KAMA MAHUSIANO YAKO BADO HAYAJAVUNJA UNGO KAA KIMYA TULIZA MDOMO!
Umeingia kwenye mahusiano, mahusiano bado ni mapya kabisa, yaani hata mahusiano yenyewe hayajavunja uongo ushaanza kutamba kwa mashoga zako. Baby wangu hivi, siwezi kutoka leo Baby anataka kunitoa, Baby kasema nisiwe nafanya hivi, leo baby kanipa hii, Baby hiki Baby kile. Ni kweli mpenzi wako anakufanyia mambo ambayo X wako alikua hakufanyii, uko kwenye ile hatua mpaka unawaza huyu ndiyo mwenyewe, unasisimkwa mpaka unawaza hivi kwanini nilichelewa kumjua!
Hii hasa kwa wadada ndiyo wana hizi mbwembwe, mwanaume akituma meseji kumi tu kwa siku wanachanganyikiwa na kuona ndoa hii hapa! Dada yangu tulia, subiri mahusiano yakomae ndiyo uanze hizo mbwembwe, naomba nikupe sababu mbili tu kwanini uachane na huo utoto;
(1) Huyo mwanaume anaweza kuwa anaigiza; Unamkumbuka X wako, kumbuka miezi mitatu ya kwanza alikujae na wakati mnaachana alikuaje. Basi huyo naye ni hivyo hivyo miezi mitatu mpaka sita ya mwanzo ya mahusiano wanaume wengi huigiza, ila akishakuzoea basi hata SMS ni za shida, kula pamoja, kuoga pamoja na vitu vingine vingine utakuja kusikia tu kwenye ndoto! Kwa maana hiyo acha kuchanganyikiwa, tulia umjue, kama ataendelea hivyo wmaka bsi ni tabia zake ndiyo hata uanze kutamba ila ukishaanza kujishaua hivyo akija kukubadilikia unaona aibu hata kumuacha unavumilia tu kwakua ulishamfanya malaika mbele za watu, tulia dada.
(2) Wanawake hawana muda wa kurafuta mtu mwingine; Wewe kila siku unamsifia mtu wako wakati yeye kila sikua anpigwa matukio, mtu mwenyewe hata hajakupenda vizuri, basi ndiyo mwanzo wa shemeji kuwa shemeji, basi watajipeleka kutaka raha unazopata na katika kufanya hivyo basi watamuambia vitu vyako vingi mpaka utashangaa mshikaji anabdilika unashangaa unaachwa hujui nini kumbe shoga yako anamtaka yeye na asipomtaka kwakua raha zako zinamboa anakuharibia kwa kumueleza madhaifu yako.
Najua umeumizwa muda mrefu, najua sasa hivi unasikia raha kujaliwa hivyo ila dada yangu, nenda kwa stepu, acha kupaniki, acha kuwa kama zuzu kudhani ndibyo alivyo, kula raha zako taratibu, lakini kama unajiona kuwa ukiwa na mashoga zako huwezi maliza siku nzima bila kumtaja mpenzi wako, bila kusimulia kitu ambacho mpenzi wako kakufanyia basi jua unaoa mapenzi yako. Narudia kama mahusiano yenu hata hayajavunja ungo (Mahusiano yanavunja ungo kuanzia miezi sita) lakini kila ukikaa na marafiki zako ni flani hivi flani vile basi unavunja mahusiano yako taratibu, asipokupiga matukio huyo mwanaume hao mashoga zako unawasimulia kana kwamba nawenyew ehawataki watakupiga matukio na huaamini!
No comments: