SIMULIZI; HATA MIMI NI MTOTO WAWATU MAUMIVU ATAKAYOPATA MAMA YANGU NATAKA NA NYINYI MYAPATE!
t...
See moreNilirudi kutoka kazini, nilikuta mtoto wangu analia sana pale nnje, alikua mchafumchafu makamasi yanamtoka, kajisaidia, inzi wamemzunguka kila mahali, alikua analia sana hakuvalishwa hata nguo, alikua uchi wa mnyama kakaa chini analia. Kidogo nidondoke kwa mstuko lakini nilimkimbilia na kumnyanyua, bila kujali uchafu wake nilianza kumbembeleza, nilimchukua na kumpeleka ndani kisha nikamsafisha na kumnyonyesha kwanza kwani alionekana alikua na njaa sana.
Baada ya kumhudumia mwanangu nilianza kazi ya kumtafuta Dada wa kazi, binti ambaye ndiyo nilimuachia mtoto, nilihisi kuna kitu kibaya kimemtokea kwani haikua kawaida yake. Ni binti ambaye nimekaa naye kwa muda mrefu tangu nina ujauzito mpaka kujifungua na sasa mtoto ana miezi sita. Alikua anampenda mwanangu kama wake kabisa na mtoto alikua anampenda Dada yake kuliko hata alivyokua ananipenda mimi.
Kusema kweli wakati mwingine niliona mpaka wivu kwani kuna wakati mtoto hataki hata kunyonya kama yule binti hayuko pembeni na kucheza cheza naye. Nilihisi kuna kitu kibaya, nilihisi labda kaondoka katoroka, lakini niliwaza ni kwanini amuache mtoto katika hali ile. Mbona asubuhi niliondoka akiwa na furaha kabisa nilifikiria sikuwaza ni kitu gani nilikua nimemkosea, niliwaza labda mume wangu lakini nilisema hapana.
Mume wangu hakua akijishughulisha na wasichana wa kazi muda mwingi alikua bize na kazi zake hakaua hata na mazoea. Niliamua kumpigia simu lakini iliitia ndani chumbani kwake, nilienda na hakukua na mtu. Nilikaa kama nusu saa hivi nikasema nimpigie simu mume wangu kumuambia labda alikua anajua kitu, lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
Nyumba tunayokaa ni ya uzunguni kidogo, hivyo majirani ni mpaka kutembea kama mita mia tatu hivi, sikujali ingawa najua hana mazoea na majirani lakini nilienda kuuliza na hawakumuona. Wakati narudi nyumbani niliona Gari ya mume wangu imepaki nnje ya geti la nyumba yetu, nilijua mume wangu alikua karudi hivyo nilienda kumuangalia. Wakati nakaribia nilimuona mume wangu akishuka na kufungua geti.
Alipokua anarudi kwenye gari ili aliingize ndani macho yetu yaligongana, nilijajribu kumuita lakini harakaharaka aliingia kwenye Gari na kukanyaga mafuta ili kuingia, nikama alikua ananikimbia nilishangaa. Nilijikuta bila kuamua naongeza mwendo, ile naingia tu kwenye geti namuona Binti wa kazi anashuka harakaharaka kwenye Gari la mume wangu, anataka kama kukimbia kuingia ndani, lakini anaonekana kama vile hawezi nikama anachechemea.
Mume wangu naye anazima Gari palepale kabla hata hajalipeleka kwenye sehemu ya kupaki kwa nyuma, anashuka kwenye gari bila kuongea na mimi anarudi na kutoka nnje kabisa kwenye geti anatokomea. Narudi kwa Dada wakazi ambaye ashafika mlangoni, anakaribia kuingiandani lakini namzuia, naanza kumuuliza alikua wapi na mume wangu na kwanini alimuacha mtoto peke yake anageuka.
Najikuta napigwa na mshangao kwani naona nguo kwambele ni kama zimeloa damu, anajaribu kuniongelesha lakini anaishiwa nguvu anadondoka na kua kama amepoteza fahamu. Pale sasa ndiyo nachanganyikiwa, namkalisha mtoto pembeni na anza kumpepea, nataka nimpeleke Hospitalini lakini nasita. Namkagua na moja kwa moja nagundua kuwa yule binti amebakwa, nasema amebakwa kwani mimi ni Daktari hivyo najua mtu aliyebakwa nishakutana nao wengi.
Ukiangalia mikono inaonyesha ilishikwa kwa nguvu, kama vile alibanwa chini na mtu, hajachafuka hivyo inaonekana walikua sehemu nzuri, lakini itoshe tu kusema najua amebakwa na kwa ilivyoonekana najua ni mume wangu kamfanyia kile kitendo. Sasa naogopa hata kumpeleka Hospitalini kwani itabidi nitoe taarifa Polisi na mume wangu ataishia jela. Kwakua ni mtalaamu napima mapigo ya moyo, hajazimia kabisa ni kama ameishiwa nguvu tu.
Sijui nimepata wapi unguvu namnyanyua namuingiza ndani, namtengenezea maji ya Glucose nampa anapata nguvu kidogo na kunyanyuka. Anataka kuomngea lakini namkataza, sitaki kusikia, sitaki kujua alichofanyiwa namuambia anywe maji kisha aingie chumbani kwake akaoge na kuwa vizuri. Amepata nguvu kidogo namsaidia kunyanyuka mpaka chumbani kwake namuacha alale.
Naondoka harakaharaka kwani sitaki anisimulie. “Dada lakini Baba amenibaka…ameni…” Anaanza kuongea wakati huo nishafika mlangoni, kqwa uchungu najifanyua sijasikia natoka nnje. Naingia chumbani najikuta naanza kulia kama mtoto mdogo huku nikiwaza mume wangu umefanya nini? Nataka kumsaidia yule binti lakini siwezi bila kumuangamiza mume wangu, najua nikiripoti Polisi ni miaka thelathini.
Lakini hata kama asipofungwa ni aibu, nitaweka wapi uso wangu, nasema poteli ya mbali, binti atapona nitamrudisha kwao na nitaongea na mume wangu maisha yataendelea. Jioni mume wangu anarudi, binti bado kalala ndani, alitaka kuamka kufanya kazi za ndani nikamkataza. Naongea na mume wangu ambaye anajifanya hajafanya chochote yeye alimuokota vile, namuambia najua ulichofanya.
Haombi hata msamaha ananiuliza “Kwahiyo umeamua nini? Unaondoka au la, kama unaondoka ondoka sijali.” Nashindwa hata cha kusema najikuta nayamaza, mume ananinunia wiki nzima kana kwamba mimi ndiyo nimekosea, kama mjinga namuomba msamaha, najifanya kumuomba msamaha kwa kumshutumu na kumsingizia mambo ya uongo. Ananisamehe lakini kwa shariti yule binti aondoke pale hamtaki.
Ndoa ndiyo ina miaka miwili tu na yule ndiyo alikua mfanyakazi wetu wa kwanza, nawaza hivi akiondoka nikaleta mwingine si atamfanyia hivyo hivyo. Namuambia sawa lakini mpaka nipate mwingine. Kweli naanza kutafuta kwani kanipa wiki moja tu ya kutafuta msichana mwingine, Napata huko Kijijini hivyo inabidi nimfukuze huyu kabla huyo mwingine hajaja ili asijemuambia kilichompata na akaniharibia.
Nawahi kurudi nyumbani ili angalau nimpeleke Shoping akawanunulie ndugu zake zawadi, najua alichomfanyia mume wangu hivyo nataka asiondoke kwa ubaya, nikama nataka kumlipa hivi ilia nyamaze. Nafika nyumbani, najaribu kugonga mlango haufunguliwi, nashuka kwenye Gari nafungua geti dogo naingia kisha nafungua kubwa naingiza Gari. Nafika mpaka ndani naanza kuita, naita naita we sisikii mtu.
Naamua kwenda chumbani kwa Dada kumuangalia, namkuta amelala na mtoto kalala pembeni, Napata ahueni kidogo. Narudi kujiandaa naoga na kuabdili nguo, kisha narudi tena chumbani kwake nakuta bado amelala, nasema hapana si kawaida yake ngoja nimuamshe. Najaribu kumgusa ni wabaridi, nastuka, namgeuza nakuta mapovu yamemjaa mdomoni, Mungu wangu, sijiulizi mara mbili amekunywa sumu.
Naangalia mapigo ya moyo nakuta tayari alishapoa zamani, nachnganyikiwa siwezi hata kumnyanyu, sitaki kupiga kelele na kumuamsha mtoto, natoka nnje nampigia simu mume wangu ili aje kabla ya kwenda popote. Namuambia kila kitu ananiambia nisifanye chochote mpaka aje kwani inaweza kuleta shida, nashindwa hata kurudi chumbani kumuangalia akili ni kama zimeniruka.
Baada ya kama nusu saa hivi mume wangu anarejea ananiuliza nini nampeleka mpaka chumbani. Namuambia aingie polepole mtoto amelala sitaki aione ile maiti pale. Anaingia na kusema tumtoe pale kwani tukimgusa mtoto ataamka, tunataka kumshika lakini kabla ya kumgusa tunaona kakaratasi pembeni yake. Nakachukua harakaharaka na kukasoma.
“Dada unajua mume wako amenibaka sikutaka kufanya lakini hukujali, nilikua bado bikra ameniaribia usichana wangu sasa mimi nitaolewa na nani. Nimeamua kuchukua maisha yangu lakini nataka mpate uchungu kama atakaoupata Mama yangu na mtoto wenu naye nimempa sumu.” Ujumbe unaishia hapo, nadondosha kile kikaratasi ndiyo napata wazo la kumgusa mwanangu, namgeuza nayeye naona mapovu tu, alishapoa muda mrefu, nguvu zinaniishia nadondoka na kupoteza fahamu.
Ni mwaka wa pili sasa tangu tukio hili litokee lakini kwangu ni kama jana. Nashindwa hata kumlaumu mume wangu najilaumu mimi kwani ndiyo nilificha madhambi yake na kumuacha binti wa watu akiteseka katika msongo wa mawazo. Kama Daktari nilikua na wajibu wa kumsaidia yule binti na kama Mama nilikua na wajibu wa kumlinda na watu kama mume wangu lakini nilichagua upande wa udhalimu, ndiyo sina tofauti na mume wangu aliyembaka yule binti.
***MWISHO***
No comments: