Simulizi: Je haya ni mapenzi? Sehemu Ya 44

Nyumbani kwakina Sabrina nako hali haikuwa nzuri kutokana na maneno ya shangazi yao,
"Kwakweli mimi kukaa kimya siku zote sitaweza, ipo siku nitasema ukweli tu"
Mama wa Sabrina alimuangalia wifi yake kwa jicho la chuki ya wazi wazi kwani yeye hakupenda mwanae aathirike kisaikolojia kabisa.
"Ila wifi yangu kwanini unakuwa hivyo jamani? Hayo mambo si yalishapita tayari ila wewe kutwa kucha kuyafufua sijui una matatizo gani wewe. Najuta hata kumpa mwanangu jina lako"
Muda huo James na mkewe Joy walikuwa wanajiandaa kuondoka, shangazi mtu akaona kachukizwa na kuwaambia,
"Nyie watoto kabla hamjaenda nina mazungumzo nanyi"
"Uzungumze nao nini sasa? Mbona unapenda kukuza mambo jamani? Ndiomana kipindi kile ukasumbuliwa na majini kwa umbea wako"
"Aaah mie mbea wifi? Leo umeamua kunitusi si ndio, sasa subiri nitakuonyesha umbea wangu vizuri ulivyo"
Shangazi akawa amechukia na kuchukua mkoba wake na kuondoka.
James na Joy walipotoka ndani wakashangaa kutokumkuta, James akamuuliza mama yake,
"Shangazi yuko wapi?"
"Achaneni nae yule, huwa ana matatizo kwenye akili yake"
James hakutaka kumuhoji zaidi mama yake kwani alimuona tayari akiwa amevimba kwa hasira.
Kwahiyo wakamuaga na kisha wao kuendelea na safari yao kwa wakati huo.

Sam naye aliingia chumbani na kumuangalia Sabrina akimnyonyesha yule mtoto.
Kisha Sam akawa kama anamchungulia mtoto na kusema,
"Mtoto ni mzuri sana, Mungu amsaidie asifate tabia yako"
Sabrina akamuangalia tu Sam, muda kidogo simu ya Sam ikaanza kuita, kuangalia mpigaji alikuwa ni mama yake.
Sam aliongea na ile simu huku akitabasamu ila kiuhalisia alikuwa akifikicha macho.
Alipomaliza kuongea nayo akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Mama anakusalimia sana"
"Nashukuru"
Simu ya Sabrina nayo ikaanza kuita na aliyekuwa anapiga kwake alikuwa ni mama yake, Sam akamwambia Sabrina aweke sauti kubwa ili naye amsikie.
Sabrina hakusita na kuweka,
"Sabrina, hivi bado unamnyonyesha huyo mtoto?"
"Ndio mama"
"Muachishe ziwa mwanangu, si u mjamzito wewe!"
"Kwani kuna tatizo mama?"
"Ndio ni tatizo, utamuharibu mtoto. Nenda umtafutie maziwa ya kopo ya watoto au ya ng'ombe umpe ila usimnyonyeshe tena"
Kisha wakamaliza maongezi yao, Sam akamuangalia Sabrina na kumwambia,
"Starehe zako na tamaa yako vinakuponza sasa, vinafanya mtoto wako akose haki yake ya msingi. Hivi Sabrina ulijifikiria nini hadi kubeba mimba tena? Tena mimba isiyokuwa ya mumeo? Ulijifikiria nini Sabrina?"
Sabrina hakujibu ila alikazana kumnyonyesha mtoto,
"Hivi alichoongea mama yako hujakisikia au ni nini?"
Sabrina machozi yakamtoka,
"Nisamehe Sam"
"Sio nikusamehe, mtoto huyu kila siku anaharisha kumbe ni sababu ya maziwa yako machafu unayomnyonyesha. Muache nikamnunulie maziwa"
Sam aliinuka na kuondoka.
Sabrina alijifikiria sana, alishindwa kujielewa mambo anayoyafanya.
Alimuangalia mtoto wake, aliangalia tumbo lake kisha machozi yakamtoka.
Ila muda wote alijiuliza,
"Je haya ni mapenzi? Sielewi, huyu Sam simuelewi"
Alijiuliza tu na alikuwa ameshika tama hadi pale Sam aliporudi na maziwa ya kumkorogea mtoto.
Walimpa mtoto maziwa na kulala bila ya kuongezea neno lolote lile.

Kulipokucha, asubuhi na mapema kama kawaida Sam aliinuka na kujiandaa kisha kuondoka.
Sabrina hakuwe9a kuuliza ingawa alijua wazi kuwa ile ni siku ya mapumziko yani mwisho wa wiki ila anaanzaje kumuuliza ikiwa tayari anamajanga.
Sam alipoondoka, ndipo Sabrina nae alipoinuka na mtoto na kuanza kumsafisha.
Alipomaliza kazi zake za hapa na pale, akataka kutoka nje angalau akaone mwanga wa jua.
Ila alipojaribu kufungua mlango wa kutokea nje akaona mlango ni mgumu na kugundua kuwa umefungwa kwa nje.
Akajiuliza kuwa kwanini mlango ufungwe, akaenda dirishani na kufungua dirisha kisha kumuita mlinzi ambapo mlinzi alifika na kumsikiliza,
"Mbona mlango umefungwa kwa nje?"
"Sijui kwanini, ila mzee mwenyewe alisema kuwa umpigie simu na kumuuliza yeye"
Sabrina alitulia kidogo na kurudi kukaa sebleni huku akijiuliza kuwa kwanini Sam amfungie nje? Na kumuuliza alishindwa na kujipa moyo tu ndani kuwa amsubirie arudi.

Dorry baada ya kuona kuwa hakuna chochote alichoulizwa na Sakina, akaamini kuwa Mungu amejibu maombi yake kwa kumfanya Sakina asijue chochote kuhusu ile mimba kuwa haihusiani na mtoto wake.
Muda kidogo Sakina mwenyewe akampigia simu,
"Nimekukumbuka sana Dorry, utakuja lini mwanangu?"
"Nitakuja mama, usijali"
"Vipi na mjukuu wangu tumboni huko anaendeleaje?"
Dorry akacheka kidogo na kujibu,
"Anaendelea vizuri tu"
"Uje jamani, mwenzenu nimewakumbuka huku. Napatwa na majanga peke yangu ila mkija nyie itakuwa kheri"
Dorry akafurahi na kumuahidi Sakina kuwa ataenda kwake hivi karibuni.

Sakina alipomaliza kuongea na Dorry, akampigia simu Sabrina.
Ila alimshangaa Sabrina kuwa mnyonge vile.
"Ila mdogo wangu ubishi utakuponza, mi nilikwambia kuhusu yule mtaalamu umekataa bure tu. Mwenzio toka siku ile mauzauza hayapo tena, watu wabaya sana duniani. Yule mtaalamu anasaidia mdogo wangu"
"Sawa dada nimekuelewa, basi acha nifikirie kwanza"
"Fikiria mdogo wangu na utakapokuwa tayari niambie nikupeleke, yani mwenzio hapa naishi kwa amani na furaha saivi, yale mauzauza hayapo tena"
Walipomaliza mazungumzo yao na kuagana, Sabrina akaikata ile simu na kuwaza kuwa huenda mtaalamu huyo anaweza kumsaidia,
"Hofu yangu ni moja tu, hawa wataalamu hawakawii kunipa masharti ambayo hayana maana yoyote kwangu. Mi nawaogopa jamani ila nitaangalia tu"
Alikuwa akingoja kuona pale atakapofika mwisho kabisa wa mawazo yake basi ndio akubali kwenda kwa huyo mtaalamu.

Mama wa Sabrina akiwa ametulia nyumbani kwake, muda kidogo akajiwa na ugeni na kumfanya ashangae.
"Kheee James!!"
"Ndio ni mimi, au unadhani umeona mzimu? Maana siku ya mahari ulizimia"
Mama wa Sabrina alikaa kimya na kumkaribisha.
"Karibu sana"
"Asante nimeshakaribia"
Moja kwa moja James akaingia ndani na kukaa, kisha akamwambia mama wa Sabrina,
"Joy, nimekuja kwako leo. Naomba uniambie ukweli wa mambo yote"
"Unamaanisha nini? Mbona sikuelewi?"
"Hunielewi nini? Niambie ukweli kuhusu mtoto wangu Joy, mi sielewi yani sielewi kabisa ila nimeambiwa kuwa kuna mtoto wangu na ukweli wote unaujua ila ulinificha, tafadhari nakuomba Joy niambie ukweli"
"Hivi ni nani amekwambia hayo maneno James jamani? Nani huyo aliyekuletea hayo maneno ya uongo jamani?"
"Joy, mtu aliyeniambia ni wa kuaminika kabisa. Tafadhari niambie wewe mwenyewe ukweli kabla sijagundua kwa namna nyingine"
Joy akafikiria na kuona wazi kuwa kuna uwezekano wifi yake Sabrina atakuwa ameyapeleka yale maneno kwa James.
Hata hakujua ni kitu gani amwambie huyu James ili aweze kumuelewa ikiwa tu ameshaambiwa kila kitu.
James akamshtua tena kwa kumwambia,
" Nangoja ukweli Joy tafadhari niambie"
Muda kidogo akasikia mlio wa gari, kuangalia alikuwa ni mumewe amekuja yani baba yao na wakina Sabrina.

Sam alikuwa maeneo ya baa na mmoja wa rafiki zake, ambapo alimshangaa Sam kwa ule muonekano wake wa siku hiyo,
"Hivi Sam mbona leo upo hivyo? Unaonekana kuwa na mawazo"
"Ni kweli nina mawazo, zamani nilikuwa nashangaa sana kusikia mume kaua mke na watoto wake. Kumbe huwa kuna sababu nyuma ya pazia inayompelekea kufanya hivyo"
Rafiki wa Sam aliyashangaa maneno ya Sam na kumuuliza,
"Sijakuelewa Sam, unamaana gani?"
"Maana yangu ni hiyo hiyo unayoifikiria wewe"
"Nieleweshe tafadhari"
"Aaaah tuachane na hizo mada, hapa tunywe halafu kila mmoja akapumzike kwake"
Muda kidogo Sam akaonekana kama akifikiria kitu fulani kisha akainuka na kumuaga rafiki yake kuwa anarudi nyumbani kwake.

Sabrina akiwa amekaa sebleni kwa muda huu bila ya kuwa na habari yoyote zaidi ya kufikiria matatizo yanayomkabili.
Muda kidogo akasikia mlango ukifunguliwa, kisha Sam akaingia ndani.
Akamsogelea Sabrina na kutoa bastora kisha akailengesha kwenye kichwa cha Sabrina na kumfanya Sabrina ashangae sana kuwa Sam amepatwa na nini.
Muda huo huo simu ya Sabrina ikaanza kuita, akamsikia Sam akisema kwa ukari
"Pokea hiyo simu Sabrina na uweke loudspeaker"
Sabrina alipoiangalia ile simu akaona ni namba ya nchi za nje, moja kwa moja akapatwa na hisia kuwa mpigaji atakuwa ni Jeff na kumfanya atetemeke zaidi.

Muda huo huo simu ya Sabrina ikaanza kuita,
akamsikia Sam akisema kwa ukari
"Pokea hiyo simu Sabrina na uweke loudspeaker"
Sabrina alipoiangalia ile simu akaona ni namba ya
nchi za nje, moja kwa moja akapatwa na hisia kuwa
mpigaji atakuwa ni Jeff na kumfanya atetemeke
zaidi.
Sabrina akiwa ametawaliwa na uoga, akashtuliwa tena na sauti kali ya Sam,
"Pokea hiyo simu Sabrina, ole wako ikatike"
Sabrina aliipokea ile simu huku akitetemeka sana na kuiweka sauti kubwa kama alivyoamriwa na Sam.
Moja kwa moja upande wa pili ukaanza kuongea,
"Shikamoo Mamdogo"
Sabrina hakuamini masikio yake kuwa ni Jeff kamsalimia hivyo na kujikuta akijibu kwa kutetemeka,
"Marahaba"
"Kheee mamdogo kimya kabisa tangu nimeondoka, huwa nawasiliana na bamdogo tu. Unaendeleaje lakini?"
"Naendelea vizuri"
"Vipi mdogo wangu Cherry hajambo? Nimekakumbuka sana hako katoto"
"Hajambo"
"Mbona unanijibu kwa mkato hivyo mamdogo? Una matatizo gani au unaumwa?"
"Hapana siumwi"
"Sasa mbona unaongea kwa kupooza kiasi hicho? Utakuwa unaumwa wewe, ngoja nitampigia simu bamdogo nimuulize. Mi nilikuwa nakusalimia tu, wasalimie wote hapo"
"Haya"
Kisha ile simu ikakatika, Sabrina bado hakuamini kama aliyekuwa akiongea nae kwa muda huo alikuwa ni Jeff kweli, bado alikuwa kaduwaa kuwa imekuwaje Jeff akaongea kistaarabu kiasi kile.
Akamuona Sam akishusha ile bastora yake na muda kidogo simu ya Sam nayo iliita, naye aliipokea kwa kuweka sauti kubwa, mpigaji alikuwa ni Jeff yule yule.
"Shikamoo bamdogo"
"Marahaba, hujambo"
"Sijambo, muda mfupi uliopita nimeongea na mamdogo anaonekana kupooza sana sijui anaumwa?"
"Aah usijali, nipo nae hapa"
"Sawa basi mi nilikuwa nawasalimia tu"
Kisha akaagana nae na kukata simu.
Sam akamuangalia Sabrina kisha bila ya kusema chochote akaenda chumbani.

Mama wa Sabrina akamkaribisha mumewe ndani, na kumfanya ashangae ule ujio wa James pale.
Kitu pekee alichokijua Deo kuhusu James ni kuwa baba mzazi wa mkwe wao Joy ila alisahau kabisa kama huyu James ndiye aliyekuwa mwalimu wa kwaya wa mke wake.
Kwahiyo alipomuona hapo hakushangaa sana na kujua kuwa amepita kusalimia ukizingatia wameshaweka kama undugu kwa watoto wao kuoana.
Deo akamsalimia James pale na kumkaribisha bila kujua jambo lililompeleka James pale nyumbani kwake.
Mama wa Sabrina alijifanya kwenda jikoni kumuandalia mumewe na kumfanya James aage na kuondoka zake.

Sabrina hakuamini kama amepona kweli, pia hakujua kwanini Sam alimnyooshea bastora,
"Inamaana leo ndio ingekuwa mwisho wangu, maisha gani haya ya kuishi roho juu juu kiasi hiki?"
Alikuwa pale pale akisikitika.
Muda kidogo Sam alitoka chumbani huku akiwa amembeba yule mtoto wao mdogo Cherry na kufika nae sebleni kisha kukaa nae karibu na Sabrina, na kuanza kusema,
"Nampenda sana huyu mtoto, siku zote mshukuru huyu mtoto Sabrina kwani huyu mtoto ndiye aliyeokoa maisha yako. Ulipata mimba kwa kubakwa ndio, hilo sijakataa wala kupinga. Ila swali linaloisumbua akili yangu kwasasa ni kuwa hiyo mimba nyingine uliyonayo ni ya nani? Najua hapo hukubakwa na baba wa mtoto unamjua vilivyo, nataka kujua ni nani huyo?"
Kisha akainua kichwa chake na kumtazama Sabrina ambaye aliinamisha kichwa chini tu, na kumfanya Sam aendelee kuongea,
"Najua hili swali huwa ni gumu sana kwako, tafadhari Sabrina. Nahitaji kujua mwenye hiyo mimba, nakupa siku mbili uniambie muhusika wa hiyo mimba"
Sabrina alikuwa akitetemeka kwa aibu tu wakati akiambiwa maneno hayo na mumewe.
Walitulia pale mpaka muda wa kulala ulipofika na kulala.

Kulipokucha kama kawaida, Sam aliondoka na kwenda kazini ila Sabrina alifungiwa ndani kama alivyofanyiwa jana yake.
Njiani Sam alikuwa akiwaza tu, kwani mwanzoni alikuwa na hisia za uhakika kabisa kama muhusika ni Jeff lakini jana ile simu ya Jeff ilimshangaza kwani aliamini kuwa lazima wangeongelea mambo ya kimapenzi ambayo yangempa hasira zaidi Sam na kumfanya atende kile alichokitarajia.
Lakini kilichomshangaza ni yale mazungumzo yao yaliyoonyesha kuwa Jeff hana hatia hata kidogo kwani alikuwa akimuheshimu sana Sabrina.
Sam hakupata jibu na kumfanya ajipe matumaini ya kuendelea kuchunguza huku akijilaumu kwa kile kitendo chake cha kumnyooshea bastora Sabrina.
"Nampenda sana, ningewezaje kumuua? Sabrina ana sura ya upole, siku zote anaonekana kuwa hana hatia ingawa anafanya makosa, nawezaje kummaliza Sabrina? Nawezaje kummaliza mtoto mdogo malaika wa Mungu asiye na hatia Cherry? Ooh Mungu nisaidie nisije rudia tena kile kitendo na kujiku......."
Akashtuka gafla na kufunga breki mbele ya mtu yani ilikuwa bado kidogo tu amgonge, alishuka upesi kwenda kumuomba msamaha ambapo alimkuta kajawa na hasira na uoga wa kugongwa.
Kumuangalia vizuri alikuwa ni yule yule Neema, wakati huo Neema nae alishangaa kumuona kuwa ni Sam.
"Kumbe ni wewe Sam ulitaka kuniua tena?"
"Tafadhari nisamehe Neema, yani hata sijui nina matatizo gani"
Ikabidi watoke pale na kuingia kwenye gari ya Sam na kuacha watu walioanza kukusanyika katika eneo lile.

Sam hakwenda moja kwa moja ofisini bali alipita kwenye baa ya karibu ili kupata supu na Neema.
Walifika na kukaa na kuagiza,
"Nisamehe bure Neema, kwakweli hata sijui kuna nini kati yetu maana si jambo la kawaida hili"
"Na kweli si jambo la kawaida maana ni mara ya pili hii unataka kunigonga. Mi nahisi kuwa kuna kitu kipo kati yetu"
"Inawezekana, ila nisamehe sana"
Wakanywa supu pale, kisha wakainuka ili Sam ampeleke Neema alipokuwa anaelekea na yeye kwenda ofisini kwake.

Sabrina nyumbani bado alikuwa na mawazo ya kutosha kabisa, na kikubwa alijiuliza kuhusu Jeff hakuamini kabisa kama Jeff ndiye aliyeongea nae jana.
Moja kwa moja akachukua simu yake na kuingia kwenye mtandao wa facebook kuangalia kuwa Jeff atatoa hoja gani.
Na alipoingia tu akashtuliwa na ujumbe toka kwa Jeff ambaye humo alijiita Prince J.
"Hellow, jana usiku nimeota. Huwezi amini mamy ila nimekuota kuwa tupo pamoja tukifurahia mapenzi yetu"
Sabrina akaamua kumuuliza Jeff,
"Hivi ni wewe kweli uliyenipigia simu jana mchana?"
"Wow, upo hewani mamy. Ni mimi ndio kwani kuna tatizo gani?"
"Nimekushangaa, mbona jana umeongea kwa ustaarabu sana?"
"Nilikumiss sana, muda kidogo kuna roho ikaniambia nikupigie simu. Ulipopokea nikahisi kama kuma mtu anasikiliza maongezi yetu ndiomana nikaongea vile. Kiukweli mimi nakupenda sana, na kuna kitu muhimu sana kati yetu ingawa wewe hutaki kukubali wala kuamini hilo"
Sabrina alisoma meseji hii mara mbili mbili na kuhisi kuwa huenda kuna kitu kweli kati yake yeye na Jeff, kisha akamuaga ila kabla hajafunga ukaingia ujumbe wa mwisho kutoka kwa Prince J naye akimuaga pia,
"Nakupenda sana, milele nitaendelea kukupenda haijalishi kitu mimi nitakupenda siku zote"
Sabrina alifunga simu yake na kujifikiria, hii ndio aina ya upendo alioutaka yeye kwani siku zote upendo wa Sam juu yake hakuuelewa kabisa kwahiyo alihitaji huu upendo anaouhisi upo kwa Jeff tu.

Sakina sasa akaamua kufunga safari na kwenda tena kwa yule mtaalamu wake ili kujua mambo yake yameishia wapi.
Alimkuta na kuanza kumuulizia,
"Nimekuja kukushukuru mtaalamu na pia unisaidie mkwe wangu arudi nyumbani"
"Usijali, mkweo lazima arudi hata usiwe na wasiwasi. Tena atarudi siku sio nyingi"
"Sawa nashukuru baba, vipi kuhusu swala la yule mdogo wangu?"
"Yule mdogo wako namsaidia sana, mwambie aje nimtengeneze. Namuhurumia sana, amezungukwa na watu wabaya, jitahidi uje nae nimsaidie kwa karibu zaidi."
"Sawa nitakuja nae hakuna tatizo hata usijali"
Yule mtaalamu akampatia Sakina dawa zingine za kuweka ndani ya nyumba yake ili azidi kuwa salama.
Kisha Sakina akaondoka zake.

Sakina akiwa njiani akashangaa gari ikisimama mbele yake na dereva kushuka, alikuwa ni Sam na kumfanya asimame na kuanza kusalimiana nae.
"Panda kwenye gari nikupeleke shemeji"
Sakina hakusita na kupanda kwenye gari ya Sam kisha safari ya kwenda nyumbani kwake.
"Hivi umeongea na Jeff shemeji? Anakusalimia sana"
"Ni jana tu hapo katoka kunipigia simu, huwa nafurahi sana shemeji"
"Vipi umemfatilia na mkwe wako Dorry?"
"Ndio niliongea nae akasema atakuja"
"Usijari, mi nitamfata na kumleta. Unatakiwa kumpenda sana yule binti, mtu kaamua kubeba mimba ya kijana wako bila tatizo unatakiwa kumpenda sana"
"Hata hivyo nampenda sana, yani hapa natamani huyo mjukuu wangu azaliwe leo kesho jamani. Natamani sana kubeba damu ya mwanangu kwenye mikono yangu"
Wakaongea mengi hadi walipofika nyumbani kwa Sakina ambapo Sakina alishuka na kumuaga Sam.
Wakati Sam anaondoka aliamua kumpigia simu Dorry na kumsihi kuwa arudi kwavile mambo yote yapo sawa.
"Huku hakuna tatizo Dorry, jitahidi tu urudi ili mtoto wako alelewe huku"
"Sawa nimekuelewa"
Kisha akakata ile simu.

Dorry alizidi kumshangaa Sam kwani ukweli wote aliujua ila bado alimsisitiza kuwa arudi kwakina Jeff ili mtoto wake akalelewe kule,
"Lazima Sam atakuwa na mipango binafsi tu, maana sio kitu rahisi eti yeye afurahie tu kuona mtu analea mimba isiyo muhusu"
Alifikiria sana lakini aliona ni jambo jema katika kumsaidia yeye malezi ya mimba na mtoto.

Deo akiwa ametulia pale nyumbani kwake na kumuuliza mke wake kuhusu watoto wao.
"Vipi huyu Sabrina hajui kama nimekuja nini? Maana naona leo siku inapita bila ya yeye kuja kuniona. Maana katika wanangu wote huyu ndio kiboko yao kwa kunipenda"
"Nilimpigia simu jana ila hakupokea, nimemtumia na ujumbe lakini hajajibu natumaini atakuja tu hata usiwe na wasiwasi"
"Wasiwasi lazima, nimewakumbuka wanangu. Wajukuu na kila kitu"
Kisha akafikiria kidogo na kuuliza,
"Na yule mkwe wetu jana alifata nini?"
"Alipita kusalimia tu"
"Mbona akaondoka aliponiona?"
Mama wa Sabrina aliamua kubadilisha mada, kwani alijua kitakachoendelea hakitakuwa sawa kabisa.

Sabrina alitulia akingoja muda ufike na Sam arejee,
"Sijui leo kutakuwa na tukio gani jipya"
Akatazama tumbo lake na kusema,
"Eeh mimba wee, siku nitakapokuzaa nitapumua kwakweli maana sina raha kabisa. Najutia yote niliyoyatenda nyuma"
Sam nae akawa amewasili na kumkuta Sabrina akiongea peke yake pale.
Alimuuliza swali moja tu,
"Umekula?"
"Ndio nimekula"
"Basi vizuri"
Kisha Sam akaenda zake chumbani na kulala.

Sabrina alibakia pale pale sebleni peke yake kwani muda huo hata mtoto wao naye alikuwa ameshalala.
Sabrina akajikuta akipitiwa na usingizi pale kwenye kochi.
Wakati amelala, akajiwa na njozi.
Akajiona anaolewa tena, kumuangalia mwanaume anayemuoa alikuwa ni Jeff tena sura yake ikiwa imejawa na furaha sana.
Sabrina nae alikuwa amejawa na furaha, Jeff akamsogelea na kumwambia.
"Siamini kama leo nakuoa mwanamke wa maisha yangu"
Sabrina akatabasamu, Jeff akamsogelea ili ambusu Sabrina mdomoni mara akatokea Sam karibu yao.
Hapo hapo Sabrina akashtuka na kujiona kuwa bado yupo sebleni.

Sam akiwa amelala, akashtuliwa na mlio wa simu yao.
Kuangalia mpigaji kwa usiku ule alikuwa ni Neema.
Sam hakutaka kupokea ile simu na kuicha iendelee kuita tu.
Alitazama mule chumbani bila kumuona Sabrina, aliamua ainuke ili aende sebleni kumfata.

Sabrina pale sebleni baada ya ile ndoto, akajikuta akikaa na kuchukua simu yake moja kwa moja na kuingia kwenye mtandao wa kijamii ili kumwambia Jeff kuhusu alichoota.
Alipoingia tu akakutana na ujumbe toka kwa Prince J ukionyesha umetumwa muda sio mrefu,
"Yani huwezi amini mamy, nimetoka kukuota muda sio mrefu eti tunaoana"
Sabrina akashangaa kuwa inakuwaje ameota ndoto moja na Jeff.
Kabla hajajibu chochote, akashangaa kumuona Sam mbele yake
"Nipe hiyo simu Sabrina, tena usibonyeze chochote"
Sabrina aliona sasa mwisho wa ujanja wake umefika.


Sabrina akashangaa kuwa inakuwaje ameota ndoto
moja na Jeff.
Kabla hajajibu chochote, akashangaa kumuona Sam
mbele yake
"Nipe hiyo simu Sabrina, tena usibonyeze chochote"
Sabrina aliona sasa mwisho wa ujanja wake
umefika.
Mwili wote ulimuisha nguvu Sabrina ukizingatia pale alikuwa akiwasiliana na Jeff kwa njia ya meseji, na ubaya zaidi yalikuwa ni maneno ya kimapenzi.
Kilichomuumiza kichwa zaidi ni ile picha ambayo alitumiwa na Jeff wakiwa wote kitandani kuwa Sam akiiona je itakuwaje.
Sabrina akataka kumpa simu Sam ili liwalo na liwe, ila nafsi yake nyingine ikamshauri kitu na kumwambia kuwa asikubali kushindwa kirahisi namna ile.
Alichokifanya Sabrina ni kuibamiza chini ile simu kisha na yeye kuanguka.
Sam alimuangalia Sabrina na kutikisa kichwa, akataka kumfata pale chini ila akasita na kuamua kumuacha pale pale na kurudi chumbani.

Sam alikaa chumbani na kusikitika sana, kama kawaida yake akaanza kumuweka Sabrina kwenye kundi la wanawake wasiokuwa na akili.
Aliona wazi kuwa alikosea sana kumuoa Sabrina,
"Ni kheri nisingemuoa tu, mambo gani haya ya kuishi na mwanamke asiyekuwa na akili? Mwanamke gani huyu wa kubwaga simu na kujifanyisha kuzimia ili nisimseme kwa makosa yake? Ni wazi alikuwa akiwasiliana na mwanaume, sijui cha kufanya kwa huyu kiumbe kwakweli"
Sam aliwaza sana na kujilaza pembezoni mwa kitanda kwani akili yake ilishavurugika kwa wakati huo.

Kulipokucha kama kawaida, aliinuka na kwenda kuoga bila ya kujali kuhusu Sabrina.
Alimaliza na kuvaa, ila alipoangalia kitandani akagundua kuwa Sabrina bado yupo sebleni, akatikisa kichwa chake na kumfanya azidi kumpunguza akili Sabrina.
Alipomaliza kuvaa akamuona mtoto wao kitandani akiwa ameamka huku akicheza cheza, akaamua kutoka mule chumbani ili akamshtue Sabrina kuwa mtoto alishaamka tayari.
Ila kufika sebleni akashangaa kumuona Sabrina akiwa pale pale chini, akatikisa kichwa,
"Hivi huyu mwanamke ana akili kweli?"
Akamsogelea na kumpiga teke kumuonyesha kwamba hataki ujinga kwa wakati huo.
Ila ile teke lilifanya kama kumsogeza Sabrina kidogo.
Sam akashangaa na kushtuka baada ya kuona damu pale ambapo kililala kichwa cha Sabrina na kumfanya ainame haraka kumchunguza.
Ni kweli kwenye sura ya Sabrina kulijaa damu na ilionekana ikimtoka mdomoni.
Sam hofu ikamjaa na huruma pia, aliamua kumbeba Sabrina juu juu na kutoka naye nje hadi kwenye gari yake huku akimuamuru mlinzi wao afungue geti kwa haraka.

Geti lilifunguliwa kwa haraka sana, kisha Sam akaondoa gari kwa kasi na kusahau kuwa kuna mtoto wamemuacha ndani ya nyumba yao.

Inaendeleah



USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

No comments:

Theme images by pollux. Powered by Blogger.