*MSHAWISHI MUMEO KILA SIKU*
Tunapomshawishi mtu huwa tunatumia njia mbalimbali ili kumvutia na kumvuta...
Kwa mwanamke, hutumia njia mbalimbali kumkamata mtu anayemtaka...
Kwa mwanamke, hutumia njia mbalimbali kumkamata mtu anayemtaka...
Huvaa mavazi Maridhawa, hutumia manukato mwanana, tabasamu tamu, jicho lenye mvuto na hujaribu kuulizia mambo ambayo mtu huyo anayapenda ili kumvuta...
Siku za mwanzo za uhusiano wa ndoa zetu, mambo huwa motomoto...
Mabusu mwanana, tabasamu zenye vionjo adhimu, kumbatio lenye uvuguvugu, na mambo kayaya yenye ladha tamu...
Ni kipindi hiki ambacho neema ya ndoa huonesha umaridhawa wake...
Tunaposonga mbele zaidi, mazoea hayo hubadilika, hususan kama hakuna utaratibu wa kuyaamsha...
: _Sasa ni namna gani unavyoweza kuendelea kumshawishi mumeo na kuufanya moto wa mahabba uendelee kuwaka ndani ya ndoa yenu...?...fuatana nami..._⬇
1. Tabasamu la kudumu, tabasamu la kila siku...
Anaporudi nyumbani mpokee kwa tabasamu na umuulize kuhusu mihangaiko yake ya siku hiyo...
2. Daima mbusu, mbusu kila siku kwa mahabba, na lifanye hilo kuwa sehemu ya ndoa yako...
3. Mtumie meseji za Mahabba...
"Ninakupenda sana mfalme wa moyo wangu", "ninakutakia siku Maridhawa"...
Katika kufanya hivyo uruhusu moyo wako uteme lulu za maneno ghali kutoka sakafu ya moyo...
: 4. Ukiweza jitahidi sana kula pamoja nae, na lifanye jambo hili kuwa jambo adhimu la ndoa yenu...
5. Kuwa Maridhawa Mbele yake, jipambe kwa ajili yake, hata kama mkiwa hamfanyi chochote...
Jirembe khaswaa, lifanye kuwa jambo endelevu katika kipindi chote cha uhai wako...
: 6. Kutembea mkiwa mmeshikana mikono ni jambo muhimu sana...
Daima mfanye ahisi kuwa wewe ni sahibu wake, badala ya kuwa inspekta wake...
7. Jambo muhimu sana ambalo hutakiwi kulisahau daima, ni kumpikia chakula anachokipenda...
Kama hujui kupika ulizia muongozo wa mapishi kutoka hata hapa mafunzo ya ndoa...
Chakula hicho sio tu kwamba kinaenda tumboni, bali huelekea moyoni pia...
Upendo wowote unahitaji kujitoa mhanga (sacrifice), tena kwa dhati, sio kwa majaribio...
Dawa yoyote hufanya kazi pindi inapotumika...
Tambua silika zake na umteke kupitia silika hizo...
: Kila jambo hutoa matokeo linapofanyia juhudi, tenda, usiweke mkono shavuni, chukua dozi hiyo kutoka famasia adhimu kabisa ya Mafunzo ya ndoa...
Kupitia ulimwengu wako wa moyo unaweza kuibadili shubiri kuwa asali...
Uhusiano ni mbegu katika bustani, inahitaji kutunzwa...
Tena matunzo ya kila siku...
*MWISHO*...
No comments: