Faida za kutoka out na yule umpendaye

Wapo baadhi ya wanadoa wengi wao ukiwauliza mara  ya mwisho walitoka out lini na wanza wao? huenda majibu yao yakakunyima raha kabisa, huenda majibu yao yakakunyima raha kwa sababu wapo wataokwambia hawajawahi kabisa kufanya hivyo, lakini wapo baadhi watakaokwambia mara ya mwisho walifanya hivyo walivyokuwa kwenye hatua ya uchumba pamoja na majibu mengine kama hayo. 

Ila ukweli ni kwamba moja kati ya vitu vinavyongeza radha mwanana katika mahusiano ya ndoa ni pamoja na kutoka matembezi na yale umpendaye (out). Kutoka matembezi (out) kuna faida lukuki katika mahusiano miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuonesha unamjali na kumheshimu sana yule umpendaye.

Kutoka matembezi huenda kwako ukaona kama ni kitu cha kipuuzi sana,  ila usichojua ni kuwa  kutoka out wakati mwingine  kunasaidia sana kumpa uhuru yule uliyenaye kwenye mahusiano ya ndoa kuweza kuongea hata yale ambayo mtu huyo mara nyingi alikuwa haongei.  Nadhani kwa wale wenye tabia hii ya kutoka out na wenza wao watakubalina na ukweli huo. 

Kutoka out husaidia sana kwenye mahusiano ya ndoa kwa sababu wakati mwingine huenda huko out mkapanga mipango ambayo ni mziuri itakayowasiaidia kuweza kupata maendeleo yenu binafsi na yenye kuleta mafanikio makubwa sana maishani mwenu. 

Enyi watu wote mlioko kwenye mahusiano ya ndoa jifunzeni kutoka matembezi (out ) maana kuna faida sana. Usiwe ni mtu ambaye upo bize kwa siku zote 365 kwa mwaka bali, jitahidi kutenga siku kadhaaa kati hizo kwa ajili ya kufanya matembezi na yule umpendaye.

Na; Benson Chonya.






USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.