ANAYEBEBEKA ANABEBWA NA ANAYEVUMILIKA ANAVUMILIWA.

Beautiful model woman kissing red rose flower Stock Photo - 36332712
Kwenye mapenzi ukiona mtu anamsifia na kumuongelea vizuri sana mume au mke wake, haimaanishi kwamba huyo anayesifiwa ni mkamilifu au yuko perfect, na kama ulidhania hivyo basi akili yako ina shida kidogo.
.
Iko hivi, kwenye mapenzi hatutafuti au kuishi na mtu mkamilifu bali mtu ambaye mazuri yake yanazidi maradufu madhaifu yake na yale madhaifu hayana nafasi kuathiri mtazamo wa huyu anayesifia.
.
Kwenye mapenzi tunatafuta anayebebeka na kuvumilika maana hayo ya kuvumilika kwake hayazidi yale yasiyovumilika, nasema hivi maana wapo ambao hawabebeki, hawachukuliki na hawavumiliki kwa jua wala kwa mvua.

Yamkini hawa ndio wale ambao huzitamani ndoa za wenzao, huwatamani wake na waume wa wenzao na hupandwa na povu sana wanapoona mtu anamsifia mpenzi wake japo sio afya njema kuanika mahaba yenu mitandaoni kwakuwa mnampa wepesi shetani kuwamulika awachome muachane ili mpate kazi kufuta post zenu na kuchapisha maneno kama Bwana ndiyo tegemeo langu,mwamba na ngao yangu,mapenzi basi tena,wanawake/wanaume wote ni mbwa nk.

Ndoa/Mapenzi ni safari, hivyo jali safari yako na ujue kuyalinda kwa akili na hekima.
Sio kila tukio ni la kupost mitandaoni kuhusu maisha na familia yako.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.