
"Yameanza lini tena mbona alikuwa sawa tu jamani!"
"Mmh leo nilipomtazama ndio nikagundua hilo swala"
"Basi usijali Sabrina, itabidi tufanye kitu"
"Tufanyeje sasa?"
Kabla Jeff hajaanza kumjibu Sabrina, tayari Sam alikuwa chumbani kwa Sabrina na kumpokonya ile simu na kuiweka sikioni mwake huku akimzuia Sabrina kupiga kelele.
Jeff nae bila ya kujua akajikuta akitoa maelezo,
"Mie nakwambia usijali, huyu Sam anataka kutuchezea akili tu juu ya huyo mtoto wetu, nitajua cha kufanya. Ila kumbuka kwamba nakupenda sana na hakuna mwanamke nitakayempenda kama wewe Sabrina"
"Eeh kumbe ndio mnachoongeaga eeh!"
Jeff alikata simu kwa haraka sana baada ya kusikia sauti ya Sam.
Kisha Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Chagua adhabu wewe mwenyewe. Nikuue au nilale na wewe."


Jeff alikata simu kwa haraka sana baada ya kusikia sauti ya Sam.
Kisha Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Chagua adhabu wewe mwenyewe. Nikuue au nilale na wewe."
Sabrina akakaa kimya kwa muda akifikiria zile adhabu alizoambiwa achague kwani aliona zikifanana ukizingatia kulala na Sam ni sawa na kuuwawa.
Kwahiyo Sabrina akakaa kimya bila ya kutoa jibu lolote ambapo Sam akamuuliza swali lingine,
"Kwani nilikwambia nini Sabrina kuhusu swala la kuongea na simu usiku? Haya yote tisa, kumi ni huyu mtu uliyekuwa ukiongea nae. Hivi unayajua maumivu ya mapenzi Sabrina? Hivi unajua ni jinsi gani anayekupenda anavyoumia tena kama mimi ambaye hata utamu wako sijaufaidi. Sasa una faida gani kwangu? Nimekwambia chagua adhabu, najua unaona hizi adhabu mbili nilizokutajia kuwa zinafanana ila kiukweli hazifanani kwani nikiamua kukuua kwa bastola hapa hutopata hata muda wa kusema kwaheri ila nikifanya nawe mapenzi utapata muda wa kuaga ndugu zako. Chagua mwenyewe kabla sijakuchagulia mimi"
Bado Sabrina alikuwa kimya kwani hata uwezo wa kujibu kwa kuchagua adhabu hakuweza, na alikuwa anamuangalia Sam kwa jicho la huruma tu.
"Kwahiyo unataka nikuchagulie mimi?"
Sabrina alionekana kutia huru ma sana kwani aliona leo hakuna msamaha.
Sam alimuangalia Sabrina kisha akatoka nje na kumfanya Sabrina apumue kidogo huku akiamini ameshasamehewa kwani ukizingatia ni tabia ya Sam kuweka vitisho kwake.

Muda kidogo Sam akaenda tena mule chumbani kwa Sabrina tena muda huu alikuwa ameshika bastora ambapo alifika pale na kumnyooshea Sabrina.
Kwakweli Sabrina sasa akaamini kama Sam alikuwa akimaanisha juu ya lile swala la kumwambia yeye achague adhabu kwani muda huu alikuwa mbele yake na bastora akitaka kumpiga nayo.
"Nahesabu hadi tatu, maliza sala zako zote nikumalize ukapumzike na wenzio ili mkajidiliane vizuri kuhusu Sam na jinsi alivyowasumbua duniani"
Sam akamlengeshea vizuri sasa ile bastora Sabrina, ila alipotaka kuftatua kile cha kufyatua kikagoma na kumfanya ashangae kuwa kwanini kimegoma.
Muda kidogo Cherry akaamka na kumfata Sam aliposimama kisha Sam akamuinua na kutoka nae kwenye chumba kile.
Sabrina alibaki huku akijishangaa tu kuwa Sam alidhamiria kweli kumfyatua au ni vipi.
Raha ya maisha ilimuisha kabisa na kukaa tu kitandani huku akitafakari.

Alfajiri na mapema, Jeff akapigiwa simu na Aisha. Akamsikia akilia kwenye simu huku akimuomba aende kwao.
Jeff akapatwa na huruma sana kwenye moyo wake, kwahiyo akaamka muda huo huo na kujiandaa haraka haraka kisha kuelekea alipoelekezwa na Aisha ili badae ndio aende kule ofisini kwa Sam.
Jeff aliondoka kwao na moja kwa moja akaelekea alipo Aisha, ilikuwa ni kwenye hoteli kubwa sana.
Jeff alienda hadi kwenye chumba alichoelekezwa na Aisha na kumkuta akilia tu.
Aisha alipomuona Jeff aliinuka na kumkumbatia kwa nguvu sana kisha akamuomba amsaidie kumrudisha nyumbani kwao ambapo Jeff akakubali na kutoka nje kwenda kutafuta gari ya kukodi kwanza na alipoipata tu akatoka pale na Aisha huku akimsaidia kutembea mpaka kwenye gari kisha safari ikaanza.

Walifika nyumbani kwakina Aisha ambapo Jeff alimsaidia Aisha kushuka na kuingia nae ndani ila hawakukuta mtu yeyote ndani zaidi ya mlango kuwa wazi tu.
Aisha alimshukuru sana Jeff kwa ile hali ya kujitolea na kwenda kumsaidia.
Walipokaa huku Jeff akiwa karibu na Aisha alimuuliza kwanza kilichompata,
"Kwani umepatwa na matatizo gani Aisha?"
"Jana si nilikuaga Jeff, najuta mimi kwa kutosikiliza ushauri wako"
Aisha aliinama akilia,
"Pole sana Aisha, ila niambie kilichokipata"
Aisha akamueleza Jeff vile alivyopigiana simu na Sam hadi kufikia kuonana.
"Kwakweli alichonifanyia sitoweza kusahau hadi naingia kaburini"
Kisha akaeleza alichofanyiwa na Sam huku akilia,
"Kwakweli Sam hana huruma kabisa, nakumbuka dada Neema alishawahi kunionya juu ya wanaume wa aina ya Sam. Nadhani nae alipatwa na kilichonipata mimi, hata sijui nitafanyaje"
"Pole sana, kumbe Sam ndio mkatili kiasi hiko jamani! Mi nilijua huwa wanamsingizia, na mbona hukupokea simu yangu ule usiku ili uniambie? Huyu Sam inabidi tumfungulie mashtaka tu"
Jeff alijikuta akiongea mwenyewe kwani Aisha hakumjibu tena, alipojaribu kumshtua aliona ni kimya kabisa.
Hapo Jeff hakuelewa kitu kwa muda huo, kwani hakuelewa kuwa Aisha ameshakufa kwa staili ile.
Muda kidogo ndugu wa Aisha nao walikuwa wamerudi, wakashangaa vile Jeff alivyokuwa akimtikisa tikisa Aisha kwahiyo wakajikuta wakiuliza kwa muda mmoja kuwa kuna nini.
Na waliposogea karibu waliweza kuona ni jinsi gani Aisha alivyolegea na kuonekana wazi amekufa.
Muda huo huo walianza kupiga kelele na kufanya watu wajae pale ndani kwao, ingawa wenyewe walikuwa wawili ila kwa makelele yao utadhani walikuwa watu kumi.
Watu walivyojaa pale walitaka kujua ni nini tatizo, wale ndugu wa Aisha wakasema kwamba wamekuta ndugu yao amekufa pale ndani akiwa na yule kijana yani Jeff kwahiyo kwa vyovyote vile ni Jeff ndiye aliyemuua ndugu yao.
Baadhi ya watu walitaka kumshambulia Jeff kwa kumpiga bila ya kujua chanzo huku wengine wakimsaidia Jeff na kuona ni vyema waite polisi ambapo baada ya muda mfupi walifika na kumpeleka Jeff rumande huku Aisha akipelekwa hospitali ili kupata uhakika zaidi.

Kwa upande wa Sam, kulipokucha aliamka kama kawaida na kujiandaa kisha akatoka na kumuacha Cherry sebleni halafu yeye akaondoka zake.
Alifika ofisini huku akimngoja kwa hamu huyo Jeff kwani alitaka yale maneno aliyokuwa anaongea kwenye simu basi ayaongee mbele yake kabisa,
"Na atanieleza kila kitu leo maana ameniudhi sana, haiwezekani mtu nimemuita kwa lengo la kumpa kazi halafu yeye ananifanyia ujinga jamani"
Kidogo akahisi moyo wake ukimuuma na hapo hapo akatambua kwamba lazima Aisha atakuwa amekufa tu,
"Dah masikini Aisha, ila ni nani aliyemwambia anipigie simu jana? Sikuwa na nia yoyote mbaya kwake ila tatizo kanitafuta siku ambayo nilikuwa na mtihani tayari. Kwanini Aisha? Pole sana na unisamehe bure huko uendako."
Akatulia kimya kwa muda kamavile kuna kitu alikuwa akitafakari.
Sam alikaa kwa muda sasa bila ya Jeff kufika na moja kwa moja akahisi kuwa huenda Jeff ameogopa kwenda kutokana na alichokifanya jana.
Sam aliamua kuendelea na kazi zake huku akiangalia kama Jeff atamtaharifu chochote.

Baada ya kimya kirefu na muda nao kuwa umeenda sana, Sam akatafakari kidogo kuhusu Jeff na kuona ni vyema kama amuuliza kwanza kuwa kwanini hajaenda, hivyobasi Sam akachukua simu yake na kupigia Jeff.
Ile simu iliita na kupokelewa ila aliyeipokea hakuwa Jeff,
"Hallow namuomba Jeff tafadhari"
"Huyo mtu yupo rumande, mimi ni askari"
Ikabidi Sam aulize vizuri alipopelekwa Jeff ili aende.
Walipomuelekeza ikabidi aachane na kazi zake pale, na kwavile walikuwa wanakaribia kufunga ikabidi aondoke na kumuachia majukumu meneja wake wa pale.

Sam alienda mpaka kwenye kituo cha polisi alichoelekezwa ili kujua kisa na mkasa wa kilichompata Jeff ukizingatia kwa kipindi hiko Jeff hakuwa na mtetezi wa aina yoyote ile kwani mama yake alikuwepo tu kama wale watoto matahira yani hakuweza kusema na wala hakuwa na utambuzi wowote.
Sam alifika kwa askari moja kwa moja na kuomba kuzungumza na Jeff huku akitaka kumtolea dhamana,
"Hii kesi ni kubwa sana mzee, kesi ya mauaji hii na siku zote kesi ya mauaji huwa haina dhamana kwahiyo ni ngumu sana kumuwekea dhamani"
Sam akaomba kuonana na mkuu wa kituo, akaelekezwa na kuelekea huko.
Sam alipoingia tu akamgundua yule mkuu wa kituo kuwa ni kati ya wakuu wa vituo wanaomfahamu vilivyo.
Kwahiyo haikuwa kazi ngumu kwake kupewa dhamana kwaajili ya Jeff kisha Jeff akaruhusiwa kwenda nae.

Jeff alishangaa alipoambiwa kuwa ametolewa kwa dhamana na hakujua ni nani aliyejitolea kufanya hivyo kwani wakati anaingia rumande hakuweza kumwambia mtu yoyote kwani akili yake ilishajiwekea kuwa hakuna wa kumsaidia. Tegemeo lake lilikuwa kwa Sam ila kwa alichofanya jana hakuweza tena kumpigia Sam na kumwambia kilichompa huku akiamini kuwa Sam hawezi kumsaidia ukizingatia kuwa yeye ndiye muhusika.
Ila alipofika nje akashangaa kumuona Sam huyo huyo ambaye hakumdhania kuwa anaweza kumsaidia.
Sam akamwambia waondoke mahali hapo kisha Jeff akaingia kwenye gari ya Sam na kuondoka naye.
Njiani Sam akamuuliza kilichotokea hadi yeye kukamatwa, Jeff akaona ni vyema amwambie ukweli tu ili hata huyo Sam atambue kabisa kuwa Jeff anatambua kila kitu kilichompata Aisha hadi yeye kufikia hatua ya kupelekwa rumande.
"Pole sana Jeff, wewe kesho tulia nyumbani tu yani usiende popote kisha niachie mimi nitamaliza hii kesi"
Jeff akatulia tu kwani anaelewa ni jinsi gani Sam ameelewa kosa alilolifanya kwa Aisha.
Walifika kwakina Jeff halafu Sam akamuacha Jeff ashuke huku akimsisitiza kwa swala la kwenda popote.
"Tulia tu hadi nitakapokwambia"
Jeff akaitikia na kuingia ndani kisha Sam akaondoka.

Jeff alimkuta Keti na mama yake wakiwa wamekaa tu, Jeff aliamua kumwambia Keti kwanza kuhusu Aisha,
"Keti unamkumbuka yule dada aliyekuja jana halafu mimi nikamsindikiza?"
"Ndio, si ulisema kuwa anaitwa Aisha?"
"Ndio ni huyo huyo, basi amekufa bhana"
Keti akashangaa sana na kuuliza maswali mfululizo,
"Amekufaje? Kwani alikuwa anaumwa? Mbona alionekana mzima tu jamani? Au amepata ajari?"
"Amekufa gafla tu yani, wee acha tu nahisi hata kuchanganyikiwa hapa"
Jeff akaelekea chumbani kwake na kumuacha Keti pale akisikitika tu huku akiwa haamini kile alichoambiwa.

Jeff alikaa kitandani kwake huku akiwaza nguvu ya pesa katika maisha. Alifikiria jinsi gani Sam alivyowamaliza hao wadada kwa nguvu ya pesa,
"Kwahiyo alimmaliza Neema na sasa kammaliza Aisha. Na huenda hata huyo dada yangu kamuua yeye tu kwani hata maelezo ya huyu Aisha na maelezo ya Amina hayana tofauti. Makosa yake lakini kesi yangu, na yeye ndio mwenye maamuzi. Namchukia Sam ila nitafanya nini? Sam kawamiliki watoto wangu wote, sina haki na mtoto hata mmoja sababu tu ya pesa. Sabrina hawezi kuwa na mimi sababu ya Sam, sio kwamba anampenda ila ni sababu ya pesa zake tu. Kuna wakati natafakari kuhusu mapenzi hadi akili inapoteza uelekeo"
Jeff akawaza pia siku aliyoomba kuondoka na Cherry na yale majibu aliyopewa na Sam.
Roho ilikuwa inamuuma sana ila hakuwa na jambo sahihi la kufanya kwa wakati huo ukizingatia hakuwa na pesa wala chanzo kizuri cha kumuingizia pesa zaidi ya kutegemea madili tu na kumtegemea huyo huyo Sam.

Sabrina akiwa nyumbani akapigiwa simu na Jeff ambapo akapewa habari ya kifo cha Aisha na kumfanya ashtuke sana.
Jeff alimueleza Sabrina kwenye simu kila kitu alichoambiwa na Aisha,
"Kuwa makini Sabrina, kwakweli Sam ni mtu katili sana. Asije akakuweka mashakani, kwakweli nakupenda sana"
Ndipo Sabrina alipoamua kumueleza yaliyotokea jana yake baada ya kumfuma akiongea na simu.
"Basi tupunguze mazoea ya kuongea na simu ila kama kuna jambo lolote usisite kunishirikisha Sabrina. Tupo kwenye wakati mgumu sana, pesa isiwe sababu ya kuharibu heshima na utu wetu tafadhari"
Kisha Jeff akakata simu kwa kuhofia yasije yakatokea ya jana.
Sabrina akajikuta akitafakari kuhusu swala la Aisha aliloambiwa na Jeff, moyo ukamuuma kuwa kwanini Sam anazidi kufanya vile ingawa anajua wazi kuwa anaumiza wanawake.
Kwakweli hata yeye Sabrina akiwa kama sehemu ya hao wanawake wanaoumizwa alikuwa akiumia sana katika moyo wake.

Sam aliporudi nyumbani, Sabrina aliamua tena kujitoa muhanga kwa kujaribu kumuuliza,
"Samahani Sam, nasikia Aisha amekufa"
"Ndio amekufa, nani kakwambia?"
"Jeff ndio kaniambia"
"Kwahiyo hukukoma jana eeh! Ila bahati yako umeongea ukweli, swala ni kwamba Aisha amekufa kweli na kilichomuua ni mambo yale yale yaliyomuua dada yake"
Sam aliongea kawaida kabisa kanakwamba jambo la kifo ni la kawaida kutokea.
Sabrina alimuangalia Sam na kumuuliza,
"Sasa kwanini umeamua kumfanyia hivyo Sam? Kwanini umeamua kumfanyia Aisha kitu ambacho unajua wazi kitammaliza jamani Sam? Watu wangapi watakuwa wanalia huko sababu yako?"
"Huna sababu ya kunilaumu Sabrina, hili lililotokea umelitaka mwenyewe"
Sabrina akashangaa kuwa amelitaka mwenyewe kivipi ikiwa na yeye binafsi anaogopa kufanyiwa na Sam vile anavyowafanyia wanawake wengine,
"Yani Sam, mimi nitake mwenyewe kivipi?"
"Aliyekwambia jana uniambie kuwa macho ya mtoto yanacheza cheza ni nini? Muangalie sasa kama macho yake yanacheza cheza tena"
Kisha Sam akaelekea chumbani na kumuacha Sabrina pale sebleni ambaye alimvuta mtoto wake Cherry na kumuangalia machoni, ndio hapo akagundua utofauti wa macho ya Cherry kwa alivyoyaona jana na leo.
Sabrina alitulia kwa muda na kujiuliza kuwa uhusiano wa kurekebisha macho ya mtoto na kumuua Aisha ni upi? Akakosa jibu.
Sabrina akaamua kumtumia ujumbe mfupi Jeff huku akimueleza alichoambiwa na Sam kuhusiana na kifo cha Aisha.

Usiku wa siku hiyo Sabrina hakupatwa na usingizi kabisa alikuwa macho tu akitafakari kilichotokea siku hiyo.
Wakati huo watoto wake walikuwa wameshalala tayari na alikuwa nao kitandani ila tu yeye ndio hakuweza kulala kwani usingizi haukumfikia hata kidogo.
Wakati Sabrina akijigalagaza pale kitandani, mara gafla akaona kivuli cha mtu mule ndani na kumfanya ashtuke sana na kukaa huku akitazama pande zote kuwa mtu huyo yupo sehemu gani ila hakuona mtu zaidi ya kile kivuli kikizidi kusogea.

Wakati Sabrina akijigalagaza pale kitandani, mara gafla akaona kivuli cha mtu mule ndani na kumfanya ashtuke sana na kukaa huku akitazama pande zote kuwa mtu huyo yupo sehemu gani ila hakuona mtu zaidi ya kile kivuli kikizidi kusogea.
Sabrina akapatwa na uoga zaidi na kuanza kutetemeka, akashangaa kile kivuli kikienda alipolala Cherry na kikapotelea kwenye mwili wa Cherry.
Kwakweli ile hali Sabrina hakuweza kuivumilia na kujikuta akitaka kukimbia ila alianguka chini na kuzimia.

Kulipokucha Sam aliamka kama kawaida na kujiandaa ila alipotoka sebleni leo akashangaa kwa kutokumuona Sabrina na kujiuliza kuwa imekuwaje Sabrina hajaamka mpaka muda huo.
Wakati akifikiria hayo, Cherry akatoka huku akitabasamu na kumfanya Sam amuulize,
"Mama yuko wapi?"
"Bado amelala"
Sam akasogea mule chumbani kwa Sabrina kisha akatoka na kumuaga Cherry kwa kumbusu kwenye paji la uso kisha akaondoka zake na kama kawaida akafunga mlango kwa nje kwani hakuwa na imani na Sabrina akibaki peke yake.

Sabrina nae aliamka na kujiangalia vizuri pale kitandani, kwanza akashangaa jinsi alivyochelewa kuamka kwani haikuwa kawaida yake kuchelewa kiasi kile.
Akakaa na kufikiria kilichotokea kumbukumbu yake ikamjia na kuanza kukumbuka usiku wake.
Akakumbuka mara ya mwisho kuwa alianguka chini na kuzimia sasa mbona yupo kitandani.
Akajiuliza kuwa ni nani aliyemuinua na kumuweka kitandani? Akaangalia pembeni yake hakuwaona watoto wake, uoga ukamshika tena na kumfanya ainuke haraka pale kitandani.
Akashangaa kuona mlango wa chumbani kwake ikambidi tu atoke nje.
Alipofika sebleni akashangaa kumuona Cherry akiwa ametulia huku akitazama televisheni, wakati huo yule mtoto wake mdogo alikuwa amekalishwa tu kwenye kiti chake huku akichezacheza.
Sabrina alishangaa tu na kuwasogelea watoto wake, kwavile alishamzoea Cherry kuwa anaongeaga maneno ya kiutu uzima, akaamua kumuuliza
"Nani kawaleta hapa sebleni? Na nani kawawashie Tv?"
"Baba huyo"
"Haya, nani ameniinua kutoka chini na kuniweka kitandani?"
"Baba huyo"
Sabrina akakaa kimya kwa muda kisha akarudi tena chumbani kwake.

Sabrina alienda kuangalia mlango wa mule chumbani akakumbuka wazi kuwa aliufunga tena kwa funguo na komeo la ndani sasa Sam amewezaje kufungua? Akajiuliza sana,
"Hata kama alikuwa na funguo nyingine ila vipi kuhusu komeo!! Nani amefungua?"
Sabrina alikuwa na maswali bila ya majibu mule ndani.
Akakumbuka pia kilichomfanya aanguke chini ni kivuli tena kivuli hicho kilienda kuishia kwenye mwili wa Cherry.
Kwakweli Sabrina alijiuliza maana za haya mambo bila ya majibu.

Safari ya Sam leo ilikuwa ni kwenda polisi kwanza ili ile kesi isifike kokote kule na mambo yazimike kabisa.
Wakati anakaribia kwenye kituo cha polisi akasikia kitu kikimwambia kuwa hana haja tena ya kwenda kwavile hiyo kesi ilishaisha ila kwavile alikuwa ameshakaribia akaona ni vyema aende tu.
Alipofika pale, alimkuta yule askari wa jana ambaye alimkatalia kuhusu dhamana.
Akamsalimia na kumuuliza kuhusu mkuu wa kituo,
"Hayupo ila niambie naweza kukusaidia"
Sam akamueleza kidogo kuhusu ile kesi yao ya jana na kuwa amekwenda kuripoti.
"Kesi gani hiyo?"
Ingawa Sam alimwambia huyu askari maelezo ya ile kesi ila askari alionekana kutokukumbuka chochote kile huku akijaribu kufunua majarada yao ya kesi ila hakuona kitu.
"Nadhani haikuletwa kituo hiki, hebu kajaribu kufatilie vituo vingine kwanza ndio uje huku. Itakuwa umesahau mzee"
Sam hakutaka kuongea zaidi na kuondoka huku moyo wake ukimwambia,
"Si nilikwambia kama unajisumbua bure tu"
Sam akatabasamu kisha akaelekea ofisini kwake.

Alipofika ofisini, akampia simu Jeff na kumwambia aende ofisini kwake.
Ingawa Jeff alikuwa tayari anamkera kila siku ila Sam aliona ni vyema ampatie huyu Jeff kazi ili akose muda wa kumfatilia Sabrina maana kile kitendo cha Jeff kumfatilia Sabrina kilikuwa kikimuumiza na kumkera sana.

Jeff aliondoka kwao ila yale mawazo ya jana hakuweza kuyatoa kwenye kichwa chake kwani kila akifikiria jinsi Aisha alivyokuwa akilia mpaka kufa kwake kwakweli Jeff alikuwa akiumia sana na kuna wakati alihisi kama akili yake haiposawa kabisa.
Alifika ofisini kwa Sam na moja kwa moja akaenda kuonyeshwa majukumu ya kuanza kazi siku hiyo hiyo.
Jeff alianza kazi huku akijiuliza maswali mengi sana kuhusu Sam kwani aliona wazi kuna kitu ambacho Sam anakitengeneza ukizingatia hakumuuliza chochote kuhusu ile simu aliyompigia Sabrina na wala hakumuuliza tena kuhusu yale yaliyotokea jana yake.

Muda wa kazi uliisha jioni sana na kumfanya Jeff arudi nyumbani akiwa amechoka ukizingatia ile ilikuwa ni siku yake ya kwanza kazini.
Akiwa anakaribia nyumbani kwao kuna mtu alikutana nae njiani ambapo alimsimamisha na kumuuliza,
"Samahani kaka, kuna siku nilikuona na bosi Sam hotelini. Vipi ni ndugu yako?"
"Ndio ni ndugu yangu kwani tatizo nini?"
"Kumbe ni nduguyo ndiomana wale watoto wake wanaufananofanano na wewe. Ila kuna jambo naomba niongee kwako kidogo"
"Ongea tu hata usiwe na mashaka"
"Kaka jamani mwambie kaka yako aache kutumaliza mabinti. Anatumia pesa yake vibaya sana, anatumaliza wakati hatuna kosa. Umasikini wetu usiwe sababu ya yeye kutumaliza jamani"
"Anawamalizaje sasa?"
"Ni historia ndefu ila mimi nimesimuliwa na rafiki yangu na sasa ni marehemu tayari. Mwanzoni tuliposikia stori zake tulijua watu wanamzushia kwavile ni tajiri ila kwa kifo cha rafiki yangu imefanya nijue ukweli wote"
Kisha huyu dada akamsimulia Jeff vile alivyosimuliwa na rafiki yake.
Kwakweli Jeff alikuwa akitetemeka tu kwa hasira kwani aliweza kujua ni jinsi gani Sam ameweza kuwamaliza wadada kwa kutumia pesa yake kisha akamwambia yule dada,
"Pole kwa matatizo dada yangu ila usijali nitajaribu kuongea na kaka yangu ili nimuulize vizuri maana hii habari ndio kwanza naisikia kwako. Pole sana"
Kisha Jeff akaagana na yule dada kisha akaondoka zake.

Huyu dada alikuwa ni yule yule aliyempa ujumbe Sakina kwahiyo aliamini kwamba ujumbe wake umefika sehemu husika ukizingatia siku ya kwanza alimpa ujumbe Sakina huku akiamini kuwa ni ndugu wa Sabrina kisha leo akampa ujumbe Jeff huku akiamini kuwa ujumbe umefika mahali husika sasa kwani aliamini kwamba Jeff ni ndugu wa Sam.
Kwahiyo sasa akaondoka huku moyo wake ukiwa umesuuzika kabisa.

Sam naye alirudi nyumbani kwake na kumkuta Sabrina akiwa na mawazo sana, akaona ni vyema leo amuulize ili asimfanye ajihisi vibaya zaidi,
"Sabrina mama angu nini tatizo jamani? Mbona umepooza na unaonekana kuwa na mawazo sana? Nini tatizo Sabrina wangu?"
"Tatizo ni wewe Sam, unajua sikuelewi yani sikuelewi kabisa. Kama wewe ni binadamu wa kawaida, umewezaje kufanya haya unayoyafanya?"
"Jamani Sabrina si nilishakueleza kila kitu kuhusu mimi! Sio kosa langu bali ni kosa ya chuki nilizowekewa wakati wa udogo wangu. Hebu fikiria kama ningezaliwa na kulelewa kwenye mazingira uliyokulia wewe unadhani ningekuwa hivi? Mimi sina baba Sabrina licha ya hivyo nilikuwa sipendwi na karibia ndugu wote kwani waliniona kama mtoto wa laana je unafikiri mimi niweje?"
"Siongelei hayo matatizo yako ya ukatili Sam ingawa nalo hilo ni tatizo pia ila naongelea kile ulichofanya leo ni cha kustaajabisha sana na hakuna mwanadamu wa kawaida anayeweza kufanya hivyo"
"Ni kitu gani hicho Sabrina hebu nieleweshe ili nipate kuelewa"
"Jana usiku nilianguka ila leo asubuhi nimeamka nikiwa kitandani na mlango umeshafunguliwa wakati jana kabla ya kulala nilifunga mlango kwa funguo na komeo la juu, kwakweli sijaelewa umefunguaje wakati ulikuwa kwa nje?"
Sam akamueleza alivyoamka na kumkuta Cherry sebleni na alivyomuuliza,
"Aliniambia bado umelala, nami nikaja kukuchungulia na kukukuta kweli umelala kisha nikaondoka zangu. Sasa na wewe ilikuwaje hadi ukaanguka chini?"
Sabrina akashanga yale maelezo ya Sam, kisha akamueleza kilichomfanya aanguke chini yani kile kitu alichokiona usiku,
"Kheee labda ulikuwa unaota Sabrina"
"Hapana, hata haikuwa ndoto ile maana nilikuwa macho kabisa kwahiyo swala la kuniambia kuwa ile ni ndoto napingana nalo kwakweli"
"Pole, sasa wewe unadhani ni kitu gani?"
"Mi sijui, halafu huyu Cherry mbona nilivyomuuliza akasema mlango umefungua wewe?"
Wakamuangalia Cherry kwa pamoja ila alionekana kucheka tu, ni hapo Sabrina akamwambia Sam,
"Unajua kwamba huyu mtoto simuelewi jamani! Yani kama sio mtoto wangu"
"Sabrina acha kuongea maneno hayo kwa mtoto kwani mwisho wa siku utamjengea chuki ukubwani. Hebu uendelee na mambo mengine tu yani hayo yaliyopita tuachane nayo kwani yaliyopita si ndwele tugange yajayo"
Kisha Sam akaelekea chumbani kwake na kumuacha Sabrina akiwa pale sebleni huku akijiuliza maswali mengi mengi ambayo hakuwa na majibu nayo.

Sam akiwa chumbani akatabasamu kwa kile alichoambiwa na Sabrina kwani aliona kuwa mambo yanazidi kuwa mazuri na yanazidi kuwa kamavile atakavyo yeye.
"Huyu mtoto ni vyema alizaliwa kwakweli, ndiomana watu husema kuwa usitupe mtoto. Ona sasa ilivyokuwa rahisi kwa mambo yangu, yani yanazidi kuninyookea tu. Kweli mvumilivu hula mbivu, ingawa Sabrina alinifanyia mambo mabaya ila kaniletea mtoto wa msaada kwangu, mtoto wa kufanikisha mambo yangu. Najua Sabrina hawezi fanya chochote ukizingatia ni mtoto wake, kweli mpango wangu umetiki sana kwa mtoto huyu"
Sam alitabasamu tu huku akifurahia vyote vinavyotendwa na mtoto wao Cherry.

Jeff aliona afanye kazi kwa bidii ili mwisho wa siku aweze kuokoa kizazi chake kwani alijua wazi kuwa hawezi kupambana na Sam kirahisi bila ya kutumia ujanja na akili ya ziada.
Kwahiyo akaona ni vyema afanye kazi kwa bidii ili aweze kufanikisha wazo lake.

Kimya kirefu kilipita bila ya mawasiliano kati ya Jeff na Sabrina na hii ilitokana na Jeff kuwa na majukumu mengi sana yaliyomfanya akose muda wa kuwasiliana na Sabrina.
Hali hii ilimfanya Sabrina ahisi kwamba Jeff alikuwa karibu sana na yeye kwavile alikosa kazi za kufanya ila kwasasa amepata kazi na kumsahau kabisa yeye.
Sabrina aliumia moyo ukizingatia kwa kipindi hiki alikuwa akimpenda Jeff.

Baba Sabrina nae alipokuwa Arusha alikutana na rafiki yake wa kike waliyefahamiana kwa kipindi kirefu sana na kujikuta wakikumbushiana mambo mbali mbali,
"Ila tumechelewa kuonana jamani Sabra, nimekaa hapa Arusha inapata mwezi sasa na kesho narudi zangu Dar"
"Siunajua tena kukosa mawasiliano huku, ila na mimi nataka kwenda Dar kumsalimia kaka yangu maana ni muda mrefu sijaonana nae halafu nasikia anaumwa umwa ndiomana nataka kwenda"
Wakaongea na kukubaliana kuonana kesho yake wakati wa safari.

Kesho yake ilipofika, yule rafiki yake alikuwa ameongozana na mtu mwingine.
"Deo, huyu ni mdogo wangu najua umemsahau maana nimewahi kukuonyesha picha yake siku moja tu"
Basi Deo akasalimiana na yule mdogo mtu ambapo alionyesha kama kumfahamu ila hakukumbuka ni wapi alimuona kwa mara ya mwisho, ila Deo akaongea kidogo
"Halafu kama nimewahi kukuona!"
"Hata mimi kumbukumbu zangu zinasema kuwa tumewahi kuonana ila tu sikumbuki ni wapi"
"Basi hakuna shida, tutakumbuka tu"
Kisha safari ikaanza ya kwenda Dar.

Walipofika Dar wakaagana na kuachiana mawasiliano ili kama ikiwezekana watafutane kesho yake huku Deo akiwaambia kuwa atawakaribisha nyumbani kwake ili wakapafahamu.
Kisha Deo akarudi nyumbani kwake na kumkuta mkewe yani mama Sabrina akiwa pale kama kawaida.
Alifika ndani ila alimuona mama Sabrina kuwa na mengi sana ya kumueleza,
"Yani kuna mambo ya ajabu yanatokea hapa Deo mpaka napatwa na mawazo"
"Mambo gani tena?"
Akajaribu kuelezea kidogo alivyomkuta Sakina kaanguka na jinsi alivyosasa na vile mtoto wao alivyo.
"Sabrina nae anasema hamuelewi mtoto wake yule Cherry eti anaongea maneno ya kiutu uzima"
"Hapo kwa mtoto unataka kunichekesha sasa, inamaana hamkutaka mtoto aongee? Na kama anaongea maneno ya kiutu uzima si ndio vizuri hivyo mjukuu wetu anaupeo mpana"
"Mmh na wewe, nilijua utasaidia kwa mawazo kumbe nawe unapongeza"
"Ndio kwamaana sioni tatizo hapo. Kesho kuna watu watakuja hapa nyumbani ni marafiki zangu wa siku nyingi sana"
"Hakuna tatizo, wanakaribishwa sana tu"
Kisha wakaendelea na mambo mengine.

Siku hiyo aliporudi Sam nyumbani, Sabrina aliamua kuzungumza nae
"Sam, nina ombi tafadhari"
"Ombi gani?"
"Nahitaji kwenda nyumbani, nimepata taarifa kuwa baba amerudi"
"Unataka kwenda lini?"
"Kesho"
"Basi ngoja, nikitoka kazini nitakupeleka"
"Sasa si muda utakuwa umeenda sana?"
"Usijali nitawahi kwaajili yako"
Sabrina hakutaka kubishana na Sam zaidi ya kukubaliana nae tu.

Kesho yake kama ambavyo baba Sabrina alivyoahidi kuwa patakuwa na wageni wake.
Na kweli wakampigia simu na akaenda kuwachukua kwenye stendi ya daladala na kwenda nao nyumbani kwake ambapo mama Sabrina aliwakaribisha bila kinyongo kwani hakutaka kujali jinsia yao pale.
Walikuwa wakiongea tu vizuri hadi jioni.
Muda walipokuwa wakiaga ndio muda ambao Sam, Sabrina na watoto wao walifika mahali hapo.
Waliingia ndani na kukutana na wale wageni mlangoni.
Mama mmoja katika wale wageni alipomuona Sam alipiga kelele,
"Sam!!"
Kisha yule mama akaanguka chini na kuzimia.

Muda walipokuwa wakiaga ndio muda ambao Sam, Sabrina na watoto wao walifika mahali hapo.
Waliingia ndani na kukutana na wale wageni mlangoni.
Mama mmoja kati ya wale wageni alipomuona Sam alipiga kelele,
"Sam!!"
Kisha yule mama akaanguka chini na kuzimia.
Yule mama mwingine naye alimuangalia Sam na kumfata karibu kisha akamuuliza,
"Sam!! Kumbe upo?"
Sam naye akajibu kwa ujasiri kabisa,
"Nipo ndio kwani kuna tatizo?"
Yule mama akamnasa kibao Sam na kumwambia,
"Muuaji mkubwa wewe"
Akili ya Sam ikacheza haraka haraka na kuona wazi kuwa wale wamama huenda ni kati ya mabinti aliowamaliza.
Sasa hapo aliamua kumaliza haraka haraka kabla mambo hayajavurugika kwa baba mkwe wake.
Alichokifanya Sam ni kuinama kwa yule mama aliyezimia huku akionyesha kusikitika sana na kuonyesha hali ya kumsaidia.
Ila muda kidogo yule mama alizinduka na kuanza kulia huku akionyesha kusikitika.
Sam alipoona vile akaona bora aondoke tu ili wale waongee halafu badae yeye aweze kuwaelewesha wakwe zake ila aliamua kuondoka na Sabrina ingawa Sabrina alikuwa anakataa kuondoka,
"Tafadhari Sabrina, twende tu hapo kwa Sakina. Haitakuwa vyema wewe ubaki hapa, tutarudi wote mama yangu"
Sabrina akamuonea huruma Sam na kukubali, kisha wakatoka na kuondoka.
Kwakweli pale mama Sabrina hakuelewa chochote kwani yule mmama wa chini alikuwa akipiga kelele tu, ikabidi wamtulize kwanza kisha wamuulize yule mama aliyemzaba kofi Sam.
"Eti Sabra, kwani tatizo ni nini?"
"Huyu kijana kaua watoto wetu wawili tena sio wetu tu yani kamaliza mtaa halafu akatoweka. Mama yake akatupa taarifa kuwa na yeye amekufa na wakafanya msiba"
"Khee mbona makubwa"
Mama Sabrina alishangaa sana na kuuliza kwa makini,
"Amewauaje?"
"Huyu kijana inasemekana kuwa ana laana na akilala na mwanamke yeyote yule lazima huyo mwanamke afe. Yani huyu kijana kamuua hadi mtoto wa baba yake hata tumeshangaa kumuona tena hapa. Usimuone ndugu yangu analia hivyo, hao watoto walikuwa ni watoto wake ndiomana ndugu yangu kachanganyikiwa kabisa"
Mama Sabrina akauliza tena,
"Ila mbona sielewi, yani mnasema kuwa akilala na mtu tu basi mtu huyo anakufa. Sasa huyo kijana kamuoa binti yangu na wana watoto wawili sasa kwahiyo nashangaa kusema kuwa anaua watu"
Yule mama akashangaa kwanza kusikia Sam ana mke na watoto wawili ila akaongea,
"Jamani, mimi niko radhi kumlipia nauli mama wa huyu kijana aje ili mumsikie kwa masikio yenu tena nitataka kujua kuwa ni kwanini alitudanganya kuwa mwanae amekufa. Huyu mtoto hafai jamani, ni muuaji na ameshamaliza wengi sana"
Kazi iliyobaki sasa ilikuwa ni kumtuliza yule mama aliyekuwa analia kwani alionekana kushikwa na uchungu sana kupita maelezo ya kawaida.
Walipotulia ndipo walipoamua kuaga tena na kuondoka kwani yule mama hakuweza tena kukaa mahali hapo.

Sabrina na Sam walipokuwa kwenye gari wakaanza kubishana,
"Si umesema kuwa tunaenda kukaa kidogo kwa Sakina wewe! Sasa vipi tunaenda nyumbani?"
"Tafadhari Sabrina, nipo tayari kukuleta kesho asubuhi ila leo naomba twende nyumbani"
"Hivi Sam mimi unaniweka kwenye kundi gani? Kunioa sio utumwa jamani, kumbuka kwanza uliniambia kuwa tunaenda kwa Sakina hapo halafu tutarudi tena, ila muda huu unasema twende nyumbani kwakweli Sam hunitendei haki. Nyumbani kwenyewe unanifungia yani hata nje siwezi kutoka. Kwanini unanifanyia hivi lakini Sam? Kwanini wanifanya kama mtumwa? Yani nakosa raha, furaha wala amani kwakweli si haki kwa unachonifanyia"
"Nisamehe Sabrina, wewe unajua siri zangu nyingi sana na kama ningekuwa na nia ya kukufanyia ubaya basi ubaya huo ningekufanyia siku nyingi sana ila sina sababu ya kumfanyia hivyo mwanamke nimpendae"
Sam alikuwa akiongea hayo huku akiendesha gari yake kurudi nyumbani kwao.

Walifika nyumbani ndio ila Sabrina alikuwa amenuna tu kwani moyo wake ulimuuma sana kwa kile anachotendewa na Sam kwani aliona kama utumwa ukizingatia hata nje haruhusiwi kutoka.
Ila walipoingia ndani Sam akamwambia Sabrina,
"Sabrina, wewe ni msaada mkubwa sana katika maisha yangu, tafadhari hata wazazi wako wakikuuliza naomba unitetee maana wewe ndio mtetezi wangu wa maisha haya. Tafadhari Sabrina mama angu!"
Sabrina aliitikia tu ukizingatia hata yeye mwenyewe hawezi kujieleza kwa wazazi wake kuwa wale watoto kazaa na Jeff kwahiyo ile dhana ya wazazi wake kufahamu kuwa watoto ni wa Sam ilikuwa ni afadhari kwake na kwenye maisha yake ingawa kila siku alikuwa akiona ni mateso kuishi na Sam.

Walipoondoka wale wageni, Deo akapata ya kumuuliza mkewe sasa,
"Kwahiyo Sabrina na huyo Sam wameona ni vyema wao kuondoka kabisa?"
"Labda wamefanya vile kuepusha shari mume wangu"
"Shari gani? Mbona unapenda kutetea ujinga Joy? Na hivi huyu Sabrina amekuwa na akili gani siku hizi? Yani hajaonana na mimi kwa kipindi chote hiki halafu anakuja kuchungulia kisha anaondoka na mume wake tena mume ambaye alimtelekeza wakati mgonjwa hivi huyu mtoto ana akili gani karogwa au? Kesho naenda huko huko"
"Wamehama sio kule unakopafahamu wewe"
"Basi utanipeleka"
"Nimewahi kwenda mara moja tu, njia siijui vizuri"
"Hivi na wewe Joy akili yako ipo kweli? Mbona unafanya mambo ya ajabu jamani yani hupakumbuki anapokaa mtoto halafu wanaume wenyewe ndio hawa wa kisasa wakina Sam kweli kabisa hujisumbui kujua anaishi wapi na anaishije? Aaah unakera kwakweli yani wewe upo upo tu, nilikwambia mtoto asiondoke hapa umemuachia kaondoka halafu humfatilii. Hivi una matatizo gani wewe?"
Deo alionekana kuchukizwa tu kwani katika moyo wake alijikuta akimchukia Sam kwa wazi wazi kabisa.

Usiku ule Sabrina aliamua kumpigia simu Jeff, kwanza kabisa ni kwaajili ya kumlaumu kuwa kwanini siku hizi hamtafuti na pili ilikuwa ni kumwambia kuhusu matukio ya siku hiyo ila Jeff alipopokea simu alilalamika kuwa ana usingizi sana na hakuweza kuongea zaidi.
"Yani Jeff kuzungumza na mimi tu ndio una usingizi sana jamani!"
"Hapana Sabrina ila nina usingizi kweli hata tukizungumza hatutaweza kuelewana"
"Hivi si niwewe uliyedai kuwa unanipenda sana, na huwezi kuwa na mwingine zaidi yangu! Vipi leo ushindwe kuzungumza na mimi? Inamaana hunipendi tena?"
"Hapana Sabrina, nakupenda sana na siwezi kukusaliti kwakweli ila ndio hivyo nina usingizi mama angu"
"Unanifanyia kusudi Jeff, mbona zamani haikuwa hivi? Iweje leo unifanyie hivi?"
Jeff alikuwa tayari kashalala kwahiyo hakumjibu Sabrina tena na kumfanya achukie maradufu hadi akakosa usingizi kabisa huku akiyalaani mapenzi.
Sabrina alijiona kama anaonewa tu.
Wakati anawaza, mwanae Cherry aliamka kisha akamsogelea alipo na kumkumbatia kwakweli Sabrina alijikuta akipata hali ya amani katika moyo wake na kusema kuwa watoto wake ndio kila kitu katika maisha yake kisha naye akamkumbatia mwanae, ambapo mwanae alimtazama na kama kumpa ishara kuwa walale, ndipo Sabrina alipoamua kulala kwa muda huo.

Kulipokucha Sam aliamka na kwenda kumgongea Sabrina ambaye naye aliamka kisha akamuomba ajiandae na kuwaandaa watoto ili waende tena kuwaona wazazi wa Sabrina.
Muda alipomaliza kuwaandaa alimsikia Cherry akimwambia Sam,
"Nakuonea huruma leo"
Sam naye alimuangalia huyu mtoto na kumuuliza tu kuwa anamuonea huruma kwanini,
"Nitakwambia badae"
Mazungumzo haya yalizidi kumpa mashaka Sabrina dhidi ya mwanae hususani kwa ile tabia ya mwanae ya kuongea kama mtu mzima.
Alimuangalia huyu mtoto na kukosa jibu kabisa kisha wakatoka pale ndani kwaajili ya safari yao ya kwenda huko kwa wazazi wa Sabrina.

Walipofika kwakina Sabrina walimkuta mama wa Sabrina tu kwani baba yake hakuwepo.
Sabrina aliuliza kuhusu baba yake na kujibiwa kuwa ametoka,
"Yani ameondoka mapema sana hapa nyumbani leo sijui kuna vitu gani anaviwahi huko alipoenda"
Basi Sam naye akaaga pale na kusema kuwa atarudi badae kwaajili ya kuwachukua wakina Sabrina.
Kwahiyo Sabrina alibaki na mama yake ambapo mama Sabrina aliamua kumuuliza mwanae maswali,
"Hivi mwanangu unaishije na huyu mumeo?"
"Naishi nae vizuri tu mama"
"Sabrina, kumbuka kuwa mimi ni mama yako. Unapaswa kunieleza kila kitu. Kutunza siri hakutakusaidia kitu zaidi ya kukuumiza moyo wako tu. Hebu jiangalie unavyokonda usiku na mchana, kila siku unaisha mwanangu. Unaishi nyumba nzuri, magari ya kutembelea yapo na mumeo ni mtu mwenye pesa ila kwanini kila siku unakonda? Inaonyesha wazi kuwa huna furaha mwanangu, niambie ukweli mimi mama yako ili nijue kuwa ni jinsi gani nakusaidia"
"Mama, ipo siku nitakwambia kila kitu kuhusu mimi lakini sio sasa"
"Utaniambia lini sasa? Mpaka nife au mpaka ufe? Jana umeshuhudia mwenyewe wale wamama walivyochanganyikiwa kuhusu Sam. Niambie ukweli mwanangu"
"Muda ukifika nitakwambia mama"
"Muda gani Sabrina? Muda ndio huu mwanangu"
Sabrina akakaa kimya kwa muda huku akifikiria kama amwambie ukweli mama yake au afanyaje? Alikuwa akifikiria jinsi mama yake atakavyokuwa akigundua kuwa wale watoto ni wa Jeff pia alifikiria jinsi alivyoambiwa na Sam kuwa amtunzie ile siri.
Mwisho wa siku alikuwa kimya tu bila ya kuzungumza chochote ingawa mama yake alikuwa akimwambia maneno ya ushawishi ili aseme ukweli ila bado Sabrina alikuwa mgumu kuzungumza ukweli kuhusu mume wake.

Mida ya mchana aliwasili shangazi wa Sabrina na kufanya wafurahiane kuonana ukizingatia ni kipindi kirefu kiasi kimepita tangu walipoonana kwa mara ya mwisho.
Wakazungumza mengi sana ila shangazi wa Sabrina alionekana kumuangalia sana yule mtoto wa Sabrina mpaka Sabrina aliamua kumuuliza shangazi yake,
"Mbona unamuangalia hivyo huyu mtoto shangazi?"
"Jamani, naona kabisa kuwa huyu mtoto huyupo sawa"
Mama Sabrina akadakia kwa kuuliza,
"Hayupo sawa kivipi?"
"Kwani nyie mnamuonaje huyu mtoto jamani? Hayupo sawa huyu"
"Ila shangazi mbona mimi namuona kuwa yupo sawa tu, sasa inatakiwa utuambie kuwa hayupo sawa kivipi?"
Shangazi akatulia kidogo na kumuangalia yule mtoto wa Sabrina ambapo yule mtoto naye alimuangalia kwa makini sana kana kwamba ana hamu ya kusikia ni kitu gani yule shangazi anataka kusema.
Muda kidogo yule shangazi akacheka na kuwaambia,
"Hivi mmeona alivyoniangalia lakini?"
Sabrina na mama yake wakamtazama Cherry aliyeonekana akicheza cheza tu ndipo Sabrina akamuuliza tena shangazi yake,
"Mbona sikuelewi shangazi, niambie ni kitu gani cha tofauti unachokiona kwa mwanangu"
"Tuambie wifi jamani, najua wewe kuna kitu unakijua"
"Ni kweli kuna kitu nakijua kuhusu huyu mtoto, kwani kuna vingi nimeota juu yake ila hapa nimeweza kujua ukweli wa zile ndoto nilizoota kwani nikimtazama tu naona kabisa kuwa kuna kitu kinaendelea kweli kwa huyu mtoto."
"Basi ndio utuambie wifi"
Shangazi wa Sabrina akapumua kidogo ili aweze kuongea ila akashangaa gafla kapata na kigugumizi.

Muda kidogo kabla shangazi hajaweza kuongea alifika Sam pale nyumbani kwakina Sabrina na kufanya aanze kusalimiana nae na kusahau kabisa kuhusu swala la kumuongelea Cherry kitu ambacho Sabrina aliamua kuuliza tena kwa shangazi yake,
"Mbona hujasema shangazi kuwa huyu mtoto ana tatizo gani."
"Nitasema tu Sabrina ila kwasasa ngoja niache tu maana tatizo la huyu mtoto sio rahisi hata kusema nababaika, ngoja nikipata uwezo wa kusema nitasema tu"
"Na mbona ulitaka kusema ila ni kigugumizi tu ndio kilikuzuia, kwanini usiseme sasa hata bac yake nae asikie na ajue jinsi ya kutusaidia"
Shangazi alicheka tu huku akitikisa kichwa, Sam nae alikuwa kimya akiwasikilizia kisha alipoona kuwa hakuna hoja inayoendelea alimuomba Sabrina kuwa waondoke.
Sabrina hakupinga ila alienda kujiandaa ili waondoke.

Sabrina alipomaliza kujiandaa, akatoka nje na kumfanya Sam ainuke ili aanze kuaga.
Muda kidogo baba wa Sabrina akarejea pale nyumbani ila alimsogelea Sam na kumnasa vibao mfululizo na kufanya kila mmoja pale ndani ajiulize kuwa tatizo ni nini mpaka iwe vile.
Sam alimuangalia baba mkwe wake bila ya kusema chochote ila akashtukia akipigwa ngumi ya pua iliyomfanya Sam kuanguka chini.

Sabrina alipomaliza kujiandaa akatoka nje na kumfanya Sam ainuke ili aanze kuaga.
Muda kidogo baba wa Sabrina akarejea pale nyumbani ila alimsogelea Sam na kumnasa vibao mfululizo na kufanya kila mmoja pale ndani ajiulize kuwa tatizo ni nini mpaka iwe vile.
Sam alimuangalia baba mkwe wake bila ya kusema chochote ila alishtukia akipigwa ngumi ya pua iliyomfanya Sam kuanguka chini.
Kile kitendo kilimshtua sana Sabrina na kumfanya asogee pale alipo baba yake ambapo mama na shangazi yake nao wakasogea ili baba Sabrina asiendelee kumpiga Sam.
"Tafadhari Deo, kwani huyu kijana kafanyaje?"
Baba Sabrina akajibu kwa jazba sana,
"Huyu kijana ni mpumbavu sana, kashaua mabinti wengi sana na sasa anataka kummaliza binti yangu si unaona jana alivyomkimbiza binti yangu hapa ili nisizungumze nae!"
"Jamani baba Sabrina, amewaua wakina nani na kwa ushahidi gani ulionao?"
"Sio ushahidi Joy, ngoja mwanetu naye afe ndio utajua umuhimu wa maneno yangu. Huyu kijana hafai, wale wamama jana walikuwa wanasema ukweli kabisa kwani ameshaua mabinti wengi kwa kutembea nao. Namchukia sana huyu kijana"
Deo akataka tena kwenda kumshindika ngumi nyingine Sam ila Sabrina aliingilia kati kwa kukaa mbele ya Sam na kwa muda huu Sabrina aliamua kujitoa kwa kumtetea Sam,
"Baba nisikilize mimi binti yako, usisikilize maneno ya watu. Huyu Sam ni mume wangu na nimefunga nae ndoa takatifu kabisa na kuzaa nae hawa watoto wawili Cherry na Sam, na kama ingekuwa Sam ni muuaji basi angeanza kwa kuniua mimi niliyeweza kuishi nae kwa muda mrefu."
Kisha Sabrina akamuangalia Sam pale chini na kumpa mkono kama ishara ya kumuhitaji anyanyuke, naye Sam akanyenyuka kisha yeye na Sabrina pamoja na watoto wao wakatoka na kuondoka.

Deo alibaki pale akisikitika sana,
"Sijui huyu kijana kampa nini binti yangu jamani"
Kisha akamuanga lia mke wake na kumwambia,
"Unajua mambo ambayo nimeenda kukutana nayo huko yani si ya kawaida hata kidogo. Nasikitika sana kwa mwanangu kuolewa na huyu kijana, hata sijui nilikubali vipi"
"Kwani leo ulienda wapi baba Sabrina?"
"Kwanza kabisa nilienda kwa wale wageni wetu wa jana, nimezungumza nao vya kutosha. Nimeona wazi kabisa kuwa yale mambo Sam hata hajasingiziwa kwani wale wameongea kwa uhakika kabisa. Nilipoondoka pale nikaamua kwenda alipokuwa anaishi huyo Sam zamani yani moyo wangu tu umejitolea kufanya hivyo.
Nilipofika pale nikaona geti limefungwa ila muda kidogo akapita mdada ambaye alisimama pale kisha machozi yakamtoka. Nami nikaona ni vyema kumsogelea na kumuuliza. Kwakweli kanisimulia mambo ya kutisha sana ambayo dada yake amefanyiwa na huyo Sam. Mama Sabrina, pamoja na wewe dada yangu Sabrina tujitahidi jamani tumuokoe mtoto, yupo katika hali mbaya sana. Sam ni muuaji jamani"
"Deo, mimi sipingani na wewe mume wangu ila swali langu ni kuwa kama Sam ni muuaji mbona ameishi na Sabrina kwa kipindi chote hiki? Na kama kweli anawaua wanawake kwa staili hiyo mliyosema je amewezaje kuzaa na Sabrina tena watoto wawili? Mi sidhani kama madai hayo yana ukweli Deo maana kuna watu wengine hufanya vitu kwaajili ya kumchafua mtu tu."
"Kumchafua? Wale wamama jana wamchafue Sam kwa lipi? Na huyu mdada niliyekutana nae leo amchafue Sam kwangu kwasababu gani na ili iweje? Hili jambo ni hakika na dhahiri kwamba lipo"
"Mmh ila Sam anampenda Sabrina jamani"
"Kumpendaje? Yule Sam ni muuaji"
Shangazi wa Sabrina alikuwa kimya kabisa ila sasa aliamua kuongea,
"Jamani mkishamalizana na huyo Sam muanze sasa kumuangalia na huyo mjukuu wenu wa kwanza. Yule mtoto hayupo sawa, ipo siku mtakubaliana na maneno yangu"
"Tunakuelewa ila tushirikiane katika kuliondoa hili tatizo, sipo tayari kuona binti yangu akiteketea kwa mtu ambaye hata sijui alipotoka"
Deo aliinama huku akitafakari maneno yale aliyoambiwa na yule binti waliyekutana nae.
Ila shangazi wa Sabrina naye akaaga na kuondoka.

Sam alifika nyumbani na Sabrina huku akimshukuru sana kwa jinsi alivyomtetea,
"Nashukuru sana Sabrina, wewe ni mke bora kwakweli. Mungu amekupa moyo wa ujasiri, upendo na uvumilivu laiti kama ungekuwa kama wengine basi huenda na wewe ungekuwa umekufa au hata sijui ingekuwaje. Kwakweli siamini kama kweli umenitetea kiasi hiki leo"
"Sam, mimi sina ubaya wowote na wewe na wala sijawahi kukuwaza jambo lolote baya ingawaje umeshawahi kunipa vitisho mara kwa mara hata unafikia hatua ya kunifungia mlango ili hata jua nisiweze kuliona."
"Sabrina, nisamehe sana. Wewe ni mwanamke jasiri kwakweli, sikutegemea kwa ulilonifanyia leo. Ngoja nikupe siri nyingine iliyojificha, siri hii ni ya mwanamke mmoja mrembo na mtaratibu sana. Niliyetokea kumuamini kupita maelezo ingawa sikuwahi kumwambia siri ya maisha yangu"
Sabrina alitulia kumsikiliza Sam ili apate kujua kuhusu Janeth ukizingatia ni jina ambalo aliwahi kulisikia na likatoweka gafla,
"Ni hivi, Janeth ni mwanamke niliyewahi kufahamiana nae kabla yako. Alikuwa mtu wangu wa karibu sana, nilimpa kila alichohitaji ila sikuthubutu kutembea nae kwa kipindi hiko kwani sikutaka kumuumiza wala kumpoteza. Ila kwavile Janeth alipenda kuwa na pesa na maisha mazuri niliamua kumuingiza kwenye biashara yangu ya madawa ya kulevya"
Sabrina akashtuka na kuuliza kwa mshangao,
"Madawa ya kulevya?!"
"Ndio ni madawa ya kulevyo, mbona unashangaa hivyo? Hiyo ni biashara kama biashara zingine na huwezi amini ila biashara hiyo ndio yenye pesa kuliko biashara yoyote unayoijua wewe"
"Kwahiyo Sam unauza madawa ya kulevya"
"Ndio kwani tatizo ni nini?"
"Hakuna tatizo"
Sabrina akatulia kwani alimuona Sam kuwa binadamu anayefanya mambo ya ajabu kuliko wote duniani na kila alipomueleza mambo yake aliyaona kuwa mazito sana kupita kawaida.
Sam akaendelea kuzungumza,
"Mimi nauza madawa ya kulevya ndio ila wanaweza wakakamatwa wauza madawa wote kasoro mimi kwani nayauza kwa akili sana.
Janeth nilimpeleka nje na kumsomesha huku gharama zote na hela za matumizi nikimtumia kama nilivyokuwa nafanya kwako ila tofauti yako na Janeti ni kuwa wewe ulikuwa unasoma tu ila Janeth alikuwa anasoma huku akiangalia mchongo wa madawa ulivyokaa. Kwakweli Janeth ni mchapakazi, nakili kupoteza mtu mashuhuru na mchapakazi kama Janeth kwani aliniingizia faida kubwa sana kwenye kampuni yangu.
Nimefanya kazi na Janenth kwa kipindi kirefu sana na kumnunulia nyumba aliyokuwa akiishi na gari la kutembelea.
Safari za nje zilikuwa nyingi sana kwa upande wake kiasi kwamba tulikuwa hatuonani na ndiomana ikawa ngumu kwa Janeth kujua kwamba nimeoa.
Kwa akili ya Janeth aliwaza kuwa mimi nitamuoa kwavile nilimsomesha na kumpa maisha mazuri."
Kisha Sam akamueleza Sabrina kilichotendeka kwa Janeth na kufanya na yeye aende na maji kama wenzie.
"Mmh Sam, kwahiyo na yeye ukammaliza!"
"Sikuweza kujizuia kutokana na vishawishi alivyoweka kwangu ukizingatia huyo Janeth alikuwa ni binti mrembo na wa kuvutia."
"Hivi Sam kwanini umeamua kuniambia yote haya?"
"Kwasababu nakupenda sana Sabrina. Huwa nakufanyia mambo mabaya si kwa kupenda bali ni kutokana na wewe mwenyewe ila nakuapia Sabrina sitatenda jambo lolote baya tena kwako ukizingatia umeniletea mtoto mzuri sana huyu Cherry"
Sabrina akapata na lingine la kumuuliza Sam,
"Na kwanini unampenda zaidi huyu Cherry kushinda huyu mdogo?"
"Kwakweli Sabrina itakuwa ngumu sana kwako kujua ila huyu Cherry ananisaidia sana kwenye mambo yangu na hata hivyo ni mtoto wa kwanza tena wa kike acha tu nimpende"
Sabrina akatulia kidogo huku akijiuliza moyoni kwa ni vitu gani ambavyo Sam anasaidiwa na huyo Cherry? Alitafakari na kukosa jibu kabisa kisha akainuka na kwenda kuandaa chakula cha usiku.

Deo alikosa raha kabisa kisha akawapigia simu wale marafiki zake wa jana na kuwaomba mama yake Sam atumiwe nauli ili yeye binafsi aweze kuzungumza nae.
"Mimi nitawatumia nauli ili mumtumie huyo mtu"
Wakakubaliana pale na kukata simu ila mama Sabrina alikuwa bado akimshangaa mumewe,
"Kwahiyo unataka mama yake aje, si tulikuwa nae kwenye harusi yake jamani?"
"Ni kweli ila hawa vijana wa sasa hivi kwakweli sina imani kabisa, huenda alituletea watu ambao sio wazazi wake. Mi namtaka huyo mama ili anithibitishie tabisa za mwanae kwani nimeambiwa kuwa anazijua vilivyo"
Mama Sabrina hakutaka kubishana na mumewe kwahiyo akakubaliana nae vile vile alivyokuwa anataka mwenyewe.
Basi wakaamua kulala kwani muda nao ulikuwa umeenda tayari.

Kwa upande wa Jeff, leo alikuwa amechoka sana na kumfanya ajisikie uvivu wa kufanya mambo mengi sana na kuamua kulala.
Akiwa kwenye usingizi mzito kabisa akajiwa na ndoto.
Akamuona mtoto wao Cherry akiwa amelala, mara kikatokea kitu cha ajabu sana na kuingia kwenye mwili wa Cherry halafu akamuona Cherry akishuka kitandani na kwenda mlangoni ambapo alirefuka gafla na kuwa kama mtu mzima kisha akafungua mlango ule uliokuwa umefungwa kwa komeo la juu kabisa na kutoka nje. Mara akamuona yule mtu aliyemvaa Cherry kwa urefu ule ule akigeuka na kumchekea ambapo sura yake ilionekana kutisha sana yani kupita hali ya kawaida.
Jeff alishtuka usingizini huku akihema sana na jasho jingi kumtoka.
Sasa alikaa kitandani kwani uchovu wake wote ulitoweka gafla na hakuwa na furaha tena hata uoga ulimshika.
Huku akitetemeka akachukua simu yake na kumpigia simu Sabrina bila hata ya kujali kuwa ni usiku ila ile simu ilipokelewa na kabla Jeff hajazungumza chochote, akasikia akiambiwa kwenye simu,
"Si ushakatazwa wewe kumpigia mama simu usiku?"
Jeff akakata ile simu huku akijihisi kutetemeka kabisa na kumfanya akose raha huku akizidi kuona uhalisia wa ndoto aliyoota kwa usiku huo.
Jeff akajikuta akitafakari vitu vingi sana ikiwemo hali ya mama yake.

Kulipokucha kama kawaida Sam aliamka na kujiandaa kisha akaiaga familia yake kuwa anaenda kazini kama kawaida.
Sabrina alibaki na watoto wake, mud a huu alishika simu yake na kuiangalia.
Akaona kuwa Jeff alipiga na simu hiyo ilipokelewa, akashangaa sana kwani hakuwa na kumbukumbu za kupokea simu hiyo.
Kisha akamuangalia Cherry na kumwambia,
"Halafu wewe umepokea simu yangu eeeh!"
Cherry nae akajibu kwa ujasiri kabisa,
"Ndio nimepokea"
"Khee halafu wewe mbona unaongea kama mtu mzima!"
"Mimi ni mtu mzima ndio"
"Kheee makubwa haya, ingekuwa sijakuzaa mimi ningesema nibadilishiwe. Una nini wewe mtoto lakini?"
Cherry akajibu kwa ukali,
"Nimekwambia mimi sio mtoto"
Sabrina akajishika mdomo kwani alikuwa haamini kile kinachoendelea mbele yake kwa muda huo.

Sam akiwa ofisini kwake akapigiwa simu na mama yake mdogo,
"Sam, nasikia mama yako anataka kuja huko sijui ni wewe uliyemwambia aje?"
"Hapana mamdogo sijazungumza na mama kabisa si unajua vile ambavyo hanipendi! Hawezi kuja huku"
"Nimeambiwa anakuja, hebu jaribu kumtafuta hewani kwanza"
"Sawa ngoja nifanye hivyo"
Sam aliamuomba mamake mdogo namba kisha kumtafuta mama yake hewani kwani hakuwasiliana nae kwa kipindi kirefu sana ambapo alipopokea tu akamsihi kuonana nae kwanza.
"Ila mimi siji huko kwasababu yako Sam"
"Naelewa mama, ila je hupendi kuwaona wajukuu zako mama yangu? Mimi ni mwanao tu, na mtoto akinyea mkono usiukate bali usafishe tu"
"Hivi ni kweli una watoto Sam?"
"Ndio mama na huwa nakukumbuka sana mama yangu jamani. Karibu uone wajukuu zako mama yangu"
Mama wa Sam alikubali tu.

Jioni Sam akawasiliana na mama yake kuwa amefika kisha akaenda kumpokea na kwenda naye moja kwa moja nyumbani kwake ambapo alimkaribisha na kumtambulisha kwa Sabrina ila Sabrina alikuwa akimshangaa tu ingawa Sam alishawahi kumueleza ukweli kuhusu wazazi wake.
Ila mama Sam nae alikuwa akimshangaa tu mwanae na mwisho akaamua kuongea,
"Hivi kweli mwanangu, nyumba kubwa yote hii na magari yote hapo nje umeshindwa hata siku moja kusema nimtumie nauli mama yangu aje mjini! Hivi Sam nilikuzaa mtu au jini? Mbona una roho mbaya kiasi hiki? Kwa kosa gani nililofanya mama yako hadi ushindwe kuwa karibu na mimi? Tulikutenga kwasababu ya makosa yako ila wewe hukutakiwa kututenga sisi"
Huyu mama aliongea kwa uchungu sana kuhusu huyu mtoto wake.

Jeff alipotoka kazini alipita kwa mama Sabrina lengo lake lilikuwa ni kuongelea ndoto aliyoota usiku uliopita ila baba Sabrina alipomuona akamuomba muda huo huo awapeleke nyumbani kwa Sam kwani mama Sabrina alidai kutokujua njia kabisa.
Jeff hakusita na kuamua kwenda nao.

Sam nae aliendelea kumuomba msamaha mama yake,
"Mama, nilijua bado mnanichukia yani bila ya mamdogo kuniambia nisingejua chochote kama umefika mjini. Nisamehe mama yangu"
Wakasikia kengele ya getini ikipigwa na kujua kuwa kuna mtu getini, ikabidi Sabrina aende kufungua kwani muda huo Sam alikuwa kwenye mazungumSabrina akawaongoza hadi sebleni ambapo walimkuta Sam akizungumza na mama yake.
Ila yule mama Sam alipowaona moja kwa moja macho yake yakamtazama baba Sabrina ambapo huyu mama Sam aliinuka na kumzaba kibao baba Sabrina.

Ila yule mama Sam alipowaona moja kwa moja macho yake yakamtazama baba Sabrina ambapo aliinuka na kumzaba kibao.
Wote mule ndani wakamshangaa kuwa ana matatizo gani ambapo aliyekuwa wa kwanza kuuliza ni mama Sabrina,
"Vipi kwani kuna nini?"
Yule mwanamke hakujibu ila alimkunja baba Sabrina ambaye alikuwa amesimama tu akimuangalia.
Ikabidi Sam nae aingilie kati na kumuuliza mama yake,
"Kwani kuna nini kati yenu mama?"
Yule mama alijibu kwa jazba kabisa,
"Huyu mwanaume ni shetani sana"
Sam akasogea karibu zaidi na kujaribu kumtoa mama yake mikono kwani alikuwa amemkunja baba Sabrina,
"Niache Sam, niache kabisa hujui tu alichonitenda huyu binadamu"
Sam ikabidi tu afanye juu chini kuwaachanisha kwani mama yake alionekana kuwa na hasira iliyopitiliza.

Sam alipofanikiwa kuwaachanisha ikabidi aulize sasa kuwa imekuwaje na kwanini mama yake amekuwa na hasira kiasi kile,
"Mama punguza hasira na uniambie kuwa tatizo ni nini? Hata kama huoni haja ya kuniambia kwavile hunipendi mama yangu ila naomba tu uniambie kwanini umemchukia na huyu pia"
Mama Sam alikaa kimya kwanza bila ya kuongea chochote na kufanya Sam aongee tena,
"Mama unakuwa na chuki hadi kwa familia yangu jamani, maana toka umefika hapa hata kusema uwaone wajukuu zako hakuna yani ndio kwanza mimi ndio nakazana kukuomba msamaha haya sasa umeanza na baba mkwe wangu"
Yule mama aliposikia neno baba mkwe akacheka sana,
"Yani kumbe huyo binti huyu ndiye baba yake? Kheee msinichekeshe jamani, kwahiyo Deo unajisikiaje sasa mwanao kuwa mkweo?"
Deo akashtuka na kuuliza,
"Mwanangu kuwa mkwe wangu kivipi?"
Mama Sam akacheka tena na kusema,
"Sasa moyo wangu umeburudika, kwa taarifa yako tu Deo huyu Sam ni mwanao na wewe Sam huyo Deo ndio baba yako kuhusu kufa nilikudanganya tu sababu ulikuwa unanisumbua sana"
Mule ndani kikatawala kimya cha muda mfupi kwani ilionekana kama watu mule kutokuelewa kile kilichokuwa kikizungumza na mama Sam.
Deo akamuuliza tena mama Sam,
"Unasemaje wewe? Unajua sikuelewi?"
"Hunielewi nini? Si umeoza watoto wako? Si hao wameoana? Nadhani ushetani wote wa Sam umeenda kumalizikia kwa dada yake"
Kisha huyu mama akacheka sana kwa furaha kabisa kisha akamuangalia Sam na kumwambia,
"Mwanangu Sam, hata sikuwa na haja ya kukuchukia ila huyo Deo ndio aliyesababisha nikuchukie mwanangu ukijumlisha na zile tabia zako za kishetani ndio kabisa ila chanzo ni huyo"
"Kwahiyo mama huyu ndio baba yangu? Huyu ndiye aliyefanya unichukie na kunitenga? Huyu ndio chanzo cha mimi kufanya maovu na huyu ndio mtu anayeongoza kunichukia kwenye familia yao!"
Kisha Sam akamuangalia Deo na kumuuliza,
"Kwanini unanichukia? Kwanini umetokea kutokunipenda kabisa kwanini? Inamaana gani kwangu mimi kuzaliwa na wazazi wa aina yenu? Inamaana gani mimi kuwa na wazazi? Nilishakubali kuwa yatima kitambo sana kwahiyo sioni umuhimu wenu kwangu"
Sam akatoka pale na kuelekea chumbani kwake, jambo hilo likampa mashaka Sabrina ukizingatia anamfahamu Sam vizuri sana kwani ndiye mwanamke pekee aliyeweza kuishi nae ndani ya nyumba kama mke na mume tena kwa muda mrefu.

Wakiwa wamekaa pale sebleni wakitazamana kwani kila mmoja alikuwa na maswali yasiyo na majibu, gafla Sam alitoka chumbani akiwa na bastora mbili mkononi, moja alimlengeshea Deo na nyingine akamlengeshea mama yake.
Sabrina aliamua kumsogelea Sam kwa haraka sana kwani alikuwa akiitambua akili yake vilivyo ukizingatia kwa muda huo ni yeye tu anayemuelewa.
"Tafadhari Sam usifanye hivyo nakuomba Sam"
Alijaribu kumbembeleza na kumsihi sana, muda kidogo mtoto wao Cherry nae alitoka na kumfata Sam pale ambapo alimuangalia Sam na kumfanya Sam kushusha zile bastora chini kisha yule mtoto aligeuka na kuwaangalia wengine huku akionekana kuwa na hasira iliyoambatana na chuki ya wazi wazi kisha akatoa kauli moja tu,
"Ondokeni hapa"
Ile kauli ilikuwa ya ukali sana na hata kuwaogopesha wazazi wa Sabrina na huyo mama Sam, na kwakweli waliamua kutoka nje.
Sam alimnyanyua Cherry na kwenda nae chumbani kwake kwahiyo pale sebleni alibaki Sabrina tu kwani wengine wote walitoka nje.

Jeff aliwasihi wote kuwa warudi nyumbani wakaelewane kidogo kwani hata yeye kwa kiasi fulani alianza kumzoea Sam ukizingatia hata yeye alishawahi kutishiwa bastora na huyo Sam.
Wakamsikiliza pale ikabidi waungane na wote kuelekea kwakina Sabrina pamoja na mama Sam bila ya kujali kuwa ndiye aliyeanzisha ule mzozo.
Ila kabla hawajaondoka, Sam alitoka ndani na kuwafata nje kisha kuwaomba warudi ndani.
Kile kitendo kiliwafanya watazamane kwa hofu kwani kila mmoja alikuwa na uoga wa kuelekea ndani kwa Sam tena ila muda kidogo Mama Sam akajitoa muhanga kwa kuwa wa kwanza kuingia ndani na kuwafanya wote waingie kisha Sam akawaambia,
"Naomba kuongea na nyie wawili tu bila ya uwepo wa mtu mwingine yeyote.
Sabrina akaomba awepo mama yake kwani aliamini kuwa mama yake ni mwenye busara na angeweza hata kutoa ushauri wa kufaa.
"Aah basi, kuna kitu nimegundua hapa. Twende pia na mama mkwe wangu asiyekuwa na makuu twendeni tukazungumze."
Akaelekea nao kwenye chumba cha wageni ili wapate kuzungumza halafu pale sebleni alimuacha Sabrina, Jeff na watoto.

Waliingia kwenye kile chumba cha wageni kisha Sam alihitaji kujua hoja ya mmoja baada ya mwingine.
"Haya ningependa nianze kusikia maelezo kutoka kwa wewe mama yangu kuwa kwanini huyu ni baba yangu? Kwanini si mwingine na kwanini hukunitajia siku zote hizo? Kwanini uliniambia kuwa amekufa?"
"Mwanangu ingawa umechukulia hasira sana ila huu ni ukweli kabisa kuwa huyu ni baba yako.
Nilikutana nae miaka ya nyuma huko, alikuwa ni mpenzi wangu. Kuna mahali alikuwa anafanya kazi na ndio huko nilipokutana nae, mahali alipokuwa anaishi nilikaa nae hapo mwezi mzima nikipika na kupakua na kufanya shughuli zote anazopaswa kufanya mke.
Muda kidogo akaniambia niende nyumbani kupumzika kwakuwa yeye anaenda kusalimia kwao, mi nilikubali kwavile nilikuwa nikimpenda kweli.
Niliporudi nyumbani ukapita mwezi mzima bila ya barua wala nini, nikajigundua kuwa nina ujauzito ikabidi nifunge safari na kwenda kule nilipokutana nae ila kule nilikutana na marafiki zake tu ambao waliniambia kuwa Deo alikuwa pale kwa kazi ya mkataba tu na ameondoka kwavile mkataba wake umeisha. Ikabidi niwaambie ukweli wale rafiki zake kuwa nina ujauzito wake nao wakasema kuwa watawasiliana nae. Nilizunguka hapo siku nzima nikingoja majibu, ilipokuwa jioni rafiki yake akaniita na kunipa majibu haya,
'Sabra, Deo amesema kuwa haitambui hiyo mimba yako kwakuwa alikuwa na wewe kujifurahisha tu na hata hivyo ana mke wake na wanapendana sana na huyo mke wake ni mjamzito kwasasa kwahiyo usimsumbue tena'
Kwanza nilishtuka kusikia kuwa Deo alikuwa na mke kwavile mimi hakuniambia kama ana mke na siku zote nilijua hivyo ila nilivyoambiwa vile na rafiki yake nikakosa raha kabisa.
Kurudi nyumbani akajitokeza kijana aliyetaka kunioa ila alipogundua kuwa nina mimba ni hapo akaahirisha swala zima la ndoa juu yangu halafu familia yangu nzima ikanitenga kutokana na ule ujauzito na ndiomana nikatokea kuichukia mimba yangu. Nakiri wazi kujaribu kuitoa ile mimba ila ilishindikana hadi nilipojifungua ila kiukweli sikuwa na upendo wowote na mwanangu naomba tu unisamehe Sam yani kuna muda nilikuwa nakuhurumia sana na ndiomana alipokuja mdogo wangu na kujitolea kukulea nikafurahi sana kwani niliamini ungekuwa katika maadili mema ingawa ulikuwa na roho ya tofauti kabisa hadi kufikia kuua watoto wa baba yako wa kambo ila haikutakiwa ufanye vile Sam ingawa unalalamika kuwa nilikutenga ila hujui jinsi gani na sisi tulitengwa na ndiomana tukafanya msiba kuwa umekufa ili watu wapunguze kunitenga maana Sam mwanangu umemaliza watoto wa watu pale mtaani tena bila hata makosa. Hata sijui una kitu gani, nilipoambiwa unaoa sikuja kwani sikutaka kuwa shuhuda wa kifo cha binti unayemuoa"
Aliongea huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini, ila Sam kwavile alishajiandaa kwa maswali akamuuliza Deo sasa,
"Eeh na wewe kwanini ulinikataa?"
Deo aliongea kwa masikitiko kwani bado alikuwa haamini kile kinachotokea mahali hapo.
"Kwanza kabisa bado siamini kinachoendelea, pili naomba msamaha kwa wote. Sabra, mimi nilikuwa Mwanza kikazi kweli ila kipindi nipo na wewe nilikuwa nimecha mke wangu Dar ni mke ambaye nimefunga nae ndoa takatifu kabisa ambaye ndio huyu hapa. Nilikuwa nampenda kweli ila kitu kilichokuwa kikinikera kwake ni lile swala la yeye kushinda kwenye kwaya kila siku. Kitu kingine nilirudi Dar na kukaa huku Mwezi mzima na mke wangu nae akawa mjamzito ndipo napokea simu kuwa Sabra ni mjamzito sasa simu yenyewe niliambiwa kuwa mimba ya Sabra inaonekana kuwa na wiki moja au mbili hivi ningekubali vipi wakati niliachana nae miezi miwili iliyopita? Ndiomana ikawa ngumu kwangu kukubaliana na hilo swala. Ikapita miaka na miaka bila ya mimi na yeye kuonana nae, nikakutana na wajina wake yule ni rafiki yake kabisa nilimuuliza naye akaniambia kuwa Sabra ameolewa na anafamilia yake ni hapo nilipogundua kuwa Sabra alitaka kunibambikizia mimba maana kuna mambo nilijaribu kumuhoji huyo rafiki yake na nikapata majibu yaliyonyooka kabisa. Ila kinachonishangaza ni kuwa kwanini Sabra aligombana na Sam pale kwangu na kusema kuwa atampigia simu mama yake ili tuhakikishe. Kwanini hakuniambia kuwa mama wa Sam ni wewe wakati wewe ni rafiki yake au urafiki wenu ulikufa?"
"Urafiki wetu ulikufa kweli na yote chanzo ni huyu Sam kwani alimaliza mabinti wa mtaa mzima"
Sam akatabasamu na kusema,
"Hivi mnajua kama sababu zenu hazina mashiko ya kunichukia mimi? Mnalitambua hilo lakini? Bado hamjanipa sababu stahiki za kunichukia, haya mama umesema umenichukia sababu ulikataliwa na mambo ambayo mimi niliyafanya. Haya sasa na wewe baba ni kitu gani kilichokuwa kinakupeleka kunichukia ingawa hukujua kama mimi ni mwanao?"
"Sam, jaribu kunielewa tafadhari sikujua kama mwanangu unateseka, mimi ni binadamu mwenye huruma sana na hata sikuwa nikikuchukia kiasi hicho yani chuki yangu ilitokana na kilichotokea kipindi kile. Kwakweli hii dunia haina haki jamani, mimi nimelea mtoto wa mwenzangu bila kinyongo na nikampenda na kumuhudumia kwa kila kitu kumbe mwanangu alikuwa akiteseka? Halafu sijui mimi nafanyaje jamani hawa watoto wangu wote hawa. Sijui hata sura yangu inakaaje kwenye maelezo"
Mama Sabrina alikuwa kimya kabisa akiwasikiliza kwani hata kwake yale mambo yote yalikuwa mageni kabisa.
Sam akazungumza tena,
"Najua una mawazo ya kuhusu mimi na Sabrina ila swala hilo tuachie wenyewe tunajua jinsi ya kulitatua. Ila tu leo nimegundua kuwa kwanini nampenda sana Sabrina, nimegundua kuwa kwanini siwezi kumdhuru Sabrina. Nawashukuru kwa kunifanya hivi nilivyosasa ila muda mtakapogundua kuwa nipoje kwasasa mnaweza ichukia ile siku ya kwanza mliyopanda kitandani na kupata raha zenu zilizopelekea kutungwa kwa mimba yangu. Na pia mtachukia zile chuki zenu zilizonikuza, nawaambia kweli mkinijua vizuri mtanichukia kushinda mlivyokuwa mkinichukia mwanzo. Mimi ni mwanadamu mwenye huruma sana ila pia nina roho mbaya kushinda maelezo ya kawaida. Mimi Sam, nawahakikishia kabisa mkinifahamu vizuri mtanichukia zaidi, nimemaliza. Kwasasa naomba kila mmoja akapumzike na kuyatafakari haya mambo nyumbani kwake"
Mama Sam akadakia,
"Sasa na mimi nitaenda wapi?"
Sam akacheka na kuwaambia kuwa maongezi yameisha kwahiyo ni muda wa kuondoka.

Sabrina na Jeff walikaa pale sebleni kwa muda mrefu sana wakisubiria wale wamalize maongezi yao hadi na watoto nao wakalala pale na kwenda kuwalaza.
Ila wakati wakiendelea kukaa pale walijikuta wakitazamana sana kisha Jeff akamsogelea Sabrina na kuanza kumbusu mdomoni, muda huo Sam na wale wazazi wao wakafika pale sebleni na kuwashangaa.

Ila wakati wakiendelea kukaa pale walijikuta wakitazamana sana kisha Jeff akamsogelea Sabrina na kuanza kumbusu mdomoni, muda huo Sam na wazazi wao wakafika pale sebleni na kuwashangaa.
Kwakweli kitendo kile kilimfadhaisha sana Sam na kumfanya atamani kuwafanya chochote kile kibaya kwani ndiye aliyetoa hamaki kubwa na kufanya Jeff na Sabrina kushtuka.
Sam akawafata karibu kisha akamuinua Sabrina na kumpiga kofi moja lililompeleka hadi chini halafu akamgeukia Jeff na kumpa ngumi moja ya pua iliyomfanya apatwe na kizunguzungu, ikabidi Deo aingilie kati lile swala ila Sam alionekana kubadilika sana na kujawa na hasira kupita maelezo ya kawaida.
Alichokifanya Deo ni kumtoa Jeff nje ya nyumba hiyo, wakati huo mama Sabrina aliinama na kumuinua Sabrina pale chini.
Deo aliingia tena ndani ili kuwataka Sabrina na mama yake watoke nje, ila Sam akaongea kwa ukali kuzuia kuwa Sabrina asiende popote pale.
Ikabidi na wengine wasimame kwani ilikuwa ngumu kumuacha Sabrina pale ilihali Sam alionekana kuwa na hasira sana,
"Naomba muende ila Sabrina muacheni hapa hapa"
Sabrina aliwaona wazazi wake walivyokuwa na mashaka, kwahiyo nae akajitoa kwa kuomba waende,
"Mama, nendeni tu msijali kuhusu mimi"
"Hapana mwanangu, unakuwa salama kweli?"
"Nitakuwa salama ndio yani hata msiwe na mashaka juu yangu"
Wazazi wa Sabrina walitoka pale huku miyoyo yao ikijawa na mashaka kuhusu mtoto wao ukizingatia kwa ile hali ambayo alikuwa nayo Sam.

Mule ndani kwa Sam alibaki Sam mwenyewe, Sabrina na watoto pamoja na mama Sam ambapo Sam alielekea chumbani kwake ila mama yake alikuwa kimya kabisa akitafakari kile alichokiona muda mfupi uliopita na kile kilichofanywa na Sam kwa huyo Sabrina, hofu ya huyu mama ikawa ni juu ya Sam kumdhuru Sabrina ukizingatia kwenye kile kikao aliwahakikishia kabisa kuwa yeye ni mtu mbaya sana na kama wakigundua ubaya wake watazidi kumchukia.
Kwakweli huyu mama alimuhurumia sana Sabrina kwani alimjua fika mwanae kuwa ni mtu asiye na huruma kabisa.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walipofika nyumbani wazazi wa Sabrina na Jeff, ikabidi mama Sabrina avunje ukimya kwa kumuhoji Jeff maswali kidogo,
"Jeff unajua sijawaelewa kabisa pale wewe na Sabrina"
"Nisameheni tafadhari"
"Unaomba msamaha wakati hujatuweka wazi? Tuambie kwanza kuwa nini kinaendelea ndipo uombe huo msamaha. Ilikuwaje wewe umbusu Sabrina mdomoni?"
Jeff alifikiria kidogo na kuona ni bora afunguke tu kwa hawa wazazi wa Sabrina,
"Naomba mnisamehe sana ila kwakweli mimi nampenda sana Sabrina"
Wazazi wa Sabrina wakashtuka na kumuuliza vizuri Jeff kuwa anampenda kivipi.
Kabla Jeff hajaweka sawa maelezo yake simu yake ya mkononi ikaita na kuipokea kwani mpigaji alikuwa ni Sam na alihofia kutokuipokea kibarua chake kingeota nyasi.
Sauti ya Sam kwenye simu ikamwambia Jeff kwa ukali,
" Ole wako uwaambie ukweli hao wazazi wa Sabrina"
Kisha ile simu ikakatwa na kumfanya Jeff abakie nayo sikioni tu.
Mama Sabrina akamshtua ili waendelee na mada yao ila Jeff akawaomba ruhusa kidogo ya kutoka hapo na kwavile waliona hayupo sawa gafla waliamua kumruhusu tu.
Ila walibaki na maswali,
"Hivi umemuelewa huyu kijana?"
"Sijamuelewa kabisa, halafu huyu kwa Sabrina si ni kama mtu na mdogo wake?"
"Ndio ipo hivyo na kila siku huitana kwa heshima sana kwakweli leo nimeshangaa. Yani leo imekuwa ni siku ya ajabu sana kwangu, angalia muda ulivyoenda yani sasa hivi ni saa sita usiku ila bado tupo macho."
Baba Sabrina akatoa ushauri wa kwenda kulala ingawa mawazo yake yote yalikuwa juu ya mtoto wao Sabrina.

Na leo Sabrina nae hakuweza kulala kabisa akimfikiria Sam na kujiuliza mambo mengi sana kuwa imekuwaje kuwaje hadi Sam kuwa ni kaka yake na vipi baada ya kugundulika hivyo ni nini kitaendelea kati yao?
Na pia Sam atachukua uamuzi gani mwingine tena wa kumuadhibu yeye kwa kosa la kumkuta akimbusu Jeff.
Kwakweli Sabrina hakuweza kulala kabisa ingawa Sam hakumuita wala hakumwambia chochote toka ule muda aliomnasa kibao.

Kulipokucha Sam aliingia chumbani kwa Sabrina na kumkuta yupo macho kwani ukweli ni kuwa hakulala usiku kucha.
Sabrina nae kumuona Sam akashtuka sana ila Sam akamwambia Sabrina,
"Sitaki umwambie chochote huyu mama yangu kuhusu mimi na wewe, pia usiwaeleze chochote wazazi wako. Sawa?"
Sabrina aliitikia kwa kutikisa kichwa. Kisha Sam akatoka na kuondoka zake.
Sabrina akapumua kidogo na kuangalia watoto wake ambao walikuwa wamelala kwa muda huo kisha yeye akainuka pale kitandani na kuelekea sebleni.

Alimkuta mama Sam amekaa sebleni huku amejiinamia tu na kumsalimia.
Ila yule mama kabla ya kuitikia salamu alimuuliza swali Sabrina,
"Hivi mnaishije humu ndani? Baba anatokea kushoto na mama kulia?"
"Ila mama na wewe si umeshuhudia changamoto ya jana kuwa Sam ni kaka yangu!"
"Kwahiyo kama ni kaka yako ndio ukaamua jana umbusu mwanaume mwingine mbele yetu? Na yule kijana ni nani?"
Sabrina alikaa kimya kwavile alikosa majibu kwa muda huo.
Huyu mama nae alizidi kumuuliza maswali Sabrina,
"Eeh uliwezaje kuishi na Sam hadi kufikia hatua ya kuzb nae? Uliwezaje?"
"Mimi na Sam tunapendana na ndiomana niliweza kuishi nae"
"Mbona swali la nyuma yake hujajibu? Yule kijana wa jana ni nani kwako?"
Kwakweli hapa Sabrina akaona ni kupotezeana maana kwani hata hakujua vya kumjibu na kujikuta akiinuka na kuondoka pale sebleni akaelekea jikoni.

Sam alimpigia simu Jeff na kumuhitaji ofisini kwake kabla ya kazi yoyote ile ya siku hiyo, naye Jeff alitii na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Sam ambapo alimkuta Sam akiwa ametulia kwa kumngoja.
Swali la kwanza lilikuwa,
"Ulijisikiaje uliposikia jana kuwa Sabrina ni dada yangu?"
Jeff alikuwa kimya tu akitafakari kile alichoulizwa na Sam.
"Tafadhari nijibu Jeff tena unijibu ukweli mtupu kwani ukiniongopea tu nitajua. Niambie kuwa jana ulijisikiaje?"
Jeff aliamua kujibu huku akitetemeka,
"Nilifurahi"
Sam akapiga makofi,
"Jibu zuri sana hilo halafu ni jibu la ukweli, ngoja na mimi nitakufurahisha zaidi. Haya niambie, ndio ukaamua kumbusu mke wangu baada ya kusikia kuwa ni dada yangu?"
"Nisamehe, ilikuwa bahati mbaya"
"Acha kunichekesha Jeff, bahati mbaya kumbusu mke wa mtu tena nyumbani kwa mume? Leo kabla hujaondoka uje tuzungumze tena, haya nenda kaendelee na kazi."
Jeff aliinuka pale na kwenda kwenye kazi sasa huku akiwa na mawazo mengi kupita maelezo ya kawaida.

Wazazi wa Sabrina walikuwa na mawazo sana kuhusu binti yao ukizingatia mambo yaliyotokea jana yake hayakuwa mambo ya kawaida.
Ila mama Sabrina nae akakumbushia kidogo kwa kile ambacho kimewahi kutokea huko nyuma huku akilinganisha na mambo ya jana.
"Kumbe kipindi kile umeenda Mwanza Deo ndio ulienda kuishi na yule mwanamke jamani na kunidanganya mimi!"
"Hebu na wewe unyamazage tu maana kati ya mimi na wewe nani muongo? Nilirudi hapa ukanidanganya kuwa mimba ni yangu hata nikamkataa mwanamke aliyebeba mimba yangu kweli, nikalea na kumlea mtoto pia......"
"Basi yaishe"
"Yaishe nini? Hapa umeyaanzisha mwenyewe na hayawezi kuisha haya, nimelea mtoto asiye wangu kumbe wangu anateseka na kukataliwa. Ila nakumbuka nilijaribu kumtafuta yule mwanamke kipindi kile bila ya kumpata yani eti nagundua kuwa mwanangu ameishi maisha ya kupandikizwa chuki jamani eti alikuwa hapendwi na jamii iliyomzunguka jamani, Mwisho wa siku Mungu ananipiga kofi, nimemuozesha mwenyewe binti yangu kwa mtoto wangu. Kwakweli hili swala linaniuma sana. Hii dunia haitendi haki, dunia haina usawa kabisa. Nimelea watoto wa wenzangu katika maadili mema na wamekuwa watoto wazuri sana wenye kujitambua. Eti mwanangu kamuoa dada yake na bado ananitishia kuhusu hili. Tafadhari Joy niambie kuwa na kwa Sabrina ulichakachua ili angalau nipate amani ya moyo"
Kwakweli hii kauli ya Deo ya kusema amwambie kuwa alichakachua na kwa Sabrina ilimpa hali ya kucheka mama Sabrina ila akatulia kwani alijua kuwa Deo anasema vile ili angalau apumzishe moyo wake kwa mawazo aliyokuwa nayo.

Mama Sam nae kwavile alihitaji kujua mengi kwa Sabrina aliamua kumfata kule kule jikoni,
"Niambie ukweli tafadhari, nieleze vile unavyoishi na Sam"
"Naishi nae kawaida tu"
"Hivi unajua ni mabinti wangapi kawaua kule mtaani? Unajua kama aliua hadi watoto niliokuwa naishi nao waliomuona kama kaka yao kwa kipindi hicho unalijua hilo?"
"Najua ndio"
Mama Sam alimuona Sabrina kuwa ni mtu mwenye dharau kwani majibu alikuwa akiyatoa kwa mikato na hiko kitu kilimkera sana mwanamke huyu ambaye alihitaji kujua mengi kuhusu Sam na huyo Sabrina ila kwavile Sabrina hakuwa na majibu yaliyonyooka akaamua aachane nae kwa muda kwanza.

Sam kama ambavyo alivyopanga, muda wa kutoka akamuita Jeff na kuongozana nae kisha wakaenda kukaa mahali penye utulivu kidogo ambapo Sam alimwambia Jeff,
"Tafadhari nieleze toka siku ya kwanza ulipolala na Sabrina hadi leo. Usinifiche kitu, nieleze ukweli wako wote na huo ukweli ndio utakaokuokoa wewe na kama ungenificha unaweza kujutia huu muda na kutamani masaa yarudishwe nyuma hata kama haitawezekana"
Jeff akafikiria kwa muda, kisha akaamua kufunguka tu kuwa siku ya kwanza alimuwekea madawa kwenye kinywaji na kumfanya aweze kumuingilia kimwili.
"Kwahiyo kumbe ni kweli ulimbaka?"
Jeff akaitikia kwa kichwa,
"Haya sasa endelea"
Jeff akaeleza ukweli wa jinsi gani anampenda Sabrina na akaeleza vile ambavyo alilala na Sabrina kwa mara ya pili na kumpa mimba tena.
"Haya nimekuelewa Jeff tena nimekuelewa sana. Sasa unaweza kwenda nyumbani kwenu na ukayatafakari yote uliyoniambia muda huu"
Jeff aliondoka pale huku akiwa haamini amini kama Sam amemuachia huru na salama kabisa kiasi kile.

Jeff akiwa njiani kuna mdada alikuja na kumsalimia, kisha akamuuliza kuhusu Sam na kumpa stori ile ile aliyowahi kuambiwa kabla.
Ikabidi Jeff amuuize huyu dada,
"Samahani dada, umekuja na kunisalimia kisha umeanza kunipa maelezo kuhusu Sam. Je ni nini tatizo? Kwanini umekuja kuniambia mimi?"
"Wewe ni kaka wa marehemu Amina si ndio?"
Jeff akashtuka kidogo na kumshangaa huyu dada kujua undugu wake na Amina ila akaitikia hivyo hivyo kuwa ni kweli ana undugu naye,
"Ndiye aliyenituma nikwambie, anataka uipiganie damu yake. Anataka umpiganie kama ndugu yake, huyu Sam ameshamaliza wengi sana. Nduguyo Amina anataka ufanye kitu Jeff, fanya kitu kwaajili yake"
Jeff akashtuka tena baada ya kumsikia huyu dada akimtaja kwa jina kabisa na kugundua kuwa lazima anamfahamu vizuri ila imekuwaje huyu akajua kilichomuua Amina ikiwa maelezo toka kwa Amina aliyapata yeye na mama yake tu? Jeff akashikwa na hofu na kumtazama vizuri huyu dada ila huyu dada alitabasamu na kuondoka.
Jeff alisimama kumuangalia alipokuwa akielekea ila yule dada alipotaka kukata kona aligeuka nyuma na kumpungia mkono Jeff kisha kuondoka.
Kwakweli Jeff alishtuka sana kwani aliiona sura ya Amina kabisa kwa yule dada.

Mama Sam nae aliendelea na swala lake la kumfatilia Sabrina.
Jioni hii alienda kukaa karibu na Sabrina ili ajaribu kumuuliza tena ila muda huu Sabrina alikuwa kampakatia mtoto wake mdogo huku Cherry akicheza cheza pembeni.
Mama Sam akamuuliza Sabrina,
"Mbona hawa watoto wanafanana na yule kijana wa jana?"
Mara akajibiwa na Cherry,
"Kwani wewe unatakaje?"
Kwakweli mama Sam akashangaa sana na kuuliza,
"Aliyeongea ni mtoto au mtu mzima?"
Cherry akajibu tena,
"Mtu mzima kushinda wewe"
Hii kauli ikamshtua na Sabrina pia, wakajikuta kwa pamoja wakimtazama Cherry na gafla alikuwa tofauti na watoto wengine mbele ya macho yao.

Kwakweli mama Sam akashangaa sana na kuuliza,
"Aliyeongea ni mtoto au mtu mzima?"
Cherry akajibu tena,
"Mtu mzima kushinda wewe"
Hii kauli ilimshtua na Sabrina pia, walijikuta kwa pamoja wakimtazama Cherry na gafla alikuwa tofauti na watoto wengine mbele ya macho yao.
Wakatazamana kwa mshangao ila walipogeuka ili wamtazame tena Cherry hakuwepo katika eneo lile.
Sabrina aliamua kuita ili ajue yuko wapi kwani ni muda huo huo tu ambao walishangaa kuwa hayupo pale.
Sabrina aliita ila Cherry hakuitika, Sabrina alitaka kuinuka ili akamuangalie vyumbani ila mama Sam akamzuia,
"Sabrina tafadhari tulia hapo, sijakujua vizuri ila nakupenda kuliko unavyonifikiria. Najua unaupendo na mwanao ila hii hali sio ya kawaida. Subiri hapo atarudi mwenyewe, sipendi upate matatizo kwasababu ya maswali ambayo nilikuwa nayauliza mimi. Sawa Sabrina?"
Sabrina akaitikia kwa kichwa tu ila alikuwa na mawazo mengi sana kumuhusu mtoto wake huyo mwenye majibu kama mtu mzima na kupoteza kumuonekano wa mtoto wa kawaida kabisa.

Familia ya Sabrina kwa kipindi hiki haikuwa sawa kabisa kwani muda mwingi Deo alikuwa na mawazo na kujiona akionewa sana kwa adhabu aliyoipata dhidi ya mtoto wake.
"Kwanini kwangu mimi? Ni ubaya gani niliotenda mimi? Mbona mimi nilimkubali mtoto wa nje? Kwanini wangu hakukubaliwa? Kwani wangu kaoana na dada yake? Kwanini wangu amekuwa na chuki moyoni mwake? Hivi maisha gani haya? Mbona hali ni mbaya kwangu?"
Kwakweli Deo alikuwa ni mtu wa kujiuliza maswali bila ya majibu na hakuwa na raha kabisa, kila muda alikuwa akikumbuka malezi aliyompa James ingawa alijua wazi kuwa si mtoto wake, sasa swala la kuambiwa kuwa mwanae alinyanyasika na hakutakiwa kabisa na baba yake wa kambo lilimfanya aumie moyo wake kila muda.
Mama Sabrina alijaribu kukaa naye karibu ila haikusaidia kitu kwani maswali yake yalikuwa ni yale yale ila hayakuwa na majibu yoyote.

Sam akiwa anarudi nyumbani kwake aliona mdoli akiuzwa na kuvutiwa na mdoli huyo huku akili yake ikimlenga Cherry tu kuwa akachezee mdoli huyo.
Aliamua kusimamisha gari yake na kumnunua huyo mdoli kisha kuondoa gari yake akielekea nyumbani kwake.
Akili ya Sam ilimfikiria Sabrina katika aina mbili kama mke na kama dada yake.
Katika kufikiria huko alimfikiria pia mtoto Cherry kwa kitendo chake cha kumtumia katika mambo yake ila hakuwa na jinsi ya kubadilisha alichokitengeneza kwa mtoto huyo ukizingatia yeye binafsi aliona ila tabia kuwa sawa kabisa na hakufikiria kama kuna kipindi itakuwa na madhara kwenye maisha ya mtoto huyo.

Sam alifika nyumbani kwake na kumkuta mama yake pamoja na Sabrina wakiwa pale sebleni.
Baada ya salamu swali la kwanza ni kuulizia alipo Cherry,
"Yuko wapi Cherry, nina zawadi yake"
Sabrina na mama Sam wakatazama, na hapo hapo wakamsikia Cherry akijibu,
"Mimi hapa"
Walitazama sauti ilipotokea na kumuona amekaa tu kwenye kochi, Sabrina na mama Sam walishtuka ila Sam mwenyewe alimfata Cherry pale na kumwambia,
"Umdogo sana mwanangu hadi sijakuona jamani kumbe upo hapa hapa"
Kisha akamkabidhi yule mdori na kunyanyuka nae akielekea chumbani kwake.
Mama Sam akamtazama tena Sabrina na kumuuliza,
"Unaelewa lakini?"
"Sielewi kitu mama"
"Pole sana ila kuwa makini, Sam ni mwanangu ila huwa simuamini"
Kisha huyu mama nae akanyanyuka na kuelekea chumbani.
Sabrina alibaki pale sebleni akitafakari ile hali halisi ya mtoto wake kwani kadri siku zilivyokwenda ndivyo alivyozidi kutokumtambua mwanae wala kwa anayoyafanya.
Kisha akainuka na kwenda kuandaa chakula ingawa moyo wake ulikosa amani kwa mambo ya mwanae kwa siku hiyo.

Sabrina alipomaliza kuandaa chakula alienda kumgongea Sam na kumuita ili asogee mezani kula, kisha akaenda kumuita mama Sam ili wajumuike kwa pamoja.
Walipokuwa mezani wakila, mama Sam aliamua kuukata mzizi wa fitina na kuongea mahali pale,
"Sam mwanangu, nimeishi hapa yapata wiki sasa ukiachana na yale majanga na misukosuko. Naomba kuongea ya moyoni"
"Sasa hayo ya moyoni mama umeshindwa nini kuongea tutakapomaliza kula hadi utake kuongea muda huu?"
"Sam, tukimaliza kula nakupata wapi wewe na unakimbilia chumbani?"
"Haya ongea ila ukipatwa na matatizo sababu ya kuongea wakati wa kula mi simo"
Mama Sam hakujali vitisho vya Sam kwani alishadhamiria kuongea muda mrefu sema tu ilikuwa ngumu kupata muda wa kujadili mambo na Sam.
"Sikia Sam mwanangu, ni kweli wazazi wako tulifanya makosa tena makubwa sana. Na ni kweli mmefunga ndoa takatifu na huyu Sabrina ila kumbuka kuwa kwasasa mmefahamu kuwa ninyi ni ndugu watoto wa baba mmoja, na kwa mila zetu sisi ni laana na dhambi kubwa kuona kaka na dada wamefunga ndoa. Tafadhari muhurumieni Deo, yule ni baba yenu"
"Yani uliposema una ya moyoni nilidhani ni mambo ya maana sana kumbe ni hayo! Usitake kunichekesha mama, hivi kwa fikra zako sisi tunamuhurumia vipi? Kumbuka tumefunga ndoa tena wewe mwenyewe umekiri hapa kuwa ndoa takatifu sasa unataka tufanye nini? Tuachane? Wakati tuna watoto wawili tayari! Kama kosa mlishalifanya hapo ni mkubaliane na makosa yenu tu"
"Hapana Sam, hebu jiweke nafasi ya baba yenu kwasasa na ujaribu kujua kuwa anajisikiaje"
"Kwakweli mama kama huna hoja bora unyamaze tu na tuendelee kula kwa amani. Usiniletee khabari za huyo mtu kwani mimi sina baba na huyo simtambui kama baba yangu ila namtambua kama baba mkwe wangu."
Mama Sam akapumua kidogo na kuendelea kumshawishi Sam ili angalau apatwe na moyo wa huruma ila ilishindikana.
Akaamua kuweka hoja nyingine sasa ya kuhusu Cherry,
"Halafu Sam, huyu mtoto wenu mbona haeleweki, mara anaongea kama mtu mzima, mara anachezesha macho isivyo kawaida na mara anabadilika. Nina mashaka kuwa huyu mtoto huenda akawa......"
Mama Sam akapaliwa na kukwamia hapo kwani alikohoa kwa mfululizo hata yeye mwenyewe akajionea huruma.
Alikohoa hadi akatoa machozi, Sabrina alienda kumletea maji ili anywe ila bado haikusaidia na kumfanya ainuke na kuelekea chumbani ambapo Sabrina alimfata ili kuangalia hali yake ila Sam alimalizia kula muda ule kisha akainuka na kwenda chumbani kwake kulala bila ya kujali kuwa mama yake alikuwa akikohoa hapo kwa kupaliwa kamavile roho inatoka.

Sabrina alikaa na yule mama hadi alipotulia na kulala, kisha yeye akatoka na kuelekea chumbani kwake ambapo alimkuta Cherry amekaa tu kitandani,
"Vipi leo mwanangu hulali wewe?"
"Mpaka wewe ulale"
"Mmh haya, mimi nalala basi"
Sabrina akajilaza ila mawazo yake yote ni juu ya mtoto wake huyu kwani alimuona kuwa mtoto asiye wa kawaida kwani alifanya mambo ya tofauti sana.
Sabrina hakuweza kulala kabisa na alikuwa macho akijigeuza huku na kule kwani kila alipomfikiria na baba yake ilikuwa ni sababu kwake kukosa raha na usingizi kiasi kile.
Ila kila alipogeuka na mwanae naye alikuwa macho ila alipomuuliza hakujibiwa safari hii ila alimuona mwanae akicheka tu kila alipomuuliza swali la kutokulala.

Kulipokucha alfajiri na mapema, simu ya Sabrina ilipata ujumbe.
Alipoangalia ule ujumbe ulikuwa unatoka kwa mama yake,
"Tafadhari Sabrina mwanangu rudi nyumbani, muhurumie baba yako. Huku hali, hanywi wala halali. Hebu fanya urudi mwanangu, baba yako anateseka sana"
Sabrina aliumizwa na ule ujumbe kwani kila alipokumbuka malezi aliyopewa na baba yake, upendo alioonyeshwa na baba yake alijiona wazi kuwa na kila sababu ya kurudi kwao na kuachana na Sam ili baba yake awe na furaha ila je hapo kwa Sam anaondokaje? Anafanyaje kuweza kumkimbia Sam na kuelekea kwao ikiwa anamtambua vyema Sam alivyo! Kwakweli Sabrina aliumizwa sana na kujikuta akipatwa na mawazo zaidi.
Muda kidogo Sam alipita na kuwaaga kuwa anaenda ofisini.

Sabrina aliamua kwenda kumuangalia mama Sam anavyoendelea kwa asubuhi hiyo, alimkuta kitandani akiwa hata hawezi kuongea kabisa,
"Vipi mama hali ndio imekuwa mbaya hivi?"
Huyu mama aliitikia kwa kichwa tu kisha akaomba karatasi na peni kwa ishara ili aweze kuandika kile kinachomsibu.
"Naumwa sana Sabrina, tafadhari nifikishie ujumbe kwa Sam kuwa nahitaji kurudi kwangu. Tafadhari aje anisafirishe, siwezi kuendelea hapa"
Sabrina alilisoma hili karatasi na kumuhurumia huyu mama pia kwani alikuwa anatia huruma haswa, kwakweli Sabrina alitamani kama angekuwa na uwezo basi angemsafirisha mwenyewe muda huo huo.
Sabrina aliamua kumpigia simu Sam ili kumpa ujumbe aliopewa na mama wa Sam ila Sam alipoambiwa alionekana yupo kawaida tu wala hakushtuliwa na kile ambacho aliambiwa na Sabrina.
"Wee Sam wee, hivi wewe ni mtu wa aina gani jamani? Kwanini usimjali mama yako wewe? Ni nani kama mama duniani, huwezi pata mama mwingine zaidi ya huyu"
"Mama anayekiri wazi kabisa kuwa alitaka kutoa mimba yangu? Kwanza kitendo cha mimi kuishi nae tu hapo nyumbani ni kumuheshimu ila asijali nakuja kumchukua nimsafirishe arudi kwa wanae"
Kisha Sam akakata ile simu na kumfanya Sabrina abakiwe na mawazo tu dhidi yake kwani alishindwa kabisa kumuelewa Sam ukizingatia alitoka na kufunga milango kama kawaida ili wa mule ndani wasiende popote haswaa Sabrina.

Mama Sabrina alitumaini kuwa mwanae ataelewa ule ujumbe aliomtumia asubuhi ila hadi jioni inafika hakuweza kumuona Sabrina pale, ni hapo hofu na mashaka vilipomtawala.
Akakumbuka maisha ya nyuma ya Sabrina alivyokuwa akiwasikiliza wazazi wake ila toka ameolewa na Sam kwakweli Sabrina ameonekana ni mtu asiyesikiliza kabisa anayoelekezwa bila ya kujua kuwa ni vitu gani vimempata Sabrina.
Wakati mama Sabrina akitafakari namna ya Sabrina kurudi nyumbani, mara baba Sabrina akatoka chumbani na alipofika sebleni alianguka na kupoteza fahamu.
Kwakweli mama Sabrina alichanganyikiwa sana kwa hilo tukio na kujikuta akipiga simu kwa mtoto wake mkubwa bwana James ili afike kumsaidia ila Sabrina simu yake iliita tu bila ya kupokelewa.
James alifika na kuanza kusaidiana na mama yake. Muda kidogo mdogo wa Sabrina naye aliwasili na kuanza kusaidiana dhidi ya baba yao.
Kwakweli mama Sabrina aliamua kuwaeleza ukweli tu watoto wake hawa ambao kwa pamoja walijikuta wakimsikitikia baba yao,
" Kwahiyo mama, yule mume wa dada Sabrina ni ndugu yetu? Mbona makubwa haya?"
"Ni ndugu ndio, halafu mnafanana majina sijui hata ilikuwaje. Ila tafadhari mwanangu Sam usiwe kama huyo Sam mwingine maana siku tuliyoenda alikuwa akitutishia tu"
"Usijali mama yangu, kwanza nashukuru kuwa nimerudi ingawa nimemkuta baba akiwa kwenye hali mbaya ila nakuhakikishia mama kuwa baba atapona tu tena nakuhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Sijawahi kuzungumza sana na huyo Sam ila kwasasa utafurahia uwepo wangu mama kwani nakuhakikishia kabisa kuwa wote tutakuwa salama, kisha huyu Sam akakumbatiana na mama yake kama ishara ya kumtia moyo na kumuhakikishia kuwa yote yanawezekana.
Halafu akarudi nyumbani na kumuacha mama yao hospitali.

Muda wa kulala ulipofika Sabrina alimuhimiza Cherry ainuke ili wakalale ndani kwani alikuwa amekazana kuchezea yule mdoli wake,
"Mwache huyo utamchezea kesho"
Ila Cherry bado alimng'ang'ania, ikabidi Sabrina ampokonye Cherry yule mdole na kumrushia kwenye kiti kingine kisha akamuinua Cherry na kwenda nae chumbani ambapo alilia kidogo na kulala.
Usiku wa leo pia Sabrina hakulala kwani usingizi haukumjia kabisa kutokana na mawazo aliyokuwa nayo ila watoto wake wote walikuwa wamelala.
Wakati akijigeuza geuza pale kitandani akashtushwa na mlio wa simu yake, akaichukua na kuangalia mpigaji alikuwa ni Jeff akashangaa kuwa imekuwaje Jeff kumpigia siku hiyo tena muda huo wa usiku wa manane wakati kwa kipindi hiki alikuwa kimya kabisa.
Sabrina akapokea ambapo moja kwa moja Jeff akaongea,
"Sabrina, nimeota ndoto mbaya sana. Hebu muangalie mtoto wetu Cherry"
Wakati Jeff akiongea macho ya Sabrina yalikuwa yakimtazama Cherry na kumfanya Sabrina ashtuke sana kwani muda huo huo badala ya kumuona Cherry pale kitandani alimuona yule mdoli akiwa amelala kama Cherry.

Wakati Jeff akiongea macho ya Sabrina yalikuwa yakimtazama Cherry na kumfanya Sabrina ashtuke sana kwani muda huo huo badala ya kumuona Cherry pale kitandani alimuona yule mdoli akiwa amelala kama Cherry.
Sabrina hakuweza kuendelea kuongea na simu na kujikuta akiiangusha pale kitandani kisha yeye kuinuka na kukimbilia nje ya chumba huku akihema sana.
Akataka kwenda kukaa kwenye kochi sebleni ila alipoangalia akamuona yule mdoli pale kwenye kochi, Sabrina alijikuta akipiga kelele bila ya kujielewa na kumfanya Sam atoke chumbani na kumkuta Sabrina akiwa mwenyewe pale sebleni huku akipiga kelele,
"Vipi wewe una mashetani?"
Sabrina alipomuona Sam akamkimbilia na kumkumbatia kwa uoga aliokuwa nao kwa wakati huo.
"Vipi Sabrina nini tatizo?"
"Sam, kuna mambo ya ajabu humu ndani"
"Mambo ya ajabu kivipi? Yapi hayo ya ajabu?"
Sabrina akamuonyesha Sam,
"Unamuona huyo mdoli kwenye kochi?"
" Ndio, kwani kafanyaje?"
"Twende"
Sabrina akamvuta Sam hadi chumbani kwake na kumwambia aingie ili ajionee mwenyewe.
Sam aliingia bila ya kuona chochote cha tofauti,
"Wee Sabrina mbona hamna kitu?"
Sabrina akaingia na kushangaa kumuona Cherry akiwa amelala kama kawaida.
"Haya niambie kitu gani cha tofauti hapo"
Sabrina alikuwa katoa mimacho tu kwani hata hakuwa na jibu, ikabidi Sam amuulize kuwa tatizo ni nini.
"Tatizo ni yule mdoli, nilimuona huku chumbani kisha namuona sebleni"
"Acha kunichekesha Sabrina, hayo ni maruweruwe tu"
"Maruweruwe! Sam kwasababu hujaona ndiomana unasema hivyo. Kwakweli mimi siwezi kulala tena yani siku hizi ni afadhari mchana kwangu kuliko usiku. Tafadhari Sam nipe ruhusa nirudi nyumbani"
"Ili ukafanye nini?"
"Sam kumbuka mimi ni dada yako"
Sam akacheka kwa ile hoja ya Sabrina,
"Sasa kama wewe ni dada yangu ndio nini kwa mfano? Si nilishakuoa wewe au umesahau kama tumefunga ndoa ? Umesahau kama tulikula kiapo kuwa hatutaachana hadi kifo kitakapotutenganisha! Iweje sasa utumie hoja ya udada na ukaka Sabrina? Wewe tulia tu hapa, mimi hata sibabaishwi na undugu kati yetu ilihali tulishafunga ndoa yani wewe tulia tu"
"Jamani Sam"
"Hakuna cha jamani, kama unaogopa kulala nenda kawashe Tv uangalie hadi kunakucha au njoo ulale na mimi chumbani. Halafu kesho namsafirisha huyo mama kwahiyo utaendelea kubaki kama kawaida na watoto wako"
Kisha Sam akaenda zake chumbani kwake.
Sabrina alirudi kitandani akakaa na kuwatazama watoto wake.
Alikuwa anaiwaza ile siku ya kwanza yeye kufahamiana na Sam, akakumbuka mambo yaliyomfanya hadi akakutana na Sam ni mapenzi tu kwani ndio yaliyomkimbiza mji hadi akaenda kukutana na kiumbe huyo ambaye mwanzoni alimfanyia mambo mema na mazuri ila badae aligeuka kuwa mbwa mwitu.
Ingawa amegundua kuwa ni kaka yake ila amebaki na maswali tu kuwa baba yake amewezaje kutoa mtoto mwenye roho mbaya kama huyo.
Sabrina hakulala hadi panakucha.

Kama ambavyo Sam alivyoahidi, asubuhi na mapema alimshtua mama yake kisha akajiandaa kwa kuianza safari.
Yule mama alitoka akimtazama Sabrina kwa huruma sana, alimkumbatia na kumuaga kwani bado sauti haikuweza kutoka.
Walipoagana wakatoka na Sam, na kama kawaida ya Sam akafunga milango ya nje na kuondoka na mama yake kwahiyo alimuacha Sabrina ndani na watoto wake, kwakweli Sabrina hakuwa na raha kabisa ikabidi ajitoe fahamu na kumwambia mwanae Cherry,
"Cherry mwanangu, mimi ni mama yako nakupenda sana. Tafadhari usinitishe mama yako, nakupenda jamani mwanangu"
Cherry akatabasamu tu kisha Sabrina akaenda kuwaandalia chakula watoto hao.

Sam aliagana na mama yake stendi kisha yule mama akapanda kwenye basi na safari ikaanza.
Alipokuwa kwenye basi alijaribisha kuongea na kujiona anaweza kabisa kuongea, wakati huo huo akachukua simu yake na kumpigia mdogo wake,
"Narudi Arusha mdogo wangu, tafadhari nipokee nina mengi ya kuzungumza na wewe"
"Na mbona ulikuwa kimya siku zote hizi? Nakupigia simu hupokei kwanini lakini?"
"Nitakusimulia mdogo wangu ni makubwa sana yaliyonipata hata sijui huyu Sam ulimlea vipi kwakweli"
Akakubaliana na mdogo wake pale kuwa atamsimulia vizuri akifika.

Sam akiwa ofisini siku ya leo akapatwa na mgeni aliyepelekwa pale na Jeff.
"Karibu"
"Unanikumbuka lakini!"
"Hebu nikumbushe kidogo"
"Mimi wajina wako, ni mdogo wa Sabrina"
Sam kusikia hivyo akafurahi sana na kumkaribisha vizuri sasa, ikabidi Jeff awaache ili waweze kuendelea na mazungumzo.
"Nadhani ingekuwa ni vyema tukapata mahali tuzungumze"
Sam hakupinga na kwavile ofisi ilikuwa yake basi alikuwa na uwezo wa kufanya chochote anachojisikia.
Kwahiyo akaamua kutoka hapo na huyo mdogo wa Sabrina kisha wakaelekea hoteli ya karibu na kukaa kwaajili ya mazungumzo huku wameagiza vinywaji.
"Eeh nakusikiliza sasa ila kabla ya yote napenda kujua kuwa wewe unakuwaga wapi? Mambo yote yanayotokea kwenye familia yenu wewe huwa haupo"
"Ni kweli huwa sipo sababu mara nyingi huwa najishughulisha na maswala ya utafutaji."
"Haya sasa tuendelee na hoja"
Mdogo wa Sabrina akamueleza Sam jinsi alivyoambiwa kuwa wana undugu na yote yaliyotokea,
"Kwanza huwezi amini, niliposikia kuwa wewe ni ndugu yetu nilifurahi sana yani nilitamani jana ile ile nionane na wewe ila ndio hivyo ikashindikana ndiomana leo nimemfata Jeff ili anilete ofisini kwako kwani mama aliniambia kama anafanya kazi kwako"
"Sasa kilichokufurahisha baada ya kusikia kuwa mimi ni ndugu yako ni kitu gani ilihali nishamuoa dada yako?"
"Unajua nini kaka! Huwezi jua ni kitu gani kilikuwepo kwenye moyo wangu juu yako. Nilishawahi kupinga juu ya ndoa yenu ila sikusikilizwa na ndiomana mimi nilikuwa sijishughulishi kabisa katika mambo yenu"
"Sasa unafikiri sasa itakuwaje?"
"Ninachojua mimi kila kitu hufanywa kwasababu, hakuna jambo lililokosa sababu duniani. Mfano nilipokuja kujua kuwa kaka James si mtoto wa baba nilishangaa sana ila nilishangaa zaidi vile baba alivyokuwa akimuhudumia kaka James, nimeshangaa sana kusikia kuwa baba alikuwa anajua toka mwanzo kuwa kaka James si mtoto wake ila alimuhudumia na kumlea vizuri sana. Leo hii kuna mtoto wake wa ukweli sasa ambaye kalelewa katika mazingira mengine na kumchukia yeye. Nilipomuona baba na kupewa maelezo nilimuhurumia sana"
"Kwani kafanyaje?"
Sam akamueleza kama baba yao yupo hospitali.
"Kule hospitali anaangaliwa na mama pamoja na James hata mimi nilikuwa huko ila hatuna msaada wowote kwake kwani anachohitaji kwasasa ni kukuona wewe tu"
Sam akatulia na kujifikiria kama aende au asiende na kumfanya mdogo wa Sabrina aendelee kuongea kwa kumuomba,
"Tafadhari fanya hivi kwaajili yetu, tuhurumie sasa nawe utaweza kuona uzuri wa huyu baba mwenye moyo wa kulea watoto hata wasio wake."
"Ila hata mimi nina moyo huo"
"Kivipi?"
"Tuachane na hayo, inuka twende nikamuone"
Mdogo wa Sabrina hakutaka kuuliza zaidi kwani alihofia kwa Sam kubadilisha maamuzi.

Walifika hospitali na kuwakuta ndugu wa Sabrina akiwemo shangazi wa Sabrina ambapo wote kwa pamoja wakampisha Sam kwenda kumuona Deo na kwenda kuzungumza nae.
Muda huu mama Sabrina nae akamsogelea wifi yake mdogo na kumuuliza,
"Wifi mbona swala hili hukuliona jamani? Hukuona kama kaka yako ana mtoto wa nje au ulikuwa unanionaga mimi tu jamani!"
"Sasa ndio maswali gani hayo mama Sabrina hapa hospitali?"
"Sio maswali gani, wewe mwenzetu huwa unaona yaliyojificha na ndiomana nimekuuliza kuwa jambo hili hukuliona jamani hadi watoto wa kaka yako wakaoana?"
"Sitakujibu kwasasa hayo maswali yako kwamaana hayana mantiki"
Mama Sabrina akatabasamu utafikiri mumewe hakuwa mgonjwa pale.
Baada ya muda mrefu kupita wakamuona Sam akitoka pamoja na Deo kisha akawaomba wote kuelekea nyumbani ambapo waliondoka kwa pamoja na kuelekea nyumbani kwakina Sabrina.
Walifika na kukaa kikao kidogo ambapo Sam hakuhitaji swali lolote kwa wakati huo ila mama Sabrina aliuliza kuwa Sabrina atarudi lini nyumbani ambapo Sam naye akamuuliza,
"Kwani ni vibaya kwa dada na kaka kuishi nyumba moja?"
"Hapana si vibaya ila...."
Sam akadakia tena,
"Ila nini mama? Umekiri mwenyewe kuwa si vibaya basi hakuna tatizo, Sabrina atarudi tu muda ukifika."
Kisha akawaaga na kuondoka zake.
Ndugu walibaki wakitazamana tu ila muda huo Deo alikuwa kimya kabisa na walipomuandalia chakula alikula tu bila ya tatizo lolote na kumfanya mama Sabrina aamini kuwa kuna kitu ambacho Deo amekubaliana na Sam na ndiomana amerudi katika hali ya kawaida ukizingatia kuwa jana yake alikuwa na hali mbaya sana.
Wakazungumza pale kama ndugu kisha wakasambaratika na kila mmoja kurudi nyumbani kwake.

Sam alipoondoka hapo hakuelekea nyumbani kwake bali alielekea kwenye baa ambako huko aliagiza vinywaji mbali mbali na kuanza kunywa kama njia ya kujipotezea mawazo aliyokuwa nayo kwa siku hiyo.
Alikunywa sana kama enzi zake za zamani hadi akalewa kabisa leo.

Sabrina kama kawaida pale nyumbani na watoto wake bila hata ya kuweza kutoka nje aliamua kuchukua simu na kumpigia Jeff ili amsimulie kidogo kuhusu jana.
Jeff alipokea ile simu na muda huo Sabrina akaanza kumueleza ya jana,
"Basi jana ulivyonipigia simu, yani niliona mambo...."
Jeff akamkatisha kidogo na kumuuliza tena,
"Jana nilikupigia simu?"
"Ndio Jeff ulinipigia simu usiku"
"Una uhakika Sabrina kuwa jana nimekupigia simu?"
"Ndio, kwani hukupiga?"
"Kwanza siku hizi nikipiga simu zangu huwa hupokei halafu hiyo jana hata sijakupigia simu kabisa"
"Jeff usilete masikhara bhana, jana umenipigia simu usiku. Na lini uliyonipigia simu bila ya mimi kupokea? Kwanza siku hizi hunipigiagi simu, ni jana tu umenipigia hata mimi mwenyewe nikashangaa. Haya sasa unakataaje?"
"Kwakweli kwa swala la jana kukupigia simu nakataa kabisa, kwanza jana simu yangu ilizima chaji na huku hapakuwa na umeme. Kwakweli sijakupigia simu jana Sabrina labda kama kuna mtu mwingine aliyekupigia"
Sabrina akakaa kimya kidogo akitafakari kauli ya Jeff kuwa hakumpigia simu jana, Jeff naye akaendelea kuongea ambapo alimuuliza swali Sabrina,
"Na kwanini siku hizi huwa hupokei simu?"
"Simu zipi ambazo huwa sipokei?"
"Mama yako mwenyewe alikupigia simu na hukupokea. Halafu baba yako anaumwa, aliangu..."
Simu ikakatika kabla hata Jeff hajamaliza maneno yake.
Sabrina akajaribu kupiga tena akapewa jibu kuwa namba anayopiga haipatikani, kwahiyo akaamua aache tu huku akitafakari kuwa aliyempigia simu usiku alikuwa ni nani na alikuwa anamaana gani ya kumtisha yeye hadi akaona maajabu ya mtoto wake kwa usiku ule.

Mama Sam alipofika tu Arusha moja kwa moja alienda kuonana na mdogo wake ambapo alimueleza kila kitu kuhusu baba wa Sam,
"Kheee yule baba kumbe ndio baba wa Sam duh! Mbona makubwa haya, sasa itakuwaje hapo maana mie hata sielewi"
"Ni ngumu kuelewa ila wewe ndio mtu pekee unayeweza kuzungumza na Sam na akakuelewa. Tafadhari nenda mjini, nenda kwa Sam ukazungumze nae. Jaribu kumuelekeza, mwambie amwache dada yake awe huru kwakweli kuishi kwa Sam ni sawa na kuishi jela. Tafadhari sana mdogo wangu naomba ukazungumze hayo na Sam"
Kwakweli huyu mdogo mtu hakuwa na kinyongo wala pingamizi ukizingatia ni kweli huwa anasikilizwa sana na Sam kuliko mtu yeyote yule.
Na kwa hali aliyoambiwa akaamua kupanga safari ya kesho yake ili aweze kuonana na huyo Sam.

Sam akiwa amelewa sana aliamua sasa kwenda kupanda gari yake ili arudi nyumbani kwake.
Kwavile alikuwa amelewa alijikuta akiendesha gari hovyo hovyo.
Muda kidogo gari ya Sam ikapata ajali mbaya sana kwani iligongwa na gari ya mizigo.

Sam akiwa amelewa sana aliamua sasa kwenda kupanda gari yake ili arudi nyumbani kwake.
Kwavile alikuwa amelewa alijikuta akiendesha gari hovyo hovyo.
Muda kidogo gari ya Sam ikapata ajali mbaya sana kwani iligongana na gari ya mizigo.
Kila mmoja aliyebahatika kuishuhudia ajali ile alitambua wazi kuwa kwa vyovyote vile dereva na watu wote waliokuwamo kwenye ile gari ndogo watakuwa wamekufa kwani ile gari ilikuwa nyaka nyaka yani lilikuwa limeharibika vibaya sana ila kwavile ilikuwa ni usiku na hapakuwa na askari wale wa usalama barabarani basi mwenye ile gari kubwa akatumia nafasi hiyo kukimbia na gari yake kwani aliona mlolongo ungekuwa mrefu kama wangesubiria askari wa barabarani na ukizingatia gari yake haikuharibika sana kama ile gari ndogo ya Sam.

Muda huu usiku Sabrina akiwa sebleni akimngoja Sam kwa mara ya kwanza siku hiyo tu ndio alikaa sebleni na kumngoja Sam kwani haikuwa kawaida yake kabisa kumsubiria Sam ukizingatia Sam huwa anafunga mlango kwa nje na kuondoka na funguo hadi muda atakaorudi.
Kwahiyo siku hiyo Sabrina alijisikia tu kumsubiria Sam hapo sebleni.
Muda wa saa tano usiku akamuona Cherry akitoka chumbani kwa kasi sana, na alipofika sebleni akawa kama anamshika Sabrina mkono ili aweze kutoka naye nje.
Sabrina akahamaki,
"Tutatokaje nje mwanangu ilihali mlango umefungwa kwa nje?"
Cherry akamuangalia mama yake kwa yale macho ambayo Sabrina akiyaona huwa anakosa imani na mtoto wake na kumfanya Sabrina aanze kupatwa na hofu.
Ila kabla Sabrina hajafanya chochote kile, alimuona mwanae akinyoosha mkono na kuwa mrefu sana na kumfanya yeye aogope na kujikuta akianguka chini na kupoteza fahamu.

Kwavili siku iliyofuata ilikuwa siku ya mwisho wa wiki, basi kulipokucha tu Jeff aliamua kujihimu asubuhi na mapema ili akaweze kuonana na Sabrina na hata kuzungumza nae ukizingatia jana aliongea nae kwenye simu ila simu ilikatika kabla hata ya wao kumaliza mazungumzo.
Kwahiyo Jeff aliondoka kwao na kuanza kuelekea nyumbani kwa Sam.
Akiwa njiani, aliona mahali watu wakiwa wamejaa sana na akagundua wazi kuwa lile eneo palitokea ajali, ikabidi naye asogee eneo la tukio.
Alishangaa kuona gari ikiwa imepondwa vibaya sana kwa mbele na kujikuta akiulizia alipo dereva kwani alijua kwa vyovyote vile basi dereva atakuwa mochwari.
"Duh hii hatari, dereva yuko wapi?"
"Hata hajulikani alipo, hii ajali inamshangaza kila mmoja hapa"
Jeff alipoangalia vizuri ile gari iliyopata ajari akagundua moja kwa moja kuwa ni gari ya Sam na kumfanya ashtuke sana na kuuliza tena kuhusu majeruhi wa ile ajali ila kila mtu alijibu kuwa hajui kwavile ajali yenyewe ilitokea usiku kwahiyo ni wachache walioishuhudia na hawakufikiriwa kuwa kwenye eneo hilo.
Jeff alijikuta akipatwa na mawazo mengi huku akiri yake ikiwa imesongwa na vitu vingi, ni hapa alipoamua kuchukua simu tena na kumpigia Sabrina ila simu ilijibiwa kuwa haipatikani na kumfanya Jeff aanze kubebanisha matukio yote yaliyotokea tangu jana.
Cha kwanza, alifikiria alivyopigiwa simu na Sabrina usiku na jinsi walivyozungumza kidogo kisha simu kukatika na kuijaribu bila ya kumpata tena hewani tangu ile usiku kwani alijibiwa kuwa simu anayopiga haipatikani.
Cha pili ni vile alivyoona hapo kuwa ni gari ya Sam ndio imepata ajali, hofu ikamtawala moyoni mwake kuwa inawezekana ni Sam na familia nzima waliopata ajali hapo ila kila alipouliza kuhusu ajali ile alipewa majibu yaliyokinzana kwani hakuna aliyejua undani wa ajali ile.
Ni hapa sasa akatokea jamaa mmoja na kudai kuwa alishuhudia ila aliogopa kusogea eneo la tukio.
"Yani mimi nilikuwa upande ule wa barabara, niliiona kabisa hii gari ndogo ikiendeshwa vibaya na muda kidogo nikashtukia mlio mkubwa wa ajali ila ilipita kama dakika kadhaa lile gari kubwa lililogangana na hii gari ndogo ikaondoka. Nilikuwa na wenzangu watatu ila kila mmoja aliogopa kusogea kwani eneo lilikuwa na giza sana na tukaamua kuondoka kwa kuogopa ushahidi ila kulipokucha tulikuja kuangalia na kukuta watu wamejaa na miongoni mwa wale kulikuwepo na wengine waliosema waliona tukio la ajali toka usiku na waliposogea eneo la ajali hawakuona dalili yoyote ya mtu. Kwakweli hapo hatuelewi, labda wale wenye gari kubwa walishuka na kuwaokoa kwenye gari ndogo ila haiwezekani kwavile kitendo cha wao kuondoka baada ya ajali kilikuwa cha haraka sana."
Bado Jeff hakuelewa kitu kwakweli na alijaribu kutafakari sana ila aliamua tu kuendelea na safari yake ili kama akifika kule na kukuta kimya basi aanze kufatilia kwenye hospitali mbali mbali.

Mama Sabrina akiwa na mumewe kwa siku ya leo aliamua pia kumuuliza alichoongea na Sam kwa jana yake ili aweze kujua jambo ambalo lilirudisha furaha yake.
"Kwani ulikubaliana nini na yule Sam jana?"
"Ameniambia kuwa kila jambo litakuwa sawa hivi karibuni"
"Atawekaje sawa? Je ataenda kuachana na Sabrina au itakuwaje? Na vipi kuhusu wale watoto aliozaa nae?"
"Joy tafadhari usinichanganye, elewa kile nilichokwambia usitake kunichanganyishia mada na khabari zitakazozidi kuchanganya akili yangu. Nishakwambia kuwa nimeambiwa kila kitu kitakuwa sawa sasa ukiniuliza tena kivipi kwa hakika sitakuwa na jibu la kukwambia kwakweli. Naomba uniache niwe na amani kwa muda tafadhari"
Ikabidi mama Sabrina aombe msamaha na kuachana na zile mada ingawa lengo lake kubwa lilikuwa ni kujua hatma ya binti yake tu.
Muda kidogo wakipigiwa simu na mtoto wao Sam mdogo ambaye siku hiyo asubuhi na mapema alitoka nyumbani kwao.
Mama Sabrina alipokea ile simu ambapo mtoto wao moja kwa moja aliomba mawasiliano ya dada yake,
"Vipi tena kwani kuna tatizo?"
"Mmh hapana ila kuna gari nimeiona hapa imepata ajali ni kama gari ya yule Sam tulilopanda jana"
"Wee unasemaje? Hebu angalia vizuri kwanza usinipe khabari nusunusu"
Mama Sabrina alivyokata ile simu hakutaka kumwambia mumewe alichoongea na mtoto wao kwani alijua wazi kuwa angepaniki zaidi ya mwanzo kwahiyo akawa kimya huku akijigelesha na kumtafuta Sabrina kimya kimya ili aweze kujua undani wa kile alichoambiwa huku akimuomba Mungu kuwa isitokee kuwa khabari mbaya kwake.

Jeff alifika nyumbani kwa Sam na kuona jinsi ukimya ulivyotawala kwenye nyumba hiyo, na hata kuelewa kwa haraka kuwa hapakuwa na mtu yeyote mule ndani yani ni hapa ambapo Jeff alipomlaumu Sam kuwa na nyumba kubwa kiasi kile na kushindwa kuweka mlinzi kwani ingekuwa rahisi kwake kumuuliza mlinzi wa nyumba hiyo.
Kwavile geti lilikuwa limefungwa, Jeff akaamua kupanda ukuta ili aweze kuingia ndani ya nyumba hiyo, ni kweli alifanikiwa kuwa ndani ila bado ule ukimya ulimshangaza, akayaangalia magari ya Sam yaliyopangana pale na kugundua kutokuwepo kwa lile gari lililopata ajali ila bado alijiuliza,
"Hivi Sam anajiamini kitu gani? Anawezaje kuacha magari yake nje kama hivi tena bila ya mlinzi yoyote mmh? Na mbona nyumba ipo kimya sana? Inamaana hata Sabrina na watoto hawapo?"
Ila bado hakukata tamb kwani alienda mlango wa ndani akigonga huku akijaribu kuita ili kuona kama ataweza kuitikiwa ila bado kimya kilitawala na kujikuta akigonga pale hadi lisaa lizima likamkutia akiwa pale pale mlangoni akigonga.
Wakati akikata tamaa na kutaka kuondoka gafla akasikia kama mlango ukifunguliwa na kumfanya ashtuke huku akingoja kuona kuwa ni nani huyo aliyekuwa akifungua ule mlango.
Akiwa amesimama pale nje, akashangaa kumuona Cherry akitoka nje kisha akatazamana nae ambapo Cherry alitoa sauti ya kiutu uzima ya kumkaribisha.
"Karibu"
Jeff aliganda pale nje kwa muda kidogo kisha akaingia ndani akiambatana na Cherry.
Ila bado alizidi kushangazwa na ukimya wa mule ndani, kisha akamuuliza Cherry,
"Mama na baba yako wako wapi?"
"Mama kalala ila baba yangu si wewe hapo"
Jeff akamuangalia Cherry kama mtu aliyeumbuliwa nae vile.
Kisha akamuuliza tena,
"Yule baba yako mwingine naye yuko wapi?"
"Amelala pia"
Jeff akawa ameganda kidogo na maswali yake kwani alikuwa akijidadisi cha kuendelea kuuliza zaidi ya maswali ya mwanzo ila ikawa kamavile Cherry anajua ni nini Jeff anataka kumuuliza kwani alimshika mkono na moja kwa moja akampeleka chumbani kwa mama yake ambapo Jeff akamuuliza,
"Eeh unataka nifanye nini?"
"Mwamshe mama"
Jeff akafanya alichoambiwa na alipomtikisa kidogo tu Sabrina akaamka na kukaa kitandani ila kabla ya Jeff kuongea chochote na Sabrina. Cherry akamshika tena mkono na kutoka nae mule chumbani kisha moja kwa moja akampeleka kwenye chumba anacholala baba yake kisha akamwambia Jeff kuwa amwamshe baba yake ambapo Jeff alifanya vile alivyoambiwa na Cherry na haikupita muda Sam akaamka na kukaa huku akijishangaa na kulalamika maumivu ya kichwa huku akiongea,
"Hivi mimi nimepona kweli? Mimi nimepona? Kweli Mungu mkubwa ingawa kichwa kinaniuma."
Kisha akamtazama Jeff na Cherry waliokuwa mbele yake wakimuangalia, akainuka na kuwaambia
"Jamani, nimepona kweli au masikhara haya. Au ndio nimekufa mnaniaga mara ya mwisho, hebu ongeeni kidogo na mimi niamini kuwa kweli nina uzima"
Cherry akawa wa kwanza kuongea,
"Umepona baba, twende nje sasa"
Kisha akamshika mkono na kuanza kutoka nae nje ingawa mpaka wanafika sebleni bado Sam alikuwa hajiamini kama kweli amepona kwani bado alikuwa na maruweruwe ya ajali aliyopata usiku wa jana.

Wakiwa sebleni, Sabrina nae alitoka chumbani huku akilalamikia maumivu ya kichwa kwa wakati huo.
Alikuwa akiwashangaa tu pale sebleni kisha akauliza,
"Hebu niambieni jamani ni kitu gani kimetokea maana mpaka muda huu sielewi kitu na sijielewi kabisa"
Sam akamuuliza,
"Kwani kuna matatizo yaliwapata hapa nyumbani Sabrina?"
"Hapana ila kuna hali ya kutokueleweka ilinipata jana usiku yani hapa mpaka muda huu nashindwa hata kuelewa kabisa hata sijui nianzie wapi na kuishia wapi. Kwani wewe Sam ulichelewea wapi jana?"
"Jamani jana kiukweli nililewa sana ila njiani nilipatwa na ajali mbaya sana na nimeishuhudia kwa macho yangu yani hata najishangaa nimepona ponaje na ni nani aliyeniokoa pale kwenye ajali"
Cherry alikuwa kimya tu akiwaangalia wanavyopokezana kwa hoja mbalimbali ambazo yeye anajua mwanzo na mwisho.
Kisha Jeff nae akasimulia jinsi alivyolikuta gari la Sam likiwa limeharibika vibaya mno na kumfanya apatwe na mashaka na kuamua kuja pale.
"Kwakweli nimeruka ukuta ili niingie huku jamani"
Sam akamshangaa Jeff kwa uhodari wa kuruka ukuta,
"Duh! Sasa mlango wa ndani ni nani alikufungulia?"
Kabla Jeff hajajibu, simu yake ikaita na aliyekuwa anapiga alikuwa ni Sam mdogo wa Sabrina, ikabidi Jeff apokee na kuzungumza nae ambapo alikuwa akiongelea kuhusiana na ile ajali aliyoiona na jinsi alivyopewa namba ya Sabrina na kujaribu kumpigia bila ya kumpata hewani.
Ikabidi Jeff amwambie ukweli wa hali halisi kuwa wote ni wazima wa afya njema kabisa na muda huo yuko nao.
Ni hapa ambapo huyu Sam akaomba apewe maelekezo ili naye afike kuwaona na ajiridhishe na moyo wake.
Jeff alimwelekeza vizuri kabisa kisha akakata simu na kuendelea na maongezi yao ila Cherry aliyakatisha kwa kudai kuwa njaa inamuuma sana.
Hapo ikabidi Sabrina ainuke ili akakoroge hata uji ingawa mtoto wake mdogo alikuwa amelala tu kwa muda huo.

Sabrina akiwa anakoroga uji, bado akawa anawaza yale mambo ya usiku, picha ikamjia vizuri sasa kuwa mtoto wake alibadilika kabisa na kumfanya aogope na kumpulizia vitu vilizompoteza fahamu kabisa.
Sabrina alitafakari na uoga nao ukazidi kumjaa dhidi ya mtoto wake ambapo wakati anawaza hayo Cherry naye alienda kule jikoni na kumfanya Sabrina ashtuke sana kumuona mwanae.

Wakiwa pale sebleni, Jeff akapigiwa simu na mdogo wa Sabrina kuwa amefika stendi akamfuate, ikabidi naye afanye hivyo ambapo Sam alitoka naye na kwenda kufungua geti kisha yeye akarudi zake ndani huku akitafakari tu kuhusu ile ajali aliyopata ambapo moja kwa moja aliamua kwenda chumbani kwake.
Akiwa na mawazo yake, akashangaa kumuona Sabrina akiwa ameingizwa chumbani mule na Cherry halafu Cherry akatoka na kuwaacha wakiwa wawili tu chumbani.

Jeff na mdogo wa Sabrina walifika, ila kwavile Jeff hakuwaona wakina Sabrina pale sebleni ikabidi amuulize tena Cherry,
"Mama yako yuko wapi?"
"Yupo chumbani kalala na baba"
Jeff na mdogo wa Sabrina walijikuta wakitazamana kwa hii kauli.

Jeff na mdogo wa Sabrina walifika, ila kwavile Jeff hakuwaona wakina Sabrina pale sebleni ikabidi amuulize tena Cherry,
"Mama yako yuko wapi?"
"Yupo chumbani kalala na baba"
Jeff na mdogo wa Sabrina walijikuta wakitazamana kwa hii kauli.
Kisha wakamuangalia tena yule mtoto na kujikuta wakiuliza tena,
"Umesema wako wapi?"
"Nimesema wako chumbani"
Wakatazamana tena huku kila mmoja akiwa na maswali yasiyokuwa na majibu kwa wakati ule ila ikabidi wakae tu wakiwangoja kuwa watatoka huku wakimuangalia sana Cherry.
Mdogo wa Sabrina akajikuta akimuuliza Jeff baada ya kumuangalia sana Cherry,
"Dogo vipi, mbona huyu mtoto kafanana sana na wewe?"
Cherry akadakia,
"Kwani hujui?"
"Sijui nini?"
Kabla Cherry hajaongea, Jeff akakatisha yale maulizo kwa kumwambia Cherry kuwa akamwite mama yake hivyo hivyo ambapo Cherry alitoka pale na kwenda kufanya kile alichoagizwa.

Jeff akiwa kabaki pale na mdogo wa Sabrina akaulizwa tena swali,
"Hivi huyu mtoto una muelewa kweli?"
"Kivipi?"
"Mbona anaongea kama mtu mzima?"
"Huyo mtoto mzoee tu sababu ukitaka kujiuliza maswali juu yake unaweza kujikuta ukichanganyikiwa bure"
"Mmh lazima kuna kitu dhidi ya huyu mtoto ila nyie hamjui tu"
"Sam, nakutahadharisha tena. Habari za huyo mtoto achana nazo kabisa, achana na mambo yake hatutaki kukupoteza ndugu yetu. Laiti ungejua waliomfatilia wamepatwa na nini basi hata usingeendelea kujipa maswali juu yake."
"Wewe Jeff unaongea tu kwavile huyu mtoto hakuhusu, ila mimi huyu ni damu yetu na lazima niumizwe kama kuna chochote kibaya juu yake"
"Basi unakomalizia wewe kuumia mimi mwenzio ndio naanzia hapo. Ninaumia kupita maelezo, na unapoishia wewe kuhusiana na huyu mtoto mie ndio naanzia"
"Kivipi?"
Jeff akatulia kimya kidogo kwani aliona dalili za kuanza kuropoka yale yanayomuhusu na mwisho wa siku kuharibu kabisa kwahiyo akawa kimya kwa muda.

Cherry aliwafata wazazi wake chumbani na kuwakuta wakiwa wamekaa kisha akawaambia kuwa wanasubiriwa sebleni halafu yeye akaondoka na kumfanya Sabrina amuulize Sam,
"Unajua hata huyu mtoto alichoniletea huku chumbani kwako sikijui kwakweli. Au ulimwambia kuwa aniite?"
"Ingekuwa nimemwambia basi toka umeingia humu ningekuwa nimeshakwambia nilichokuitia. Inawezekana alitaka tu kutuona pamoja."
Sabrina hakuuliza zaidi ila akainuka na kuelekea sebleni ambapo Sam alimfata kwa nyuma.
Walifika na kumkuta mdogo wa Sabrina na Jeff pale sebleni ambapo mdogo wa Sabrina alisalimiana na dada yake pale kisha akamueleza jinsi alivyokuwa na mashaka.
Hata Sam nae alipofika sebleni akaelezewa jinsi gari lilivyokuwa nyaka nyaka pale kwenye ajali.
"Kwani ulimuachia mtu lile gari au ilikuwaje maana mpaka muda huu sijaelewa"
"Hata mimi mwenyewe sielewi ila lile gari nilikuwa naliendesha mwenyewe ila hadi sasa sielewi kitu chochote kile."
Wakaongea pale mawili matatu kisha Jeff na mdogo wa Sabrina wakaaga na kuondoka zao.

Jeff akiwa nyumbani kwao alikuwa na mawazo sana kuhusu Cherry kwani alikuwa anafanya mambo ambayo yalizidi kumpa mashaka Jeff na kuungana na maneno yaliyosemwa na mdogo wa Sabrina kuwa yule mtoto lazima atakuwa na matatizo tu.
Jeff akafikiria sana na akatafakari ya kufanya bila ya kupata majibu ya aina yoyote ile, alitamani sana kujua cha kufanya dhidi ya mtoto wake ila hakuwa na majibu yoyote yale.
Usiku alipokwenda kulala akajiwa na njozi.
Alimuona Cherry akiwa mdogo huku kashikwa na Sam halafu kulikuwa na mtu nyuma ya Sam ambaye hakuweza kuonekana na wengine.
Gafla akamuona Sam akifunga macho kisha yule mtu akaingia kwenye mwili wa Cherry.
Jeff akashtuka usingizini huku jasho jingi likimtoka na kujikuta akikaa huku akitafakari ndoto aliyoiota huku mwili wake wote ukitetemeka na kumfanya ashindwe kulala kabisa hadi panakucha.

Nyumbani kwakina Sabrina alikuwepo mdogo wa Sabrina akijaribu kuelezea kile ambacho alikutana nacho kwa Sabrina na Sam,
"Yani mama kiukweli hata ukiwauliza wenyewe hakuna anayeweza kuelezea kuwa ilikuwaje kuwaje ila gari ya Sam nimeikuta nyaka nyaka halafu Sam yupo nyumbani na hata hajui kilichotokea ila ukimuuliza atakujibu kuwa ni yeye aliyekuwa kwenye gari"
"Mmh makubwa haya, na je kuna uwezekano wa Sabrina kurudi nyumbani kweli?"
"Kwakweli mama pale hata hapaeleweki, halafu yule mtoto wa Sabrina sidhani kama yupo sawa yule"
"Kwanini?"
"Sijui kama mmejaribu kumchunguza mtoto yule kwani nilipojaribu kuulizia habari za mtoto yule Jeff akaniambia niachane kabisa na khabari za yule mtoto ila kiukweli yule mtoto hayupo kawaida yani sio sawa na watoto wengine"
"Hebu nieleze vizuri Sam"
"Kwakweli mimi sijui ila cha muhimu mnatakiwa kuwa karibu na yule mtoto ili kujua undani wake kwani nina uhakika kabisa kuwa yule mtoto hayupo sawa"
Kisha mdogo wa Sabrina akainuka na kumuaga mama yake huku akimuacha mama huyo na mawazo dhidi ya mjukuu wake.

Jeff naye alijiandaa kwenda kazini huku akijipa moyo wa kuikomboa familia yake kwa kutumia ule mwanya wa undugu wa Sam na Sabrina,
"Natakiwa nisimame kiume sasa, najua Mungu alikuwa na makusudi yake kuyafanya yote haya. Mimi kama Jeff natakiwa nisimame kama mwanaume, natakiwa kumtetea Sabrina na watoto wetu bila hata ya kujali kuwa watu watanifikiriaje"
Alijitafakari kisha akatoka nje na kuondoka.

Sam hakuondoka nyumbani kwake siku hiyo ila alikuwa akitafakari mambo mbali mbali haswa kuhusu ajali iliyompata ila akajikuta nyumbani bila jeraha wala alama yoyote ya michubuko.
Aliwaza na kutambua kuwa lazima aliyemsaidia ni Cherry tu ila hakujua kuwa alimsaidiaje.
Ila bado moyo wake uliumizwa na undugu aliougundua kati yake yeye na Sabrina na kujikuta akijiuliza sana kuwa kwanini Sabrina ni ndugu yangu.
"Kwahiyo kwa dhana hiyo itakuwa nimemuumiza mtoto wa ndugu yangu ila nawezaje kumuachisha wakati nilishakubaliana nae? Nawezaje wakati ananisaidia kiasi hiki?"
Akakosa jibu kisha akamuita Cherry ambapo Cherry alifika pale alipo Sam na kukaa karibu yake.
Sam alimuangalia mtoto wao huyo na kumshukuru,
"Asante sana"
Cherry alitabasamu ila muda huu Sabrina nae alikuwepo karibia na jikoni huku akiangalia mazungumzo baina ya Sam na Cherry.
Wakati Cherry akitabasamu, Sam akasema
"Umenisaidia sana ingawa gari yangu haifai tena"
Cherrya akamwambia,
"Si utanunua nyingine"
"Uwezo wa kununua upo ila lile gari nilikuwa nalipenda sana"
"Kwahiyo unalitaka kama lile?"
Sam akatabasamu na kusema,
"Najua haitawezekana maana pale zimebaki kama skrepa tu"
Gafla Cherry akamwambia Sam,
"Fumba macho"
Sam akatii na kufunga macho yake ambapo baada ya muda kidogo Cherry akamwambia Sam kuwa afumbue macho kisha akamwambia watoke nje.
Walipotoka nje, Sabrina nae aliwafata nyuma ili kujua mazungumzo yao yanaishiaje.

Kufika nje Sam mwenyewe akashtuka baada ya kuona gari yake ikiwa pale nje tena nzima kabisa yani bila ya mchubuko wowote ule.
Kwakweli Sam hakuamini kile anachokiona na kumuuliza Cherry kwa mshangao,
"Umewezaje!"
Cherry akatabasamu kisha akageuka nyuma na kumuangalia mama yake aliyekuwa akitetemeka tu wakati huo.
Ila Sabrina alivyotazamwa vile tu na binti yake akaamua kurudi ndani huku akizidi kutetemeka tu kadri muda ulivyozidi kwenda mbele.

Sabrina alikaa sebleni huku akiwa hana raha wala amani.
Muda kidogo Sam na Cherry nao wakarudi sebleni kisha Cherry akamuuliza mama yake,
"Umeona nini?"
Sabrina alijibu huku akiwa hana amani na jibu lake,
"Nimeona gari"
Cherry akacheka kisha akamwambia mama yake,
"Kuona gari tu unatetemeka hivyo je ungeona lilivyorudishwa"
Maneno haya ya Cherry yalizidi kumtetemesha Sabrina na kujikuta akishindwa hata kuongea.
Ni hapa ambapo Cherry akawa na lafudhi ya kitoto na kumdai mama yake chakula ila hata hivyo bado Sabrina alishindwa hata kuinuka hadi pale Sam alipoamua kumwambia maneno ya kumpooza na kumbembeleza.

Jeff alienda kazini na kufanya kazi zake kama kawaida ila kwavile leo bosi hakuwepo ofisini ikamfanya Jeff awahi kutoka ili akaendelee kujadili na moyo wake namna atakavyoweza kuikomboa familia yake kutoka kwa Sam.
Muda huu Jeff alikuwa njiani na kujikuta akikutana na mdogo wa Sabrina kwenye lile eneo ambalo Sam alipata ajali.
Ilibidi Jeff asimame na kumuuliza mdogo wa Sabrina kuwa imekuwaje maana watu walikuwa wamejaa tena eneo lile,
"Vipi tena? Watu bado wanaishangaa ile ajali?"
"Sio kwamba watu wanashangaa ajali ila wanashangaa tukio ambalo limetokea hapo muda mfupi uliopita"
Jeff akauliza kwa mshangao,
"Tukio gani tena?"
"Angalia mwenyewe kama lile gari lililoharibika lipo"
Jeff akaangalia na kuona kuwa halipo,
"Mbona halipo?"
"Ni kweli halipo"
"Labda limetolewa na askari"
"Hivi Jeff unafikiri kama askari wangetoa lile gari ndio watu ungewakuta wakishangaa hivyo?"
Ikabidi Jeff aulize kwa makini sasa kuwa ni kitu gani kilichotokea,
"Yani unaambiwa kuwa hapo imekuwa ni kitendo cha kufunga macho na kufungua, gari haijaonekana tena. Kila mmoja hapa anashangaa kuwa imekuwaje"
Jeff akatafakari kitu kisha akamuuliza mdogo huyu wa Sabrina,
"Hivi wewe ni mwandishi wa habari eeh maana matukio kama haya unayapenda sana"
"Ni kweli kuwa mimi ni mwandishi ila habari kama hii imenishtua kwakweli. Unadhani inawezekana vipi kwa gari kujiondoa lenyewe gafla? Hili ni jambo la ajabu sana."
Walijikuta wakitumia muda mrefu pale kujadili ajali iliyotokea na kilichotokea muda mfupi uliopita.

Wakati Sabrina akiendelea kubembelezwa na Sam kuhusu kumuandalia mtoto chakula huku akisitasita kwenda kuandaa, muda kidogo simu ya Sam ikaita na kumfanya aipokee moja kwa moja na kuongea nayo.
Mpigaji alikuwa ni mama mlezi wa Sam na alidai kuwa yupo stendi akimuomba Sam aende kumchukua,
"Sawa mama usijali nakuja kukuchukua"
Kisha Sam akakata ile simu na kumwambia Sabrina mustakabali mzima wa ile simu.
"Kwahiyo ndio unaenda kumpokea?"
"Ndio Sabrina, unauliza majibu tena!"
"Hakuna tatizo wewe nenda tu ila ngoja nikuombe kitu"
"Usiwe na wasiwasi Sabrina niambie tu"
"Naomba uende na huyo mtoto"
"Yani niende na Cherry?"
"Ndio"
Sam akacheka kwani alijua wazi kuwa Sabrina ameanza kumuogopa mtoto wake mwenyewe kutokana na yale aliyoyaona muda mfupi uliopita.
Kisha Sam akainuka na kumnyanyua Cherry kisha akatoka nae nje ili waweze kuondoka.
Ila walipokuwa nje, Cherry akachagua gari lile lile lililopona muda mfupi uliopita kuwa ndio waende nalo.
Sam hakuwa na tatizo ukizingatia lie gari lilionekana kuwa zima kabisa kana kwamba hakuna chochote kilichotokea.

Sam na mtoto wake wakiwa njiani wakati wanakatisha lile eneo ambalo ajali ilitokea, walishangaa kuona watu wakisambaratika na kila mmoja kuelekea anapopajua yeye na wengine walionekana kukimbia hovyo hovyo.
Sam hakutaka kujali jambo lile kwani hakujua ni kipi kimewakumba watu hao.
Kisha alimuangalia Cherry na kumuuliza,
"Umewaelewa hawa watu kweli?"
Cherry alimuangalia tu Sam bila ya kujibu ila muda kidogo akalalamika kuwa njaa inamuuma kama alivyolalamika nyumbani kabla ya kuondoka.
"Pole mwanangu"
Kisha Sam akasimamisha gari na kumnunulia Cherry juisi na biskuti ili aweze kupooza hiyo njaa anayoilalamikia.
Kisha safari ikaendelea.

Kwenye lile eneo ambalo gari ya Sam ilipita, iliwafanya wote wasambaratike hata mdogo wa Sabrina na Jeff nao walikimbia bila ya kuwa na muelekeo kamili na mwishn wa siku walifika kwa pamoja nyumbani kwakina Sabrina na kumfanya mama Sabrina awashangae.

Sabrina sasa alibaki nyumbani na yule mtoto wake mdogo, alipumua sasa ila akili yake ikamtuma kuwa bora atoroke tu kwani mambo ya pale aliona yakimzidia kwahiyo ilikuwa ni vyema kwake kutoroka na yule mwanae mdogo kisha apange jinsi ya kumchukua Cherry ili akamchunguze tatizo lake.
Sabrina alimchukua mwanae mdogo na kumbeba mgongoni kisha akaanze kutembea kuelekea mlangoni ila kabla hajafungua mlango akasikia sauti,
"Unaenda wapi"
Hofu ikatawala kwenye moyo wa Sabrina, na alipogeuka nyuma akamuona Cherry.

Sabrina alimchukua mwanae mdogo na kumbeba mgongoni kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni ila kabla hajafungua mlango akasikia sauti,
"Unaenda wapi?"
Hofu ikatawala kwenye moyo wa Sabrina, na alipogeuka nyuma akamuona Cherry.
Kwakweli Sabrina alishtuka sana na kuanguka ila kabla hajafika chini kuna mtu alimuwahi na kumdaka kwa nyuma, jambo hilo lilimpa mashaka zaidi Sabrina na kumfanya afunge macho kwa nguvu.
Ila yule mtu alimpeleka hadi kwenye kochi na kumsaidia kumshusha yule mtoto mdogo mgongoni ila Sabrina alikuwa kajiziba kabisa macho yake kwa mikono kwani hakutaka kujua kinachoendelea na wala hakutaka kujua kuwa yule mtoto wake mdogo anapelekwa wapi kwani alihisi kama yupo kwenye ndoto ya kutisha iliyomfanya kuogopa kufungua macho yake huku akihofia kukutana na vitu vya ajabu.
Kwahiyo Sabrina alijikunja pale kwenye kochi huku mikono ikiwa kwenye macho kwa uoga.

Sam alifika alipo mama yake mdogo na kumpokea vizuri sana, huyu mama alifurahi kumuona tena mtoto wa Sam akiwa amekua kua sasa kwani mara ya mwisho alimuona akiwa mdogo sana.
Kwakweli alimchukua yule mtoto na kumbeba mikononi huku akimfurahia na kumpongeza Sam,
"Hongera mwanangu, kwakweli umekuza"
"Asante mama"
"Nimefurahi kumuona akiwa amekuwa hivi na afya njema"
"Yani hata yeye nyumbani alikataa kubaki kabisa yani kang'ang'ania kuja kukupokea mjukuu wako"
Huyu mama alionekana kuwa na furaha tu na kusahau hata yale aliyosimuliwa na dada yake.
Wakapanda kwenye gari kisha safari ya kuelekea nyumbani kwa Sam ikaanza.

Muda mwingi yule mama alionekana kumuuliza Sam maswali mbali mbali ila mtoto wa Sam yani Cherry alikuwa kimya kabisa huku kapakatwa na yule mama, muda kidogo akawa amelala kabisa hadi huyu mama akajiona ana baraka sana,
"Huyu mtoto kanifurahia hadi kalala mwilini mwangu."
"Utampenda zaidi ukikaa nae huyo ana vituko sana na anafurahisha"
"Kwani anaongea?"
"Ndio, tena anaongea kama cherehani yani huyo ni kinanda utachoka wewe mama"
Huyu mama akafurahia tu.
Walipokuwa wanakaribia nyumbani kwa Sam kuna kitu alikiona huyu mama na kumfanya ashtuke.
Kitendo hicho kilifanya Sam amuulize kuwa tatizo ni nini,
"Nini tatizo mama? Mbona umeshtuka?"
"Kuna kitu nimekiona halafu kimenikumbusha jambo"
"Jambo gani hilo tena?"
"Tukifika nitakwambia, ila usitake kulijua kwasasa kwani nitakwambia tu."
Ikabidi Sam awe mpole kwani aliifahamu fika tabia ya mama yake huyo kuwa hapendi swala la kushurutishwa, anataka aseme kitu kwa hiari yake kwahiyo ikabidi Sam akubaliane na hali halisi.
Safari ikaendelea hadi nyumbani kwa Sam ila kabla hawajashuka, huyu mama akamzuia kidogo Sam kushika kisha akamuuliza,
"Yuko wapi Janeth?"
"Janeth? Mama yani upo serious kabisa unamuulizia Janeth? Wa nini? Na kwanini umuulizie sasa?"
"Nijibu kwanza, yuko wapi Janeth?"
"Hivi mama unajua kama nilishaoa na kwenye harusi ulikuwepo sasa unamuulizia Janeth wa nini?"
"Nijibu swali langu basi mbona unanizungusha?"
"Hebu tuingie ndani kwanza kisha nitakujibu hilo swali mama"
Huyu mama akakubali ila kwa shingo upande kwani aliona kamavile Sam anataka kupoteza mantiki ya swali lake.
Kisha Sam akashuka na kufungua geti halafu akaingiza gari.

Walifika na kuingia ndani ambapo walimkuta Sabrina akiwa pale sebleni huku amejikunyata na kujiziba macho halafu mtoto akiwa pembeni yake.
Kwakweli Sam hakumuelewa Sabrina na kuamua kumsogelea karibu na kumshtua ila bado Sabrina hakutaka kufumbua macho yake,
"Sabrina, Sabrina nini tatizo jamani? Tumerudi tayari"
Sabrina bado alikuwa na uoga uliotawala kwenye moyo wake, na uoga huo ndio uliompelekea aogope kufumbua macho ingawa ni kweli alisikia sauti ya Sam kwa muda huo.
Ila Sam aliendelea kumuuliza Sabrina dhidi ya tatizo lililompata.
Sabrina nae alipojiridhisha kuwa yule ni Sam, aliamua kutoa hoja moja tu
"Naomba kwenda kwetu Sam"
Huku akiwa bado kajiziba macho,
"Ila hata hapa ni kwenu Sabrina"
"Nataka niende kwetu kabisa"
"Sabrina tulia kwanza, huko kwenu utaenda tu hebu jitoe mikono hiyo umsalimie mama yangu kwanza"
Imani kidogo ikamrejea na kujikuta akitoa mikono huku akiangalia kushoto na kulia ili kuhakikisha kuwa hakuna jambo la ajabu kweli.
Huyu mama alimsalimia Sabrina kisha akamuonyesha Cherry aliyekuwa amelala kuwa akamlaze chumbani ila Sabrina alijikuta akipiga kelele tu za kutaka kurudi kwao.
"Kwani una matatizo gani wewe?"
"Siwezi tena kuishi kwenye hii nyumba, siwezi kubaki humu ndani"
"Kwahiyo unataka turudi ile nyumba ya awali?"
"Ile ndio siitaki kabisa"
"Sasa unataka nini?"
"Nataka kurudi kwetu"
"Kwenu utarudi Sabrina, basi nenda ukamlaze mtoto ili tuje tuyapange"
"Nikamlaze mtoto gani?"
Sabrina aliuliza kwa hamaki,
"Si huyu mwanao Cherry jamani!"
"Msiniletee hizo khabari, mwekeni hapo kwenye kochi. Mbona mwenzie kalala hapo, na wewe mwekeni hapo hapo"
Sam hakujua kuwa ni kwanini Sabrina kawa vile kama mtu asiyejielewa.

Mdogo wa Sabrina alijikuta akitafakari namna ya kumsaidia dada yake na familia yake kwani aliona wazi kuwa hawako sawa kabisa na walihitaji msaada wa karibu mno, wazo lililomjia haraka ni kuonana na shangazi yao ili apate kuzungumza nao kwenye mustakabali mzima wa kitu cha kufanya.
Kwa upande wa Jeff alikuwa na wazo hilo hilo la mdogo wa Sabrina ila yeye aliongezea na yale aliyokuwa anayafanya mama yake kwani wazo lake lilimjia moja kwa moja kwa wataalamu wa jadi kushughulikia swala lile ukizingatia mama yake kwa kipindi chote hiki alikuwa vile vile na ule ulemavu alioondoka nao kwenye nyumba ya Sam.

Sabrina bado hakutaka kusikia chochote zaidi ya kukazania hoja yake tu kuwa anahitaji kurudi nyumbani kwao.
"Nimekwambia utarudi Sabrina"
"Basi naomba niondoke muda huu, tena nitaondoka na huyu mtoto mdogo tu huyo mkubwa nakuachia"
Sabrina aliongea hayo kwavile bado alikuwa na uoga na mwanae Cherry kwani hakuelewa kabisa kinachoendelea kati yao.
Ila Sam bado alimsisitiza kuwa asiondoke kwani alitaka kesho ampeleke mwenyewe ila bado kwa Sabrina lile neno la kesho ilikuwa ni mbali sana kwake kwani hakutaka kupoteza muda kwenye nyumba hiyo.
Sam aliamua kuweka mada ili aweze kumfanya Sabrina asiondoke ila bado Sabrina alionekana kuwa na harakati na lile swala lake.

Muda huo yule mama wa Sam alijaribu kukaa na Sabrina ili azungumze nae mawili matatu,
"Hivi unafikiri hata nakuelewa mama? Yani hapa sielewi kitu maana akili yangu haipo sawa kabisa"
"Akili yako haipo sawa kivipi?"
"Mama, hawa watoto ni wangu tena nimewazaa mwenyewe kwa uchungu wa uzazi kabisa lakini mkiona nafikia hatua ya kukubali kuondoka hapa na mmoja halafu mwingine namuacha basi mjue nimefanya maamuzi magumu sana ila ni maamuzi yenye maana sana kwangu. Ninachowaomba ni mniruhusu tu niondoke hapa."
"Sabrina usipaniki hivyo, unajua mimi nimetoka Arusha na kuja hapa kwaajili yetu! Tena nina maana kubwa sana ya kuja hapa kwani nataka hata kama mkitengana wewe na Sam kutokana na undugu wenu basi mtengano wenu uwe wa amani kuliko hivi nilivyokukuta"
Sabrina aliamua kumuuliza swali huyu mama,
"Leo si utalala hapa?"
"Ndio, mie nipo hapa wiki nzima"
"Basi naomba ujishuhudie leo kwa usiku mmoja tu, tena naomba ulale na mwanangu huyo"
Kisha Sabrina akainuka na kumchukua yule mwanae mdogo pale kwenye kochi na kumbeba tena mgongoni kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni, Sam akataka kumfata ili amrudishe ila mama yake mdogo akamzuia na kumwambia kuwa amuache tu aende,
"Mama jamani!"
"Muache Sam, huyo ni mtumzima na anauwezo mpana wa kutafakari na kujua jema na baya, mwache awe huru"
Sam akarudi kukaa na kumuacha Sabrina atoke na kuondoka.

Ndani kwa Sam sasa alibaki yeye, mama yake mdogo na mtoto Cherry.
Na ule muda alioondoka Sabrina tu, huyu mtoto Cherry naye aliamka na moja kwa moja akamfata Sam ambapo Sam alimchukua na kumpakata kisha akamuuliza,
"Mbona umepooza sana leo mwanangu?"
Ila Cherry alikuwa kimya kabisa na kumfanya Sam ahisi kuwa huenda mtoto huyo atakuwa na njaa tu ni hapo alipoinuka na kumkorogea maziwa kisha akampa na kuanza kuyanywa halafu Sam na mama yake mdogo wakaendelea na maongezi yao ambapo huyu mama bado swali lake lilibaki kuhusu Janeth,
"Niambie Sam, Janeth yuko wapi?"
"Kwanini unamuulizia Janeth mama?"
"Niambie kwanza alipo ndio nitakwambia kuwa kwanini namuulizia"
Sam akainama chini kwanza, kisha akajibu
"Janeth alikufa"
Huyu mama alishtuka ila hakushtuka sana kisha akasema,
"Nilijua tu Sam na ndiomana nikakuuliza alipo Janeth. Haya umemfanyaje na yeye? Usinifiche kitu Sam kumbuka najua kila kitu kuhusu wewe, na mimi ndio mtetezi wako niliyebaki, niambie ulichomfanya Janeth"
Sam alitulia kimya kwani aliona si kitu sawa kabisa kuzungumza yale mambo na mama yake kwani haikuwa heshima kabisa,
"Nilimkuta tu amekufa mama"
"Usinidanganye Sam, huyo Janeth alinipigia simu kabla ya kifo chake. Wewe ndiye uliyemuua Janeth, hivi ulikuwa hujishtukii kuwa kwanini siwasiliani na wewe? Ungejishtukia kidogo basi ungeelewa kuwa kwanini mimi nilikuwa kimya kwa kipindi chote hiki. Nilikuwa nakutafakari katika akili yangu, sikutegemea kama Janeth ungemfanyia vile kwa stahili hiyo hata huyo Sabrina ana haki ya kuogopa kukaa humu ndani kwani unaweza kumgeuka pia muda wowote. Kwanini umekuwa hivyo Sam? Sikufikiria kama wewe ni muuaji kiasi hiki kwakweli, yani sikutegemea kabisa. Na swala la uchawi je ni nani aliyekufundisha? Yani unafikia hatua hadi ya kumroga mama yako mzazi kweli? Mimi mlezi je si ndio balaa, ila kwa mimi kama kuniroga niroge tu ila ukweli lazima nikwambie"
Huyu mama akatulia kidogo kwa muda, wakati huo Sam alikuwa akimuangalia tu.

Sabrina alishukuru sana kutoka kwenye nyumba ya Sam kwani alijiona kamavile alikuwa kifungoni.
Alipofika nje tu akanyanyua mikono yake juu kushukuru kisha akaendelea na mwendo ili aende stendi akapande daladala.
Njiani alikutana na mdada aliyemsimamisha na kumsalimia, Sabrina alisimama ili aweze kusikia hoja ya yule mdada ambapo kabla ya yote yule mdada alianza kwa kumsifia Sabrina,
"Kwakweli wewe dada ni mzuri sana, ni wazi Mungu hakukosea kwenye uumbaji wako"
"Asante"
"Sawa dada ila ningependa nikusindikize kidogo"
Sabrina alimshangaa huyu mdada ila hakuikataa kampani yake, kwahiyo akaanza kuongozana nae wakielekea stendi ya daladala.
Na walipofika kuna daladala ilifika na kusimama ambapo Sabrina alipanda na yule dada alipanda pia na wakaenda kukaa kwenye siti moja ambapo Sabrina alimgeuzia mwanae mbele ili aweze kukaa nae vizuri na baada ya muda kidogo Sabrina akapitiwa na usingizi mule ndani ya daladala.

Maswali ya mama mdogo wa Sam yaliendelea juu yake ambapo sasa mama huyu alimuuliza Sam kuhusu Sabrina,
"Haya sasa naomba tumuongelee huyu Sabrina, je unampenda?"
"Yani hapo mama umeniuliza majibu maana Sabrina nampenda kuliko hata ninavyojipenda mwenyewe na kwa hakika naamini kuwa Sabrina si dada yangu ila tu wamefanya fitna ili niwe mbali nae. Nampenda sana Sabrina na siwezi kumuacha"
"Haya sasa, kama unampenda Sabrina ni kwanini anakuogopa? Ni kwanini anaogopa kuishi na wewe? Umesikia wapi mapenzi yanalazimishwa?"
"Nani kakwambia kama Sabrina hataki kuishi na mimi?"
"Mama yako kanieleza kila kitu Sam, hata hivyo leo nimeweza kujionea hali halisi ilivyo. Sam kiuhalisia kabisa namuona Sabrina kutokuwa na mapenzi juu yako? Hivi Sam unaelewa kama mapenzi ni kupendana? Pesa, mali, majumba na magari ya kifahari si vitu pekee kwenye mapenzi kwani mapenzi yanahitaji maridhiano, je kiuhalisia Sabrina karidhika kuwa na wewe?"
Sam akafikiria na kuamua kukatisha mada kwa kumwambia mamake mdogo kuwa muda umekwenda sana kwahiyo waende kula na kulala.
"Najua kama muda umeenda ila naongea vitu kiuhalisia kabisa, hata kama Sabrina asingekuwa ndugu yako unapaswa kumuacha huru kwani mapenzi hayalazimishwi"
Kisha wakatoka na kwenda kula hotelini halafu kurudi nyumbani.
Muda wa kulala, mama mdogo wa Sam alilala na Cherry hadi panakucha bila ya tatizo lolote.

Kwa upande wa Sabrina, alishtuka usingizini na kujiona bado yupo kwenye daladala huku akitazama nje aliona kabisa pamekucha.
Kwakweli hakujielewa kwa muda huo na kuanza kupiga kelele za kutaka kushushwa na lile gari lilisimama na kumshusha.
Aliangalia pale kituoni na kugundua kuwa ni kituo cha nyumbani kwao.
Sabrina aliamua kuongoza moja kwa moja hadi kwao na alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.
Alipofika kwao alimkuta mama yake akifagia uwanja, moja kwa moja bila hata ya kumsalimia akaingia ndani hata mama yake akamshangaa.
Kisha moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, alipofika chumbani macho yake yakatua kwenye kitanda chake, akashtuka sana baada ya kumuona Cherry amelala pale kitandani.


Alipofika kwao alimkuta mama yake akifagia uwanja, moja kwa moja bila hata ya kumsalimia akaingia ndani hata mama yake akamshangaa.
Kisha moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, alipofika chumbani macho yake yakatua kwenye kitanda chake, akashtuka sana baada ya kumuona Cherry amelala pale kitandani.
Sabrina akapiga kelele zilizomfanya mama yake ashtuke na kwenda kuangalia kuwa kuna kitu gani ila alikutana na Sabrina sebleni katika harakati za kutaka kukimbia ndipo alipomshika ili asikimbia na kwa bahati baba yake nae alikuwepo na kutoa ndani kwa haraka kuja kujua kinachoendelea kwa wakati ule kwani hata yeye alishtushwa na zile kelele.
"Nini tatizo Sabrina?"
Sabrina hakuwajibu kitu ila alikuwa akiwaonyeshea chumbani kwake akiashiria kwamba chumba chake ndio kina matatizo.
Ila walimshika vile vile na kwenda kuangalia kule chumbani ila hawakuona chochote kile cha kufanya washtuke au washangae.
Ndipo walipoamua kumuuliza Sabrina vizuri kuwa tatizo ni nini,
"Nimemuona Cherry hapo kitandani"
"Khee kwanza imekuwaje Sabrina? Na huyo Cherry yuko wapi yani umemuacha wapi?"
Sabrina hakujibu ila walirudi sebleni na kukaa ambapo mama Sabrina aliamua kumshusha yule mtoto mdogo mgongoni kwa Sabrina kwani mtoto huyo alionyesha kuchoka sana.

Sabrina aliinama chini akijaribu kuvuta kumbukumbu zake na akakumbuka kabisa kuwa kwa Sam aliondoka jioni sasa iweje afike kwao asubuhi?
Akamkumbuka yule mdada aliyekutana nae njiani na jinsi alivyokuwa akimsifia hadi wakapanda daladala moja ila tu hakukumbuka kuwa ameishia wapi.
Akainua kimya na kumwambia mama yake,
"Mama, unajua nimeondoka kwangu kule jana jioni!"
"Kwahiyo hukulala kwako? Umelala wapi sasa na huyu mtoto?"
"Hata sijui mama yani sijui kabisa, hata mi mwenyewe ndio nashangaa hapa kuwa imekuwaje nimefika hapa nyumbani asubuhi?"
Baba Sabrina nae akashangaa hilo swala na kumuuliza binti yake,
"Vipi mwanangu umeanza kuchanganyikiwa?"
"Hapana baba, naongea haya nikiwa na akili timamu kabisa yangu. Ninachoongea ni ukweli mtupu baba yangu, sijui ni kitu gani kimenipata ila nimeongea jambo la kweli"
Wazazi wake walimuangalia na kumuhurumia ambapo mama yake alimuomba akaoge kisha aende kupumzika.

Mdogo wa Sabrina kama alivyokuwa amepanga siku hiyo, alienda moja kwa moja kwa shangazi yake ambaye alifurahia kumuona na alikaribishwa vizuri sana kisha wakajaribu kuongea nae mawili matatu kwani aliamua kumuelezea yale anayoyahisi yeye na kusikiliza ushauri toka kwake,
"Unajua nini Sam, tatizo la pale kwenu ni ubishi, na sio kwamba hawajawahi kukumbwa na mambo mabaya hapana ila ubishi umewajaa. Niangalie mimi, nimepitia majanga makubwa mno hadi nikawa kama mtu niliyechanganyikiwa ila kilichoniponza ni tamaa kwani nilitamani vitu vizuri na maisha mazuri ila mwisho wa siku niliteseka na kuumia. Hiko kitu ndio kinachomtesa hata dada yako pale, tamaa aliwaza kuwa akitoka kwa yule atapata wapi maisha mazuri? Ngoja nikufichulie siri"
Mdogo wa Sabrina akawa makini sana kumsikiliza shangazi yao,
"Nifichulie shangazi"
"Kwanza Sabrina anaishi na yule Sam huku kampachika watoto wasio wake, hilo analitambua ila kwanini anaendelea kuishi nae? Kwavile anatambua wazi kuwa kwa baba mzazi wa watoto wale hatoweza kuyapata maisha kama anayoyapata pale. Anaona aibu kumuelezea mwanaume aliyezaa nae kwa madai kuwa haendani nae ila swali ni kuwa kama haendani nae amewezaje kuzaa nae? Tena watoto wote wawili! Ingekuwa mmoja tungesema ni bahati mbaya ila wawili mmh!"
"Kweli leo umenipa siri shangazi ila hiyo siri nadhani ni habari njema kwa familia pia ukizingatia Sam ni ndugu ila tatizo linalonisumbua kichwa ni kuhusu yule mtoto wa kike wa Sabrina, yule mtoto hayupo sawa shangazi yani hayupo sawa kabisa"
"Ni kweli kuwa yule mtoto hayupo sawa na hawezi kuwa sawa hadi yule mwanaume akubali na kama akikubali basi yeye atakuwa mashakani. Yule mtoto ni kazi nzito ifanyike juu yake, tena tusipokuwa makini basi ukoo mzima unaweza kuchukia uwepo wa yule mtoto"
"Kivipi shangazi? Twende ukatusaidie basi"
"Sina uwezo wa kuwasaidia kwa hilo, yangu hapa yananishinda sembuse hayo? Mnatakiwa mkae chini kwanza mule ndani kwenu mpange cha kufanya, ni bora tungemuwahi wakati kazaliwa tu ila sasa jambo limekomaa na limekuwa gumu zaidi"
Kwakweli ilikuwa ngumu kwa mdogo wa Sabrina kumuelewa shangazi yao kwa haraka kwani aliona kama anazidi kuchanganyikiwa haswa akikumbuka na ile kauli ya Jeff kuwa aachane na habari za yule mtoto.

Jeff nae kama alivyopanga aliamua kwenda kwa mganga mashuhuri na huko akamueleza mganga huyo kuhusu familia yake ambapo mganga alikiri wazi kutoiweza hiyo kazi,
"Nisaidie mganga, ile ni damu yangu"
"Najua kama ni damu yako ila kwakweli sitaweza kukusaidia kwani naweza kupoteza uhai wangu"
"Hautapoteza Mganga, nisaidie"
Yule mganga akacheka na kumwambia Jeff,
"Nini? Eti sitapoteza? Kulikuwa na mganga mashuhuri hapa mjini na alikuwa akitegemewa na wengi sana kwa tiba bora na zenye uhakika ila yuko wapi sasa? Alitaka kupambana na huyo mtu ila hakumuweza na badala yake yeye ndio akauwawa, kwakweli sitaki kupotea kizembe namna ile"
"Sasa nani atanisaidia? Mama yangu anateseka na mtoto wangu ndio huyo"
"Yote mliyataka wenyewe, kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua. Wewe kama mwanaume ilikuwaje ukubali watoto wako wapewe baba mwingine? Ungesimama kiume toka mwanzo haya yote yasingetokea ila tatizo lako uliona ni sawa tu ili mfiche siri haya sasa siri ndio hiyo inawatesa. Sina cha kukusaidia kwakweli"
Jeff aliinuka na kutoka huku akiwa na mawazo mengi sana kwani aliiona akili yake kukosa uelekeo.
Muda huu aliamua kurudi nyumbani kwao kwanza.

Kwa upande wa Sam na mama yake mdogo waliamka wakiwa na amani kabisa naye Cherry alikuwa kawaida kama watoto wengine ila alionekana kutaja neno moja tu ambalo ni mama na hapo ikawafanya kuelewa kuwa ni jinsi gani Cherry amemkumbuka mama yake ukizingatia hajaonana nae tangu jana.
Sam akamshika mtoto huyo na kumwambia maneno ya kumpa moyo,
"Usijali mtoto mzuri, mama atarudi tu muda sio mrefu"
Ila Sam alipomuangalia mtoto huyo akagundua kuwa kuna kitu kimepungua kwani hakuwa kama anavyokuwaga.
Alimuangalia sana hata mama yake mdogo akagundua hilo,
"Na mbona unamuangalia kiasi hicho huyo mtoto?"
"Hamna kitu mama ila namuangalia tu mwanangu alivyomzuri. Halafu nilikuwa nakusikia usiku kama ulikuwa unaongea hivi?"
"Inamaana sauti yangu ilifika hadi chumbani kwako?"
"Hapana, nilikuja sebleni kidogo ndio nikakusikia"
"Nilikuwa nasali mwanangu"
"Kheee umeokoka siku hizi?"
"Nimeamua kumtegemea Mungu maana bila yeye hakuna kinachowezekana. Nimepitia mengi sana katika maisha yangu kwahiyo nimeona ni vyema nikirejea kwa Mungu"
"Makubwa haya, unataka akusaidie nini mama yangu? Wataka kupata mtoto au? Umri si umeenda tayari mama!"
"Ni kweli umri umeenda ila kumbuka yule mke wa Ibrahimu yule Sarah alizaa na umri gani? Umri kuwa mkubwa sio kigezo cha kushindwa kuzaa. Hata hivyo kushindwa kwangu kuzaa sio kigezo cha kumkufuru Mungu wangu, nimeamua kumtumikia na nitamtumikia hadi naingia kaburini. Haijalishi nimesemwa na wangapi kuhusu uzazi au wangapi walioninyooshea vidole kuwa sizai na hata waliothubutu kunidharau na kunichukia sababu ya kukosa kizazi ila Mungu bado ananipenda na nitamtumikia tu"
"Mmh kweli Mungu kakushukia mama yangu yani maneno hayo yanakutoka wewe! Nakumbuka kipindi kile nilikuwa nakwambia mama kanifukuza nyumbani ulikuwa unalia tu na vile bamdogo nae alivyokufukuzaga ila hukunitupa ndiomana napenda kukusikiliza sana mama yangu. Ila niambie ndio kawaida yako ya kuamka usiku na kusali?"
"Unajua nini! Wakati naingia humu ndani jana niliona nyumba ikiwa nzito sana, tulikuwa tukizungumza hapa ila nilikuwa nikiomba kimoyo moyo. Na kabla ya kulala huwa nasali, pia huwa napenda kuamka usiku na kusali kwakuwa usiku una mambo mazito sana na pia napata muda uliotulia kuongea na mungu wangu"
Sam akamsikiliza mama yake huyu kisha akakaa kimya kwa muda kidogo halafu akamuuliza,
"Mama, unarudi lini Arusha?"
"Mmh Sam umenichoka tayari? Mbona mapema sana kuniuliza swala hilo? Nitaondoka mpaka pale mambo ya hapa yatakapokuwa sawa"
Sam akatulia tena kisha akainuka na kuelekea chumbani kwake ila pale sebleni alimuacha Cherry na huyo mama yake mdogo.

Jeff akiwa anaelekea kwao, njiani akakutana na mdogo wa Sabrina ambapo walisalimiana na kuongea mawili matatu.
"Umetokea wapi mwenzangu mbona unaonekana kuwa na mawazo sana?"
"Acha tu shemeji"
"Shemeji? Shemeji kivipi tena?"
"Aah nimejisahau Sam, nina mawazo tu naenda nyumbani kwanza kupumzika kidogo"
Mdogo wa Sabrina alimtazama Jeff kwani ingawa alijiona yeye kuwa na mawazo sana ila aliweza kugundua kuwa Jeff ana mawazo zaidi yake na kuamua kuagana pale kisha kila mmoja kuelekea kwao.

Jeff alifika kwao, akaiangalia hali ya mama yake na kumfanya huruma imjae zaidi kwani kila akifikiria kosa la mama yake kufanya aadhibiwe kiasi kile hakuliona.
Alienda chumbani kwake kutafakari yote aliyoelezwa na yule mganga na jinsi alivyolaumiwa kwa kuficha ile siri kwa muda mrefu.
"Natakiwa nisimame sasa, kila siku nasemaga hivi hivi ila tu huwa nakosa ujasiri ila sasa natakiwa kusimama kiume. Nichukue maamuzi sasa, natakiwa niende nyumbani kwakina Sabrina na kuwaeleza ukweli juu ya Sabrina na mimi na kuhusu wale watoto. Familia nzima inapaswa kujua kuwa wale watoto ni damu yangu, kwakweli nitasema tu na lolote lile linalotaka kuwa na liwe tu"
Jeff alishaamua jambo moja tu kwa wakati huo kwani hakutaka tena kukaa na ile siri yake kwenye moyo wake na aliamini kuwa ni ukweli tu ndio unaoweza kumuweka huru bila ya kujali chochote kile.

Sabrina akiwa amepumzika chumbani kwake, akajiwa na taswira ya mtoto wake Cherry ambaye alionekana kuwa pembeni mwa kitanda chake na kumwambia,
"Unadhani ni rahisi hivyo kunikimbia mimi? Kokote uendako tutaenda pamoja yani mimi ulipo nipo"
Huyu mtoto akaanza kucheka na kumfanya Sabrina ashtuke sana huku akiangaza kwenye chumba chake na kujikuta akiongea mwenyewe,
"Kwanini unitese mwanangu? Kwanini unifanyie hivi? Kwani kosa langu ni nini?"
Akasikia sauti,
"Sikutesi, ila na kwanini uniogope?"
Sabrina akatetemeka sana na kujikuta akiinuka pale kitandani na kutaka kukimbilia sebleni ila alipofika mlangoni akagundua kuwa ule mlango umefungwa tena kwa funguo na kumfanya Sabrina uoga umzidie.
Akageuka nyuma na kumuona mwanae kakaa huku kashika funguo na kuuning'iniza huku akisema,
"Njoo uchukue, funguo hizi hapa"
Sabrina hakuweza kuvumilia lile tukio na kujikuta akianguka chini na kuzimia.

Mamdogo wa Sam alishangaa kuhusu Cherry kwani alimkuta tofauti na alivyosimuliwa na dada yake,
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Huyu mtoto mbona ni wa kawaida tu jamani! Kwanini dada alisema kuwa si mtoto wa kawaida? Na mbona namuona kutokuwa na tatizo lolote lile? Halafu nimeambiwa kuwa ana majibu ya kikubwa sasa mbona yupo kawaida tu!"
Akamjaribisha kuongea nae na akamuona akiongea kitoto sana hata maneno mengine hakueleweka kuwa anatamka vitu gani.
Jambo hili lilimfanya mama mdogo wa Sam kuona kuwa huenda dada yake alikuwa anamatatizo binafsi ukizingatia na yale aliyosimuliwa kuhusu kukutana na baba Sam mahali hapo.
"Itakuwa dada yangu kavurugwa tu sio bure"
Kisha yeye akaendelea kucheza cheza na mjukuu wake huyo.
Muda kidogo Sam alitoka na kumuaga mama yake mdogo kuwa anatoka kidogo na atarudi badae.
"Ila usipike mama, nitarudi na chakula"
"Sawa hakuna tatizo"
Kisha Sam akatoka na kuondoka.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.