JIMAMA TAMU SEHEMU YA 35

Image result for JIMAMA TAMU
JIMAMA TAMU
Mtunzi-Mniga Mputa
Sehemu. Ya. 35
WhatsApp:0678926045
Akasikia watu wanaongea kiswahili huku wanapika msosi walikuwa ni madume tupu hapo mniga akasogea hadi pale,
"'Oi niaje mazee, aliongea mniga na kusababisha jamaa wale kumuangalia,

'"safi nambie mzee baba, alijibu mmoja kati ya wale jamaa,
'"sory jamaa Mimi ni mtanzania sijuwi nyinyi wenzangu, aliongea mniga,
'"sisi pia ni watanzania, alijibu yule jamaa,
'"Oh sawa nilikuwa nashida ndugu zangu Kama mnavoniona hapa mwenzeni ni mgeni nchi hii nilikuja kikazi na bosi kanifukuza harafu hajanipa hata hella na Mimi sijuwi sehemu yoyote hapa natembea tembea tu naomba msaada wenu jamani, aliongea mniga kwa upole Sana,
'"Duuh kwanza Pole Sana ndugu yetu maana watanzania tukikutana kwenye nchi ya watu ni ndugu sasa usiogope tutakusaidia ndugu yetu wewe kaa hapa na tupike tule tunalala kwenye gari humo juu sisi tunarudi Tanzania kesho kutwa, aliongea yule jamaa na mniga hakuamini masikio yake maana ucku ule engeenda wapi,
'"asante Sana ndugu zangu jamani, alionge mniga na kukaa zake pale chini wakaendelea kupiga stori nyingine hadi pale chakula kikaiva na wakapakuwa na kuanza kula chakula huku stori nyingi Sana wanapiga basi walipotosheka mniga akawaambia,
'"asante Sana jamani kwa ukalimu wenu sasa nilikuwa naomba simu niwajulishe nyumbani Kama nimefukuzwa, aliongea mniga,
'"Oh usijari chukuwa tu ndugu yetu, aliongea jamaa mmoja na kumpa mniga simu ambapo alichukuwa na kuandika namba ya Salome ambae aliikalili kichwani na kuipiga ikaita kidogo na kupokelewa,
'"hallo nani mwenzangu, ilikuwa ni sauti ya Salome,
'"Mimi mniga mpenzi wako Salome, aliongea mniga,
'"Oh mbona nakupigia simu yako hupokei kwanini lakini harafu unanipigia kwenye namba nyingine, aliongea Salome,
'"Duuh ni stori ndefu Sana mpenzi wangu nimefukunzwa na mjomba yako Kama mbwa tena usiku Kama huu jamani ila sikuwa na namna hadi simu nguo vyote nimeviacha kwa mjomba wako, aliongea mniga,
'"pole Sana mpenzi wangu kwa misuko suko kwa sasa upo wapi, aliongea Salome,
'"Mimi sasahivi nimepata watanzania wenzangu na wamenisaidia hadi kunipa simu yao, aliongea mniga,
'"sawa basi kesho Mimi ntakuja na tutarudi nyumbani yani ntaondoka na ndege ya asubuhi Sana mpenzi, aliongea Salome,
'"sawa hakunashida usiku mwema, aliomgea mniga na kukata simu akaenda kumpa simu jamaa yule mwenye simu,
'"asante Sana maana nimepiga namba za wazazi wangu hawapatikani ndo nikampigia mchumba wangu kaniamba kesho asubuhi anakuja hapa, aliongea mniga,
'"Oh hakunashida jembe letu sasa twende kwenye gari tukalale tu, aliongea yule jamaa na kuongozana hadi kwenye gari wakapanda juu na kulala,
Itaendelea..............


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.