MWANAUME EPUKA KUZUNGUMZA MAMBO HAYA SITA (6) NA MKEO MTARAJIWA
Kuna mambo mengi ambayo ni bora usiyazungumzie unapokuwa na mkeo mtarajiwa. Japokuwa yanaweza kuwa muhimu, lakini matokeo yake baadaye yanaweza kuwa mabaya au anaweza kukutazama kwa tahadhari na shaka. Hilo litaathiri maisha yenu kwa kiasi kikubwa. Hapa nitakuletea mambo 6 ambayo unatakiwa kujizuia kuyazungumza mbele yake:
- MAPENZI YAKO YA ZAMANI:
Japokuwa uwazi ni jambo zuri kati ya washirika wa maisha, lakini miongoni mwa makosa makubwa ni kuzungumza na mkeo/ mchumba wako kuhusu tajriba na uzoefu wako wa kimapenzi wa zamani, iwe kwa uzuri au kwa ubaya. Lichukulie kuwa ni jambo lililopita na ufunge ukurasa wake, kwa sababu ukilizungumzia kwa uzuri itampa wivu na ghadhabu pia, jambo litakalomfanya ayatilie shaka mapenzi yako ya dhati kwake na hivyo kuyafanya maisha yenu kuwa ya wasiwasi. Ukilizungumzia kwa ubaya, ukaliponda kwa lugha kali na mbaya kabisa, itamfanya abaini upande wako wa pili ambao ni mbaya na ambao umeshapita na hauna faida na manufaa kuuzungumzia.
- MATATIZO YA FAMILIA YAKO:
Kuzungumzia matatizo ya familia yako na kuonesha kuwa unamchukia mmoja wa wanafamilia yako au una ugomvi naye, inaweza kukufanya uonekane kuwa mtu asiyeaminika. Anaweza kuwa na shaka kwamba mumewe mtarajiwa si mtu wa kutunza siri za nyumba yake kama ambavyo anavyoshindwa kutunza siri za familia yake.
Aidha, usithubutu kuwataja wazazi wako kwa ubaya, kwa sababu hilo litamuonesha kuwa huwaheshimu wazee wako, na hivyo hutoweza kuwaheshimu wazee wake. Hilo litakuwa wingu jeusi ambalo huwa ni vigumu kuliondosha.
- MATATIZO YAKO BINAFSI:
Kuzungumzia matatizo yako muda wote mbele ya mkeo mtarajiwa inaweza kumfanya aone kwamba wewe ni mtu dhaifu ambaye huwezi kutatua mambo yako na matatizo yako. Ni bora ukawa na mtazamo chanya na uoneshe kuwa unajiamini na unaweza kukabiliana na vizuizi vyovyote.
- TENDO LA NDOA:
Katika kipindi hiki epuka kabisa kuzungumzia tendo la ndoa na mkeo mtarajiwa, kwa sababu kuzungumzia jambo hilo kunaweza kumfanya aamini kwamba umevutiwa naye kwa ajili tu ya matamanio yako ya kimwili na sio moyo na hisia za upendo wa dhati. Aidha, jambo hilo linaweza kumfanya akuonee soni au anaweza kujitenga nawe kabla hajawa mkeo. Hivyo, kulinyamazia jambo hilo ni hatua bora mpaka muda wake utakapofika.
- KUWAKOSOA MARAFIKI ZAKE:
Epuka kuzungumza vibaya kuhusu marafiki zake, hasa wale walio karibu naye, kwa sababu hilo litautia dosari uhusiano wenu na kumfanya awe na kazi ya kuchagua kuwa upande gani kati yako na marafiki zake. Hivyo, epuka sana jambo hilo. Epuka kuwazungumzia vibaya marafiki zake ili asichague kujitenga nawe badala ya kuwa karibu nawe.
- FAMILIA YAKE:
Usingumze kuhusu familia yake wala usijiingize kwenye mambo yao kwa sababu hilo litamfanya akutazame tofauti sana. Akitaka maoni yako kuhusu tatizo fulani la familia yake, basi tumia diplomasia katika mazungumzo yako. Mwambie kuwa kila familia duniani inapitia changamoto mbalimbali na hakuna changamoto ya kudumu. Utajijengea heshima moyoni mwake, atakupenda na ataiheshimu familia yako pia.

No comments: