Yafuatayo ndiyo mambo matano ya kuficha unapokuwa kwenye maisha ya ndoa;
Tendo
Maisha yenu ya mahusiano ya kimwili (sex) na mwenzako ni marufuku kumwambia mtu yeyote kwa gharama yoyote. Funga mdomo; iwe ni nzuri au mbaya. Ni mwiko kuwambia watu! (watu ni pamoja na mama yako, ndugu, marafiki, viongozi wa dini, n.k.)
Utamaduni
Utaratibu wenu wa kufanya mambo na mtindo wa maisha. Kwa mfano, sio lazima kuwaambia watu mambo yenu ya ndani ikiwemo mipango yenu ya baadae ya kifamilia au biashara, mambo ya watoto wenu, n.k. Ikibidi kusema, basi iwe ni kwa sababu maalumu sana ya kujenga watu wengine na kufundisha wengine sio kuanika tu maisha yenu hovyo; hasa mtandaoni. Ni muhimu kuchagua kwa makini kitu cha kuweka hadharani kwa maana ukitoa jambo hutaweza kulirudisha wala kulizuia lisisambae; litaenda hadi usikotaka, litaendea tu!
Ugomvi
Hakuna faida yoyote ya kusema magomvi yenu ya kwenye ndoa. Mara nyingi, tabia ya kusema magomvi yenu itawapunguzia heshima mbele ya jamii. Mara chache sana tabia hiyo ina faida, ila kila palipo na faida ya kusema magomvi, hasara ni kubwa zaidi kuliko faida. Chagua mwenyewe!
Pesa
Kipato chenu na pesa zenu ni siri. Wacheni watu waone kazi zenu na jinsi mnavyowasaidia wengine sio kujisifia pesa!
Siri
Ni mwiko kutoa siri za ndoa! Kama mwenzako kasema, “hii ni siri” au “usimwambie mtu!” Au “nimekwambia wewe tu!”, n.k. Hakikisha husemi kwa gharama yoyote, la sivyo hatakuamini tena! Na hasara yake ni kwamba, hatakuamini hata katika mambo mengine mengi tu! Tabia ya kutoa siri ni mbaya na inaweka ufa usiozibika kwa urahisi.
No comments: