Mo Dewji atoa ahadi kwa wachezaji wa timu ya Simba SC


Mwekezaji wa Simba SC, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameahidi kuwapa bonasi ya shilingi milioni tano wachezaji wa timu hiyo wagawane kwa kila mechi watakayoshinda kati ya mechi nne walizobakiza, ikiwemo ya jana dhidi ya Ndanda.

Mo alitangaza neema hiyo mara baada ya kukutana na wachezaji wa Benchi la Ufundi la timu hiyo na kula futari kwa pamoja kwenye moja ya hoteli kubwa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo wachezaji hao watapewa bonasi hiyo kwenye michezo minne waliyoibakisha ya ligi ukiwemo wa jana walipocheza dhidi ya Ndanda FC.

Mo ameongeza dau hilo, ukiachana na Sh 400,000 ambazo amekuwa akitoa kwa kila mchezaji kila wanaposhinda, tangu ligi imeanza.

Mtoa taarifa huyo alisema, Mo amewaongezea bonasi hiyo kwa ajili ya kuwaongezea morali na hamasa ili wafanikishe malengo ya kutwaa ubingwa.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.