Katika makala yangu ya “Kama mumeo anafanya mambo haya 15 ni mume bora kabisa”, nilielezea mambo 15 makubwa ambayo mume humfanyia mkewe. Lakini kwa kuwa ndoa ni muungano kati ya watu wawili, washirika wote wawili wanapaswa kuyatambua mambo mazuri ambayo wenza wao huwafanyia.
Kama mkeo anakufanyia mambo haya 15, mshikilie kabisa. Kwa ujumla, mke wa aina hiyo sio rahisi kumpata:
MWAMINIFU KWAKO ASIYEKUFANYIA UHAINI
Anajeheshimu, na kwa sababu ya hilo, anaufanya ukaribu wa kimahabba na wewe tu, hakusaliti wala kukufanyia hiana.
ANAKUAMINI
Hakutilii shaka kwa unachosema au kukifanya.
ANAKUPA FURSA YA KUWA PEKE YAKO
Anakupa muda ambao utautumia kuwa peke yako, marafiki zako au kufurahia mambo unayoyapenda. Halalamiki kama unataka kwenda kutembea au kwenda kucheza soka au michezo mingine ukiwa na marafiki zako.
ANAKUHESHIMU
Anakuheshimu na kuonesha kwa vitendo thamani yako adhimu kwake.
NI MBEMBEZI
Haachi kukubusu na kukupa joto la kumbatio lake bila hiana na kwa umaridadi wa kimahabba.
ANAKUJUA
Anajua unachokipenda na kukifurahia, hivyo anavipenda vitu hivyo na kuvithamini pia.
NI MKWELI KWAKO
Hakuachii shaka kichwani. Daima unajua kwamba anachokueleza ni ukweli.
HUFURAHI PAMOJA NAWE
Unashirikiana naye matukio yenye fuaraha na vicheko hata wakati wa siku yenye majukumu kayaya.
NI MAMA MZURI
Hakuna mama mkamilifu, lakini unatambua kuwa anafanya juhudi ya kuwa mama mwema kwa watoto wako.
ANAIHUDUMIA NA KUITUNZA NYUMBA
Anaihudumia nyumba kama njia ya kuonesha shukrani kwako.
ANAJITUNZA
Kuna siku utamkuta amevaa sweta na shati yako ya zamani, lakini pia anapenda kuvaa kwa ajili yake na kwa ajili yako pia.
NI MWENYE FURAHA
Hakika kuna siku ambazo ni ngumu, lakini anajitahidi kuyakabili maisha kwa ujasiri na uthubutu.
ANAKUSAIDIA
Anakuunga mkono na kukusaidia katika changamoto za kazi, familia na matatizo ya kiuchumi. Ni msaidizi wako namba moja na ni bandari salama kwako na kwa moyo wako.
ANAFURAHIA UTANI WAKO
Utamuona anacheka hata kama utani wako si wenye kuchekesha.
ANAKUVUMILIA
Bila shaka kutokana na changamoto na msongo wa kila siku, ni rahisi kwa wanawake wengi kushindwa kudhibiti jazba zao. Lakini iwapo anakuvumilia licha ya msongo na shinikizo anazokumbana nazo, basi hiyo ni ishara kwamba anakupenda kwa dhati.
Hakika hakuna mke mkamilifu. Sote tuna matatizo na changamoto kayaya, lakini hamu ya kuwa mtu bora kila siku ndio kitu cha muhimu. hivyo, iwapo mkeo anafanya mambo haya 15, muoneshe ni kwa kiasi gani unampenda na kumjali, kamwe usimuache, mshikilie.
No comments: