TAMBUA NAMNA YA KUISHI NA MTU MWENYE TABIA ZA MTOTO MCHANGA/MDOGO KATIKA MAHUSIANO (Ndoa).
Imani kubwa inayojengwa na mtu katika Safari ya kuelekea kwenye mahusiano ya uchumba na hatimae maisha Kamili ya Ndoa, ni kuwa na matamanio ya kuishi maisha yasiyo na bugudha na kutarajia mazuri tu.
Lakini ni Muhimu kutambua kuwa, malezi(Tabia) ya kila mtu hutofautiana, na kutofautiana huko ndiko kunakoleta baadhi ya changamoto ambazo zinamhitaji mtu aliye katika mahusiano kutumia Akili ya namna ya kuishi na mwenza wake.
Tabia za mtoto mdogo/Mchanga hupenda kila jambo/kitu afanyiwe maana anaamini kuwa yeye ndie anaestahili kufanyiwa kila kitu bila kujali gharama ya kitu chenyewe.
Mtoto mdogo/Mchanga hata anapokosea na kuonywa au kuadhibiwa, katika akili yake hujihesabia kuwa ameonewa Wala hakustahili kufanyiwa hivyo.
Hata katika Mahusiano ya Uchumba au ndoa unaweza ukawa na mtu mzima lakini tabia zake ni Kama mtoto mchanga, ambaye kila kitu atajihesabia Kama mtu anayestahili kufanyiwa.
Kama ni suala la heshima, atahitaji yeye aheshimiwe zaidi kuliko anavyoweza kumheshimu mwenzake.
Katika suala la zawadi, yeye atahitaji aletewe kila Mara Ila yeye hayupo tayari kabisa. Hizi ni tabia za watoto wachanga.
Pia Ukiona mtu ana tabia ya kususia kila Jambo, Tambua huyo ni mtoto mdogo ambaye yeye hujihesabia haki kwa kila kila kitu, maana yeye anahitaji asikilizwe kuliko anavyoweza kumsikiliza mwenzake.
Ukiona unaishi au unaelekea kuishi na mtu mwenye tabia Kama hizo, huna budi kuvaa moyo wa Mama mzazi ambapo utaishi nae Kama mtoto mchanga huku ukitumia Hekima ya ki Mungu kumpandikizia tabia za mtu mzima katika mahusiano.
Kuibeba roho ya mama mzazi itakusaidia Sana kuishi na mtu huyo, kwa sababu utamchukulia Kama mtoto wako ambaye utamvumilia kwa tabia hiyo.
Maana sio rahisi kuvuka hatua katika ukuaji bila kupitia katika stage ya mtoto mchanga hatimae kuelekea katika hatua ya kuwa mtu mzima(Mkubwa ki akili).
Mtoto mchanga muonyeshe tabia yako, atajifunza kikamilifu kupitia tabia yako.
The Light Of Universe Ministry
Ejide Andrew Noah
Ejide Andrew Noah
No comments: