UKIMCHOKA MWENZAKO USIMTAFUTIE SABABU ZA KUMUACHA WEWE FUNGUKA TU.
Haijalishi una mwingine anayekushawishi uachane na huyo wa sasa, au humtaki tu kwa sababu zako binafsi, ni vizuri uachane nae pasipo visa wala ugomvi. Hakuna sababu ya kuanza kumtangaza mwenza wako vibaya kwa watu ili tu aonekane ni mbaya, wakati pengine si mbaya, ila unataka tu kuachana naye kwa sababu zako.
Ndugu, hapa duniani tunapita, hakuna sababu ya kutendeana mambo mabaya. Kama umuhitaji tena katoka maisha yako jitahidi tu kuwa wazi, mwambie ukweli kwamba "kweli nilikupenda lakini hatuwezi tena kuwa pamoja kwa sababu kadha wakadha. Ni kweli ataumia, lakini ipi bora kuendelea na visa au kumueleza wazi ajue moja, kama ni maumivu ya mara moja, iko siku yataisha. Jambo jema ni kuelezana ukweli.
Lakini jambo moja la kujua ni kwamba, ikiwa utamuacha mtu kwa sababu tu ya kumnyanyasa, hana kosa lolote, unaweza kupata mtu ambaye atakuja kuwa mbaya kuliko yule ambaye utamuacha kwa kumuonea wakati anakupenda.
Kumuacha mwenza wako kwa sababu zisizo na maana ni kujitafutia laana. Ili kuepukana kuachana ni vizuri kabla ya kuanzisha uhusiano kujuana kwa kina, ridhika na nafsi yako kabla ya kuamua kuwa na mtu.
Ni muhimu kuzungumza kuhusu dini, maana wengine wanakaa weee baada ya muda ndipo wanaanza kusema, eeeh bwana dini yetu si moja, ndugu wamekataa tusioane. Siku zote mlikuwa wapi kuzungumzia hili?
No comments: