Simulizi :Beyond Pain Sehemu Ya Nne (4)
Sheila bado alikuwa katika usingizi mzito kutokana na madawa aliyowekewa na mganga, hakuwa akijitambua.Mama msaidizi wa mganga akaingia katika kibanda kile ambacho Sheila alikuwa amelala akamtazama kwa macho makali na kumsogelea ,akamnasa vibao viwili .Sheila akastuka kama mtu aliyekurupushwa usingizini.Akajiangalia na kujikuta akiwa mtupu kabisa.Akaanza kujishangaa kwa hali ile.Akaanza kuhisi hali fulani katika mwili wake ambayo si ya kawaida.Akaupeleka mkono wake sirini na kugundua dalili za kuingiliwa kimwili.Akaanza kujishangaa.Mama msaidizi wa mganga alikuwa amesimama kando yake akimtazama kwa macho makali.Hakuwa amependezwa na kitendo cha mganga kulala na kufanya mapenzi na Sheila.
" Mama nini kimetokea ? mbona niko hivi ? naona kama..kama......" akashindwa kusema Sheila kutokana na wasi wasi.Mama yule msaidizi wa mganga hakumjibu kitu.Akaendelea kumtazama kwa macho makali.
" Mama nini kimetokea?Dawa zimeshafanyika? akauliza sheila bado akiwa na wasi wasi mwingi.
Mama msaidizi hakumjibu kitu akainua mkono wake na kumuonyesha sheila mtungi mkubwa ulioku nje ya kibanda kile.
" Mtungi ule una maji,nenda kaoge haraka" akasema yule mama.Sheila akainuka na kupiga hatua mbili akasimama na kumtazama yule mama.
" Mama mbona sijielewi nini kimenitokea? Mbona sehemu zangu za siri zimeloa maji? Dawa tayari imefanyika? akauliza Sheila.
" Tayari dawa imefanyika" akasema yule mama na kutoka nje ya kile kibanda huku akiongea maneno ambayo Sheila hakuweza kuyafahamu.Taratibu Sheila akauendea ule mtungi mkubwa uliojaa maji akaanza kuoga akiwa amesimamiwa na yule mama.
" Jamani mbona sijielewi? Nini kimenitokea? Mbona naona kama nimeingiliwa kimwili? Ninachokumbuka kabla sijapitiwa na usingizi mganga aliniamuru niiname nijifukize baada ya hapo sikumbuki nini kiliendelea.Nina wasiwasi na yule mganga ameniingilia.Ouh masikini sijui itakuaje kama ni kweli atakuwa ameniingilia kimwili." akawaza Sheila na kuacha kuoga akasimama .Mama msaidizi ambaye alikuwa amesimama kando yake akamuamuru Sheila aendelee kuoga haraka.Sheila akaendelea kuoga akiwa na wasiwasi mwingi.Alipomaliza kuoga akapewa nguo ya kaniki akajifunga na kupelekwa katika jiwe moja kubwa akaamriwa kuketi hapo.Mwili ulikuwa ukimtetemeka kutokana na maji ya baridi aliyoyaoga.
" Emmy mizimu imepokea sadaka yako na imefurahi mno na imekuahidi kuifanya kazi yako kama unavyotaka." akasema mganga baada ya kurejea sehemu alikomuacha Emmy.Alikuwa akihema kwa kasi.Emmy baada ya kuisikia kauli ile ya mganga akatabsamu .
" nashukuru sana mzee kwa msaada wako.Nakuahidi kukuletea zawadi kubwa baada ya mambo yangu kwenda sawa." akasema Emmy.
" Usijali Emmy.Mizimu itapokea kila kitu utakachokitoa kwa moyo kama shukrani kwao.Lakini bado kuna jambo moja ambalo mizimu imenielekeza kulifanya ili kuikamilisha dawa." akasema mganga.
" Niko tayari mganga kwa lolote lile ili mradi mambo yangu yafanikiwe." akasema Emmy.
" Dawa iliyobaki ni ya kukuondoa katika nuksi na mikosi yote iliyokuzunguka.Baada ya hapo nyota yako itakuwa imesafishwa na hutakuwa na mikosi ya namna yoyote tena..Kila utakachofanya kitakuwa ni nuru kwako.Uko tayari kwa ajili ya kumalizia dawa yetu ? akasema mganga .
" Niko tayari mganga" akasema Emmy kwa ujasiri.
Mganga akamshika mkono na kumuongoza hadi nyuma ya jiwe moja kubwa akamuamuru Emmy atoe ile nguo aliyokuwa amejifunga.
" Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.Nimekwisha kula ng'ombe mzima ngoja nimalize na mkia uliobakia." akawaza Emmy wakati akivua ile nguo aliyokuwa amejifunga na kuitupa pembeni.
Mganga akamsogelea na kuanza kumpiga na usinga huku akiongea maneno ambayo Emmy hakuyafahamu.Alikuwa akimzunguka huku akipiga na usinga katika sehemu zote za mwili.Akautupa pembeni usinga na kumshika Emmy kichwani kwa mikono yake akaanza kuongea tena maneno yake ya kiganga.Akaendelea kuzishika sehemu mbali mbali za mwili Aliendelea na zoezi lile huku uume wake ukiwa umesimama wima.Akaukota tena usinga wake na kumchapa nao Emmy kichwani na ghafla Emmy akahisi mabadiliko ,akajikuta akipandwa na ashki baada ya kutomaswa na mganga.Akamkumbatia mganga kwa nguvu.Mganga alikuwa akihema kwa nguvu na hakutaka kuendelea kupoteza muda tena akaanza kufanya mapenzi na Emmy.
Baada ya kumaliza kitendo chake akachukua usinga wake na kumchapa nao Emmy kichwani na ghafla akarejewa na fahamu zake za kawaida akastuka akaona aibu na kuiokota nguo yake haraka haraka akajifunika.
" Dawa imekamilika.Mizimu imekuondolea mkosi wote na sasa uko safi.Ila kumbuka ukishaondoka hapa usiwashe simu yako na wala usiwasiliane na mtu yeyote bali nenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa wazazi wako na hapo ndipo dawa itakapokuwa imekamilika." akasema mganga na kumuamuru Emmy amfuate.
Taratibu kulianza kupambazuka.Kiza kikaanza kutoweka na nuru ikaanza kuchukua nafasi.Watu wakaanza kuamka na kuanza kjiandaa kwa shughuli za siku mpya.Watu walikuwa wengi katika nyumba ya wazazi wa Emmy.Kwa muda mrefu nilikuwa nimekaa na baba mkwe yaani baba yake Emmy katika kona ya nyumba ile tukijadiliana mambo mbali mbali ya kufanya katika ule msiba.Tuliongea mambo mengi kwa kirefu na hususan suala zima la maisha ya Emmy.Kulipoanza kupambazuka tukamaliza maongezi yetu na kujumuika na waombolezaji wengine kuanza maandalizi ya msiba ule. Watu walianza kuwasili na vilio toka kwa akina mama vikaanza kusikika. Kifo cha Baraka kiliwastua watu wengi hasa kutokana na namna kilivyotokea ghafla.Wengi walijiuliza alipo Emmy wakakosa jibu. Ni mimi na Chris pekee katika hadhira ile tuliokuwa tukifahamu kilichokuwa kinaendelea lakini hatukumweleza mtu yeyote yule hadi tutakapopata uhakika.
Saa nane za mchana wakati tukiendelea na shughuli za msiba gari ya Emmy ikawasili .Minon'gono na vilio vikaanza kusikika tena.Watu wakageuza shingo zao ili kumtazama Emmy.Shughuli zilisimama kwa muda .Haraka haraka mlango wa gari ukafunguliwa na Emmy akashuka.Nilikuwa karibu na mahala aliposimamisha gari lake na niliushuhudia uso wake ukiwa na wasi wasi mwingi.Kushuka kwa Sheila kukanifanya niamini kwamba ni kweli walikuwa wamekwenda kwa mganga kama msichana yule niliyemkuta katika nyumba niliyomuachia Emmy alivyonieleza.Nilikabwa na donge kubwa kooni.Nikapandwa na hasira za ghafla.Nilitamani nimvae mzima mzima na kumshushia kipigo na kuanika mambo yake hadharani ili kila mtu afahamu unyama wa mwanamke huyu. Kabla sijafanya lolote ,Emmy akatembea kwa haraka kuelekea ndani lakini baada ya hatua tatu akaanguka chini.Kikaamka kizaazaa hapo msibani.
Emmy alipoteza fahamu.Haraka haraka akainuliwa na kupelekwa chini ya mti mti akalazwa na kuanza kupatiwa huduma.Sheila naye aliangua kilio kikubwa na kuanza kujigala gaza chini akina mama wakamfuata na kumsaidia kumsitiri ,wakamuingiza ndani.Nilikabwa na kitu rohoni kwa kitendo walichokifanya wanawake wale wawili Emmy na mwenzake Sheila.Nilitamani kama ingekuwa ni kwa amri yangu wasingekanyaga pale msibani.Nilimchukia Emmy kupita kiumbe yeyote yule hapa duniani.Nilijilaumu sana kwa kumfahamu na kufunga naye ndoa.Nilifanya kosa kubwa sana ambao sintalisahau katika maisha yangu yote.Emmy amegeuka na kuwama ni mwanamke mwenye roho ya kinyama .Nilishukuru kwa maamuzi ya kuachana naye kwa sababu angeweza hata kunitoa uhai kama ningeendelea kuishi naye.Tayari amejiingiza katika mambo ya kishirikina na mwisho wake utakuwa mbaya sana..
Nilikuwa nimesimama nikiwaza ,nikastuliwa na baba mkwe aliyenishika bega na kuniita pembeni.
“ kama kusingekuwa na umati mkubwa hivi wa watu ,ningemtimua huyu mtoto hapa nyumbani.yaani mwanae anafariki dunia yeye hana habari ,amenisikitisha sana Emmy” akasema baba mkwe ambaye alionyesha kuwa na hasira nyingi.mawazo yake yalikuwa kama yangu.Sikutamani Emmy awepo pale msibani.laiti kama watu wagefahamu alichokifanya huyu mwanamke nina imani wangeweza hata kumkata vipande vipande.Kifo cha ghafla cha baraka kiliwastua na kuwaumuza watu wengi.
“ Baba,nafahamu ni jinsi gani Emmy alivyowakasirisha watu wengi kwa kitendo chake hiki cha kujali starehe kuliko mwanae hadi amefariki dunia akiwa hana habari lakini naomba tuwe na uvumilivu ili tuweze kumaliza shughuli hii kwa amani. Baada ya kumzika Baraka kila mwenye neno la kusema atalisema” Nikamsihi baba mkwe.
“ nakubaliana nawe wayne lakini mambo yote haya ambayo yameanza kumfika emmy ni laana zinazotokana na mambo yake anayoyafanya.Alikufanyia mambo mabaya sana na hata kufikia hatua ya kutudharau sisi wazazi wake .Huu ni mwanzo tu na bado yatamfika makubwa zaidi.Siku moja atakuja kukupigia magoti akiomba umsamehe.Atakuja akitembea kwa magoti akilia akiomba msamaha wako.Mimi kama baba yake mzazi ninakwambia wayne kama ukikubali kurudiana na mtoto huyu kamwe usikanyage ndani ya nyumba hii..” akasema baba mkwe akiwa na hasira kali.
“Baba mimi na Emmy tumekwisha fika mwisho na hatutaweza kuwa na mahusiano ya namna yoyote tena.Nina imani hatathubutu kurudi na kuomba msamaha eti turudiane tena..na kama unavyofahamu baba,kwa sasa tayari niko katika mahusiano mengine,nashukuru Mungu huyu mwanamke niliyenaye kwa sasa ananijali na kunithamini.” Nikasema.
“ nashukuru kama umempata mtu ambaye ameweza kukusahaulisha mateso na machungu yote aliyokusababishia huyu shetani..Mtoto huyu sitamani hata kumuona tena..” akafoka baba mkwe.
Kuzidi kumuongelea mwanamke yule kulinifanya nizidi kuwa na hasira naye.
Ilinibidi nianzishe maongezi mengine ili tuache kuongelea masuala ya Emmy.
Emmy alizinduka na kupelekwa ndani.Alikuwa analia kwa nguvu sana.Akina mama walijaribu kumtuliza na kumtaka awe mvumilivu.Kulia kwake kulisababisha kuwepo na mingong’ono mingi pale msibani.Kila mmoja alionekana kuwa na sura yenye kukasirika kwa kilio kile cha emmy ambacho waliamini kilikuwa ni cha kinafiki.
Ghafla kikatokea tena kizaa zaa kingine mle ndani.Emmy alipandisha mashetani na kuanza kuongea lugha ambayo hakuna aliyeielewa.Alikuwa akiongea maneno mengi .Alionekana kama mtu aliyerukwa na akili.Akina mama walijaribu kumshika na kumzuia kwani tayari alianza kuvua nguo na kuzitupa.Ikazuka tafrani kubwa mle chumbani.Hakutaka mtu yeyote amsogelee.Watu wakaanza kutoka mle chumbani wakikimbia wakiogopa asije akawadhuru.Watu tuliokuwa nje tulistushwa na hali ile na wakati tukijaribu kujua nini kilichokuwa kinaendelea ndani mara Emmy akatoka mbio mle ndani na kusababisha watu waanze kukimbizana hovyo ili kumkwepa .Aliangaza angaza pale nje na mara akaanza kuja mahala tulipokuwa tumesimama.Wote tulibaki tunashangaa.
“ Leo utanirudishia mwanangu…..!! Nasema leo lazima umrudishe mwanangu !!..kwa nini umemuua mwanangu? Alikuwa akiyasema maneno haya kwa sauti kubwa huku akikimbia kwa kasi kuja mahala tulipokuwa tumesimama.Tulijiandaa ili tumzuie lakini ghafla akanirukia kwa nguvu zake zote na kuniangusha chini kisha akanikaba kooni.Nilimuangalia usoni ,macho yake yalionyesha kwamba hakuwa akitania kwa kile alichokusudia kukifanya.
“ leo nakuua wayne..namtaka mwanangu..! nirudishie mwanangu.!! Akasema Emmy huku akinikaba kooni.Nilipandwa na hasira za ghafla,nikakusanya nguvu zote nilizokuwa nazo na kumsukuma Emmy pembeni akaanguka .Nilipotaka kuinuka akaniwahi na kutaka kuniangusha tena chini lakini safari hii niliwahi nikamshika fulana yake aliyokuwa ameivaa nikamnasa kofi zito lililompelekea mpaka chini.Aligala gala pale chini akilia.Nikamuendea tena nikamuinua na kumpiga tena kofi lingine zito akaanguka chini.
Pamoja na makofi yale mazito bado emmy aliendelea kutaka kupambana na mimi.Alikuwa anaongea maneno katika lugha ambayo sikuifahamu.Aliokota jiwe kubwa akalirusha kwa nguvu .Almanusura jiwe lile linipate.Nilipandwa na hasira zisizomithilika kwa kukoswa na jiwe lile kubwa ambalo kama lingenipata ingekuwa ni habari nyingine tena.Pengine kungekuwa na msiba wa pili. Sikuwahi kumpiga Emmy hata maramoja ,huu ulikuwa ni wakati muafaka wa kumfundisha adabu.Nilimvaa na kuanza kumshushia kipigo kikali.Ndani ya dakika kadhaa Emmy hakuwa akijitambua kwa kipigo kikali nilichompa
Wakati namshushia Emmy kipigo kile kikali,baadhi ya watu walionekana kukubaliana na kukifurahia kitendo kile na baadhi ya akina mama wakishabikia nimuadhibu zaidi.Wengi wamezisikia taarifa za mwanamke huyu na mambo yote aliyonifanyia.Namshukuru Chris kwani yeye ndiye aliyenishika kwa nguvu nisiendelee kumpa Emmy kipigo zaidi.Emmy alikuwa ametakapaa damu.Akachukuliwa na akina mama wakampeleka ndani na mimi nikachukuliwa na kupelekwa nje ya nyumba.
" Wayne tafadhali naomba ujaribu kudhibiti hasira zako.Wote tuliopo hapa tumeumizwa na kifo cha Baraka na kitendo alichokifanya mama yake na kama wote tukishindwa kuzizuia hasira zetu nina imani hapatakuwa na amani eneo hili.Tujitahidi ili tumalize suala hili kwa amani halafu masuala mengine yatafuata " Chris akanishauri.Sikumjibu kitu nilikuwa bado nina hasira sana.Nilimshukuru Chris kwani bila ya yeye ningeweza kusababisha madhara makubwa kutokana na hasira nilizokuwa nazo..
Tukiwa nyuma ya nyumba ,Emmy aliingizwa garini na kukimbizwa hospitali.Alikuwa anatokwa na damu nyingi puani kutokana na kipigo nilichompatia.Sikuona uchungu wala kustuka kwa namna yoyote ile.Wakati bado mjadala unaendelea kuhusiana na kilichotokea muda mfupi uliopita simu yangu ikaita.Nikaitoa mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa ni Clara.Nikajitenga na wenzangu na kuipokea simu
" Hallo Clara" nikasema
" Pole sana Wayne..Hajakuumiza yule mwanamke? akauliza Clara
" hapana hajaniumiza.Niliwahi kumdhibiti"
" Pole Wayne..Naomba uwe makini sana na mwanamke huyu kwani anaonekana ni kama amechanganyikiwa .halafu jitahidi usiwe na hasira naye kwani unaweza ukasababisha masuala mengine tena Vile vile si vizuri kupigana hasa katika hadhira kama hii" akasema Clara.
" Nimekuelewa Clara ,lakini halikuwa lengo langu kumpiga.Ni yeye ndiye aliyenilazimisha nikafanya vile." nikasema
" Anaonekana ameumia sana.Wamemkimbiza hospitali.Wayne nimeanza kuogopa asije akanidhuru hata mimi mara atakaporudi.Inaonekana amepania kufanya vurugu "
" usijali Clara.hawezi kukufanyia jambo lolote lile.Nimekwisha choka naye na iwapo atajaribu kukufanyia kitu chochote kile,ninaapa nitamtoa roho .."
Shughuli ziliendelea kama kawaida hapo msibani.maandalizi ya mazishi yalikamilika.Ndugu wa kutoka mikoani waliendelea kuwasili.Siku iliyofuata ilipangwa tumzike Baraka.
Jioni baba mkwe akaniita pembeni kwa maongezi.
" Wayne pole sana kwa matatizo yaliyotokea mchana.Ninakupongeza ulifanya kazi nzuri sana.Ulimfundisha adabu.Nilitaka watu wakuache kwanza ili umfundishe adabu shetani yule.Nina imani kwa kipigo ulichompa tayari amekuwa na adabu" akasema baba mkwe akiwa na chupa ndogo ya konyagi mkononi.
"Nashukuru hakuweza kusababisha madhara kwa sababu alidhamiria kunidhuru" nikasema.Baba mke akaifungua ile chupa ya konyagi akanywa kidogo.
" Kwa nyakati kama hizi huwa ninapenda kutumia kinywaji hiki ili niweze kupunguza mawazo niliyonayo" akasema baba mkwe.Sikumjibu kitu.
" Wayne nimekuita hapa ili tuweze kujadili suala moja la muhimu sana.Kesho ni siku ya mazishi lakini tumekwisha fahamu baba halisi wa baraka ni nani? akauliza baba mkwe.Nilitafakari kidogo na kusema
" Suala hili ni gumu kwetu sisi na anayeweza kutoa jibu la swali hili ni emmy peke yake.yeye ndiye anayemfahamu baba halisi wa Baraka ni nani.Awali nilidhani ni mimi ,kumbe si mimi,akasema ni Chris, lakini kumbe si Chris sasa hatujui baba wa baraka ni nani..Hii ni siri yake mwenywe." nikasema
" Dah ! Sikutegemea kama Emmy angebadilika na kuwa namna hii..Sikutegemea kabisa.Litakuwa jambo la busara kama tutamzika mtoto bila kumfahamu baba yake? akauliza baba mkwe.
" iwapo kutakuwa na ulazima ,itatubidi tufanye hivyo.Sina hakika kama Emmy yuko tayari kumuweka wazi baba wa Baraka kwa sasa.Inavyoonekana hata yeye mwenyewe hamjui ni nani" nikasema
" kama ni hivyo inawezekana ikawa ni tabia yake kutembea nje ya ndoa.Inaonekana ametembea na wanaume wengi sana kiasi cha kutofahamu hata baba wa mtoto wake ni nani.Dah ! mkosi gani huu nimeupata mimi" akasema baba mkwe huku akishika kichwa chake.
" Baba lisikuumize kichwa suala hili.Mimi nitasimama kama baba wa Baraka.Amezaliwa mikononi mwangu,nimemlea na kumtunza kama mwanangu .Hata baada ya kubainika kwamba hakuwa mwanangu wa damu bado nimeendelea kumpenda na kumuhesabu kama mwanangu.Nitasimama kama baba yake." nikasema.
" Nashukuru sana wayne kwa maamuzi hayo.Suala hili lilikuwa linaniumiza kichwa sana .sikujua ingekuwaje." akasema baba mkwe.Tuliongea mambo mengi na wakati tukiongea Clara akanipigia simu akaniomba nimpeleke hotelini ili akabadili nguo pamoja na kuoga.Tuliondoka msibani tukaelekea hotelini.
" Wayne mbona uko kimya sana leo? Unamuwaza Emmy? akauliza Clara baada ya ukimya kutawala garini.
" Hapana mpenzi wangu.Siwezi hata dakika moja kumuwaza yule shetani ." nikasema
" Pole sana.Hakuwahi kukuumiza yule mwanamke?
" Niliwahi kumdhibiti.Kama nisingewahi alikuwa na dhamira ya kunidhuru." nikasema huku nikiwa makini kwenye usukani.
" Niliogopa sana pale alipoanza kuongea maneno kama mtu aliyerukwa na akili.Alikuwa ni kama mtu aliyepandisha mashetani.Alikuwa analia na kupiga kelele akidai wamrudhishe mwanae.Alikuwa anakutaja wewe kwamba umrudishie mwanae." akasema Clara.
" Haya yote ni malipo kwa mambo yote ya kikatili anayoyafanya.Inasikitisha sana Baraka amefariki bila kumfahamu baba yake ni nani.Kesho itanibidi nisimame kama baba wa baraka wakati wa mazishi kwa sababu amezaliwa mikononi mwangu na nimemlea mimi hadi hapa alipofika." nikasema
" Hilo ni jambo la msingi sana Wayne kwa sababu hata mimi nilikuwa najiuliza itakuaje kuhusu baba yake Baraka? akasema Clara.
" Mimi ndiyo baba yake anayenitambua hadi alipofariki." nikasema.
"Wayne nimeanza kuwa na wasi wasi sana hata kukaa msibani kwa sababu ninaogopa Emmy anaweza akanifanyia kitu kibaya.Anaweza akaamua hata kuniaibisha.Ninahisi anaweza kuwa na matatizo ya akili" akasema Clara.
" Usijali Clara.Hataweza kukufanyia chochote kile.Iwapo atathubutu kukugusa atakiona cha moto.Kuwa na amani kabisa mpenzi wangu."
" wayne kuna kitu nakifikira pia.Nafahamu jinsi ulivyoumia moyoni kwa kifo cha Baraka Unaonaje kama baada ya mazishi tuondoke na twende mahala tukapumzike kwanza halafu tutarejea.Hii itakusaidia hata wewe mwenyewe kupunguza machungu ya kufiwa na Baraka." akasema Clara wakati tunarejea msibani.
" Hilo ni wazo zuri sana Clara.Kwa kweli ninahitaji kuipumzisha akili yangu baada ya mambo yaliyotokea." nikasema.Sikuhitaji maongezi mengi kwa usiku huu na Clara akalitambua hilo.
Tulirejea tena msibani kwa ajili ya kulala hapo kwa siku ya pili.
" Wayne,ulifanya vizuri sana kumpa kipigo Emmy" Chris aliniambia baada ya kuniita pembeni akidai ana maongezi na mimi.Sikumjibu kitu .
" Emmy anastahili kipigo kile.Ni mwanamke mshenzi sana huyu.Ninamchukia sana Emmy alisababisha nikafanya mambo mabaya sana ambayo yananipa machungu mengi kila nikifikiria.Emmy alisababisha nikakosana nawe ...." akasema Chris lakini kabla hajaendela mbele zaidi nikawahi kumzuia
" Chris tafadhali naomba tusiyaongelee mambo hayo kwa sasa..Tumejikuta tukiongea tena kwa sababu ya msiba wa Baraka na kama isingekuwa ni msiba huu mimi na wewe tusingeongea kamwe..Naomba tufanye mambo yanayohusiana na msiba halafu baada ya hapo tutaangalia kama kuna chochote tunachoweza kuongea mimi na wewe." nikasema kisha nikaondoka na kwenda kujiunga na kundi la watu waliokuwa wanacheza karata.Chris bado alibaki amesimama mahala nilipomuacha.Ni wazi alihitaji kuongea nami.Alihitaji kuzimaliza tofauti zetu zilizojitokeza lakini sikuwa tayari kwa sasa.Alnifanyia kitendo kibaya sana na si rahisi kukisahau kwa haraka namna hii.
Nikiwa pale katika lile kundi la watu waliokuwa wakicheza karata huku wakiendeleza utani mwingi wa makabila kama ilivyo kawaida katika misiba,mara nikavutwa shati, nikageuka na kukutana na baba mkwe.Akanivuta pembeni tukaenda kukaa katika viti na kuanza kuongea.
" Wayne , nimemuona yule baradhuli Chris.Toka usiku wa jana yuko hapa..Mmekwisha elewana? Nilitamani nimtimue kabisa asionekane hapa kwangu lakini nimeogopa kufanya hivyo ili kumlindia heshima japokuwa yeye hakuijali heshima yako wakati anaanzisha mahusiano na Emmy" akasema baba mkwe akionyesha kukerwa na kitendo cha Chris kuonekana pale msibani.
" Baba mimi na Chris haujaelewana na sina hakika kama hilo linaweza kutokea.Kilichopelekea awepo hapa nilimpigia simu jana ili nimuulize kama anaweza akafahamu mahala tunakoweza kumpata Emmy.Nilimfahamisha kwamba Baraka amefariki ghafla ,akastuka na akaja kuungana nasi katika kumtafuta Emmy.Hata mimi sijisikii vizuri ninapokuwa karibu na mtu ambaye aliwahi kutembea na mke wangu wa ndoa.Ninajilazimisha kufanya hivyo ili tuweze kumaliza salama shughuli hizi za msiba.Katika sehemu kama hizi tofauti zote huwa zinawekwa kando.Lakini suala la kumsamehe silifikirii kwa sasa.Alinifanyia kitendo kibaya sana" nikasema huku nikitazama mahala alikokuwa amekaa Chris akiwa na baadhi ya waombolezaji Kila ninapomtazama kuna kitu kilikuwa kinanikaa rohoni na kunifanya nizidi kuwa na hasira naye.
" Nakubalina nawe Wayne,tuziweke tofauti zetu pembeni ili tumalize suala hili kwa amani japokuwa sina amani kila nikimuona hapa kwangu nadhani hata yeye amelitambua hilo na ndiyo maana anajificha sana ili asionane na mimi. Tuachane na hayo..Huyu laana Emmy alikuwa wapi muda wote tuliokuwa tunamtafuta ? Kwa kweli Emmy amenitia aibu kubwa.Kila mtu hapa mtaani anamuongelea yeye." akasema baba mkwe.Nilitamani nimweleze ukweli lakini nikaona tutaamsha mambo mengine nikaamua kuachana na suala hilo .
" Baba,Emmy unamfahamu vizuri ni mwanamke anayependa sana starehe.Nina hakika alikuwa katika starehe zake na ndiyo maana hakuwa na taarifa juu ya kilichotokea kuhusu mwanae.Inasikitisha sana" nikasema
" Wayne usinione nimekaa kimya,lakini moyoni nimeumia sana kwa matendo ya huyu mtoto.Ninajuta hata kwa nini alizaliwa na mimi." akalalamika baba mkwe.
" Baba ,unapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.yeye ndiye anayetupa watoto kwa hiyo hata Emmy kuzaliwa na wewe ilikuwa ni kwa mapenzi yake.Kitu kikubwa tunachotakiwa kukifanya ni kumuombea sana ili aweze kubadilika.Tunatakiwa kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuombea .." nikasema na kumfanya baba mkwe acheke.
" Kamwe sintathubutu kushinda na njaa kwa sababu ya laana kama Emmy. Kama ameshindwa kutusikiliza sisi wazazi wake ulimwengu ndio akaomfunza adabu.Siku zote asiyefunzwa na wazazi atafunzwa na ulimwengu." akasema baba mkwe na kunifanya na mimi kucheka.Kikapita kimya kidogo baba mkwe akauliza.
“ Wayne yule msichana uliyekuwa naye ndiye mwanangu mpya uliyempata?
" Ndiyo baba..Anaitwa Clara.Anajishughulisha na ubunifu wa mitindo na kwa sasa makazi yake ni nchini Afrika ya kusini.Nimekutana naye siku kadhaa zilizopita akiwa katika harakati zake za kutoa semina kwa wanamitindo.Tumetokea kuwa marafiki na kwa muda huu mfupi tuliokuwa pamoja amenifanya niyasahau yale machungu yote niliyofanyiwa na Emmy. Utanisamehe baba kwa kuyasema haya mbele yako" nikasema.Baba mkwe akatabasamu na kusemahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Wayne huna haja ya kuogopa.Wewe ni kijana wangu na ninakupenda sana na siku zote ninakutakia mema.Nimeyashuhudia kwa macho yangu mambo aliyokufanyia mwanangu Emmy. Sikuhadithiwa na mtu yeyote.Kwa kuwa siku zote ninapenda uishi katika maisha mazuri yenye amani na furaha,ninakuunga mkono kabisa kama huyo mama uliyempata sasa hivi unaona anaweza kukufaa na siyo huyu shetani Emmy.Mimi nakuombea tu uwe na maisha mazuri yenye furaha ila nakuomba usije ukathubutu kurudiana tena na Emmy.Atakufanyia kitu kibaya sana.Umeona kitendo alichokifanya mchana wa leo.Kama usingekuwa hodari ukakwepa lile jiwe alilolirusha sasa hivi tungekuwa tunaongea mambo mengine tena.Kwa hiyo jitahidi sana kumuepuka ,kaa naye mbali kabisa.Muache atange na dunia na itakapomfunza atarudi kuomba msamaha na kugundua kwamba amekwisha chelewa kwani mlango umekwisha fungwa." akasema baba mkwe.Ninachompendea baba mkwe siku zote amekuwa upande wangu na amekuwa akishirikiana na mimi katika kila jambo.
*************
Wakiwa katika sofa lililokuwapo mapokezi, akina mama waliompeleka Emmy kutibiwa katika zahanati ya Samaria inayomilikiwa na masista wa kanisa katoliki ,walistuliwa na muuguzi ambaye alitumwa na Emmy amuite mtu anayeitwa Sheila ana maongezi naye.Japokuwa akina mama wale walitaka sana kuingia na kumuona Emmy anaendeleaje lakini muuguzi yule alikataa kata kata kwa madai kwamba mgonjwa hakuhitaji kuonana na mtu yeyote yule kwa wakati ule zaidi ya Sheila pekee. Akiwa ameongozana na muuguzi,Sheila akaingia katika chumba alichokuwa amepumzishwa Emmy aliyekuwa amefungwa plasta kadhaa usoni kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kipigo.
" Emmy pole sana..Unajisikiaje sasa ? akasema Sheila akikaa kitandani
" Naendelea vizuri ..Ibilisi yule Wayne alitaka kuniua,lakini nitapambana naye..Atanitambua mimi ni nani" akasema Emmy kwa sauti ya chini. Muuguzi yule akatoka nje na kuwaacha Emmy na Sheila pekee mle chumbani.Emmy ambaye alikuwa ametundikiwa chupa ya maji akamuomba Sheila amsogelee karibu zaidi.Alipomtazama katika macho yake alikuwa anatoa machozi.
" Emmy nyamaza kulia mpenzi.Jipe moyo haya ni mambo ya kawaida na yatakwisha." akasema Sheila akijaribu kumtia moyo Emmy.
" Sheila nimemuua mwanangu" akasema emmy kwa sauti ya chini.
" Unasemaje Emmy? Mbona sikuelewi? akauliza Sheila.Emmy akakohoa kidogo akarekebisha koo lake na kusema
" Sheila nimemuua mwanangu Baraka." akasema tena Emmy na kumfanya Sheila astuke,kumuangalia kwa macho ya mshangao.
" Sikuelewi unasema nini Emmy?" akauliza tena Sheila.
" Naomba unisaidie kuniinua niweze kukaa" akaomba Emmy na Sheila akamsaidia kumuinua,akakaa kitandani.
" Sheila tukiwa pale kwa mganga,aliniambia kwamba ili kunifanyia kazi yangu mizimu inahitaji sadaka.Akaniuliza kama nipo tayari kuitoa sadaka ile kwa mizimu ili inifanyie kazi yangu nikakubali na akanipa kisu nikichome katika beseni la maji .Baada ya kukichoma kisu kile katika lile beseni la maji nilisikia sauti kama ya mtu ninayemfahamu akilia na baada ya muda mfupi sauti ile ikapotea kabisa.Kumbe alikuwa ni mwanangu Baraka.Nilipokichoma kile kisu katika beseni nilikuwa namuua mwanangu bila kujua.Ouh Sheila nitafanya nini mimi? Emmy akashindwa kujizuia akaanza kulia.
" Nyamaza usilie Emmy.Usiongee kwa nguvu watu watakusikia na yatakuwa mambo mengine tena.Sasa ikawaje shoga yangu Emmy ukakubali kutoa sadaka bila kuuliza ni sadaka gani unayotakiwa kuitoa?
"Hata sielewi ilikuwaje Sheila.Nadhani nilikuwa nimepumbazwa na dawa za yule mganga.Mshenzi sana yule mganga ameniulia mwanangu na akadiriki hata kufanya mapenzi na mimi tena bila hata kutumia kinga.Ouh Mungu wangu kwa nini nilikubali kirahisi rahisi namna ile kila alichokuwa akiniambia? Halafu alifahamu kabisa kwamba tayari mwanangu amekwisha fariki ndiyo maana akaniambia kwamba nitakaporudi nisipite sehemu yoyote ile na breki ya kwanza niifunge nyumbani kwetu.Alinihakikishia kwamba Wayne lazima atarudi kwangu lakini kwa hali niliyoiona leo sina hakika kama hilo litawezekana." akasema Emmy kwa uchungu huku akilia.Sheila akamfuta machozi.
" Emmy unasema ulifanya mapenzi na yule mganga? akauliza Sheila.
" Ndiyo ! Kwani vipi?
" Mshenzi sana yule babu..Hata mimi alinilewesha dawa zake halafu akaniingilia. Kumbe alitufanyia mchezo huu wote.." akafoka Sheila na kumfanya Emmy azidi kudondosha machozi.
" Basi usilie shoga yangu.Yameshatokea na hatuna tena namna nyingine ya kufanya." akasema kwa unyonge Sheila.
" Sheila naomba ufanye kila utakavyoweza ili uweze kunitoa hapa hospitali na unipeleke kwa yule mganga usiku huu anirudishie mwanangu.Nataka amrudishe mwanangu Baraka" akasema Emmy.
" Emmy hilo ni suala lisilowezekana hata kidogo.Sahau suala la kumrudisha Baraka.Tayari ameshafariki na hawezi kurudi tena "
" Baraka hajafa Sheila.Nakuomba Sheila nipeleke kwa mganga usiku huu kabla mwanangu hajazikwa kesho.Najua anao uwezo wa kumrudisha.Na kama akishindwa kumrudisha mwanangu nitamuua" akasema Emmy.Aliongea kama mtu aliyechanganyikiwa.Sheila akajitahidi kumtuliza lakini bado Emmy akaendelea kupiga kelele akimuomba Sheila amtoe pale hospitalina kumpeleka kwa mganga.Sheila alipoona mambo yamekuwa magumu akakimbia kwenda kuwaita wauguzi ambao walikuja haraka na kumdhibiti Emmy kisha wakamchoma sindano ya usingizi na baada ya muda akalala usngizi.
" Masikini Emmy amemuua mwanae kwa ujinga wake mwenyewe.Inaniuma sana kwa kitendo hiki alichokifanya.Anahangaika kumtafuta mchawi wakati mchawi ni yeye mwenyewe.Yeye ndiye aliyeiroga ndoa yake.Ameshindwa kumlea mume wake na badla yake kumfanyia vitimbi kila kukicha halafu leo hii anataka kumtafuta mchawi anayeiroga ndoa yake.Amenisababishia hata mimi matatizo.Amenipeleka kwa yule babu mshenzi amenipumbaza kwa dawa zake na kufanya mapenzi na mimi.Sijui nitaoga na sabuni gani ili niweze kuiondoa shombo ya yule mganga mwilini mwangu.Emmy ameniingiza katika matatizo makubwa sana.Sikutegemea kabisa kama mimi Sheila ningekuja kulala na kibabu kama yule mchawi mkubwa. Najuta kuambatana na Emmy.Sitaki urafiki naye tena.Baada ya msiba huu wa mwanae kumalizika sitaki tena urafiki wala ukaribu naye.Ni msichana mbaya na anaweza akakupeleka pabaya.Itakuaje kama yule babu akawa ameniambukiza virusi vya ukimwi? Mungu nisaidie hilo lisinitokee." akawaza Sheila akiwa amesimama chini ya mti huku machozi yakimchuruzika.
Hatimaye kulipambazuka na shughuli zikaanza kwa kasi.Siku hii ilikuwa ni siku ya mazishi ya Baraka hivyo toka asubuhi kulikuwa na pilika pilika nyiingi.Kijua kilipoanza kuchomoza nilimpeleka Clara hotelini kwa lengo la kuoga na kubadili nguo.
" Emmy hakurudi jana ,inasemekana aliongezewa damu kwani alipoteza damu nyingi kwa kipigo ulichompa" akasema Clara tukiwa garini kuelekea hotelini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Ingekuwa vizuri kama angekufa kabisa.Sitaki hata kumuona katika macho yangu yule mwanamke" Nikasema .
“ Usiseme hivyo wayne.Kama ungemuua, ungekumbana na mkono wa sheria na mimi ndiye ningeumia zaidi .Sikatai kwamba Emmy amekufanyia mambo mengi na yasiyovumilika na ninakubali kwamba anastahili adhabu,lakini next time kabla hujafanya maamuzi yoyote yale,try to think about me also.” akasema Clara.
“ Nimekuelewa Clara.Wewe ni mtu mwenye thamani kubwa sana na siku zote nitakupa kipaumbele kwa kila jambo ninalolifanya” nikasema.
“ Wayne tayari nimekwisha pata tiketi za ndege kama nilivyokuwa nimekueleza kwamba baada ya mazishi ya Baraka itatubidi tuondoke Arusha na kwenda kupumzika mbali katika sehemu tulivu ili tutulize akili.Mambo mengi yametokea kwa muda mfupi sana “ akasema Clara.
“ Ouh safi sana mpenzi wangu.Umemtuma nani ashughulikie tiketi hizo? nikauliza na kumfanya Clara acheke
“ C’mon sweetie,siku hizi mambo yote yanafanyika kielektroniki..” akasema Clara huku akicheka na mimi nikacheka kidogo.
“ Umepanga twende tukapumzike wapi? nikauliza
“ Its just a suprise Wayne..Utaona wewe mwenyewe.Nina hakika utapapenda sana.” akasema Clara huku akitabasamu
Tulifika hotelini nikajitupa sofani wakati Clara akioga.Nikapitiwa na usingizi.Ni Clara ndiye aliyenistua toka katika usingizi mzito pale sofani..
“ Baba mkwe anapiga simu” akasema Clara akiwa ameishika simu yangu mkononi.
“ Hallo baba” nikasema
“ Wayne uko wapi? akauliza baba mkwe
“ Nimekuja huku hotelini mara moja kuoga na kubadili nguo”
“ Sawa Wayne usichelewe sana kwani shughuli nzima ya hapa inakutegemea wewe.Bado tuna mambo mengi ya kushughulia asubuhi hii halafu tuelekee hospitali tukauchukue mwili na kuuleta hapa nyumbani”
“ Sawa baba ninakuja si muda mrefu.”
Niliingia bafuni nikajimwagia maji,nikabadili nguo na tukaondoka kurejea msibani.Mida hiyo ilipata saa tatu za asubuhi.Tulifika msibani nikaegesha gari nikashuka na kumfungulia mlango Clara.Wakati Clara akishuka gari ya Emmy ikaingia na kuegesha karibu kabisa na lilipo gari letu.Mlango ukafunguliwa na akashuka Emmy akiwa na majeraha kadhaa usoni yaliyotokana na kipigo nilichompa jana. Akina mama wakamsaidia kushuka garini na ghafla akageuza shingo na kukutanisha macho na Clara.Akamuangalia kwa macho ya chuki.Safari hii niliapa kumfanyia kitu kibaya sana endapo angethubutu kumgusa Clara au hata kumtolea neno lolote la kumtusi.
“ Usiwe na hofu Clara,hataweza kukufanyia kitu chochote.Safari hii sintamvumilia kwa kitu chochote kile.Nitampa kipigo kikali kuzidi nilichompa jana . Kuwa na amani “ nikamwambia Clara.
“ wayne tafadhali mpenzi wangu nakuomba usipigane tena na huyu mwanamke. Kupigana si kitendo cha kistaarabu hata kidogo na hasa katika sehemu kama hii yenye kadamnasi ya watu.Usimpige tena Emmy tafadhali.Endapo atanikosea heshima au kunitolea lugha yoyote ile ya matusi na kashfa,leave it to me.I’ll handle it my way “ akasema Clara akiwa ameuweka mkono mmoja begani kwangu.Clara alikuwa ni mwanamke mwenye roho ya ajabu sana.pamoja na vituko vyote vya emmy lakini bado aliendelea kumuonea huruma.
“ Nimekuelewa Clara.hata mimi sipendi kugombana mbele za watu,lakini jana ni yeye ndiye alinisababisha nikapoteza ustaarabu wangu na kuamua kupigana naye.Hata ungekuwa ni wewe usingeweza kuvumilia.” Nikasema
“ hayo yameshapita mpenzi wangu,naomba tuyasahau na tuelekeze macho yetu katika shughuli ya leo.” Akasema Clara.
“ Clara juzi usiku wakati tukiwa na Chris tunamtafuta Emmy,ulinipigia simu na kuniambia kwamba kuna maneno umesikia yanaongelewa na ungenieleza mara tutakaporudi.Kutokana na kuwa na shughuli nyingi nimeshindwa hata kukuuliza ni maneno gani yalikuwa yanaongelewa?
Clara akasita kujibu akaniangalia usoni.
“ Ouh never mind Wayne..Its nothing” akasema huku akitabasamu
“ Niambie Clara,ni maneno gani ambayo yalikuwa yanaongelewa? Niliisikia sauti yako wakati ule ulikuwa na wasi wasi sana”
“ wayne si masuala ya msingi sana.Mimi nimekwisha yapuuzia” akajibu
“ Naomba uniambie Clara na mimi niyasikie hayo yaliyokuwa yanaongelewa.” Nikasisitiza
Clara akaniangalia usoni na kusema
“ Kuna maneno niliwasikia akina mama wakiyaongea .Nilikuwa nimekaa nao karibu na hawakujua kama mimi na wewe tuna mahusiano.Walikuwa wanasema…” Clara akasita kuendelea.
“ walikuwa wanasemaje Clara? Nikauliza
“ walikuwa wanasema eti wewe ndiye uliyemuua Baraka baada ya kupatwa na hasira kwamba si mwanao wa damu..”
Kwa sekunde kadhaa nilibaki nikimuangalia Clara ambaye naye alikuwa akinitazama.Nikatabasamu na kumuuliza
“ Do you believe them?
“ Ofcourse not..Mimi nimekuwa nawe kwa muda huu wote wa matatizo ya Emmy.Ninalifahamu sakata zima jinsi lilivyo na ninakuamini huwezi ukafanya vitu kama hivyo.Ninafahamu ni jinsi gani ulivyompenda Baraka .” akasema Clara.Nikatabasamu
“ Nashukuru kwa kunielewa na kuniamini” nikasema huku nikifunga mlango wa gari..Clara akaelekea ndani kuungana na akina mama wenzake.Maneno yale aliyoyasema Clara yalinipa hasira japokuwa sikutaka kuonyesha wazi wazi.Nilimpenda sana Baraka na kamwe nisingeweza kufanya kitendo kama kile kama wale akina mama walivyokuwa wakifikiri.Nashukuru Clara aliyapuuza maneno yale kwani ni yeye pekee niliyekuwa nikimuhofia asije akaumizwa na maneo yale yasiyokuwa na ukweli wowote.
Maandalizi ya msiba yaliendelea vizuri.watu walikuwa ni wengi sana .Baada ya kila kitu kuwekwa sawa tukaanza safari ya kuelekea hospitali kuu ya mkoa kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Baraka na kuuleta nyumbani kwa heshima za mwisho kwa waombolezaji. Bado picha ya Baraka ilikuwa inanijia kichwani mwangu.Sikuamini kama ni kweli Baraka ambaye nilimzoea na kumpenda sana muda mchache ujao tutamfukia ardhini na sintamuaoa tena maishani.Kuna nyakati nilikuwa nadondosha machozi .Nilikuwa na uchungu mwingi sana.Kadiri tulivyokuwa tunaikaribia hospitali ya Mount Meru ndivyo hofu yangu ilivyokuwa ikizidi.
Tulikamilisha taratibu zinazotakiwa kabla ya kuchukua maiti kisha tukakabidhiwa mwili wa Baraka.Alikuwa amelala ndani ya jeneza amefumba macho kana kwamaba amelala usingizi.Alivaa suti yake nyeusi aliyokuwa anaipenda sana.Nilishindwa kujizuia kuangusha machozi.Katika maisha yangu sijawahi kuumia moyo wangu kama siku hii.Msiba usikie kwa mwenzako usiombe ukupate wewe. Watu mbali mbali walinifariji na kuniomba nijikaze japo kuwa inauma.Nikanyamaza.Sikutaka jeneza lile lifungwe.Nilitamani niendelee kumuangalia Baraka pengine angeweza kuamka.
“ Kwa heri baraka..Sikutegemea kama ungeondoka mapema namna hii. Nilikupenda na nitaendelea kukupenda hadi mwisho wa uhai wangu..” nikasema nikiwa nimeuweka mkono wangu katika paji la uso wa Baraka.Watu walinionea huruma sana.Imezoeleka kwamba wanaume ni watu majasiri na ni nadra kuangusha machozi msibani.Usemi huu uliwekwa kando kwa siku ya leo na karibu kila mtu aliyekuwapo hapa aliangusha chozi japokuwa kila mtu kwa namna yake.Ilikuwa ni simanzi kubwa.Baba mkwe akanisogelea akaninong’oneza kwamba muda unakwenda hivyo wanahitaji kuwapa nafasi watu wengine waliofika pale hospitali kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa baraka.Niliuvua mkufu wangu wa dhahabu nikamvisha Baraka.Nakumbuka ni baraka ndiye aliyenichagulia mkufu huu mzuri siku moja tulipokwenda kufanya manunuzi ya mavazi.
Baada ya watu waliokuwepo pale hospitali kumaliza kutoa heshima zao za mwisho kwa miwli wa Baraka tukaanza safari ya kurejea nyumbani.Ulikuwa ni msafara mkubwa wa magari.Kifo cha Baraka kiliwaumiza wengi.Mara tulipowasili nyumbani vikaamka vilio vikubwa toka kwa akina mama.Baadhi yao walianguka na kupoteza fahamu baada ya kuliona jeneza lenye mwili wa baraka likiingia ndani. Jeneza liliwekwa katika jukwaa maalum na bila kupoteza muda shughuli ya kutoa heshima za mwisho ikaanza.Ulikuwa ni msururu mrefu wa watu ambao ulipeleka zoezi lile kuchukua muda mrefu.Saa tisa alasiri tukaelekea kanisani kwa ajili ya ibada.Pale kanisani likafanyika pia zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa wale ambao hawakuwa wamefanya hivyo.Niliinuka na kwenda kumtazama Baraka kwa mara ya mwisho.Sikutegemea kumuona tena katika maisha yangu.
“ Kwa heri mwanajeshi wangu “ hilo ndilo neno pekee nililosema kumuaga Baraka.Jeneza likafungwa na ibada ikaanza.Baada ya ibada kumalizika ukaanza msafara wa kuelekea makaburini Njiro.Hiki kilikuwa ni kipindi kigumu mno.Tulifika makaburini , ikafanyika ibada ndogo ya mazishi halafu jeneza likashushwa kaburini.Emmy alianguka na kupoteza fahamu wakati jene za linashushwa kaburini akatolewa na kupekewa pembeni kwa ajili ya msaada.Baraka akazikwa bila ya mama yake kushuhudia.Miguu yangu iliishiwa nguvu lakini nikajikaza kiume.Japokuwa bado nilikuwa na hasira naye lakini namshukuru Chris ambaye alikuwa nami kwa muda wote kunipa moyo na kunitegemeza pale nilipoishiwa kabisa na nguvu.Babu na bibi yake Baraka ndio waliokuwa wa kwanza kutupia udongo katika kaburi.baada ya hapo nikafuata mimi kama baba yake.mama yake hakuwepo alikuwa poteza fahamu hivyo wakaendelea kuweka udongo watu wengine na baada ya zoezi lile kukamilika Kaburi likaanza kufukiwa.
Ndani ya muda mfupi tayari kaburi lilikwisha fukiwa.Baraka alikuwa amezikwa tayari na nisingemuona tena maishani.Ni Mungu pekee awezaye kuyafahamu machungu niliyokuwa nayo siku ile. Kisha fukiwa likafuata zoezi la kuweka shada za maua .Yaliwekwa maua mengi sana juu ya kaburi la mtoto huyu.Nililitazama kaburi lile nikapandwa na hasira.Sikutamani tena kumuona Emmy mwanamke mwenye roho ya kikatili sana.Yeye ndiye aliyesababisha uchungu huu.Padre akalibariki kaburi na huo ndio ukawa mwisho wa safari ya Baraka hapa duniani.Watu walianza kurejea katika magari yao kwa ajili yakurejea nyumbani.sikutaka kuondoka pale makaburini.Chris na watu kadhaa walijaribu kunisihi lakini nikawaomba waniache kwa muda..Nilitaka nipate muda kidogo wa kukaa karibu na kaburi la Baraka.Chris akawaambia wale watu waliobakiname wanipe nafasi.Wakajitenga nami na kwenda kukaa mbali kidogo .Nikabaki peke yangu katika kaburi lile.Nikapiga magoti pembeni na kulia sana.Nililia kwa uchungu mkubwa.Nilimlaani Emny kwa laana zote za dunia hii.
“ Kwa heri Baraka.Nitakuwa natembelea hapa kila mara kuja kulitazama kaburi lako” nikasema huku nikigeuka na taratibu nikaanza kuelekea garini.Chris akanishika mkono nakuniongoza hadi garini kisha tukaanza kurejea nyumbani.Niliegemeza kichwa kitini nikafumba macho na kwa mbali wimbo uitwao Gone to soon wa Michael Jackson ukawa unasikika mle garini .
Like A Comet
Blazing 'Cross The Evening Sky
Gone Too Soon
Like A Rainbow
Fading In The Twinkling Of An Eye
Gone Too Soon
Shiny And Sparkly
And Splendidly Bright
Here One Day
Gone One Night
Like The Loss Of Sunlight
On A Cloudy Afternoon
Gone Too Soon
Like A Castle
Built Upon A Sandy Beach
Gone Too Soon
Like A Perfect Flower
That Is Just Beyond Your Reach
Gone Too Soon
Born To Amuse, To Inspire, To Delight
Here One Day
Gone One Night
Like A Sunset
Dying With The Rising Of The Moon
Gone Too Soon
Gone Too Soon
Ni kweli Baraka alikuwa ameondoka mapema mno.Bado alikuwa na ndoto nyingi sana za maisha yake lakini zote zimeondoka naye.Alitamani sana kuwa mwandishi mahiri wa vitabu lakini hata ndoto yake hiyo nayo imetoweka.Taifa limempoteza kijana mwenye ndoto nyingi kubwa na nzuri .Yote hii imesababishwa na mwanamke mmoja tu Emmy.Kila nilipolikumbuka jina emmy nilimalizia na laana nyuma yake.Nilimlaani kwa kila laana.Nilimuombea kila baya japokuwa maandiko yanatuambia kwamba tuwapende maadui zetu na tuwaombee maisha mema na marefu..
Nyumbani kilichokuwsa kikiendelea ni kupata chakula kwa waombolezaji. Nilishindwa kabisa kula.Sikuwa na hamu ya chakula licha ya kubembelezwa sana na wenzangu.Kwa mbali kijua kilikuwa kikimalizikia .watu walikuwa wanatawanyika baada ya shughuli ndefu ya siku ya leo.Nikiwa nimekaa pembeni kabisa nikiwa na Chris na rafiki zangu wengine wawili ,akatokea Clara akiwa na sahani ya hakula.
“ Wayne ,nafahamu huna hamu ya chakula ,lakini nakuomba ule japo kidogo chakula hiki .Unahitaji kupata nguvu.” Akasema huku akinikabidhi sahani ile ya chakula.Nilishindwa kumkatalia nikaipokea na kuanza kula .Alikuwa amekaa pembeni yetu na nilipomaliza kula akachukua sahani yake akaondoka.Mara baba mkwe akajitokeza.Chris na wale rafiki zangu wawili wakaondoka pale na kutucha sisi wawili..
“ Wayne pole sana.Nafahamu ni jinsi gani ulivyoumia lakini haya ndiyo maisha yetu sisi wanadamu.Wote tutapitia hatua hii.Baraka yeye amekwisha maliza safari yake na kwa sisi tuliobaki hatuna budi maisha yaendelee kama kawaida japokuwa itatuchukua muda mrefu sana kusahau tukio hili.Kwa upande wangu napenda nikushukuru sana kwa msaada wako mkubwa tumeweza kufanikisha mazishi ya Baraka bila matatizo.Ninachokuomba Wayne ni kitu kimoja tu.” Baba mkwe akanyamaza kidogo akanywa konyagi kama kawaida yake kisha akaendelea
“ nakuomba umsahau kabisa Emmy.Futa kabisa picha yake katika kichwa chako.Endelea na maisha yako na huyu uliyempata sasa hivi.Siku zote mimi nitaendelea kuwa msaada kwako .Endapo utarudiana na Emmy atakuua.”
“ Nimekuelewa baba .Mimi na emmy tumefikia mwisho na sintathubutu kamwe kurudiana na Emmy.” Nikajibu kwa ufupi kisha tukaendelea na maongezi mengine hadi usiku mwingi.Tulilala hapo msibani siku hiyo.
****************
Kulipambazuka asubuhi na kiubaridi kikali cha Arusha.Wakati nikipiga mswaki Clara akatokea.
“ Morning darling.Pole na baridi ya usiku” akasema huku akitabasamu.Pamoja na kujitanda mavazi haya ya msiba bado Clara alizidi kuonekana mrembo zaidi.Nikamtazama nikatabasamu na kusema
“ Nashukuru Clara.Umeamakje?
“ Mimi nimeamka salama pia.” Akajibu
“ nafurahi kusikia uko salama.”
“ wayne ratiba ya leo ikoje? Nini kinaendelea leo?
“ Ratiba ya leo,asubuhi hii tutaenda makaburini kuwasha mishumaa katika kaburi la Baraka halafu tutarejea nyumbani na saa nne kutakuwa na kikao cha wanandugu na msiba utamalizika rasmi. Baada ya kikao hicho sisi tutawaaga na kuondoka zetu.” Nikasema .Nilimshukuru sana Clara kwa mapenzi makubwa aliyoyaonyesha kwangu kwani licha ya jina kubwa alilokuwa nalo na utajiri wake mkubwa lakini bado ameweka hayo yote kando na amekuwa nami bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu nilichokuwa nacho.Amenidhihirishia kwamba ananipenda kwa dhati ya moyo wake.
Baada ya kuachana na Clara akaja Chris.
“ wayne umeamkaje? Akanisalimu
“ Nimeamka salama Chris.” Nikajibu huku nikiendelea kunawa.
“ Ok wayne,niliona nikusalimie na kukuaga.Ninaondoka zangu kwani shughuli zilizobaki hapa ni za wanandugu.Tutazidi kuonana Wayne” akasemaChris huku akipiga hatua kuondoka.
“ Chris ! ..” Nikaita akageuka
“ Nashukuru sana kwa msaada wako jana.Bila wewe jana sijui ningefanya nini.By the way naomba tusameheane yale yote yaliyopita.Mambo mengi yametokea baina yetu lakini naomba tutafute muda tuongee na tuyamalize.Nitatafuta muda mzuri tutakaa na tutayamaliza.Thanx for everything.” Nikasema huku nikimpa mkono Chris.hakuamini kama ningeweza kuongea maneno yale.
“ wayne nakushukuru sana .Sina neno la kusema lakini niko tayari muda wowote kukaa nawe,tuongee na tuyamalize haya mambo.” Akasema Chris tukaagana akaondoka.
saa mbili za asubuhi tukaelekea tena makaburini .Tukawasha mishumaa katika kaburi la Baraka pamoja na kufanya maombi.Tulirejea nyumbani na saa nne za asubuhi kama ilivyokuwa imepangwa kikaanza kikao cha wanandugu kwa ajili ya kumaliza rasmi shughuli za msiba.Kwa mshangao wa wengi Emmy hakuwepo katika kikao kile. kila mtu alikuwa anashangaa kwa sababu hata pale nyumbani hakuwepo..Tukaanza kuulizana emmy kaenda wapi lakini hakuna aliyekuwa na jibu.Baba mkwe hakutaka kuahirisha mambo ,akaamuru kikao kiendelee bila ya emmy kwani hata wakati baraka anafariki yeye hakuwepo.
Kikao kilimalizika mimi na Clara tukaaga na kuondoka zetu kwenda kupumzika hotelini
Asubuhi na mapema wakati watu wameanza kuamka,Emmy alimuamsha rafiki yake Sheila na kwa haraka wakaingia katika gari na kuondoka.Hakuna aliyefahamu walikuwa wanaelekea wapi asubuhi hiyo.Emmy ambaye macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia alionekana kuwa na hasira nyingi.Sheila ndiye aliyekuwa akiendesha gari lile.
“ Emmy una uhakika na kitu unachotaka kukifanya ? akauliza Sheila.
Emmy akainua uso wake uliokuwa na hasira akamtazama Sheila kisha akasema
“ Sheila ninajua ninachokifanya endesha gari twende.” Akasema Emmy.
“ Naomba usichukie Emmy lakini nimepoteza kabisa matumaini na yule mganga kama ana uwezo wa kukusaidia kumrudisha Wayne kwako .Badala yake amesababisha kifo cha mwanao na zaidi sana Wayne ameonyesha wazi kuzidi kukuchukia.Sidhani kama kurudi tena kwa mganga litakuwa suluhisho la matatizo yako.Yule mganga hana msaada.Tayari amekwisha tusababishia matatizo makubwa.” Akasema Sheila
“ Sheila ,mimi ndiye mwenye matatizo.Nina imani atanisaidia na ana uwezo wa kunisaidia.Mbona alimsaidia rafiki yangu akarejewa na mumewe? Kwa nini mimi ishindikane? Iwapo atashindwa nakuapia ni lazima atamrejesha mwanangu.Ama zake ama zangu.Nataka nikiwa kwake leo hii Wayne anipigie simu na kama atashindwa ni mimi na yeye.Ametudhalilisha sana kwa kufanya nasi mapenzi na bado amemuua mwanangu .Leo ama amrejeshe mwanangu Baraka ama amrejeshe Wayne kwangu” akasema emmy akiwa na hasira
“ Emmy wewe ni rafiki yangu mkubwa lakini naomba nikuweke wazi kwamba sifurahii hata kidogo kurejea tena kwa mganga kutokana na mambo aliyotufanyia na isitoshe mimi siamini kabisa katika mambo haya ya ushirikina.Iwapo atasema kwamba dawa inafanyika usiku wa leo siko tayari kulala kule tena.Nitaondoka na kukuacha peke yako.Naomba ulifahamu hilo Emmy ili tusije kulaumiana baadae.” Akasema Sheila .Emmy hakujibu kitu.
“ Rafiki yangu amepotea sana. Huku alikojiingiza katika ushirikina ni sehemu hatari mno na siku zote ushirikina mwisho wake huwa mbaya .Hii ni mara yangu ya mwisho kumsindikiza kuja huku kwa mganga kumtafuta mchawi wa ndoa yake wakati mchawi ni yeye mwenyewe.Ameivuruga ndoa yake kwa ujinga wake mwenyewe na hapaswi kumlaumu mtu yeyote yule.Alipata bahati ya kumpata mume anayempenda sana lakini ameshindwa kuitumia bahati hiyo na sasa anaanza kuhaha kumtafuta mchawi.Siko tayari kuendelea na imani hizi.Hii ni mara yangu ya mwisho kushirikiana naye katika mambo haya ya kishenzi..Kile kizee kilitufanyia udhalilishaji mkubwa.Najilaumu sana kila nikikumbuka kitendo alichotufanyia.Mpaka sasa nikikumbuka nahisi kutapika .Sijui nitaoga na sabuni gani ili niweze kuiondoa mbaya harufu ya yule babu ambayo ninaisikia kila siku.Emmy amenifanya nidhalilike namna hii...Nimeanza kumchoka Emmy.Kama akiendelea na tabia yake hii sintakuwa na njia nyingine zaidi ya kuachana naye..Sintakubali kuwa na rafiki mwenye tabia kama za Emmy” akawaza Sheila huku gari likiendelea kwenda kwa kasi.
Saa sita za mchana waliwasili nyumbani kwa mganga.Wakasimamisha gari na kushuka wakaingia ndani.Mama msaidizi wa mganga akawapokea.
“ Karibuni wanangu” akasema
“ Ahsante “ akasema Sheila Emmy yeye hakusema kitu alikuwa amenuna.
“ kwema huko mtokako? Akauliza yule mama
“ Huko kwema mama japo si kwema sana” akasema Sheila
“ Huyu mganga tumemkuta? Akauliza emmy kwa ukali.Yule mama akamuangalia kisha akawaomba waingie ndani
“ Naomba unipe jibu moja mganga yupo au hayupo? Akahoji Emmy huku akimtazama yule mama kwa macho makali sana.
“ Mganga yuko ndani..” akasema na kuwaongoza Emmy na Sheila hadi ndani.
“ karibuni hapa mketi.Mganga ana shughuli akimaliza atakuja kuwahudumia.” Akasema yule mama na kuondoka akawaacha akina Emmy mle chumbani.
“ Leo ama zake ama zangu..” akasema emmy kwa sauti ndogo .Sheila hakumjibu kitu.
Baada ya masaa mawili yule mama akarejea tena akawaomba Emmy na Sheila wamfuate.Moja kwa moja wakainhgi akatika chumba cha mganga.
“ karibuni wanangu.Limekuwa jambo jema mmerudi tena….habari zsa huko mtokako? Akasema mzee Mtuguru huku akitabasamu na mkononi akiwa anaupunga usinga wake.Emmy akamuangalia kwa jicho la chuki na akiwa bado amesimama akasema
“ Mzee leo sijaja hapa kufanya mzaha.Unajua ulichokifanya kwa hiyo nimekuja hapa kwa mambo mawili tu.Aidha unirudishie mwanangu au unitimizie ninavyotaka.” Akasema Emmy kwa ukali.Mganga akamtazama kisha akamwambia
“Binti naomba ukae chini..”
“ Sintakaa hadi umenijibu kwamba utanirudishia mwanangu uliyemuua au utamrudisha Wayne kwangu.” Akafoka Emmy
“ Binti nimekwambia kaa chini.Hii si sehemu ya kuja na kuanza kupayuka.Hii ni sehemu ya mizimu na inaweza ikakuadhibu vikali kwa kukosa adabu.Nakuamuru kwa mara ya mwisho kaa chini” akafoka mzee Mtuguru ambaye naye alikwisha aanza kukasirishwa na tabia aliyoionyesha Emmy.
“ Emmy kaa chini shoga,yasije anza mambo mengine bure” akasema Sheila na Emmy akaketi mkekani.
Mganga akaongea maneno yake ya kiganga halafu akachukua usinga wake akaupunga hewani.
“ Emmy umeikasirisha sana mizimu kwa utovu wa nidhamu uliouonyehsa na kwa maana hiyo unatakiwa kuiomba msamaha ama sivyo litakupata jambo baya sana .Mizimu itakuadhibu vikali.” Akafoka mzee Mtuguru .Emmy akastuka baada ya kusikia kwamba mizimu inaweza kumuadhibu.
“ Mambo yako hayakwenda kama ulivyokuwa umetarajia kwa sababu bado kuna kazi moja ambayo unatakiwa uifanye wewe kwa mkono wako.kabla ya shughuli hiyo itakulazimu kwanza kuiomba msamaha mizimu .Msamaha huo huambatana na sadaka ya kuchinja mnyama.Nina mbuzi katika zizi langu hapo ambao hutumika kwa ajili ya sadaka kwa mizimu.Shughuli itaanza leo saa moja jioni hadi usiku mwingi.Hala……” kabla mzee Mtuguru hajaendelea Emmy akaingilia kati
“ Mzee siwezi kulala hapa kwako usiku wa leo..Kitendo ulichotufanyia bado sijakisahau..” akafoka Emmy
“ Kama hutalala hapa basi ni ishara ya kuidharau mizimu na lazima ikuadhibu “ akasema mzee Mtuguru.Emmy akabaki kimya.
“ Unakubali kulala hapa ili dawa yako imalizike usiku wa leo au unarudi Arusha ?” akauliza mganga kwa ukali
“ Nitabaki” akajibu Emmy baada ya kufikiri kwa muda
“ Mimi naenda kuandaa mbuzi kwa ajili ya shughuli ya usiku.” Akasema mzee Mtuguru na kutoka nje.
“ Shoga mimi silali hapa kwa mganga kama nilivyokwambia” akasema Sheila baada ya mganga kutoka mle chumbani
“ Itakubidi ulale Sheila si umesikia mganga alivyosema? Emmy akajibu
“ Mimi hayanihusu.Nimesema sintalala hapa.Kitendo alichonifanyia siwezi kukisahau hata kidogo.”
“ Sheila usiondoke ukaniacha huku peke yangu” Emmy akaomba
“ Hapana Emmy..siwezi kulala huku.Lazima nirejee Arusha leo hii.hayo yalikuwa ni makubalinao yetu” akasema Sheila huku akiinuka.
“Usiniache Sheila…” akasema Emmy lakini Sheila hakumjali akaenda kuchukua mkoba wake akamuomba mama msaidizi wa mganga amsaidie kumtafutia usafiri wa kumfikisha barabara kuu ambako angeweza kupanda mabasi yanayoelekea Arusha.
“ Sitaki tena mambo ya kipuuzi.Sitaki kushiriki katika mambo ya ushirikina tena.hayana manufaa yoyote..” akawaza Sheila akiwa juu ya piki piki akipelekwa stendi ya mabasi kusubiri usafiri wa kuelekea Arusha.
*******************
“ Clara come here close to me..” nilimwambia Clara tukiwa chumbani hotelini.Clara aliyekuwa amekaa sofani akitazama Luninga akainuka na kuja kitandani.Siku nzima ya leo tumeitumia kupumzika baada ya siku kadhaa za msiba wa Baraka.
“ I’m here my love “ akasema Clara akinitazama usoni.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Clara kwanza napenda nichukue nafasi hii kukushukuru sana kwa upendo wako wa pekee wa kusitisha shughuli zako zote na kuwa pamoja nami hasa katika kipindi kile kigumu cha msiba wa baraka.Wewe ndiye uliyekuwa mfariji wangu mkubwa katika siku hizi ngumu na bado utaendelea kuwa mfariji wangu kwani jambo hili halitakwisha leo wala kesho kichwani mwangu.Itanichukua siku nyingi kulisahau.Nina deni kubwa kwako na ambalo sijui nitalilipa vipi.Deni la upendo wako wa kweli na wa dhati..” nikamwambia Clara na kumfanya atabasamu.
“ Wayne ,wewe una thamani kubwa kupita mali ,biashara na kila nilichonacho.Hivi vyote ni vitu ambavyo vinapatikana kwa juhud na kufanya kazio kwa bidii lakini mtu kama wewe si rahisi kupatikana katika ulimwenmgu wa sasa.Niko tayari kufanya lolote lile ili mradi niwe nawe kila sekunde.Nilistahili kuwa nawe msibani kwa sababu ulikuwa ni msiba wetu sote .Ulimpenda Baraka halikadhalika nilimpenda pia.” Akasema Clara.
“ Pamoja na yote yaliyotokea nina kitu ninataka kukueleza.” Nikasema
“ Usihofu Wayne nieleze kitu chochote kile unachohitaji kunieleza” akasema Clara.
“ Clara maisha yangu ya nyuma yametawaliwa na historia inayoniumiza mno na hasa historia ya maisha yangu na Emmy.Sitaki kukumbuka maisha ya nyuma kwa sababu tayari nimeanza maisha mapya yenye furaha na amani.Pamoja na maisha haya mapya niliyoanza kuyaishai lakini bado kuna tatizo.” Nikanyamaza na kumtazama Clara ambaye alionyesha uso wa wasi wasi.
“ Kuna tatizo gani Wayne ? akauliza Clara
“ Kama utakumbuka tuliafikiana kwamba tutafute nyumba ya kuishi hapa Arusha kwa sababu ni sehemu unayoipenda sana.Nakubaliana na mawazo yako kwa sababu hata mimi ninaipenda Arusha.Baada ya kufikiri kwa kina nimegundua kwamba iwapo ninataka kuishi maisha yenye raha na amani itanilazimu kuhama Arusha na kwenda kuishi mbali, mahala ambako Emmy hatapata nafasi ya kuwa karibu nami.Mwanamke huyu ataendelea kutuandama kila uchao tukiendelea kukaa hapa Arusha.Wazo langu ni kwamba tutafute nyumba jijini Dar es salaam.Lile ni jiji kubwa na tutaishi kwa amani.” Clara akatabasamu na kunishika mkono wangu.
“ Wayne hata mimi nilikuwa na wazo kama hilo lakini nikaogopa kukueleza kwa kujua kwamba unapenda sana kuishi Arusha.Kwa kweli nilimtazama Emmy tukiwa msibani bado ana chuki kubwa na wewe chuki ambayo sina hakika kama itakwisha.Nakubaliana na mawazo yako kwamba hatutaweza kuishi maisha ya raha na amani kama tukiwa karibu naye.Utanisamehe kwa kusema hivi lakini that woman is a monster “ akasema Clara
“ nashukuru sana Clara kwa kuliona hilo na kukubali tukaishi sehemu nyingine mbali na arusha.Unapendekeza kwenda kuishi mkoa gani?
“ Wayne ni mapema sana kuamua ni sehemu ipi tukaishi.Mimi ninaweza kuishi nawe sehemu yoyote ile hata kama ni shambani.” Akasema Clara na kunifanya nicheke.
“ Usicheke Wayne.Ni kweli ninaweza kuishi nawe sehemu yoyote ile.Usiumize kichwa kuhusu sehemu ya kuishi mimi na wewe.Tutapanga na kuamua vizuri baada ya kumaliza mapumziko yetu.Kesho tutakapoondoka jiji la Arusha tutapunga mkono wa kwaheri kwani hatutarudi tena.Safari ya maisha yetu ya pamoja tayari imeanza.” Akasma Clara .Nikamvuta kwangu na kumbusu .
“ Mbona hutaki kuniambia tunaelekea wapi kupumzika? Nikamuuliza
“ Hapana Wayne sintakwambia.Just wait and see.Its a surprise” akasema huku akitabasamu.
********************
Ni saa nne za usiku sasa bado shughuli ya uganga ilikuwa ikiendelea.Emmy alikuwa amevishwa vazi jeusi na kupakwa dawa nyeupe usoni.Zoezi la kwanza la kuchinja mbuzi na kuomba msamaha kwa mizimu likakamilika kisha likafuata zoezi la pili .
Mzee Mtuguru akampa Emmy chungu akishike kisha akamuamuru amfuate.Walipita katika msitu mnene wenye kiza na milio ya kutisha.baada ya mwendo wa masaa mawili wakafika katika shamba moja la mihogo ambalo kati kati yake kulikuwa na kibanda kidogo cha udongo..Akamuamuru Emmy amfuate mle ndani.Kulikuwa na giza nene .Mganga akaongea maneno yake ya kiganga ambayo Emmy hakuyaelewa halafu akawasha kibatari na chumba ikawa na mwanga .Akachukua dawa fulani na kumpaka Emmy na ghafla Emmy akaanza kuona mambo mengi ya ajabu ajabu na ya kutisha.Mle ndani ya kile chumba aliweza kuwaona watu kadhaa wake kwa waume wakiwa wamekaa wamejikunyata.walikuwa na nywele ndefu .Walikuwa wanatisha.Emmy akaogopa na kutetemeka.Hakuwahi kuyaona mambo ya kutisha namna hii.Nje ya kibanda kile alisikia milio ya wanyama na midudu ya kutisha. Mganga akamkabidhi kisu mkononi.
“ Unatakiwa ukamilishe kazi iliyobaki ili mambo yako yafanikiwe” akasema mganga lakini Emmy hakujibu chochote.Bado alikuwa anaogopa sana.Mganga akaliendea tenga moja kubwa lililokuwa pembeni ya kile chumba akaliinua na mara Emmy akaona kitu ambacho hakukiamini kama ni kweli. Aliogopa na kutetemeka mwili.Nguvu zilimuisha.Katika ile pembe ya nyumba alionekana mwanae Baraka akiwa amejikunyata.Alikuwa anatia huruma sana.
“ Baraka !! “ Emmy akasema kwa mshangao..Baraka hakujibu kitu chochote aliendelea kumuangalia kwa macho ya huruma..
“ Baraka kumbe bado uko hai !! ..Mganga nakuomba unirudishie mwanangu” akapiga kelele Emmy huku machozi yakimtoka.
“ Baraka umekwisha mtoa sadaka kwa mizimu na hawezi tena kurudi.Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumkata ulimi kwa hicho kisu nilichokupa.” Akasema mzee Mtuguru
“ What !! …siwezi kufanya upuuzi wa namna hiyo..Mwanangu yule pale ni mzima kabisa na siwezi kamwe kumkata ulimi.” Akafoka Emmy akakitupa kisu chini.Mganga akamtazama kwa hasira kisha akasema
“ Muda mchache uliopita tumetoka kuiomba msamaha mizimu kwa sababu ya utovu wa nidhamu uliouonyesha kwao.Nakuonya kwa mara nyingne tena kwamba mizimu haitakuwa na uvumilivu kwa tabia yako hii.Inaweza hata kukuua kwa kuikosea heshima.Nakuomba ufanye kama unavyoelekezwa kufanya.Kwa hiyo inua kisu sasa hivi na umsogelee Baraka umkate ulimi wake haraka.”akafoka mzee Mtuguru.
Emmy alikuwa analia alipomuona mwanae amejikunyata pembeni ya kona.Mganga akachukua tena dawa nyingine na kumpata kichwani.Mara Emmy akajikuta akiwa na ujasiri wa ajabu sana.Akainama akakiokota kisu na kumkaribia mwanae.Akamtazama akamshika na kumfumbua mdomo.Baraka hakuweza kuongea chochote. Emmy akaukata ulimi wa baraka kama alivyokuwa ameelekezwa kisha mzee Mtuguru akamuamuru atoke nje na yeye akaendelea na shughuli zake za uganga mle ndani .Baada ya masaa mawili akatoka na kumkuta Emmy amekaa pembeni ya nyumba ile akilia.
“ usilie Emmy.Kwa hivi sasa mambo yako yote yanakwenda kuwa mazuri .” akasema mganga kisha wakaanza safari ya kurudi.
“ Emmy mizimu imefurahi na ninakuhakikishia kwamba safari hii Wayne anarudi kwako.Ninachotaka kufahamu toka kwako ni kitu gani tumfanye huyu mwanamke aliyenaye? Tumuue? Akauliza mzee Mtuguru.Emmy akafikiri kidogo kisha akasema
“ Ninachokitaka mimi ni kumfanya ateseke maisha yake yote.Asiweze kutembea wala kufanya kazi yoyo tile.Maisha yake yatawaliwe na mateso makali.”
Mzee mtuguru akampa Emmy pembe jeusi lililozungusiwa ushanga na kumwambia
“ Sema mbele ya pembe hili unataka mizimu imfanye nini huyu mwanamke aliye na mume wako”
Emmy akaikamata pembe ile kisha akasema
“ Nataka apewe ugonjwa ambao utamfanya aishi maisha ya mateso na maumivu makali hadi siku ya kufa kwake.Asiweze kufanya kazi yoyote ile tena katika maisha yake” akasema Emmy.
“ Mizimu imekusikia na itafanya kama ulivyoiomba” akasema mganga.
************************
Saa tatu za asubuhi tayari tulikwisha funga mizigo yetu kwa ajili ya safari.Nilimuomba rafiki yangu Beka atupeleke uwanja wa ndege wa Kilimajnaro halafu abaki na gari langu.Saa tatu na nusu safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.Nilikuwa na furaha isiyo kifani kwani nilitegemea kwamba sasa karaha zote za Emmy nitaziacha nyuma na mimi kuishi maisha ya furaha na amani nikiwa na malaika wangu Clara.Tuliwasili uwanja wa ndege tukaagana na Beka na sisi kuingia sehemu ya kusubiria ndege .
Hatimaye muda wetu ukafika na tukaombwa tuelekee ndegeni.Taratibu tukiwa tumeshikana mikono tukaungana na abiria wengine kuelekea mahala ilipokuwa ndege tutakayosafiri nayo.Kabla hajaikanyaga ngazi ya ndege Clara akasimama.
“ Wayne naishiwa nguvu ..siwezi tena kunyanyua mguu wa…….” Hayo yalikuwa maneno ya mwisho ya Clara.Akaanguka na kabla hajafika chini nikawahi kumdaka.
Emmy alikuwa amesimama mbele ya kioo kikubwa akiwa amefura na hasira na sura yake ameikunja..Kwa muda wa saa moja sasa alikuwa amesimama akitazama kioo kile kikubwa mfano wa luninga ,kilichokuwa kikimuonyesha kila kilichokuwa kinaendelea kati ya Wayne na Clara.Hakuwa ameongea chochote toka alipoanza kutazama luninga ile ikiwaonyesha Wayne na Clara walivyokuwa wanajiandaa kwa safari. Wayne na Clara wakiwa uwanjani walionekana ni wenye furaha kubwa .Walikuwa wamekaa wakisubiri zamu yao ya kupanda ndegeni ifike na baadae wakashikana mikono na kuanza kuelekea ndegeni.Clara akauma meno kwa hasira
“ Damn you Wayne..huwezi kunikimbia..Nitakutafuta usiku na mchana.Na huyo mwanamitindo wako ambaye amekupagawisha na kukufanya unitaliki atakiona cha moto..” akawaza Emmy .Muda wote huu mganga alikuwa amesimama pembeni yake akiwa na usinga wake mkononi akiupunga huku na huko huku akiongea maneno yake ya kiganga.
“ Emmy Wayne na Clara wanaondoka na bado haujafanya maamuzi yoyote.hii ni nafasi yako usiiache ikapita..Ukiacha wakiingia ndegeni na wakaiacha ardhi ya Arusha ,kurudi tena itakuwa vigumu mno.Kama bado unataka kuendelea na ile dhamira yako basi huu ndio wakati wake.Yeyote utakayemfunga siku ya leo hatapona hadi siku utakapokufa wewe.” Akasema mganga huku akimuonyeshea Emmy meza iliyokuwa na wanasesere wawili .Emmy hakusema kitu akageuka na kuiendea meza ile kisha akachagua mwanaserere mwenye umbo la mwanamke.Mganga akampa sindano.Emmy akasimama tena mbele ya kile kioo akawashuhudia Wayne na Clara wakikaribia kufika katika ngazi za kupandia ndege.Kwa hasira akauinua mkono wake wa kulia uliokuwa umeshika sindano ndefu na kuichoma upande wa kulia wa yule ukatoka moshi mweupe na sekunde ile ile Clara ambaye alikuwa anajiandaa kuikanyaga ngazi ya kupandia ndegeni akaanguka na hakuweza kuongea wala kuinuka tena.Emmy akatabasamu
" Leo nimekupata " akasema Emmy huku akitabasamu.
“ Kazi imekwisha” akasema mganga.
“ Kwa sasa huyu mwanamke kazi yake imekwisha.Nakuhakikishia Wayne lazima arudi kwako ndani ya muda mfupi. Atakufuata yeye mwenyewe.” Akajigamba mzee Mtuguru.
“ Nashukuru sana Mganga. Nakuahidi zawadi nzuri mno kama Wayne atafanikiwa kuja kwangu.” Akasema Emmy huku akitabasamu
“ Usiseme kama atarudi kwako.nakuhakikishia lazima arudi kwako na safari hii hataweza kuondoka tena.” Mganga akazidi kumpa moyo Emmy.
*************************
Clara..!! Clara !! ..” Niliita kwa nguvu baada ya kumdaka Clara alipotaka kuanguka lakini hakuweza kusema chochote..Nilichanganyikiwa ghafla.Mtu ambaye sekunde chache zilizopita tumekuwa tukiongea vizuri na kucheka lakini ghafla hawezi kuongea tena.Haya yalikuwa ni mambo ya ajabu sana kunitokea.Sikujua Clara amepatwa na ugonjwa gani uliomtokea ghafla namna ile.
Watu waliokuwa karibu wakanisaidia kumbeba Clara na kumuweka pembeni.Bado kichwa changu kilikuwa kizito kuamini kilichotokea.Nilihisi ni kama mchezo wa kuigiza lakini kadiri dakika zilivyokuwa zikisonga ndivyo nilivyojikuta nikilazimika kuamini kwamba Clara alikuwa amepatwa na ugonjwa wa ghafla ambao sikufahamu ni ugonjwa gani.Pamoja na ujasiri wangu wote niliokuwa nao nilijikuta nikitetemeka kila nilipomuona Clara na hali aliyokuwa nayo.Macho yalikuwa yamefumba,hakuweza hata kufumbua jicho.Mwili wake haukuweza hata kutikisika.Machozi ya uchungu yakanitiririka.Wanaume wawili wa makamo ambao nao walikuwa ni wasafiri wakanivuta pembeni baada ya kuiona hali nilioyokuwa nayo.
“ Jipe moyo ndugu yangu..Mungu atakusaidia..” akasema mmoja wao aliyekuwa amevaa suti nyeusi..
“ Tatizo hasa la mwenzio ni nini? Akauliza mwingine aliyekuwa amekaa kushoto kwangu..Nikajikaza na kusema
“ Sifahamu tatizo ni nini ..imetokea ghafla tu akapatwa na ugonjwa ule..” nikajibu kwa ufupi.Tayari uongozi wa pale uwanjani ukataarifiwa kuhusiana na kilichokuwa kimetokea na kwa haraka likatolewa gari kwa ajili ya kumkimbiza Clara katika hospitali ya Rufaa ya KCMC.Kwa kasi ya aina yake wahudumu wa pale uwanjani wakampakia Clara katika gari na mimi nikaingia ndani ya gari lile kisha tukaondoka uwanjani pale kwa kasi kubwa.
Kila nilipokuwa namuangalia Clara nilishindwa kujizuia kutokwa na machozi.Sipati neno ambalo linaweza kuelezea uchungu niliokuwa nao kwa wakati ule.Rangi ya ngozi ya Clara ikaanza kubadilika na kuwa na weusi weusi..nikazidi kuogopa.Nawashukuru watu niliokuwa nao mle garini walijitahidi kwa kila namna walivyoweza kunipa moyo ingawa hata nao nyuso zao zilionyesha mstuko na uoga wa dhahiri.
“ Ouh Clara..nini kimekupata malaika wangu?.. Nilisema kwa uchungu nilipomtazama Clara akiwa amelala mle ndani ya gari hajitambui.Niliogopa sana kwa hali aliyokuwa nayo. Gari ilikuwa inakwenda kwa mwendo mkali sana lakini niliona kama inachelewa kufika hospitali ili Clara aanze kupatiwa matibabu.
Hatimaye tukawasili katika hospitali ya rufaa ya KCMC mjini Moshi na kwa haraka wauguzi wakampokea mgonjwa na kuanza kumshughulikia mara moja. Sampuli za damu na vipimo vingine vikachukuliwa na kupelekwa maabara kwa uchunguzi.
Nilitoa malezo mafupi kwa madaktari kuhusiana na jinsi ugonjwa ule wa Clara ulivyoanza halafu wakaniomba nikasubiri nje ili waendelee na uchunguzi wao.Niliwaomba madaktari wale wafanye kila linalowezekana ili kuokoa maisha ya Clara kwani hali aliyokuwa nayo ilikuwa inaogopesha mno.Miguu haikuwa na nguvu nikatafuta sehemu nikakaa.Bado kichwa changu kilikuwa na mawazo mengi sana juu ya kilichotokea.Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana na ilikuwa vigumu sana kuamini kilichotokea.Nilivuta picha ya kuanzia asubuhi tulipokuwa tunajiandaa kwa safari hii ambayo Clara hakutaka kuniambia tunaelekea wapi ingawa tiketi zetu zilionyesha kwamba tulikuwa tunaelekea Dar es salaam.Nikakumbuka tulivyoliacha jiji la Arusha nikiwa na matumaini kwamba nimeyaacha nyuma matatizo yote yaliyotokea kati yangu na Emmy.Sikutarajia kurejea tena Arusha.Niliamini kwamba ninakwenda kuanza maisha mapya nikiwa na malaika wangu Clara.Nilikumbuka tulivyoagana na rafiki yangu Beka pale uwanja wa ndege naye akarejea Arusha na gari langu.Nilimuahidi kuwa nikifika huko tunakokwenda ningemtaarifu kwa simu.Nikakumbuka pia tulivyokuwa tukipiga hatua kuelekea katika ndege na mara kumbu kumbu ambayo mpaka leo nikiikumbuka huwa inaniliza ikanijia kichwani. Ilikuwa ni kama ninatazama filamu.Clara alikuwa tayari ameinua mguu wake ili akanyage ngazi za ndege lakini hakuweza kufanya hivyo kwani alianguka ghafla na hakuweza kuongea tena.machopzi yakaanza kunitiririka tena.Nikafuta machozi nikachukua simu yangu na kumtaarifu rafiki yangu Beka kilichokuwa kimetokea.Hakuamini hata kidogo na alidhani ninamtania.Nilipomuhakikishia kwamba haukuwa utani aliamini na kunitaarifu kwamba tayari anaanza safari ya kuja Moshi kuungana nami katika wakati ule mgumu.Baada ya kuongea na Beka nikampigia simu baba mkwe na kumtaarifu kilichotokea halikadhalika naye akanitaarifu kwamba yuko njiani anakuna Moshi.Nikamtaarifu pia na Chris ambaye tayari tumekwisha maliza tofauti zetu . Kila mmoja niliyemtaarifu alistuka mno .hakuna aliyeamini moja kwa moja.
Nikiwa bado nimekaa pale nje nikiwasiliana na watu mbali mbali kuhusiana na kilichotokea,nikaitwa katika chumba cha daktari.Haraka haraka nikaingia na kuketi kitini.daktari akanitazama kisha akasema
“ Wayne tumemfanyia uchunguzi mgonjwa wako na tumegundua kwamba mgonjwa wako amepatwa na ugonjwa wa kupooza…”
“ What ? ..Unasema ??......Nikauliza kwa mshangao nikiwa nimesimama na macho kunitoka.Nilianza kusikia joto la ghafla.Hii ilikuwa ni taarifa ya kustusha sana.
“ Dakatari tafadhali naomba unielezee vizuri kwa ufasaha ili nikuelewe.Umesema Clara anaumwa nini? Nikauliza tena nikiwa bado nimesimama.
Kabla hajaendelea kunipa taarifa kuhusiana na ugonjwa wa Clara akaniomba niketi chini..
“ wayne mgonjwa wako amepatwa na ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa kulia.”
“ Ouh my God !! ..” Nikasema kwa sauti kubwa mikono yangu ikiwa kichwani.Daktari akanitazama na kusema
“ Tulidhani labda tatizo hili limetokana na shinikizo la damu lakini kwa Clara kila kitu kiko katika hali ya kawaida.Vipimo vyote vinaonyesha hakuna tatizo.Bado tunataka kundelea kufanya uchunguzi zaidi ili tuweze kufahamu nini chanzo cha ugonjwa huu.Hata sisi imetushangaza kidogo” akasema Daktari kisha akanyamaza akanitazama na kuendelea.
“ Ugonjwa huu umekuwa ukiwapata watu wengi kwa siku za karibuni .Lakini kwa upande wa Clara hali ni tofauti kidogo hivyo itatulazimu tufanye uchunguzi wa kina tujue nini chanzo cha tatizo hili Kwa sasa kuna kipimo kimoja ambacho tunahitaji kukifanya lakini kwa bahati mbaya mashine yetu imeharibika kwa hiyo itakulazimu uende jijini arusha kwa ajili ya kipimo cha CT Scan.” Akasema daktari..
“ Daktari naomba uniambie tafadhali..Clara atapona ? Ataweza kutembea tena kama zamani? Nikauliza maswali mfululizo.Daktari akanitazama na kusema
‘ Wayne usiwe na hofu ,mgonjwa atapona ingawa siwezi kukwambia lini anaweza akapata nafuu.Tiba kubwa ya ugonjwa huu ni mazoezi .Baada ya kujiridhisha na vipimo vyote kwamba hakuna tatizo lingine basi tutaanza kumfanyisha mazoezi mara moja ” Akasema daktari..
Pamoja na maneno yale ya kutia moyo ya daktari,niliinama na kuzama katika mawazo mengi sana.Nilijaribu kutafakari lakini nikakosa majibu . Nilihisi kama dunia inaniadhibu..
Niliongozana na daktari kwenda kumuona Clara aliyekuwa amelazwa katika chumba maalum cha peke yake.
Nilidondosha machozi nilipomshuhudia mwanamke ambaye masaa machache yaliyopita alikuwa na uzuri usioelezka lakini kwa sasa hata sura yake ilikuwa imebadilika.Alikuwa amelala kitandani hajitambui,rangi ya ngozi yake ilianza kuwa na weusi na mdomo wake ulikuwa umepinda tofauti na ulivyokuwa awali.
Beka na Chris wakawasili kila mmoja na gari lake na kila mmoja alistuka mno kwa hali aliyokuwa nayo Clara.
“ Wayne nina ushauri mmoja..” akasema Chris .
“ Kwa nini tusimuhamishe Clara na kumpeleka jijini Arusha.Kwa sasa kumefunguliwa hospitali moja kubwa ya kimataifa inayotibu magonjwa kama huu uliompata Clara.Kuna mabingwa wa kutibu ugonjwa huu toka nchini Marekani” akashauri Chris.Kwa pamoja tukashauriana na kuafikiana kwamba tumuhamishe Clara na kumpeleka katika hospitali hiyo mpya aliyoshauri Chris.
***************************
" Mganga nakuahidi kurudi tena nikiwa na zawadi nzuri sana ambayo hutaamini." akasema Emmy akiwa na tabasamu pana sana.
" Emmy nimekuhakikishia kwamba huyu mwaanume lazima atarudi kwako na hataondoka tena.Safari hii atakupenda kupita maelezo.Atafanya kila utakalomuamuru alifanye." akasema mganga
" Sipati neno la kukushukuru mganga..lakini utaona mwenyewe zawadi nitakayokuletea " akasema Emmy.Mganga akatoka kidogo na baada ya muda akarejea akiwa na kibuyu chenye dawa.
" Emmy ninakupa dawa hii.Hii ni dawa yenye nguvu sana na unatakiwa uipake mwilini pale tu unapokwenda kuonana na Wayne.Kwa sasa unatakiwa umtafute kwa udi na uvumba hadi umuone lakini usijaribu kumpigia simu.Unatakiwa umstukize .Wakati unakwenda kuonana naye unatakiwa ujipake dawa hii pekee na usichanganye na mafuta ya aina yoyote ile.Hilo ndilo sharti pekee la dawa hii.Ninakuhakikishia kwamba Wayne akikuona tu atastuka mno na dakika hiyo hiyo atakuomba msamaha na mtarudiana tena..." akasema mzee mtuguru na kisha wakaagana na Emmy akaanza safari ya kurejea Arusha.
" Wayne huwezi kunikimbia hata kidogo..wewe ni wangu pekee na siku zote utakuwa wangu..Hahahahaaa namuonea huruma huyo mwanamitindo wako..kwisha kazi yake.Sasa tuone hayo maringo na mikogo yake kama vitakuwepo tena.Nilimuonya asicheze na mali za watu lakini hakusikia.Hahahaaa..ukiona vimeng'aa ujue vimeng;arishwa." akawaza Emmy akiwa katika gari akirejea jijini Arusha.Alikuwa na furaha isiyo kifani nantabasamu halikukauka usoni mwake.
" Japokuwa bado nina majonzi ya kufiwa na mwanangu Baraka lakini ninafuraha kwa upande mwingine kwa sababu ninakwenda tena kurudiana na Wayne.Mimi ni mwanamke wa shoka nimempigania Wayne na mpaka sasa nimefanikiwa kumrejesha tena mikononi mwangu.Safari hii habanduki na hata hao wanga waliokuwa wananiroga ili nigombane na Wayne kwa sasa hawaniwezi tena.Kwa tiba niliyopewa mimi ni kisiki cha mpingo.Hakuna atakayeniweza kwa sasa.Nimejaa kinga kila mahala." akaendelea kuwaza Emmy.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Kuna kitu nimekumbuka.Sheila alinidokeza kwamba James anaweza akarejea muda wowote katika wiki ijayo.Sijui itakuwaje akisikia kwamba mwanae Baraka amefariki dunia.Ah ! hilo halinihusu kwa sasa akili yangu yote ni kwa Wayne.Baada ya kumrejesha Wayne kwangu ndiyo nitaanza kushughulika na James.Nitamuweka sawa na atanielewa japokuwa itamuumiza sana kwa sababu hakuwahi kumuona mwanae kwani alipoondoka kwenda masomoni Urusi aliniacha nikiwa na mimba changa kabisa na toka wakati ule hajawahi kurejea tena.Ataumia lakini hakuna namna ya kufanya kumrejesha Baraka.Inauma sana lakini nimefanya haya yote kwa ajili ya kulipigania penzi langu.Safari hii ninataka nipate mtoto na Wayne.Nilifanya makosa makubwa sana kuzaa nje ya ndoa.Laiti kama ningezaa na Wayne haya yote yasingenikuta.Sijielewi ni kwa nini sikuwa naridhika na mume wangu hadi nikawa natoka na kwenda kubadilisha wanaume kama nguo .Wayne alinipa kila nilichokihitaji lakini bado nilitoka nje ya ndoa.Lazima nilikuwa nimerogwa.Safari hii watanikoma.." akawaza Emmy
*********************
Emmy alikuwa akiendesha gari lake kwa kasi kubwa kuwahi jijini Arusha.Uso wake haukukaukiwa na tabasamu .
" Ngoja nimpigie simu Sheila simu nimtaarifu juu ya mambo yanavyokwenda japokuwa alikimbia na kuniacha peke yangu." akawaza Emmy kisha akapunguza mwendo wa gari akachukua simu na kuzitafuta namba za simu za Sheila rafiki yake mkubwa akampigia.
" Halo Emmy, niambie shoga yangu" akasema Sheila baada ya kupokea simu ya Emmy
" Sheila mambo yanakwenda vizuri sana" akajibu Emmy huku akitabasamu
" Kivipi Emmy? akauliza Sheila ambaye sauti yake ilionekana dhahiri hakuwa akiyafurahia maongezi yale na Emmy
" Sheila yule mwanamitindo wa Wayne kwisha habari yake."
" Kwisha habari yake ! Mbona sikuelewi Emmy una maanisha nini ? akauliza Sheila
" Tayari nimekwisha mdondosha.Hatainuka tena" akajibu Emmy huku akicheka kicheko cha chini chini.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
" Hallo Sheila upo ." akaita Emmy baada ya kimya kile cha ghafla.
" Nipo Emmy..Nimestuka sana kwa jambo uliloniambia.Ina maana amekufa yule mwanamitindo? akauliza Sheila
" Hapana sijamuua japokuwa nilikuwa na nafasi hiyo. Nilichokifanya ni kwamba nimempa ulemavu wa kudumu na hatainuka tena katika maisha yake.Hivi ninavyokwambia amepelekwa hospitali na hataweza kuinuka wala kutembea tena.Amepooza mwili.Hili ni fundisho kwake kuvamia mabwana wa watu" akasema Emmy.Sheila akavuta pumzi ndefu
" Sheila niko njiani ninarudi.Tutaongea mengi nikisha fika.Bado kuna kazi ninataka unisaidie "
" Nikusaidie tena?.Kuna kazi unataka nikusaidie? .Sheila akauliza kwa mshangao.
" Ndiyo ..mbona umestuka?
" Lazima nistuke Emmy .Wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu na lazima nikueleze ukweli.Kwa sasa unatakiwa utulie Emmy.Vitendo unavyoendelea kuvifanya si vya kiungwana na havitakupeleka popote. Nakwambia hivyo kama rafiki yako na mtu ninayekupenda . Nimekwisha ona mwisho wa watu waliojihusisha na masuala hayo ya ushirikina .Siku zote mwisho wao huwa si mzuri hata kidogo.Angalia shoga yangu ni hivi majuzi tu umempoteza mwanao Baraka.Hata wiki moja haijapita Clara naye anapatwa na matatizo. Mpaka lini Emmy utaendelea kuwatesa watu? Hadi lini utaendelea kumtesa Wayne? Clara unayemtesa kitandani amekukosea kitu gani? Watu wengi wanazidi kuteseka kwa sababu yako Emmy. Tafadhali hebu achana na hayo mambo ya kishirikina.Muache Wayne aendelee na maisha yake.Ulishindwa kumtunza na kwa sasa muache afurahie maisha mengine aliyoyanza.Mtegemee Mungu na kama ikimpendeza kumrudisha Wayne kwako atafanya hivyo lakini si kwa kuwategemea waganga wa kienyeji..Emm................" Kabla Sheila hajaendelea Emmy ambaye uso wake ulikwisha jikunja kwa hasira kutokana na maneno ya shoga yake akainglia kati.
" Sheila unaongea maneno gani hayo? Mbona sikuelewi ? Wewe ndiye wa kuniambia maneno kama hayo leo ..?akafoka Emmy.
" Emmy ngoja nimalizie kile ninachotaka kukwambia...." akasema Sheila.Emmy akapunguza mwendo wa gari na kuliegesha kandoni mwa bara bara.
" Emmy napenda ufahamu kwamba mimi sikukifurahia kabisa kitebdo cha kunishirikisha katika masuala yako ya kishirikina.Wazazi wangu hawakunikuza katika misingi ya kuamini mambo kama hayo.Kitendo cha kunipeleka kwa yule mganga na kusababisha akanifanyia kitendo kama alichonifanyia bado kinaniuma mno.Sijui hata nifanye nini ili niweze kuifuta taswira ya kitendo kile katika akili yangu.Nimeumia sana Emmy na kwa maana hiyo naomba ufahamu kwamba urafiki wetu kwa sasa utakuwa na mipaka.Kama unataka urafiki wetu uendelee nakushauri achana kabisa na hayo mambo ya kishirikina ambayo hayana faida yoyote kwako.Ndoa yako umeivuruga wewe mwenyewe na kwa sasa umeanza kuhangaika kumtafuta mchawi wakati mchawi ni wewe mwenyewe.Nakushaur........................."
" Bastard.....!!!" Emmy akakata simu kwa hasira na kuitupa kitini.
" Stupid girl !!..akasema kwa hasira.
" Sheila leo anathubutu kunitamkia maneno kama haya ? Bado siamini kama hata Sheila naye amenigeuka.Mimi nimekuwa mtu wake wa karibu na nimemsaidia katika mambo yake mengi ikiwa ni pamoja na kumkopesha hata mtaji wa kufungua saluni ile anayoringia kwa sasa halafu leo hii ananitamkia maneno kama haya .!!..Hapana siwezi kukubali kudharauliwa na paka kama Sheila. Anaishi mjini kwa sababu yangu mimi na hakupaswa hata kidogo kunidharau.Kwa kuwa naye ameamua kunidharau basi nitamjumuisha katika orodha ya maadui zangu.Nitamuonyesha kazi.Nitamfundisha adabu.Nadhani bado hajanifahamu vizuri" akawaza Emmy akiwa amefura kwa hasira.
" Ninaapa Sheila lazima alikimbie jiji.Nitayafanya maisha yake magumu sana na lazima aje anipigie magoti..." akasema kwa sauti ya hasira kisha akawasha gari lake na kuendelea na safari ....
*************************
Wazo alilolitoa Chris la kumuhamishia Clara katika hospitali kubwa ya St Patrick inayomilikiwa na wamisionari lilikubaliwa hata na madaktari wa pale hospitali ya rufaa ya KCMC. Bila kupoteza muda taratibu zikaanza kufanyika na baada ya dakika chache kila kitu kikawa tayari Clara akapakiwa katika gari la wagonjwa na safari ya kuelekea Arusha ikaanza.Clara alikuwa amelala kitandani macho ameyafumba.Nilishindwa kujizuia kudondosha machozi niliposhuhudia akipakiwa garini.Chris aljitahidi kunisihi niwe mvumilivu katika wakati ule mgumu.Hata kama ungekuwa ni wewe mpenzi msomaji sina hakika kama ungeweza kuvumilia kumuona mtu unayempenda ambaye muda mfupi uliopita ulikuwa ukiongea naye na kucheka lakini ghafla anabadilika na haongei tena.
" Chris sijui nimemkosea nini Mungu .Ninaona ni kama ninaadhibiwa kila kukicha.Wakati nikiamini kwamba kwa sasa matatizo yote ninayaacha nyuma lakini linaibuka tena tatizo lingine. Sikutegemea kama lngetokea jambo kama hili kwa wakati kama huu.Clara alikuwa mzima wa afya na hakuwa na dalili zozote za ugonjwa .Sielewi ni kwa nini mambo haya yote yananitokea mimi tu..." nikamwambia Chris nikiwa katika gari lake tukielekea jijini Arusha tukimpeleka Clara katika hospitali ya St Patrick.
" Wayne naomba usife moyo ndugu yangu.Mungu wetu ni mwema sana na siku zote amekuwa akitusamehe makosa yetu hata tunapomkosea namna gani.Hii ni mitihani tu ya maisha ambayo hatuna budi kukabiliana nayo na inaweza ikampata mtu yeyote yule.Kitu cha msingi ni kukabiliana na ugonjwa huu wa Clara hadi apone.Nina uhakika katika hospitali ile ya St Patrick watamsaidia Clara na atapona kwa sababu kuna mama wa rafiki yangu naye alipatwa na matatizo kama haya ya Clara na akapelekwa pale lakini alipona na hadi sasa hivi huwezi kuamini kama alikuwa amepooza na hakuweza kuongea kwa muda wa miezi zaidi ya sita.Nina uhakika mkubwa sana hata Clara atapona na ataendelea na maisha yake kama kawaida." akasema Chris.
" Ninafikiria labda nimuhamishie nje ya nchi.." nikasema.
" Hapana Wayne.Bado ni mapema sana kufanya maamuzi hayo ya kumpeleka Clara nje ya nchi.Ugonjwa huu unaweza ukatibika hata hapa nchini.Kama litakuwa ni suala la kumpeleka nje ya nchi basi madaktari watatushauri hivyo lakini sina hakika kama kuna ulazima wa kumpeleka nje ya nchi" akasema Chris.
Sura ya Clara haikuweza kuondoka kichwani kwangu.Bado niliendelea kumuona akiwa katika tabasamu na kicheko chake kidogo
" masikini Clara..!!.." nikasema na kutoa kitambaa nikayafuta machozi ambayo nilishindwa kuyazuia kunitoka
" Its ok Wayne..usihuzunike sana .Clara atapona tu.Tunachopaswa kwa sasa ni kumuomba Mungu ampe uponaji wa haraka" akanipa moyo Chris.
" Chris hakuna ajuaye uchungu ninaousikia moyoni mwangu kwa sasa.Ninahisi ni kama moyo wangu unakatwa vipande vipande na kisu kikali sana.Ninasikia machungu ambayo hayaelezeki kwa maneno.Clara alikuwa ni maisha yangu.Clara alikuwa ni kila kitu kwangu. Clara amenifanya niyafurahie maisha japo kwa muda huu mfupi niliokaa naye. Clara ni mwanamke wa tofauti sana.Ana moyo wa ajabu na wa kipekee kabisa.Ana upendo wa dhati na wa kweli.Upendo wake unatoka ndani kabisa ya moyo wake.Kwangu mimi Clara namchukulia ni kama malaika anayeishi..Sikutegema hata siku moja kama angeweza kupatwa na maradhi kama haya.She doesnt deserve this Ouh Clara.why you..!!!..."
Chris akanitazama kisha akaendelea kuendesha gari.
" pamoja na yote yaliyotokea bado upendo wangu kwa Clara hauwezi kupungua.Hata kama itamchukua maisha yake yote akiwa kitandani..nitampenda Clara hadi siku ninaingia kaburini." nikasema nikiwa nimeinama chini.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Chris akasema
" Wayne kuna kitu nakifikiria"...Nikainua kichwa na kumtazama
" Kitu gani Chris? nikauliza
" I'm sorry to say this but I have bad feelings" akasema Chris
" What feelings? nikauliza.Chris akakaa kimya kidogo halafu akasema
" Inawezakana Emmy akawa anahusika na ugonjwa huu wa Clara" akasema Chris.Maneno yale ya Chris yakaifanya akili yangu ianze kufunguka .Muda huu wote sikuwa nimemuwaza tena Emmy.Akili yangu haikuweza kumkumbuka tena.
" Kwa nini umewaza hivyo Chris.? nikauliza
" Nimewaza hivyo kwa sababu ninamfahamu Emmy ana roho ngumu sana.Kama ameweza kumuua mwanae wa kumzaa mwenyewe hatashindwa kufanya kitu kama hiki kwa Clara.Hayo ni mawazo yangu tu Wayne na sina uhakika kama yanaweza kuwa ya kweli ama la" akasema Chris.Nilikuwa ni kama mtu niliyepigwa na bumbuwazi.Nilizama ghafla katika mawazo mengi.
" Wayne unawaza nini? akauliza Chris
" Chris umenikumbusha jambo ambalo sikuwa nimelitilia maanani kabisa.Maelezo yako yamenifanya nipate picha fulani .Usiku ule alipofariki Baraka dakika chache tu kabla ya kupokea simu ya baba mkwe akinitaarifu kwamba Baraka amefariki dunia ,Clara alikurupuka ndotoni .Alikuwa anaweweseka na jasho jingi kumtoka.Nilimuuliza amepatwa na nini akaniambia kwamba ameota ndoto ya ajabu sana na ya kutisha.Nilimuuliza ni ndoto ya namna gani aliyoota lakini hakuwa tayari kuniambia.Aliniomba tupige magoti tusali na tumtegemee Mungu.Sikuelewa alimaanisha nini kwa maneno yale.Baada ya muda mfupi baba mkwe akanipigia simu na kunitaarifu kwamba Baraka amefariki dunia.Ni usiku ule ambao Emmy alikuwa amekwenda kwa mganga Tanga.Jana asubuhi Emmy hakuonekana tena msibani.Hakuna aliyefahamu alikuwa amekwenda wapi.Nimeanza kupata picha kwamba Emmy anahusika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huu wa Clara.Aliapa kwamba atayafanya maisha yangu magumu na hii ndiyo kazi anayoifanya.Kwa nini amtese Clara kiasi hiki? Amemkosea nini? Kama alikuwa na kisasi na mimi alitakiwa kunitesa mimi na si Clara asiye na kosa lolote lile.Niliyemuacha ni mimi na hakupaswa kabisa kumgusa Clara. Kama ni kweli ni yeye ndiye aliyemfanya Clara hivi I swear this time ameingia katika moto.Mungu atanisamehe kwa nitakachomfanyia hayawani huyu" nikasema huku nikiuma meno kwa hasira.Chris akanitazama na kusema
" Wayne,ninamfahamu Emmy ni mwanamke mwenye roho ngumu sana na siku zote huwa hakubali kushindwa kwa maana hiyo anaweza akafanya jambo lolote lile ili kukipata kile anachokitaka. Kama lengo lake lilikuwa ni kupamaba na wewe basi nina uhakika mkubwa kwamba anaweza akawa amemfanyia Clara vile ili kulipa kisasi kwako..." akasema Chris.
" I swear this time I'm going to kill her " nikasema kwa hasira
" Wayne usiseme hivyo na wala usiweke ahadi yoyote ya kulipiza kisasi.Bado hatuna uhakika kwamba ni yeye ndiye aliyefanya hivi.Hizi ni hisia zetu tu.Kama ni yeye ndiye aliyefanya kitendo hiki basi fahamu kwamba hizi ni kazi za shetani.Shetani si lolote mbele za Mungu.Tunachotakiwa kufanya sisi ni kumtegemea Mungu na atamponya Clara.Mungu ni muweza na hashindwi na lolote. Siku zote tunaambiwa tumtegemeze yeye pekee.Tumuombee Clara apone na tumuombee pia Emmy." akasema Chris.Nilishangaa kidogo baada ya kumsikia Chris akiongea maneno yale.Toka nimemfahamu Chris sikuwahi kumsikia akiongea maneno kama haya .
" Chris ! umeongea maneno ambayo yamenistua sana.Sikuwahi kukusikia hata mara moja ukiongea maneno kama haya uliyoyaongea leo." Chris akatabasamu kidogo kisha akasema
" Wayne sikuwa nimekuambia lakini mimi kwa sasa nimeamua kujiweka karibu zaidi na Mungu na kuachana na haya mambo ya kidunia.Nimamua kupokea wokovu.Baada ya kitendo kile kilichotokea baina yetu niliamua kupokea wokovu na kwa sasa mimi ni mtu mpya kabisa na ndiyo maana nina uhakika mkubwa kwamba Clara atapona kwa nguvu za Mungu" akasema Chris.Ni kweli Chris alikuwa amebadilika sana kuanzia tabia na maisha yake kwa ujumla.Bado niliendelea kumshangaa.
" Usisahangae Wayne.Nimeamua kuyabadili maisha yangu.Kwa sasa moyo wangu una furaha na amani.Ninayafurahia maisha yangu ya sasa.Nitamuomba baba askofu ambaye atakuwa anamfanyia maombi Clara kila siku .Kwa maombi yetu na jitihada za madaktari wetu Clara atakuwa mzima tena." akasema Chris.Maneno yale yakaanza kuniingia.Kwa wakati huu nilikuwa tayari kwa lolote lile ambalo lingeweza kumsaidia Clara aweze kupona.
Mara simu yangu ikaita alikuwa ni baba mkwe.Alitaka kufahamu hali ya mgonjwa ilivyokuwa inandelea.Yeye alikuwa katika maandalizi ya kuja Moshi nikamtaarifu kwamba tunamuhamishia Clara katika hospitali ya St Patrick jijini Arusha kwa hiyo hana haja ya kusafiri kuja Moshi.Baba mkwe akaniambia kwamba anatangulia hapo hospitali na tutamkuta pale.Nilifarijika sana kwa namna watu walivyoonyesha kuguswa na ugonjwa ule wa ghafla wa Clara.Tulikuwa nyuma ya gari la wagonjwa lililokuwa likienda kwa kasi kubwa huku likipiga king'ora kuashiria kwamba lilikuwa na mgonjwa ndani yake.
Emmy aliwasili jijini Arusha .Alikuwa na hasira zisizo kifani kutokana na maneno aliyokuwa ameambiwa na rafiki yake kipenzi sheila.Moja kwa moja akaelekea nyumbani kwa wazazi wake.
" Ngoja kwanza nielekee nyumbani nikawasalimu kwa sababu nafahamu , lazima watakuwa walijiuliza maswali mengi sana kwa namna nilivyopotea ghafla.Niliondoka bila kumuaga mtu yeyote yule.Sitaki mambo yangu yajulikane kwa mtu yeyote .Nikishaweka mambo sawa pale nyumbani nielekee nyumbani kwangu nikapumzishe kichwa changu nitafakari namna nitakavyoanza mapambano upya.Kwa sasa ameongezeka adui mpya katika orodha ya maadui zangu.Sheila atanitambua.Sijafurahishwa hata kidogo na kashfa alizonipa. Bado hajaufahamu upande wangu wa pili ukoje.Amefanya kosa moja kubwa sana katika maisha yake.Hakupaswa kunitamkia maneno ya kashfa namna ile.Ameniudhi sana na kwa hili sintamsamehe hata kidogo.Nitamuhamisha katika jiji hili." Akawaza Clara.
Alifika nyumbani kwao na kuingia ndani.Mama yake pamoja na baadhi ya ndugu jamaa na majirani ambao bado waliendelea kuomboleza msiba ule wa Baraka walikuwa wamekaa sebuleni kwa majonzi.Mara Emmy akaingia ndani na kuwafanya wote wastuke wakabaki wamemtumbulia macho kama wameona mzuka.Emmy akawasalimu kisha akapita akaenda katika chumba kingine.Wote wakabaki midomo wazi kwa tabia ile ya Emmy.Mtu ambaye amefiwa na mwanae lakini haonyeshi hali yoyote ya majonzi wala kujali .Mama yake Emmy akamfuata Emmy chumbani na kumkuta amekaa peke yake katika mkeka.Akasimama akamuangalia bila kusema chochote
" Mama mbona unaniangalia namna hiyo? akauliza Emmy.Mama yake akamsogelea na kuketi pembeni yake.
" Emmy mwanangu umepatwa na matatizo gani?
" kwa nini mama? akauliza emmy
" Kwani hujui matatizo uliyonayo mwanangu? akauliza kwa upole mama yake.
" mama mimi mbona niko sawa na wala sina tatizo lolote lile."
" Emmy mimi ni mama yako na ninakupenda sana .Sikutegemea kabisa kama ungekuja kuwa namna hii."
" Kwani nikoje mama? akauliza Emmy huku ameinama chini
" Emmy umekuwa ni mtu wa ajabu sana.Kila mtu anashindwa kukuelewa.Mwanao Baraka amefariki dunia na wewe hukujulikana uko wapi. Umeendekeza starehe na ukamsahau kabisa mwanao.Mpaka leo hii hujui na wala hujauliza nini kilimuua mwanao. Kwako wewe umechukulia hili ni jambo rahisi sana lakini kwa kweli Emmy sisi wazazi wako tumeumia mno.Umetuumiza mno Emmy.Kingine ambacho umetufanya tuumie zaidi na tushindwe kukuelewa ni kitendo cha kuondoka msibani bila kuaga siku moja tu baada ya mazishi ya mwanao.Emmy wewe ni binadamu wa namna gani? Kila mtu anakusema wewe.Hapa mtaani tumepata aibu ambayo haielezeki." akasema mama yake Emmy .Emmy hakujibu kitu alikuwa ameinama chini .
" Baba yuko wapi ? akauliza Emmy.Mama yake akamtazama na kusema
" Ina maana hujasikia kilichompata mwenzako?
" Mwenzangu nani?
" Clara.Yule mwanamke ambaye yuko na Wayne kwa sasa"...akasema mama yake Emmy na kumfanya Emmy acheke kicheko kikubwa
" Mama unanishangaza sana.Clara atakuwaje mwenzangu wakati yeye ndiye aliyemchukua mume wangu? Kwani amefanya nini huyo Clara? akauliza Emmy kana kwamba hajui kilichomtokea Clara
" Amepatwa na ugonjwa wa ghafla na amepelekwa hospitali.Inasemekana amepooza mwili ."
" Amepelekwa hospitali gani?
" Nasikia amepelekwa St Patrick Hospital."
Huku akitabasamu Emmy akasema
" Mama mimi siwezi kusema kwamba nimeumia au ninasikia uchungu wowote kwa sababu ni huyu huyu Clara ndiye aliyefanya mimi na Wayne tukatengana. Kwangu mimi nimefurahi sana kwani hii ndiyo dawa yake na akome kurukia mabwana wa watu.." akasema Emmy huku akicheka.Mama yake akamuangalia kwa macho makali
" Emmy huna haya hata kidogo ..wewe ndiye unaweza ukasimama na kuthubutu kutamka hayo maneno uliyoyatamka? Huna aibu hata kidogo.Umemfanyia Wayne mambo mabaya na ya aibu ambayo hayaelezeki .Baada ya mambo yote haya uliyomfanyia mwenzio unaweza kweli leo hii ukathubutu kusimama na kumlaumu Clara..Hayawani mkubwa wewe" akasema mama yake Emmy ambaye alianza kupandwa na hasira.
" Mama kosa langu nini hadi uniite hayawani? akauliza Emmy
" Ndiyo wewe ni sawa na hayawani.Umekuwa na roho ya kishetani hasa siku hizi.Hata mwanao amefar............." akasema mama yake kwa ukali lakini kabla hajaendelea zaidi Emmy akasimama.
" Stop it mother...Tafadhali naomba mniache mimi na maisha yangu. Msinifuate fuate .Tayari umekwisha niita mimi hayawani na ninaomba uniache na maisha yangu kama hayawani.Narudia tena mama nawaombeni mniache mimi na maisha yangu na sitaki mtu yeyote yule ayafuatilie maisha yangu.Hakuna hata mtu mmoja aliye upande wangu kwa hiyo niacheni niishi mwenyewe.Niacheni nilie mwenyewe..." akasema Emmy kwa ukali huku akiinuka na kuondoka kwa kasi mle chumbani akapanda gari lake na kuondoka zake .Mama yake akabaki chumbani akilia.
" Kuanzia sasa sitaki kabisa mtu yeyote ayafuatilie maisha yangu.Si wazazi wangu au mtu yeyote yule mwenye ruhusa na maisha yangu .Nitayaendesha maisha yangu kwa namna ninavyotaka mimi na si kwa namna wanavyotaka watu..." akasema Emmy akiwa amefura kwa hasira
" Kumbe Clara amepelekwa St Patrick hospital..hahahaaa..nitakwenda kumtembelea jioni ya leo.Kwanza ninaanza na Sheila halafu nitakwenda kumtembelea Clara jioni ..Mimi ndiyo Emmy bwana.hahahaaa.." Emmy akaongea mwenyewe huku akicheka wakati akikata kona ya kuingia nyumbani kwake.
Baada tu ya kuingia ndani mwake Emmy akajitupa sofani.
" Uuphh ! siku ilikuwa ndefu sana." akasema Emmy kisha akainuka akaelekea katika friji akachukua vipande vya barafu na chupa ya mvinyo akajimiminia katika glasi.
" Home sweet home “ akasema Emmy akiwa amekaa sofani
“This is my life now..Haya ndiyo maisha yangu mapya.Nyumba imepoa utadhani hakuna binadamu anayeishi humu.Lakini haya ni mambo ya mud amfupi tu kwa sababu muda si mrefu nina hakika Wayne atarejea na nyumba itakuwa na furaha tena. Nataka niwakate vilimi limi wale wote waliokuwa wakinicheka kwamba nimeachika. Najua wako wengi ambao walikuwa wakinicheka baada ya Wayne kuniacha.Baada ya Wayne kurudi kwangu watanikoma. Kwa kweli nilimfanyia Wayne vituko vingi sana na sikufahamu thamani yake kwa wakati ule lakini kwa sasa ndiyo ninaiona thamani yake.Japokuwa nina kila kitu .Ameniachia nyumba,gari na biashara zote lakini vyote hivi haviwezi kunipa furaha ya maisha yangu. Kwa mara ya kwanza ninaliona pengo la Wayne katika maisha yangu. Ninaapa nitatembea hadi mwisho wa dunia hadi nihakikishe Wayne anarudi katika nyumba hii.Lazima niishi naye tena.Sintaweza kumpata mwanaume mwenye moyo wa upendo na uvumilivu kama yeye." akawaza Emmy huku akipiga mafunda ya mvinyo mfululizo .
" Sina muda wa kupumzika ngoja kwanza nimuendee Sheila .Amenidharau kiasi ambacho siwezi kuvumilia.Mimi huwa sipendi kudharauriwa na hilo analifahamu fika.Alikosea sana kunitolea maneno yale ya kashfa." akawaza Emmy kisha akaingia bafuni kuoga.
" Baba na mama watakuwa wamechukia sana lakini watanisamehe kwa sasa.Niko katika kipindi kigumu mno cha kumpigania Wayne.Siwezi kukubali kupokonywa Wayne toka katika mikono yangu.Lazima nipambane kumrudisha kwangu.Ninafahamu katika mapambano haya mambo mengi yatatokea na moja wapo ni hili la kumpoteza mwanangu Baraka .Inaniuma kumtoa mwanangu sadaka kwa mizimu lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya .Yote haya nimeyafanya kwa ajili ya kumrudisha Wayne kwangu." akawaza Emmy akiwa bafuni amejilaza katika jakuzi.Mara akakumbuka kitu akastuka.
" Nimemuwaza Baraka nimekumbuka kuhusu baba yake.Sheila aliniambia kwamba James anaweza akarejea siku yoyote katika wiki ijayo.Sijui nitamueleza nini ili aweze kunielewa lakini hilo haliniumizi kichwa.Kitu pekee ambacho kinaniumiza kichwa kwa sasa ni kumrejesha Wayne kwangu.Hili la James ni suala dogo tu.Nitamuelewesha kwamba mwanae alifariki ghafla na atanielewa.Isitoshe hajawahi kumuona Baraka hata mara moja kwa hiyo haliwezi kuwa suala litakalomuumiza sana." akawaza Emmy kisha akatoka mle bafuni akavaa na kuondoka.
Breki ya kwanza iilkuwa katika saluni ya Sheila.Ni moja kati ya saluni kubwa na ya kisasa jijini Arusha na ambayo kila dakika huwa inajaa akina mama wanaokuja kujiremba.Emmy akashuka garini na moja kwa moja akaelekea ndani ya saluni ile.Hakuitika salamu ya mtu yeyote na moja kwa moja akamfuata Sheila aliyekuwa anamsuka nywele mteja.
" Nimekuja sasa.Naomba unieleze mbele ya macho yangu yale maneno yako uliyoniambia katika simu" akafoka Emmy bila hata salamu.Watu wote mle ndani ya Saluni wakapatwa na mshangao. Emmy na Sheila wamekuwa marafiki wakubwa kwa miaka mingi na hakuna mtu aliyetegemea kama siku moja wangefikia hatua hii.Sheila akamuacha yule mteja aliyekuwa anamsuka na kumgeukia Emmy.
" Emmy tafadhali kama unataka kuongea na mimi si wakati huu.NItafute kwa muda wako tuongee na si sasa hivi." akasema Sheila ambaye naye sura yake ilionyesha kuwa na hasira kwa ujio ule wa Emmy
" Sina muda wa kukutafuta.Nimegundua kwamba wewe ndiye mchawi wangu.Sikujua Sheila kwamba wewe ni mwanamke mbaya sana na kumbe kuachana kwangu na Wayne umefurahia sana.Hasidi mkubwa wewe" akafoka Emmy
" Mchawi ni wewe mwenyewe wala usinitake maneno.Umeshindwa kumtunza bwana kwa uzembe wako mwenyewe hadi akakuacha.Waache wenye kujua kulea wamchukue wamtunze.Nakwambai utatafuta mchawi hadi mwisho wa dunia lakini mchawi ni wewe mwenyewe.Acha kuumiza watoto wa watu ambaohawana makosa " akasema Sheila.Emmy akapandwa na hasira akataka kumvaa Sheila lakini watu waliokuwemo mle ndani wakawahi kumzuia.
" Sheila naomba unisikilize vizuri.Kuanzia sasa mimi na wewe urafiki wetu umekwisha .Nimekuweka katika kundi la maadui zangu.Nitapambana na wewe na nitakuonyesha kwamba mimi ndiye Sheila .Nakwambia ndani ya siku saba utakuwa umelihama hili jiji.Pili nataka mpaka kesho jioni uwe umenirudishia milioni saba zangu ama sivyo nitakuja kuchukua kila kitu humu saluni kwa sababu hii ndiyo inakupa kiburi na dharau .Narudia tena kesho unirejeshee pesa zangu.Ukisihindwa kuzirejesha mpaka kesho jioni utanitambua mimi ni nani" akafoka Emmy kisha akachukua mkoba wake akauvaa begani na kuanza kutoka kwa hasira.Shughuli ndani ya saluni hii zilikuwa zimesimama kwa muda watu wote wakiushuhudia ugomvi kati ya marafiki wawili wakubwa.Hakuna aliyeamini kama urafiki wa Emmy na Sheila ungefikia hatua hii.Walikuwa ni zaidi ya marafiki lakini kitendo hiki cha kurushiana maneno kilizua maswali mengi sana miongoni mwa watu walioufahamu vizuri urafiki wao.Sheila alikuwa kimya na hakutaka kuzungumza lolote licha ya baadhi ya shoga zake kutaka kufahamu sababu iliyopelekea yeye na Emmy kutoleana maneno makali namna ile hadi kutaka kupigana. Sheila hakutaka kuongea lolote kuhusiana na kilichotokea,akapanda gari lake na kuelekea nyumbani kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ukweli niliompa Emmy umemuuma sana na sasa anataka mapambano na mimi.Mimi haniwezi bado ni msichana mdogo sana yule `kupambana na mimi.Anatakiwa ajipange vizuri kupambana na mimi. Anajivunia pesa alizonazo na uchawi anaotaka kujifunza.Mimi hanitishi kwa lolote lile na kama akihitaji kupambana na mimi nitapambana naye na atajuta kupambana na mimi.Mimi si kama hao akina Wayne ambao walikuwa wakimchekea kila alipokuwa akiwafanyia dharau." akawaza Sheila akiwa garini kuelekea nyumbani kwake.
" Najua lengo lake kwa sasa ni kutaka kuniaibisha kwa kunidai pesa alizonikopesha. N i pesa nyingi ambazo siwezi kumlipa kwa sasa.Amesema hadi kesho jioni niwe nimemlipa pesa zake na nisipofanya hivyo anaweza akaniaibisha kweli hayawani yule.Lazima nizitafute pesa hizo kwa kila jinsi leo hii ili niweze kumrejeshea Emmy kuinusuru saluni yangu .Saluni ile ndiyo pekee ninayoitegemea hapa mjini na lenbo lake ni kuifunga ili nikose kitu chochote cha kutegemea.Siwezi kukubali hilo litkee.Nitazitafuta pesa zake nimrejeshee.Lakini nani anayeweza kunipatia pesa hizo zote kwa muda huu mfupi? Sheila akazidi kuumiza kichwa.
" Mwanaharamu huyu amenipa wakati mgumu sana wa kuzitafuta pesa hizo.Lakini hakuna shaka nitazipata tu halafu nione atanitafutia wapi tena. Sikutegemea kama Emmy angefikia hatua hii aliyofika sasa hivi.Amemuua mwanae kwa ajili ya mwanaume ambaye hamtaki tena.Na siku ikitokea jamii ikajua kwamba amemuua mwanae kwa sababu ya kumrejesha Wayne kwake sijui watamfanya nini.James baba yake Baraka anarejea wiki ijayo sijui atafanya nini wapo ataufahamu ukweli kwamba Emmy alimtoa mwanae kafara kwa mizimu kwa ajili ya kurudiana na Wayne.Ninazifahamu siri nyingi za Emmy na ninaweza kuzitumia kumbomoa kabisa lakini sitaki kufanya hivyo .Kitu cha msingi ni kuachana naye kabisa na kumfuta katika orodha ya marafiki zangu.Kuna wazo nimelipata pengine linaweza kunisaidia kulitatua tatizo hili." akawaza Sheila.
" Chris anaweza akanisaidia kupata hizo pesa.Ninamfahamu Chris ni mtu pekee ambaye ananiamini na anaweza akanipatia kiasi hicho cha pesa kwa makubaliano ya kumrejeshea kidogo kidogo. Chris ni mtu mwelewa sana na isitoshe anamfahamu vizuri Emmy hivyo anaweza akanisaidia .Hata kama hatakuwa na fedha hizo anaweza akanidhamii mahala nikazipata.Ngoja nikifika nyumbani nimpigie simu" akawaza Sheila..
***********************
Clara alipokelewa katika hospitali ya St Patrick na kwa haraka akaanza kushughulikiwa.Huduma zilizokuwa zikitolewa na madaktari na wauguzi wa hospitali hii zilitia moyo sana.Kwa muda swa masaa mawili sasa tulikuwa tumekaa katika sehemu za kupumzikia tukisubiri taarifa ya madaktari waliokuwa wakimshughulikia Clara.Hospitali pale nilikuwa na rafiki zangu Beka na Chris pamoja na baba mkwe.Hawa ndio waliokuwa watu wangu wa karibu sana katika kipindi hiki kigumu cha ugonjwa wa Clara.Nilikuwa nimeinama nikiwa na mawazo mengi sana.Sikuwa naongea chochote kile.Nilikuwa katika maumivu makali sana ya moyo.Nilikuwa nikitafakari kwa kina juu ya kilichotiokea lakini sikuweza kupata jibu la haraka haraka nini hatima ya maisha yangu na mambo yanayozidi kunikuta.Tukiwa tumeketi pale sofani katika sehemu hii ya kupumzikia Chris akapigiwa simu akainuka pale sofani na kuijtenga mbali nasi.Wakati akiongea na simu baba mkwe akanigeukia na kusema
" Wayne nakuomba usihuzunike sana kijana wangu.Hii ni mitihani ya maisha ambayo inamkuta kila mtu kwa hiyo nakuomba uwe mvumilivu na tuzidi kumuombea Clara.Mungu atamsaidia atapona.Mungu ni muweza wa yote na hashindwi na kitu chochote.Tumtegemee yeye pekee." akasema baba mkwe.
" Ahsante baba.Ninaamini Clara atapona lakini ninaumia sana kumuona akiwa katika hali ile. Kuna wakati ninawaza sijui ni kwa nini nilikutana naye.Endapo nisingekutana naye haya yote yasingemfika.Ninaona ni kama vile mimi ndiye nliyesababisha haya yote kumtokea" nikasema
" Usiseme hivyo Clara.Jambo kama hili lingeweza kumtokea mtu yeyote yule na wala usijilaumu kabisa kwa jambo kama hili kumfika Clara.Kitu cha msingi tumkazanie matibabu atapona na kurejea katika hali yake ya kawaida." akasema baba mkwe.
Chris akarejea na kujiunga nasi pale sofani.Usoni pake hakuonekana kawaida.Sikumjali nikaendelea na tafakari zangu.Saa kumi na moja za jioni tukaitwa katika ofisi ya daktari Daktari yule mzungu ambaye alikuwa akifahamu Kiswahili kidogo alitutaarifu kwamba wamemchunguza Clara na wamegundua kuna ufa katika fuvu la kichwa na tayari matibabu yake yamekwisha anza mara moja.Alitusihi tuwe wavumilivu kwa wakati huu ambao Clara ameanza kupatiwa matibabu.Alitueleza mambo mengi kuhusiana na ugonjwa ule na kutupa moyo kwamba Clara atapona na wala hakuna haja ya kuwa na wasi wasi.
Baada ya maelezo yale ya daktari alitusihi tukapumzike kwani pale hospitali mgonjwa wetu atapata kila aina ya huduma inayotakiwa. Kabla hatujaondoka nilimuomba daktari anipeleke nikamuone Clara.Daktari akaniongoza hadi katika chumba alichokuwa amelazwa Clara .Nilimuinamia pale kitandania alipokuwa amelala amefumba macho. Sura yake nzuri ilikuwa imebadilika sana.Nilidondosha machozi kwa uchungu niliousikia.
" I'm sorry Clara kwa mambo haya kukupata.Nitaendelea kukupenda hadi mwisho wa uhai wangu" nikasema kimoyomoyo halafu nikatoka mle chumbani.
" Wayne jipe moyo ndugu yangu.Clara atapona tu.." akasema Beka baada ya kuniona jinsi nilivyobadilika baada ya kutoka katika chumba cha Clara.
" Wayne nina wazo moja." akasema Chris.
" Sikushauri urejee tena hotelini ulikokuwa unaishi.Nina nyumba kubwa na ninakuomba ukaishi pale kwangu kwa muda wote utakaohitaji.Wewe ni zaidi ya ndugu yangu nakuomba tukaishi wote nyumbani kwangu tafadhali." akasema Chris.Ulikuwa ni ushauri mzuri kwa sababu mpaka wakati huo nilikuwa sijapata nyumba ya kuishi.Nilikuwa nikiishi hotelini na Clara baada ya kumuachia Emmy nyumba yangu.Sikuwa na ubishi wowote kwa sababu tayari mimi na Chris tulikwisha zimaliza tofauti zetu.
Tuliwasili katika nyumba ya Chris maeneo ya Njiro.Chris alikuwa akishi na mdogo wake mmoja pamoja na mfanyakazi wa ndani.Nilikaribishwa ndani na kuonyeshwa chumba changu cha kulala.Nilimshukuru sana Chris kwa ukarimu wake huu mkubwa.Amekuwa ni msaada mkubwa sana kwangu kwa sasa.Baada ya kuoga niliitwa sebuleni kwa ajili ya chakula.Japokuwa sikuwa nikijisikia kula chochote niliamua kujilazimisha kula ili niweze kupata nguvu.Baada ya kula tulikaa sebuleni tukiangalia muziki wa Injili katika runinga kubwa iliyokuwamo mle sebuleni.Tukiwa bado sebuleni tukitazama muziki huku Chris akijaribu kunipa maneno ya faraja akinukuu vifungu vya biblia , mara akaingia mtumishi wa ndani.
" Kaka kuna mgeni wako" akasema yule mtumishi .
" Mkaribishe ndani" akasema Chris.
Nilishikwa na mshangao mkubwa baada ya kumuona Sheila akiingia pale mlangoni.Nilimtolea macho makali nikimtazama kama ni yeye kweli au nimemfananisha.Alikuwa ni mwenyewe .Sheila naye alistuka mno aliponiona nikiwa pale nyumbani kwa Chris.Nadhani hakutegemea kunikuta pale kwa Chris mida kama ile.Tulibaki tunatazamana .Nilikabwa na fundo kubwa moyoni kwani huyu ndiye alikuwa mshirika mkubwa sana wa Emmy.
***********************
Saa kumi na mbili za jioni Emmy akasimamisha gari katika maegesho ya hospitali ya St Patrick.Akashuka na kuelekea moja kwa moja eneo la mapokezi.
“ habari yako dada” akasema Emmy akimsalimu muuguzi aliyekuwapo mapokezi.
“ Nzuri dada karibu sana ” akajibu yule muuguzi
“ Samahani dada naomba kuuliza.” Akasema Emmy
“ Bila samahani dada unaweza ukauliza” akajibu yule muuguzi
“ Nina ndugu yangu mmoja ameletwa hapa mchana wa leo akitokea hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi.Nimeambiwa amelazwa hapa.” Akasema Emmy
“ Anaitwa nani mgonjwa wako?
“ Anaitwa Clara.”
Muuguzi yule akatazama katika kompyuta yake na kulikuta jina la Clara.
“ Clara ambaye amepatwa na matatizo ya kupooza mwili? Akauliza yule muuguzi.
“ Ndiye huyo huyo.” Akajibu Emmy
“ Amelazwa katika Private ward namba 4.” Akajibu yule muuguzi.
“ Ninaweza kuruhusiwa kumuangalia .?
“ Samahani dada yangu kwa muda huu huwa haturuhusu watu kuingia wodini kuwatazama wagonjwa.Mwisho wetu hapa huwa ni saa kumi na mbili za jioni” akasema yule muuguzi
“ Ninaomba unisaidie dada yangu ili niweze walau kumuona ndugu yangu .Nimekuja na ndege toka Dr es salaam baada ya kupata taarifa zake.tafadhali naomba unisaidie nimuone tu japo hata kwa dakika moja.Nakuomba sana dada yangu.” Akaomba Emmy.Muuguzi yule akaingiwa na roho ya imani akaamua kumsaidia Emmy kwenda kumuona Clara.Muuguzi yule akamuomba muuguzi mwenzake amshikie kwa muda pale katika dawati lake wakati anampeleka Emmy kumuona Clara.
“Mgonjwa wako ni huyu” akasema yule muuguzi walipofika chumbani kwa Clara.
Moyo wa emmy ukapatwa na furaha ya ajabu baada ya kumuona Clara akiwa amelala pale kitandani hajitambui.
“ Haya ndiyo malipo yako Clara kwa kupenda kuvamia waume za watu.Kama huu ndio mchezo wako basi safari hii uliingia sehemu mbaya sana.Na hili ni onyo kwa wengine wote ambao watajaribu kutaka kuwa na wayne.Wote nitawafanya hivi hivi.Wayne ni wangu na atabaki kuwa wangu milele.Nakusikitikia sana Clara kwa sababu utalala hapo kitandani kwa maisha yako yote yaliyobaki na utashangaa pale utakaposhudia Wayne akirudiana na mimi tena.Ona ulivyobadilika ghafla.Uzuri wako wote umepotea.Umekuwa ni kama kituko mbele za watu.Na huu ni mwanzo utateseka kwa maisha yako yote mshenzi wewe.Tena una bahati sana nilikuonea huruma ,nikaamua kukuacha hai.Wayne aliachana na mimi kwa sababu yako wewe.Wewe ndiye mchawi wa ndoa yangu lakini kwa sasa ujanja wako wote umekwisha .” akawaza Emmy wakati akimuangalia Clara aliyekuwa amelala pale kitandani.
“ dada nadhani kwa leo inatosha.twende tuondoke kwani daktari akikukuta huku juu saa hizi nitakuwa katika matatizo makubwa” akasema yule muuguzi.
“ nashukuru sana dada yangu kwa msaada wako” akasema Emmy kisha akaifungua pochi yake na kuchomoa bunda la noti nyekundu akampatia yule muuguzi kiasi cha shilingi elfu hamsini.
“ Chukua hizi ni ahsante yangu kwa msaada wako” akasema Emmy na kumpatia yule dada pesa zile ambaye alibaki akishangaa asiamini macho yake..
“ Ahsante sana ” akasema yule muuguzi huku akiufunga mlango wa chumba kile cha Clara.
“ Hujaniambia jina lako unaitwa nani ? akauliza Emmy wakati wakishuka ngazi
“ Ninaitwa Agnes “ akajibu yule muuguzi
“ Nafurahi kukufahamu Agnes.mimi ninaitwa Emmy” akajibu Emmy
“ hata mimi nafurahi kukufahamu Emmy “ akajibu Agnes.
“ Agnes kama hutajali unaweza ukanipatia namba yako ya simu? Ninaweza kuwa nakupigia ili kujua maendeleo ya mgonjwa wangu. kwa sababu mimi ni mtu wa kusafiri safiri sana .”
Bila kusita Agnes akampa Emmy namba yake ya simu halafu naye akachukua ya Emmy.
“ nashukuru sana kwa msaada wako Agnes.Tutazidi kuonana.Nitakuwa nikija mara nyingi tu kumjulia hali ndugu yangu” akasema Emmy
“ Karibu sana dada Emmy.Mara nyingi huwa ninakuwepo zamu ya usiku.” Akajibu Agnes.
Emmy akaingia katika gari lake na kuondoka.
“ Clara kwisha habari yake kwa sasa uwanja ni mpana kwangu kumrudisha Wayne.Namshukuru sana mzee Mtuguru kwa msaada wake huu.Nitamtafutia zawadi kubwa sana yule mzee .Hizi tiba za asili zinasaidia mno lakini watu wanazidharau.Ingawa wakati mwingine zinaweza kukugharimu uhai wa mtu kama ilivyonigharimu mimi lakini zinasaidia sana.Kwa sasa ninahesabu masaa tu kabla ya Wayne hajarejea tena nyumbani kwangu.Ninachotakiwa ni kuanza kufanya maandalizi kuanzia pale nyumbani. Itanibidi nipake nyumba rangi ,ikiwa ni pamoja na kubadilisha fenicha na kila kitu ndani ili Wayne atakaporejea tena nyumbani akute mabadiliko makubwa sana . “ akawaza Emmy huku akitabasamu usoni .
Nilipandwa na hasira kwa kumuona Sheila pale nyumbani kwa Chris.Nilisimama huku uso wangu ukiwa umejikunja kwa hasira.Midomo ilikuwa inanitetemeka.Huyu ndiye alikuwa rafiki mkubwa wa Emmy na ndiye alikwenda naye kwa mganga Mombo na kumuua Baraka.Chris aliniangalia mimi halafu akamuangalia na Sheila ambaye bado alikuwa amesimama akitetemeka alikosa neno la kusema.Midomo yake ilikuwa inamtetemeka.
“Sheila unatafuta nini huku? Emmy amekutuma uje unipeleleze? Amekutuma uje unimalize na mimi? Haya yote miliyoyafanya hayawatoshi hadi mnifuate huku? Nimewakosea nini hadi mnifanyie ukatili wa kiasi hiki? Clara amewakosea nini mpaka mumtese kiasi kile? Nikasema kwa ukali huku nikimuangalia Sheila kwa macho makali,akaogopa sana.Akiwa bado amesimama pale mlangoni ghafla kwa kasi ya ajabu nikamfuata na kumshika mkono nikamvuta kumtoa nje
“ Toka ndani ya nyumba hii muuaji mkubwa wewe.Kamwambie huyo aliyekutuma kwamba siku zake zinahesabika na malipo ni hapa hapa duniani” nikasema kwa ukali.Chris akaniwahi na kunizuia
“ Wayne ! tafadhali punguza hasira.” Akasema Chris
“ siwezi kupunguza hasira Chris..Huyu ndiye mshirika mkubwa wa Emmy na ametumwa aje animalize.Tafadhali Chris niache nimshughulikie.Wamemuua Baraka ,na sasa wanamtesa Clara ambaye hana kosa lolote na kama haitoshi bado wananifuata hadi huku..” nikasema kwa ukali
“Wayne nakuomba ndugu yangu punguza hasira na tumsikilize Sheila amekuja kutafuta nini.” Akasema Chris huku akimshika mkono Sheila na kumuingiza ndani.Alikuwa analia.Nilitamani kumshushia kipigo kitakatifu mwanamke Yule lakini nikaheshimu ushauri wa Chris kwamba tumsikilize Sheila amekuja kutafuta nini usiku ule.
“ Sheila karibu sana.Habari za huko utokako? Akasema Chris .Sheila akafuta machozi na kusema kwa sauti ndogo
“ Kwema”
“ Nashukuru kusikia hivyo.Karibu sana” akasema Chris
“ ahsante Chris”
“Sema kilichokuleta na uondoke hapa haraka sana.Una bahati hapa ni nyumbani kwa Chris .Ingekuwa ni nyumbani kwangu nakuapia ningekukata shingo.Nakuchukia sana Sheila wewe na shoga yako Emmy” nikasema na kumfanya Sheila aendelee kuangusha machozi.
“ Hutaki kueleza alichokutuma muuaji mwenzako? Nikasema kwa ukali huku nikisimama kumuendea pale sofani
“Sijaja hapa kwa sababu ya Emmy na wala hajanituma chochote” akajibu Sheila baada ya kuona ninamuendea.
“Nini kimekuleta hapa basi kama Emmy hajakutuma? Nikauliza
“ Nimekuja kwa ajili ya maongezi na Chris na sikutegemea kama nitakukuta huku” akasema Sheila.Nikarudi mahala pangu na kukaa
“Nakusikiliza Sheila.ulikuwa na shida gani nami? akauliza Chris
“ Samahani Chris tunaweza tukaongea nje?
“ Hapana tuongelee hapa hapa mbele ya Wayne.Una tatizo gani?
Huku akisita Sheila akasema
“Nimekuja ninahitaji msaada wako Chris”
“ Msaada gani Sheila?
“Ninahitaji unikopeshe fedha”
“ Shilingi ngapi unahitaji?
“ Nahitaji shilingi millioni saba”
“ Millioni saba? Mimi na Chris tukastuka kwa pamoja
“ Ndiyo ninahitaji unikopeshe kiasi hicho cha fedha au hata kama huna basi nitafutie hata kwa marafiki zako na nitakurejeshea ndani ya kipindi kifupi”
“ Dah ! hizo ni fedha nyingi sana Sheila..una zihitaji lini na kwa tatizo gani?
“ Ni kweli ni fedha nyingi lakini ninakuahidi nitazirejesha ndani ya kipindi kifupi.Ninazihitaji kabla ya kesho jioni”
“ Kabla ya kesho jioni? Hilo haliwezekani Sheila.fedha hizi ni nyingi na hakuna uwezekano wa kuzipata ndani ya kipindi kifupi namna hiyo.Inahitaji muda kuzitafuta” Akasema Chris.Sheila akaonyesha uso wa kukata tamaa kwa jibu lile
“naomba unisaidie Chris.Nina shida kubwa na ya haraka” akasema
“ Una tatizo gani Sheila? Nikauliza.
“ kweli Sheila hebu tueleze una tatizo gani ili tufahamu pengine kunaweza kuwa na namna bora zaidi ya kukusaidia kulitatua tatizo lako” akasema Chris.Sheila akajikaza na kusema
“Nimekorofishana na Emmy na amenitaka nimlipe pesa zake alizonikopesha kwa ajili ya kufungua ile saluni.Ameahidi kunidhalilisha kama mpaka kesho jioni sintakuwa nimempatia pesa zake zote” akasema Sheila.Nilishindwa kujizuia nikacheka
“ Sheila huo uongo wako kamdanganye mtu mwingine na si mimi .Chris tafadhali usimsikilize huyu mwanamke.Kuna jambo lililomleta hapa na si hilo.Huyu hawezi hata siku moja kukorofishana na Emmy.Huyu ndiye mshauri wake mkuu na mambo yote haya ambayo Emmy amekuwa akiyafanya huyu ndiye mshauri wake” nikasema
“ Ni kweli Wayne nimekosana na Emmy naomba mniamini.”
“ Nini kimesababisha mkakorofishana? Akauliza Chris
“Kwanza kabisa naomba nikiri kwamba ni kweli kama anavyosema wayne kwamba mimi na Emmy tulikua marafiki wakubwa na kila mara Emmy alikuwa anakuja kuniomba ushauri lakini jambo moja ambalo nyote hamlifahamu ni kwamba sikuwa namkubalia Emmy katika masuala yote aliyokuja kuniambia lakini alikuwa mbishi na nyote mnamfahamu Emmy akiamua jambo hataki mtu mwingine amshauri visivyo”
“ Usitudanganye Sheila.Wewe si uliambatana na Emmy kwenda kwa mganga Mombo na mkamuua Baraka? Nikauliza.Sheila akakaa kimya
“ Mbona hujibu? Kama si kweli weka wazi” nikasema
“Ni kweli Emmy aliniomba niambatane naye kwa mganga kule Mombo” akasema Sheila
“ Nini lilikuwa dhumuni la kwenda kule na kitu gani kilifanyika? Nikauliza
“Emmy alidai kwamba kuna mtu aliyekuwa anamroga na ndiyo maana ukaamua kuachana naye kwa hiyo alitaka kwenda kumfahamu mtu huyo.Tulifika pale na dawa ikafanyika usiku…” Sheila akasita
“ Nini kikaendelea? Nikauliza
“ Ndiyo kama hayo yaliyotokea.Tulipofika hapa tukaambiwa kwamba Baraka amefariki ghafla” akasema
“Unataka kututhibitishia kwamba hamkujua toka mkiwa kwa mganga kwamba Baraka amefariki dunia?
“Mimi nilikuja kufahamu baada ya kufika huku Arusha lakini Emmy alionekana kufahamu kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa akifanyiwa dawa usiku ule na hata wakati wa msiba aliniambia kwamba hakujua kama Baraka alikuwa anatolewa kafara kwa mizimu kama malipo ya kukurudisha mikononi mwake.” Akasema Sheila na kwa hasira nikainuka.Chris akaniwahi na kuniomba niketi
“Jana alinitaka nimsindikize tena kwa mganga lakini nikakataa akaenda mwenyewe.Wakati akirudi akanipigia simu na kunitaarifu kwamba tayari amekwisha mmaliza Clara.Nilimweleza ukweli kwamba anachokifanya si kitu kizuri na kwamba aache kuwaumiza watu wasio na makosa.Kauli ile hakuipenda ndiyo maana akaamua kuja na kutaka kunidhalilisha.Kwa hivi saa urafiki wetu umekufa.wayne ninaomba msamaha sana kwa kushirikiana na Emmy.Najua tumekukosea sana na sijui nitafanya jambo gani ili uweze kunisamehe.” Akasema Sheila huku akitoa machozi.Nikamuangalia kwa macho makali na kusema
“ Kitu kimoja tu ambacho unaweza ukafanya kitakachonifanya nikusamehe.Nataka Clara arudishwe katika hali yake ya kawaida.Hapaswi kuteseka bila kosa.Ukiweza kulifanya hilo nitakusamehe Sheila na nitajua kwamba ni kweli unajutia ulichokifanya” nikasema na Chris akageuka na kunitazama..Sheila akainama chini
“ Unaweza ukafanya hivyo? Nikamuuliza
“ Wayne aliyefanya mambo haya ni mganga wa kienyeji na mimi sina nguvu zozote za kuweza kutengua uchawi huu alioufanya.Ninachoweza kufanya mimi ni kwenda kumuomba Yule mganga aweze kumponya Clara na amrudishe katika hali yake ya kawaida” akasema Sheila
“Unapakumbuka mahala anakoishi huyo mganga? Nikauliza
“Ndiyo napakumbuka”
“ Kesho asubuhi mimi na wewe tunaongozana hadi kwa mganga Mombo.Nataka nikaongee naye mimi mwenyewe na kama akishindwa kufanya ninavyotaka basi ama zake ama zangu” nikasema kwa hasira
“ Wayne..!! akasema Chris
“Chris niache niende kwa huyo mganga siku ya kesho.Nataka akatengue kila kitu alichomfanyia Clara.Siko tayari kumuona akiendelea kuteseka namna ile bila kosa” nikasema huku machozi yakinilenga kila pale sura ya Clara iliponijia kichwani
“Wayne sikushauri uende huko kwa mganga.Hizi ni nguvu za giza na siku zote nguvu za mwovu si lolote mbele ya nguvu za Mungu.Tumtumaini Mungu pekee na atamponya Clara.Atazivunja vunja nguvu zote za giza na Clara atakuwa mzima tena.Nimekwisha ongea na baba askofu na ameniambia kwamba kuanzia kesho atakuwa akienda kumfanyia maombi Clara mchana na jioni.Tafadhali naomba tumuachie Mungu tatizo hili” akashauri Chrishttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ Chris najua kwa sasa wewe umeokoka na unamuamini Mungu na hata mimi ninamuamini Mungu lakini kwa hali aliyonayo Clara inanilazimu kumfuata huyo mganga na kumtaka atengue uchawi wote aliomroga Clara.Clara hawezi kuendelea kuteseka wakati mtu aliyemroga yupo na anajulikana.Kesho asubuhi ninamfuata huko huko Mombo” nikasema halafu kikapita kimya kifupi
“ Chris kwa hiyo utanisaidia kuhusu ule msaada niliokuomba? Akauliza Sheila
“Nashinda kukupa jibu Sheila kwa sababu mambo yangu kifedha hayaniendei vizuri sasa hivi.Nadhani ungenipa muda wa kama siku mbili hivi ili nikutafuitie hizo pesa” akasema Chris
“ Nitakukopesha mimi hizo fedha lakini mpaka baada ya kurejea toka kwa huyo mganga huko Mombo.” Nikasema
* * * *
ITAENDELEA SEHEMU YA MWISHO KESHO SAA SITA MCHANA HAPA HAPA
No comments: