Zijue faida zitokanazo na kula nyanya chungu/Ngongwe

Baadhi yetu tunapendelea kula vitu vitamu vitamu na vile ambavyo tunahisi havina ladha au vyenye ladha ya ukakasi tukawa tunavipa mgongo. Asikudanganye mtu licha ya Nyanya chungu kutokuwa na ladha (kuwa chungu) kama jina lake lakini ina faida lukuki mwilini mwako.

Baadhi ya faida hizo ni kama:-
Chanzo kikubwa cha Vitamin A, B na C.
Kuimarisha kinga ya mwili.
Kuzuia magonjwa ya Kisukari.
Kuzuia maradhi ya Moyo.
Chanzo cha madini chuma na Potassium.
Zina kiwango kikubwa cha maji.
Kurekebisha mzungumko wa hedhi kwa wanawake.
Kutibu matatizo ya tumbo la uzazi, kusafisha na kulinda mfuko wa uzazi.
Ina Vitamin K ambayo huboresha mzunguko wa damu mwilini (Mzunguko mzuri wa damu ni muhimu zaidi kwa wanaume).
Kuongeza ashki na stamina ya mapenzi, ikiliwa kwenye mboga au juisi pamoja na maganda yake.
Kupunguza maumivu ya tumbo la hedhi.

Mbali na hayo, ngogwe ni dawa inayofanana na antibiotic, hivyo ni tunda zuri endapo likitumiwa mara kwa mara husaidia kuua vijidudu vya aina mbalimbali mwilini.

Aidha Vitamin K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.


USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.