STORY: KISA MAPENZI TU SEHEMU YA: 22 (MWISHO)




******************
ILIPOISHIA .
Lakini Prisca alinipa moyo na kuniambia kila kitu kitaenda sawa basi tukaweza kulala huku tukiisubiria kwa hamu hiyo kesho Prisca anipeleke huko nyumbani kwa wazazi wake Mikocheni ili akanitambulishe!.

πŸ‘‡ENDELEA NAYO πŸ‘‡
Kiukweli sasa niliweza kujisikia kuwa na Amani kabisa ndani ya moyo wangu hofu yote iliweza kunitoka kwa sababu ya Prisca kuniambia maneno ya kunipa faraja kuwa nisiwe na wasiwasi juu ya huko tutakapoenda kwa wazazi wake. Usiku tuliupitisha kwa Mapenzi motomoto na Mahaba mazito ambayo atukuwahi kupeana hapo kabla kama haya tuliyopeana kwa usiku huu wa maraha kwa hakika ilikuwa ni burudani tosha kwetu sisi wawili kuiburudisha miili yetu pamoja na mioyo yetu kimapenzi na baada ya kupeana Dozi nzito ya kutosha hatimaye tukaweza kulala usingizi mzito.
Asubuhi na mapema ya siku iliyofuatia tukaweza kuamka salama huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha ndani ya moyo wake. "Jose yaani hata siamini mpenzi wangu, kama ni kweli hii leo nakupeleka kwa wazazi wangu" Prisca aliniambia huku akiwa amejilaza juu ya kifua changu majira haya asubuhi. Japo tulikuwa tumeshaamka tayari lakini bado tuliendelea kubakia tumejilaza hapa kitandani huku tukichezeana kwa Mahaba. "Hata mimi siamini pia Prisca, kwani mitihani niliyopitia ni mizito sana kwenye maisha yangu" nilisema kwa sauti ndogo. "Mitihani gani tena Jose, kama ni kuhusu hao wakina Benny na Eddy sasa ni kuwasahau tu kwenye maisha yetu" aliniambia Prisca. "Hapana sijamaanisha wakina Benny, nimemaanisha juu ya maisha yangu kwa ujumla kumbuka uliponikuta na kunitoa kule nilipokuwa naishi kwenye yale maisha ya dhiki" nilisema. Prisca akatabasamu na halafu akaniambia: "Jose bhana hivi ni kwanini lakini unapenda kukumbuka mambo ya nyuma yaliyopita? Hebu naomba uache  kuzunguumzia vitu hivyo, kwa sasa tuongelee mapenzi yetu yatakavyokuwa" aliniambia Prisca. "Sawa mamy lakini bila ya wewe leo hii nisingekuwa nafikiria kitu mapenzi kabisa, maana kwa maisha yale niliyokuwa naishi ingechukua muda sana mimi kuwa na mpenzi au nisingekuwa naye kabisa" nilisema  huku nikimchezea nywele zake ndefu Prisca. "Hebu twende bafuni kwanza tukaoge tujiandae kuondoka, naona bado unaendelea tu kuongea vitu vilivyopita" alisema Prisca huku akijiondoa mwilini mwangu na kutoka kitandani  halafu akasimama. SHABASHIIII!! Prisca alikuwa yupo mtupu hana nguo hata moja mwilini mwake kama jinsi tulivyolala usiku wa jana yake. Mwanaume nikajikuta mzuka umepanda baada ya kuuona mwili wa mrembo wa Prisca kama vile ndio Mara ya kwanza nauona na  wakati nimelala naye usiku kucha kitandani pamoja! Hata sikujua nilinyanyuka kitandani muda gani yaani nilijikuta tu tayari na mimi nimesimama mbele yake na kumnyanyua juu kwa juu na kuelekea naye huko bafuni kwa ajili ya kuoga. Uzuri bafu ni ndani kwa ndani humuhumu chumbani sio mpaka tutoke kwenye korido, baada ya kufika bafuni kwanza kabla atujafungulia maji kulowanisha miili yetu tukaanza kuipasha moto kwa kuliamsha Dude tena. Baada ya kujiburudisha vya kutosha tukaweza kuoga na kujisafisha vizuri sana miili yetu na tukarudi chumbani ambapo bila ya kupoteza muda Prisca akanichagulia nguo nzuri na za heshima ambazo ni maalumu kwa ajili ya mimi kwendea huko nyumbani kwao kutambulishwa. "Duuh hizi nguo ulikuwa umeziandaa muda gani mbona sijawahi kuziona kabisa?" nilijikuta namuuliza hivyo wakati alipokuwa ananifunga vizuri Tai shingoni. Mwanaume leo hii navaa Suti ya gharama  na wakati tangu nizaliwe sijawahi kuvaa vazi hili kama nilivyoamini Suti ni vazi la matajiri tu. "Hii Suti niliinunua kwa ajili ya Benny wakati nilipokuwa Marekani, lakini baada yΓ  kurudi hapa na kumkuta na tabia za ajabu ajabu nikaghaili kumpa kama zawadi na hatimaye leo nakuzawadia wewe hapo baby wangu" aliniambia Prisca huku akitabasamu. "Ooho Ahsante sana mpenzi wangu, sijui hata nikupe nini kwa jinsi unavyonijali" nilisema huku nikim'busu shavuni. "Mapenzi yako tu Jose kwangu ni zawadi tosha, nafurahi sana kuwa na wewe mpenzi wangu" aliniambia Prisca na kunikumbatia ambapo tulikumbatiana kwa muda kidogo huku tukinyonyana denda na kupapasana mwilini. "Mmh mpenzi wangu basi inatosha, tutashindwa kwenda tukianza mambo hayo" nilisema na kumshtua Prisca ambaye tayari alishakuwa amenogewa na joto langu. "Baby yaani kila muda natamani niwe nimekuganda mwilini mwako sijisikii kukuchoka Jose wangu jamani" aliniambia Prisca kwa sauti yake laini. Basi baada ya kumaliza kuvaa na kupendeza wote wawili tukatoka humu chumbani na kuelekea mpaka sebuleni ambapo tuliikuta Chai ya nguvu tayari imeshaandaliwa mezani na wale mabinti wanaomsaidia kazi Prisca hapa nyumbani kwake. Baada ya kumaliza kunywa Chai na mapochopocho yote ya mezani mimi na Prisca tukaondoka zetu na kuingia kwenye gari ya kifahari sana ambayo ni moja ya magari manne anayoyamiliki Prisca hapa mjengoni kwake. Mwanaume nilijihisi kama vile nipo peponi kwa jinsi ninavyoyafurahia haya maisha. "Jose mpenzi wangu naomba ujiamini huku tunapoenda  ukifika mbele ya wazazi wangu, usiwe na hofu yeyote kabisa moyoni sawa?' aliniambia Prisca wakati akiiondoa gari hiyo nje ya geti na kuanza safari. " Sawa mpenzi wangu nimekuelewa, ninapokuwa na wewe najihisi ni mwenye furaha" nilisema huku nikitabasamu. Safari yetu ya kuelekea Mikocheni nyumbani kwa wazazi wake Prisca ikaendelea.
**************
Hatimaye tukaweza kufika mpaka huko Mikocheni na baada ya kukaribishwa vizuri ndani ya mjengo wa kifahari hapa nyumbani kwa akina Prisca sasa nilikuwa nipo mbele ya wazazi wake Live bila chenga huku moyo wangu ukianza kunidunda kwa mbali sababu ya hofu niliyokuwa nayo mimi mtoto wa Masikini. Prisca bila ya kupoteza muda akaanza kujieleza na kunielezea mimi mbele ya wazazi wake na kuwaambia lengo la yeye kunipeleka mimi pale kwao ni kunitambulisha kuwa mimi ndio mpenzi wake wa sasa na anaomba Baraka zao kama wazazi wake wamkubalie aweze kuwa na mimi ikiwezekana tufunge ndoa kabisa. "Kwanza pole sana kijana, tumepata taharifa zako kwa kupitia huyuhuyu mchumba wako Prisca kuwa ulitekwa na kutakiwa kufanywa vitendo vibaya na akina Benny pamoja na Eddy ambao hivi sasa ni marehemu" alisema baba yake Prisca. Mzee mmoja wa makamo na mtanashati sana halafu akaendelea tena kuongea: "Sisi kwa upande wetu hatuna kipingamizi chochote juu ya binti yetu Prisca kuwa na wewe, kwani alishatuambia kila kitu kuhusu wewe na maisha yote uliyoyapitia na mpaka sasa mko pamoja hivyo kijana jisikie kuwa Amani ukiwa na mwenzako" baba yake Prisca aliniambia na kunifanya nipatwe na mshangao huyu Prisca aliwaambia lini na muda gani hawa wazazi wake juu ya maisha yangu! Lakini niliona afadhali bora kitu kipo wazi. "Nashukuru sana baba yangu nafurahi kusikia hivyo" nilisema huku nikitabasamu. "Sawa kijana, lakini kama kweli umempenda binti tunaomba umpende kweli sisi hatuna shaka yeyote juu yake yeye kukupenda wewe Prisca anakupenda kweli mwenyewe hilo unalijua" Mzee aliniambia. "Ndio baba najua hilo na mimi pia nampenda sana" nilisema. "Ok basi ni vizuri sana kama ni kweli mnapendana, sisi tunachotaka mpendane kwelikweli msije tena huko mbele mkaleteana mambo ya ajabu" alitoa tahadhari baba yake Prisca. "Hapana baba mimi na Jose tunapendana sana" Prisca aliingilia kati na kusema hivyo. "Basi kama ni hivyo kila kitu ni Ruksa sisi hatuna kipingamizi na nyie juu ya mapenzi yenu jiachieni kwa raha zenu, Jose tutakuhesabu kama ni mtoto wetu ukichukua nafasi ya Eddy japo wewe ni mkwe wetu" alisema baba yake Prisca kwa furaha na wote tuliweza kufurahi kwa pamoja kwa hakika ilileta raha sana. πŸ˜€
Siku na majuma yalipita na sasa ni miezi mitatu imepita tangu niingie rasmi kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo Prisca yaani ni mapenzi motomoto ambayo sikutarajia kama siku na mimi nitakuja kuyapata. Kwani maisha yangu mpenzi msomaji najua utakuwa unayakumbuka tangu nilivyokuwa naishi kule Kipawa Karakata 'Uswahilini' nilivyokuwa navaa yeboyebo na kushindia kunywa Uji wa chumvi pamoja na kuzunguka kwenye yale magodauni ya wahindi kutafuta kibarua (Kazi) lakini sasa mambo yote ni motoooo!
Mimi na Prisca tukaweza kusafiri pamoja mpaka kijijini kwetu huko mkoani Morogoro na kwenda kumuona bibi yangu ambaye alifurahi sana kuniona na nikamtambulisha Prisca kwake bibi naye akaweza kutoa Baraka zake kwetu sisi. Na hata tulipomuambia mpango wetu ni kumchukua na kwenda kuishi naye mjini Dar es salaam bibi yangu hakuweza kukataa kwani naye alikuwa tayari ameshajichokea na maisha ya huku Kijijini aliyokuwa anaishi kwa shida na kukosa msaada pamoja na usimamizi. Tukaondoka na bibi kwenda naye mjini.

MWAKA MMOJA BAADAE

Mapenzi yetu yalizidi kushamiri na hatimaye tukaweza kufunga ndoa kubwa na ya kifahari sana hapa mjini ambayo ilikuwa ni gumzo kila kona. Sasa mambo yalikuwa mazuri shida zote ziliweza kuisha kwa upande wangu na hata vile vitisho pamoja na ule ukatili niliotaka kufanyiwa na Benny pamoja na Eddy niliusahau kabisa kwani hata na Wale watuhumiwa wengine waliobakia akiwemo Samson na yule Daktari wa kichina (Lee Chen) aliyetaka kulikata 'Gobole' kwa maagizo ya Benny kipindi  kile wote walihukumiwa kifungo cha miaka thelathini (30) jela kila mmoja sambamba na kazi ngumu ili iwe fundisho. Kwa upande wetu huku napo  Biashara na miradi yote ya wazazi wake Prisca waliweza kutukabidhi mimi na mke wangu Prisca ndio tuisimamie na tuliweza kuisimamia vyema bila ya matataizo yeyote pia Mungu aliweza kuleta Neema yake kwa Prisca na sasa ni mjamzito wa miezi sita (6) tunasubiria mtoto wetu na sisi tuwe wazazi tuitwe Baba na Mama. "Siamini Jose kama leo umekuwa ni Mume wangu wa ndoa, nakupenda sana" aliniambia Prisca tulipokuwa tumelala kitandani. "Hata mimi pia siamini Prisca kama leo hii umekuwa ni Mke wangu wa ndoa kwa hakika Mungu Mkubwa na nitakupenda siku zote za maisha yangu" nilisema huku nikimkumbatia Prisca wangu. "Nami pia nitakupenda Jose mpaka mwisho wa uhai wangu hapa duniani" aliniambia Prisca na baada ya hapo mambo  mengine yaliyoendelea tunayajua sisi wenyewe kwani tuliendelea kula rahaaa kwa kwenda mbele yaani full kujiachia!!.
πŸ”πŸ”πŸ”πŸ” MWISHO πŸ”πŸ”πŸ”πŸ”

SHUKRANI KWA WADAU WOTE MLIOISOMA SIMULIZI HII KUANZIA HAPO MWANZO MPAKA LEO INAISHIA #AHSANTENI SΓ€NA, PIA KAMA NILIKUKWAZA MDAU WANGU NAOMBA UNISAMEHE KWA MAPUNGUFU YANGU.
One Love πŸ‡ΉπŸ‡Ώ πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ By A-J πŸ“







USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.